JINA LA SIMULIZI............................LISA

AUTHOR...........................JOMBA WAJO

SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY

WHATSAPP..........................0628924768

SEHEMU YA................................208-209


Sura ya: 208


“Subiri…” Lisa alimvuta nyuma ghafla.


"Nini?" Hakuwa amechukua hatua ya kumzuia kwa muda mrefu. Uso mzuri wa Alvin ulichanua tabasamu la kejeli. “Huwezi kuvumilia kuniona nikiondoka?”


Lisa aliuma midomo yake na kuinua mkono wake wa kushoto, na kuona mkono wake umefungwa kwa bandeji. “Umejeruhiwa na nini?”


"Ni jeraha dogo tu." Sura isiyo ya kawaida iliangaza machoni mwa Alvin, na mara moja akatoa mkono wake.


“Umeumia vipi?” Lisa alimkazia macho. “Ikiwa ni jeraha dogo tu, kwa nini utetemeke kwa maumivu kwa kuguswa kidogo tu?”


“Una wasiwasi na mimi?” Alvin alikunja midomo yake kwa tabasamu. Sauti yake nzito ilijawa na furaha. "Moyo wako unaumia kwa ajili yangu?"


",.. Toka nje." Lisa alikasirika kutokana na aibu. Alifikiri kwamba anamjali, lakini ... ilikuwa ni kwa sababu bado alikuwa mume wake kwenye karatasi.


Alvin alitabasamu kwa upendo na kwenda uani. Ndani, uso wake mzuri ulibadilishwa na wimbi la maumivu. Alifunua safu ya bendeji kwa safu. Ndani, jeraha kali lilikuwa limeunda mapele mekundu, na mistari minene ya hasira usoni kwake ilionekana kuwa ya kutisha. Alikaa hapo kwa dakika sita au saba. Kisha, simu yake ya mkononi iliita nje.


Lisa aliitazama simu iliyokuwa kitandani na kusema. "Mama yako anapiga simu."


Alvin aliifuata simu iliyokuwa kitandani, na sauti jeuri ya Lea ikasikika. "Una muda? Nataka tule chakula pamoja kama mama na mwana.”


"Si tulikuwa tayari kukata mahusiano yetu kama mama na mwana? Ulisema wewe mwenyewe.” Alvin alimkumbusha.


Lea akafoka, “Alvin Kimaro, usiende mbali sana. Mimi ndiye niliyekuzaa.”


“Ndiyo ulinizaa, lakini hukuchukua jukumu la kunilea. Wewe ni mama mzuri sana lakini si mlezi bora." Alvin alidhihaki. “Najua unataka nifanye nini. Sitakuja.”


“Wewe…” Lea alivuta pumzi kwa jazba. “Sawa, kama hukubaliani, basi usinilaumu kwa kwenda kwa mkeo Lisa Jones. Unafikiri atakuonaje nikimwambia kuhusu ugonjwa wako?” Uso wa Alvin ulibadilika ghafla. "Alvin, kila mtu anaogopa udhaifu wake zaidi, na wewe umeonyesha udhaifu wako sasa," Lea alisema kila neno wazi wazi.


"Utajuta kwa hili." Alvin akakata simu.


Lisa alimtazama. Machale yake yalimwambia kwamba kuna kitu kilikuwa hakiko sawa kati yake na mama yake. Macho yake yalikuwa yakimeta kwa damu kana kwamba yangetoka wakati wowote. Kusema kweli, aliogopa kumuona vile. Hata hivyo, alijua lazima mama yake alisema jambo lisilopendeza sana. Akiwa kama mtazamaji tu, aliona Lea Kimaro ni mkatili kweli. Ni mama gani ambaye angekosa huruma kwa mwanawe?


"Nini tatizo?" Alinyoosha mkono kumshika Alvin. Alikuwa na huzuni kali sana kiasi cha kumfanya aumie kidogo moyoni.


“Si kitu. Natoka mara moja.” Alvin alitikisa kichwa na kugeuka kuondoka.

