JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA...............................182-183
Sura ya 182
Alvin alikuwa amemaliza tu kuongea wakati simu yake ilipoita. Alipoitoa nje ili kuona, Lisa aliona neno 'Bibi' kwenye skrini. Alvin akatoka nje na simu. "Bibi, kuna kitu kilitokea?"
“Siwezi kukupigia kama hakuna kilichotokea? Unashughulika na nini siku nzima? Hujarudi kwenye makazi ya familia kwa siku kadhaa. Mama yako amerudi, kwa hivyo lazima uje kujumuika na familia leo."
Alvin alitazama kwenye mlango wa chumba cha kulala na kukataa. "niko busy."
“Uko busy na mambo gani?" Bibi Kimaro aliuliza kwa hasira, “Lazima uje. Familia nzima itakula pamoja leo.”
Alvin alidhihaki, “Hivi kweli ni mlo tu au kuna ajenda nyingine? Mnataka kunilazimisha nimrudishe Jack?”
Bibi Kimaro alihema. “Alvin, usisahau hii, ni kwa sababu mimi na babu yako tuliendelea kusisitiza kwamba wewe uchukue jukumu la kuongoza kampuni na kumzuia mama yako asisimamie mambo ya kampuni. Tulikuruhusu wewe na Jack kuwa kwenye kampuni licha ya mama yako kuwa hajaridhika na hilo. Kila mtu anajua kwamba Jack ni kipenzi cha mama yako. Ukimchokoza Lea, hata hivyo, haitakuwa rahisi katika siku zijazo atakaporudi kwenye kampuni.”
Alvin alicheka. “Sawa, nitamruhusu arudi.”
"Hiyo ni nzuri." Bibi Kimaro alifurahi sana. "Kwa hiyo utakuja kula chakula cha jioni nami?"
"Bibi, nimekuambia niko busy kwa sasa." Alvin alisisitiza.
Bibi Kimaro alikasirika tena. “Hauko tayari hata kunisindikiza kwa chakula cha jioni? Unafanya nini huko nje, una mwanamke? Usifikiri mimi ni mzee. Nilisikia kwamba ulimpeleka mwanamke Oasis hapa juzijuzi na kulala naye.”
Alvin alicheka. Ni lazima kuwa Melanie ndiye aliyempelekea bibi yake udaku huo. Ni yeye tu aliyeiona siku hiyo, na aliapa angemfunza namna ya kufunga mdomo wake siku nyingine. "Bibi, mimi si mwanamume, kwani kipi cha ajabu?"
“Melanie hakutoshi?” Bibi aliuliza kwa hasira.
“Simpendi na sitaki kumsikia. nakata simu sasa hivi.” Alvin alimjibu kijeuri bibi yake, akakata simu.
Asubuhi iliyofuata Lisa aliposhuka chini, alimuona mtu wa ziada kwenye jumba hilo la kifahari. Alikuwa ni Shangazi Yasmini, ambaye aliwahi kukutana naye huko kwenye makazi ya familia ya Kimaro hapo awali.
Shangazi Yasmini alitabasamu kwa upole. "Bwana Kimaro alinihamisha hapa kutoka kwa makazi ya zamani ili kukutunza."
“Asante, Shangazi Yasmini.” Lisa alikuwa na aibu kidogo. Baada ya yote, Aunty Yasmini alijua utambulisho wake na angeweza kumdharau moyoni mwake.
Shangazi Yasmine aliweza kusoma mawazo yake na akasema kwa kawaida, “Nilimlea Bwana Kimaro. Mimi ndiye mtu ambaye ananiamini zaidi katika makazi ya familia, kwa hiyo lazima awe anakujali sana ikwa kuniomba nikuhudumie.” Lisa alitabasamu kwa huzuni. Alimwonea aibu sana bibi yule.
Punde, Alvin alibadili nguo zake na kutoka nje. Walikaa pamoja kwa kifungua kinywa. Kifungua kinywa cha Shangazi Yasmini kilikuwa kitamu na Lisa alikipenda sana, lakini Alvin hakula sana.
Aunty Yasmini akahema. “Bwana Kimaro, huwezi kula kidogo namna hii. Unapaswa kula zaidi, au mwili wako utachoka."
