JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA...............................186-187
Sura ya 186
Melanie ghafla akakumbuka kwamba kulikuwa na mwanamke amejificha katika jumba lake la kifahari siku moja. Alitafuta mtu wa kuchunguza baadaye lakini hakuweza kupata chochote.
"Oh, nilikumbuka ghafla, nilimwambia amchulie Queen kabla ya hii." Bibi Kimaro alipiga kichwa chake. "Nina kumbukumbu mbaya sana."
"Oh, kumbe!" Melanie alionekana kuridhika kidogo.
Saa moja na nusu usiku, kijakazi mkuu alikuja ghafla na rundo la vitu vya gharama kubwa baada ya chakula cha jioni. Bibi Kimaro alisema, “Unapomrudisha Melanie baadaye, peleka vitu hivi kwa familia ya Ngosha pia. Melanie na wewe mtapata cheti chenu cha ndoa kesho.”
Mara moja Melanie alishusha uso wake kwa haya na kumtazama Alvin kwa matarajio, lakini Alvin alionekana kuwaka na kuuliza, “Nilikubali kufunga ndoa lini?”
"Ikiwa hautaoa sasa, unapanga kusubiri hadi lini?" Bibi Kimaro hakukasirika mara chache, lakini safari hii alipaza sauti. “Ndio hivyo, umemrudisha Jack salama, lakini sasa hivi kuna tetesi huko nje kwamba unataka kumuua ndugu yako mwenyewe. Melanie ni binti ya akina Ngosha, na familia ya Ngosha ni mojawapo ya familia kumi bora nchini.
Wanaheshimiwa na watu, kwa hiyo kwa kuoa binti wa familia na kuonyesha upendo wako, unaweza kurejesha sifa yako.”
“Haya.” Alvin alionekana kama amesikia utani. Cheko la chinichini lilimwagika kooni. "Kwa uwezo wangu na ustadi wangu, bado ninahitaji kufanya maigizo ili kujisafisha machoni pa watu?"
Bibi Kimaro alisema, “Kwa jinsi mtandao ulivyoendelea sasa, utajisafisha vipi bila kick?” Hee, mpaka bibi yule alijua mambo ya kiki, lakini Alvin bado hakumwelewa.
“Sijali.” Alvin akasimama. “Kama unafikiri nina sifa mbaya, basi mwache Jack aketi kwenye kiti cha mwenyekiti. Nina uwezo na mamlaka, hivyo sijali wengine wanasema nini.”
“Unajaribu kunipeleka kwenye kaburi langu?” Bibi Kimaro alipiga meza kwa hasira.
"Mwili wako ni mgumu sana, kwa hivyo hautakufa." Alvin aliifuta midomo yake kwa umaridadi na kwenda juu. Dakika mbili baadaye, alibeba kikapu cha strawberry na kuelekea mlangoni.
Uso wa Melanie ulikuwa mweupe wa karatasi, na Bibi Kimaro akasema kwa hasira, “Subiri. Mrudishe Melanie nyumbani.”
“Sawa.” Kulikuwa na mwanga wa hasira kwenye macho ya Alvin alipokubali. Melanie alikimbia kwa furaha na kuufuata mlango na kuingia kwenye gari lake.
Kabla hajafunga mkanda, gari la Alvin lilifyatuka kama roketi. Alvin alionekana kama anarusha kombeo badala ya kuendesha gari. Gari lililokuwa likiyumba njia nzima. Gari hilo lilifikia mwendo wa karibu kilomita 200 kwa saa, jambo ambalo lilimtisha Melanie hivi kwamba alipiga kelele njia nzima.
Baada ya kuufikia mlango wa makazi ya akina Ngosha, Alvin alifunga breki na Melanie akatapika mara baada ya kushuka kwenye gari. Alvin alitoka nje ya gari kwa umaridadi na kumpa kitambaa. Melanie alishangaa sana na kukipokea, lakini sekunde iliyofuata, alisikia sauti yake ya kupendeza ikipiga masikio yake. "Kama ningekuwa wewe, ningeachana kabisa na uhusiano huu."
"Unamaanisha nini?" Melanie alikuwa na wasiwasi kidogo.
Alvin akawasha sigara na kuing'ata huku akivuta pumzi. Kitendo hicho kilikuwa kizuri, lakini macho yake yalikuwa hayajali. “Huoni? Sivutiwi na wewe hata! Kwanini usiseme tu ukweli kwa kila mtu kuwa mimi na wewe hatuendani ili tuachane tu kwa amani.”
