JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................216-217
Sura ya: 216
Mkurugenzi Majuto na Bwana Thompson walihisi magoti yao yakigongana walipokumbuka kwamba wote wawili walikuwa wamemfedhehesha Alvin hapo awali. Hakukuwa na maana ya wao kulia juu ya maziwa yaliyomwagika sasa.
“Bwana Mkubwa… Bwana Kimaro, nilikosea kwa kutoona mbali. Kwanini usivunje tu mkono wangu?” Mkurugenzi Majuto alikuwa kwenye hatihati ya kulia sasa. "Au labda ungependa kunipiga kofi usoni?"
Alvin alinyoosha mkono kulibana shavu lililokuwa na mafuta ya mwanaume huyo. "Ulionekana kuwa na kiburi hapo awali, huh? Ulisema mke wangu alikugusa?"
"Bwana kimaro, samahani sana." Mtu huyo alipiga magoti chini.
"Nenda kumsihi Jack badala yake. Angalia kama anaweza kutengeneza Cement ya teknolojia mpya ndani ya wiki moja ili kukusaidia. Hakuna mtu anayekwenda na wakati ambaye atataka jengo lake litengenezwe na simenti ya teknolojia ya zamani.” Alvin aligeuza midomo yake kwa tabasamu kabla ya kutembea akiwa ameshikana mkono na Lisa kuelekea mlangoni. Kwa wakati huo, hakuna mtu aliyethubutu kuwazuia. Hata Jerome na Melanie hawakutulia na walikuwa na wasiwasi.
Alipokaribia tu kuufikia mlango, ghafla aligeuka na kuutazama umati huo kwa ujeuri kabla ya kumwambia Jerome. "Bwana Campos, nitakumbuka kila wakati tukio hili ulilonipangia."
Midomo ya Jerome ilitetemeka. Matokeo yalikuwa nje ya matarajio yake.
“Mbali na hilo, hakuna mtu anayeruhusiwa kumdhalilisha mke wangu, Lisa Jones. Yeyote anayethubutu kusema kwamba yeye si mrembo ananiudhi waziwazi.” Kisha, akaweka mkono wake kiunoni mwa mkewe na kuondoka eneo hilo kwa madaha.
Melanie nusura apoteze akili alipotazama umbile la mwanamume huyo lililokuwa likipungua taratibu machoni mwake. Alikuwa amemchagua Jerome tu kwa sababu alifikiri Alvin asingepanda tena juu ya ngazi. Bila kutarajia, utukufu bado ulikuwa uking'aa sana kwa Alvin. Mbali na hilo, bila kuzuiliwa na KIM International, bila shaka angepanua himaya yake zaidi.
“Babu… Babu, kuna nini…” Mtu mmoja ghafla alipiga kelele nyuma. Sherehe ya uchumba iligeuka kuwa machafuko tu.
Mzee Kimaro alihisi moyo wake ukikaza kwa sababu ya hasira kali. Wanafamilia ya Kimaro mara moja walimpeleka mzee huyo kwenye chumba cha mapumziko.
"Jack, njoo hapa." Mzee Kimaro alimuashiria mjukuu wake mdogo.
“Babu…” Jack akasogea mbele, akihisi kukosa raha.
Mzee Kimaro alishika fimbo yake na kuitupa kwenye chumba kwenye mabega ya kijana huyo. "Kwanini hukutuambia kuhusu timu ya Simon kuacha kazi kwenye kampuni?"
“Baba tulia. Alvin hana lolote.” Mara Lea akasogea mbele kumkinga mwanae.
"Ulijua kuhusu hili kabla ya leo?" Mzee Kimaro alikohoa. "Ni wazi, Alvin amepanga hili kama mpango mbadala. Nisingekuwa na ugomvi naye kama ningejua mapema.”
“Baba, huoni? Alvin ana matamanio makubwa na anapanga kuchukua udhibiti kamili juu ya KIM International,” Valeria alisema kwa wasiwasi, “Anataka mamlaka uliyonayo mikononi mwako. Nini kitatupata ikiwa familia itakuwa chini ya udhibiti wake?”
Bibi Kimaro akadakia. "KIM International itafanya nini mara tu Alvinarah itakapofanya mkutano wa kuzindua simenti yao ya teknolojia mpya wiki ijayo? Jack, unaweza kupata timu nyingine ya kufanya kazi kwenye mradi wa Cement? Hata hivyo, Alvinarah labda atakuwa ametoa toleo la pili la Cement wakati tutakapofaulu.”
