JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA..................................206-207
Sura ya: 206
Kwa upande mwingine, mahojiano ya Alvin yaliibua taharuki kwenye Mtandao. Hisia za watu kwenye mtandao pia zilibadilika haraka sana.
[Sh*t! Kwa hivyo kama Bwana Kimaro amefunga ndoa na Lisa Jones zamani sana, ina maana yeye si mchepuko hata kidogo. Ni kawaida kabisa kwa mume na mke kulala pamoja. Melanie Ngosha ndiye alikuwa mchepuko badala yake.]
[Hebu fikiria hilo, zaidi ya ile picha alipokuwa akichuma strawberries na Melanie Ngosha, sijawahi kumuona akiwa na Melanie Ngosha hata siku moja. Kinyume chake, Alvin Kimaro amemkumbatia Lisa Jones na kumnunulia pete ya uchumba. Yeyote mwenye jicho kali anaweza kuona hayo ni mapenzi ya kweli.]
[Sasa nadhani Lisa Jones hana raha. Familia ya Kimaro haimkubali, na sote tulikuwa tukimsema hovyo pia. ]
[Bwana Kimaro, tulikosea. Wewe ni mwanamume kweli, wewe si fisadi hata kidogo, Ulipigana na familia za kitajiri Nairobi kwa ajili ya mke wako. Uko poa sana!]
[Mwishowe wa siku ile familia ya Kimaro iliondoa nafasi yake ya uenyekiti kwa sababu Alvin Kimaro alitaka kuwa na Lisa Jones. Walikunea sana!]
[Ee Mungu wangu, Alvin Kimaro aliachia kiti chake kwa ajili ya Lisa Jones? Siamini kama watu wema kama yeye bado wapo katika huu ulimwengu.]
Sikupaswa kugomea bidhaa za Alvin Kimaro. Kuanzia leo nitaunga mkono bidhaa zote anazowekeza.]
[Hakika Alvin Kimaro, wewe ni mwanamume wa ndoto zangu.]
•••
Katika familia ya Ngosha.
Melanie Ngosha na Nina Mahewa walipandwa na hasira kwa kuona taarifa hiyo. Joel alikuwa amezoea kutazama mama na bintiye wakivunja vitu karibu na nyumba kama vile wagonjwa wa akili.
"Hiyo haiwezekani. Ahh, inawezekana vipi Alvin na Lisa Jones kufunga ndoa miezi minne iliyopita?” Uso mzima wa Melanie ulikuwa umepinda. “Anasema hajawahi kuchumbiana nami kabisa. Kwanini anafanya hivyo? Alipofika nyumbani kwetu kwa chakula cha jioni hata alinishika mkono. Mama, kila mtu huko nje ananiita mchepuko sasa. Wote wanasema sina aibu…”
“Huyo Alvin Kimaro ni mshenzi sana. Sikuwahi kufikiria angeweza kufanya hivi.” Nina pia alipigwa na butwaa.
Tukio hilo lilitokea wakati ambapo Nina alikuwa amezama katika furaha ya uchumba kati ya bintiye na familia ya Campos. Alidhani Alvin Kimaro alikuwa amekwisha na asingeweza kuinuka tena. Hata alimtaka Melanie ajenge picha ya hali ya juu ya mtu ambaye alikuwa amekomaa katika mahusiano, kwamba angeweza kumpenda mtu au kumwacha ikiwa angehitaji kufanya hivyo. Hata hivyo, hakutarajia mashua yao kuzama siku iliyofuata. Alvin alikuwa na cheti cha ndoa mkononi mwake. Ulikuwa ukweli mgumu usioweza kupingika.
Kwa jazba, Nina aligeuza hasira yake kwa Joel. “Ulijua hili tangu mwanzo? Ukatuzuga kwamba Kelvin Mushi ndiye mchumba wa Lisa. Unatuchukuliaje kwa mfano?” Joel alimpuuza tu.
Melanie alihuzunika sana hivi kwamba alishindwa kujizuia pia. “Baba mbona hukuniambia? Mimi hunipendi hata kidogo. Unachowaza kichwani mwako ni kumsaidia Lisa tu."