•••

Saa 4:00 usiku, Chester alifika kumtembelea. "Vipi hali hali kwa sasa?"


"Siwezi kula sana, vinginevyo tumbo litauma," Lisa alimjibu kwa umakini.


"Kula polepole. Kula kidogo lakini mara nyingi. Unapaswa kuondoka hospitali kesho kutwa. Kuhusu uso wako… njoo kila baada ya siku mbili upate matibabu…”


“Dokta Choka, unajua jinsi Alvin alivyoumia mkono wake?” Lisa alimtazama ghafla.


Chester alisimama kwa muda huku akiifuta miwani yake. “Alvin alikuambia nini?”


"Hakuniambia chochote."

“Kwa vile hakuzungumza nawe kuhusu hilo, basi si wajibu wangu kusema lolote pia.” Chester alitabasamu kwa heshima. “Si lazima ufikiri kupita kiasi. Ujue tu kwamba Alvin anakupenda.”


Kwa hivyo kila mtu alijua kwamba anampenda? Lisa aliinamisha macho yake taratibu. Hata hivyo, kwa namna fulani, kulikuwa na hisia mbaya moyoni mwake ambayo haikuweza kufutika kwa maneno mepesi tu ya Dokta Chester.


“Lakini nataka kujua ni nani aliyemuumiza. Nina wasiwasi aliikasirisha familia ya Kimaro kwa sababu yangu…”


“Alvin si mtu wa kawaida, hivyo familia ya Kimaro haiwezi kumfanya chochote. Usijali. Sasa hivi ni wewe tu unayeweza kumdhuru.” Chester alipouendea mlango, aligeuka na kutabasamu. “Umeanza pia kumjali Alvin. Ina maana uko tayari kumsamehe?”


Lisa alipigwa na butwaa kwa sekunde chache, na uso wake ukalegea kidogo. Chester akacheka. “Naomba ukae naye. Alvin ana hasira kidogo, lakini inahusiana na malezi yake. Kama unavyoona, watu wengi katika familia tajiri ni wabinafsi na wanafikiria tu masilahi yao wenyewe. Alvin kwa kweli anasikitisha sana.”


Baada ya kuondoka, msemo 'Alvin anasikitisha sana' ulijirudia akilini mwa Lisa kwa muda mrefu. Nani angefikiri kwamba mtu tajiri zaidi katika Nairobi nzima angefafanuliwa kuwa mwenye kuhuzunisha? Hata hivyo, alipofikiria jinsi alivyotengwa na kuachwa na kila mtu wa familia ya Kimaro, moyo wake haukuweza kujizuia kumuonea huruma.


Wakati huo, Shangazi Yasmini aliingia na kumuuliza, “Bibi mdogo, naweza kukuandalia uji kwa chakula cha jioni leo?”


Lisa alitikisa kichwa na kuongeza muda mfupi baadaye, “Tengeneza supu ya kuku pia, na uchemshe pamoja na ndizi.”


Shangazi Yasmine alikuwa na shaka. "Lakini daktari alisema tumbo lako halitaweza kuyeyusha vyakula vigumu kwa wakati huu..."


"...Hapana, ni kwa ajili yako na Alvin." Lisa aliitazama simu yake haraka haraka ili kuficha aibu yake.


Shangazi Yasmine aliingiza midomo yake kwenye tabasamu. Alikuwa ameona kwa muda mrefu mapenzi ya watu hawa wawili kwa kila mmoja. Sasa kwa vile bibiye huyo alikuwa tayari kumjali bwana mkubwa, alitarajia siku zao ziendelee kuwa bora.


“Ni kweli nitatengeneza, lakini Bibi mdogo nitamwambia bwana mdogo kuwa wewe ndiye uliyeniomba nifanye, vinginevyo, hatakula. Kama unavyoona, kwa kawaida hayuko tayari kula chakula changu.”


Lisa aliuma mdomo. Alijua kwamba Alvin angefurahi sana kujua kwamba alimjali tena. Hakutaka kuona sura yake ya kihuni.


