JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA..................................202-203
Sura ya:202
“Nilimuuliza Shangazi Kollo mimi mwenyewe, na pia nikaona uso wa Lisa. Yeye ni mwanamke wangu. Unajua jinsi sura ilivyo muhimu kwa mwanamke?" Mikono ya Alvin ilikuwa ikitetemeka kutokana na hasira yake. “Amekukosea nini hasa? Una kinyongo gani dhidi yake?”
“Sijui unazungumza nini, mimi sikufanya lolote.” Valeria alijificha nyuma ya Bibi Mzee na kutetemeka.
“Usifikiri sijui. Ni Nina Mahewa na bintiye walikuambia ufanye hivyo, sivyo? Uko karibu nao sana. Walikuahidi faida gani?” Macho ya Alvin yalichomwa na hasira, kana kwamba angeweza kupoteza busara wakati wowote..
Valeria akijua kwamba hawezi kuficha ukweli, aliuma meno yake na kusema. "Sawa, ikiwa ningefanya hivyo? Alvin, mimi ni mam’dogo wako. Je, utaniua kwa sababu ya mtu wa nje?”
“Yeye si mtu wa nje. Yeye ni mwanamke wangu. Sitakuua, lakini nataka umlipe kwa uso wako.” Alvin alitembea kuelekea kwa Valeria hatua kwa hatua.
“Huwezi kufanya hivyo.” Bibi Kimaro alimtetea Valeria na kusema kwa hasira, “Alvin, shangazi yako ni binti yangu. Ukimdhuru, sitakusamehe kamwe.”
Spencer Kimaro naye aliongea. “Alvin, tulia. Teknolojia ya matibabu imeendelea sana sasa. Tunaweza tu kumpeleka Lisa nje ya nchi na kumpa sura mpya.”
Lea naye alikasirika. “Ukithubutu kumdhuru mam’dogo wako, nitavunja uhusiano wetu wa mama na mtoto.”
“Unafikiri kweli kwamba ninajali uhusiano wetu wa mama na mtoto?” Alvin akamsogeza Bibi yake pembeni na kumsukumia Valeria pale mezani. Akachukua kisu cha matunda.
Valerie aliogopa sana hivi kwamba alitetemeka kama jani linalosukumwa na upepo. “Alvin, usifanye hivyo. Nilikosea. Sitathubutu kufanya tena. Nitaomba msamaha kwa Lisa, sawa?"
“Kama kuomba msamaha kutarudisha sura yake, wacha niuchonge uso wako kisha nikuombe msamaha…” Alvin alitabasamu kwa hasira.
Valeria karibu alowe maji. "Wewe chizi. Bibi na Babu yako hawatakusamehe ukifanya hivyo.”
“Vizuri, mam’dogo Valeria. Hakika nitauchonga uso wako vizuri.” Macho ya Alvin yalimtoka kwa mng'ao wa kichaa, akakizungusha kisu usoni mwake.
“Alvin, acha.” Sauti ya Lisa ilisikika kutoka mlangoni na kumfanya Alvin asitishe zoezi lake. Kila mtu alimtazama na kushtuka alipoona sura yake waziwazi.
Mzee Kimaro akaamuru mara moja, “Lisa, umefika kwa wakati. Mzuie kichaa huyo.”
Lisa alikunja uso kwa kuchukia, lakini bado alienda kumshika mkono.
"Ondoka," Alvin aliamuru, hakutaka kuona upande wake wa kikatili.
“Sihitaji ulipize kisasi,” Lisa alisema kwa sauti ya chini. "Mbali na hilo, sio yeye ambaye anataka kuniumiza."
“Ndiyo ndiyo, nilikuwa nimepagawa kwa muda tu.” Valeria alidakia kwa haraka.
"Ninajua. Haijalishi ni nani, nitawalipa mmoja mmoja, nikianza na wewe." Alvin alibaki bila wasiwasi.
“Yeye ni familia yako. Sitaki… sitaki upoteze familia yako kwa sababu yangu. Mimi sina thamani.” Lisa alimkazia macho.
