JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................188 -189
Sura ya 188
Mawimbi ya mjadala yalielea hewani, lakini Lisa hakujishughulisha na kusikiliza, alitazama tu skrini kubwa iliyokuwa mbele yake iliyosema 'Kimaro Foundation Charity Night'.
‘Huu ulikuwa ni usiku wa hisani ulioandaliwa na familia ya Kimaro? Je, Alvin atakuwa hapa?’ Lisa alijiuliza akiwa amejawa na hofu.
Alipotazama huku na huko, alihisi kama atazimia. Sio Alvin pekee bali hata Melanie, Bibi Kimaro, Mzee Kimaro, Lea, Valeria na wanafamilia wengine wa Kimaro wote walikuwepo. Hata Nina na Joel walikuwepo pia. Pia walishangaa kuwaona watu hao wawili.
Lisa alihisi tu miguu yake ikitetemeka. Sasa, aliweza kumuona Alvin tu machoni pake. Alikuwa amevalia suti nyeusi. Macho yake meusi na mazito yalikuwa yakimtazama kwa ujumbe ambao yeye pekee ndiye aliuelewa.
"Si ulisema ... hakutakuwa na mtu yeyote ninayemjua?" Alimtazama Jack kwa hasira kidogo.
“Ungekujaje kama sikusema hivyo?” Jack alitabasamu na kumkonyeza. “Huoni kwamba Nina na Melanie wako hapa pia? Nilikuleta hapa makusudi ili uwakoshe.”
“Jackson…” Lisa alitaka kulia. Alikuwa na nia nzuri, lakini mpango wake ulikuwa unaenda kinyume.
“Wacha waone kwamba kuna uhusiano maalumu na mimi. Tutaona ni nani atakayethubutu kukuonea siku zijazo.” Jack alimshika mkono kwa nguvu na kuelekea kwenye umati wa watu.
"Lisa Jones, kwa nini uko hapa?" Melanie alikuwa karibu kulipuka kwa hasira. "Una wivu kwa sababu Alvin yuko nami kwa hivyo ukajipendekeza kwa Jackson Kimaro ili akutungoze?"
"Mimi ni Jack Kimaro ni marafiki." Lisa alishusha pumzi ndefu kabla ya kueleza, akihakikisha Alvin anamsikia.
Alvin akazungusha glasi ya mvinyo mkononi mwake. Uso wake mzuri ulikuwa umekunjamana na haukubadilika, lakini Mzee Kimaro ndiye aliyesema kwa sauti nzito, “Jack ulimkaribia lini? Una miaka mingapi hapa Nairobi? We Jack kwanini unashindwa kuwa macho zaidi?”
Joel akamvuta Lisa pembeni yake. "Mzee Kimaro, Lisa ni binti yangu, sio mgeni."
Nina naye alidhihaki, “Mpenzi, huelewi? Binti haramu ni binti haramu tu. Waheshimiwa na wasomi wote kutoka matabaka mbalimbali wapo hapa usiku wa leo. Uwepo wake utafanya kila mtu acheke. Itaathiri sifa yako."
Jack alinyoosha mikono yake. “Mnafanya nini jamani? Ni mwenza niliyemleta. Usiingiliane ikiwa hujui ni nini kimenikutanisha naye. Utafanya mambo kuwa mabaya zaidi.”
"Inatosha, acha ugomvi," Lea alizungumza ghafla, "Jack alizungumza nami juu ya jambo hili hapo awali. Nilikubali kumruhusu aje naye.”
Kila mtu alishangaa, na macho ya Alvin yalimtoka. “Wewe…”
“Tayari utafunga ndoa na Melanie na Jack si mtoto tena,” Lea akamkatisha.
Nina alikataa kukubali. “Lea, unaweza usijue hili, lakini Lisa ni sawa na mama yake. Tabia yake—”
“Kwa kawaida najua tabia yake ni ya namna gani. Sihitaji wengine kunielekeza.” Lea alikuwa amesimama katika nafasi ya juu kwa muda mrefu. Alipotazama juu, shinikizo lilimfanya Nina ashindwe kusema neno lolote.