Lisa akanyamaza. Hakuwa anakula? Kwa chakula alichokuwa akipika yeye angeweza kula sahani mbili au tatu kwa kila mlo. Alionekana kuwa amepoteza uzito mwingi baada ya kurudi Nairobi.
“Shangazi Yasmini, sina njaa.” Alvin alipomaliza kuongea simu yake iliita tena. Wakati huu, alijibu na ghafla akashtuka, sura yake ikibadilika. "Sawa, nitarudi kwenye kampuni mara moja."
“Shangazi Yasmini, mtengeneze Lisa chakula kitamu zaidi saa sita mchana ili kuutunza mwili wake.” Alvin alienda kwa Lisa ili ambusu kichwa kabla ya kugeuka kuondoka.
Lisa hakujua kilichotokea na aliona tu kwamba alikuwa na haraka. Baada ya kifungua kinywa, kipande cha habari kilitokea kwenye simu yake. Jack Kimaro alikumbana na hatari huko Sudan Kusini na kwa sasa hakujulikana alipo.
Habari kuhusu familia ya Kimaro zilikuwa zikizungumzwa zaidi nchini humo. Habari hiyo ya kutoweka kwa Jack Kimaro ilikuwa ni miongoni mwa habari zilizovuma na kutafutwa sana mitandaoni nchini humo. Pia alionekana kujadiliwa kwenye mada mbalimbali za vipindi vya televisheni na redio nchini humo.
Kutoweka kwa Jack Kimaro: [Nilisikia kwamba Jack Kimaro alilazimishwa kwenda Sudani Kusini na kaka yake mwenyewe. Vita mara nyingi huzuka Nchini humo kwa sasa. Ni dhahiri nini kingetokea ikiwa angepelekwa huko kwa wakati huu.]
Kutoweka kwa Jack Kimaro: [Nilisikia kwamba mzozo wa nchi ya Sudan Kusini asubuhi ya leo ulisababisha kurushiana mabomu na kulikuwa na majeruhi wengi. Bwana Jack Kimaro huenda kilipatwa na bahati mbaya.]
Kutoweka kwa Jack Kimaro: [Alvin Kimaro hana huruma kabisa. KIM International tayari ni yake, lakini hatamuacha mdogo wake mwenyewe.]
Habari kuhusu kutoweka kwa Jack Kimaro ilikuwa ni habari ya mjini kwa Kenya nzima. Uso wa Lisa ukazidi kufifia. Jack alipata ajali? Iwapo Jack asingemsaidia, asingepelekwa huko na Alvin. Hii ilimaaanisha kuwa alikuwa na hatia kwenye hilo, lilikuwa kosa lake lote!
•••
Ndani ya KIM International, Alvin alikuwa amefika tu kwenye ghorofa ya juu wakati mama yake, Lea Kimaro, alipomkaribisha kwa kofi la uso. Akamshika mkono. Nywele za Lea zilikuwa zimechafuka huku macho yake mekundu yakiwa yamejawa na hasira. "Alvin, ikiwa chochote kitatokea kwa Jack, hakika utazikwa pamoja naye!" Mwili wake ulitetemeka, na mkono wake chini ya mkono wa Alvin ukatetemeka kidogo.
Kwa upande mwingine, Mason Campos, baba yake na Jack, alifunga mkono wake kwa bega la Lea. “Lea tulia. Jambo muhimu zaidi sasa ni kwenda kumtafuta Jack. Nimemwambia sekretari aandae tiketi. Nitasafiri kwa ndege hadi Jubah baadaye.”
“Wewe?” Lea alionekana kuwa na wasiwasi. “Lakini hali ya huko ni ya machafuko sana sasa. Vita vinaweza kuzuka. Ikiwa chochote kitakupata—”
“Hata kama Jack amekufa, bado ni lazima nitafute mwili wake na kumrudisha.” Mguso wa maumivu makali ulipitia macho ya Mason.
“Hakuna haja ya hilo. Nitakwenda mimi mwenyewe,” Alvin aliongea bila kujali na kugeuka kuondoka.
“Hapana. Nitajuaje ikiwa un mpango wa kwenda kummaliza Jack huko? Nenda na Mason,” Lea akaamuru, “Lazima umrudishe salama.”
