JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................220-221

Sura ya: 220

“Hapana,” Nina. akasema, “Joel ni mume wangu. Ninawezaje kukuacha umtunze? Nikizungumza kuhusu madaktari mashuhuri, ninawafahamu wengi pia.”
“Hiyo ni kweli,” Melanie alitikisa kichwa na kusema kwa chuki, “Hata kama mtu mwingine angelazimika kumtunza Baba, angekuwa mimi. Hutaweza kuwa na nafasi. Usisahau kwamba hata hujaorodheshwa kwenye daftari la ukoo wa Ngosha.”
"Ikilinganishwa na familia ya Choka, unafikiri unawajua madaktari bingwa zaidi kuliko wao?" Lisa aliuliza.
Nina alikosa la kusema kwa muda lakini akasisitiza na kusema, “Hata hivyo, sitawahi kukupa haki za kumtunza Joel. Sikuweza kushindana dhidi ya mama yako hapo awali. Sasa Joel amepoteza fahamu, usiniambie kwamba siwezi hata kushindana na binti wa Sheryl.” Akiwa na huzuni, alianza kulia tena.
Maneno ya Lisa yalikuwa yamewagusa wote wawili Mzee Ngosha na Bibi Ngosha, waliona wazi kuwa haikuwa haki kwa Nina kumtunza mumewe.
Lisa alimpuuza Nina na kumkazia macho tu Mzee Ngosha. "Babu, unajua vizuri zaidi kuliko mtu mwingine yeyote kwamba Baba amekuwa akisisitiza kuhusu talaka na Nina hivi karibuni. Sasa, kwa kuwa sasa Baba amepata ajali, atawezaje kumhudumia kwa upendo? Kwa hivyo, ugawaji wa mali ya baba yangu utaenda kwa mwanaye na wazazi wake.”
Mzee Ngosha alishikwa na butwaa. Hapohapo Nina alijitupa kwa Lisa na kumsukuma kwa hasira. “Unajaribu kumaanisha nini? Unataka kusema kwamba nimepanga kumuua Joel? Lisa, wewe ni mwanamke katili, lakini usiwafikirie wengine kuwa katili kama wewe. Nampenda Joel. Ninampenda kuliko mtu mwingine yeyote.”
“Sikusema umepanga kumuua baba. Nawakumbusha tu Babu na Bibi nini kitatokea ikiwa baba hataamka.” Sauti yake ilikuwa kali. “Bila shaka, sina shaka kwamba una nia potofu. Nafikiri ni afadhali kuwa macho kwani familia tajiri si kama familia za kawaida.”
Bibi Ngosha aliamini. “Sawa, nimekubali kukuacha umtunze Joel.”
“Mama, unaamini maneno yake kwamba nitamuumiza Joel?” Nina alilia kwa mfadhaiko, “Ikiwa watu wa nje wangesikia haya, wangefikiriaje?”
"Anti, ninafanya hivi kwa faida yako mwenyewe." Lisa alikuwa na uso wa dhati. “Kwa kuwa baba yangu amepata ajali, kampuni ya Ngosha lazima iingie kwenye hali mbaya sasa. Je, wewe na Melanie hamhitaji kuendesha kampuni? Mtawezaje mambo ya kampuni huku mkimhudumia baba? Kwa kawaida, Melanie anajua tu jinsi ya kujipamba na kwenda kufanya shopping. Ni wakati wa kuanza kuchukua majukumu sasa. Unapaswa kumsaidia kama wewe ni mama yake."
Melanie alishangazwa na maneno yake. Nina alifungua kinywa chake ili kujibu, lakini Damien, mdogo wake na Joel, ambaye muda wote alikuwa ameketi kimya kwenye kiti cha magurudumu, alisema hivi ghafula, “Lisa aliyosema ni maneno ya busara. Kama mke, unapaswa kuchunguza chanzo cha ajali ya gari pia."
",..sawa." Nina alimkazia macho Lisa. “Lazima umtunze Joel ipasavyo. Ikiwa chochote kitampata, sitakuacha salama.”