Aunty Yasmine akasema. “Hutakiwi kuwa na aibu. Afya ya Bwana Kimaro ni muhimu zaidi. Hajapata chakula cha kueleweka kwa muda mrefu, na huwa anahangaika sana linapokuja suala la chakula.”  Lisa alifikiria juu ya jeraha lake na kutikisa kichwa kwa huruma.


Jioni, Alvin alifika na kukuta chakula cha jioni kimeandaliwa. Shangazi Yasmini alitenga chakula huku akitabasamu kwa unyonge. "Hii ndio supu ya kuku ambayo Bibi mdogo aliniomba nikuandalie."


Macho ya Alvin yaliangaza na kumgeukia Lisa, lakini aliinamisha kichwa kwa haraka ili ale na kukwepa kukutana na macho yake.


“Kwa kuwa kilipangwa maalum na mke wangu, lazima nile.”  Alvin akaachia tabasamu la kufoka. Alikunywa bakuli kubwa la supu mpaka hakuna kilichosalia. Alimaliza hata ndizi zote na kutamani kulamba kabisa hadi bakuli.


Shangazi Yasmine alishangaa sana. "Bibi mdogo lazima utoe neno ndipo mumeo ale? Sijawahi kumuona Bwana Mkubwa akila chakula kingi hivi.”


Lisa alikosa la kusema. Alikuwa mlaji mzuri tu alipokuwa Dar es Salaam, lakini aligeuka kuwa na tabia nyingi mbaya aliporudi Nairobi.


“Siwezi kujizuia. Kwa kuwa Mm’wagilia roho yangu amezungumza, ni lazima nisikilize kwa utiifu, la sivyo hataniruhusu nilale karibu naye usiku.” Tabasamu la furaha lilienea usoni mwa Alvin.


Lisa alishindwa kuvumilia kumsikiliza kwa aibu na kumpiga teke kali.


"Teke la mpenzi haliumi." Alvin aliinua uso wake mzuri. Alionekana kana yuko tayari kupokea mateke zaidi. Lisa alikuwa hoi kabisa dhidi yake na aliweza tu kula chakula chake kimyakimya.


Saa tatu na nusu usiku, Lisa alikuwa tayari kuzima taa ili alale, lakini Alvin alivua nguo ghafla na kuingia ndani haraka.


“Alvin Kimaro, ondoka...” Walikuwa wamelala katika vitanda tofauti tangu Lisa alazwe hospitalini, hivyo alimfukuza kwa vile hakuzoea.


"Oh, teke lako limeanza kuniuma." Alvin alijieleza kwa uchungu.


“Acha kuigiza. Mguu wangu hauwezi kukujeruhi.” Lisa alimfokea.


“UNaumia sana, labda nikilala karibu na wewe ndiyo nitapona…” Alvin alimtazama kwa uchungu.


Sura ya: 209


Wakati huo huo, Lisa alishukuru kwamba alikuwa amezima taa mapema. Vinginevyo, Alvin angeona kinyaa kumtizama kwenye mashavu yake. Uso wake ulioharibika bila shaka ungekuwa na kidonda.


“Sikuwa…”


“Hakika ulikuwa unajaribu kunilemaza. Kwanini usiniangalie na kuona kama nimejeruhiwa?” Akacheka vibaya masikioni mwake.


"Hakika, nitaangalia baada ya kukupa teke lingine." Hatimaye, akainua mguu wake kwa mara nyingine. Alvin aliitikia haraka na kumshika mguu wake uliokuwa ukining'inia hewani.


"Msichana wangu mzuri, unataka kunitia ulemavu?"


Lisa alihisi kutetemeka kwa mgongo wake baada ya kusikia neno hilo la kupendeza. Kwa kweli alishindwa kuelewa ni kwanini mwanaume huyo hakujali kabisa kuhusu sura yake mbaya. “Alvin, unaweza kuacha masihara yako? Nataka kwenda kulala.”