Upande wa mdomo wa Alvin ulijivuta kwa ujeuri kabla hajaondoka.
Hans alikasirika sana aliposikia maneno ya Lea. “Bi. mkubwa naye amezidi sana. Hata iweje, wewe pia ulitoka tumboni mwake. Bwana Kimaro, ukiniuliza, hupaswi kwenda kabisa. Acha tu hao wawili baba na mwana wakafie huko.”
“Si unaona jinsi ninavyoshambuliwa kwenye mtandao? Picha yangu kwa sasa imeharibika, kwa hivyo nitaenda huko ili kusafisha jina langu, na… Sidhani kama Jack amekufa. Baada ya yote, habari zimeenea haraka sana. Naamini kwamba kuna mtu aliyeivumisha kimakusudi.” Alvin alidhihaki.
Kabla ya kuingia kwenye ndege, Alvin alimpigia simu Lisa. “Kuwa makini. Lazima niende kwa safari ya kikazi kwa siku chache, kwa hiyo chukua dawa zako na ukae nyumbani kwa utiifu.”
Baada ya kimya cha sekunde chache, Lisa aliuliza kwa sauti ya chini, “Niahidi kwamba hutamdhuru Jack?”
Ilionekana kana kwamba kuna kitu kinapasuka kifuani mwake. Moyo wa Alvin ulikuwa mzito na mchungu ghafla. Wapendwa wote walio karibu naye hawakumwamini, akiwemo yeye. Kila mtu alisema kuwa Sudan Kusini ilikuwa hatari, lakini hakuna aliyejali yeye kwenda huko, kila mtu alimhurumia Jack.
“Sawa.” Alicheka na hakutaka kueleza zaidi. Haijkuwa na maana hata hivyo.
Baada ya kukata simu, alimgeukia Hans. “Umeniletea dawa nilizokuwa nikinywa?”
Hans alipigwa na butwaa. Kisha, akikumbuka jinsi Chester alivyosema kwamba huenda hali ya Alvin ilikuwa imerudi tena, hata hivyo alimkabidhi dawa.
Sura ya 183
Wiki moja baadaye, Pamela aliongozana na Lisa hadi hospitali ili kuondolewa mshono wa nyuzi. Chester binafsi alikwenda kwenye maegesho ya hospitali ili kukutana na watu hao wawili. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Lisa kukutana naye, na ilibidi aseme kwamba marafiki wa Alvin wote walionekana kama wanamitindo bora.
Chester alivaa koti jeupe la kidaktari na miwani. Umbo lake lilikuwa refu na alionekana mpole. Tabasamu kwenye mdomo wake lilimfanya aonekane mpole na mwenye urafiki, mtu mzuri na asiyejali.
Pamela alishtuka alipomona na kutania kwa sauti kubwa, “unaonekana kama si daktari bali mwanamitindo wa kiume anayepiga picha mbele ya kamera kwa ajili ya filamu."
"Una utani mzuri, Pamela." Chester alitabasamu. “Twendeni. Nimeshaandaa daktari atakayekuhudumia huko.”
“Pole kwa usumbufu. Naweza kwenda peke yangu.” Lisa aliona aibu. Baada ya yote, alikuwa akienda kwenye idara ya magonjwa ya wanawake.
Chester akatikisa kichwa na kutabasamu. “Hapana, hakuna shida kabisa. Alvin mwenyewe alinipigia simu na kunisisitiza nikuhudumie mimi mwenyewe.”
Lisa alishindwa kujizuia kuifikiria ile simu aliyoipokea usiku wa kuamkia jana yake. Kweli Alvin alikumbuka na kumpiga simu kumkumbusha akatoe nyuzi.
Wakati watu hao watatu wanakaribia kupanda lifti, ghafla sauti ya mwanamke aliyemfahamu ilitoka nyuma yao. “Dokta Choka…”
Watu wale watatu wakageuka, na uso wa Lisa ukainuka kidogo. Alikuwa Melanie. Kando yake alisimama mwanamke mwenye hadhi na mrembo aliyejipodoa vilivyo. Alionekana kana kwamba alikuwa na umri wa miaka 50 hivi, na mwili wake mnene kiasi na mrefu ulitoa haiba kama vile alikuwa ameishi katika tabaka la juu kwa muda mrefu. Alimfanya Melanie aonekane kama kijakazi wake tu.
