JINA LA SIMULIZI............................LISA

AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................184-185

Sura ya 184

“Jitizame mwenyewe. Ulikuwa binti shupavu sana, lakini kakutesa kiasi kwamba umekuwa kama panya mdogo.” Pamela alikuwa akifa kwa hasira. “Nitakuambia ukweli. Nilipokuomba umsaidie katika kesi wakati huo, maneno yote niliyosema yalikuwa ya uongo. Hakuwa na uhusiano wowote nayo. Nilifanya hivyo kwa sababu ikiwa angeenda gerezani, nisingeweza kukutana naye tena. Hajui lolote hata kidogo.”

Lisa alipapasa paji la uso wake na kutazama jinsi sura ya Alvin inavyozidi kuwa nyeusi kama wino. Alisimama mbele yake na kumwambia kwa upole. "Pamela alifanya hivyo ili kuniokoa. Haina uhusiano wowote naye, kwa hiyo usimdhuru.”

Alvin aliona jinsi alivyokuwa akiigiza kama kuku anayemlinda kifaranga wake, moyo wake ukaudhika na kufadhaika. Alimwona kama shetani sasa?

"Sogea kando, nina njaa."

“Heeh?” Lisa alishangaa.

“Hukunisikia? Nimesema nina njaa.” Alvin akamshika mkono na kukaa kwenye benchi.

Meza ilikuwa imejaa vyakula vyenye viungo vikali, vilivyochomwa, na vilivyokaangwa. Alvin akakunja uso. "Mbona hakuna chakula kwangu?"
Alijua kwamba hawezi kula chakula cha viungo vikali.

Lisa aliganda. "Nilidhani hautakula hivi."

“Siwezi kujizuia. Ikiwa unapenda kula hivi, kwa hiyo naweza tu kwenda pamoja nawe.” Alvin alichukua uma na kuchungulia mezani. Angeweza tu kula mishikaki iliyojazwa pilipili ya kutosha. Hakujua ikiwa ni kwa sababu hakuwa na mlo mzuri huko Sudan Kusini, lakini baada ya kujaribu nyama choma, aligundua kwamba ilikuwa limechomwa vizuri na yenye ladha tamu bila kutarajia. "Agiza nyama choma nyingine."

Lisa na Pamela walitazamana kwa kutoamini. Kisha, Lisa aliagiza nyama zisizo na viungo kwa ajili ya Alvin. Yeye alianza kula mishikaki ya pilipili na Pamela.

Mishikaki ilikuwa mitamu sana, lakini pilipili nayo ilikuwa sana mdomoni mwake. Kwa kweli Alvin hakuelewa kwanini alihisi mishikaki ile kuwa mitamu japo hakuwa mpenzi wa vyakula vya migahawani. Hata hivyo, aliona kwamba uso wa Lisa ulikuwa ukionyesha sura ya kuridhika kwa nadra hivyo akanyoosha mkono kumchukua mshikaki kutoka kwenye sahani ake. "Nitakulisha."

“Kohkohhhoooh!” Lisa alipaliwa kwa mshtuko.

Alvin akampa glasi ya maji na kunywa midomo kadhaa kabla ya kutulia. kisha akasema kwa woga, "Hapana, nitakula mwenyewe."

Pamela akachombeza, “Jamani, mwache tu akulishe. Kuna umuhimu gani wa kuwa na wanaume kando yako, basi?.”

Alvin akaguna, hivi kweli mwanamume alitakiwa kufanya hivyo ili kuonyesha upendo wake kwa mwanamke? Alvin Kimaro, ambaye alikuwa ameishi kwa karibu miaka 30, alikuwa akimlisha mwanamke kwa mara ya kwanza hadharani maishani mwake. Alisogeza kijiti kilichochomekwa mishikaki iliyochomwa vizuri mdomoni mwa Lisa, baada ya Lisa kuibana kwa meno yake na kuivuta kutoka kwenye kijiti, alimwacha atafune huku akimtazama kwa mahaba. Lisa alihisi raha iliyochanganyikana na uchungu. Kwa kweli, Alvin wakati mwingine alikuwa romantic sana, na wakati mwingine haeleweki kabisa.

Alvin alimwita mhudumu na kuamuru, "leta mishikaki mingine kumi."
Kisha, akamgeukia Lisa na kusema, “Ukiwa uko pamoja nami, huhitaji kula kwa mikono yako tena.”

