JINA LA SIMULIZI............................LISA

AUTHOR...........................JOMBA WAJO

SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY

WHATSAPP...........................0628924768

SEHEMU YA...............................198-199


Sura ya:198

 

Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa muda mrefu ambapo Lisa alikuwa akimpigia simu Alvin kwa hiari yake mwenyewe. Baada ya muda mrefu, simu hatimaye iliunganishwa. Hata hivyo, ilikuwa ni sauti ya hasira ya Rodney iliyosikika. “Lisa, wewe ni msumbufu sana. Ulimwacha Alvin katika hali mbaya sana.”

 

“Yuko wapi?” Moyo wa Lisa ulizama.

 

"Familia tisa za juu zenye ushawishi zinaangalia suala hili. Alvin amekamatwa kwa uchunguzi,” Rodney alisema huku akitabasamu. “Kama si wewe, Alvin asingeishia katika hali hii!”

 

“Wewe ni nani hata unikosoe?” Lisa alikanusha kwa hasira. “Kama usingeniteka nyara usiku huo, video hiyo isingekuwepo! Yatch ni yako, kwa hivyo sasa video imetolewa, kama si wewe uliyeitoa ni nani? Una jukumu kubwa pia!"

 

Rodney alikasirika sana hivi kwamba alipoteza maneno kwa muda. "Wale watu wenye ushawishi wanataka kumwacha Alvin juu ya kuti kavu. Mambo si rahisi kama inavyoonekana.”

 

Lisa alikata simu moja kwa moja na kutaka kumpigia Hans ili kujua hali ya Alvin ilivyokuwa. Ghafla, mfululizo wa hodi za haraka zikasikika kutoka chini. Alivaa nguo zake na kutoka nje. Mlinzi mkuu wa nyumba ya familia ya Kimaro, Mwamba Kisiki, aliingia akiwa na kundi kubwa la walinzi. "Bi Jones, tafadhali fuatana nasi kwenye makazi ya familia ya Kimaro."

 

Shangazi Yasmini alisema mara moja, “Bw. Kisiki, huwezi kusubiri Bwana Kimaro arudi…”

 

“Bwana Alvin Kimaro amepelekwa kwenye idara ya mahakama kwa uchunguzi.” Uso wa mlinzi wa nyumba ulikuwa wa baridi. "Tukio hilo linatokana na yeye, kwa hivyo sina budi kumchukua usiku wa leo."

 

“Ni sawa, Shangazi Yasmini. nitaondoka naye.” Lisa alishuka ngazi. Kwa muda mrefu alitarajia kwamba familia ya Kimaro ingemtafuta. Ilikuwa ni suala la muda tu.

•••

Saa moja baadaye, katika makazi ya familia ya Kimaro kulikuwa na watu wa kutosha. Ilikuwa ni mara ya pili kwa Lisa kutembelea makazi hayo ya kifahari. Alipoingia ndani, kila mtu wa familia ya Kimaro alikuwepo, na wote walikuwa wakimtazama kwa chuki na hasira.

 

Mbele ya familia hiyo maarufu, macho ya Lisa yalikuwa ya utulivu na yasiyopendeza. Mambo mengi yalikuwa yametokea tangu alipoingia Nairobi, na alikuwa amepitia maisha mengi magumu hadi wakati huo. Tayari alikuwa hana woga.

 

“Kinyume na matarajio yangu yote, unaonekana mtulivu sana. Si ajabu umeweza kumroga Alvin. Wewe ni mjanja sana, huh?" Macho ya Mzee Kimaro yalikuwa yakimtazama. Ingawa alikuwa na umri wa miaka 70, aliendelea kuwa na nguvu kama vile kichwa cha familia tajiri zaidi.

 

Lisa hakusema neno. Alipoona jinsi anavyoonekana mtulivu, Mzee Kimaro alidhani ni jeuri, alikasirika sana akachukua kikombe cha kahawa na kumpiga nacho kichwani. Ghafla mtu akajitokeza ghafla kumkinga kutoka upande, na kikombe kilitua kwa Jack.

 

"Unafanya nini Jack?" Hasira ilimpanda Lea. "Bado unampenda, huh?"

