JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................218-219
Sura ya: 218
"Vipi, unaipenda?" Alvin alitabasamu kwa upole kabla ya kuinamisha kichwa chake upande mmoja kutazama majibu ya Lisa.
“Kwa nini umeninunulia gari ghafla wakati nina magari mengi tu?” Alijaribu kila awezalo kujiondoa katika mshtuko wake.
“Hayo magari hayana kile ninachokitaka kwa mke wangu. Nataka uwe na kilicho bora zaidi." Alibonyeza kitufe cha ufunguo na milango ikatanda kama mbawa za mwewe, ikionyesha mambo ya ndani ya kifahari na ya kuvutia.
“Naipenda. Asante." Lisa alitikisa kichwa kwa dhati. Huenda angeikataa zawadi hiyo hapo awali, lakini, kwa vile alikuwa mke wake sasa, aliona inafaa.
“Umeipenda kweli?” Alvin aliinua macho yake kumwangalia, akionekana kutoridhika. "Unataka nini kingine?"
Mwonekano huo wa uso wake ulimfanya Lisa aone haya mara moja. “Nitake nini tena? Mimi ni mke wako, hivyo kilicho chako ni changu.”
“Hiyo ni sawa. Hata mwili wangu ni wako.” Akasogea karibu na kumkandamiza mlangoni. Baada ya busu refu na la mapenzi, alijiondoa kwa kusita. “Mtoto mzuri, unazidi kuwa mrembo kila kukicha.”
“Asante mume. Niache nikapumzike sasa.” Hakuweza kumudu tena mahaba ya Alvin, mtu yule aliyekuwa na kiburi hapo awali ambaye muda huo alikuwa romantiki kupita kiasi. Hiyo ilimpa hisia fulani za usalama. Alvin hakujali sura yake mbaya; bado alimjali kama hapo awali.
•••
Kesho yake Lisa aliendesha gari lake jipya barabarani asubuhi na mapema akielekea kazini.
Gari hillo la kifahari lililokuwa na plate namba ya kipekee lilivutia macho mengi kutoka kwa wapita njia. Alikuwa amekwama kwenye njia panda akisubiri taa ya kijani imruhusu kupita wakati Pamela alipomrushia video fulani kutoka whatsapp ikiwa na maelezo yafuatayo:
[Lisa, nimeona video hii kwenye group la whatsapp ikanivutia sana. Limelipenda sana hili gari.]
[Kwa hiyo?] Lisa aliuliza kwa mshangao. hakuwa ameelewa point ya Pamela.
[Nasikia ndiyo mara ya kwanza kuonekana nchi nzima. Wadau mtandaoni wanasema gari hilo lina thamani ya takriban dola laki mbili na ni toleo maalum. Hata hivyo, plate namba yake imenikosha sana, 4EVA, ina maana ya milele, Inamaanisha mengi zaidi ya kusema tu nakupenda.]
[Kwa hiyo una maanisha nini?] Lisa alizidi kumzingua Pamela ambaye alionekana hajui kama gari hilo ni lake.
[Namaanisha mwambie Alvin akununulie pia. Yeye ni tajiri na atamudu. Ningekuwa na bwana tajiri kwa kweli nisingemwelewa hadi aninunulie kitu kama hicho.]
[Pole wee! Ina maana hujui?... Hiyo gari ni mali yangu.] Lisa alimwambia ukweli.
[Nini?] Pamela alikuwa haamini bado.
[Alvin alinizawadia jana. Nimeanza kuliendesha nusu saa tu iliyopita, sasa nashangaa imesambaaje haraka hivyo mtandaoni?] Lisa hakujua kuwa wakati anatoka tu nyumbani kuna mtu alichukua video ya gari hilo na kuiposti kwenye group la whatsapp.
Kulikuwa na ukimya wa muda mfupi upande wa pili wa whatsapp kabla ya Pamela kuanza kulalamika, [😣Unataka kuwafanya watu wasioolewa kama mimi tuwe na wivu? Alvin alikuwa mtu jeuri asiyejua jinsi ya kuonyesha mapenzi. Tangu lini amekuwa romantiki hivi?]