Alvin alishikwa na butwaa. Ingawa sura ya mwanamke huyo iliharibiwa, maneno yake bado yangeweza kugusa moyo wake kama hapo awali.
"Hapana, unastahili." Alisema kwa sauti ya chini.
Lisa alinyamaza kwa muda kabla hajashusha macho yake. “Fikiria bibi yako. Akimwona mjukuu wake akimdhuru bintiye, unafikiri ataweza kuvumilia? Yeye tayari ni mzee sana."
Alvin aliduwaa na kugeuka nyuma kumtazama Bibi Kimaro aliyekuwa akimwangalia kwa macho ya kusihi. Kisu mkononi mwake kikalegea, na Valeria akatoroka haraka kana kwamba ameokolewa.
“Njoo, twende nyumbani.” Lisa alimshika mkono.
‘Nyumbani?’ Sehemu ya maumivu ilitanda kwenye uso mzuri wa Alvin.
Hapo zamani za kale, hiyo ilikuwa nyumba yake, lakini, mahali pekee palipoonekana kama nyumbani kwake sasa ni pale alipokuwa pamoja na Lisa.
“Sawa.” Baada ya muda mrefu, Alvin alitikisa kichwa. Alimshika na kuwaacha akina Kimaro bila kuangalia nyuma.
Valeria alipoona umbo la Alvin lkitoweka, alitetemeka na kusema, “Mama, Baba, nadhani ni lazima Alvin atakuwa mgonjwa tena. Alikuwa anatisha sana sasa hivi. Ilikuwa kama kipindi kile alipokuwa akiwaumiza wengine…”
“Imetosha.” Bibi Kimaro alimpiga kofi usoni kwa kukata tamaa. “Vipi una ujasiri wa kusema hivyo? Hutosheki kwa familia ya Kimaro? Unawezaje kuhongwa na watu wa nje kufanya mambo ya ajabu namna hii?”
Jack kwa hasira alimshutumu pia. "Mam’dogo Valeria, wewe ni mkatili sana."
Kwa aibu, Valeria alikunja ngumi kwa huzuni. Alimchukia sana Alvin mpaka meno yalimuuma. Alipanga kulipiza kisasi naye.
•••
Gari lilipanda kwenye miinuko ya Mlima wa Sherman. Hans aliendesha gari huku Alvin akiendelea kutazama mwili wa Lisa uliochoka. Lisa alijua jinsi uso wake ulivyokuwa wa kutisha na alikasirishwa na kutazamwa kwake. “Si lazima uchukue nilichosema mapema kwa uzito. Sikutaka tu umdhuru Valeria na kugombana na familia ya Kimaro. Ikiwa jambo fulani litatokea kwako, ninaweza kufungwa kwenye jela ya familia yenu tena au sehemu mbaya zaidi.”
“Najua." Alvin alipandwa na hasira, lakini alirudi katika hali yake ya kawaida haraka. Hakuwahi kufikiria kwamba Lisa angemsamehe kirahisi hivyo baada ya tukio hilo lenye kuumiza. Alijihisi hatia kubwa kwamba alikuwa hana maana kabisa kwa Lisa. Alidai kwamba angemlinda, lakini mwishowe, hakuweza kufanya hivyo. Maumivu makali ya moyo yalishika moyo wake. Mkono wake ukatetemeka kwa nguvu tena kana kwamba anakaribia kushindwa kujizuia.
“Simamisha gari.” ALvin alitoa amri ghafla. Hans akasogea mara moja.
“Mpeleke hospitali. Nitaenda kwenye gari la nyuma kwa ajili ya kuvuta sigara.” Alvin alishuka haraka kwenye gari.
Hans alimtazama kabla hajaondoa gari na Lisa akamtazama kwenye kioo cha nyuma na kumwona akiingia kwenye gari la nyuma yao. Kisha akacheka na kusema, “Hans, ninanuka! Ni lazima iwe vigumu kwake kuvumilia.”