Lisa akaguna na kumwangalia Pamela kwa aibu. Hata hivyo, ilipendeza sana kulishwa—hata zaidi wakati mtu aliyemlisha alikuwa ni Alvin, mtu mgumu kabisa kuyateka mapenzi yake.

Kando, Pamela, ambaye alikuwa akila mishikaki yake taratibu, ghafla alihisi kama alikuwa amevamia tu meza ya wapendanao. Shetani alaaniwe, walikuwa wanamrusha roho kwa kuwa yeye alikuwa singo? Baada ya kumaliza mlo wao, Pamela alitoa kisingizio cha dharura na kuondoka haraka. Alvin alimshika Lisa mkono na kuongozana naye hadi kwenye gari. “Ulipanga kwenda wapi tena?” Lisa alichanganyikiwa. "Sinema?"

Alvin aliinua kichwa chake na kumwita Hans. "Kodisha ukumbi wote wa sinema wa Northern Sky Mall. Nitatazama filamu na Lisa baadaye.”

Lisa akapigwa na butwaa. Kukodi ukumbi mzima wa suinema kwa ajili ya filamu ya wao wawili tu? Kulikuwa na filamu maalumu alitaka kutazama naye, au pengine hakutaka tu wengine wamwone kwenye sinema pamoja naye? Nusu saa baadaye, Alvin alimpeleka kwenye jumba la sinema huko Northern Sky Mall. Meneja mkuu wa jumba hilo aliwapokea na kuwapeleka kwenye ukumbi wa wanandoa wa VIP.

Lisa alichagua filamu ya ‘action’ kwa sababu kulikuwa na mtu mwigizaji wa kiume aliyempenda sana, James Bond. Wakati wakitazama sinema, Alvin alimweka Lisa kifuani mwake. Mgongo wa Lisa ulikosa raha baada ya muda mrefu, lakini Alvin hakugundua. Simu yake iliita mara mbili na kugundua kuwa simu ya kwanza ilikuwa ya Melanie huku nyingine ikitoka kwa Bibi Kimaro.

Akainyamazia simu na kuitupa mfukoni. Akainamisha kichwa chake kwa Lisa na kumuuliza, "unapenda aina hizi za sinema?"

"Nadhani." Kwa kweli alipenda hisia za kutazama sinema na watu wengi kwenye sinema.

“Nitafuatana nawe mara nyingi wakati wowote ninapokuwa huru." Vidole vya Alvin vilikiminya kiuno chake taratibu. “Bado kinauma?”

Lisa alifikiri alitaka kumfanya tena usiku hivyo akakaidi. "Bado nahitaji mwezi mwingine mzima, angalau."

Alvin alishusha macho na kumtazama kwa kina. “Si lazima unikumbushe. Daktari tayari aliniambia. Nauliza kwa sababu Daktari Melisa alisema unaumwa leo.”

“Sijambo. Haina uchungu sasa,” Lisa alisema kwa uaminifu.

Alvin alihisi amekasirika na aliweza tu kumvuta kwenye mapaja yake. Alimbusu kwa upole na kusema kwa sauti ya upole, “Nakuahidi, sitafanya hivyo tena.”

“Mmh.” Lisa hakuamini. Haikuwa rahisi kwake kusahau tukio lile.

Baada ya filamu, Alvin alimrudisha kwenye makazi yake mapya ya New Metropolis. Lisa hakuweza kujizuia kuuliza, “Umeondoka kwa zaidi wiki moja. Si urudi kwenye makazi ya familia?"

"Hapana." Alvin alikataa kabisa. Baada ya kuoga alipitiwa na usingizi muda si mrefu akiwa amejilaza kitandani. Ilionekana wazi kutoka kwa uso wake kuwa alikuwa amechoka sana siku hiyo.

Lisa akawasha simu yake. Makala juu ya habari hiyo ilionyesha picha ya Alvin akirudi nyumbani na Jack. Jack alikuwa akishushwa kwenye ndege akiwa juu ya machela na alionekana kuwa hajitambui Uvumi ulienea kwamba alikuwa amejeruhiwa.

