JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA...............................192 -193

Sura ya 192

Hans hakuridhika kabisa, akamkumbusha Alvin kwa uchungu. “Kusema kweli, KIM International ilijiendeleza vyema mikononi mwa mama yako miaka minane iliyopita, lakini baada ya kuingia madarakani, ulienda ng’ambo mara nyingi na ukaalika watu wenye vipaji vya hali ya juu, ukaanzisha maabara binafsi, na kupanua uwanja wa sayansi na teknolojia.

Ni wewe uliyeipa umaarufu familia ya Kimaro kama familia tajiri nchini, na ukaiongoza KIM International katika makampuni kumi bora ya Afrika, lakini sasa, yote yanaenda kwa Jack? Jack Kimaro alifanya nini? Ulipokuwa bize kulala saa nane za usiku na kuamka saa kumi alfajiri, alikuwa nje ya nchi akijivinjari na akapata cheo cha juu mara tu aliporudi.”

"Ninaonekana kama mtu ninayeweza kuwapa tu wengine kile nilichofanyia kazi kwa bidii?" Alvin aliinua uso wake ghafla. Hans alinyamaza. Alvin alikitupa kitambaa alichomaliza kujifutia na kubadilisha mada. “Uchunguzi wa tukio la jana usiku ulikwendaje?”

"Mvinyo uliokunywa ulizimwa kwa glasi ya divai ambayo husaidia kusisimua nguvu za kiume." Hans alisema. "Baadaye, mtu alimwambia Melanie Ngosha kwamba Bi Jones aliletwa kwa lazima kwenye chumba ulichokuwamo na Mkurugenzi Amiri."

"Kwa hivyo ndivyo ilivyokuwa?" Alvin aliitikia kwa kichwa. Jana yake usiku, yeye, Melanie, Lisa, na Mkurugenzi Amiri wote walikuwa vibaraka mkononi mwa Jack. ni mchongo uliotengenezwa vizuri sana na Jack ili kumdhalilisha Alvin.

Alvin alitazama chumba cha kulala cha juu na kumgeukia Aunty Yasmini. “Nenda ukamwangalie Lisa.”

Punde, Aunty Yasmini alishuka kutoka ghorofani na kusema kwa wasiwasi, “Bi. Jones amelala bila kujigeuza kitandani na anakataa kula hata kunywa chochote. Nadhani hali yake ni mbaya sana. Anaonekana kama mtu asiye na matumaini wala dhamira ya kuendelea kuishi.” Maneno yale yalikuwa yakitoka kwa uchungu kwenye kinywa cha Aunty Yasmini.

"Anagoma kula?" Macho ya Alvin yalimtoka kwa hasira. Akainuka na kwenda juu.

Kama Shangazi Yasmini alivyosema, macho ya Lisa yalikuwa yamefungwa na uso wake ulikuwa umekakamaa. Hata hivyo, Alvin alijua kwamba alikuwa macho.

“Unamaanisha nini kwa kufanya hivi?” Alvin alidhihaki, “Lisa Jones, lini umekuwa mnyonge kiasi hiki?”

Kope za Lisa zilitetemeka. Ndio, hapo awali, alifikiria kuwa wazazi wake wa kibaolojia walikuwa Jones Masawe na Salome Urassa ama Mama Masawe. Walijaribu kumuua tena na tena, wakamfanyia hata njama aende gerezani na hata kumtesa hadi karibu kufa. Baadaye, alipata habari kwamba bibi yake aliuawa. Alikuwa amekata tamaa, lakini wakati huo, alikuwa tayari amekutana na Alvin kama bahati mbaya tu, na akageuka kuwa msaada wake mkubwa. Ni yeye ambaye alikuwa amempa joto na matumaini. Sasa, alikuwa kama mlima mkubwa. Hakukuwa na jinsi angeweza kupanda juu. Hakuona matumaini hata kidogo!

"Simama." Alvin alinyanyua blanketi na kumvuta kutoka kitandani. “Hutaki kuchunguza chanzo cha kifo cha mama yako?”

“Hapana…” Lisa alijibu kwa sauti ya chini. Alijua ikiwa Alvin angekuwa karibu naye, asingeweza kamwe kulipiza kisasi.