Lisa alitabasamu kwa uchungu. "Bila shaka nitafanya. Hakuna faida kwangu ikiwa baba ataaga dunia. Ikiwa nahitaji uwepo kwake, siwezi kumuona kama akifa. Hata kama ninahitaji utajiri wake, sitapata hata senti moja ikiwa atakufa. Ikilinganishwa na mimi, Melanie ana bahati zaidi ikiwa baba atakufa…”
Alisikika kama mtu asiyejali, lakini Mzee Ngosha na Bibi Ngosha walikuwa na akili za haraka. Mara moja walielewa ni nani angepata manufaa zaidi ikiwa Joel angekufa. Kwa kawaida, ingekuwa ni Nina na binti yake. Kila kitu kilikuwa sawa wakati wote, lakini ajali ya gari ilitokea ghafla. Hilo liliwafanya wawe na mashaka.
“Baba, mtendaji mkuu wa kampuni alipiga simu na kusema kwamba waandishi wengi wanakusanyika mbele ya jengo la kampuni. Hali si shwari sasa,” Damien alisema.
“Ndugu yako atakuwa amepoteza fahamu kwa muda mrefu. Utasimamia kampuni kwa muda sasa. Kuhusu Melanie, anahitaji kwenda kwa kampuni mara moja pia. Unapaswa kumsaidia vyema.”
Damien alitabasamu kwa huzuni. "Lakini mimi si mzuri katika kushughulikia masuala ya kampuni..."
"Lazima uifanye hata kama huwezi." Mzee Ngosha alikuwa na sura ya ukali. "Familia ya Ngosha haiwezi kuanguka."
“Sawa, nitafanya niwezavyo.” Damien aliitikia kwa kichwa.

Baada ya kumkalisha Joel, Mzee Ngosha na wengine walitoka wodini. Walikutana na Alvin ambaye alikuwa akija kwa kukimbia.
“Bwana Mkubwa Kimaro…” Akifikiria maendeleo ya baadaye ya Alvin, Mzee Ngosha alipanda haraka na kumpa mikono.
“Habari babu Ngosha. Nilisikia kuhusu hali ya Baba kutoka kwa Chester. Hakika nitatafuta daktari bora zaidi kwa matibabu yake.” Sauti ya Alvin ilibeba heshima ambayo mdogo anapaswa kuwa nayo kwa mkuu wake. Mtazamo wake ulikuwa tofauti kabisa na pale alipoongozana na Melanie kwenye karamu ya siku ya kuzaliwa ya Mzee Ngosha.
"Asante." Mzee Ngosha alimkazia macho Lisa. Ilionekana wazi kuwa Alvin alimjali sana huyu mjukuu wake.
Ilionekana kwamba wangetakiwa kumjali sana Lisa na kumtendea vizuri zaidi katika siku zijazo. Kwani akina Ngosha walipoteza tegemeo baada ya Joel kupata ajali. Bado walilazimika kuwategemea waume wa wajukuu zao.
Mzee Ngosha alifikiria kwa muda kisha akamgeukia Lisa na kusema, “Usiwe na huzuni kupita kiasi. Bado wewe ni mchanga na unapaswa kuendelea kutembea kwenye njia yako. Unaweza kufika nyumbani mara kwa mara ili kututembelea. Ukitaka kuingia Ngosha Corporation, tuambie wakati wowote.”
Lisa alishangaa, lakini alielewa haraka. Watu wa familia ya Ngosha walikuwa wapuuzi kwelikweli waliojua kujipendekeza haswa.
“Babu, unawezaje kukubali kumruhusu Lisa aingie kwenye Kampuni ya Ngosha?” Melanie alipiga kelele. Hakuweza kukubali hata kidogo.
“Inatosha. Lisa bado ni dada yako, na anaweza kukusaidia katika siku zijazo pia.” Mzee Ngosha aliondoka na Bibi Ngosha baada ya kumaliza kuzungumza.
Melanie alikanyaga miguu yake kwa kutoridhika. Aligeuka na kumwangalia Lisa, lakini sura ya Alvin yenye mvuto mkali ilikutana na macho yake badala yake. Moyo wake ulipiga bila mpangilio. “Bwana Kimaro…”
Alvin hakumtazama hata kidogo. Akasogea na kuizungusha mikono yake kiunoni mwa Lisa, akimfariji kwa upole. “Usiwe na huzuni. Uko nami kuanzia siku zote.”
Melanie alikuwa anakaribia kuwa wazimu kutokana na wivu alipotazama tukio hilo. Alvin hakuwahi kumfanyia mahaba kama hayo hapo awali. Japokuwa Jerome alijitahidi kumwonyesha mapenzi, bado alikosa hekima ukilinganisha na Alvin. Isitoshe, Jerome hakuwa na umbo zuri kama Alvin pia.
