JINA LA SIMULIZI............................LISA

AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................167 -168

Sura ya:167

Kufikia wakati anatoka majini, kijakazi alikuwa ametoweka. Lisa aligundua kitu. Kijakazi hapo awali alikuwa amemtumia Bibi Kimaro kama kisingizio cha kumvuta hadi eneo hilo hivyo alijua alikuwa ameingia kwenye mtego. Hakujua mbaya wake alikuwa ni nani, kwa hiyo ilimbidi kuondoka haraka. Alitoa simu yake ili ampigie baba yake, lakini ilikuwa imezama ndani ya maji hivyo ilikuwa haifai tena. 
 
“Nani wewe?” Nyuma ya msitu wa mianzi, mwanamume mmoja alitembea kwa ghafla akiwa kifua wazi. Sehemu ya chini ya mwili wake ilikuwa imefungwa kwa taulo ya kuogea, na uso wakehau kuwa mgeni kwake… Alikuwa Willie Kimaro!
 
Wakati huo, Lisa alielewa picha iliyokuwa ikiendelea. Alipumua kwa nguvu na kucheka. 
 
"Lisa, unafanya nini hapa?" Willie alishtuka na kujifunika kifua kwa haraka. “Ondoka haraka. Alvin ataniua kama ataniona na wewe hapa.”
 
"Nimedanganywa na mtu hapa." Lisa akatoka kwenye maji. Nywele zake zilikuwa zimelowa, na nguo zake ziling’ang’ania umbo lake lenye utata. Ikiwa ni mtu mwingine yeyote, Willie bila shaka angegeuka kuwa mnyama, lakini hakuwa na ujasiri huo kwa Lisa Jones.
 
“Nguo zako zimelowa. Kwanza—” Kabla hajamaliza kusema, sauti za hatua zilisikika kutoka nje ya ua.
 
Lisa aliogopa sana. Ikiwa watu wangemwona kajiloweka kwenye chemchemi ya maji moto ambayo Willie alikuwa akiogelea ndani yake, asingeweza kujieleza akaeleweka.
 
Willie alimvuta pembeni haraka na kumwambia, “fanya haraka, kimbilia ndani kupitia upande huu. Chumba cha kwanza kwenye ghorofa ya pili ni cha Alvin. Nitamjulisha baadaye.”
 
Baada ya Lisa kukimbia, Willie alirudi haraka kwenye chemchem ya maji moto na kukutana na Valeria, Nina, Queen, na wengine wengi waliokuwa wakitembea haraka. Hata mama yake, Iveta, alikuwepo pia.
 
“Nyie wote mnafanya nini hapa? Mmekuja kunitazama nikioga?” Willie alitabasamu na kuwazuia.
 
“Toka!” Iveta alimkazia macho. "Nilisikia mtu akisema kwamba Lisa Jones yuko pamoja nawe huku. Alikuwa anafanya nini? Hujamfanya chochote?” Iveta alijua mwenendo wa mwanawe na aliogopa kwamba alikuwa amefanya jambo la kipuuzi tena. Hakutaka kumuudhi Joel Ngosha na pia alimdharau binti wa nje kama Lisa. Hakutaka kabisa kusikia mwanaye anajihusisha kimapenzi na Lisa.
"Unasema nini?" Willie alichanganyikiwa. "Nilikuwa najiloweka tu kwenye chemchemi ya maji moto."
 
“Willie, kijakazi aliona kwa macho yake kwamba hapo mapema ulimpelekea matunda Lisa kisha baadaye akakufuata kwenye chemchem ya maji mtoto. Tunajua wewe ni mtu wa aina gani. Usiniambie umemfanyia kitu.” Valeria hakuamini kabisa kama Willie katoweka kimaajabu.
 
“Mam’dogo Valeria, kwanini uniheshimu hata kidogo? Ina maana mimi ni mnyama kiasi hicho?” Willie alikasirika sana.
 
"Inatosha. Niondokee!" Iveta alimsukuma mbali kwa haraka.
 