Alvin alipigwa na butwaa na kusema kwa hasira, “Ukiendelea na mawazo yako ya kuachana na mimi, nitaiharibu kabisa kampuni ya Mawenzi na kumpoteza kabisa Kelvin Mushi. Nitahakikisha nawakandamiza Joel Ngosha na hata Pamela Masanja. Maadamu hawa ni watu wa karibu sana kwako, sitamwachilia yeyote kati yao.”

“Alvin Kimaro, kwa nini usiniue tu?” Lisa alikuwa mwisho wa akili zake na kufumbua macho yake. Alichukua mto na kumrushia.

Alvin kumuona hivyo akashusha pumzi. Akamkumbatia kwa nguvu. “Lisa, sitakuua. Nataka ukae upande wangu milele. Nitakuoa na kukutendea mema. Usiniache.”

Macho yake ya mapenzi yalimfanya Lisa kuzama kwenye butwaa kwa muda, lakini muda si mrefu alidhihaki. “Unadhani nitakuamini? Niangalie usoni. Hivi ndivyo unavyomaanisha kunitendea mema?”

"Jana ... ilikuwa ajali," Alvin alielezea kwa huzuni.

“Unadhani nitakuamini?” Macho ya Lisa yalikuwa yamejaa kejeli na karaha.

“Ni kweli. Jana, divai yangu ilitiwa kichocheo. Nilidhani nilikuwa nimekunywa kupita kiasi.” Midomo ya Alvin ilijikunja na kuashiria kujidharau.

Lisa alipigwa na butwaa. Alipofikiria kwa makini jinsi alivyokuwa jana yake usiku, kwa kweli ilionekana kuwa jambo lisilo la kawaida. Hata hivyo, mwishowe, ni kwa sababu wengine walikuwa wakijaribu kupanga njama dhidi yake. Alikuwa tu mwathirika ambaye alilengwa kufanyiwa fedheha.

“Kuwa mwema. Nenda ukanawe na kula chakula. Ngoja nikukamulie dawa ya meno.” Alvin alipoona haongei, alimpapasa kichwani kwa mbwembwe na kuchukua hatua ya kwenda bafuni kumminya dawa ya meno pamoja na kumwagia glasi ya maji ya uvuguvugu kwa ajili ya kusuuza mdomo wake.

“Nitafanya mimi mwenyewe." Lisa hakumzoea Alvin kuwa vile, akachukua mswaki mwingine kabla ya kwenda chooni. Kujitazama alivyokuwa mnyonge kwenye kioo, ghafla alihisi ajabu. Sasa, hakuweza hata kujijua kama alikuwa hai ama mfu. Hakuweza kujua kama alikuwa anaota au ilikuwa ni kweli. Je, angeendelea kujitoa na kuishi maisha duni kama yale mpaka lini? Hapana, asingeweza kufanya hivyo. Kwa kuwa hakuogopa kifo tena, kulikuwa na nini tena cha kuhangaikia? Alimradi bado anapumua, angepigana na mtu huyo!

Alipotoka tena, Alvin alimtazama na kuona amebadilika. “Naweza kukusindikiza kwenda kufanya shopping, au nikupeleke likizo mahali fulani?”

“Naenda ofisini.” Lisa aliingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo na kutafuta mavazi ya kikazi.

Alvin alimtazama usoni kwa sura isiyo ya kawaida. "Unaenda ofisini ukiwa namna hii?"

"Kwani namuogopa nani? Au itawatisha wengine?" Macho ya Lisa yalikuwa meusi na tulivu, kana kwamba alikuwa hazungumzi juu yake mwenyewe.

Alvin alikunja uso lakini akasema baada ya muda, “Fanya upendavyo.”

Lisa hakujali. Ilikuwa ni bora kwenda kutafuta kitu cha kufanya huko, kuliko kubaki na kufia nyumbani.