“Sikuamini." Melanie karibu kulia. “Alvin, unanipenda. Vinginevyo, kwa nini ulicheza nami na kuja nyumbani kwetu kwa chakula cha jioni?"
“Wewe ni kipofu.” Alvin alimtemea mate kuyasindikiza maneno hayo matatu moja kwa moja.
Melanie karibu kuvunjika. Angewezaje kumdhalilisha hivi? “Sitaki kuachana na wewe Bwana Kimaro, nimekupenda kwa muda mrefu. Siwezi kuishi bila wewe.”
"Inaonekana hunielewi." Alvin aliinua uso wake.
Melanie alishika mkono wake na kusema kwa huzuni, “Bwana Kimaro, Najua una mwanamke mwingine nje. Naweza kulifumbia macho. Babu na Bibi Kimaro pia wananipenda na watafurahi tukioana. Sifa yako imeharibiwa sasa, kwa hivyo ikiwa habari kuhusu wewe kuwa na mwanamke mwingine itaenea sasa…”
“Unanitisha?” Alvin akamshika kidevu.
Melanie alitetemeka, lakini aliuma meno na kujipa nguvu. “Bwana Kimaro, sitaachana na wewe. Ni wewe uliyechukua hatua ya kunifuata kwanza.”
"Sawa, wacha tucheze mchezo wa kuigiza." Alvin alimuachia na kuingia kwenye gari.
Melanie alilitazama gari lake likiondoka kwa macho yaliyojaa hofu na woga. Nina na yeye walikuwa na nafasi katika familia ya Ngosha kwa sababu walikuwa na familia ya Kimaro kama msaada wao. Hata Mzee Ngosha aliwatendea adabu mama na binti yake kwa sababu tu Melanie alikuwa mkwe wa familia ya Kimaro. Asingeweza kupoteza kizembezembe Bwana Kimaro. Aliamini ni lazima kulikuwa mhalifu nyuma yake aliyekuwa akimchochea. Ikabidi ajue huyo mhalifu ni nani na kumuua.
Akiwa ndani ya gari, Alvin alimpigia simu Lisa. "Unafanya nini? Niko njiani kurudi nyumbani.”
"Ninafanya kazi kwa muda wa ziada ofisini." Lisa alishtuka, si alisema hatarudi?
"Kwa nini unafanya kazi ya ziada wakati tayari usiku umeingia sana?" Sauti ya Alvin haikufurahishwa. “Subiri hapo nitakuchukua.”
Lisa aliitazama simu yake huku akihisi kuchukizwa kidogo. Alichukia sana alipokuja kumtafuta baada ya kuwa amechoka kujiachia na Melanie. Nusu saa baadaye, gari la Alvin lilisimama nje ya jengo la kampuni hiyo na Lisa akaingia kwenye gari. Gari lilijaa harufu ya manukato ya mwanamke. Ilikuwa ni harufu aliyokuwa ameisikia kwa Melanie hapo awali. Alikuwa na hakika kabisa kwamba alikuwa ametoka tu kumrudisha Melanie nyumbani. Je, hakuchoka kushughulika na wanawake wawili kwa wakati mmoja?
“Angalia nilichokuletea.” Alvin alinyanyua kikapu cha stroberry kwenye kiti cha nyuma na kukiweka kwenye mapaja yake. “Nilizichuma mwenyewe kwenye bustani ya Bibi Kimaro. Ni tamu sana.”
Alitazama macho yake kwa kutarajia kwamba angefurahia. Ilikuwa mara yake ya kwanza kujaribu kujipendekeza kwa mwanamke. Lakini, kilichomkatisha tamaa ni kwamba Lisa alizitazama tu na kutabasamu, ila tabasamu hilo lilionekana wazi kuwa la kujilazimisha tu.
"Asante." Lisa alichukua sitroberi moja kutoka kikapuni.
"Hii inaonekana kama sisi." Alvin alimshika mkono kwa nguvu, macho yake ya kupendeza yakizunguka kwa upole huku yakionyesha mwonekano wake. Lisa alisikiliza sauti yake ya upole na ya sumaku. Alipomtazama, alipoteza mawazo kwa muda. Mwanaume huyo alijua kutongoza sana. Hata baada ya kumfanyia mambo hayo mabaya, alipochagua kuwa mpole, ilikuwa vigumu kwake kujiondoa.