Lisa alicheka. Mazingira ya jela yalikuwa ya kuchukiza sana, lakini alikula, kunywa, na kulala katika chumba kila kila siku. Zaidi ya hayo, hakuweza kuoga wala kupiga mswaki. Hata yeye hakuweza kustahimili uvundo uliokuwa umeenea kwenye gari.
Hans alieleza kwa haraka, “Bi Jones, haukuelewa. Bwana Mkubwa Kimaro…” Alisita ghafla baada ya kukosa maneno sahihi. Asingeweza kumwambia kwamba Alvin alikuwa mgonjwa na alihitaji kwenda kwenye gari lingine kuchukua dawa yake au labda ... kujidhuru tena ili kupunguza hasira yake!
“Si lazima unifafanulie. Najua.” Lisa aliona jinsi Hans alivyokuwa akijaribu kutafuta kisingizio cha kumtetea Alvin lakini hakuweza. Hans alikuwa hoi. Alijua Lisa hakuelewa ni kwa kiasi gani Alvin alimjali.
Sura ya:203
Baada ya kufika City General Hospital, Chester alipanga madaktari bingwa hospitalini wamfanyie Lisa uchunguzi wa kina wa kimwili. Matokeo yalitoka haraka sana.
Chester alimtazama Lisa aliyedhoofika pale kitandani akihema kwa huruma. “Viashiria vyote haviko kwenye kiwango. Hypoglycemia, upungufu wa damu, upungufu wa maji mwilini, utapiamlo, na kidonda cha peptic.”
Lisa aliitikia kwa kichwa. Mwili wake ulikuwa wake mwenyewe. Nyakati hizo mara nyingi alikuwa akitapika na kusumbuliwa kwa maumivu ya tumbo, kwa hiyo alijua yote hayo.
Alvin alikunja ngumi kwa hasira iliyochanganyikana na huzuni. Alijua kwamba Lisa hakuwa na afya nzuri, lakini sasa hali yake alikuwa imezidi mbaya zaidi.
“Pole sana Lisa, unapaswa kupumzika kwanza.” Chester ghafla akamwambia Alvin, “Njoo uchukue dawa…”
“Dokta Choka, unaweza kusema lolote mbele yangu, hata kama linahusiana na uso wangu…” Lisa alitabasamu kumtazama. "Huna haja ya kunificha."
Chester alimtazama kwa huruma. "Sawa, kusema ukweli, majeraha usoni kwako yamekuathiri sana. Nimewasiliana na wataalamu kadhaa wakubwa wa ngozi, na watafanya kadiri wawezavyo kukurekebisha, lakini… si rahisi kwa sura yako kurudi kama hapo awali.”
"Dokta Choka, unaweza kueleza kwa undani zaidi?" Lisa alimtazama.
Kadri Alvin alivyoona jinsi alivyokuwa mnyonge na mwenye wasiwasi ndivyo moyo wake ulivyozidi kumuuma. “Hakuna haja ya kumuuliza. Ikiwa teknolojia ya hapa haitoshi na huwezi kurekebishwa ndani ya nchi, tutaenda ng'ambo. Teknolojia ya urembo hapa nchini sio ya kiwango cha kimataifa.”
"Sitaki kufanyiwa upasuaji wa plastiki kwa ajili ya uso mpya." Lisa akamkatisha.
Alvin aliifuta miwani yake na kumwamngalia kwa udadisi. "Kutakuwa na makovu yanayotofautiana."
"Naelewa." Lisa aliitikia kwa kichwa na kuegemea mto. "Asante kwa kujali lakini nitaridhika na matokeo."
"Usijali. Teknolojia inakua kwa kasi sana sasa, kwa hivyo hupaswi kukata tamaa.” Chester alimfariji.
'Ni sawa. Lakini haina haja." Lisa alikuwa na tabasamu hafifu usoni mwake tangu mwanzo, lakini mtu yeyote mwenye jicho la utambuzi angeweza kusema kwamba hakuwa na matumaini tena. Alikuwa amekata tamaa na kujisalimisha kwa hatima yake. Hakujali tena.
