JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA...............................194-195
Sura ya:194
“Ina maana hujaona habari zinazovuma sasa hivi kwenye mitandao?” Chester akamsogelea. “Ni habari za kusisimua zaidi. Watu wote wanazungumza juu yake."
Lisa alipoteza mawazo kwa muda. Alijua kwamba Chester hamdanganyi, lakini hakufikiri kwamba Alvin alifukuzwa kwenye kampuni ya familia kwa sababu alitaka kumuoa. “Hiyo ni kawaida sana. Mwenendo wake haukuwa sahihi. Alikuwa na rafiki wa kike lakini bado alimnyakua kwa nguvu dada mkubwa wa mpenzi wake pia. Hakuweza hata kutawala sehemu ya chini ya mwili wake na kuharibu chakula cha jioni cha hisani kilichokuwa na familia ya Kimaro. Baada ya kufanya vitendo hivyo vya kuchukiza, bila shaka, ataondolewa kwenye nafasi yake.”
Chester aliganda. Muda kidogo, badala ya kukasirika kwa sababu rafiki yake amedhihakiwa, alicheka kwa furaha. "Tathmini yako ni ya moja kwa moja. Alvin kwa kweli ni mtu wa kudharauliwa na ana tabia mbaya."
Lisa alikunja uso, akishangaa kicheko chake. “Hilo ni jambo la kuchekesha?”
"Inasikitisha." Chester alikunja mdomo wake “Lakini baadhi ya ulichosema si sawa. Usiku ule baada ya Alvin kumpeleka Bibi Kimaro hospitali, familia ya Kimaro iligombana. Mzee Kimaro alisema muda wote Alvin amuoe Melanie Ngosha ili kusuluhisha suala hilo, lakini Alvin alikataa na kusema anataka kukuoa wewe tu jambo ambalo lilimkasirisha bwana mzee.”
"Anioe?" Lisa alionyesha kutokuamini.
Chester alimtazama kwa maana. "Nusu ya KIM International ya sasa ilijengwa na Alvin kwa mikono yake mwenyewe. Kucheza na wanawake sio kitu kipya kwa mtu kama Alvin, kwa hivyo bwana mzee asingemwondoa kwa sababu hiyo. Kosa la Alvin lilikuwa ni kuonyesha msimamo wake kwako, kuonyesha kuwa yupo serious na wewe, jambo ambalo lilimkera kabisa bwana mzee.”
Wakati anatoka hospitalini, Lisa alionekana kuwa na mawazo. Siku zote alikuwa akifikiria kwamba Alvin alimuweka kuwa mpenzi ambaye hatawahi kuona mwanga wa siku. Alikuwa kama kikaragosi ambaye hakumpenda na angemtumia tu pale alipomuhitaji. Hata hivyo,alichokisikia kutoka kwa rafiki yake kwamba Alvin alifukuzwa kazi kwa sababu aliweka msimamo wa kumuoa.
Mwenyekiti wa KIM International… Ilikuwa nafasi ambayo ilimweka juu ya wengine 10,000. Ilikuwa ni nafasi ambayo watu kutoka kote nchini waliitazama kwa uchu. Sasa, alikuwa ameanguka kutoka madhabahuni. Je, KIM International iliyompoteza Alvin Kimaro ingekuwa sawa na hapo awali?
Lisa alipoingia tu kwenye gari, Joel alimpigia simu ghafla. “Lisa, uko huru? Tukutane.”
",..sawa." Lisa alijua kwamba mambo fulani hayangeepukika.
Dakika 40 baadaye, baada ya kufika kwenye mgahawa waliokubaliana kukutana, Joel alikuwa tayari ameshamaliza kikombe cha chai. Jozi ya baba na binti wakiwa wameketi pamoja hawakuwa wamewahi kuwa na hali mbaya sana kama hiyo hapo awali. Mwishowe, bado Joel ndiye aliyevunja ukimya. "Uso wako bado unauma?"
Maneno machache ya wasiwasi yalikaribia kumtoa Lisa machozi. Kwa kweli, alikuwa jamaa yake pekee aliyebaki ulimwenguni. “Sijambo.”
“Nina na Melanie walikuwa na hasira sana jana usiku. Usijali, hata mimi nilishtuka…” Joel alitabasamu kwa uchungu. “Lisa, najua kwamba Melanie na wengine walienda kwenye kampuni asubuhi ili kukusababishia matatizo. Unaweza kuzungumza na Alvin Kimaro na kumwacha awaachie?”
