JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................212-213
Sura ya: 212
Hotel Pavilion Intercontinental. Mombasa!
Hoteli hii ya nyota tano karibu na bahari ilijengwa katika miaka ya hivi karibuni huko Mombasa. Ilikuwa na ufukwe wa kibinafsi na mikahawa saba ambayo ilihudumia vyakula vya kila aina kutoka kote ulimwenguni. Watu wengi matajiri na watu mashuhuri walipenda kufanya harusi zao za kifahari katika eneo hilo maarufu.
Sherehe ya uchumba ilifanyika kwenye ufukwe wa kibinafsi wenye bustani ya kifahari. Melanie alikuwa akifurahia pongezi kutoka kwa wageni wake.
"Jerome ni mkarimu sana hata amekutengea hoteli nzima," Aunty Irene alisema huku akitabasamu.
“Hiyo ni kweli, Melanie. Nina wivu sana,” Yvonne Ngosha, binamu wa Melanie, aliunga mkono.
“Nyie wawili mnatia chumvi. Ama kwa hakika, Jerome ndiye mwekezaji mkubwa wa hoteli hii la sivyo isingekuwa rahisi sana kwake kuhifadhi eneo lote hili,” Melanie alijigamba kana kwamba anazungumzia Jumba la White House.
“Oh, kwa hiyo hoteli hii ni mali ya Jerome! Nilisikia kwamba mauzo ya hoteli hii kwa mwaka ni sawa na mauzo ya hoteli tatu bora nchini Kenya. Hiyo inavutia.”
"Hiyo ni sawa." Melanie alielekeza macho yake kwa Jerome ambaye alikuwa amezungukwa na umati wa watu. Mwanaume huyo alipendeza sana, ingawa hakuwa mtanashati sana wala hakuwa sawa na Alvin Kimaro. Mbali na hilo, mustakabali wake ulikuwa umejaa fursa na uwezo.
Kila mtu kutoka familia ya Kimaro alikuwepo siku hiyo, bila kusahau majina mengine makubwa yenye ushawishi katika uwanja ya siasa na biashara.
Alijiona kuwa anajulikana kwa kuwa na wageni kama hao kwenye sherehe ya uchumba wake. Hiyo ndio harusi ambayo alikuwa akiiota. Alimini Alvin angejutia chaguo lake baada ya kufika pale baadaye. Lilikuwa kosa lake kukataa kumuoa. Kwa kuongezea, Lisa pia angekuwepo. Kwa kufikiria hivyo, Melanie alihisi huyo mwanamke aliyeharibika sura lazima angemuonea wivu sana.
“Tazama, Bwana Kimaro anaingia! Ameongozana na Lisa Jones.”
Aunty Irene alipiga kelele ghafla.
Kila mtu aliyekuwepo kwenye ufukwe wa hoteli hiyo aligeuza kichwa chake kwenye lango kuu. Alvin aliingia huku akiwa amevalia suti nyeupe. Ni mara chache sana alionekana katika hafla za umma akiwa amevaa nguo nyeupe lakini kwa wakati huo, alifanana na Prince Charming kutoka kwenye zile muvi za katuni za Disney. Wageni wengine wa kiume waliokuwepo hawakuweza kufananishwa naye.
Kando na hilo, Jerome, bwana harusi mtarajiwa pia alikuwa amevalia suti nyeupe siku hiyo. Alionekana wa wastani sana ukilinganisha na mwonekano wa kupendeza wa Alvin. Kwa hasira, Jerome akaivunja glasi ya mvinyo mkononi mwake baada ya kumuona Alvin amempiku kwa mvuto.
Kwa upande mwingine, Melanie pia alikuwa ameshindwa kuzuia hisia zake za wivu. Hii ilikuwa ni kwa sababu aliona gauni la jioni la rangi ya samawati ambalo Lisa alikuwa amevaa wakati huo, likiwa kali kuliko lake. Alikuwa akitaka kuvaa kipande hicho cha kazi ya ustadi kutoka kwa mbunifu mtaalamu Bonny King kwa sherehe yake ya uchumba lakini alishindwa kupata walau mkono wake tu licha ya kutoa pesa nyingi. Hata hivyo, Lisa sasa alijitokeza kwenye sherehe hiyo akiwa amevalia mavazi hayo!