Alvin alitabasamu na kuinamia kumbusu kwenye midomo yake.
Midomo yao ilipokaribia kukutana, harufu ya manukato ya Melanie ndani ya gari ilimfanya ageuze uso wake, na busu lake likakwama.
Hewa yenye utata iliibuka mara moja. Muwasho ulimtoka ghafla Alvin kifuani. Alikumbuka jinsi alivyokuwa mpumbavu mapema kuchuma strawberry kwa ajili yake akifikiri kwamba angezipenda. Hata hivyo, alichopata ni majibu ya nusu nusu tu.
Hata hivyo alijua haikuwa sahihi kumlaumu na akashusha pumzi ndefu. Akamgusa kichwa. “Ninavuna nilichopanda. Nilikuumiza, lakini muda utaniruhusu kufungua moyo wako. Usijali, nina muda wa kutosha.”
Lisa alishangaa. Alifikiri kwamba angekasirika tena, badala yake alijutia matendo yake na kuahidi kutomuudhi tena. kwa kweli hakuweza kumudu matokeo.
Kisha, Alvin akawasha gari na kumrudisha Lisa hadi New Metropolis Park. Shangazi Yasmini aliosha yale matunda, na Lisa alikula matunda kwa utii. Kama Alvin alivysema, strawberry zilikuwa tamu sana na nzuri.
Walipoenda kulala usiku, Alvin alimkumbatia na kushika sikio lake, akisema kwa uchungu, “Ikiwa unazipenda, nitakuchumia nyingine wakati ujao.” Lisa alitetemeka kwenye kumbato lake na kuinamisha macho yake kwa kutabasamu.
Sura ya 187
Kesho yake asubuhi Lisa alipoinuka tu kitandani aliwasha simu yake. Alikuwa na mazoea ya kuwasha simu yake kutazama barua pepe alizotumiwa kutoka kwa watendaji wake wa kampuni na kutazama habari zilizovuma. Hoja kubwa iliyovutia watu kwenye mitandao ya kijamii ni picha zilizokuwa zikimwonyesha mwenyekiti wa kampuni kubwa ya KIM International Alvin Kimaro akiongozana na mpenzi wake mpya kuchuma strawberry.
Katika picha hiyo, Melanie alikuwa akiinamisha kichwa chake kumtazama Alvin huku macho yake yakiwa yamekunjamana kwa tabasamu. Walionekana watamu sana. Alikuwa ameshika sitroberi iliyoshikamana na strawberry nyingine, na Alvin alikuwa akimtazama kwa uso wake mzuri. Mwangaza wa machweo ya jua uliangukia kwenye nyuso zao, na kuwafanya waonekane kama jozi ya wapendanao wanaobadilishana mapenzi wao kwa wao.
Ghafla alikumbuka kile Alvin alichosema jana usiku. "Je, stroberi hii haifanani na sisi?" Heh, ni ujinga gani. Alikuwa amechukua stroberi ambayo Melanie aliichuma na kumwambia mwanamke mwingine vile. Je, hakuona aibu hata kidogo?
Naam, kulikuwa na nini cha kuonea aibu? Angeweza hata kuchuma stroberi kwa bibi yake akiwa na mpenzi wake. Ukosefu wake wa aibu ulikuwa wa kushangaza.
"Unaangalia nini?" Alvin, ambaye alikuwa amelala amemkumbatia, aliinama kutazama skrini ya simu yake. Picha iliyokuwemo ilimtia hofu na kusema haraka, “Usielewe vibaya. Bibi yangu alinilazimisha niende naye jana.”
“Mmh, ni sawa.” Lisa alisema kwa utiifu na uso uliotulia.
Uso wa Alvin ulikuwa mgumu na ulijawa na alama za kuuliza juu yake. “Unamaanisha nini kusema hivyo?”
Lisa hakuelewa kwa nini alikosa furaha ghafla na aliweza kusema ukweli tu, “Yeye ni mpenzi wako, kwa hiyo ni kawaida nyinyi wawili kuchuma strawberry pamoja. Sitakuwa na wivu. Najua mahali pangu.”
