JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA..................................204-205

Sura ya: 204 

“Pamela…” Lisa alitaka kumzuia lakini Pamela aliwahi kumkatisha.

“Lisa nyamaza, wala usiseme chochote. Najua anaweza kuwa mtoto mwingine wa kishua kutoka kwenye familia tajiri, ila siogopi hata kidogo. Kama ni kuniharibu acha waniharibu tu hata nifanane na wewe, nina deni kubwa kwako. Kama nisingemchanganya Alvin Kimaro kwa mtu mwingine, usingejihusisha nae na haya yote yasingekukuta. ” Pamela nusura alie kwa majuto.

"Oh, kwa hiyo yote yalianza kwa sababu yako. Nilijua wasichana wajinga kama wewe wanajua kuongea tu, kumbe huna maana hata kidogo?" Rodney alisema kwa ukali.

"Funga mdomo wako, wewe mwanamke,” Pamela alimfokea.

“Unasema nini?” Uso mzuri wa Rodney ulikuwa karibu kugeuka kuwa kama zimwi.

“Nimesema chochote kibaya, wewe ni mwanaume uliyevaa shati la pinki, unaonekana mrembo kuliko wanawake na unaongea zaidi ya mwanamke, wewe ni mwanaume au mwanamke?” Pamela alikuwa kachanganyikiwa.

"Wewe mwanamke mjinga. Nisipokuua..." Rodney alikuwa karibu kumrukia kwa hasira, lakini Sam alimzuia kwa haraka. "Bro, tulia."

“Si umemsikia mwenyewe akinitukana, nitulie vipi? Rodney alikasirika.

Pamela akaongeza kwa jeuri, "hata ukikasirika, wewe bado ni mrembo tu, kwa hivyo unaonekana mzuri hata ukiwa na hasira."

Lisa aliumwa na kichwa na ikabidi amwambie ukweli, “Pamela, inatosha. Yeye ni bosi wako. Ni Rodney Shangwe, mwenyekiti wa Osher Corporation.”

Pamela alokosa la kusema, eti nani? Hakuwahi kukutana na mwenyekiti wa kampuni yake, hata siku ile alipomuaga Lisa kuwa anaenda kukutana na mwenyekiti kwa kikao cha dharura hakuonana naye kwani alileweshwa pombe kabla hajafika. Ila kama mfanyakazi wa kampuni alifahamu kuwa mwenyekiti wa kampuni ni Rodney Shangwe. Kulingana na fununu alizozisikia, Rodwy alikuwa mtu mwenye nidhamu na mcheshi, lakini mbona aliyemwona alikuwa tofauti kabisa?

Pamela Masanja, umekwisha." Rodney alimdhihaki.

“Sawa, nimeelewa, najua madhara ya kumkosea heshima bosi wangu, lakini ulistahili. Nitaacha kazi tu, nitarudi kufungasha vitu vyangu.” Pamela hakujali hata kidogo.

“Usisahau mkataba uliosaini na kampuni.” Rodney alimkumbusha. “Mkataba wako ni tofauti na wafanyakazi wa kawaida. Ulisaini mkataba wa usiri. Ukithubutu kuacha kazi yako bila kibali nataka kuona ni nani atathubutu kukuajiri katika siku zijazo." Rodney alitisha.

"Bwana Rodney, rafiki yangu alikasirika tu kwa sababu ya kile kilichonipata. Natumai hutachukulia hili jambo kibinafsi." Ilimbidi Lisa amgeukie Alvin. "Pamela anaongea kwa mihemko, lakini fikiria juu yake. Kama ni wewe uliyeharibika sura, marafiki zako wasingekasirika vile vile? Kama vile mara ya mwisho Bwana Rodney aliponifundisha somo…"

"Nini ?Alikufundisha somo gani?” Pamela alimkazia macho Rodney, "Wewe bado ni mwanaume kwa kumnyanyasa mwanamke?"

"Ukisema neno lingine, nitakuthibitishia kuwa mimi ni mwanaume." Rodney alionya,

"Inatosha, acheni kulumbana. Hii ni wodi ya hospitali na sio uwanja wa malumbano. Mgonjwa anahitaji kupumzika." Alvin aliingilia kati kwa ukali, na watu wote wakanyamaza mara moja. Macho ya Alvin yalizunguka chumba kile na kutua kwa Rodney, “Rodney wewe ni mwanaume, uwe mkarimu, Pamela ni rafiki wa Lisa, achana naye.”