Siku mbili baadaye, Lisa aligundua Jack alikuwa hospitalini. Alimtembelea akiwa na zawadi na maua. Baada ya kutomuona kwa muda wa nusu mwezi, Jack alikuwa amebadilika ngozi na kukonda. Paji la uso wake lilikuwa limefungwa kwa chachi, na alikuwa akicheza na simu kitandani ili kujisahaulisha maumivu yake. Alipomwona Lisa akiingia, aliinua mkono wake kumsalimia.

Lisa alikaa chini na kusubiri kwa muda. Alipoweka simu yake chini, hatimaye aliuliza, "Je, unacheza gamme gani?"

“Wallock. Unataka kucheza pia? Niongeze kama rafiki." Jack alitabasamu, akionyesha safu zake mbili za meno meupe.

Lisa alimwambia kitambulisho chake na wawili hao wakaongezana kuwa marafiki. Kisha, alisema kwa shida, "Nilisoma habari na nikasikia kwamba kuna jambo lililokupata huko Sudan Kusini.."

"Ndio, nilinaswa na waasi." Jack alitabasamu kwa uchungu. "Nilikosa chakula kwa siku chache na hata kujeruhiwa."

"Samahani." Lisa alijisikia hatia. Kama Jack asingemsaidia kwa kamishna wa ardhi, asingemkasirisha Alvin.

“Unaomba msamaha wa nini?” Jack alicheka. "Nilikuwa na bahati mbaya tu."

"Jack, uko vizuri leo?" Mlangoni, Lea Kimaro na Mason Campos waliingia pamoja. Lisa hakutarajia kukutana nao akainuka haraka. Macho yake hayakuweza kujizuia kumtazama Mason, baba mzazi wa Jack na baba wa kambo wa Alvin. Alionekana mpole na mstaarabu kabisa.

“Kwa nini uko hapa?” Lea alikunja uso alipomuona Lisa.

“Mama, unamfahamu?” Jack akatabasamu. “Ni yule niliyekuambia hapo awali, ambaye gari lake lilichezewa na nusura afe kwa ajali. Lakini mwishowe, alichukua njia ya ujasiri na utulivu ambayo iliokoa maisha yake. Anaitwa Lisa Jones."

“Oh.” Lea mara chache aliona mwanawe akimsifia mwanamke namna hii. Alikunjua uso wake kwa tabasamu.

Sura ya 185

“Uncle, Aunty, tutaonana tena. nitaondoka sasa hivi.” Lisa hakutaka kubaki. Aliondoka baada ya kuwasalimia.

Lea aliuliza bila kuficha, "Jack, unampenda?" Macho ya Jack yaliangaza huku akiinamisha kichwa chake. "Kidogo, lakini ana mpenzi."

Lea alipigwa na butwaa na kutoridhika. "Yeye ni binti haramu wa familia ya Ngosha na hafai kuwa nawe. Isitoshe, niliona kwamba anafahamiana na Chester Choka pia. Unapaswa kujua vizuri jinsi Chester anavyopenda mabinti kama hawa.”

“Mama, Lisa si mtu wa aina hiyo. Usimwite tu binti wa haramu. Ili kuiweka wazi, nilikuwa pia mtoto haramu zamani,” Jack alijibu kwa kutoridhika.

“Wewe…” Kifua cha Lea kilijaa kwa hasira.

"Sawa, acha kubishana," Mason alisema kwa upole, "si ulisema Jack atafute mtu ambaye anapenda kuwa mpenzi wake ili asifuate nyayo zako?"

Lea akahema. “Naogopa tu utanyanyaswa sana. Alvin atamuoa Melanie. Akikutana na binti wa haramu wa familia ya Ngosha, utakandamizwa na Alvin maisha yako yote, unaelewa?"

Jack aliganda. “Alvin atamuoa Melanie?”

"Inaonekana babu na bibi yako wanataka kumpangia ndoa, haswa kwa sababu ulipata ajali hivi majuzi huko Sudan Kusini na sifa yake kuharibiwa. Joel Ngosha ni mtu mashuhuri nchini, hivyo Alvin anaweza kuokoa sifa yake kwa kuoa binti ya Joel.”

Lea alikuwa amemaliza kuongea ghafla aliposikia Mason akisema, “Bi. Jones, mbona umerudi?”