“Nyie ni wagonjwa kweli. Siwezi kuishi na nyie tena. Siitaki nyumba hii. Baada ya ndoa ya Melanie katika familia ya Campos, tutapeana talaka.” Joel alishindwa kuvumilia, hapohapo alifungasha vitu vyake na kuondoka katika jumba la familia yake.
“Utachumbiwa na familia ya Campos hivi karibuni. Usijali sana mwanangu wengine wanasema nini kuhusu wewe.” Nina alimshika mkono Melanie. "Kwa kuwa familia ya Campos inatuunga mkono, ni suala la muda kabla ya Alvin Kimaro na Lisa Jones kushughulikiwa."
Melanie aliitikia kwa kichwa. Bila shaka angerudisha matusi kwa Alvin mara elfu. “Mama, ni kweli baba atakutaliki?”
"Babu yako hataweza kukubali." Nina alijigamba.
•••
Katika makazi ya kifahari ya familia ya Kimaro.
Asubuhi na mapema Mzee Kimaro nusura afe kwa hasira kwa sababu ya mahojiano ya Alvin kwenye runinga, hasa alipoonesha cheti cha ndoa. "Huyu kijana ni mshenzi, sikufikiria kuwa alimuoa Lisa Jones zamani sana."
Bibi Kimaro akajipapasa paji la uso. Bado alikuwa hajapata fahamu zake vizuri kutokana na mshtuko. “Naam, sasa ni mtu mzima, na ametudanganya sote. Hata nilihangaikia ndoa yake kama mpumbavu.”
Valeria alisema kwa hasira, “Mama, yale ambayo Alvin alisema kwenye TV yalikuwa mengi sana. Familia yetu ilimlea na kumkuza, lakini mwishowe, ameifanya familia yetu ionekane kama wapuuzi.”
“Unazungumza kana kwamba sisi si wapuuzi kweli,” Willie Kimaro hakuweza kujizuia.
“Willie, unatutukana?!” Spencer alimwangalia.
“Kama si upuuzi ni nini?” Willie alikazia, “tunamzungumzia tu Alvin ambaye amejua kucheza karata zake vizuri, kwanini tusiangazie familia badala yake? Sasa, sifa ya Alvin inabadilika. Ikiwa kutakuwa na tatizo na maendeleo ya siku za usoni katika KIM International, bila shaka tutageuka kuwa kituko.”
Kila mtu mara moja akamgeukia Jack. Mzee Kimaro alimtazama na kusema. “Jack, bora usiniangushe. Nimesikitishwa sana na Alvin.”
Jack akatabasamu. “Babu, usijali. KIM International ndio biashara kuu Afrika Mashariki. Ingawa baadhi ya watu wanasema ni Alvin aliyeifanya KIM International jinsi ilivyo leo, nadhani ni miunganisho ambayo familia yetu ilipata kutoka kwa vizazi na uwezo wetu wa kifedha ambao ulimsaidia. KIM International ina vipaji vingi, hivyo kutokuwepo kwake hakutakuwa na athari kubwa.”
“Uko sawa.” Mzee Kimaro aliridhika sana. “Alvin ana kiburi sana. Atajuta mapema au baadaye. Kwa kuwa sasa ameondoka KIM International, yeye si lolote.”
Range Rover nyeusi iliondoka kwenye jumba la kifahari la familia ya Kimaro. Lea, ambaye alikuwa ameketi kwenye kiti cha nyuma, aliuliza kwa kawaida, “Jack, vipi maendeleo ya utafiti na uendelezaji wa teknolojia mpya ya cement? Mkutano na waandishi wa habari utafanyika mwezi ujao."
"Mama, mhandisi mkuu wa utafiti, Simon Mbugui, aliongoza kikundi cha wafanyakazi wenzake kuwasilisha barua zao za kujiuzulu." Jack alishika usukani kwa nguvu. Uso wake mzuri ghafla ukageuka kwa huzuni. "Sikuidhinisha, lakini hawajafika kiwandani kwa siku kadhaa."
