JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA...............................196-197

Sura ya:196

Alvin alishikwa na butwaa. Alimuachia Lisa na kupiga hatua mbili nyuma. Mikono yake ilikuwa ikitetemeka, na haikuonekana kama ilikuwa karibu kuacha.

Lisa alitazama nyuma na kumtazama kwa woga. “Alvin, unaweza kuwa hujui, lakini siku zote lazima niwe makini ninapokuwa na wewe. Wewe ni mtu wa kiburi, wa kutisha, na mwenye hasira sana. Nina wasiwasi kila wakati kwamba nitaishia kuwamhanga wa hasira zako. Kwangu mimi, wewe ni shetani. Umeona mtu yeyote akiangukia kwa shetani?!”

“Inatosha. Acha!" Kwa macho yenye damu, Alvin alifagia kifungua kinywa chote kilichokuwa mezani hadi sakafuni. Hakuwa na nia ya kumuumiza, lakini kwa nini ilimbidi kumchokoza hivi? Kama binadamu, moyo wake ungeumia pia.

Alipokaribia kushindwa kujizuia, alifungua mlango kwa nguvu na kuondoka. Harakaharaka akaingia ndani ya gari na kuchukua dawa kwenye chupa mara moja. Hata hivyo, hiyo haikutosha kwake. Kwa kuhofu kwamba hasira zake zisingeweza kushuka haraka, alichukua wembe na kujikata mkono. Maumivu yaliyompata yalipunguza hasira zake kwa kiwango fulani.

Katika chumba cha chakula. Lisa alitazama kwa huruma pale sakafuni, na ushanga wa jasho ukamtiririka kwenye paji la uso wake.
Macho ya Alvin yalikuwa ya kutisha sana. Alihisi kana kwamba alikuwa ameonana na shetani mwenyewe.

Kwanini Alvin alikuwa na hasira hivyo? Alikuwa akitaniana naye kwa upole dakika moja, na iliyofuata aligeuka kuwa mbogo. Kwanini hakutambua upande wa kutisha wa Alvin hadi wakati huo?
Hapana, ilimbidi aondoke. Asingeweza kuolewa naye tena kwa uhakika!

Lisa alipogeuka, ghafla alimuona Aunty Yasmini akiwa amesimama kwenye mlango wa jikoni, akitazama tukio hilo kwa wasiwasi.
Alitaka kumfumbia macho lakini ilibidi amwambie ghafla, "Bi Jones, tafadhali usimkasirishe Alvin zaidi."

“Najua. Sitathubutu kufanya tena.” Lisa alilazimisha tabasamu la kujidharau kwenye uso wake uliopauka.

Shangazi Yasmini aliogopa sana. Alitaka kumweleza kwamba Alvin alikuwa na ugonjwa, ugonjwa mbaya sana wa kupoteza udhibiti wa hasira zake. Hata hivyo, kama angemwambia ukweli, Lisa si angemwogopa moja kwa moja Alvin?

•••
Hospitalini. Akiwa anaufunga mkono wa Alvin, Chester aliutazama uso wake uliopauka na mzuri na kusema. "Ni Lisa ndiyo kakusababishia hali hii?"

"Sikutaka kuzidiwa na hasira na kumuumiza tena." Alvin alitazama nje ya dirisha. Alipokumbuka maneno ya kuumiza ambayo Lisa aliyasema, alianza kuchemka kwa hasira tena. Kwa nini mwanamke huyo alidai kuwa hana hisia naye tena baada ya kmnunulia pete ya uchumba na kuonesha nia ya kumuoa?

“Haya, inatosha. Tulia. Nimefunga mkono wako sasa hivi, na damu inavuja tena.” Chester alilazimika kuufungua tena mkono wake.

"Unaweza kuniongezea kipimo cha dawa?" Sura ya kero ikamtoka Alvin.

"Itaharibu tumbo lako zaidi," Chester alijibu kwa mshtuko. "Hata hivyo, ni muda gani haujapata mlo mzuri?"

Alvin aliinua midomo yake na kusema kwa huzuni, "Sitaki kulazwa tena katika hospitali ya magonjwa ya akili."