“Asante mama,” Jack alisema huku akitabasamu.
Lisa alichanganyikiwa kabisa. Hakuwahi kufikiria kuwa Lea angemtetea. Ilikuwa ni upuuzi.
"Kaa chini, chakula cha jioni kiko karibu kuanza." Bibi Kimaro alimpa jicho la maana Lisa. Kulikuwa na mambo ambayo hayakuhitaji kuharakishwa. Kwa vyovyote vile, asingekubali Jack na Lisa kuwa pamoja. Lisa alikuwa binti haramu na hakustahili kuwa na mjukuu wake.
Kulikuwa na watu mashuhuri wachache waliohudhuria chakula cha jioni cha hisani usiku huo. Baada ya kila mmoja kuketi, Alvin alipanda jukwaani akiwa mwenyekiti wa mfuko na kutoa hotuba. Umbo lake kamili lilikuwa limefungwa kwa suti, na kumfanya aonekane mtukufu na mashuhuri.
Hata alipokuwa akikabiliwa na mikwaju mingi mikubwa chini ya jukwaa, haiba tulivu iliyotoka kwenye mwili wake ilifanya umati kumsifu.
Melanie alimtazama mwanamume huyo jukwaani na kuzidi kupendezwa.
Aliapa ni lazima amshikilie kwa nguvu kabisa mwanamume mrzuri na mtanashati kama Bwana Kimaro.
Nina aliweza kuwaza ni nini binti yake alikuwa akifikiria na kumnong'oneza sikioni, "Ikiwa unataka kumshinda mwanamume kabisa, lazima ushinde kwanza mwili wake."
“Lakini huwa haniruhusu nimguse…” Melanie alikuwa na wasiwasi.
“Chukua fursa hiyo usiku wa leo anapolewa. Nitamwambia bibi yake akuruhusu uende chumbani kumtunza Bwana Kimaro.” Nina alitumbua macho yake kama mchawi.
Wazo lilimjia Melanie. Alipofikiria kuwa mwanamke wa Alvin, uso wake mdogo ulikuwa na aibu, lakini alikuwa akitarajia. “Mama, Lisa hataweza kupatana na Kimaro wa Pili, sivyo…?”
“Anafikiri yeye ni nani? Hastahili. Yeye ni mhalifu kama mama yake." Uso wa Nina ulikuwa umejaa dharau. "Utaona jinsi nitakavyoshughulika naye usiku wa leo."
Baada ya Alvin kushuka jukwaani, waimbaji maarufu walicheza kwa zamu jukwaani. Onyesho lilipokaribia kwisha, Jack aliinama kwenye sikio la Lisa na kusema, “Nitaenda nyuma ya jukwaa kuchukua pesa zilizokusanywa. Nitarudi baadaye.”
“Sawa.” Lisa alitingisha kichwa.
Tukio hilo lilitua machoni mwa Alvin, na kufanya kifua chake kujaa moto wa hasira. Mwanamke aliyelaaniwa! Mara tu alipotazama pembeni, alijibizana na mwanaume mwingine? Wakati huu, alikuwa hata na mdogo wake, Jack. Alikaribia kuivunja glasi ya mvinyo mikononi mwake.
Baada ya kutulia, alitoa simu yake na kumtumia Lisa ujumbe: [Nisubiri kwenye Chumba namba 408.]
Lisa alipokea ujumbe huo. Alimtazama Alvin na kumuona akitazama kwa umakini wasanii waliokuwa wakicheza jukwaani. Alimlaani moyoni. Mnafiki gani!
Kwa kweli hakutaka kwenda kukutana naye. Ilikuwa hatari sana. Aliinamisha kichwa chake na kujibu: [Unaweza kusubiri mpaka turudi?]
Alvin: [Nina hasira sana sasa. Usijaribu kuniudhi zaidi.]