Saa nne asubuhi Lisa aliingia kwenye ofisi ya kampuni ya Mawenzi Investiments jijini Nairobi., Lisa alitoka kwenye lifti akiwa amevalia suti nyepesi ya rangi ya kahawia. Mwili wake ulikuwa umenyooka kama zamani na umbo lake lingeweza kupachikwa kwenye gazeti la mitindo, lakini kwa bahati mbaya, chachi iliyofunika uso wake siku hiyo iliwafanya wafanyakazi kumwangalia kwa sura za kushangaza. Hata hivyo, hakuna aliyethubutu kuuliza. Ni baada ya kupita tu ndipo baadhi ya watu walianza kunong'ona na kujadiliana.

“Ni nini kilitokea kwenye uso wa Mwenyekiti Jones? Je, alifanyiwa upasuaji?"

“Mjinga wewe. Ina maana hujui? Alikamatwa akifanya uzinzi kitandani na kupigwa?”

"Hapana, tayari ni tajiri sana lakini bado anataka kuwa mchepuko?"

“Nilisikia kuwa ni binti wa nje ya ndoa. Wakati huo, mama yake pia aliharibu ndoa ya mtu, na sasa, alimtongoza mchumba wa dada yake mdogo. Hana maadili hata kidogo.”

"Ni kweli, mmejuaje mengi hivi juu yake?" Sauti ya Lisa ilisikika ghafla kutoka nyuma yao, na wanawake wale wakaruka kwa hofu.

“Mwenyekiti- Jones… Kwanini umerudi?”

“Unataka nijieleze kwako kama nani? Jibu swali langu." Lisa alitoa mtazamo wa kimamlaka na wa kuogofya.

“S-Someone alichapisha notisi mlangoni asubuhi. Watu wengi waliiona,” mfanyakazi huyo wa kike alijibu kwa tahadhari, “samahani, Mwenyekiti Jones. Sitathubutu kusema tena.”

“Si ulisema sina maadili? Watu wasio na maadili kama mimi lazima wawe na tabia mbaya, kwa hivyo kuna faida gani ya wewe kufanya kazi kwenye kampuni ya mtu asiye na maadili? Kuna kampuni nyingi sana za watu wenye maadili mema huko mitaani. Kwa hiyo paki vitu vyako uondoke." Lisa akageuka na kurudi ofisini kwake.

Sura ya:193

"Hiyo notisi ya mlango imeondolewa?" Lisa alimuuliza msaidizi wake mara baada ya kuingia ofisini.

'Imeondolewa, lakini habari kuhusu hilo kimsingi imeenea kupitia kampuni," msaidizi wake alisema kwa kigugumizi, "Mwenyekiti Jones, usichukulie kwa uzito uvumi wa watu wengine."

'Sio uvumi. Ni ukweli.” Lisa alimtazama moja kwa moja.

Wakati huo huo, katibu wake ghafla akaingia ndani na kusema, "Mwenyekiti Jones, kuna habari mbaya. Kuna mtu alileta watu kwenye kampuni ili kufanya vurugu. Walipoingia mlangoni walianza kuvunja-vunja vitu na kusema wanataka kukuona.”

“Nitashuka.” Lisa akainuka.

Katibu huyo alishangazwa sana na Lisa. “Mwenyekiti Jones, hilo si wazo zuri. Wamebeba kamera. Lazima watakurekodi na kukuweka mtandaoni.”

“Haijalishi.” Lisa alishuka chini.

Akiwa njiani kuteremka chini ghafla alipokea simu kutoka kwa Alvin. “Usishuke. Tayari nimemjulisha Shani. Atamleta mtu kushughulikia hilo.”

"Hakuna haja. Nitalishughulikia mwenyewe.” Lisa alikuwa mbishi.

“Lisa, usiwe mbishi. Farres Mahewa ni mmoja wa watu waliokuja. Wao si watu unaoweza kujadiliana nao.”

Lisa alicheka kwa dhihaka. “Tangu nilipokufahamu vizuri Alvin, naweza kuchagua tu kujifunza kukabiliana na mambo haya mwenyewe. Baada ya yote…huwezi kunilinda kila wakati.”

Alikata simu na kutoka nje ya lifti. Mara moja, yai lililooza likampiga kwenye paji la uso wake, na papo hapo kuchafua shashi usoni mwake. Ilikuwa ni jambo la kutisha sana.