[Sijui.🤣🤣🤣] Lisa aliweka emoji za kucheka kwa furaha. [Tafuta mwanaume kama yeye ikiwa una wivu. Ni muda mrefu umepita tangu uhamie Nairobi. Bado hakuna mtu anayekumezea mate?😜]
[⛹️♀️⛹️♀️Sihitaji uhusiano kwa sasa…]
[Huhitaji uhusiano kwa sababu bado haujamuacha Patrick?] Lisa akashusha pumzi.
[Usitaje jina lake. Inanifanya niwe mgonjwa.]
[Sawa, basi. Endelea kuwa na wivu juu ya gari langu la 4EVA.]
[Kipi cha ajabu kuhusu hilo? Nitamwomba kaka yangu aninunulie pia.🙄🙄🙄] Pamela akakata simu.
Lisa akatikisa kichwa, akitabasamu. Alipata pongezi nyingine tena baada ya kufika ofisini.
Harvey Ngugi, msaidizi wake, aliingia na tabasamu. “Mwenyekiti Jones, unaonekana mzuri sana siku hizi na baraka tele zinazidi kukumiminikia. Kila mtu hapa Nairobi anajua jinsi Bwana Kimaro anavyokudekeza kama mtoto mdogo. Sawa, huu ni mwaliko wa chakula cha jioni cha biashara kutoka kwa kampuni ya Holt... Na huu ni mwaliko kutoka kwa mwanadada wa Heaven Fashions kwa hafla ya onyesho la mitindo ya mavazi yake…”
Lisa hakuwa na la kusema alipotazama rundo nene la mialiko.
"Kampuni ya Alvinarah inakaribia kuzindua brand ya Cement yao mpya, kwa hivyo kila biashara inajaribu kujenga mahusiano mazuri na Alvin Kimaro. Kwa hiyo watu wanajaribu kunitumia mimi waweze kujenga uhusiano na mume wangu. wafanyabiashara ni wajanja sana. Ilikuwa vigumu sana kupata hata mwaliko mmoja kama huu hapo awali.” Alitabasamu kwa kejeli. "Kwa kweli, kujipendekeza kunamaanisha kila kitu huku Nairobi."
“Ni kwa sababu Bwana Alvin Kimaro ana uwezo. Mwenyekiti Jones, una bahati sana naye." Harvey alidokeza.
Lisa alikosa la kusema. “Peleka mialiko hii kwa wajumbe wengine wa bodi. Wanaweza kushiriki kwa niaba yangu.”
“Hakuna tatizo bosi, ikiwezekana na mimi nipatie moja wapo.” Harvey alijipigia debe wakati akiondoka.
Baada ya Harvey kuonndoka, Lisa alipokea simu kutoka kwa namba isiyojulikana. “Lisa, muda umepita. Nimefika Nairobi. Tunaweza kuonana kwa chakula cha mchana?" Sauti ya Patrick ilisikika kupitia kwenye spika.
•••
Lisa alikutana na Patrick kwa mara nyingine tena. Ni wazi kwamba mwanamume huyo hakuonekana yuko sawa wakati huo. Alionekana amekonda sana kuliko mara ya mwisho walipokutana. Alionekana kuchoka kimwili na kiakili, kama mtu aliyepoteza matumaini kabisa.
"Muda mrefu ... sijaona." Mshtuko ulimtoka Patrick baada ya kuona sura ya Lisa.
“Unaweza kuokoa wakati kwa kuzungumza ulichoniitia hapa na kuacha kushangaa sura yangu,” Lisa alisema kwa uthabiti.
"Ok, samahani. Najua hali yako ni tofauti sasa. Kila mtu anajua kuwa mwenyekiti wa Mawenzi Inventments ni mke wa Bwana Alvin Kimaro. Inaonekana kwamba siku zote nilikudharau zamani.” Sauti ya Patrick ilidhihirisha ishara ya majuto.
Lisa bado alimuona kama anatapatapa tu. “Nenda kwenye point.”
“Nataka kujua Pamela yuko wapi. Amebadilisha namba yake ya simu,” alieleza kwa unyonge, “sijaweza kuwasiliana naye tangu aondoke Tanzania.”
“Muda wote huo?” Lisa alicheka kwa kejeli. "Pamela amebadilisha namba zake zote za simu na whatsapp hata akaacha kuwasiliana na marafiki zake wa zamani baada ya kuhamia Nairobi. Lakini namba yangu ya whatsapp ni ileile. Ungeweza kunipigia simu wakati wowote lakini hukunipigia. Miezi mitatu ameondoka mpaka leo hujamtafuta, kweli?”