Jack alikunja mikono yake kuwa ngumi. Sura ya aibu ilitanda usoni mwake lakini hakuna neno lililotoka kinywani mwake.
Mzee Kimaro alitingisha kichwa chake katika hali ya kukata tamaa mbele yake. Alvin alidharauliwa, lakini aliweza kujua ni yupi kati ya wajukuu zake alikuwa na uwezo wa kweli.
Macho ya Valeria yalitiririka kwa uzuri. "Baba, tunaweza kumtaka Alvin kukabidhi data za mradi Cement au tutatangaza ugonjwa wake wa akili na kuonyesha jinsi ambavyo alijaribu kumuua mtu. Hakuna mtu ambaye angethubutu kushirikiana na mfanyabiashara mwenye ugonjwa wa akili.”
“Unawezaje kusema hivyo?” Bibi Kimaro alipaza sauti, "Yeye bado ni mpwa wako!"
"Mama, karibu aniharibu sura, umesahau? Hata mara moja hajanichukulia kama mam’dogo wake.” Alikoroma kabla ya kumgeukia dada yake. “Lea, una maoni gani kuhusu wazo langu? Kwa kuwa anamjali sana Lisa, tutamjulisha kuhusu ugonjwa wake na nina uhakika hatathubutu kuwa naye tena baada ya hapo.”
Hisia ngumu iliyotokea katika moyo wa Lea. Ingawa alikuwa amemtisha Alvin kuhusu hilo hapo awali, bado hakuwa tayari kuafiki. Aligeuka kutazama upande mwingine. "Alvin ni damu ya familia ya Kimaro, baada ya yote. Hatuwezi kuvuka mstari. Isitoshe, sote tunawajibika kwa ugonjwa wake.”
“Anataka kuangusha biashara ya familia tuliyoijenga kwa miaka mingi halafu bado mnamkingia kifua?—” Valerie alipiga kelele, akionekana kukasirika.
“Nyamaza!” Mzee Kimaro hatimaye akaruka kwa hasira. “Wazo gani la kijinga kama hilo? Rudini ofisini mara moja mkajadiliane kupata suluhu.” Mzee Kimaro alishusha pumzi ndefu baada ya wengine kuondoka.
Bibi Kimaro akammiminia glasi ya maji. "Kweli, katika umri huu, unaweza pia kuachia nguvu zote? Kusema kweli, hakuna hata mmoja wa wajukuu zetu aliye na uwezo zaidi kuliko Alvin. Haifai kupoteza cheo chetu kama familia tajiri zaidi kwa hili.”
"Inanikera sana kwamba kijana huyo ni muasi sasa." Mzee Kimaro akapiga kifua chake kizito. “Lakini hana huruma, hilo ni la uhakika. Hakuna mtu mwingine katika familia anayeweza kulinganishwa naye. Lea ana uwezo lakini yeye si kitu ukilinganisha na Alvin.”
"Anapaswa kuwa mkatili ili kudumisha nafasi yake katika familia tajiri zaidi nchini.” Bibi Kimaro alimkumbusha.
•••
Sehemu ya maegesho ya hoteli.
Baada ya kuingia ndani ya gari, Lisa alishindwa kujizuia kumuangalia Alvin aliyekuwa amekaa karibu yake huku akifunga mkanda wa usalama. Kiti cha dereva cha hali ya juu kilifunika umbo lake dhabiti. Ilibidi akubali kwamba mwanamume huyo alikuwa anavutia sana, hasa jinsi alivyozungumza kwenye sherehe ya uchumba mapema… Ilipendeza sana!
Aliuona uso huu kila siku lakini uzuri wake usio na kifani bado ulimfanya moyo wake kwenda mbio.
“Niangalie unavyotaka. Hakuna ubaya kuthamini sura nzuri ya mumeo. Sitasema lolote.” Alvin akageuka pembeni na kumshika macho yake ya wizi kwa mara nyingine tena.
Lisa akatabasamu kwa aibu. “Sikuwa nakutazama. Nilikuwa nikinyoosha shingo yangu tu. Inahisi kuwa ngumu zaidi." Alichungulia dirishani baada ya kusema hivyo.