Jack alimtazama kando Lisa ambaye hakuonekana kuwa mnyenyekevu wala mwenye kiburi kando yake na akatabasamu kwa unyonge. “Bibi, tuzungumze mambo. Ukimdhuru, naogopa Kaka atapandwa na hasira akirudi.”


Bibi Kimaro alidhihaki, “Anaweza kufanya hivyo? Kuachiliwa kwake bado hakuna uhakika.”

 

“Unamjali Kaka zaidi, Bibi. Hakika utamsaidia.” Jack akatabasamu.

 

“Msaada?” Bibi Kimaro alimtupia jicho Lisa. “Ameniangusha sana muda huu. Niambie ulitumia mbinu gani kumroga Alvin? Wewe ni mjanja kabisa. Ulipokuja hapa mara ya mwisho, nilikuona ukimkonyezakonyeza. Kwa kweli mmetufanya sisi sote kama wapumbavu.”

 

"Mama, mwanamke huyu ni mjanja," Valeria alisema kwa dharau. “Anamtongoza Jack akiwa kwenye uhusiano na Alvin. Pia nimesikia tayari ana mchumba. Anatufanya sisi ni wajinga tu.”

 

“Ndio. Si ulisema una mchumba?” Bibi Kimaro alizidi kuchukizwa naye. “Unawezaje kuwa mchepuko wakati una mchumba? Unatamani sana wanaume? Aibu kwako!"

 

Macho ya Lisa yalitazama sakafuni. Aliendelea kukaa kimya huku akiwa hajui la kusema. Ingekuwa haina maana kukanusha madai yao hata hivyo. Mlinzi mmoja alimpiga Lisa teke la magoti kwa nguvu, akapiga magoti chini kwa maumivu.

 

Lea alisema bila kujali, “Sema kitu. Kwa kuwa ulikuwa na ujasiri wa kufanya hivyo, kwa nini usithubutu kueleza?”

 

“Hasa. Hakuna maana kuwa na aibu sasa,” Queen alisema huku mdomo ukimsisimka. "Alvin yuko kwenye shida sana wakati huu kwa sababu yako."

 

"Kwa kawaida yeye ni mtu mpole, kwanini aliishia hivi?" Spencer Kimaro alisema kwa mawazo. "Baba na mama wameweka bidii nyingi ndani yake."

 

Mzee Kimaro alipiga meza. "Huwezi kukaa Kenya tena. Ninakupa chaguzi mbili sasa. Nitakupa tiketi ya ndege kuondoka Dar es Salaam na usirudi tena Kenya. Chaguo jingine ni kwamba unaweza kubaki hapa, lakini nitakupeleka kuzimu.”

 

Lisa aliinua kichwa chake ghafla na kupigwa na butwaa kwa muda.

Kuondoka Nairobi na kupoteza biashara zake alizoanzisha Kenya? Alifikiria kumkimbia Alvin alipomtesa hapo awali. Hata hivyo, kwa kuwa sasa aligundua kwamba Alvin aliziudhi familia zote za kifahari jijini Nairobi kwa ajili yake, hakufikiri angeweza kuondoka akiwa na dhamiri safi.

 

"Nataka kujua nini kitatokea kwa Alvin." Lisa aliuliza kwa msisitizo akiwa amekunja ngumi. “Mtamwokoa, au mtamwacha afungwe?”

 

“Inategemeana na yeye. Akiendelea kuwa mkaidi, nitamkana kuwa mjukuu huyu.” Mzee Kimaro alikoroma. “Hata hivyo, sifa yake imechafuliwa tangu alipovunja mikono ya vijana tisa kutoka kwa familia mashuhuri jijini Nairobi. Sasa kila mtu kutoka tabaka la juu anamsusia, na familia hizo zinaishinikiza familia yetu. Kwa kuzingatia kwamba ameharibu sifa ya familia yetu ya miaka mia moja, atakuwa na bahati ikiwa ataokoka.”

 

Macho ya Lisa yalimtoka kwa wanafamilia wote wa Kimaro. Aligundua kuwa hakuna hata mmoja wao aliyeonyesha wasiwasi na Alvin, pamoja na mama mzazi wa Alvin, Lea.

 

Mara Lisa alimuonea huruma kidogo Alvin. Ikiwa haya ndiyo mazingira aliyokulia, haikuwa ajabu alikuwa katili sana na wakati mwingine kukosa huruma.