Waligeuka kutazama mlangoni na kukuta Lisa alikuwa amesimama. Uso wake ulikuwa umepauka kidogo. "Nimesahau simu yangu." Lisa alichukua simu yake na kuondoka mara moja, lakini alichokuwa akikisikia kichwani mwake ni maneno ya Lea tu. Kifua chake kilihisi kama kimepigwa ngumi kali, na kichwa kilikuwa kikipasuka kwa maumivu.

Lisa alijicheka kwa dharau moyoni! Alvin alikuwa akipanga kuoa. Jana yake tu, alikuwa amemlisha mishikaki kwa mahaba kama yote na kutazama naye filamu, na kumpa maneno mazito ya mapenzi.
Hah, kwa hiyo alitaka kuwa nao wote na kumfanya mmoja mke na mwingine mchepuko?

Jack alitazama sura ya Lisa ikipotea na mwanga wa ajabu ukaangaza machoni pake. “Mama, nampenda Lisa. Wakati mwingine, hadhi ya mtu si muhimu. Kwa kukosa maneno bora, Melanie ni mtu asiyefaa kitu, lakini Lisa ni tofauti na alikulia katika shida. Ikiwa binti haramu kama yeye atamwangusha Melanie katika siku zijazo, je, hilo halitapendeza?”

Lea akanyamaza. Hiyo ilikuwa kweli. Alikuwa amekutana na Melanie, naye alikuwa tu binti mjinga mwenye kiburi aliyedekezwa. Kuhusu Lisa
Jones…“Sawa, nitaangalia historia yake.” Lea alimwambia Jack kinyonge.

Alasiri hiyo, rundo la habari kuhusu Lisa liliwasilishwa kwenye dawati la Lea. Kilichomshangaza Lea ni kwamba Lisa alikuwa amechukua udhibiti wa kampuni kubwa ya Mawenzi ndani ya mwezi mmoja hivi. Aliwafunga wanahisa wote kwenye kidole chake. Kilichomshangaza zaidi ni kwamba Alvin alikuwa akiikandamiza Mawenzi kwa siri tangu siku chache zilizopita. Jack alikuwa amemsaidia Lisa mara moja kuhusu Mawenzi na mara akatupwa Sudan Kusini na Alvin.

Mason Campos alikuwa kishaelewa kisa cha Jack kutupwa Sudan Kusini. “Jack alimkasirisha Alvin kwa sababu alikuwa akijaribu kumsaidia Lisa Jones.

"Nafikiri Melanie lazima alimshawishi Alvin amkomeshe Lisa, lakini hakutarajia Jack angeingilia kati, kwa hivyo alikosa furaha." Lea alikasirika zaidi baada ya kugundua ukweli.

Mason akampiga bega. "Achana nayo. Si Alvin tayari amemrudisha Jack? Nadhani Lisa sio mbaya, na Jack anampenda msichana huyu sana. Ni kwamba ataweza kumsaidia sana atakapoonewa na familia ya Ngosha.”

Moyo wa Lea ulitetemeka. "Ingawa yeye si mzuri kama nilivyokuwa zamani, bila shaka atakuwa bora kuliko Melanie katika siku zijazo."

Alifikiria maneno ya Jack. Ikiwa Mawenzi Investiments ingeweza kuinuka haraka na kushamiri huko Kenya, Lisa angeweza hata kuwa jiwe kuu la kukanyagia la Jack. Jambo muhimu zaidi ni kwamba Joel alimpendelea Lisa zaidi kati ya binti zake wawili, kwa hiyo ikiwa wangemsaidia, Joel angekumbuka wema wao na kwa hakika kuchukua upande wa Jack katika siku zijazo.

“Wacha wawasiliane. Tutaona jinsi mambo yanavyokwenda.” Lea alikuwa mfanyabiashara na alikuwa akifikiria kila wakati kwa faida ya kampuni yake.

Ofisini, Lisa alitazama wakati. Ilikuwa saa kumi na mbili jioni hivyo ilibidi ajiandae kurejea nyumbani mapema. Wakati huo Alvin alimtumia ujumbe ghafla. [Sitarudi usiku wa leo. Nenda ulale mapema.]

Ilionekana kana kwamba hakukuwa na haja ya kurudi haraka. Aliwasha tena komyuta yake ili aendelee na kazi lakini hakuwa na mood hata kidogo. Kichwa chake kilivamiwa na maswali ya ajabu ajabu. Je, angekuwa akijivinjari na Melanie usiku huo? Au alikuwa anarudi kwenye makazi ya rasmi ya familia ya Kimaro kuzungumzia harusi yake?