Melanie aliuma mdomo wake kwa chuki na kusema, “Usijidai sana Lisa. Babu alifanya hivyo tu kwa heshima ya Bwana Mkubwa Kimaro. Kama sivyo, huwezi kuwa sehemu ya familia ya Ngosha.”
Lisa alishindwa kabisa kuyaelewa mawazo ya Melanie. “Melanie, nimevutiwa sana na wewe. Baba amepoteza fahamu sasa, lakini wewe, kama binti yake, bado unapata wivu juu ya mambo kama hayo.”
“Hiyo haikuhusu” Melanie alidhihaki, "Ngoja nikuambie. Kuna mtu ambaye Bwana Kimaro anamthamini. Huyo ni mtu ambaye huwezi kamwe—”
“Melanie Ngosha.” Alvin alimkatisha kwa nguvu huku macho yake yakionyesha onyo kali. "Ukithubutu kusema neno lingine, nitakufanya ujute kuwa na ulimi."
“Bwana Mkubwa Kimaro, Melanie yuko katika hali mbaya. Anaongea ujinga tu.” Nina alihisi kwamba Alvin alikuwa amekasirika, hivyo mara moja akamshika Melanie na kuondoka zao.
“Alvin Kimaro, hata kama huniruhusu nizungumze, kila mtu katika familia tajiri jijini Nairobi anajua. Lisa atajua mapema au baadaye…” Sauti isiyo na kikomo ya Melanie ilisafiri kwenye korido kutoka mbali.
Wodi ilikuwa kimya isipokuwa sauti ya mashine ya electrocardiograph.
Alvin alimtazama mwanamke aliyekuwa pembeni yake kwa woga. Hata hivyo alimuona tu Lisa akiwa ametulia akichota maji ya moto ili kumfuta Joel usoni. Ni kana kwamba maneno ambayo Melanie alisema haykuyasikia kabisa.
“Babe, kuhusu yale Melanie alisema, usi…”

Sura ya: 221

“Usijali, sitafikiria sana. Siko katika hali ya kufikiria kitu kingine chochote isipokuwa baba yangu sasa,” Lisa alimkatisha tamaa.
Alvin hakujua kwamba Lisa alikuwa anajua tangu muda mrefu kuhusu kuwepo kwa Sarah maishani mwake. Pia alielewa kwamba Sara alikuwa amechongwa sana moyoni mwake. Hiyo ndiyo sababu asingeweza kujisikia vibaya. Alikuwa kaishazoea tayari. Hakukuwa na sababu ya kumfanya ajisikie kuchukizwa na jambo hilo pia. Wafu hawawezi kupigana na walio hai hata hivyo.
“Sawa, ni vizuri basi.” Pamoja na kusema hivyo, bado moyo wa Alvin ulizidi kudunda pasipo kujua.
Alihofia kwamba Lisa angeelewa vibaya au kufikiria mambo kupita kiasi. Hata hivyo, alijisikia vibaya kumuona akionyesha kupuuza kabisa jambo hilo. Baada ya yote, alihisi kwamba sababu ya Lisa kupuuzia jambo hilo inaweza kuwa ni kwa sababu hakumpenda vya kutosha. Akamkazia macho. Kero ndani ya moyo wake ilikuwa ikimrudia tena. Akatoka na kwenda kuvuta sigara mbili nje.
Alirudi nusu saa baadaye. Lisa alikuwa akimnywesha maji Joel aliposikia mlango unafunguliwa. Alimtazama kisha akakwepa macho yake.
Alvin alihisi kutokuwa na raha moyoni mwake. Alitoka wodini kwa muda mrefu, lakini hata aliporudi Lisa hakuuliza kwanini alikuwa ametoka. Ina maana aliamua kumpuuza kabisa? Hata hivyo, alipotazama hali ya Joel, alihisi kwamba moyo wa Lisa haukuwa na nafasi ya kufikiria juu ya upuuzi huo.
Alvin alikohoa kidogo na kusema, “Nilimjulisha Chester sasa hivi na kumwomba aandae muuguzi bora wa kumtunza baba yako. Pia atawasiliana na madktari bingwa wa ng'ambo ili kujadili hali ya baba…”
“Asante,” Lisa alisema kwa dhati.
“Hakuna haja ya wewe kunishukuru. Wewe ni mke wangu. Ninafanya sehemu ya wajibu wangu tu.” Alvin hakuridhika na tabia yake ya kuwa na adabu kupitiliza. "Halafu pia, ulipigania kumtunza baba yako kwa sababu ulishuku Nina anahusika na ajali yake?"