Macho ya Alvin yakafifia, akamwambia Chester, “Kwanini usitoke kwanza?”
“Sawa.” Chester alitoka na kufunga mlango.
Alvin akasogea karibu na kitanda chake na kumshika Lisa mkono kwa nguvu. Macho yake meusi yalikuwa mazito. “Haijalishi unaonekanaje, sijali. Ninakupenda wewe, sio uso wako."
"Ni kweli?" Lisa alitazama mavazi yake mapya. “Usijidanganye. Ulinikumbatia mwanzoni, lakini tayari umebadilisha nguo zako. Na kwenye gari ulinikimbia kwa sababu niilikuwa nanuka. Alvin, wewe kweli ni mwigizaji mashuhuri, unalijua hilo?”
“Hapana… sivyo…” Kwa mara ya kwanza, Alvin alijihisi kama mtoto. Alikuwa katika hali ya kutojielewa. Asingeweza kumwambia kwamba alikuwa amejiumiza na kulowesha nguo zake kwa damu kwa sababu ugonjwa wake ulimchukua tena. Ilimbidi abadili nguo safi kwa sababu nguo zake zilikuwa zimetapakaa damu. Ikiwa angejua kwamba alikuwa mgonjwa, angemwogopa hata zaidi.
“Huwezi hata kujieleza vizuri,” Lisa alisema kwa mzaha. “Alvin, kwa kweli sina huzuni kwamba sura yangu imeharibika. Kwa kweli, nina furaha. Ni jambo jema. Sasa kwa kuwa mimi ni kituko na mwenye kuchukiza kiasi cha kuwafanya watu wacheke, bado unaweza kulala kando yangu? Tunapaswa tu kuachana kwa nia njema sasa. Angalau nipe hadhi hii ya mwisho."
Alvin alikasirika. "Lisa, mimi sio mtu wa juu juu kama unavyofikiria. Nitakuthibitishia sasa hivi.”
Alvin alimvuta Lisa kwa nguvu mikononi mwake na kuifunga midomo yake na ile ya Lisa iliyokuwa imepasuka kwa vidonda. Vidonda bado vilikuwa vikitema majimaji ya usaha, na uso wake bado ulinuka vibaya kutokana na majeraha. Kusema kweli, hata Lisa mwenyewe alijionea kinyaa. Lakini, mwanamume huyu alimshika kama vile alikuwa ameshika tunda tamu lenye harufu nzuri. Busu lake lilikuwa la upole na la huzuni. Alvin alimbusu Lisa mpaka akajihisi kama anakata roho.
Busu lilipoisha, midomo yake ilianguka kwa upole kwenye jeraha kwenye shavu lake kama manyoya. Mabusu ya upole yalimpa Lisa hisia kali.
Ni kana kwamba alimpenda sana kiasi cha kutojali sura yake. Hata hivyo… Lisa bado alijiuliza. Hiyo inawezaje kuwa kweli? Ni wangapi kati ya wanaume kama hao walikuwepo katika ulimwengu huu? Hasa mwanaume mzuri kama Alvin alivyokuwa? Hata kama hakuwa yeye tena aliyesimama juu ya ufahari wa familia yao, wanawake wengi bado walikuwa tayari kujirusha kwake.
"Inatosha." Lisa aligeuka na kufunika macho yake. “Alvin, usijilazimieshekufanya hivi. Utaishia kukimbilia kutapika chooni baadaye.”
“Haijalishi. Nitaishi maisha yangu yote kukuthibitishia hilo.” Alvin akambusu paji la uso wake. “Chester alisema huwezi kula chakula kigumu kwa sasa kwa sababu tumbo lako haliwezi kumeng’enya. Nitakuletea chupa ya maziwa ya moto.” Akainuka na kwenda jikoni.
Mlango wa wodi ulisukumwa, na Pamela mara moja akaingia ndani kwa kasi. Alipomwona tu swali likamtoka moja kwa moja. "Kwa nini uso wako ..."
"Pamela, nimeharibika?" Lisa alitabasamu.