Alikuwa ni mtu tu ambaye alikuwa akimtumia kwa burudani yake. Alikuwa na utambulisho wa aibu. Alvin alimtazama kwa muda kabla ya kucheka ghafla. Lisa aliumia sana. Wema na unyenyekevu wake viliufanya moyo wake kuishia kwenye machungu. Angeweza walau kumheshimu ingawa hakumjali hata kidogo.
Alvin alikuwa na wasiwasi kwamba angeelewa vibaya na hata akajieleza kwa haraka. "Wow, Lisa Jones, wewe ni mkarimu sana. jana nilitumia nafasi hiyo kumwambia Melanie kuwa simpendi, anajidanganya tu kuwa nitamuoa" Alvin alicheka kwa ujeuri. Ghafla akainua blanketi na kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo.
Dakika mbili baadaye, alifunga mlango na kuondoka. Lisa hakumuelewa. Je, alitarajia kumwona akilia na kupata wivu? Ni yeye aliyesema kuwa Melanie atakuwa ameshika wadhifa wa Bi Kimaro, huku yeye akiishia kulala naye tu kwenye kitanda kimoja. Ingekuwa zamani angepata wivu, lakini kilichobaki sasa ni chuki yake kwake. Moyo wake ulikuwa umeganda na haukudunda kabisa kwa ajili ya Alvin.
Alvin alienda kwenye kampuni akiwa na uso uliopooza sana na mara akampigia simu Bibi Kimaro. “Ulipiga hiyo picha?” Ni watu wa familia ya Kimaro pekee ndio wangeweza kumpiga picha akiwa ndani ya nyumba hiyo.
"Ustadi wangu wa upigaji picha wa Bibi ukoje?" Bibi Kimaro alicheka. "Nimewafanya monekane vizuri pamoja, sivyo?"
“Bibi…” Alvin alipaza sauti yake akiwa amejawa na hasira.
“Unapiga kelele nini? Unajaribu kunitisha?” Sauti ya Bibi Kimaro ilikuwa kubwa kuliko yake. "Nini? Wewe ni mjukuu wangu. Siwezi kukupiga picha?”
"Hupaswi kuziposti picha zangu kwenye mitandao ya jamii bila ridhaa yangu." Alvin alijipapasa na kusaga meno.
“Kwa hiyo kama nimeziposti utanifanya nini?” Bibi mzee hakununua maneno yake hata kidogo.
Alvin alikosa la kusema kwa hasira. Bibi Kimaro alifoka kwa hasira. “Umeona kila mtu kwenye mtandao anachosema kuhusu picha yako na Melanie? Wote wanasema kwamba nyinyi wawili ni wanandoa wanaofaa na kwamba ninyi wawili mnapendana sana. Kila mtu anakusifu kwa kuwa mzuri na kumsifia mpenzi wako. Nitaruhusu idara ya PR ikutengenezee mtu anayependa mke kwa ajili yako.”
"Mimi ni mwenyekiti wa kampuni, sio nyota wa filamu anayetafuta kucheza muvi kwa mara ya kwanza." Alvin alikasirika sana akashindwa kuendelea kuongea nae tena akakata simu moja kwa moja.
Alvin aliingia kwenye mtandao na kugundua kwamba watu wengi kweli walikuwa wakimsifu yeye na mke wake mtarajiwa. Kilichomchukiza zaidi ni kwamba kulikuwa na watu wake wa karibu ambao walitoa habari kwamba alikuwa karibu kuoana na Melanie mwezi ujao. Ilikuwa ni fujo kabisa.
Kwa hasira alimpigia simu meneja wa idara ya uhusiano wa umma na kumuamuru aondoe haraka habari hiyo kwenye mitandao.
Meneja alihisi si sawa kuiondoa habari hiyo hasa ukizingatia kuwa watu walianza kusahau sifa mbaya dhidi ya Alvin na kuanza kumpongeza. "Lakini bosi sifa zako zilianza kubadilika.,,"
"Bosi ni mimi au wewe?" Alvin alimkatisha kwa ukali.
"Sawa, nitaondoa habari mara moja." Meneja alitikisa kichwa kwa huzuni.
Ingawa habari hiyo ilifutwa mara moja kwenye mitandao yote ya kijamii, suala hilo lilikuwa tayari likivuma. Kila mtu nchini Kenya alijua kuhusu hilo. Kila mtu alijua kwamba Melanie na Alvin walikuwa wanandoa sasa.