“Ndiyo, ninashuku huenda aligundua kuwa baba yangu alitaka kunihamishia asilimia 35 ya hisa. Mwanamke mwenye ubinafsi kama Nina, na Farres nyuma yake, angeweza kufanya chochote kulinda faida zake.”
“Kweli.” Alvin aliitikia kwa kichwa. "Tayari nimeweka mtu wa kuchunguza chanzo cha ajali."
Lisa alizama kwa muda katika mawazo yake. "Lakini ... Kuna mtu mwingine ambaye ananipa hisia isiyo ya kawaida."
"Nani?"
“Damien.” Lisa alitamka waziwazi na kuendelea. “Nilipoomba kumtunza baba yangu hapo awali, Nina aliendelea kugoma na kufanya fujo. Lakini Damien alipomshawishi, Nina alikubali ghafla. Pia nadhani aliendelea kubadilisha mada ili kumsaidia Nina, iwe kwa makusudi au la. Mara ya kwanza nilipoenda nyumbani kwa akina Ngosha, aliongoza mada ili kunilenga mimi na kila alichoongea Nina alisapoti na yeye akasapoti kile Nina alisema. Ingawa yeye ni mtu wa maneno machache, nadhani yeye sio mtu rahisi kama anavyoonekana.”
Baada ya Lisa kumaliza kuongea, aligundua kuwa Alvin alikuwa akimwangalia kwa kina. "Nini? Kuna kitu usoni mwangu?" Lisa alijishtukia na kujigusa usoni.
"Hapana, nadhani hisia za mwanamke wangu zinazidi kuwa kali." Alvin alibana uso wake mdogo. "Kama nilivyotarajia kwa mwanamke ambaye nimempenda."
Lisa alikosa la kusema. Hakuwa katika hali ya kubebishana naye muda huo.
“Sawa, sikuweza kujizuia kukusifu.” Alvin aliutoa mkono wake kwa unyonge na kuweka uso ulionyooka. “Nisingeona kama usingetaja. Damien huyu hakuwa wa kuvutia macho hata kidogo. Nilisikia kwamba ana ulemavu wa kuzaliwa. Alikuwa mlemavu wakati wa kuzaliwa, hivyo kila mtu katika familia ya Ngosha ni mzuri kwake. Hata baada ya kukua, bado anaishi chini ya ulinzi wa baba yako na familia ya Ngosha. Bado hajaoa.”
“Kwanini? Una maanisha hawezi kufanya ngono?” Maneno ya Lisa yalikuwa ya kushangaza.
Alvin alitafakari maneno yake kwa muda. Kisha, akasema kwa ukali, “Tumia tafsida basi. Unafikiri inafaa wewe kama mke wa mtu kuzungumzia mambo kama hayo moja kwa moja?”
“Nina hamu ya kutaka kujua. Inawezekanaje kwa mwanamume kuhimili tamaa za mwili tangu ujana hadi uzee bila kuoa?”

Alvin aliinua uso wake na kumtupia Lisa jicho lisiloeleweka. “Bila shaka, inawezekana. Siku zote nilikuwa peke yangu kabla ya kukutana na wewe, miaka karibu mitano nimeweza kuvumilia.”
“Kwa mwanamume si rahisi, lazima ulikuwa unapoza sehemu!” Lisa alikataa kuamini.
“Mimi—” Alvin alitaka kuongea lakini Lisa akamkatisha haraka.
“Sijasema kwamba haiwezekani, inawezekana lakini inategemeana.” Lisa aliendelea kusema. “Ikiwa mwanamume hataki kuoa, ni aidha hana uwezo wa kufanya ngono, au ana mtu moyoni mwake. Nadhani Damien anaweza kuwa anampenda Nina.”
Alvin alibisha, “…Hapana.”
“Huniamini?” Lisa alikunja uso. "Silika ya mwanamke ni sahihi sana. Nilisoma vitabu vya kisaikolojia hapo awali na kuligundua hilo. Kwa wale ambao wamekuwa walemavu tangu kuzaliwa, baadhi yao wana fikra chanya na wenye furaha, huku baadhi yao wakiwa na fikra potofu na waliojikatia tamaa.”