“B*tch, unaiba mpenzi wa mtu mwingine? Unastahili! Nitakupiga hadi kufa.” Msichana mdogo aliyevalia vizuri alisimama kando ya Melanie, akionekana kuchukizwa na kutapika laana.

“Mwenyekiti Jones…” msaidizi wake alishtuka na kwa haraka akamkimbilia akiwa na kitambaa cha kujifuta usoni.

Lisa aliichana ile chachi na kudhihirisha majeraha mekundu usoni mwake.

“Mbaya kiasi gani! Alvin Kimaro atakapoona sura hii lazima atatapika!” Msichana mwingine aliyevalia mavazi ya kijanja alisema kwa kuchukiza, “Mchafu kama nini, kwanza hustahili kuonekana Nairobi. Fanya haraka upotee.”

“Samahani sana kwa kusema hivyo, lakini Alvin alikuwa bado amelala kitandani kwangu asubuhi ya leo, akinipapasa usoni kwa upole na kuniambia nisimuache.” Lisa alitabasamu kwa upole, na kumfanya Melanie atetemeke kwa hasira.

Melanie alikimbilia kumpiga kofi, akisema, "Lisa Jones, nenda kuzimu!"

Lisa alikuwa akingojea wakati huo kwa hamu. Alimshika Melanie kifundo cha mkono na kumvutia kwake huku akimpiga makofi makali kadhaa. “Hivi ndivyo ulivyonipiga jana. Nakurudishia yote leo!” Melanie alipigwa makofi kadhaa na kuanguka chini.

“Unathubutuje kumwekea mkono mpwa wangu mbele yangu?! Lazima uwe na hamu ya kifo!" Farres aliingilia kati kwa hasira.

Msaidizi wa Lisa aliruka kwa mshangao na angeweza tu kukimbilia mbele kumzuia. Farres akataka kumpiga Lisa teke, na Lisa akatoa kisu cha matunda ili kukikandamiza kwenye uso wa Melanie. Macho yake hayakuwa na huruma. "Ukithubutu kunigusa, nitaharibu uso wake."

“Mjomba, usiondoke. Siwezi kukubari kuharibika sura.” Melanie aliogopa sana hata akakaribia kulia.

"Lisa Jones, ikiwa utathubutu kumgusa Melanie, nitaondoa maisha yako!" Farres alipiga kelele kwa hasira. Alikuwa amefika hapo kumnyoosha, lakini hakutarajia kutishiwa badala yake.

"Maisha yangu? Jisikie huru tu kuyachukua. Kama ningeogopa kifo, usingesimama hapa.” Lisa alidhihaki, “Lakini Melanie ni tofauti. Bado anategemea uso wake kupanda juu ya familia ya Kimaro. Nani atamtaka ikiwa ataharibika?"

"Unataka nini?" Farres alisema kwa hasira.

"Nipatie kamera zote." Lisa akamtazama.

Farres hakuwa na budi ila kupunga mkono wake, na kamera kadhaa zilikabidhiwa kwa wafanyakazi wa kampuni ya Mawenzi. Alipomaliza kukabidhi tu, kundi la askari polisi waliingia kwa kasi kutoka nje.

"Tulipokea taarifa kwamba kuna watu wamefika kwenye kampuni ya Mawenzi kufanya fujo..."

Farres alikuwa karibu kuzungumza wakati Lisa alimsukuma Melanie kando mara moja. Alitembea hadi mbele ya polisi kwa macho mekundu. “Afisa, watu hawa waliingia tu kwenye jengo hili na kuanza kuharibu mali zetu. Hata walinirushia yai viza usoni.”

Melanie alipiga kelele, “Hapana, alijaribu kwa uwazi kuniharibu uso kwa kisu! Fanya haraka ukamkamate!”

Askari polisi alimtazama Lisa ambaye uso wake ulikuwa umejaa majeraha na kupakwa maji maji ya mayai yaliyooza kisha akamtazama Melanie ambaye alikuwa amevalia vizuri na alionekana hana hata upele kabisa. Mara moja polisi alikasirika. "Ni nani aliyejaribu kuharibu uso wa mtu mwingine? Unafikiri mimi ni kipofu?”