Akiwa amepigwa na butwaa, Chester akajibu kwa huruma, “Au… unaweza kumjulisha Lisa kuhusu ugonjwa wako na kwamba hukukusudia kumuumiza…”

“Ushauri gani huo, si itamfanya aniogope zaidi?” Kana kwamba Alvin alikasirishwa, aliongeza kwa uchungu, “Umesahau jinsi kila mtu alinichukulia kama mgonjwa wa akili niliposhindwa kujizuia zamani? Wote walitamani nifungwe, na yeye lazima atakuwa hivyo. Hakuna mtu atakayenipenda na ugonjwa wangu.” Kumsikiliza Alvin, Chester alihisi kukosa raha.

Mara baada ya bandeji kufungwa, mlango ukapigwa kwa nguvu. Rodney aliingia ndani. Alipoona majeraha ya Alvin mkononi mwake, alisema kwa uchungu, “Uko sawa, Alvin? Kuishia katika hali hii yote kwa ajili ya mwanamke?”

"Hili ni jambo langu la kibinafsi," Alvin alisema bila kujali.

“Nakuchukulia kama kaka yangu,” Rodney alisema kwa kuudhika. “Angalia Jack amefanya nini. Yeye ndiye aliyeongeza mafuta kwenye moto kwenye Mtandao na kusababisha kila mtu kukuchukia. Hata zile familia zenye ushawishi zilizokuwa zikikustaajabisha na kukuheshimu zinakukwepa kana kwamba wewe ni ukoma. Uko sawa kwa kila mtu kumpendelea Jack sasa?"

Chester alicheka. “Rodney, una hasira kupita kiasi. Unaona Alvin anaonekana kama mtu anayeshindwa kwa urahisi?”

“Lakini…”

“Si rahisi kwa Jack kuchukua kiti cha mwenyekiti wa KIM International.” Chester akahamishia macho yake kwa Alvin.

Alvin alitabasamu. “Wewe ndiye unanifahamu zaidi.”

Rodney akawa mnyonge. “Sawa. Mimi ni mtu mwenye shughuli nyingi. Ulinipiga hata kwenye boti juzijuzi.”

“Uliyataka mwenyewe…” Alvin alijibu bila kujali.

Rodney alishindwa cha kusema. Alikuwa amekasirika sana.

“Sawa. Tujaribu kusahau kuhusu mambo yasiyofurahisha. Rodney alisafiri kwa ndege hapa kutoka Dar es Salaam alipopata habari kwamba jambo baya limekutokea. Tukutane usiku wa leo.”Chester alisema.

Alvin alibaki na uso usio na wasiwasi. “Kuna faida gani ya yeye kuja hapa, kwani atanisaidia nini?”

"Kunywa na wewe." Chester alionyesha tabasamu la meno ya lulu. "Kunywa kunaweza kusaidia kupotezea huzuni za mtu."

•••

Nyumbani kwa familia ya Ngosha. Wakati Nina alipogundua kuwa Alvin alikuwa amemnunulia Lisa kipande cha vito chenye thamani ya shilingi milioni 15 za kenya, ambazo ni sawa na milionizaidi ya mia tatu za Kitanzania, alikasirika sana hadi akavunja mitungi ya maua sebuleni.

“Kuna kitu kibaya sana kwa Alvin. Melanie alimtendea vizuri sana, hata hivyo alichagua kuoa binti asiye halali. Ahhhh. Lisa, unastahili kufa kama mama yako.” Nina alilalamika.

“Inatosha. Maneno yako ni makali sana." Joel hakuweza tena kuvumilia tabia yake.

“Joel, wewe ni takataka zisizo na maana,” Nina alimkosoa huku akionyesha pua yake. “Kuna mtu alimpokonya mpenzi wa binti yako na kumdhulumu, lakini huwezi kufanya lolote kumsaidia. Sasa Melanie na Farres wamefungiwa katika kituo cha polisi, huwezi hata kuwapa dhamana. Wewe ni mwanaume wa aina gani?”

"Angalia mdomo wako, Nina." Joel alikuwa akihema kwa hasira. Ilimjaa chuki kumtazama Nina ambaye alionekana kama mwanamke kichaa wakati huo.