Lisa alihisi baridi tu moyoni mwake. “Baba, Melanie alimleta mjomba wake na marafiki kwenye kampuni yangu ili kuvunja mali zetu na kujaribu kunipiga. Ikiwa polisi hawakufika kwa wakati, kuna uwezekano kwamba ningekuwa nimelazwa hospitalini sasa. Sio kama hujui mbinu za Farres Mahewa.”
“Lakini…” Joel alisita. “Kilichotokea kwenye karamu ya chakula cha jioni… Hakika Melanie alikuwa mwathirika. Mtu yeyote atakuwa na hasira."
Lisa alimtazama baba yake ghafla akahisi hasira. “Baba, unafikiri nilimuibia Alvin Kimaro pia?”
“Lisa, sitaki uharibu furaha yako mwenyewe ili ulipize kisasi kwa Nina na Melanie,” Joel alisema kwa uchungu.
Tabasamu la kusikitisha lilipanda usoni mwa Lisa. “Kwa hiyo ndivyo unavyonifikiria mimi. Baba, umewahi kunipenda na kujaribu kunielewa? Kusema ukweli, nimemjua Alvin kwa muda mrefu. Yeye ndiye aliyenilazimisha kuwa naye. Hivi majuzi, amekuwa akikandamiza kampuni yangu na Kelvin. Yote ni matendo yake. Je, unafikiri ninafurahia kuishi maisha yasiyo na heshima? Je, unafikiri ninafurahia kuonyeshwa kidole na kukosolewa kama mtu asiye na adabu?!” Alipoendelea kuongea, hatimaye alikabwa na machozi.
"Nini?” Joel alipigwa na butwaa. “Mbona hukuniambia mapema?"
“Ingekuwa na tofauti yoyote ningekuambia?” Lisa alimtazama kwa dhihaka, “Hukuweza hata kunilinda katika nyumba yako, sembuse mbele ya Alvin?”
Uso wa Joel ulimshuka ghafla, akajiona kama mvulana mdogo na si mtu mzima wa miaka kadhaa. "Sina maana tena kwako. Ni kweli, nilikuleta Nairobi lakini nilikuacha kuonewa na wengine, naenda kumtafuta Alvin sasa hivi. Ameenda mbali sana!”
"Huna haja ya kunitafuta, nipo hapa." Mlango wa chumba hicho cha faragha cha mgahawa ulifunguliwa kwa nguvu, na umbo la Alvin refu na dhabiti likaingia ndani.
"Mbona uko hapa, Alvin?" Lisa alisimama kwa hasira.
"Sijakushika mkia, nmekufuatilia tu ili kuja kukutana na baba." Alvin alivuta kiti kilichokuwa pembeni yake na kuketi, sura yake isiyo na aibu ilimfanya Joel achemke hadi kwenye damu.
“Baba yako ni nani? Umekuwa ukimlazimisha Lisa akusikilize wakati upo kwenye mahusiano na Melanie. Hakika sitakubali binti yangu kuolewa na mtu mbaya kama wewe."
"Nimeweka moyo wangu kwa Lisa. Unapaswa kuwa wazi kuhusu hili tangu usiku wa jana." Alvin aliweka kiganja chake kikubwa nyuma ya mkono wa Lisa na kumtazama kwa macho mazito na ya upole, “Nataka kumuoa.”
Maneno hayo mawili mazito yalimshtua sana Lisa, akageuka nyuma na kumtazama kwa kutokuamini. Ni kweli angemuoa? Ina maana kila alichosema Chester kilikuwa cha kweli? “Haiwezekani!
Joel alipiga meza kwa mshtuko. "Ikiwa unataka kumuoa, kwanini uliingia kwenye uhusiano na Melanie? Kila mtu sasa anajua kwamba Melanie ni mpenzi wako, halafu waje wasikie tena unataka kufunga ndoa na Lisa. Je, umewahi kufikiria jinsi ambavyo watu watakavyomchukulia?”
"Hapo awali, tulikuwa na kutoelewana huko Dar es Salaa ..."