Alvin alikibana kiganja chake kwa kukichezea huku kicheko cha furaha kikitoka kinywani mwake. "Au ulirogwa na haiba ya mumeo sasa hivi?"
“Si kweli, ila umemchanganya kila mtu…” Kabla sauti yake haijakatika, alimshika kidevu na kufunga kinywa chake kwa midomo yake.
Lisa akapepesa macho. Alitaka kumsukumia Alvin pembeni lakini alipokumbuka namna alivyomkosha kwenye sherehe hiyo hakika nguvu zilimuishia. Lisa hakuweza kujizuia katika hilo. Hakutaka kujisalimisha, lakini hakuweza kumshinda tena na tena. Ilibidi akubali kwamba Alvin angeweza kumshinda mwanamke yoyote kwa urahisi kwa sababu alikuwa na haiba yenye nguvu sana.
Gari jeusi la kifahari lilipita taratibu na kulipita gari la kina Lisa. Kelvin, ambaye alikuwa ameketi kwenye kiti cha nyuma, aliona watu wawili walioketi ndani. Dirisha la gari la kina Alvin lilikuwa nusu limevingirishwa chini. Alvin alikuwa ameegemea kiti cha abiria huku Lisa akiwa amezungusha mikono yake yote shingoni. Walionekana wamezama sana katika busu hilo kiasi kwamba hawakujua kilichokuwa kikiendelea karibu nao.
Kelvin alikunja ngumi pamoja. Nia ya hatari ikamjaa machoni. 'Lisa Jones, hivi ndivyo ulimaanisha uliposema huna chaguo ila kurudi kwa Alvin?' Kelvin hakuweza kuvumilia alipojiwazia hayo. Hakuwahi hata kupewa busu lolote na Lisa, achilia mbali busu la midomo kama jinsi alivyokuwa akifurahia tendo hilo la karibu na Alvin. Kwa kifupi, alihisi kudanganywa na Lisa. Hakukusudia kumwacha Alvin! Ikiwa ndivyo ilivyokuwa, kwa nini alimpa tumaini tangu mwanzo? Moyo wa Kelvin ulijaa chuki!
Taratibu akainua dirisha na kufumba macho, akamwambia dereva wake. “Twende zetu.”
Sura ya: 217
Hatimaye, Alvin akajiondoa kwenye midomo ya Lisa bila kupenda. Kwa aibu, aliinua macho yake na kushangaa kuona kwamba dirisha lilikuwa limefunguliwa nusu. “Nafikiri… nilisikia gari likipita mapema…”
Lisa alihisi kutaka kujiua sekunde hiyo hiyo. Inawezekana kuna mtu yeyote aliyewaona mapema?
“Hmm.” Macho ya Alvin yalimetameta kabla hajatoa tabasamu. "Hakuna kitu kibaya kuhusu mume na mke kubusiana." Aliuma mdomo. “Hii haina uhusiano wowote na kuolewa au la. Mimi sina aibu kama wewe,” alimwambia.
“Muda ule… Kwanini ulinishika mkono?” Alvin akamtazama kwa makini.
Aibu ilibadilisha hali ya kuchanganyikiwa usoni mwake sekunde chache baadaye.
“Sijui unamaanisha nini.” Lisa alitazama upande.
"Namaanisha wakati familia yangu ilipomuunga mkono Mkurugenzi Majuto kuvunja mkono wangu, kwanini ulishika mkono?" Akainama mbele kumcheki masikioni. "Ulijisikia vibaya juu yangu?"
'Sikuwa na wazo lolote. Acha kujifikiria sana.” Akiwa amechanganyikiwa, alibadili mada ya mazungumzo ghafla. "Bado utashirikiana na Mkurugenzi Majuto na wengine?"
“Hapana.”
"Lakini wanaongoza makampuni makubwa katika nchi hii..."
"Teknolojia ya hali ya juu inakua haraka kwa wakati huu. Biashara haiwezi kuendelea kwa kutegemea bidhaa zilizotengenezwa kwa teknolojia ya zamani,” Alvin alieleza kwa kumaanisha. “Nimejifunza kitu kutokana na tukio hili. Ninapanga kusaidia kampuni mpya kukua kwa kuwekeza kwao kama mmiliki wa hisa. Ni wakati wa makampuni ya kizamani ambayo yanayojiendesha kimazoea kwa kuchukua fursa ya mazingira yanayowazunguka kuachia ngazi.”