Yvonne alifunika mdomo wake kwa mshangao kabla ya kunong'ona, "Hilo ndilo gauni lako la jioni uliloshindwa kulipata kutoka kwa Bonny King?..."
Melanie alimtazama kwa jicho la kumtoboa mara moja.
“Ni sawa. Uso wa Lisa ni wa kutisha hata hivyo. Ni sawa na bure tu hata kama gauni hilo la jioni lilianguka mikononi mwake,” Yvonne alisema sekunde chache baadaye.
“Uko sawa.” Zamani, Melanie alikuwa akimwonea wivu Lisa kwa kuwa mrembo kuliko yeye, na sasa alikuwa na furaha zaidi kuhusu ulemavu wa uso wake uliomfanya aonekane kama kinyago.
Baada ya kufurahi kidogo, Melanie alitembea kuelekea kwa wanandoa hao wapya waliowasili akiwa na Jerome. “Bwana Kimaro, uwepo wako kwenye sherehe ya uchumba wangu unaleta mwanga wa unyenyekevu katika sherehe yetu ya leo.” Jerome akasogea mbele huku akitabasamu. Licha ya salamu hiyo ya heshima, hakutoa mkono wake kwa Alvin.
Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Lisa kukutana na Jerome. Kusema kweli, mwanamume huyo alikuwa mzuri na pengine alisimama kwa urefu wa futi 5'7. Hata hivyo, alionekana mlegevu alipotabasamu. Hakuonyesha umaridadi wa heshima kama Alvin alivyofanya.
Bwana Thompson, rafiki wa Jerome ambaye alikuwa amesimama karibu, alicheka kufuatia maneno ya Jerome. "Ameleta nuru ya unyenyekevu kwenye sherehe yako? Bwana Campos, una mustakabali mzuri mbele yako. Bwana Jack Kimaro hata alitia saini mkataba mpya wa mkakati wa ushirikiano na kampuni yako baada ya kuchukua kiti cha uongozi wa biashara ya familia. Una uwezo mkubwa zaidi kuliko mtu fulani."
Melanie alikuwa juu ya mwezi baada ya kusikia hivyo. Aliunganisha mikono yake na ya Jerome kabla ya kuachia tabasamu la maana. “Bwana Thompson, hukupaswa kusema hivyo. Bwana Kimaro ndiye mfanyabiashara anayeheshimika zaidi jijini Nairobi, bila kusahau mtu tajiri zaidi nchini Kenya.
"Mtu tajiri zaidi?" Thompson alitoa mkoromo wa dharau. “Alifanikiwa kufanya hivyo kwa sababu ya msaada kutoka kwa familia ya Kimaro. Yeye si lolote sasa bila msaada wa familia yake.” Thompson alinyamaza kwa muda ili maneno yake yamwingie haswa Alvin kabla ya kumuuliza Mzee Kimaro aliyekuwa amesimama si mbali kutoka kwao, “ niko sawa, Mzee Kimaro?”
Mzee Kimaro alifoka huku akimtupia jicho la pembeni Alvin. "Ni aibu mtu mwenyewe haonekani kulitambua hilo."
Bwana Thompson hakujaribu hata kuficha dharau machoni mwake alipomtazama Alvin. “Bwana Kimaro, una bahati. Unatakiwa kufurahia karamu yako ya mwisho na watu wa hali ya juu usiku wa leo na mke wako. Labda hakuna mtu mwingine ambaye atakualika tena kwenye hafla za kipekee kama hizi katika siku zijazo.”
"Sawa, basi ninakushukuru Bwana Thompson kwa ushauri wako." Alvin alitabasamu kwa kushangaza. Hakuonekana kukasirika au kufadhaika bali alionekana zaidi kana kwamba alikuwa akitazama onyesho la vikaragosi la kipuuzi.
“Bwana Kimaro, tafadhali usifadhaike.” Melanie ghafla akatumia mkono kuziba mdomo wake kana kwamba ndo kwanza alikuwa anamwona Lisa. "Oh, nini kilitokea kwenye uso wako? Unatisha! Utadhani umeshushwa kutoka kuzimu?"