Rodney alimuangalia Pamela ambaye alimtumbulia macho tu, “Alvin huna shukrani kweli, niliongea kwa ajili yako tu kwa sababu alikuwa anakukaripia.”

Sam akamvuta na kusema kwa sauti ya chini “Rodney inatosha namuelewa Pamela, kusema kweli kumuona Lisa hivi imeniuma sana hata ninajilaumu kumpigia simu Alvin kumuita Dar es Salaam wakati huo.”

Sam alifikiri kwamba Alvin na Lisa walikuwa ni pea iliyotengenezwa mbinguni, lakini ikageuka kuwa ni hadithi mbaya ya mapenzi.

Rodney alitazama sura ya Lisa na ghafla akanyamaza, hakumpenda sana hapo awali, lakini alimhuzunikia ghafla muda ule.

"Ikiwa unanifikiria kama kaka, basi fikiria zawadi kwa ajili ya harusi yangu. Ninapanga kufanya naye harusi ya kusisimua baada ya mwezi mmoja." Macho meusi ya Alvin yalimtazama Lisa huku akisema kwa umakini, “Huniamini, lakini nataka kuuambia ulimwengu wote kwamba haijalishi sura yake, haitabadilisha upendo wangu kwake.”

Lisa aliinua macho yake ghafla na kukutana na macho yake kwa mshtuko.
Kwa kweli hakuweza kuamini kile Alvin alimaliza kusema. Alikuwa tayari ulimwengu mzima kuona anaoa mwanamke mwenye uso ulioharibika?"

Lisa alisema kila neno kwa sauti na wazi, "Nilichokuwa nataka ni ulimwengu usijue kama unanipenda kwa sababu yote hayo ni ya juu juu. Unaelewa?"

Maneno yake yalikuwa kama kisu kikali kinachomchoma Alvin moyoni. Alvin hakuelewa lolote. Alichojua ni kwamba alikuwa na deni kubwa sana. Katika maisha haya alitaka kumuweka pembeni yake daima na kumtunza.
•••
Lisa aliendelea kulazwa hospitalini kuuguza afya yake kwa siku kadhaa. Alvin alilala naye hospitalini kila siku.

Maneno juu ya Alvin kuleta watu kuzunguka makazi ya kifahari ya familia ya Kimaro ili kumuokoa Lisa yalikuwa yameenea Nairobi kote. Nyakati hizo, Nairobi ilijaa fujo na dhoruba nyingi za chini kwa chini.

Katikati ya dhoruba hizo, tukio la furaha lilishtua ghafla jiji. Binti wa familia ya Ngosha, Melanie Ngosha, na Jerome Campos kutoka familia ya Campos walikuwa wachumba waliotarajia kuchumbiana Jumamosi iliyofuata, na mshenga wao alikuwa Bibi Kimaro kutoka familia ya Kimaro.

Lisa alikuwa amepumzika wodini alipoona habari hizo. Alipigwa na butwaa. Aliwahi kusikia kuhusu familia ya Campos hapo awali. Familia ya Campos ilionekana ilikuwa familia ya kawaida sana jijini Nairobi zaidi ya miaka ishirini iliyopita. Hata hivyo, baada ya Mason Campos kumuoa Lea Kimaro, familia ya Campos haraka ikanyanyuka na kuwa mojawapo ya familia nne kuu za Nairobi kwa usaidizi wa familia ya Kimaro.

Kwa kuwa Jack alikuwa mrithi wa KIM International, ilimaanisha kuwa familia ya Kimaro ingeongozwa na Jack hapo baadaye. Kwa vile wazazi wa Jack pia walikuwa wanafamilia wa Campos, familia ya Campos bila shaka ingekuwa ya pili baada ya familia ya Kimaro hapo baadaye. Haishangazi Melanie alibadilika ghafla na kuacha kumsumbua Alvin. Kwa hivyo hiyo ndiyo ilikuwa sababu. Melanie alikuwa akisaka fursa za hadhi ya juu.

Hata hivyo, Melanie hakuwa na akili hiyo. Inaelekea ni Nina, mama yake, ndiye alikuwa injinia wa mipango yote. Nina Mahewa hakuwa mtu rahisi.

Usiku huo, Melanie alipakia video fupi mtandaoni. “Ndiyo, naingia kwenye uchumba. Najua kila mtu anashangaa kwanini nataka kuolewa ghafla baada ya kuachana na Alvin. Sababu ni rahisi. Nimechoka sana, na ni ngumu sana kumpenda mtu. Katika siku zijazo, ninataka kupata mtu anayenipenda, anayesamehe, kunithamini, kunijali na kunitendea kama binti wa kifalme, na si kama mtumwa.”