"Nini?" Lea alitazama juu kwa mshangao na mara moja akagundua. “Nakumbuka sasa. Simon Mbugui ni kipaji ambacho Alvin Kimaro alikisomesha nje ya nchi miaka mitano iliyopita. Karibu watu wote katika kiwanda waliajiriwa na Mbugui.
"Ndio, kuna uwezekano mkubwa kwamba Alvin ndiye mpangaji mkuu wa njama hizi." Jack hakuonekana vizuri. “Nilikuwa nikitafuta mtu wa kuchukua nafasi ya Simon Mbugui, lakini hatuna muda. Watu kama Mbugui hawawezi kupatikana kwa mwezi mmoja au miwili tu.”
Mason ghafla alisema, "Si ajabu, nilikuwa najiuliza kwanini Alvin aliondoka kwa urahisi sana. Amekaa KIM International kwa miaka mingi sana, lakini hakufanya fujo hata kidogo alipofukuzwa. Kumbe bado alikuwa na kadi ya kucheza."
"Utafiti huu wa simenti ni muhimu sana. Ikiwa uzalishaji utacheleweshwa, kampuni zinazoshindana nasi zitachukua fursa hiyo kuinuka, hasa hii kampuni ya Alvinarah.” Lea alikunja uso na kukemea, “Hali si nzuri, bado ulijigamba mbele ya babu yako kwamba utaweza.”
“Mama, haikuwa rahisi kwangu kutwaa KIM International. Siwezi kumruhusu babu afikiri kwamba mimi ni dhaifu kwa Alvin baada tu ya kushika wadhifa huo.” Jack alipiga kelele.
"Nitaenda kwa Alvin mchana kufanya uchunguzi…” Lea alisema.
“Kwa ajili ya nini? Nyinyi wawili mmekuwa mkitofautiana kila mara.” Mason alimpigapiga nyuma ya mkono wake. “Mshaurini tu arudi kwenye kampuni. Ndugu wawili wanaweza kufanya kazi pamoja. Kuna haja gani ya kupigana hadi kufa?”
“Baba, wewe ni mtu wa kufikiria sana. Nisipopigana, atanifukuza nje ya kampuni mara Bibi na Babu watakapokuwa hawapo. Kunatakiwa kuwa na mtu mmoja tu katika KIM International, na mtu huyo ni mimi,” Jack alisema kwa dhihaka.
"Ni kweli, hata mimi nataka pia Jack kuchukua jukumu la KIM International. Alvin anataka kumuoa Lisa Jones, lakini hana utulivu kihisia na karibu kumuumiza Valeria wakati huo. Simpendi zaidi sasa hivi.” Lea akatikisa kichwa. Ikiwa angeweza kurudi zamani, bila shaka asingemzaa Alvin.
Sura ya: 207
Baada ya chakula cha mchana.
Upepo wa utulivu na wa kustarehesha ulivuma kutoka dirishani, ukimpulizia Lisa kwa unyonge. Alifumba macho kwa kuduwaa, alitaka kulala, lakini ghafla akahisi mtu akimbusu usoni. Alikuwa ni nani?
Harufu nzuri ya kiume iliyopeperushwa kutoka kwa upande mwingine haikumchukiza hata kidogo. Macho ya usingizi ya Lisa yalifunguliwa polepole, na aliona sura ya kupendeza na kuvutia. Alionekana mtu ambaye hapo awali alikuwa kivutio cha wengi kwenye TV.
“Umeamka, nguruwe mvivu? Umelala kwa zaidi ya saa mbili.” Alvin alibana pua yake kama mtu aliyepagawa na upendo na kusema kwa sauti ya kuvuta.
Lisa alikuwa akihema kwa muda akafikiri yuko Dar es Salaam. Hata hivyo, hata huko Dar es Salaam, ni mara chache sana Alvin alikuwa mpole na mwenye kujali namna hii.