Kitu kama mwanga mkali wa moto kiliangaza machoni mwa Alvin. Alipasua midomo yake, akikusudia kulipiza kisasi lakini Lisa akaushika mkono wake na kutabasamu kwa utulivu. “Inatisha sana. Wakati mwingine, hata mimi hujichukia katikati ya usiku. Lakini kwa bahati nzuri, Alvin yupo karibu nami akinipa ujasiri ninaohitaji. Ananipenda, kunitia moyo, na kunijali. Hawapigi hata kope wanawake wengine wanaoendelea kujigongagonga kwake.”
Utulivu wa sauti yake ulifanya tusi la Melanie lionekane lisilo na maana.
Kinyume chake kabisa, maneno ya Lisa yalidokeza kwamba Melanie aliwahi kumsumbua Alvin lakini bado angependelea kuwa na mwanamke aliyeharibika sura kuliko yeye.
Melanie alikasirishwa na fedheha hiyo, lakini tabasamu la fumbo likaangaza usoni mwa Jerome. "Bi. Kimaro, wanaume huwa hawasemi ukweli. Baada ya yote, kile kilichotokea kwenye uso wako kinatia huruma sana."
Sura ya: 213
“Hiyo ni kweli, ninajisikia vibaya kwa ajili yako pia," Melanie aliunga mkono, "Mbali na hilo, wakati mwingine wanaume husema kile wanachosema kwa ajili ya heshima."
Lisa akajibu kwa kutabasamu. "Kwa kweli, ni muhimu kwa mwanamume kulinda sifa yake. Ah, Bwana Campos, nilipowasili Nairobi kwa mara ya kwanza na kusikia uvumi mbaya kuhusu wewe kujihusisha kimapenzi na mwanafunzi wa kike wa shule ya sekondari, nilifikiri kwamba msichana yeyote kutoka familia yenye hadhi asingetamani kuolewa na wewe. Kama ilivyotokea, nilikosea."
Baada ya kutulia kwa sekunde chache, Lisa alimwambia Melanie kwa uzito, “Dada yangu mdogo, kwa kuwa ni sherehe ya uchumba wako leo, ningependa kukupa neno la kweli la ushauri. Kila mwanamke atakuwa mzee au mbaya siku moja. Wanawake wazuri wapo kila mahali lakini uzuri wa ndani haufifii wala kuzeeka. Hii ndiyo siri ya kweli ya kudumisha ndoa yenye kudumu.”
“Uko sahihi mke wangu.” Alvin alisema kabla ya kugeuka kumwangalia Bwana Thompson. "Nadhani unaelewa hili vizuri. Baada ya yote, Bwana Thompson, wewe huwafuata wasichana wadogo wenye umri wa miaka 18. Nilisikia kwamba umejipatia kigori mwingine mdogo hivi majuzi. Bibi Thompson kwa kuwa anajijua kwamba yeye ni mzee, anafumbia macho yote hayo.”
Mara Lisa alijifanya kuwa na hasira na kumkodolea macho Jerome. “Bwana Campos, wewe ni rafiki mzuri wa Bwana Thompson lakini natumai hutafuata mtindo wake wa maisha. Hupaswi kumuumiza moyo dada yangu Melanie, sawa? ”
Uso wa Jerome ulikuwa umetanda kwa hasira baada ya kufedheheshwa hivyo kwenye sherehe yake ya uchumba. Melanie, ambaye alikuwa jeuri mapema, pia aliona aibu sasa. Hapo awali alifikiri kwamba Jerome alikuwa mwanamume mzuri lakini hakutarajia kusikia kuwa aliwahi kutoka kimapenzi na mwanafunzi mdogo wa shule ya sekondari, na pia rafiki yake mkubwa Bwana Thompson hakuwa mwaminifu pia. Mawazo hayo yalimtia kichefuchefu.
"Hapana. Tumeunganishwa na upendo wa mara ya kwanza kati yetu. Nitampenda na kumlinda Melanie milele.” Jerome alitabasamu kwa kujilazimisha.
“Vema, Bwana Campos, itakuwa vigumu sana kwako kujaribu kudumisha upendo huu wa upande mmoja. Mbaya zaidi unamuoa binti ambaye mawazo na mapenzi yake yote yapo kwa mwanaume mwingine, na wewe anakutumia tu kama kiboko cha kumchapia huyo mwanamume…” Lisa alifunika mdomo wake haraka kwa mkono wake. “Ah, jifanye hujasikia nilichokisema, samahani...”