Videohiyo ilipokea maoni mengi sana kutoka kwa mashabiki zake;

[Moyo wangu unauma kwako binti wa kifalme Melanie. Lazima ujipende mwenyewe kuanzia sasa. Mwambie huyo mchafu Alvin aende kuzimu.]

[Alvin amekwisha. Yeye hastahili kuwa na wewe.]

[Nilisikia aliyemtongoza Alvin Kimaro ni dada wako wa kambo. Yeye ni binti wa haramu wa Joel Ngosha.]

[Hapana, Joel Ngosha ni mmoja wa watu kumi bora nchini. Ni mtu mzuri anayejali familia yake na kumpenda mke wake. Haya ni maneno ya uwongo]

[Nina hakika sana. Mtu huyo aliitwa Sheryl Masawe, na binti yake ni mwenyekiti wa Mawenzi Invenstments. Hata nina picha yake.]

Hapo picha za Sherly Masawe zikaanza kusambaa mtandaoni zikiambatana na maneno ya ajabu ya kumdhihaki.

Sura ya: 205

Kisha, picha za Sheryl na Lisa zilienea kwenye mtandao. Lisa alipokea simu kutoka kwa kampuni yake ikisema kwamba Facebook ya Mawenzi ilikumbwa na shutuma nyingi. Bodi ya wakurugenzi ya kampuni hiyo ilikuwa ikipigia kelele kuitisha mkutano tena.

“Nitakuja kwa kampuni mara moja." Lisa aliposema hivyo, Alvin akaichukua simu yake. Kisha akatoa amri kwa upande mwingine, “Mimi ni Alvin Kimaro. Nitashughulikia mambo yote huko Mawenzi. Usimpigie simu na kumsumbua mke wangu kwa muda huu.” Baada ya hapo, akaitupa simu pembeni.

“Alvin, unafanya nini?” Lisa alikasirika sana hadi tumbo lilimuuma. “Hata huwezi kujilinda sasa hivi, unawezaje kujali mambo yangu?”

"Huwezi kuondoka hospitali katika hali hii." Macho ya Alvin yalikuwa ya upole, lakini sauti yake bado ilikuwa kubwa kama zamani.

“Lakini siwezi kusimama tu kutazama picha ya mama yangu inapoenea kwenye mtandao. Amekufa kwa zaidi ya miaka ishirini, lakini bado anasingiziwa mambo ya fedheha.” Machozi yalimjaa Lisa. Kisha, machozi yalishuka chini ya mashavu yake. Alijilaumu. “Yote ni makosa yangu. Sina maana. Sikuweza kulipiza kisasi, na siwezi hata kumwacha mama yangu apumzike kwa amani.”

“Hayo yote hayajatokea kwa bahati mbaya. Yamepangwa na Melanie Ngosha na mama yake.” Alvin alimbembeleza. “Lisa, usilie. Niamini. Nitatafuta mtu wa kuzima mada hii mara moja. Tayari nimefanya maandalizi. Kadiri wanavyoruka ndivyo wanavyozidi kujitengenezea mazingira ya kuanguka kesho.” Alvin akauzungusha mkono wake kiunoni na kuinamisha kichwa chake ili kumbusu kwenye machozi yake. Sauti yake ilikuwa laini.

Akiwa hana raha kutokana na busu lake, Lisa aligeuza uso wake pembeni, na machozi yakakoma. Alikuwa kachanganyikiwa. “Unapanga kufanya nini?”

“Sitakuambia sasa. Ni siri, lakini utajua kesho.” Alvin alikuwa akizipapasa nywele za Lisa kwa kuzirudisha nyuma. “Ngoja nikulishe kwanza.”

Baada ya hapo, alimpa bakuli la supu ambayo Shangazi Yasmini alichemsha. Akapuliza juu yake ili kuipoza taratibu na kumlisha kijiko kwa kijiko. Kila mara alibaki akimwangalia kana kwamba hakuchoka kumuona usoni, lakini, Lisa hakuweza kuvumilia. Alijitazama kwenye kioo akajua ni mbaya, hivyo hakuelewa ni kwa jinsi gani mwanaume huyu hakuwa na kinyongo hata kidogo baada ya kumtazama kwa siku kadhaa.