Lisa akawa mpole. Alitabasamu kwa uchungu na aliweza tu kuinuka kimyakimya ili kuondoka. Alipotoka tu kwenye jumba la karamu, mwanamume mlevi wa rika la makamo alimsimamisha ghafla. "Mwanamke mrembo, una wakati wa kuzungumza chumbani kwangu kwa muda?"
“Niko busy.” Lisa hakuhitaji hata kumjua kabisa, akageuka na kuendelea na mwendo wake.
Yule mtu mnene ghafla akamshika kiganja chake na kutabasamu. "Unajua mimi ni nani? Nina pesa nyingi. Ukiwa tayari kuniburudisha kwa usiku mmoja, nitakupa milioni kumi.”
“Kwanini nisikupe hiyo milioni kumi ili upotee mbele yangu badala yake?” Lisa alikwazwa sana na yule jamaa.
"Sawa, usiseme sikukupa chaguo." Yule mwanaume mnene alimsukuma ukutani na kujaribu kumbusu kwa nguvu.
“Niache!” Lisa alimpiga kofi usoni.
“Unathubutu vipi kunipiga, wewe b*tch…” Mwanamume huyo aliinua mkono wake kuuzungusha chini, lakini kiganja kikubwa kikaushika mkono wake hewani. Kisha, mwili wa mtu mnene ulitupwa kando.
“Unathubutuje? Wewe…” Alipomwona mtu mmoja mrefu alimesimama mbele yake, yule mwanamme mnene aliogopa sana hadi miguu yake ikatetemeka. “Bwana Kimaro…”
“Bwana Kimaro, umefika kwa wakati. Alinitongoza.”
"Ndio hivyo? Mkurugenzi Majuto, unathubutu kusababisha vurugu katika moja ya hafla zetu? Inaonekana huhitaji kushiriki katika karamu za jamii ya juu katika siku zijazo.” Alvin alimwambia Hans kwa upole, “Vunja mguu wake mmoja na umtupe nje.”
“Bwana Kimaro, usi…” Mkurugenzi Majuto aliogopa sana akataka kupiga magoti na kuomba msamaha, lakini alikuwa amechelewa. Hans akamtoa nje haraka.
Sura ya 189
“Jack alikuleta hapa, lakini hivi ndivyo anavyokulinda?” Alvin alicheka kwa jeuri. Alipofikiria jinsi midomo ya nguruwe huyo aliyelaaniwa ingemkandamiza usoni ikiwa angechelewa kwa hatua moja tu, alikasirika sana na alitaka kupagawa kwa wazimu.
Lisa alitetemeka huku akisema kwa unyonge, “Hii ni karamu ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na KIM International, hivyo Mkurugenzi Majuto asingenisumbua bila sababu. Mtu fulani alimwagiza kufanya hivyo.”
“Oh? Angekuwa nani huyo?” Alvin aliinua uso wake, hakuzungumza kile alichokijua.
Lisa aliuma mdomo. Hakuamini kwamba hakujua ni nani. Alikuwa akifumbia macho tu maana mtu huyo alikuwa mchumba wake. “Sijui…” Aligeuza uso wake sekunde moja baadaye.
Alvin alimtazama kwa makini kwa muda, akadharau na kumvuta juu juu.
Hakuna mtu kati ya wawili hao aliyeona kwamba muda si mrefu baada kuondoka, mtu mmoja alitoka kwenye kona aliyokuwa amejifcha akiwafuatilia. Baada ya kuingia chumbani, Alvin aliufunga mlango kwa nguvu. Akavua suti yake na tai na kuzitupa chini.
“Lisa Jones, mimi sikufai? Kwa nini unaendelea kunilazimisha kukasirika tena na tena?”
Alvin alimsogelea hatua kwa hatua, huku uso wake ukiwa umejawa na hasira. “Kuachana na Kelvin Mushi hukuridhika, kwa hiyo safari hii ni Jack Kimaro. Huwezi kunipa amani?”