"Mume na mke wanalala kitanda kimoja." Baada ya kusema hivyo, aliweka hata cheti chao cha ndoa karibu na mito, kana kwamba alikuwa na wasiwasi kwamba huenda amesahau kuhusu ndoa yao.


Lisa hakuwa na la kusema huku hisia ngumu ikitokea moyoni mwake. “Huogopi kuota ndoto mbaya kutokana na kuona sura yangu mbaya katikati ya usiku?”


"Hakuna kitu cha kuogopa. Ilimradi bado uko vile vile katika maeneo mengine.” Uso wake ulidhihirisha kuwa hakujali hata kidogo.


Kwa mara nyingine tena, uso wake ukalainika ndani ya sekunde chache. "Umekosea ikiwa hufikirii kuwa sina nguvu za kukutia kilema."


“Lisa, ninajaribu tu kukuambia kwamba hakuna kitakachobadilisha jinsi ninavyohisi kuhusu wewe. Haijalishi unaonekanaje.” Akaenda chini ya shuka ili kumkumbatia kwa nguvu. Hakuwa na hakika jinsi ya kuitikia ukweli wa sauti yake. Mtu huyu alikuwa kweli… Sigh, hakuwa na neno kwa hilo. Ina maana kweli hakujali kuhusu uso wake ulioharibika? Ilimshangaza sana.


“Unaniamini sasa? Nitathibitisha kwa matendo yangu.” Alvin alimtazama machoni kwa nguvu bila kuzuia hisia zozote.


Hilo lilimshangaza Lisa na haraka akaitikia kwa kichwa. “Sawa, acha kuongea. Nakuamini."


"Naweza kupata busu?" Akasogea karibu zaidi kutaka busu.


Lisa alisikia mapigo ya moyo yake yakidunda kwa kasi chini ya ngozi. Mwanaume huyu… kweli hakujali sura yake? Aliweza kuamini kwamba hakuwa anajifanya. Jinsi alivyombusu ilikuwa kama jinsi ile ile alivyombusu  awali kabla hajajeruhiwa. Hakuna kilichobadilika. Ilikuwa ni kana kwamba hatawahi kuchoka kumbusu hata kidogo.


Siku ya tatu, Lisa alielekea moja kwa moja hadi Mawenzi Corporations baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini. Hakuwa amejitokeza kwenye kampuni hiyo kwa takriban nusu mwezi. Jambo la kwanza alilofanya aliporudi ni kuandaa mkutano wa dharura na watendaji. Hata hivyo, watendaji wote walipigwa na butwaa baada ya kumuona sura yake. Alijua alikuwa anaonekana vibaya sasa lakini daktari alikuwa amemwambia ni muhimu kuacha majeraha yapumue. Kwa hivyo, aliamua kutofunika uso wake siku hiyo.


“Samahani. Mambo mengi yametokea hivi karibuni na uso wangu… huenda usipone. Natumai nyote hamjashtushwa sana na hili.” Aliukabili umati kwa utulivu.


Watendaji walivutiwa kuwa mwanamke huyu mchanga katika miaka yake ya mapema ya 20 aliweza kukabiliana na hali mbaya kama ile kwa utulivu kama huo. “Mwenyekiti Jones, usikate tamaa. Kwa teknolojia ya kisasa ya matibabu, muonekano wako hakika utatengenezwa. Ni suala la muda tu,” Meneja Mkuu alisema kumfariji.


“Siyo ishu kubwa kihivyo, kwa kweli. Sisimamii kampuni kwa sura yangu bali kwa uwezo wangu,” Lisa alijibu kwa mzaha nusunusu. “Sawa, wacha tuendelee kujadili maendeleo ya miradi inayoendelea katika maeneo mbalimbali…”


Mkutano uliisha saa moja baadaye.


Lisa alirudi ofisini kwake na kukutana na kadi ya mwaliko kutoka kwa Melanie na Jerome kwenye meza. Walikuwa wakifanya sherehe yao ya uchumba huko Mombasa katika Hoteli ya Pavilion Intercontinental kesho yake.