Alikuwa karibu kuoa. Ikiwa angeendelea kumbana Lisa namna ile baada ya ndoa yake, Lisa angejidharau sana maisha yake yote. Ilibidi awe na nguvu ili aweze kuachana naye mapema iwezekanavyo.

Katika makazi ya kifahari ya familia ya Kimaro, Alvin alishuka kwenye gari na kumuona Melanie akiwa amemshika mkono Bibi Kimaro huku wakienda kutembea bustanini. Alikunja uso na bila fahamu alitaka kugeuka, lakini Bibi Kimaro alikuwa amemwona. “Alvin, uko kwa wakati. Melanie nami tunaenda kwenye bustani kuchuma matunda, njoo jiunge pamoja nasi.”

“Bibi, nimechoka. Nataka kurudi chumbani kwangu—” Alvin alihisi kukereka.

“Nataka unisindikize na unasema kwamba umechoka, ina maana hunipendi kiasi hicho?” Uso wa Bibi Kimaro mara moja ukawa haupendezi. Alvin hakuwa na jinsi zaidi ya kuwafuata bustanini.

Bibi yake kwa makusudi alibaki nyuma kwa hatua kadhaa na kuwaacha wawili hao watembee mbele yake. Njiani, Melanie alizungumza na Alvin, lakini kwa kila sentensi kumi Alvin alijibu moja tu. Baada ya kufika kwenye bustani ya strawberry, Melanie alichuma moja na kuonja. Macho yake yalikuwa yakiangaza. “Bwana Kimaro, stroberi ni tamu sana.”

"Hujawahi kula strawberry hapo awali? Unahitaji kuzidisha kiasi hicho?" Alvin alishindwa kujizuia kusema kwa kejeli.

"Unasema nini?" Bibi Kimaro alimpiga na fimbo yake kwa hasira.
"Bibi, usimpige." Melanie alimsimamisha haraka yule bibi na kumtazama Alvin huku akiona haya. “Nimejitia aibu Bwana Kimaro. Stroberi ni laini na nzuri, kwa hivyo wasichana wanazipenda sana.”

Alvin akawaza baada ya kusikia maneno yake. Lisa pia angezipenda, sawa? Alionekana kumuogopa sana siku hizi, lakini bila shaka angefurahi ikiwa angemwonyeshea mapenzi motomoto. Kwa hivyo, aliinua kikapu na kuchuma stroberi kwa bidii, akichagua kubwa zaidi na nyekundu zaidi.

“Mpenzi, tazama hizi, zimeiva vizuri sana.” Wote wawili walikua pamoja kama ua la lotus. Melanie aliweza kuchuma strawberry hizo huku akitabasamu kwa furaha.

Tukio hili lilipigwa picha haraka na Bibi Kimaro ambaye hakuwa mbali. Lo, mbinu yake haikuwa mbaya. Kutoka kwenye picha, walionekana kama wanandoa wenye upendo. Alvin hakuona na akaendelea kuchukua stroberi kutoka mkononi mwa Melanie na kuiweka kwenye kikapu chake. Angemuonyesha Lisa baada ya kuirudi usiku, bila shaka angeipenda.

Melanie akaguna kwa mshangao. Alvin alimaanisha nini kwa kuiondoa bila neno lolote? Je, ilimaanisha kwamba aliipenda sana? Ilikuwa nadra kwamba Alvin alitaka kitu chake. Moyo wa Melanie ulihisi ladha ya utamu.

Baada ya kumaliza kuchuma matunda, Bibi Kimaro alimwambia mpishi, "Chukua stroberi kwenye kikapu cha Alvin na uandae keki ya strawberry."

"Nina matumizi mengine ya stroberi hizi." Alvin alichukua kikapu na kukiweka juu.

Uso wa Melanie ulibadilika kidogo. Ilionekana kana kwamba alikuwa hajafikiria juu yake. Ikiwa Alvin alichukua nyingi kiasi kile, ilikuwa dhahiri alikuwa akimpelekea mtu. Sasa ni nani huyo aliyekuwa akipelekewa hizo strawberry?.....ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.