Lisa alitoa kicheko kingine cha dhihaka, akasema, “Ulikuwa ukimdharau na kumfanyia unavyotaka, ulifikiri kwamba Pamela hawezi kukuacha kamwe? Ulifikiri angeanza yeye kukutafuta lakini baada ya kukaa kimya kwa miezi michache, sasa tu ndipo unapogundua kuwa anaweza kuwa serious, sivyo?” Patrick aliaibishwa na madongo ya moja kwa moja.
"Lisa, nimekuwa na Pamela kwa miaka michache tayari na tulizungumza juu ya kufunga ndoa mwaka huu. Huu sio mzaha. Tulicho nacho kati yetu ni cha kweli.” Patrick alijitetea.
"Samahani, lakini sidhani." Lisa aliruka kwa hasira. “Unakimbilia kwa Linda kila anapokuhitaji. Ulifanya hivyo siku ambayo ulitakiwa kukutana na wazazi wa Pamela kwa mara ya kwanza na nadhani ungefanya hivyo tena siku ya uchumba wako au hata siku ya harusi yako. Pamela naye ni mtu, ana moyo na anaumia. Lakini wewe hukumjali hata kidogo.”
“Lisa nisikilize kidogo…”
Patrick hakupewa hata sekunde ya kujitetea. “Pamela yuko sawa, unastahili kuwa na Linda kwani nyinyi wawili mnaendana zaidi. Acha kujaribu kuharibu maisha ya Pamela tena.”
“Kwa kweli mimi ninamwona Linda kama dada yangu tu…” Patrick alipata nafasi ya kuongea.
“Samahani kwa kusema ukweli, lakini hakuna mtu anayeweza kumvumilia mwanamume ambaye kila mara anamtanguliza dada yake asiyehusiana naye kwa damu badala ya mpenzi au mke wake.” Lisa alisimama baada ya kusema hivyo. “Ulikuwa unasema ninaharibu uhusiano wako na Pamela kwa makusudi. Uko sawa, sitakuacha umdhuru tena na hakika sitakuambia aliko.”
Sura ya: 219
“Lisa, usivuke mipaka. Hii ni kati yangu na Pamela.” Patrick alikasirika sasa. "Usifikiri kwamba unaweza kufanya kiburi kwa sababu wewe sasa ni mke wa Alvin Kimaro."
"Hivyo ndivyo unavyowaona marafiki wa Pamela… Hujawahi kumheshimu na hakika humstahili." Lisa alichukua mkoba wake na kuondoka baada ya kusema hivyo.
“Nitakaa Nairobi na sitaondoka hadi nionane na Pamela." Sauti ya Patrick ya hasira ilisikika nyuma yake lakini aliziba sikio lake kusikia maneno yake.
Akiwa ofisini, Alvin alimpigia simu Lisa ghafla. "Nimesikia ulienda kwenye mgahawa na mwanaume mwingine, kwanini hukunijulisha?"
"Pfff!" Lisa alitema kahawa kinywani mwake akiwa amekasirika. "Ni Shani ndiye aliyekuwambia?"
“Si yeye.” Alvin alikanusha. “Wewe ni mke wangu, na cheo hicho kinakufanya karibu kuwa mtu maarufu. Mapaparazi wanakutazama kila mahali lakini nilifanikiwa kudhibiti kabla picha hazijavuja.” Alvin alisikika akigonga vidole vyake kwenye meza iliyokuwa upande wa pili wa simu. “Unamfahamu vipi? Hata miguu yangu inaonekana bora kuliko uso wake mbaya."
Lisa akajibu kwa hasira kidogo. “Ni mpenzi wa zamani wa Pamela. Anataka kujua alipo Pamela lakini sikumwambia chochote.”
"Mhm, usitoke tena na wanaume wasiojulikana, watakupotezea heshima." Alvin alimuonya.
“Si upo bize na uzinduzi wa Cement ijumaa? Hakika unaonekana kama una muda mwingi wa bure mkononi." Lisa alichanganyikiwa baada ya kusikia sauti yake ya kibabe.