“Nitakunywa mwenyewe…” Lisa alisema kwa aibu.

“Hapana. Chester alisema kuwa tumbo lako haliko vizuri sasa, na huwezi kunywa chochote kikiwa cha moto sana au baridi, lakini wewe huwa hauzingatii kamwe hivyo ni wajibu wangu kukusimamia." Alvin alisisitiza na kuendelea kumlisha.

Lisa hakuwa na chaguo. Alihisi kuwa Alvin sasa alikuwa akiigiza kama tafsiri ya kitabu cha mtu mwema. Hata hivyo, alihisi kwamba baada ya muda Alvin asingeweza kuukubali uso wake.
•••
Siku iliyofuata, Alvin alikuwa tayari ameondoka wakati Lisa alipoamka. Ilikuwa saa tatu asubuhi, na Aunty Yasmini alikuwa amewasha TV. Mara Lisa alipoinua macho, alimuona Alvin kwenye akihojiwa na mwandishi wa runinga. Hii ilikuwa mara yake ya kwanza kuonekana rasmi kwenye TV.

Kwa nyuma kulikuwa na chumba cha kupumzika, na Alvin alikuwa amekaa kwenye sofa. Alikuwa amevalia suti ya rangi ya kijivu ya gharama iliyoukumbatia mwili wake uliokamilika. Uso wake mzuri, mashuhuri, macho makini yenye haiba ya kujiamini, pua iliyonyooka, na mikono na miguu vyote vilikuwa vya kifahari na vya kupendeza. Aliwakabili watazamaji, na macho yake ya kina yaling'aa kama yamejaa maelfu ya nyota.

Lisa alitazama skrini kwa mshtuko. Wakati huo Alvin alikuwa mtanashati kiasi kwamba hakuweza kumtoa kasoro yoyote. Kando yake, watangazaji mbele ya TV pia walionekana kumshangaa muda wote. Ingawa kila mtu alijua kuwa Alvin Kimaro alikuwa ni mzuri, hawakuwahi kufikiria kuwa mwanaume huyo angekuwa na mvuto wa pekee namna ile kuwa naye karibu.

Mwandishi alisema, “Ni nadra kwa Bwana Alvin Kimaro kukubali mahojiano yetu. Nimejaribu kufanya miadi na wewe mara kadhaa huko nyuma, lakini ulikataa kila wakati. Unaonekana ni mtu ambaye hupendi kuonekana hadharani, kwa hiyo ni sababu gani iliyokufanya kukubali wakati huu?”

Alvin alipishanisha miguu, na sura yake ilikuwa shwari. “Watu wengi wamekuwa wakinikosoa kwenye mitandao siku za karibuni. Kusema kweli, hainisumbui, na sijali jinsi wengine wanavyoniona. Lakini jana walianza kumtusi mke wangu mtandaoni. Hili ni jambo ambalo siwezi kuvumilia…”

Mwandishi alishtuka. "Mke?"

"Kama ulivyosikia." Alvin alitazamana na kamera, na midomo yake ya kichawi ikajikunja na kutabasamu. "Mwenyekiti wa Mawenzi Investments, Lisa Jones. Yeye ni mke wangu.”

Mwandishi alipigwa na butwaa. “Una ushahidi gani? Mna cheti cha ndoa?”

"Kusema ukweli, tuliffunga ndoa zaidi ya miezi minne iliyopita." Alvin alisema kwa kujiamini.

Mwandishi huyo alishangaa. "Hiyo ni ... haiwezekani."

“Ni nini kisichowezekana kuhusu hilo? Cheti hiki hapa nimekuja nacho” Alvin akatoa cheti kwenye faili. Sio tu kilikuwa na picha zao, lakini saiani zao na tarehe ya ndoa pia iliandikwa kwa uwazi. Mpiga picha aliki’zoom kwenye kamera na cheti kikaonekana vizuri kwenye skrini.

Katika wodi, Aunty Yasmini alishangaa sana hata akadondosha machungwa mkononi mwake. “Bi Jones… Hapana… Bibi mdogo, kumbe mmefunga ndoa kabisa?”

Lisa alikosa la kusema. Ndiyo, walikuwa wameoana, lakini pia walikuwa wametalikiana. Alikuwaje bado ana cheti cha ndoa? Kichwa cha Lisa kilianza kudunda. Hakuweza kujua maana ya kitu chochote.