Kwa upande, Lisa hakuwa na presha kwa sababu alikuwa kishajua siku nyingi.
Kelvin alimtumia ujumbe: [Alvin ni mkatili sana kwako. Lisa, ninajitahidi niwezavyo ili kupata nguvu zaidi. Hivi karibuni, nitakuokoa kutoka kwake]
Lisa aliguswa moyo sana na kujali kwake. Jinsi Kelvin alivyokuwa mwema kwake, ndivyo alivyohisi hatia zaidi.
Siku mbili zilizofuata, Alvin hakurudi New Metropolis Park. Lisa hakujua alilala wapi kwa siku zote hizo, wala hakuuliza.
Usiku, Jack alimpigia simu. "Niliruhusiwa jana."
“Hongera sana!” Lisa alijibu kwa upole.
"Niko hapa kukusanya madeni wakati huu." Jack alitabasamu. “Si ulisema unataka kunishukuru? Nitashiriki katika hafla ya hisani kesho, kwa hivyo nitakuomba kufuatana nami." Lisa alisita mwanzoni, lakini aliposikia kwamba lilikuwa tukio la hisani, alikubali.
Siku iliyofuata saa kumi na moja jioni, Jack aliendesha gari lake na kumchukua Lisa kwenye lango la ofisi ya kampuni yake. Lisa haraka akaingia kwenye gari. Jack alitazama nguo zake alizokuwa amevaa na kumshauri. “Umependenza sana Lisa lakini mavazi yako hayafai kwa tukio husika. Nitakupeleka mahali fulani ili ubadilishe.”
Saa moja baadaye, Lisa alitoka kwenye chumba cha kuvaa akiwa amevaa nguo nyekundu ya retro.
“Nzuri!” Jack alipiga vidole vyake.
"Kwa nini nivae hivi kwa hafla ya hisani?" Lisa alichanganyikiwa.
"Hapana, ni chakula cha jioni cha hisani," Jack alisema ghafla.
Lisa alisimama na kukunja uso. “Bwana Kimaro, ulinidanganya? Siendi.”
Ikiwa alikutana na Alvin, angemkaripia kwa kuwa mwanamke rahisi tena. Labda hata angemtesa baada ya kurudi nyumbani usiku. Alimuogopa Alvin sasa.
“Nilidanganya lini? Chakula cha jioni cha hisani bado ni tukio la hisani." Uso wa Jack haukuwa na hatia. “Unanisusia? Nitapata wapi rafiki wa kike wakati huu?”
“Bwana Kimaro, sitaki uvumi uenee…”
“Utakuwa tu mwenzangu wa kike. Usifikirie sana. Mbali na hilo, usifikiri kwamba sijui. Tayari umeachana na Kelvin Mushi.” Jack alimpasulia.
Jack alipoona hajashawishika akapiga makofi kifuani kwa kicheko. “Usijali, hakuna mtu unayemfahamu kwenye chakula cha jioni cha hisani usiku wa leo. Ulipokuja Nairobi kwa mara ya kwanza, ulisema kwamba unapaswa kwenda kwenye hafla ili kukutana na watu wengi zaidi. Unapanga utafanyaje biashara zako bila kutengeneza milango?"
Moyo wa Lisa ukadunda kwa nguvu. Ikiwa alitaka kumtupa Alvin, ilibidi ajipe nguvu kwanza. Hatua muhimu zaidi ilikuwa ni kutengeneza connections.
“Sawa, nitakupa kampani.” Lisa akajitosa.
Katika Hoteli ya ya kimataifa ya Rean, Nairobi. Tukio kubwa la chakula cha jioni cha hisani lilikuwa likifanyika. Jack Kimaro aliingia huku akiwa amemshika mkono Lisa. Alikuwa amevaa suti iliyomtoa kama mheshimiwa fulani alyekuwa akitokea bungeni. Kando yake, Lisa alikuwa kapendeza sana kwenye gauni refu jekundu lililofunika mpaka viatu na nywele ndefu zenye kuvutia zililala mabegani mwake, na mdomo wenye rangi nyekundu ya divai. Alikuwa mzuri na mwenye kung'aa, mrembo asiye na kifani katika kizazi chake.
“Yule binti kando ya Jackson Kimaro ni nani? Yeye ni mrembo sana!” Mara watu wakaanza kuulizana.
"Sijawahi kumuona hapo awali."......ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.