“Nimekosea kusema hivyo? Wewe ni dhaifu, na ndiyo sababu Melanie alidanganywa. Ikiwa hutamuokoa, basi nitatafuta njia ya kutokea.”

Kwa hayo Nina aliendesha gari hadi nyumbani kwa akina Kimaro. Mzee Kimaro aliionea huruma familia ya akina Ngosha, akajaribu kufikiria namna ya kuwaweka dhamana Melanie na Farres kutoka kituo cha polisi.

Siku ambayo Melanie aliachiliwa, alimkumbatia Nina na kulia kwa uchungu. “Mama, Alvin amekwenda mbali sana. Hajawahi kuninunulia hata bangili tu, lakini alitumia pesa nyingi kumnunulia Lisa pete ya uchumba. Nataka kumuua Lisa.”

Nina akasaga meno. “Bila shaka, nitampeleka kuzimu kukutana na Sheryl. Hata hivyo, cha muhimu zaidi kwa sasa ni kukupa kilicho bora zaidi…”

“Mama, napenda tu kuwa na Alvin milele,” Melanie alijibu huku akiwa analia.

“Nyamaza,” Nina alisema kwa hasira. “Mbona bado unamfikiria ingawa alikudhalilisha? Fikiri vizuri. Lakini sitamwacha awe na amani na ndoa yake kwani alitudhalilisha sana safari hii.”

“Mama una mpango gani? Ndiye mrithi wa familia ya Kimaro. Hatuwezi kumudu kumkasirisha…”

Nina alisema kwa upole, “Unafikiria kupita kiasi. Alvin Kimaro hana ushawishi tena kama alivyokuwa hapo awali. Hivi karibuni, atasusiwa na familia zote za kifahari jijini Nairobi, na mustakabali wake utakuwa hatarini.”

Melanie alipigwa na butwaa. “Mama sijui unasema nini. Kwanini familia za watu mashuhuri zinamsusia…?”

“Utajua juu yake muda si mrefu. Familia ya Kimaro inakuonea huruma, kwa hiyo wao binafsi wameahidi kukupangia ndoa. Ni Jerome Campos kutoka familia ya Campos.”

Farres alishangaa na kufurahi. "Jack ndiye mwenyekiti wa KIM International. Zaidi ya hayo, Jerome ni binamu wa Jack na pia mpwa wa Lea, kwa hivyo atakuwa na wakati ujao mzuri. Zaidi ya hayo, hali ya familia ya Campos inalinganishwa na hadhi ya familia ya Ngosha.”

Sura ya:197

“Ni nzuri sana. Jerome ni mtu mwenye heshima hata hivyo.” Nina alimtazama Melanie aliyekuwa ameduwaa. “Achana tu Alvin. Alikufedhehesha mbele ya kila mtu, lakini alijuta baadaye?"

Melanie alirudi kwenye fahamu zake ghafla. Hakika Alvin alikuwa akimdanganya. Hata alimwacha ateseke katika kituo cha polisi. Alimpenda sana, lakini aliishia kuwa kicheko! Ahi! Bila shaka angemfanya ajute na kuomba msamaha! Pia angemuweka Lisa kuzimu!

Mara baada ya Melanie kutoka nje ya kituo cha polisi, kundi la waandishi wa habari lilikuwa tayari likimsubiri nje kumhoji. Wakati huo, alionekana kama mtu mwingine. Machozi yalikuwa yakimlenga lenga usoni mwake.

Waandishi walimkimbilia na kumuuliza, “Bi Jones, kuna tetesi kwamba ulimshika Bwana Alvin Kimaro na yule mchepuko wake wakiwa wamelala pamoja usiku wa tamasha la hisani la KIM International. Je, hii ni kweli?”

“Achana na hizo habari.” Tabasamu la kusikitisha likapita usoni mwa Melanie. “Sitaki kuzungumzia alichokifanya Bwana Kimaro kwa sababu nimempenda kwa muda mrefu sana. Nilifurahi sana hatimaye nilipopata kuwa naye. Ninachoweza kusema ni kwamba niliangukia kwa mtu mbaya, lakini simlaumu. Namtakia maisha marefu yenye furaha.”