 

“Alvin ni mjukuu wako. Je, sifa ya familia ya Kimaro au uhusiano wa kifamilia ni muhimu zaidi?” Alishindwa kuvumilia familia ya Kimaro tena, Lisa aliinuka na kusimama. “Nyinyi nyote ni babu yake wa bibi na mama yake wa damu? Mnawezaje kuishi bila kujali? Mlimpendelea wakati alikuwa na uwezo wa kuleta heshima na faida kwa familia. Lakini kwa kuwa sasa yuko chini kabisa, mnamdharau na kumkatia tamaa, badala ya kumpa mkono wa msaada. Hatimaye hii imenifungua macho kuona familia ya Kimaro ilivyo.”

 

“Unasemaje?” Akiwa amepandwa na hasira, Mzee Kimaro alinyakua kikombe kingine na kukitupa kichwani kwa Lisa. Wakati huu, hakuna mtu aliyemzuia. Ilimuuma sana Lisa hadi akakaribia kuzimia.

 

Damu zilianza kumchuruzika, na wakati huo, alionekana kuogopa sana.

Hata hivyo, Lisa alikunja ngumi na kujikaza. Macho yake yalikuwa makali zaidi sasa. “Nimekosea? Ikiwa familia inataka kuwa na ushawishi, je, si kila mtu anapaswa kuungana na kuheshimiana? Familia kama hizi pekee ndizo zinazofika mbali.”


Kila mtu alipigwa na butwaa, ama kutoka kwa uso wake wa kutisha au maneno yake. Muda mfupi baadaye, Lea alisema kwa hasira, “Lisa, mwanzoni tulitaka kukupa nafasi ya kuishi kwa kukuruhusu kuondoka Kenya ukiwa hai. Lakini unaonekana huithamini.”

 

Lisa akamcheka. “Asante kwa kudhani kwamba ningeithamini. Ngoja niwaambie wote ukweli wangu kwamba sitaondoka.” 

 

Jack alikunja uso, na wonyesho wa wasiwasi ukaangaza machoni pake. “Ondoka tu Lisa. Ukikaa hapa, itakuwa kuzimu hai kwako. Familia ya Kimaro haitakuacha. Watakufungia kwenye jela ya familia badala yake, na inatisha sana huko…”

 

“Loo, haijalishi. Nimetembelea sehemu ambazo zinatisha zaidi.” Lisa alibaki ameduwaa bila dalili yoyote ya hofu usoni mwake.

 

Jack alipendezwa na tabia yake hata zaidi, lakini alitumaini kwamba asingechagua kubaki. "Itakuwa bure kukaa hapa. Utapoteza uhuru wako milele."

 

“Angalau… dhamiri yangu haitanisumbua.” Macho ya Lisa yalikuwa yametulia.

 

“Una dhamiri?” Valeria alitania.

 

"Hakuna hata mmoja wenu atakayeelewa uhusiano wa chuki na upendo kati yangu na Alvin," Lisa alijibu bila kujali.

 

"Basi mpelekeni kwenye jela ya familia na mumfungie." Mzee Kimaro alikoroma huku akipunga mkono. Walinzi walimwondoa Lisa kwa kumsukuma.

 

Sura ya:199


Kila mtu alimtazama Lisa kwa njia tofauti. Baada ya muda kidogo, Bibi Kimaro alisema, “Sikutarajia msichana huyu mdogo angekuwa mkaidi kiasi hiki.

 

Queen alipiga kelele. “Usimruhusu akudanganye, Bibi. Ikiwa huniamini, jaribu kumnyima uhuru kwa siku chache bila kumpa maji au chakula. Nina hakika ataomba rehema zako.”

 

"Nyamaza. Atakufa ikiwa hatakula au kunywa kwa siku kadhaa,” Jack alifoka kwa hasira.

 

“Mbona unanifokea? Hata hakupendi kwanza,” Queen alijibu kwa hasira.

 

“Sawa. Hakikisha tu kwamba hatakufa.” Bibi Kimaro alisema, “Alvin karibu aingiwe na wazimu Sarah alipofariki wakati huo. Iwapo lolote litampata Lisa, nina wasiwasi kwamba atakuwa mwendawazimu.” Kila mtu alinyamaza.