"Sijali." Joel alipunga mkono, “Unapompenda mtu, unapaswa kumheshimu na kumlinda, badala ya kumuumiza…”
Alvin alitoa msisimko kidogo.” “Mjomba Joel, ulikuwa ukimuachilia pia Aunty Sheryl. Muda mfupi tu baada ya kupata ujauzito, ulioa mwanamke mwingine, hata wewe pia ulishindwa katika mahusiano.”
Uso wa Joel ulibadilika rangi. "Ndio. Ndiyo maana ninataka kumlinda Lisa…”
"Alvin alichukua kikombe tupu cha kahawa kutoka mezani, "Ulikuwa wapi Lisa alipofukuzwa nyumbani na Nina na Melanie? Ikiwa ungemlinda jana usiku, angeumizwa na mke wako na binti yako?"
Hapo Joel alipauka sana, Lisa alitazama chini kimya, hakika Joel hakuwahi kumlinda. Hakuwa na ujasiri wa kwenda kinyume na familia ya Mahewa, ambayo pia inaeleza kwa nini alimkosea mama yake, Sheryl enzi hizo.
Macho ya Alvin yalikuwa makali, “Mimi ni tofauti na wewe. Namtaka Lisa, hata nikishindwa kuwa mwenyekiti wa KIM International na kila mtu wa familia ya Kimaro akinipinga, bado nitamuoa.” Alitamka kila neno kwa nguvu sana hadi Joel akashikwa na butwaa, na Lisa pia.
Alvin alimnyanyua Lisa taratibu kwa miguu yake na kusema mbele ya Joel. “Kwa baraka zako tu tunaweza kujumuika kihalali, zaidi ya hapo anaweza kurudi nyumbani kwa Ngosha kihalali baada ya mimi kumuoa, kwa njia hiyo hakuna atakayemdharau tena. Hutaki kuona hilo, mjomba Joel?”
Sentensi ya mwisho ilimwingia Joel. Mwishowe, Lisa alivutwa kwa namna fulani hadi ndani ya gari na Alvin. Lisa alichanganyikiwa. Ilimaanisha kwamba familia ya Kimaro ilimpokonya cheo chake cha mwenyekiti kwa sababu tu alitaka kumuoa?
“Acha kunitazama hivyo.” Alvin alisimamisha gari kwenye njia panda kisha akageuka na kumbusu mdomoni “Twende tukachague pete yako ya ndoa.”
"Sijakubali!" Lisa alikasirika. Kwa kuzingatia tabia yake ya kutisha, alikataa kufungwa naye milele.
"Lisa, nimepoteza kila kitu kwa ajili yako, lakini unakataa kuolewa na mimi?” Macho meusi ya Alvin yalikuwa yamemkazia kana kwamba ni msaliti.
Pembe za mdomo wa Lisa zilimsisimka.“Hata usipokuwa mwenyekiti wa KIM International, bado una mali zisizohesabika kwa jina lako. Naamini wanawake wengi watamiminika. kwako…”
“Sawa. Unaweza kuendelea kuwa mchepuko basi.” Alvin aliinua uso wake. “Nitamuooa Melanie, lakini sitakuacha. Ninyi dada wawili mnaweza kufurahia kuwa nami pamoja wakati huo."
“Alvin, unanichukiza sana!” Kidokezo cha hasira kilitanda machoni pa Lisa.
“Unataka kuwa mchepuko au mke halali? chagua moja.” Alvin alifunga midomo yake myembamba.
Tabia yake ilikuwa mbaya kama kawaida. Lisa ghafla alihisi kubanwa kusikoelezeka kwenye kifua chake. Angeamua kuolewa naye, lakini alikerwa na jinsi alivyomuuliza. Nani asingependa kuolewa? Tena kuolewa kimahaba? Nani angetamani kuwa mchepuko milele? Hasa inapohusisha Melanie kumtawala na kumdharau? La hasha! Kwa ajili ya Sheryl, asingewaruhusu Nina na Melanie wamdharau.
“Sawa, nimekubali.” Kwa hayo aligeuza kichwa chake na kuchungulia dirishani, akalichukulia kuwa ni dili lingine. Hapo mwanzo alikubali kuolewa naye kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa Ethan, safari hii alimuoa kwa nia ya kumshinda Nina na Melanie.
Midomo ya Alvin ilijikunja kwa tabasamu kubwa. Akawasha gari lake na punde wakafika kwenye duka la vito. Kauli mbiu iliyokuwa kwenye ubao wa kuingilia dukani hapo iliandikwa, 'The Only Love In Life.’