"Anti Lea, ni muda mrefu." Chester alichukua hatua ya kumsalimia kwa heshima. “Umerudi?”
"Ndio, Jack alipata ajali, kwa hivyo ningewezaje kubaki nje ya nchi?" Lea aliwatazama Pamela na Lisa. Wote wawili walikuwa wasichana wachanga katika miaka yao ya mapema ya 20 na walionekana warembo kabisa. Alijua kuwa Chester alikuwa mvulana wa kuchezea mabinti, kwa hivyo alifikiria tu kwamba Lisa na Pamela pia walikuwa wanawake wapuuzi. Hakujishughulisha kuwatazama vizuri.
Melanie ndiye aliyebetua midomo yake na kusema, “Lisa Jones, kwa nini uko hapa? Oh, mimi nimekupata. Lazima uwe ulillala na Dokta Choka ili kurudisha lile shamba."
“Melanie, hadhi ya Dokta Choka si ya kawaida kama unavyodhani, kwa hivyo tafadhali pitia maneno yako kwenye kichungi kabla ya kuongea. Usiwasingizie wengine kiholela,” Lisa alijibu kwa hasira.
Melanie aligeuza macho yake na kumwambia Lea, “ma’mkwe, huyu ni binti wa haramu wa baba yangu.”
Pamela alikasirika. “Unamwita nani binti wa haramu? Wewe ni mdogo kuliko yeye. Ni wazi kwamba mama yako alifanya chochote kilichohitajika ili kuolewa katika familia ya Ngosha."
"Wewe ni nani? Nani alikupa haki ya kuongea?" Melanie akatamba. "Lisa Jones, wewe ni malaya tu kama mama yako. Nakuonya usije ukaaibisha jina la familia ya Ngosha huko nje.”
Lisa alikunja uso, lakini Chester alizungumza kwa kuonya kabla hajaweza, “Binti Ngosha, angalia maneno yako. Lisa ni rafiki wa rafiki yangu. Ukisema maneno ya kashfa kama haya na rafiki yangu akagundua, atakuchanachana usoni.”
Melanie hakutarajia Chester angemsaidia Lisa na alilalamika kwa huzuni. “Dokta Choka mimi ni mpenzi wa Alvin Kimaro. Yeye pia ni rafiki yako mzuri—”
Chester alimtazama kwa upole. "Ndio hivyo? Alvin hakuwahi kunifahamisha kamwe.”
Melanie alikasirika, na Lea akasema bila subira, “Chester, ninaweza kuwa nimekasirika sana siku hizi kwa sababu ya tukio la Jack. Kifua changu kinahisi kuwa kimefungwa na kutokuwa na raha. Nifanyie vipimo.”
Chester alikuwa na wasiwasi. Lea alikuwa mzee, kwa hiyo haingefaa kumkatalia.
Lisa alisema, “Dokta Choka, usijali, we kamhudumie tu mama. Nitapanda juu peke yangu.”
"Sawa, nipigie ikiwa unahitaji chochote." Chester aligeuka ili kuondoka mara simu ya Lea ikaita ghafla. “Nini… Wamerudi? Sawa… Sawa, tutaenda kwenye uwanja wa ndege mara moja.”
Baada ya kukata simu, Lea alitoa tabasamu adimu kwa Melanie. “Jack na Alvin wamefika tu kwenye uwanja wa ndege. Twende, tutaendesha gari na kuwachukua kisha tutarudi kuchunguzwa wakati mwingine.”
“Ndiyo, ma’mkwe. Nimemkumbuka pia Alvin.” Melanie alimtazama Lisa kwa mbwembwe na kuondoka haraka na Lea.
Pamela alimpa Lisa sura ya woga na huruma lakini aliona sura yake imejaa utulivu. “Twende, lifti iko hapa.”
“Inaonekana naweza kukusindikiza tena.” Chester akawafuata ndani na kukohoa taratibu kwenye ngumi yake. "Melanie amezama tu katika mawazo yake mwenyewe. Moyo wa Alvin uko pamoja nawe. Kimsingi sisi ni ndugu zake na tunamuelewa zaidi, hivyo usifikirie kupita kiasi.”