 

Baada ya kila mtu kuendelea na mishe zake, Valeria alimpigia Nina simu mara tu aliporudi chumbani kwake.

 

Nina alifurahi sana aliposikia habari hizo. Upesi akasema, "Mradi utanisaidia kumtesa Lisa hadi kufa katika jela ya familia, nitakupa Ksh. milioni 50 ili kusaidia kampuni yako kufikia lengo lake."

 

Valerie alitikiswa kwa muda. KIM International ilikuwa na mali nyingi, na kwa muda huo alikuwa akisimamia masuala yanayohusiana na bima katika kampuni hiyo. Hata hivyo, hakuzingatiwa vyema na familia ya Kimaro kwa sababu utendaji wa kila mwaka wa kampuni haukuwa mzuri. Iwapo angefaulu kulenga shabaha kwa robo hii, Mzee Kimaro bila shaka angemwona kwa mtazamo tofauti. Hata hivyo, katika mawazo ya ugonjwa wa Alvin…Alitetemeka kwa hofu. "Siwezi kumtesa hadi kufa."

 

"Kwa nini isiwe hivyo? Bado unamuogopa Alvin? Amehukumiwa maisha. Hakuna matumaini kwake.”

 

“Kwa kweli siwezi,” Valeria akajibu. "Naweza kumfanya chochote isipokuwa kumuua."

 

Baada ya kufikiria kidogo, Nina alitabasamu kifedhuli na kusema. “Sawa basi. Wakati mwingine, ni huzuni zaidi kwa watu kuishi kuliko kufa. Kwa vile anafurahia kutongoza watu, haribu uso wake ili wanaume wamchukie.”

 

"Hakuna shida."

 

Katika chumba cha jela ya familia. Lisa alisukumwa kwa nguvu ndani. Muda mfupi baadaye, taa pekee yenye mwanga hafifu karibu na ngazi ilizimwa. Kwa kweli kulikuwa na giza totoro ndani. Hakukuwa na mtandao wa simu pia. Alitumia tochi kwenye simu yake kutazama huku na kule. Hakukuwa na kitu kingine chochote isipokuwa dirisha dogo lenye vyuma na blanketi nyembamba. Hii ilionekana kuwa sawa ikilinganishwa na kufungiwa katika makazi ya zamani ya familia ya Masawe hapo awali. Alipewa blanketi hapa, angalau.

 

Alijizuia kutumia simu yake kwa kuhofia kwamba betri ingeisha kabla hajapata msaada wowote na kwa hali hiyo, asingejua wakati. Asubuhi iliyofuata, kuna mtu alimletea bakuli la uji. Kwa kweli alifarijika sana kupewa japo kitu cha kula na uji haukuwa umechakaa. Chakula chake cha mchana pia kilikuwa ugali. Katikati ya chakula chake, ghafla alishtuka kusikia mtu akimjia. Mpaka anaingia mlangoni ndipo alipomwona Jack.


Jack aliutazama ugali mgumu mkononi mwa Lisa kwa macho magumu. “Naweza kumsihi babu akuhurumie. Maadamu unaahidi kutorudi Kenya na kuungana tena na Alvin, unaweza kutoka humu.”

 

Lisa aligeuza macho yake na kuziba sikio kwa maneno yake. Aliendelea kujikita katika kula ugali wake.

 

“Lisa, hukusikia nilichosema? Hutaweza kustahimili mambo haya milele. Ni giza na baridi sana hapa. Si mahali pa wanadamu,” Jack alisema kwa wasiwasi. "Mtu aliyekaa hapa mara ya mwisho alipatwa na kichaa baada ya nusu mwezi."

 

“Kweli? Sidhani kama nitakuwa mwendawazimu.” Lisa alitabasamu kwa unyonge. "Nimekaa katika sehemu ambazo ni mbaya zaidi kuliko hizi. Mahali hapa si pabaya sana. Chakula siyo kichungu na maji pia ni mazuri, na kuna blanketi hapa.”