"Haijalishi, hii ni dhana yako tu. Lazima kuwe na ushahidi.” Alvin alisema. “Lakini mtu aliyemuumiza baba yako lazima aogope kwamba atarudiwa na fahamu. Mtu huyo anaweza hata kuja kummalizia mwenyewe…”
“Nafikiri hivyo pia.” Lisa aliunga mkono hoja. “Sasa tutasubiri. Maadam atajitokeza, ni hapo tu ndipo tunaweza kumshika injinia wa ajali hii.”
Lisa alibadilishana macho na Alvin na akaelewa mara moja. Kama alivyotarajia kwa mwanamke wake. Hapo awali alihofia kwamba Lisa asingeweza kukabiliana na utata na mikimikiki ya jiji la Nairobi. Alikuwa akifanya maendeleo haraka kuliko vile alivyofikiria.
Siku iliyofuata, kama vile anga lilivyoangaza, Hans alileta matokeo ya uchunguzi. “Hakuna tatizo kwa dereva wa lori lililohusika katika ajali hiyo. Sedan ya Mkurugenzi Ngosha ndiyo ilishindwa kujizuia na kuligonga lori hilo kwa mbele. Polisi walimfanyia uchunguzi dereva wa Mkurugenzi Ngosha na kubaini kuwa tumbo lake lilikuwa na kiasi kikubwa cha dawa za kulevya.”
"Dereva alipoteza udhibiti wa gari kutokana na kutumia dawa za kulevya?" Lisa alishangaa.
"Hii inapaswa kuwa sababu kuu ya ajali hiyo. Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu waliomchunguza, dereva huyo hakuwa ametumia dawa za kulevya tangu azaliwe, hivyo huenda alizitumia kimakosa. Lakini dereva amekufa, hivyo hakuna anayejua alikuwa akiwasiliana na nani alipokuwa hai na ni nani aliyempa dawa hizo. Watu waliokufa hawaongei.” Hans aliweka kituo kifupi na kumalizia, “Farres pia alichunguzwa, na inaonekana hana uhusiano wowote na kesi hii."
Lisa alikata tamaa kidogo, lakini alitarajia kwamba kwa vile kuna wahalifu waliothubutu kumuumiza Joel, wangekuwa wamejitayarisha vya kutosha.
“Tufanye taratibu. Mradi tu tukifuatilia kwa karibu, mtu huyo hakika atafahamika.” Alvin alimtuliza.
Lisa aliitikia kwa kichwa. Alijua hakukuwa na faida ya kuwa na papara.
"Mume, kampuni yako inafanya mkutano na waandishi wa habari kesho kutwa. Kila kitu kiko tayari?" Lisa alimkumbusha Alvin ghafla.
"Tunahitaji kujiandaa na nini?" Alvin alimshangaa.
Lisa alipigwa na butwaa kwa muda. "Kwanini unaniuliza hivi? Mimi sijui chochote kuhusu makampuni ya saruji. Kila mtu nchini Kenya kaandaa macho yake kwenye mkutano huo na waandishi wa habari kesho kutwa.”
“Usijali. Nahitaji tu kula nyama choma ya nguruwe iliyotengenezwa na mke wangu na sitakuwa na shida kabisa.” Alvin alijieleza kwa utulivu, lakini macho yake yalijawa na matarajio.
Lisa alinyamaza. Alihisi Alvin lazima ali’miss sana nyama ya nguruwe choma. Hans, ambaye alikuwa amesimama pembeni, alishindwa kujizuia na kuangua kicheko.
“Unacheka nini? Toka nje.” Alvin alimfurusha bila huruma.
“Mbona unakuwa mkali sana kwake?” Lisa aliutazama mgongo wa Hans kwa huruma wakati anaondoka. Hans ni mtu pekee ambaye alikuwa na uwezo mkubwa wa kustahimili hasira za Alvin.
“Yeye si mke wangu hata hivyo. Unasema kwamba ni lazima niwe mpole kwake?” Alvin alimshika mkono. "Nina uwezo wa kuwa mpole kwako tu."
Lisa aliishiwa na akili kwa muda, lakini alipata fahamu haraka. Tayari alikuwa amefunikwa na majeraha, na moyoni mwa Alvin alibaki kuwa mtu asiyeweza kufutika.

"Ninajaribu kuwa na wewe kimapenzi, lakini kila nikikuweka karibu unarukaruka tu kwanini?" Akiwa amehuzunika, Alvin alimvuta kwenye kumbatio lake na kumng’ata mdomoni kana kwamba ni adhabu. “Unanipenda au hunipendi?”....ITAENDELEA.....

Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.