Lisa alielewa karibu mara moja. “Unataka kujenga himaya ya biashara ambayo ni yako peke yako, ambapo umesimama juu ya uongozi?”
“Unaweza kuiweka hivyo. Sitaki kuendelea kufanya biashara ili kumfurahisha mtu mwingine.” Macho yake yalidhihirisha dhamira huku sauti yake ikiakisi ubabe.
Lisa akavuta pumzi kwa kasi. Tamaa ya Alvin ilikuwa mbaya kuliko alivyofikiria. Ilionekana kana kwamba alikuwa anaenda kubadilisha jiji la Nairobi.
Hata hivyo… angeweza kweli kumudu mwanaume kama Alvin? Bila shaka, wanawake wengi zaidi wangekuwa wakijitupa mikononi mwake dakika ambayo angerudisha nafsi yake nyuma. Je, bado angeweza kulinda hadhi yake kama Bibi Kimaro katika siku zijazo?
•••
Siku mbili baadaye. Pambano kubwa lilikuwa likiendelea katika familia ya Ngosha.
“Joel, nitakufa kabla ya kunitaliki,” Nina alifoka kwa hasira.
“Acha kunitisha. Nitakutaliki hata ukifa.” Sauti ya Joel ilidhihirisha azimio lake lisiloyumbayumba. “Wewe ni msaliti. Ungewezaje kumshawishi Valeria aharibu sura ya Lisa? Bila kusahau jinsi ulivyomshawishi Mkurugenzi Majuto kumnyanyasa Lisa kwenye sherehe ya uchumba! Usifikiri kuwa sijui chochote.”
"Lazima ni Lisa amekujaza maneno ya uwongo tena, huh? Unaamini kila kitu anachosema kwa sababu tu ni binti wa Sheryl. Unamjali huyo mwanamke tu!” Nina aling’aka.
“Ni kweli, Sheryl ndiye mwanamke pekee ambaye nimempenda katika maisha yangu yote. Majuto yangu makubwa ni kuoa mwanamke mwenye roho mbaya kama wewe.” Joel alikuwa amechachamaa. "Una siku tatu za kusaini karatasi. Vinginevyo nitakwenda mahakamani kukata rufaa ya talaka.” Joel akasimama na kuondoka chumbani.
“Joel, mwana haramu wewe!” Nina alipiga magoti chini na kuanza kulia kwa sauti.
Simu ya Nina ilianza kuita muda si mrefu. Aliona jina la mpigaji na kupiga kelele kwenye simu, "Unataka nini sasa?"
"Joel Ngosha amezungumza na wakili kuhusu mgawanyo wa hisa zake. Lisa anapata 35% huku Melanie akipata 5%.”
"Nini?" Nina alikuwa karibu kupoteza akili. “Anamjali sana binti huyo wa nje ya ndoa halafu anataka kunitaliki mimi? Joel ni mkatili. Hakumbuki kama nilitumia miaka 20 iliyopita kujenga familia pamoja naye!”
"Kwa kweli ameamua wakati huu. Matokeo yatakuwa mabaya ikiwa makubaliano haya yatahalalishwa."
“Tufanyeje sasa?” Nina likuwa amechanganyikiwa kweli.
"Chaguo pekee tulilo nalo kwa sasa ni kumfanya Joel Ngosha afariki."
Hilo lilimshangaza Nina. “Itawezekanaje…”
"Fikiria kile alichokufanyia wewe na binti yako."
“Lakini…”
“Usijali, nitashughulikia hili. Unakumbuka jinsi Sheryl alivyokufa?"
“Sawa.” Macho ya Nina yalimtoka kwa hasira. "Hawezi kunilaumu kwa kuwa mkatili ikiwa yeye pia hana huruma."
“Sawa.”
•••
Asubuhi, Lisa alikuwa akienda kazini baada ya kifungua kinywa. Mara tu alipotoka nje ya mlango, alimwona Alvin akimfuata. Alvin alikuwa amevalia nguo zake za mapumziko na mikono yote miwili mfukoni mwake kama kawaida.
“Mbona bado unanifuata? Huendi kazini leo?” Lisa alimuuliza kwa mshangao.