“Kumetokea nini?” Pamela alizidi kuhoji kwa mshangao. “Sikuweza kukupata kwenye simu siku hizi zote. Hata nilipiga simu polisi.” Pamela alianza kulia ghafla. “Kwanini Mungu anakutendea hivi? Ulikuwa mzuri sana, mrembo zaidi tulipokuwa shuleni. Wavulana walikutazama bila kujali ulienda…”
“Inatosha. Sikukuita hapa kuzungumza mambo ambayo yangemhuzunisha.” Alvin alimkabidhi Lisa maziwa na kumkatisha Pamela kwa ukali.
Pamela alipandwa na hasira baada ya kumuona Alvin. Moto machoni mwake ukawaka. “Sihitaji hata kukisia. Lazima utakuwa unahusika kwenye madhara yaliyomfanya awe hivi. Kufikiri kuwa wewe ndiye mtu tajiri zaidi nchini Kenya kuna kupa jeuri sana Alvin. Ukiniuliza, wewe ni kipande cha takataka ambacho huwezi hata kumlinda mwanamke. Kuna faida gani ya wewe kuwa naye? Unapaswa kuishi maisha yako yote peke yako."
“Pamela…” Lisa alikuwa na wasiwasi kidogo. Ingawa aliona maneno ya Pamela yakimfurahisha, aliogopa kwamba Pamela angemkera Alvin.
“Wewe...” Ilikuwa ni mara ya kwanza Alvin kukaripiwa vikali hivyo na mwanamke tofauti na Lisa. Hasira ilimpanda tumboni mwake, lakini hakuweza kuiruhusu imtawale kichwani.
"Nini? Nimesema chochote kibaya?" Pamela aliendelea kumlaani huku macho yake yakiwa mekundu. “Lisa wangu bila shaka ni mrembo sana, angeweza kuolewa na mwanaume anayempenda na kumlinda, lakini sasa ameharibika kabisa. ”
“Hajaharibika nitamuoa,” Alvin alisema.
“Hah unataka kumuoa kisha umtupe tena baada ya siku chache, huoni talaka uliompa mara moja tayari inatosha? Ulishindwa kumpenda alipokuwa na sura yake, utampenda sasa akiwa hivi?" Pamela hakumuamini hata kidogo, machoni mwake Alvin alikuwa akiigiza tu kutokana na dhamiri yake mbaya,
“Pamela Masanja, unathubutuje kumkemea Alvin hivyo?” Kutokea mlangoni mara sauti ya mtu mwenye hasira kali ilisikika.
Pamela alitazama nyuma na kuona kuna vijana wawili wakiingia mlangoni, mmoja alikuwa Sam Harrison na mwingine alivaa shati la rangi ya pinki, kijana mzuri lakini macho yake yalikuwa yamejaa moto wa hasira. Ni yeye ndiye aliyesema maneno hayo.
"Oh, ni wewe." Pamela alimkumbuka. Aliwahi kumuona pale alipoenda hotelini kukutana na Alvin. Alikuwa akicheza karata na Alvin enzi hizo, lakini hakukumbuka kuwa alikuwa msumbufu namna hio. Aliwahi kumuona pia wakiwa na Lisa mgahawani siku moja. Anaitwa Rodney Shangwe.
Rodney alidhihaki kwa ujeuri na alikuwa anakaribia kuongea lakini Pamela ghafla akapaza sauti akamwambia, “Ziba mdomo wako. Nyote ni kundi la mbwa mwitu. Ndege wa aina moja huruka pamoja.”
"Umesema nini?" Rodney alikasirika. "Wewe mwanamke mjinga. Unajua mimi ni nani?"
"Mjinga? Nadhani wewe ndiye mjinga. Sina hata haja ya kujua wewe ni nani. wewe ni kipande cha takataka tu ... " Kwa kuwa Pamela hakumpenda Alvin, pia hakuwapenda marafiki zake.
Lisa alikuwa na wasiwasi sana kwa sababu alimjua Rodney ni nani.....ITAENDELEA.....
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.