“Hapana, sikujua alikuwa akinipeleka kwenye karamu ya chakula cha jioni. Alisema tu kwamba lilikuwa tukio la hisani. Alinisaidia kutatua mzozo wa Mawenzi hapo awali, kwa hivyo nina deni kwake.” Lisa aliingiwa na hofu na hasira iliyokuwa usoni mwake na kukumbuka jinamizi alilolipata usiku ule. Uso wake mdogo mara moja ukageuka mweupe huku machozi yakimdondoka. Alipiga magoti na kumshika mkono, akimsihi, “Hapana, tafadhali usinidhuru. Ninaogopa.
Sitathubutu kufanya hivyo tena…” Mwili wake ulitetemeka kama jani, na macho yake yalijawa na hofu na woga.
Alvin aliganda. Alimtazama na kukunja ngumi kwa maumivu. Alikuwa amepiga magoti mbele yake? Wakati fulani alikuwa mkaidi na mkorofi, lakini sasa, alikuwa akipiga magoti na kumwomba amhurumie? Je! alikuwa anamuogopa kiasi gani?
Alvin alimnyanyua kwa nguvu. “Lisa Jones, huruhusiwi kunipigia magoti. Unanisikia? Wewe ni mwanamke wangu.”
“Sawa, sitapiga magoti. Mimi ni mwanamke wako. Nitasikiliza chochote utakachosema,” Lisa alisema kwa unyenyekevu.
"Hicho sio nilichomaanisha." Alvin alimkumbatia kwa nguvu. “Huna haja ya kuogopa. Nilikuambia sitakuumiza. Nina wivu tu. Umevaa vizuri sana bado umesimama kando ya Jack. Usionane naye tena siku zijazo.”
Lisa aliitikia kwa utii. “Sawa, nilikusudia tu kumlipa fadhila nilizokuwa nazo. Sitakutana naye tena.”
“Vizuri.” Alvin aliinamisha kichwa na kumbusu midomo yake. Hakujua ni aina gani ya lipstick alikuwa amepaka lakini ilikuwa na ladha kama ya stroberi. Akambusu kwa pupa. “Nifanye nini na wewe?”
Lisa alikuwa kimya muda wote na kumruhusu tu ambusu anavyotaka.
Hata hivyo, taratibu alihisi jambo la ajabu juu ya mwanamume huyo na kumsukuma kwa nguvu. “Usifanye hivi. Hafla ya hisani bado haijaisha, na mwili wangu hauwezi…”
“Najua. Sitaenda mbali, lakini acha nikushike tu.” Alvin naye hakujua kinachoendelea. Labda ni kwa sababu alikuwa amekunywa divai nyingi chini ya ghorofa, au labda ni kwa sababu Lisa alikuwa mrembo sana usiku huo. Alitaka tu kumshika mikononi mwake na kumbusu kwa nguvu.
Lisa hakuweza kupinga nguvu za mwanamume huyo na punde si punde alimbusu hadi mwili wote ukaishiwa nguvu na kulegea kabisa.
Ghafla, mlango uliokuwa umefungwa ukafunguliwa kwa nguvu na kundi kubwa la watu wakaingia kutoka nje. “Nilimsikia mhudumu akisema kwamba Mkurugenzi Majuto alimleta Lisa hapa…”
Kabla Melanie hajamaliza, aliona umbo refu na la kupendeza juu ya kitanda. Kichwa chake kilionekana kumlipuka na kuhisi kuwa ana kichaa. “Bwana Kimaro, mbona uko hapa?”
Alvin macho yakamtoka na haraka akavuta blanketi ili kuufunika mwili wa Lisa. Lisa pia alipata hofu. Alipowaona watu walioingia mlangoni, alihisi kama ulimwengu unaelekea mwisho. Alikuwa amekwisha! Wakati huo, alihisi kweli kwamba, pale Kalivari, yote yalikwisha!
Baada ya kuishi kwa zaidi ya miaka 20, hakukuwa na wakati ambapo alihisi aibu kama alivyokuwa smuda huo. Melanie Ngosha, Jack Kimaro, Bibi Kimaro, Lea Kimaro, Joel Ngosha, na Nina Mahewa wote walikuwepo. Wakawatazama watu wawili pale kitandani kwa mshtuko. Nguo zilizokuwa juu ya mwili wa Alvin zilikuwa zimevuliwa, na uso laini wa Lisa ulikuwa umejaa haiba ya mahaba. Hata mpumbavu angeweza kujua kile ambacho wawili hao walikuwa wakifanya.