“Wewe ni mkarimu kweli Bi Ngosha. Bwana Alvin Kimaro hastahili kuwa na wewe. Je umepanga kumlipiza kisasi?” Mwanahabari mmoja wa kike aliuliza.

“Sina uhakika kama nitafanya hivyo, lakini nimechoka sana kwa sasa. Ushauri kwa kwa mabinti ni kwamba natumai kila mwanamke atajilinda, haswa mioyo ya wengi ipo hatarini."
•••
Ofisini, Lisa alipotazama mahojiano ya Melanie kupitia simu yake, alikunja uso.

Mahojiano ya Melanie yalikuwa yamepata huruma na upendeleo kutoka kwa wafuatiliaji wote. Wanaume walimsifu kwa kuwa na akili nyingi za kihisia na kujizuia, binti anayeishi kulingana na sifa yake kama mwanamke mchanga kutoka familia ya kifahari. Wanawake walimsifu kwa kuwa msamehevu na mkweli. Walimwona kuwa msichana mwenye huruma, asiye na hatia ambaye Alvin hakustahili kuwa naye na alistahili mtu bora zaidi.

Hata hivyo, Lisa alimini kwa kuzingatia kutokuwa na busara kwa Melanie, ilikuwa nje ya uwezo wake kutoa maneno hayo ya busara. Lazima kulikuwa na mtu aliyempanga kusema hivyo na pia kulikuwa na kitu kilikuwa kinaendelea nyuma ya pazia.

Akiwa katikati ya mawazo hayo, Lisa alishtushwa na simu yake ikiita. Pamela alikuwa amempigia simu ili kumsengenya Melanie. “Si Melanie anampenda Alvin? Kwanini kamgeuka na kuongea maneno hayo ya kumsukuma Alvin kwenye shimo?”

“Una wasiwasi naye?” Lisa aliuliza.

“Hapana! Ninaogopa kwamba ungekuwa na wasiwasi juu yake badala yake.”

"Hapana siwezi." Lisa alikanusha bila kujua. "Kadiri anavyozidi kuwa duni, ndivyo uwezekano wa mimi kutoroka makucha yake kama shetani unavyokuwa mkubwa."

“Sawa. Kweli, cha kushangaza, watu wana hamu ya kujua ni nani mpenzi mpya wa Alvin licha ya ugomvi huo. Cha kushangaza ni kwamba vyombo vya habari havikufichua habari zozote kuhusu wewe na Alvin, tangu mlipokuwa Dar es Salaam. Habari zako zimefichwa makusudi ili kumpa nguvu Melanie kukukosoa vikali zaidi.”

Akiwa ananyoosha midomo yake, Lisa alifahamu hilo pia. Kufikia wakati huo, aliamini kuwa ni Jack Kimaro ambaye alipanga kila kitu nyuma ya tukio hilo. Je, hakutaka kumfunua Lisa kwa sababu alimhurumia, au aliogopa kuingizwa katika jambo hilo?
Hata hivyo, Jack asingemsumbua Lisa kwa lolote. Jack alidharaulika zaidi kuliko Alvin. Alvin alikuwa jeuri dhahiri, lakini Jack alificha ubaya wake vizuri sana. Watu kama yeye walikuwa wepesi zaidi kushughulika nao.

Pamela kisha akasema, “Hata hivyo, Alvin anachukuliwa kuwa mwanamume halisi. Kwa kweli, angeweza kufichua utambulisho wako na kudai kwamba ulimtongoza, basi asingekosolewa vibaya hivyo. Lakini alichagua kunyamaza juu yake…”

Lisa alipandwa na hasira. “Wewe ni rafiki yangu au rafiki wa Alvin?”

“Hehe. Nadhani ukweli kwamba mwanamume hajali kupoteza kampuni, hadhi na sifa yake kwa ajili yako inaonyesha kwamba anakupenda kweli. Nilidhani mtu wa aina hii hayupo tena.” Lisa alikosa la kusema. Wimbi la hisia liliishinda akili iliyolegea ya Lisa.

“Kusema ukweli, sidhani kama Patrick ananipenda hata kidogo nikimlinganisha na Alvin sasa…”

“Lazima nifanye kazi. Kwaheri kwa sasa." Lisa alichukizwa sana na maneno ya Pamela.