 

Jack alipigwa na butwaa. "Unamaanisha nini? Umewahi kula chakula kilicohoza na kunywa maji machafu?" Alikuwa amepitia maisha ya aina gani? Kumwangalia mwanamke mtulivu mbele yake, Jack ghafla aligundua kuwa hawezi kuhisi sawa naye kile alichokuwa akipitia.

 

"Hakuna haja ya kuuliza maswali kama haya, Jackson." Sura ya dhihaka iliosha uso wa Lisa. "Baada ya yote, niko hapa kwa sababu yako."

 

Jack aliganda. “Hata kama nisingefanya hivyo, uhusiano wako na Alvin ungefichuliwa tu hatimaye.”

 

"Kwa hivyo ninapaswa kukushukuru?" Lisa alidhihaki, “Asante basi kwa kuweka dawa za kuchochea nguvu za kiume kwenye kinywaji cha Alvin. Asante kwa kuchukua fursa ya Melanie kwa kumleta katika chumba. Kisha, ukafanikiwa kuanika jambo hilo kwa kila mtu katika familia ya Kimaro na kuharibu sifa ya Alvin. Ulisababisha mzozo kati ya Alvin na wazee wake ili uchukue nafasi ya uenyekiti.”

 

Jack aliona aibu kwa maneno yake. "Ninakubali kwamba mimi ni mtu wa kudharauliwa, lakini ninataka kukusaidia sasa hivi..." 

 

"Inatosha, Jack. Kwa macho yangu, wewe ni mtu wa kudharauliwa zaidi kuliko Alvin. Lazima nimekuwa kipofu wakati huo. Lakini, kwa kuwa uliniokoa mara ya mwisho, wacha tufanye tumelipishana. Sina deni lako tena.”

 

“Kwanini hujithamini Lisa?” Jack alianza kushindwa kujizuia. "Haina maana kwako kukaa hapa. Hata Alvin hawezi kustahimili mwenyewe kukaa humu.”

 

"Mimi ni Mtanzania, lakini pia nina haki za kuishi hapa Kenya. Siwezi kuondoka kwa kulazimishwa. Pia… Ninaamini Alvin ataniokoa. Hataweza kushindwa na watu kama wewe."

 

Nyakati fulani, Lisa hakuelewa kwa nini alichagua kubaki pia. Kwa mawazo tu ya Alvin ambaye kwa muda huo alikuwa kwenye matatizo, hakuweza kutamani kuondoka. Uhusiano wao ulikuwa mchanganyiko wa upendo na chuki. Hata hivyo, asingeweza kusahau kwamba kila alipokuwa katika hali ngumu, Alvin alikuwepo kila mara ili kumwokoa. Aliamini kwamba angefanya vivyo hivyo wakati huo. Ingekuwaje shetani ashindwe kirahisi hivyo?

 

"Hapana. Kamwe sitamwachia nafasi ya kubadilisha mambo.” Jack alikasirika. "Kwa kuwa huna shukrani kwa kila kitu nilichofanya, jipambanie mwenyewe, basi." Kwa hayo, Jack aliondoka kwa hasira. Hakuonekana tena tangu wakati huo.

 

Upesi simu ya Lisa iliishiwa na betri, na hakuweza kutofautisha mchana na usiku. Ghafla, uso wake uliokuwa umeumia ulizidi kuwasha huku kidonda kikichubuka taratibu na kumsababishia maumivu makali. Alihisi kuwa uso wake unaweza kuharibika. Alianza kutisha katika hali ile. Alvin angemuona tena angeingiwa na woga. Lakini ingekuwa ni jambo zuri pia. Katika hali hiyo, asingemlazimisha kumpenda tena.

 

Hakuwa na uhakika ni siku gani yule bibi aliyemletea uji alikuja tena.

Lisa alitazama bakuli la uji na kuuliza bila huruma, "umekumbuka kuniletea uji tena leo?" 

 

Mikono ya bibi huyo ilitetemeka. Hakujisumbua hata kuongea neno lolote. Alitema tu mate na kuliweka bakuli na moja kwa moja akaondoka.

 

Lisa alitabasamu kwa uchungu. Hata mtumishi wa familia ya Kimaro alikuwa na kiburi sana mbele yake. Ikiwa alitaka kuishi, hakuwa na la kufanya ila kula chakula, hata ikiwa uso wake ungeoza kabisa!....ITAENDELEA......


Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.