Hah! ‘Mpenzi Pekee Maishani?’ Ilionekana kuwa ikimdhihaki Alvin na yeye.
Alvin alifungua mlango wa abiria na kumnyooshea mkono, Lisa alidondosha macho yake na kumshika mkono, kwa pamoja wakaingia kwenye duka la vito. Hakujali jinsi sura yake ilivyomletea aibu, kwanini alihangaika na jambo hilo.
“Karibu Bwana Kimaro." Meneja wa kike pale mlangoni alipomuona Alvin akiingia na mwanamke mbaya ambaye uso wake ulikuwa umefungwa bandeji, alishtuka sana hadi akashikwa na kigugumizi kidogo. Mbali na
yule meneja wa kike, sura ya ajabu ikawaka kwenye nyuso za wauzaji pale ndani.
Pia waligundua kitambo kuwa Alvin alikuwa kaingia kwenye mahusiano na Melanie, lakini hakuwahi kumpeleka Melanie kwenye duka la vito vya thamani, na vito vya bei ghali.
Alvin akajibu kwa sauti kubwa yenye nguvu na kujiamini ya kiume, “mchumba wangu yupo hapa kuchagua pete ya harusi, tuleteeni pete za kisasa zaidi, za gharama zaidi na za kuvutia zaidi.”
“Mchumba?” Meneja wa kike alipigwa na bumbuazi. “Bwana Kimaro una ladha ya ajabu!”
“Nini kibaya kwa mchumba wangu?” Alvin alijibu kwa sauti nzito, macho yake yakimeta kwa uhasama.
Sura ya:195
Bibi-mdogo ana umbile la mfano na nywele nene. Mrembo, mrembo afu mrembo tena, anakufaa vizuri.” Kwa mfululizo wa pongezi za meneja huyo wa kike, Lisa alishindwa cha kusema, meneja huyo alidhihirisha ukweli katika tasnia ya uuzaji. Alisifia sura ya Lisa iliyoharibika vibaya na hata nywele zake zilizokuwa hazifai.
Muda mfupi baadaye, vito vya mapambo viliwekwa mbele yao. Mng’aro wa vito uliufanya moyo wa Lisa kwenda mputomputo.
“Umeipenda ipi? Unaweza kuchagua chochote, hata ukitaka tupeleke vito vyote nyumbani, ni sawa tu.” Alvin alisema huku akikumbatia kichwa cha Lisa, akithibitisha nguvu ya utajiri wa mapenzi aliokuwa nao.
Lisa aliamua kuchagua pete ya almasi iliyopendwa zaidi na wadada, lakini kwa sababu ilikuwa ni nyepesi sana, Alvin alimchagulia pete nzito zaidi ya almasi yenye rangi ya waridi badala yake. Baada ya kuiingiza kwenye kidole chake chembamba, kweli alijihisi kama mwanamke mpya na mwenye furaha zaidi duniani.
Meneja wa kike alitabasamu na kusema, "Una ladha nzuri, Bwana Kimaro. Pete hii ya almasi ina uzito wa gramu 13.14."
Lisa bila fahamu aliikataa, “Hii pete ni nzito sana…”
“Ivae na usifikirie kuivua milele” Alvin aliamuru. Alikuwa na ladha nzuri, na alipenda sana rangi ya waridi. Kama jambo hilo lingetukia huko Dar es Salaam, angalifurahi sana.
Alvin akamwambia Lisa, “nichagulie pete ya kiume pia.”
Kwa kuwa alipenda vitu vikubwa, Lisa kimakusudi. akamchagulia pete ya wanaume iliyofunikwa kwa almasi. Pete hiyo inaweza kuonekana kuwa ya kitambo sana, lakini ilionekana kana kwamba ilitoka kwenye kampuni ya mitindo ya kimataifa na mara moja ilipowekwa kwenye kidole chake, ilionekana kustaajabisha bila kujali pembe zake.
Lisa alipigwa na butwaa kumuona Alvin amechanganyikiwa. “Chaguo bora lililoje?” Alvin alipapasa nywele zake kwa kuridhika. Lisa akajshindwa cha kujibu, “Mimi...” Alikuwa kajawa na furaha kupita kiasi.