Alvin akamjibu, “nitakupeleka ofisini kwako." Moyo wa Lisa ulirukaruka baada ya kusikia sauti yake ya chini iliyojaa mahaba.
Alvin aliongozana naye hadi kwenye gari na kumwendesha hadi katikati ya jiji kwenye jengo ambalo Mawezi Investments ilikuwa imepanga ofisi zake.
Lifti ya private iliyokuwa inaelekea kwenye ghorofa za juu ilikuwa chini ya uchunguzi wa usalama siku hiyo, kwa hivyo iliwabidi kutumia lifti ya umma.
Ulikuwa ni muda wa asubuhi na watu walikuwa na haraka sana kuwahi makazini, hivyo kulikuwa na harakati nyingi ndani ya lifti. Mabinti na vijana ndiyo walikuwa wengi. Lisa aligundua kuwa karibu kila binti aliyeingia kwenye lifti angeibia macho kumtazama Alvin aliyesimama karibu naye. Baadhi ya wale wenye ujasiri hata waliegemea kwa Alvin kwa hila wakati watu walipobanana kwenye nafasi ndogo ya lifti.
"Mke, mikono yangu ni ya baridi." Ghafla Alvin alimkumbatia Lisa kwa nyuma na kuweka mikono yake mbele ya kifua chake. Mwonekano huo wa kimapenzi usoni mwake uliwafanya wanawake wengine wote kuyeyuka kwa wivu.
Hata hivyo, walishangaa wakati huo huo. Ilikuwa ngumu kuamini jinsi mwanamke aliyeharibika sura anavyoweza kuwa na mwanamume mwenye sura nzuri kama huyo.
Hatimaye wapendanao hao waliiacha lifti ilipofika ghorofa waliyokuwa wakienda. Waliwaacha mabinti ndani ya lifti kwenye mjadala mkali baada ya kupiga hatua chache, baadhi ya maneno yao waliweza kuyanasa kwa mbali kabla lifti haijaondoka.
“Unamfahamu huyu mkaka? Jamani huyu kaka anajua kupenda nyie acheni! Alikodisha kipindi kizima cha TV ili tu kumtetea mke wake. Nilisikia kwamba ni tajiri mkubwa Nairobi nzima. Na hata mke wake usimuone hivyo, ni bosy lady na pesa zake za kutosha…”
Uso wa Alvin ukaanguka papo hapo. Kwa upande mwingine, Lisa alicheka bila hiari. "Mvulana wangu mzuri, unaweza kurudi nyumbani sasa. Jisikie huru tu.”
Hasira iliyokuwa ndani yake ilimwacha baada ya kuona tabasamu lile la furaha. Midomo yake ikaachia tabasamu. "Msichana wangu sukari, nipe busu na nitarudi nyumbani." Kisha, akainua midomo yake maridadi.
Lisa aliona haiaminiki kushuhudia haya. Ni nini kilimtokea Alvin yule mwenye kiburi na jeuri?
Alvin aliondoka na Lisa akaingia ofisini kuendelea na kazi. Aliporudi nyumbani baada ya kazi, alikutana na suprise nyingine kutoka kwa Alvin
“Mpenzi wangu sukari, nina zawadi kwa ajili yako.” Alvin akazungusha kichwa chake na kuashiria kulia.
Lisa alitazama upande ule na kugundua gari jeupe ‘sports car’ jipya kabisa limeegeshwa pembeni. Ilikuwa na muundo mzuri wa nje.
Hakuwahi kuona aina hiyo ya gari huko Kenya hapo awali lakini alikuwa ameona kitu kama hicho alipokuwa akisoma nje ya nchi. Kulingana na utafiti wake, gari la bei rahisi zaidi kutoka kwa brand hiyo lingegharimu angalau shilingi za Kitanzania milioni 250. Mbali na hilo, plate namba ya gari hilo ilikuwa ‘4EVA.’ Yaani ‘Daima na Milele.’
Lisa aliona aibu lakini alifurahi kwa siri kuona sahani ya gari aliyotengenezewa na Alvin. Hakuwa amewahi kufikiria kuwa Alvin alikuwa mwanamume romantiki kiasi hicho hapo awali, lakini kwa hakika alikuwa na mbinu kadhaa ambazo tayari zilikuwa zikiubomoa kabisa moyo wa Lisa na kumfanya awe nyang’anyang’a kwake!......ITAENDELEA.....
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.