Kwenye runinga, mwandishi pia alichanganyikiwa. “Lakini si ulikuwa bado unachumbiana na Melanie Ngosha kutoka familia ya Ngosha nusu mwezi uliopita…?”
"Kuhusu suala hilo, pia nina hamu sana ya kuzungumza juu yake." Mdomo wa Alvin ukavutwa kwa tabasamu la kejeli. “Melanie Ngosha. Bi Ngosha, kama unatazama habari sasa, nataka kukuuliza tu. Tangu lini nimeanza kukuchumbia? Je, nilianza kukuchumbia kwa sababu tu nilicheza nawe kwenye karamu ya chakula cha jioni huko kwenye makazi ya familia ya Kimaro? Sijawahi kukutongoza au kutangaza wazi kuwa wewe ni mchumba wangu, na nimekuwa wazi kwako tangu mwanzo. Ninaamini mtu yeyote angeweza kusema kwamba sikupendezwa nawe.”

Mwandishi alipigwa na butwaa. "Lakini hapo awali, kuna mtu alikupiga picha mbili ukichuma naye matunda ya strawberry bustanini kwenu. Nyinyi wawili mlionekana kuwa karibu sana…”

“Oh, wakati huo? Niligundua tu kwamba alikuwa pale niliporudi kwenye makazi ya familia. Bibi yangu alinivuta pamoja naye hadi kwenye bustani ili kuchuma matunda na akapiga picha hiyo kwa makusudi ili kupotosha umma. Nilimpelekea mke wangu zile strawberry ili ale. Nilipoondoka siku hiyo nilimweka wazi Bi Ngosha na kumwambia asinisumbue.”

Alvin alitazamana na kamera, macho yake yakiwa yamepoa. “Bi Ngosha, kutokana na maneno yako, Kenya yote inaniona kama mpuuzi. Unapaswa kujua vizuri kwamba sijawahi kuwa mchumba wako hata kidogo.”

Mwandishi alishtuka. "Bwana Mkubwa, familia ya Kimaro inafahamu kuhusu ndoa yako na Bibi Lisa Jones?"

Alvin akatikisa kichwa. “Wanafikiri tu kuwa nachumbiana na Lisa, lakini familia yangu inapinga hilo. Wanafikiri hadhi yake ni ya chini sana kuolewa na mimi, na hanistahili kwa sababu hawezi kuniletea manufaa katika siku zijazo, lakini sijali. Nilikutana naye Dar es Salaam, na hakujua hata hali yangu wakati huo, lakini alinipenda kwa jinsi nilivyokuwa. Siwezi kuvumilia dharau ya familia yangu kwake tena. Nimeamua kuwa nitafanya naye harusi baada ya mwezi mmoja na kila mtu ajue kuwa nina yeye tu moyoni mwangu.”

“Pia…” Alvin alinyanyuka ghafla kwenye sofa. "Ni kweli mimi ndiye niliyevunja mikono ya wale vijana kwenye boti ya kifahari. Sitazungumza kile walichokifanya, lakini hawakupaswa kamwe kumdhalilisha mke wangu. Lisa ni mstari ambao hakuna mtu anayeweza kuvuka. Maadam ninaishi, nipo radhi kweenda kinyume na ulimwengu wote kwa ajili yake.” Wakati akiongea, macho ya Alvin yalikuwa kana kwamba yanamtazama Lisa moja kwa moja mbele ya TV.

Moyo wa Lisa ulikuwa ukidunda kwa nguvu. Ilibidi akubali kwamba hawa na nguvu za kuweza kupinga jambo hilo wakati uso mzuri na mkamilifu wa mwanamume ampendae uliposema maneno yenye kutawala na yenye kusisimua ya upendo. Hata hivyo bado alikuwa na wasiwasi. Alifikiri kuwa labda alikuwa akisafisha sura yake ya kifisadi hadharani. Lisa alibaki akiwa na hisia mchanganyiko baada ya tukio hilo.


Pembeni, Aunty Yasmini alitokwa na machozi. “Bibi mdogo, nilijua Bwana Kimaro alikuwa na wewe tu moyoni mwake, lakini sikutarajia kama angeweza kuwa jasiri na kuutangazia ulimwengu waziwazi namna hii. Inashangaza sana. Jitahidi mapema na umzalie mapacha. Nitakusaidia kuwalea.”

Lisa alikosa la kusema.

Lisa aliongea na tabasamu la hasira usoni mwake. ‘'Anti Yasmine, umesahau kuwa mimi ni mbaya sasa?'’.......ITAENDELEA.....

Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.