Wawili hao walipotoka nje ya duka la vito vya thamani, kamera za waandishi ziliangaza. Kulikuwa na waandishi wa habari wakiwapiga picha mfululizo.
Lisa alipotaka kumkumbusha kuhusu jambo hilo kuenea na kuzua taharuki nyingine, Alvin hakumjali. Aliweka tu mkono wake kiunoni mwake na kumuuliza, “unaogopa chochote?”
“Hapana! Umenitesa sana hivi kwamba chochote kitakachotokea si lolote kwangu,” Lisa alidhihaki, “Vipi kuhusu wewe? Kila mtu anafahamu kwamba Melanie ni mpenzi wako.”
“Sidhani kama nimewahi kutangaza hadharani kuwa Melanie ni mpenzi wangu,” Alvin alijibu huku uso wake mzuri ukiwa umetulia.
Lisa alishangazwa sana na Alvin. Familia ya Ngosha na familia ya Kimaro walishafanya hafla kadhaa za chakula, na Alvin na Melanie walikuwa wamehudhuria hafla za aina tofauti wakiwa wawili. Hiyo yote ilikuwa ni sawa na kumtambulisha Melanie kuwa ni mpenzi wake. Ghafla, alihisi huruma kidogo kwa Melanie. Alvin aikuwa ni mbabe sana asiyejali moyo wa mwanamke hata kidogo.
Habari kwamba Alvin alimnunulia Lisa pete ya almasi siku hiyo ilienea kama moto wa nyikani kote Nairobi. Siku iliyofuata, Alvin, aliingia kwenye kilele cha habari zilizovuma kwa mara nyingine tena.
#Ushahidi Usiopingika Wa Alvin Kimaro Kumsaliti Mpenzi Wake Kwa Mwanamke Mwingine! Alvin Kimaro adhihirisha Kiburi chake Hadharani Kwa Kumnunulia Mchepuko wake Pete ya Alamasi!
#Alvin Kimaro atumia mamilioni Kununua Pete Ya Kwa ajili ya Mchepuko Wake. Hii ina Maanisha Kuwa Hana Mpango Tena na Mpenzi Wake wa Kwanza?
#Alvin Kimaro na mwanadada aliyempindua mwenzake kutoka familia ya Ngosha wanaonyesha mapenzi hadharani]
[Kwa mujibu wa mtu wa ndani, Bi Ngosha Alimfumania Alvin na mwanamke huyu wakiwa wamejificha chumbani wakati wa karamu usiku ule.]
#Bi Ngosha anatia huruma sana. Nilisikia alikwenda kumtafuta yule mwanamke mwingine akiwa na rafiki zake, lakini aliishia kutuptwa kituo cha polisi baada ya Alvin Kimaro kuvuta kamba. Bado hajaachiliwa hadi sasa.]
Hakika, Alvin Kimaro ndiye mwanamume mchafu zaidi Nairobi. Anachukiza.]
#Hatimaye naweza kuona ni kwa nini alifukuzwa kutoka wadhifa wa mwenyekiti katika KIM International.]
Katika siku moja tu, Alvin alikuwa adui wa umma katika Nairobi yote.
Lisa hata aligundua kwamba watumiaji wengi wa mtandao walikuwa wakisusia bidhaa za makampuni ambayo Alvin alikuwa amewekeza.
Mwanamume ambaye alikuwa ni milionea nchini Kenya sasa akawa msemwa hovyo mitandaoni nchini Kenya.
Lisa ghafla akajisikiaviabaya sana. Hata akajuta kwanini alichagua kumkubalia jana yake. Alimtupia macho magumu Alvin aliyekuwa anasoma gazeti pembeni yake. Alikuwa amevalia mavazi ya kulalia bado na kwa mwonekano wa mambo siku hiyo hakuwa na mpango wa kwenda kazini. Kiukweli swala hili lisingetokea endapo angekubali kuoana na Melanie na kuachana na Lisa.
Bado Lisa aliona ni ngumu kuamini kuwa Alvin angekata tamaa juu ya utajiri na upendeleo wa familia yake kwa ajili yake. Pia moyoni alihisi badoAlvin hakuwa na mapenzi naye ila alifanya hivyo kwa ajili tu ya kumkomoa Kelvin.
“Mbona asubuhi na mapema unanitazama kwa mvuto?” Alvin aliinua kichwa chake kutoka kwenye gazeti, na midomo yake ikakunja tabasamu.