"Bwana. Afisa, usipaze sauti yako. Huyu ni binti wa thamani wa familia ya Ngosha na mwanaume huyo ni Farres Mahewa kutoka kwa familia ya Mahewa. Nilisikia kwamba wanafahamiana na watu wazito wengi sana,” Lisa alisema akijifanya kuwa na woga.

Farres alizoea kutenda kwa kiburi na alikoroma kwa baridi alipomsikia yule polisi akiongea. “Unatoka kituo gani? Nitajie mkuu wako.”

Lisa aliangaza macho kwa mshangao na kuchombeza, "sikutarajia mkuu wa polisi kuwa mmoja wa watu wanaowajua. Ni ajabu kiasi gani.”

Macho ya afisa huyo yaliganda alipomfokea Farres kwa haraka, “Mkuu wetu hatajua watu kama wewe. Sijali wewe ni nani. Kamateni kila mtu aliyethubutu kuleta fujo hapa!” Punde, polisi waliwachukua Farres na wengine.

"Bwana. Afisa, asante sana. Tuna shukrani nyingi kwako kwa sababu mmewahi kutusaidia na tuko salama. Ninaahidi kutoa mchango baadaye mchana huu.” Lisa aliguswa na kuwasindikiza polisi mlangoni.

Shani, ambaye alifika tu na kukuta hali hiyo ikiendelea, mara moja alimpigia Alvin bila kuchelewa.

Alvin alitabasamu kwa furaha aliposikia jambo hilo. “Nenda ukamsalimie. Hakikisha watu hao wamefungwa kwa siku kadhaa jela, hasa mwanamke aliyemrushia Lisa yai lililooza.”

Shani alikumbusha, “Bwana Kimaro, mwanamke huyo ni binti wa familia ya Owino…”

“Kwa hiyo iweje?” Baada ya kukemea, Shani alisikia sauti ya simu ikikatika.
•••
Baada ya kutoka kituo cha polisi. Lisa aligundua kuwa uso wake ulikuwa na maumivu zaidi na ikambidi aende tena hospitali. Daktari kutoka idara ya magonjwa ya ngozi alipomsaidia kusafisha majeraha, Dokta Chester Choka aliyevalia nguo nyeupe aliingia ghafla.

“Hakikisha unatumia dawa bora kuponya majeraha usoni mwa Bi Jones haraka iwezekanavyo. Lazima kusiwe na makovu yoyote."

Lisa alikosa la kusema. Je, Dokta Chester alikuwa huru sana? Kwanini siku zote alikuja kumtafuta alipokuja hospitalini? Kusema kweli, sasa alikuwa amechukizwa sana na Alvin na hakuwa na mawazo mazuri ya marafiki zake pia. Ndege wenye manyoya yafananayo huruka pamoja. Aliamini rafiki zake hakika hawakuwa watu wazuri pia.

Baada ya majeraha yake kutibiwa, Lisa alisema kinyonge, “Dokta Choka, rudi kazini. Mimi pia naondoka muda si mrefu.”

“Usiwe na wasiwasi sana. Mimi ni shemeji yako.” Chester alitabasamu. “Isitoshe, utaolewa na Alvin hivi karibuni. Utakuwa shemeji yangu rasmi siku chache zijazo.”

Maneno hayo yalisikika kama dhihaka tu katika masikio ya Lisa. “Mimi si mtu sahihi. Unapaswa kusema hivyo kwa Melanie Ngosha.”

“Melanie Ngosha?” Chester aliitazama sura ya Lisa iliyoonekana kama ngeni kutokana na majeraha. Alvin alikuwa hana maana hata kidogo kumsukumia mbali mwanamke mzuri namna hiyo. Ilikuwa ni juu yake kumsaidia Alvin. “Hujui hili, lakini Alvin hampendi kabisa Melanie Ngosha. Hata alikubali kuondolewa kwenye wadhifa wake kama mwenyekiti wa KIM International ili akuoe.”

Lisa alipigwa na butwaa kwa muda. Alvin hakuwa tena mwenyekiti wa KIM International? Hiyo inawezaje kuwa?.....ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.