"Lisa, unafanya hivi makusudi?" Melanie alikasirika. "Nilikuwa na uamuzi mbaya siku za nyuma. Jerome ni bora zaidi kuliko Alvin kwa kila njia.”
“Naelewa." Lisa aliitikia kwa kichwa. "Hasa kwa sababu sasa Jack amechukua biashara ya familia. Vinginevyo, sidhani kama ungemtazama Campos kwa mara ya pili.”
“Acha upuuzi…” Melanie alijuta kumualika Lisa baada ya kuona furaha ikitoweka taratibu kwenye ngozi ya Jerome. Alikuwa amefikiria kumwalika Lisa ili amdhihaki lakini hakika hakutarajia kama Lisa angekuwa na ulimi mkali namna hiyo. Angewezaje kuwa na kiburi hata akiwa na ulemavu wa uso?
“Ni sawa, Melanie. Twende zetu. Tuna wageni muhimu zaidi wa kuwasalimia. Watu wa hadhi za chini kama wao hawastahili wakati wetu mwingi.” Jerome hakuweza kuvumilia kuendelea kusikiliza kejeli za Lisa tena.
“Uko sawa.” Melanie aliunganisha mikono wake na Jerome na kuelekea kwa familia ya Kimaro. Hata hivyo, wawili hao walionekana kupooza sana baada ya yale waliyoyasikia.
Alipotazama maumbo yao yakitoweka, Alvin alibana ncha ya pua ya Lisa kwa kuichezeachezea. “Si mbaya hata kidogo. Uligundua hata maisha ya zamani ya Jerome kuwahi kutoka kimapenzi na mwanafunzi wa sekondari. Ulijuaje kuhusu hilo?”
“Pamela aliniambia. Amekuwa akifahamiana na mabinti na wanawake kadhaa wa jamii za kitajiri za hapa Nairobi na kusikia porojo nyingi kutoka kwao,” alijibu huku akitabasamu. "Na wewe umewezaje kujua kuhusu masuala ya mapenzi ya Bwana Thompson? Wewe si mtu wa kufuatilia mambo ya watu."
"Najua tabia za mabosi uchwara kama hao vizuri sana." Wawili hao walitembea kuelekea kwenye umati wa watu wakiwa wameshikana mikono.
Ingelikuwa ni zamani kabla hajavuliwa cheo cha uenyekiti, Alvin bila shaka angekuwa kazungukwa na kundi kubwa la watu ndani ya sekunde chache, lakini alichopokea siku hiyo ni dhihaka na dharau. Wengi wao hata walimsengenya Lisa hadharani.
“Usiichukulie hli personal. Hivi karibuni… watu hawa wote watakuja kujipendekeza kwako,” Alvin alinong’ona.
“Haijalishi hata hivyo. Ninachojali ni kuishi kwa amani na furaha na wewe tu basi.” Lisa alijibu na kumuona Joel akielekea kwake.
Joel alimtazama Lisa usoni kwa huruma. “Lisa, kwa nini hukuniambia kuhusu sura yako? Ni nini hasa kilitokea? Alvin Kimaro, ulijigamba kwa kusema unataka kumuoa binti yangu lakini hivi ndivyo unavyomlinda?”
Alvin alikunja uso huku akionekana kutofurahishwa. Joel aliendelea kupiga kelele kwa hasira, “Sikupaswa kusikiliza ahadi zako tamu. Ningejua ningeondoka naye tu…”
“Baba, Nina alihusika na ulemavu wangu wa sura,” Lisa alimkatiza. “Si muda mrefu uliopita, nilifungiwa na familia ya Kimaro kwenye shimo lao. Nina alishirikiana na Valerie na kuwaagiza wafanyakazi kuniwekea sumu kwenye uji wangu ili vidonda kwenye uso wangu vioze.”