Bibi Kimaro alikasirika sana hata mkono wake uliokuwa umeshika fimbo ulikuwa unatetemeka.
"Lisa Jones, wewe b*tch!" Melanie alipoteza akili kabisa na kukimbilia kumpiga kama kichaa. “Una aibu kiasi gani? Umemtongoza hata mchumba wangu!”
Hata hivyo, kabla mkono wake haujatua kofi hilo, alishikwa na Alvin na kumtupa pembeni kwa nguvu. Melanie alipoteza usawa wake na akaanguka chini.
Nina alimuunga mkono kwa haraka huku akitetemeka kwa hasira. “Bwana Kimaro, kweli ulimsukuma Melanie kwa sababu ya huyu b*tch? Bibi Kimaro inabidi leo utupe ufafanuzi. Huwezi tu kuwaonea watu namna hii!”
Mwili wa Bibi Kimaro ulikuwa ukitetemeka huku nusura azimie kwa hasira. Hakufikiria kamwe kwamba mjukuu wake mwenye kiburi angefanya jambo hilo la kuumiza na la kipumbavu.
Jack haraka akamuunga mkono na kuwatazama watu wawili pale kitandani huku wakionyesha uchungu. “Kaka kampuni tayari ni yako na haikuwa rahisi kwangu kupata mwanamke ninayempenda. Kwanini umeamua kumpokonya pia?”
Lisa alipigwa na butwaa. Jack alimpenda lini?
“Kukupokonya?” Kicheko cha chini na cha kijeuri cha Alvin kilisikika ghafla masikioni mwake. Aliongea kwa ukali, "Amekuwa mwanamke wangu siku zote, kwa hivyo nilikupokonyaje?"
Kila mtu alipigwa na butwaa, na Lea naye akauliza kwa hasira, “Mmekuwa kwenye uhusiano muda wote huu?”
Mdomo wa Alvin ukafunguka, lakini Lisa aliogopa na kumshika mkono wake kwa kusihi. "Inatosha, usiseme."
Alvin alikasirika. Mwanamke gani mjinga huyu. Hakutaka kufichua uhusiano wao hata wakati kama huo? Je, kweli alitaka kuchukuliwa kama mchepuko wake tu? "Hiyo ni sawa."
Maneno hayo mawili rahisi yaliposemwa, Melanie alihisi kama anga lilikuwa karibu kuanguka. Alilia na kupiga kelele, “Nimeelewa sasa. Nilipokwenda nyumbani kwako hapo awali, alikuwa chumbani kwako, si ndiyo?"
“Melanie Ngosha, nilishawahi kukuambia kuwa haiwezekani kati yetu na hata nilipokupa nafasi ya kuanzisha uchumba, uliwahi kuniuliza kama nina mpenzi? Au ulikuwa unaashumu tu kuwa sina?” Alvin alijibu kinyonge.
“Hata kama wewe ni nyota, unawezaje kukosa chembe ya huruma? Melanie ni mzuri sana, unawezaje kumuumiza hivi?!” Bibi Kimaro alikasirika na kuokota fimbo yake ili ampige.
Alvin hakuikwepa, akatulia tu akapigwa na fimbo. Bibi Kimaro alipoona sura yake ya ukaidi, shinikizo la damu lilipanda juu. Alipoteza fahamu na kuzirai.
“Bibi…” Alvin alishtuka na kumwachia haraka Lisa kumchukua yule kikongwe. "Pigia ambulensi haraka."
Chumba kilikuwa na fujo. Melanie alipofushwa na chuki na akachukua fursa hiyo kumshambulia Lisa, huku akikuna uso wake. “Wewe mhalifu! B*tch! Nitakuua!"
“Melanie, nitakusaidia!” Nina naye aliingilia......ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.