"Ninafanya kazi lakini pia nahitaji kumtazama mke wangu kwa ukaribu zaidi," Alvin alijibu kwa uthabiti, "Wanaume wengi hapa mjini wanavutiwa na wanawake walioolewa siku hizi."
“Unawaza mambo kupita kiasi. Hakuna mtu atakayevutiwa na sura yangu ya kutisha."
“Sijui unamaanisha nini. Wewe ni mrembo kabisa machoni pangu.”
Lisa hakuweza kuvumilia maneno hayo ya huba ambayo hakuyatarajia, na moyo wake ulidunda bila mpangilio. "Kwa nini umekuwa ukiniambia maneno mengi ya asali hivi karibuni?"
“Nitayafanya masikio yako yasikie maneno matamu zaidi nikipata kula nyama ya nguruwe iliyochomwa utakayotengeneza.” Kicheko cha upole cha Alvin kilisikika kuvutia zaidi ya muziki kutoka kwa kinanda.
Maneno hayo ya mahaba yaliuosha na kuusafisha kabisa moyo wa Lisa. “Sawa, lakini unamjua mwanamume yeyote mzuri unayeweza kumpendekeza kwa Pamela? Anahitaji uhusiano mpya ili kusahau kuhusu mpenzi wake wa zamani...”
“Hapana…” Alvin alijibu baada ya kutafakari kwa ufupi. "Rodney ni mkali, Chester si mwaminifu, na tabia ya Sam haina shaka."
“Kwa hiyo wewe huna marafiki wazuri?” Lisa alijiwazia. Hata hivyo, ilimbidi akubaliane na maoni yake kuhusu Rodney na Chester. Wasingemfaa Pamela. "Nafikiri Sam Harrison si mbaya," alisema, "Yeye ni mwadilifu, mpole, mcheshi, mwonekano mzuri..."
"Sikujua kuwa unamfikiria sana." Alvin alitabasamu kiwivu-wivu. “Vipi kuhusu mimi?”
"Tunazungumza juu yako tukiwa chumbani ..." Lisa alifunika kiganja chake kwenye uso wake kwa aibu.
"Niambie sasa hivi." Sauti ya Alvin ilisisitiza maamuzi.
Lisa alifikiri juu ya hilo kwa uzito kwa muda mfupi na kusema. “Um, wewe ni handsome, genius… una moyo mzuri… tajiri… unafaa…”
Lisa hakuweza kufikiria kitu kingine chochote. Kwa upande mwingine, angeweza kuandika orodha ndefu ikiwa Alvin angemuuliza kuhusu sifa zake mbaya.
“Hata wageni wangeweza kusema mambo hayo. Unaweza kusema kitu kingine cha kipekee?" Alvin aicheka kwa mbwembwe. “Lisa, hatimaye najua ni uwongo kiasi gani ulioniambia ulipokuwa unajaribu kunitongoza huko Dar es Salaam. Hakika nimekatishwa tamaa na wewe. Hujawahi kunijali jinsi ninaivyokujali.” Alikata simu ghafla baada ya hapo.
Baada ya kutoka kazini, Lisa aliendesha gari lake kuelekea kwenye duka la nyama na kununua nyama ya nguruwe. Alifungua redio wakati akiendesha gari.
Kipande cha habari kilichomvutia kilisikika baada ya dakika kama kumi hivi nbaada ya kuwasha redio. “Tunakuletea habari zilizotufikia hivi punde. Mkurugenzi wa Ngosha Corporation, Joel Ngosha, amepata ajali baada ya gari lake kugongana na lori nusu saa iliyopita. Dereva huyo alifariki dunia eneo la tukio huku Joel Ngosha akipelekwa hospitali kwa matibabu ya dharura, lakini hali yake bado haijafahamika. Kulingana na baadhi ya habari kutoka eneo la tukio, hali ilikuwa yake ilikuwa ya kutatanisha sana…”
Maneno yaliyokuja baadaye yalipenya masikioni mwa Lisa kwa ukungu. Alikuwa katika mshtuko. Ingawa muda aliokaa na Joel ulikuwa mfupi, bado alikuwa familia yake pekee iliyobaki. Alikuwa amepata ajali? Aligeuza gari kwa haraka na kukimbilia hospitali.