"Nini?" Joel alishtuka. “Nitaenda kumtafuta huyu mwanamke kichaa…”
“Baba, wageni wengi wanaotambulika wako hapa kushuhudia sherehe ya uchumba kati ya akina Ngosha na familia ya Campos. Sio wakati wa kutengeneza tukio. Isitoshe Mzee Kimaro na wanafamilia yake wengine wapo pia. Nina hakika hawatakuelewa hata kidogo.” Lisa alijaribu kubadilisha mawazo yake.
Joel alikunja mikono yake kuwa ngumi na kuongea akiwa na hasira. “Lakini uso wako…”
“Ancle Joel, mambo mengine huchukua muda,” Alvin alisema kwa sauti ya chini, “Nitahakikisha wale waliomuumiza Lisa watalipa kwa matendo yao.”
Joel alihisi kutwishwa kitu kizito kifuani mwake. Alikuwa amefurahia umaarufu na mafanikio kwa sehemu kubwa ya maisha yake. Hata hivyo, alitambua kwamba alikuwa na deni kubwa sana kwaa binti yake huyo hivi kwamba asingeweza kumfidia kamwe. “Lisa, nimeamua kumtaliki Nina baada ya harusi ya Melanie. Sitabadili mawazo yangu hata kama kila mtu katika familia ya Ngosha angejaribu kunizuia.”
Lisa alimtazama baba yake kwa mshangao. Kusema kweli, alifikiri alikuwa mwenye moyo mpole sana kuelekea Nina na Melanie…
“Msiniangalie hivyo. Nasema ukweli.” joel aliwahakikishia. “Nina asilimia 40 ya hisa kwenye kampuni ya Ngosha Corporation. Nimeamua kukupa 35% na 5% iliyobaki kwa Melanie. Nitaiandika kwenye wosia mbele ya wakili haraka iwezekanavyo.”
“Baba…”
“Hilo linatosha. Keti tu na kupumzika huku utajiri ukianguka kwenye paja lako. Ninataka kuhakikisha kuwa unaweza kuishi bila wasiwasi kwa maisha yako yote. Kwa njia hiyo, unaweza kumudu kujinunulia kijana hata kama mumeo atakuzingua siku zijazo.” Alimtazama Alvin machoni baada ya kusema hivyo.
Lisa nusura apaliwe na mate. Hakutarajia baba yake angetamka maneno kama hayo waziwazi.
“Baba, sitamkatisha tamaa,” Alvin alijibu huku akitabasamu.
"Ha! Nitaaminije? Wanaume wamejaa uwongo." Sauti ya Joel ilisikika kwa kutoamini.
Alvin alishindwa cha kusema. Lisa alicheka bila ya kupenda. Ucheshi wa baba yake ulikuwa zaidi ya matarajio yake.
Nina, ambaye alikuwa akitazama kila kitu kwa mbali kidogo, aliuma meno yake kwa hasira. Joel alionekana kuwa na wakati mzuri na binti yake wa nje kwenye sherehe ya uchumba wa Melanie?
“Anti Nina, usijali. Nitawafundisha somo moja baadaye.” Jerome alifuata uelekeo wa macho yake huku kona za midomo yake zikibadilika na kuwa tabasamu baya. Kwa hakika aliapa kutowasamehe wawili hao kwa udhalilishaji wao hapo awali.
Nina alionekana kusitasita. “Lakini watu wengine wa familia ya Kimaro wako hapa pia…”
“Labda kuna kitu hujui. Familia nzima ya Kimaro haitaki kabisa kumsikia Alvin hivi sasa. Hakuna aliye na shauku zaidi yao kumuona Alvin akianguka.”
"Jerome, Melanie ndiye mwenye bahati ya kukupata." Nina alifurahi sana hakuweza kuacha kutabasamu.
Sherehe ilikuwa karibu kuanza. Msimamizi wa hoteli aliwaongoza Alvin na Lisa kwenye meza iliyokuwa mwisho wa ukumbi. "Samahani, hivi ni viti vyenu kwani ni watu mashuhuri tu ndio wanaoruhusiwa kwenye meza za mbele."
Nuru ilimulika machoni mwa Lisa alipotazama mbele ya ukumbi. Familia ya Kimaro na wengine walikuwa wamekaa kwenye meza ya katikati iliyokuwa mbele ya ukumbi. Valeria hata alikuwa akiwatazama kwa dharau walipopelekwa kwenye viti vya nyuma.....ITAENDELEA.....
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.