“Sivyo.” Lisa alitabasamu naye. Hakika alifarijika. Ilionekana kuwa Jack alikuwa sawa.
Alipotoka hospitalini, Pamela aliogopa kwamba Lisa angeweza kuruhusu mawazo yake yaende kinyume chake ikiwa angekuwa peke yake, akamwambia, “Twende tukapate chakula. Najua mgahawa wa kitanzania hapa Nairobi wenye chakula kizuri sana.”
“Hakika. Bado sijala kwenye mahakama za chakula za Nairobi.” Lisa aliunga mkono.
Wawili hao waliendesha gari na kuingia kwenye mgahawa mmoja uliokuwa ukipika vyakula vya Kitanzania nakuagiza chakula wakati Alvin alipopiga simu ghafla. “Uko wapi?”
“Ninakula mtori na chapati hapa kwenye mgahawa wa kichaga,” Lisa alijibu kwa woga, akiogopa kukemewa naye. Baada ya yote, alichukia kula vitu kama hivyo.
Alvin alinyamaza kwa muda kabla ya kusema, “Nitumie anuani ya eneo nitakuja kukuchukua.”
Lisa aliganda. Ina maana Melanie hakwenda kumpokea? Kwanini alikuwa anakuja kwake mara baada ya kurudi kutoka Sudan Kusini badala ya kurudi Mlima wa Sherman pamoja na mama yake na mchumba wake?
“Niko katikati ya jiji. Mazingira ya hapa ni mageni sana kwangu…”
“Usinicheleweshe.” Sauti ya Alvin ikakosa subira, Lisa hakuwa na jinsi zaidi ya kumpa anuani ya eneo.
Pamela akawa mwenye huzuni. “Anakuja hapa kwa ajili ya nini? Nitajisikia vibaya kula akiwa hapa.”
“Aling’ang’ania kuja, ningethubutu vipi kumwambia asije? Vinginevyo, anaweza kushuku kuwa niko pamoja na Kelvin tena.” Lisa alitabasamu kwa uchungu.
Dakika 20 baadaye, Alvin alionekana kwenye lango la ukumbi wa chakula. Alikuwa amerudi kutoka Sudan Kusini, na ni wazi alionekana kwamba alikuwa ameteseka kidogo huko. Ngozi yake ilikuwa nyeusi, lakini alionekana kujikaza kiume zaidi. Haiba ya mwili wake ilikuwa kama panga kali, na kuwafanya watu wajisikie kuwa hayuko katika anga za hapa.
Alvin akasogea na kukanyaga kwa bahati mbaya kipande cha tishu kilichotupwa chini. Alikwaruza kiatu chake kwa nguvu lakini hakuweza kukiondoa. Uso wake ukazidi kuwa mweusi zaidi na zaidi.
Lisa aliinama chini ili kuvuta tishu ile kutoka kwenye kiatu chake, lakini Alvin alimvuta mara moja. "Unafanya nini?"
"Nakusaidia kukiondoa." Jibu la Lisa lilikuwa la tahadhari sana.
“Nyanyuka tuondoke.” Alvin hakujali hata kusalimia Pamela.
Lisa akawa mgumu kidogo. “Unamaanisha nini kusema hivyo? Chakula ndo kwanza kimefika tu.”
Pamela naye alikasirika. “Bwana Kimaro, nilitaka kusema hili kwa muda mrefu. Lisa amechumbiwa na Kelvin Mushi, na Kelvin alipoteza figo kwa sababu ya kumwokoa. Sasa bado una shida gani na Lisa? Wewe pia umemchumbia ndugu yake bila hata aibu, na bado hujaridhika, umempiga nusura ya kumuua, lakini hujisikii hatia hata kidogo. Hata kama wewe ni mtu mzito, ndiyo utumie hadhi yako kumnyanyasa binti wa watu asiye na hatia, kwanini?"
"Pamela, acha!" Lisa aliogopa na kutokwa na jasho baridi kwa maneno hayo ya Pamela......ITAENDELEA......
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.