Kundi la watu liliingia kwa kasi na kukagua kwenye chemchem ya maji moto kwa muda mrefu lakini hawakupata mtu yeyote.
Nina alipigwa na butwaa. Hii haikuwa jinsi mchongo wao ulivyotakiwa kwenda. Aliamini mtu kama Willie bila shaka asingekuwa na uvumilivu wa mhemuko alipomuona msichana mzuri kama Lisa, lakini, sio tu kwamba hapakuwa na dalili yoyote ya Willie kumbaka Lisa, lakini pia Lisa alikuwa ametoweka kimaajabu.
 
“Mmemaliza?” Willie aliuliza kwa sauti ya hasira. “Nilwaambia mimi sijamuona hapa. Nyie mnakera sana. Mimi nimekuja peke yangu kuogelea hapa,” 
 
“Ameenda wapi? Hawezi kutoweka hewani tu!” Nina alibadilisha mbinu zake kwa haraka. “Ni mtoto wa Joel. Jambo baya likitokea kwake, nitakuwa nimekwisha.”
 
Valeria pia alisema, “Usijali, nitatuma watu wamtafute. Kwa kuwa mlikuja kwenye makazi ya Kimaro kama wageni, kwa hakika hatutaruhusu baya lolote litokee kwake.”
 
Alipoona kundi hilo la wanawake wakifanya kitendo cha ajabu kwa Lisa, Willie alituma ujumbe kwa Alvin kwa siri.
•••
Katika jumba la sinema la faragha, Alvin, ambaye alikuwa na uso uliojaa kero, aliusoma ujumbe ule na mara akasimama na kumwambia Melanie. “Nina kazi ya dharura ya kushughulikia. Unapaswa kuendelea kutazama bila mimi." Kisha, aliondoka kabla ya kumngoja Melanie ajibu.

Alvin akaelekea chumbani kwake haraka. Hakukuwa na taa hata moja, na mwanga hafifu wa mbalamwezi ukaangaza ndani kupitia madirishani. Chumba kilikuwa tupu. Alienda moja kwa moja kwenye kabati la nguo na kuwasha taa. Mwanamke aliyekuwa akivaa nguo zake alitoa sauti ya tahadhari na kuufunika mwili wake kwa mlango wa kabati la nguo. Macho yake meusi yalimfanya aonekane kama kulungu anayeogopa, na uso wake ulikuwa mweupe kwa aibu.
 
Midomo ya Alvin ilijikunja vibaya. “Vipi, tena. Mwizi anaingia chumbani kwangu na kuniibia nguo bado anathubutu kunikodolea macho?”
 
“Sina mood ya kubishana na wewe, Alvin. Watu huko nje lazima wawe wananitafuta kila mahali.” Lisa alikuwa na wasiwasi, lakini nguo zake zilikuwa zimelowa na nywele zake zilikuwa zimelowa. Hakuweza kwenda nje akiwa vile. Angeshtukiwa.
 
“Kwa hiyo… hilo linanihusu nini?” Alvin aliegemea mlango bila kujali, akionekana kutotilia maanani kabisa hali ya Lisa.
 
“Alvin…” Uso wa Lisa ulikuwa umepauka. Hakutaka kuharibu sifa ya familia ya Ngosha kwa kuhusishwa na kashfa na bwana mdogo maarufu kama Willie na kumfanya Nina asherehekee kwa hilo.
 
"Unajua kwamba mimi kamwe huwa siwasaidii watu bure?" Macho ya Alvin yaligeuka.
 
Lisa aliuma midomo, uso wake ukiwa mweupe kwa sababu ya aibu. “Alvin, usinifanyie hivyo. Mpenzi wako yuko nje."
 
 “Kwa hiyo?” Alvin hakujali, akamsogelea hatua kwa hatua, mkono wake wa kulia ukiwa umeshikilia rafu pembeni ya sikio lake. Macho yake meusi yalionekana kuwa na uga wa sumaku ambao ungeweza kuwavuta watu ndani.
 
Mapigo ya moyo ya Lisa yalimwenda mbio huku akiitazama sura ya Alvin iliyokuwa karibu sana na uso wake, midomo yao ikaumana.
Alvin akambusu kwa shauku sana, na hakuonekana kuwa na mpango wa kumwachia mapema.
 
"Inatosha. Uliahidi kunisaidia.” Lisa hatimaye alimkurupua na kugeuzia kichwa chake pembeni.
 