Lisa alirudi New Metropolis Park baada ya kufanya kazi kwa muda wa ziada hadi saa mbili usiku. Hata hivyo, Alvin hakuwa amerudi bado.
Baada ya kuoga alijilaza kitandani na kuangalia simu yake. Alibofya bila kufahamu kukutana na habari inayovuma kuhusu Alvin. Wakati huu, video ilikuwa imetolewa. Tukio hilo lilionekana kufahamika. Ilikuwa ni usiku ambao aliburutwa hadi kwenye boti ya Rodney.

Katika video hiyo, Alvin alionekana akiwa amembeba wakati Bwana Mdogo Kelly alipouliza, “Bwana Mkubwa, tumekuchokoza vipi?” Rodney alisema, “Mimi ndiye niliyewaita, Alvin. Njoo tu kwangu ikiwa una shida na hilo."

Alvin alijibu, “Kuhusu tukio la usiku wa leo… Ikiwa mtu yeyote atakuwa na ujasiri wa kutosha kueneza neno moja, picha au video, nitahakikisha kwamba familia yake yote inatoweka Kenya. Pia, wale ambao walimgusa hivi sasa hawaruhusiwi kuondoka hadi uvunje mkono wake mmoja. Kunapaswa kuwa na kamera za uchunguzi kwenye yacht."

Baada ya Alvin kumbeba na kuondoka, mkono wa kila bwana mdogo ulivunjika. Wengine walilia kwa uchungu, huku wengine wakipiga magoti wakiomba msamaha. Eneo la tukio lilikuwa la kusikitisha sana. Video hiyo ilikuwa imetazamwa mara milioni mbili tangu ilipotolewa.

[Mwishowe ninatambua kwamba Alvin Kimaro ni fisadi kuliko hapo awali. Ana kiburi sana. Anastahili kuadhibiwa.]

[Alvin Kimaro haziheshimu hata kidogo familia za kifahari jijini Nairobi. Enyi familia za waheshimiwa, jitokezeni mseme jambo.]

[Ni nani aliyetoa video hii? Alvin Kimaro atahukumiwa maisha, na yote ni kazi yake mwenyewe.]

Kufuatia hayo, familia ya Kelly ilitangaza hadharani. [Tutachunguza suala hilo kuhusu kitendo cha Bwana Kimaro kwa Kijana wa Kelly.]
Familia ya Morice ilisambaza ujumbe huo muda mfupi baadaye. [Tutalichunguza pamoja na familia ya @the Kelly]

Baadaye, familia tisa zenye ushawishi kutoka Nairobi zilisambaza ujumbe kama huo. Baada ya Lisa kusoma meseji zote, kichwa kilikuwa kikiunguruma. Kifua chake kilikuwa kimembana sana kiasi cha kuhisi anakosa hewa. Watu wengine wanaweza wasielewe kilichotokea, lakini yeye alikuwa anaelewa.

Hakuweza kusahau tukio lile la kufedhehesha kabisa usiku huo.

Alifikiri kwamba Alvin na Rodney walikuwa wameungana kumfundisha somo usiku huo. Ndiyo maana aliweka kinyongo dhidi ya Alvin tangu wakati huo. Lakini, iliibuka kuwa hakuwa na habari juu yake. Ili kuwafundisha wale vijana waliomgusa somo, hata alivunja mikono yo. Pia aliwataka wafute picha na video hizo usiku huohuo.

Kwa kweli alikuwa akimlinda, lakini hakumwambia ukweli. Alijiuliza Alvin ni mtu wa aina gani? Wakati huo maneno ya Pamela yalimshtua. Kwake, hakujali kupoteza kampuni yake, hadhi, na sifa. Hata alienda kinyume na familia zote tajiri jijini Nairobi kwake.

Kenya nzima tayari ilimdharau Alvin. Sasa familia za kitajiri jijini Nairobi zilipokuwa zikienda kulichunguza suala hilo, Lisa hakuthubutu kuwaza kitakachompata Alvin. Je, angeenda jela? Je, maisha yake yangehukumiwa? Lisa alishindwa kuzuia wasiwasi wake, akapiga namba ya Alvin.....ITAENDELEA...

Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.