“Ulikuja saa ngapi?” Alikaa haraka. Alvin alifika kwa wakati kwani Lisa alikuwa na maswali mengi ambayo alitaka kumuuliza.
“Si muda mrefu, kama saa moja iliyopita. Nimekuja kukuona ukikoroma.” Alvin alitazama saa yake na kutania.
“Sikoromagi mimi.” Lisa alimtazama Alvin na kujibu kwa aibu.
"Utajuaje ikiwa unakoroma wakati tayari umelala?" Alvin alikuwa hajamuona hivyo kwa muda mrefu, hivyo alimtania makusudi.
“…Sawa, ni vizuri hata hivyo nikoromee. Angalau hakuna mtu atakayetamani kulala nami katika siku zijazo." Lisa alimkazia macho.
“Wewe ni mke wangu. Nitalala na nani kama si wewe?" Alvin alitabasamu na kumkazia macho.
“Inatosha, Alvin.” Lisa akabadili mada ghafla. “Tuliachana muda mrefu uliopita. Hicho cheti feki cha ndoa sijui umekipata wapi…”
“Nani kasema kuwa tuliachana? Hiki siyo cheti feki. Jionee mwenyewe.” Alvin alichukua baadhi ya nyaraka, moja ambayo alipewa aliposaini hati za talaka.
Lisa aliinyakua ili kuangalia. Ilikuwa sawa kabisa na ile ya awali. "Sisi ... hukunipa talaka?"
"Kusema ukweli, tulitia saini tu makubaliano ya talaka. Bado hatujakamilisha taratibu za kutalikiana.” Alvin alimtazama kwa tabasamu. "Tuliposaini karatasi, tayari ilikuwa mwishoni mwa mwaka, na ofisi za Jiji pia zilifungwa kwa likizo. Nani alijua kwamba tungegongana mara tu baada ya kufika Nairobi. Heh? Hata ukapata na mchumba mwingine siku kumi tu baadaye."
Lisa aliona aibu. Kwa maneno mengine, yeye ndiye alisaliti katika ndoa?
“Wewe pia ulikuwa msaliti. Ulitafuta rafiki wa kike,” Lisa alijibu kwa haraka. "Halafu, ulikana moja kwa moja kuwa una uhusiano wowote naye. Niliona kwa macho yangu jinsi ulivyomshika mkono kwa upendo ulipokutana na wazazi wake, karibu nikuite shemeji.”
“Una wivu?” Alvin alizungusha ncha ya pua yake. Alikuwa mchangamfu haswa alipoona sura yake mbaya isiyo ya kawaida.
“Unawaza kupita kiasi, sina wivu.” Lisa akatazama pembeni. Alivyojichukulia mwenyewe kwa sura yake, hakustahili hata kuwa na wivu.
“Sawa, nitakuwa mkweli kwako.” Alvin alimshika mkono na kuuweka chini ya kidevu chake. “Kila nilipowasiliana na Melanie Ngosha, ni kwa sababu anafanana kidogo na wewe. Kwa hivyo hapo mwanzo nilitamani kuwa naye kwa sababu tu alifanana na wewe.”
“Sijawahi kukuelewa…” Yalikuwa maneno mawili tu, lakini Lisa alihisi ghafla kuwa ndiyo sentensi pekee ambayo alikuwa amesema hadi muda huo ambayo ilimtoka kwa kawaida na kumgusa tangu aje Nairobi.
Moyo wake ulipiga kwa kasi. Alipokutana na Melanie kwa mara ya kwanza, alihisi pia kwamba Melanie na yeye walikuwa wanafanana kidogo. Hata hivyo, hakuamini kuwa hiyo ndiyo sababu ya Alvin kumwendea Melanie. Baada ya yote, alikuwa na uamuzi wa kuachana naye wakati anaondoka Dar es Salaam. Kutokuamini kwake pia kulimuumiza sana.