Korido ya chumba cha dharura ilikuwa imejaa watu wa familia ya Ngosha.
Nina, ambaye alikuwa akipiga kelele, alipomwona Lisa, alimshtaki kwa hasira na kumpiga. “Wewe ni jini! Joel almepata ajali mara tu ulipokuja kwenye familia yetu. Yote ni kwa sababu ya mikosi yako."
Lisa aliupiga mkono wake kwa hasira. Alimkaripia kwa macho yaliyojaa damu, “Baba yangu yuko ndani, na bado haijulikani ikiwa ataishi au atakufa. Badala ya kuwa na wasiwasi juu ya mumeo, wewe, kama mke wake, unapandisha hasira yako juu yangu kwa makusudi. Unawazimu?"
“Nani kasema nakutolea hasira zangu? Bila shaka ni kosa lako.” Nina alilegea kwa sekunde moja chini ya macho makali ya Lisa. “Ni kweli, nina wasiwasi na Joel. Nina wasiwasi naye kuliko mtu mwingine yeyote.”
“Basi ushikilie hasira yako. Kila mtu ana wakati mgumu, kwa hivyo acha ugomvi. Hatimaye nilimpata baba yangu na tuliungana tena kwa muda mfupi tu. Sitaki kumpoteza.”
Lisa alijaa maombi na uchungu. Jinsi alivyomtazama Nina ni kana kwamba alikuwa mtu asiye na akili, na hilo lilimfanya Nina kuwa na hasira.
“Unamaanisha nini kusema hivyo? Ilikuwa ni wewe—”
“Inatosha, funga mdomo wako.” Bibi Ngosha aliingiwa na majonzi, lakini baada ya kusikia maneno ya uchungu ya Lisa, alifikiri pia tabia ya Nina haikubaliki. “Lisa yuko sawa. Joel bado anapambania maisha yke huko ndani. Huwezi kuwa mtulivu?”
Nina aliona aibu kwa kuambiwa hivyo. Alifunika tu uso wake kwa mikono yake na kuanza kupiga kelele kwenye korido.
Saa moja baadaye. Daktari alitoka nje na kusema kwa masikitiko, “Samahani. Tumefanikiwa kuokoa maisha ya Bwana Ngosha kwa sasa, lakini kuna uwezekano mkubwa atashindwa kuamka.”
Nina alikuwa na wasiwasi. "Unamaanisha kuwa atakuwa katika hali ya kupooza?"
“Ndiyo.” Daktari aliitikia kwa kichwa. "Lakini bado kuna matumaini. Wagonjwa wengine huamka hata baada ya kukaa kitandani kwa miaka michache au zaidi ya miaka kumi.”
“Loo, maskini Joel wangu!” Bibi Ngosha alilia kwa huzuni. “Hii imetokeaje? Mbona alikuwa sawa tu, Alipataje ajali?”
“Bibi, usiwe na huzuni. Ninaamini Baba hakika ataamka.” Melanie naye alilia. Ijapokuwa Joel alikuwa na upendeleo kwa Lisa siku za karibuni, angalau huko nyuma alimjali sana.
“Usilie mwanangu, nitafanya kila liwezekanalo ili baba yako aamke.” Nina alilia huku akifikicha macho yake. “Mama, baba, msijali. Nitamtunza Joel vizuri.”
Mzee Ngosha aliitikia kwa huzuni. Alipokuwa karibu kuzungumza, Lisa alisema kwa sauti ya chini, “Babu, ningependa kumtunza Baba mimi mwenyewe. Kwanza, muda niliokaa na Baba ulikuwa mfupi sana. Ninataka kutimiza wajibu wangu kama binti yake. Haijalishi hata kama upo katika hali ya kupooza. Angalau naweza kuutazama uso wake zaidi.”
“Asante mjukuu wangu…” Bibi Ngosha aliguswa.
“Pili, Alvin ana uhusiano wa karibu na Dokta Choka. Ujuzi wa matibabu wa Dokta Choka ni wa kipekee. Hospitali kuu za binafsi nchini Kenya zinamilikiwa zaidi na Dokta Choka pia. Hata kama Dokta hawezi kuwa na msaada wowote, Alvin ana uhusiano mpana, kwa hivyo labda anaweza kupata madaktari mashuhuri kutoka ng'ambo…”.....ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.