Melanie alikuwa akijaribu kusema nini na mwaliko huo? Akiwa anawaza hayo tu, akapokea simu kutoka kwa namba asiyoifahamu. “Dada mkubwa, umeiona kadi yangu ya mwaliko?”


“Usiniite hivyo. Sina dada mdogo ambaye alijaribu kumuiba mume wangu.” Lisa aliongea maneno hayo akiwa na uhakika wa kulindwa na cheti cha ndoa upande wake.


“Una jeuri kweli. Nani kakuibia mume?" Melanie nusura apige kelele kwa hasira lakini akavuta pumzi ndefu badala yake. “Sawa. Hatimaye nimepata furaha yangu. Wewe ni binti wa baba hata iweje na hakuna kinachoweza kubadilisha ukweli kwamba tunashiriki damu moja. Nina hakika hutakosa sherehe ya uchumba ya dada yako mdogo sawa?”


“Bila shaka nitakuwepo kwa vile umenialika kwa fadhili." Lisa alijibu kwa upole.


Melanie alishtushwa na jibu chanya ambalo hakulitarajia. “Unakaribishwa sana. Enhee kabla sijasahau, nilisikia juu ya ulemavu wako wa uso. Usisahau kuvaa barakoa kesho. Sitaki uwaogopeshe wageni wangu. Natarajia kukuona.” Alikata simu baada ya kucheka.


Hatimaye Lisa alielewa nia ya Melanie. Walitarajia nafasi ya kumdhihaki. Lakini, hakuwa na wasiwasi sana juu ya kile watu hao wasio na maana walifikiria juu ya sura yake. Labda wangekuwa wao ndio wanaojisikia kuchukizwa kesho yake.


Shani alikuja kumchukua baada ya kazi badala ya Alvin. "Bwana Kimaro anafanya kazi ya ziada usiku wa leo, kwa hivyo hakuweza kupata muda wa kuja kukuchukua." Shani alieleza baada ya Lisa kujiweka kwenye siti ya nyuma.


Hili lilimshangaza Lisa. Alijua Alvin mwanasheria na angeweza kuwa busy muda wowote. Lakini pia alifahamu Alvin alikuwa na vitega uchumi vingine hata baada ya kufukuzwa kazi kama mwenyekiti wa KIM International. Lakini, alionekana kutojua chochote kuhusu mambo yake.


"Alvin kafukuzwa KIM International. Anafanya kazi katika kampuni gani kwa sasa?" Lisa aliuliza kwa mshangao.


Macho ya Shani yalimtoka baada ya kusikia swali hilo na kunyamaza.


"Ni sawa ikiwa hutaki kujibu." Lisa alitingisha kichwa na kuangalia pembeni. "Nauliza tu kwa kawaida."




Shani alikunja uso, akiwa amechanganyikiwa kidogo. “Bwana Kimaro hakufichii mambo kimakusudi. Ninaogopa kwamba unaweza kufikiria kupita kiasi baada ya kusikia jina la kampuni hiyo.”


Lisa alitazama juu kana kwamba alikuwa amekumbuka kitu ghafla. “Je, inawezekana… kwamba jina hilo linahusiana na yule mwanamke anayeitwa Sarah?”



“Inaitwa Alvinarah,” Shani alieleza, “Lakini kampuni hiyo ilianzishwa miaka mitano iliyopita, kabla ya Bwana Kimaro kukutana nawe. Nina hakika asingetumia jina hili kama angeanzisha kampuni mpya leo.”


“Sawa.” Lisa aligeuka pembeni kutazama dirishani.


Alvinarah… Ni dhahiri lilikuwa jina lililotokana na mchezo wa maneno wa majina ya Alvin na Sarah. Jina zuri kama nini! Kama ilivyokuwa yeye, Alvin na Lisa, Alvlisa.


Lisa alifikiri kwamba labda asingekuwa katika hali hiyo ikiwa mwanamke huyo anayeitwa Sara angalikuwa hai......ITAENDELEA.....


Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.