“Mwanzoni, nilifikiri kwamba kwa vile hukuwahi kunipenda na ulinikaribia tu ili kunidanganya, ningeoa mwanamke anayefanana na wewe na kusahau hilo. Lakini sikutarajia angekuwa dada yako wa kambo.” Macho ya Alvin yalikua magumu. “Tangu nilipokutana nawe kwenye makazi ya Ngosha, sikuwahi kufikiria kutaka kuwa na Melanie tena.”
“Lakini ulikuwa unaongozana naye hadi kwenye makazi ya Ngosha. Pia, umesahau jinsi ulivyokuwa na kiburi kwa kumlinda wakati wa sherehe ya kuzaliwa kwa babu yangu?” Lisa aliuma meno kwa chuki na kumbukumbu. “Sikuhisi kama unanijali sana. Hata umenifedhehesha mara nyingi sana.”
Alvin alimtazama kwa ajabu. “Kama si kwa sababu nilitaka kukuona, unafikiri kwanini ningehudhuria sherehe ya kijinga kama ya siku ya kuzaliwa? Kwa upande mwingine ulimleta Kelvin Mushi ili akutane na wazazi wako ukiwa bado kwenye ndoa. Umewahi kufikiria hisia zangu? Ulitaka nikae naye meza moja na kuangalia jinsi wewe na Kelvin mnavyopendana?”
Lisa alimsikiliza akitoa mashtaka ya uwongo huku uso wake ukiwa wa haki. Hakuwa na furaha. "Kwani wewe hukuonyesha upendo wako na Melanie mbele yangu pia?"
Alvin alikoroma kwa ujeuri na kumuuliza. "Ilikukuuma nilipofanya?"
"…Hapana." Lisa aligeuza uso wake mbali.
Alvin alikasirika, lakini ilimbidi akubali tu pale Lisa alipoonesha tabia kama hiyo. Alichoweza kufanya ni kumshika mikononi mwake na kumkumbatia kwa nguvu. “Hata kama haujali, mimi najali. Lisa, najua unanichukia, lakini nifanye nini? Nadhani unacheza nami, lakini siwezi kukuacha uende. Ninasumbuliwa na sumu inayojulikana kwa jina la Lisa Jones.”
Kadiri alivyozidi kuongea ndivyo alivyozidi kusononeka. Akainamisha kichwa chini na kuuma mdomo wake. Akampa busu lililojaa huzuni, upendo na huruma.
Lisa alikuwa amemkataa hapo awali. Kwa namna fulani, kila mara alionekana kuwa na mkanganyiko wa hisia moyoni mwake. Alijawa na chuki dhidi yake. Lakini, kwa kuwa sasa alikuwa amemwaga moyo wake kwake, moyo wake ulilainishwa kwa busu lake bila kupenda. Hakuweza kumpinga. Alijua kwamba bila kujali kuta alizojenga, Alvin angezibomoa kidogo kidogo.
Hiyo ni kwa sababu alikumbuka jinsi Alvin alivyopigana na familia nzima ya Kimaro kwa ajili yake. Alipigana dhidi ya familia tajiri jijini Nairobi kwa ajili yake, na akaachana na nafasi ya mwenyekiti wa KIM International kwa ajili yake. Hayo yote yalikuwa ukweli. Vinginevyo, Mzee Kimaro alipompa chaguo, kama angekuwa hampendi angechagua kubaki. Lakini, aliondoka kwa sababu yake.
Alipoona kwamba kulikuwa na mabadiliko kidogo ndani yake, Alvin alifurahi sana. Alizidisha busu kabla ya kumkandamiza mwili wake taratibu. Lisa alimfikiria Shangazi Yasmini jikoni na kumshika mkono wake bila fahamu, akisema kwa upole, “Usifanye hivyo, Shangazi Yasmini yuko hapa…”
Kilichomjibu ni mkono wa mwanamume huyo unaotetemeka ghafla. Kisha, aliona mwanga wa ghafla wa maumivu katika macho yake ya kina, lakini ni kwa muda mfupi sana.
“Wewe…”
“Sawa. Ni sawa kama hutaki.” Alvin aliinua mwili wake kwa mkono mmoja.
“Naenda uani…”.....ITAENDELEA.....
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.