 
Macho ya Alvin yaliyokuwa yanawaka yalitazama midomo yake. Alitaka kumbusu hadi mwisho wa wakati, lakini, mlango uligongwa na Valeria akamwita, "Alvin, umemuona Lisa?" 
 
Alishika nguo zake kwa hofu. Akampapasa kwa upole sehemu ya nyuma ya mkono na kumvuta na kumfungia kabatini. Akaweka sawa nguo zake kabla ya kuuendea mlango na kuufungua. Valeria, Nina, na Melanie walikuwa wamesimama pale.
 
Aliwatazama kwa macho makali na kujibu. "Nimekuwa kwenye chumba cha sinema muda wote na Melanie. Ningewezaje kumuona?”
 
“Lakini… alitoweka…” Melanie alitazama chumba chake kwa wasiwasi. "Tulikuwa na wasiwasi kuwa amejificha kwenye chumba chako ..."
 
“Chumba changu? Kwanini ajifiche kwangu?" Sauti ya Alvin ilikuwa kali. Wanawake hao walijikaza, na Melanie akagundua kuwa alikuwa ameteleza ulimi.
 
Alvin akafoka taratibu, “Ni bora usngeachana na mbinu chafu unazozitumia kwa Ngosha hapa katika familia ya Kimaro. Aunty Nina, unaijua hasira yangu, kwa hiyo usinitie hasira.” Akaufunga mlango kwa nguvu na kwa kishindo. 
 
Muda si muda, akapiga namba ya simu ya mtumishi. Mtumishi mzee katika miaka yake ya 50 hivi alikuja na nguo mpya. Lisa akabadili nguo haraka haraka. Alipotoka nje, alimuona Alvin akiwa amekaa kwenye sofa huku akibana sigara katikati ya vidole vyake.
 
“Shangazi Yasmini, tafadhali mtoe nje.”
 
“Hakika. Bi Jones, nifuate.” Aunty Yasmini alitabasamu kwa upole na kumtoa Lisa nje ya chumba kile.

Sura ya:168

Wawili hao hawakugundua, lakini Jack Kimaro, ambaye alikuwa akirudi chumbani kwake, alimwona Lisa akitoka nje ya chumba cha Alvin kutoka pembeni. Alitabasamu na ghafla akaelewa kila kitu.
 
Shangazi Yasmini alimpeleka kwenye mlango mdogo wa makao makuu. Kutoweka kwa Lisa kulizikusanya pamoja familia za Ngosha na Kimaro—hata Mzee Kimaro na Bibi Kimaro walikuwa wamejumuka nao kumtafuta kila mahali.
 
Alipomwona akirudi, mara moja Nina alimkimbilia kwa wasiwasi. "Lisa, ulienda wapi bila taarifa? Ulizima hata na simu yako. Tulikuwa tunakutafuta kote. Ulitutia wasiwasi hadi kufa.”
 
“Huh? Mbona umevaa nguo tofauti sasa?” Valeria aliuliza ghafla.
 
Lisa alipepesa macho na kusema huku akihisi huzuni, “Sikuwa makini, nilipotoka kwenda matembezi nikaanguka kwenye bwawa.
Shangazi Yasmini aliniona nimelowa kabisa na kunichukua. Alinipa nguo za kubadili kuzifuta nywele zangu. Simu yangu pia ilidondoka kwenye bwawa na haiwezi kutumika tena.” Alinyamaza na kuomba msamaha, “Samahani sana. Sikutaka kuwasumbua kwa sababu mlikuwa mnatazama tamthilia”
 
"Ni kweli?" Bibi Kimaro alimtazama Aunty Yasmini. Shangazi Yasmini alikuwa amefanya kazi kwa familia ya Kimaro kwa zaidi ya miaka 30, kwa hiyo alimwamini.
 
“Ndiyo, ndivyo,” Shangazi Yasmini alisema huku akitabasamu.
 
"Sawa, ni vizuri kwamba yuko sawa. Hebu tutawanyike.” Bibi Kimaro alisugua macho yake, akihisi kukasirishwa na usumbufu huo.
 
Joel pia hakutaka kubaki tena. “Tumesababisha usumbufu mwingi kwa kila mtu usiku wa leo. Tuondokeni sasa hivi.”
 