Lisa alikodoa macho. Je, alikuwa amemtazama kwa muda mrefu? Yeye hakuwa na ufahamu wa hilo.
“Tafadhali. Nilikuwa nikifikiria tu jambo fulani.” Lisa alitazama pembeni kwa aibu.
Alvin alifunga lile gazeti kabla hajainuka na kumfuata nyuma. Akaminya mikono yake kwenye kiti. “Ulikuwa unafikiria nini?”
"Haikuhusu." Lisa alichezea glasi ya maziwa mikononi mwake.
“Hujui kuwa kila kitukinachokuhusu wewe pia kinachohusiana na mimi?” Alvin akainama na kuuegemeza uso wake mzuri kuelekea kwake.
Lisa karibu alegeze nguvu zake kwenye glasi ya maziwa. Mwanaume huyu kwa kweli alikuwa katika hali ya kumdhihaki au? Kweli alikuwa tayari kupoteza kila kitu kwa ajili yake? Hakuamini hata kidogo. Je, alikuwa kichaa?
Lisa aliuma meno kwa nguvu na kusema moja kwa moja, “Alvin, sijui nia yako ni nini kwangu, nina wasiwasi sana, sina hata amani. Naomba uniache tu. Bado unaweza kuokoa kila kitu.”
"Unamaanisha nini kwa kusema naweza kuokoa kila kitu? Sifa? Hali?" Alvin aliuliza huku akitabasamu hafifu.
“Hujui?”
"Ninajua, lakini wewe ndiye haujui." Alvin alifuta maziwa yaliyokuwa pembeni ya mdomo wake kwa kidole chake. "Lisa, huelewi kuwa kila kitu kinafaa kujitolea kwa ajili yako?"
Kila kitu kinafaa kujitolea kwa ajili yake? Sentensi hiyo rahisi ilibomoa ukuta ambao Lisa alitumia muda mrefu kuujenga ili kujikinga naye. Ghafla, moyo wake ulianza kwenda mbio. Hakuelewa!
Alikuwa ameacha kumpenda kwa muda mrefu, sivyo? Hakuhisi chochote ila chuki kwake. Alitamani kuwa angekuwa amekufa. Alitamani kwamba angeweza kukaa mbali naye iwezekanavyo. Kwake, alikuwa shetani wa kutisha. Hata hivyo, kwa nini aliguswa naye, kwanini alikuwa radhi kupoteza kila kitu kwa sababu yake?
“Ha. Usiniambie kuwa unanipenda.” Akiwa amezuia hasira yake, akajikaza kwenye kioo na kutabasamu. “Unaonyesha upendo wako kwangu kwa nguvu. Uliniumiza mwili, ukanitisha, na kunilazimisha nikusikilize. Haya ni mapenzi kweli unayotakiwa kuishi nayo kwangu?"
“Nimeshakuambia sitafanya hivyo tena. Nilofanya vilekwa sababu ya hasira tu. Ningewezaje kukuona na Kelvin?” Alvin alisema kwa kujiona kuwa hana hatia. “Samahani kwa kukuumiza mapema. Sitafanya hivyo tena, na bila shaka nitakusaidia.”
“Utakuwa umenisaidia sana ikiwa utaniacha tu.” Lisa hakutaka amtanie tena. Alikuwa na wasiwasi kwamba angesahau chuki yake kwake na maumivu ambayo alikuwa amemsababishia.
Macho ya Alvin yalitiwa giza. “Unatamani kuwa na Kelvin tena, sivyo?”
“Hapana…” Kwa kuhofia kwamba Alvin angemuumiza tena Kelvin, Lisa alijibu mara moja, “Niliamua kukubali anioe kwa sababu tu nina deni lake..”
Alvin alishtuka sana hadi akamshika bega kwa nguvu. Lisa aligeuza kichwa na kumwangalia, lakini akapata hofu kubwa machoni pake, kama vile ilipotokea siku ile alipompiga sana, ilikuwa ni dalili ileile tena. Aliogopa sana. Angewezaje kuishi naye milele mtu mwenye hasira za ghafla namna hii?
"Hivyo ndivyo ulivyomaanisha kwa kutoniumiza tena." Kwa maumivu, Lisa alitokwa na jasho baridi....ITAENDELEA.....
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.