Baada ya familia ya Ngosha kuondoka, Valeria aliona ni ajabu. Ni wazi alikuwa amepanga mtu amsukume Lisa kwenye chemchemi ya maji moto, kwa nini Aunty Yasmini alisema kwamba Lisa alianguka kwenye bwawa? Nani alimwambia Aunty Yasmini kusema hivyo? Nani alikuwa akimsaidia Lisa?
 
Wakati huo, Willie alimsogelea huku akitabasamu. "Ma’mdogo Valeria, unapaswa kuachana na biashara ya familia ya Ngosha. Babu au Bibi akigundua kwamba ulishirikiana na watu wa nje kuzusha matatizo katika familia, huenda wasikuruhusu uishi hpapa.”
 
 Valeria alishtuka na kumtazama Willie. “Wewe ndiye ulimsaidia?”
 
Willie alishtuka, hakukubali wala kukataa. “Unafikiri nini kingetokea ikiwa nitawaambia wazazi wangu kuhusu ulichokifanya usiku wa leo?” 
 
Valeria kakosa la kujibu, Ikiwa dada yake Iveta na shemeji yake Paxton Kimaro wangejua kwamba alikuwa amepanga njama dhidi ya Willie mtoto wao, wangepigana na kuzozana. Valerie alitetemeka na akajuta kumsikiliza Nina.
•••
Gari lilirudi kwenye jumba la familia ya Ngosha. Ndani ya gari, Melanie alikuwa bado analalamika, “Tafadhali toa taarifa kwa mtu wakati mwingine unapotoka badala ya kunyata kimya kimya. Hukuona kwamba Bibi Kimaro na Mzee Kimaro hawakuwa na furaha wakati tunaondoka?”
 
Lisa hakusema neno hata moja hadi alipofika sebuleni. Alimgeukia Joel na kusema, “Baba, kwa kweli niliitwa na mtumishi katika familia ya Kimaro hapo awali. Alisema kuwa Bibi Kimaro alitaka kuniona, lakini alinipeleka kwenye chemchemi ya maji moto na kunisukuma ndani nilipokuwa nimejisahau. Willie Kimaro alikuwa akijiloweka kwenye maji wakati huo, lakini kwa bahati nzuri, tunafahamiana, kwa hiyo hakunifanyia chochote na kunisaidia kujificha.”
 
"Nini?" Joel alishtuka. “Mbona hukuniambia mapema?”
 
Melanie aliziba mdomo wake kwa haraka. “Haiwezekani! Willie Kimaro alikusaidia? Yeye ni mbakaji maarufu na hupitia kila mwanamke anayemwona. Baba, Lisa atakuwa tayari…”
 
Joel mara moja akawa na wasiwasi na maneno yake. "Lisa, wewe"
 
“Baba usijali. Nilikuwa sawa kwa sababu hata dakika moja haikupita baada ya kuangukia kwenye chemchemi ya maji joto, Aunty Nina aliwaleta kwa makusudi Valerie na Queen kunitafuta.” Lisa alitoa tabasamu lisilo wazi kwa Nina. "Baada ya kutonipata kwenye chemchemi ya maji ya joto, walidhani kuwa nimepotea na kuwatahadharisha familia nzima ya Kimaro na kuanza kunitafuta kila mahali."
 
Joel hakuwa mpumbavu. Alipogundua kilichotokea, alimkodolea macho Nina.

Nina alishtuka. “Unamaanisha nini Lisa? Nilisikia kwa masikio yangu mtumishi wa familia ya Kimaro akidai kwamba ulienda kwa siri kwenye chemchemi ya maji moto. Nilidhani ulikuwa unapanga kumtongoza Willie. Kutokana na uovu wa Willie, nilikuwa na wasiwasi juu yako hivyo nikaamua kwenda huko kukuokoa…”
 
“Ndio, uliharakisha kuja huko. Lakini haikuwa kwa nia ya kuniokoa bali kuja kushuhudia akinifanyia vitendo vya ajabu kisha utangaze na sifa yangu iharibike. Familia ya Kimaro bila shaka wangeniona kama mtu nisiyefaa, kwa hiyo wangekubalije kumruhusu Willie anioe?”
 
Lisa alipumua katika hali nyepesi. “Anti Nina, kama ulikuwa na wasiwasi na mimi, ungeenda kwenye chemchemi ya maji moto peke yako kwa siri bila kupeleka familia nzima huko. Ungehisi umefarijika zaidi kwamba hukunipata badala ya kufichua jambo hilo kwa kila mtu na kuanzisha msako.”
 
Alieleza kila sentensi kwa njia iliyo wazi na yenye utaratibu. Hata kama Joel angekuwa mpumbavu, asingeshindwa kung’amua kuwa Nina alihusika na njama hizo.
 
"Nina, wewe ni mbaya sana." Joel alitetemeka kwa hasira. “Kwa nini unamchukia msichana mdogo kama huyu? Sio tu kwamba wewe na Melanie huwa mnamlenga nyumbani, lakini pia mlikuwa na wazo la kumwangamiza katika familia ya Kimaro.”
 
Lisa alikunja uso. “Baba, hukujua kwamba hata mpishi alikuwa amenilenga kimakusudi wakati wa chakula cha jioni?”
 
"Oh, karibu nisahau kuhusu hilo." Joel alipokumbuka tukio hilo, chuki yake dhidi ya Nina ilikaribia kufikia kilele. “Nakumbuka uliniambia kuwa mna uhusiano wa kirafiki na Valeria, sivyo? Nimewaona nyinyi wawili mkiwa pamoja siku nzima ya leo.” 
 
“Baba, Lisa anajaribu kututenganisha. Usidanganywe naye,” Melanie alisema kwa wasiwasi.
 
“Fumba mdomo wako,” Joel alinguruma, “Angalia jinsi mama yako alivyokulea! Wewe na mama yako nyote nhamna maana kabisa.”
 
Melanie alipigwa na butwaa, huku Nina akipandwa na hasira. “Joel, unaendelea kumtetea Lisa tangu arudi. Nadhani bado una hisia kwa Sheryl, huyo b*tch—”
 
Kabla Nina hajamalizia sentensi yake, Joel alimpiga kofi la uso moja kwa moja. “Nina, hata huonyeshi kujutia makosa yako. Kukuoa ndio majuto yangu makubwa maishani.”
 
“Unathubutuje kunipiga kofi Joel?!” Uso wa Nina ulionyesha kutokuamini huku akiwa amefunika sehemu ya uso wake iliyokuwa na maumivu. Machozi yalitiririka mashavuni mwake. “Njoo, Melanie. Twende nyumbani kwa bibi yako.” Mara baada ya Nina kumaliza kuongea, alimkokota Melanie na kutoka nje.
 
“Baba, una upendeleo. Tangu Lisa aje, hutujali tena.” Melanie alilia huku akitoka na Nina.
 
Joel alikaa kwenye kochi na uso uliopauka sana. Lisa kisha akanong’ona, “Pole, Baba. Kwa kweli sikutaka kukuambia, lakini usiku wa leo wao—”
 
“Sio kosa lako. Ni mimi ndiye nimeshindwa kukulinda.” Joel alionekana kukumbuka kitu. Kwa sura ya uchungu, alifanya uamuzi.
“Nitatafuta njia ya kumtaliki.”
 
Lisa alishangaa kwa muda, lakini alinyamaza. Kulikuwa na mzozo mkali wa kibiashara kati ya familia ya Ngosha na familia ya Mahewa. Aliona kuwa hakuna mtu katika familia ya Ngosha ambaye angekubali wazo hilo.
•••
Akiwa na kilio, Nina alirudi nyumbani kwa Mahewa pamoja na Melanie. Kaka yake, Farres Mahewa, alishindwa kujizuia mara tu alipoona jeraha kwenye uso wa Nina. “Dada nitashughulika na Lisa. Nimekuwa nikiweka chuki dhidi yake kwa sababu ya ardhi aliyonipikonya hata hivyo.”
 
Aliposikia maneno yake, Nina alifarijika. Kaka yake siku zote alikuwa mtu katili na mkorofi. Alikuwa na uhusiano na watu wengi wasio na huruma. Ingekuwa rahisi sana kwake kushughulika na Lisa.....ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.