JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................165 -166
Sura ya: 165
Jumba la kifahari la familia ya Kimaro lilikuwa katikati ya mlima na pia lilikuwa na mandhari bora katika eneo lote la Mlima wa Sherman.
Shamba kubwa lapata hekali hamsini au zaidi lilikuwa na uwanja wa mbio za farasi, uwanja wa gofu, uwanja wa mpira wa kikapu, uwanja mdogo wa ndege, mabwawa ya samaki, zizi kubwa la ng’ombe, majumba ya farasi….na…Hata Lisa, ambaye alikuwa ameona nyanja mbalimbali za jamii, alihisi kuelemewa na mazingira yale.
Baada ya kuegesha gari, kijakazi mkuu aliwaongoza wale watu wanne hadi kwenye jengo kuu. Katika sebule ya kifahari, Bibi Kimaro na binti yake wa tatu, Queen, waliketi upande mmoja. Mzee Kimaro na wanaume kadhaa walizungumza kwenye sebule nyingine ya kifahari upande mwingine.
Wale wanne walipoingia, kila mtu alitazama. Lisa, ambaye alikuwa amevaa mavazi ya gharama ya zaidi ya milioni saba mwilini mwake, ndiye aliyevutia zaidi. Midomo yake ilikuwa imepakwa lipstick nyekundu na nywele zake ndefu nyeusi zilikuwa zimejikunja kwenye mabega yake. Alikuwa na mwonekano maridadi, na urembo wake ulikuwa wa kifahari na wa kuvutia.
Karibu naye, Melanie alivaa tu kama anayekwenda matembezi ya kawaida. Kila mtu alijua kwamba alikuwa mhusika mkuu usiku huo, lakini alikuwa kama nyota iliyofunikwa na mwezi angani.
Bibi Kimaro alikuwa amesikia Melanie akimtaja Lisa hapo awali na hakumpenda tayari kutokana na mtazamo wa chuki aliomjaza. Lakini alipomuona kwa mara kwanza tena akiwa kapendeza kuliko Melanie, moyo wake ukavutiwa naye zaidi. Alitamani kama yeye ndiye angekuwa mjukuu-mkwe wake.
"Bwana Ngosha, baba yangu na kaka zangu wako huko. Unaweza kwenda kuzungumza na wanaume wenzako ikiwa hujazoea kukaa na sisi wanawake hapa.” Queen Kimaro alitabasamu na kumuondoa Joel kiakili.
"Basi nitaenda huko." Hakika Joel alikuwa anajisikia vibaya kwenye kundi la wanawake wale. Baada ya kuwasalimia huku akitabasamu, alimtazama Lisa na kuelekea kwenye sebule ya wanaume.
Mara tu Joel alipoondoka, Queen Kimaro alikunja midomo yake kwa dhihaka. “Melanie, huyu ni dada yako wa nje? Yeye ni mrembo kweli. Angalia vito vyote na dhahabu iliyopambwa kwenye nguo zake. Nakumbuka niliona hili nilipoenda Paris kwa Wiki ya Mitindo siku chache zilizopita. Seti moja inagharimu milioni sita hadi saba. Sikuweza kuvumilia kuinunua.”
Nina alitabasamu kwa heshima. “Lisa aliteseka sana siku za nyuma na haikuwa rahisi kumrudisha hapa. Nilitaka kumnunulia kitu kizuri ili kumsaidia ajisikie vizuri.”
“Kweli wewe una huruma sana. Yaani unamchukulia Lisa kama mwanao wakumzaa. Angalia ulichofanya, suala la ndoa ya Melanie na Alvin huenda likatatuliwa leo, kwa hiyo ulipaswa kumvisha Melanie vizuri badala ya kuruhusu mtu mwingine amfunike.” Valeria alisema kwa sauti ya uvivu. Valeria alikuwa ni rafiki mkubwa wa Nina na kwenye familia ya Kimaro alikuwa ni mtu wa nje kabisa. Yeye alikuwa ni mdogo wake na Iveta ambaye ni binti-mkwe wa familia ya Kimaro.
Melanie alitabasamu. “Ni sawa tu, mama yangu hana upendeleo na anatuchukulia wote sawa. Yeye anampenda sana Lisa kwa sababu ameteseka sana huko kijijini. Mimi nimekulia kwenye familia ya kitajiri kwa hiyo hivi vitu ni vya kawaida sana kwangu, ninajihisi kupendeza tu hata kwenye mavazi ya kawaida kama haya.”
Baada ya kusikiliza, Lisa alitoa tabasamu la unyenyekevu. “Kumbe nguo zangu ni ghali sana? Sikujua hilo. Leo ndo mara yangu ya kwanza ninavaa hivi. Sijawahi kuvaa nguo za kupindukia kama hizi maishani mwangu, nilikuwa sijui hata kama inagharimu pesa nyingi kiasi hicho. Asante, Aunty Nina.” Alipomaliza kuongea, aligusa kwa uangalifu lulu kwenye nguo zake, na kumfanya aonekane kama mshamba aliyeshtuka baada ya kusikia kuwa alikuwa amevaa nguo za bei ghali.
Kila mtu alibadilisha mtazamo wake. Kulikuwa na mengi ya siri kati ya mistari ya maneno ya Lisa. Kwanza, hakuwa amevaa nguo za bei ghali kabla ya siku hiyo. Pili, hakuwa na habari kama nguo alizovaa zilikuwa na thamani kiasi kile. Nani angehangaika tena na mtumshamba kama huyo?
Nina akawa na wasiwasi na kujilazimisha kucheka. “Lisa, unamaanisha nini kusema hivyo? Je, sikukununulia nguo nyingi za kifahari hapo awali? Zimejaa tele kwenye kabati lako.”
"Ndo hivyo, mimi sikujua kama zina thamani kiasi hicho. Hata hivyo ulininunulia ili watu wakusifu wewe, siyo mimi. Kwa hiyo ulinunua kwa faida yako. Ikiwa kweli unanijali mimi kama mwanao Melania basi ungeniruhusu na mimi nihudhurie karamu ya Bwana Kimaro alipokuwa anachagua mchumba. Lakini mlinificha mimi na Melanie akaja kwa sirisiri. Hapo utasema unajali kweli?”
Kila mtu alielewa sasa lengo la Nina.
Nina alichukia sana. Hakuwahi kufikiria kwamba Lisa angekuwa mjanja kiasi hicho kuharibu sura ambayo alikuwa ameijenga kwa uchungu kwa miaka mingi.
Bibi Kimaro alikunywa chai taratibu. Alikuwa amehisi kwamba Nina hakuwa mbaya sana hapo awali, lakini kwa mtazamo ule ilionekana kwamba kwa kweli alikuwa hafai. Kwa bahati nzuri, Joel Ngosha alikuwa muungwana wa kweli kwa hivyo haikuwa mbaya kwa Alvin kumuoa Melanie.
“Inatosha, sielewi haya yote yanayozungumza kuhusu mavazi ya kifahari yananiumiza kichwa tu. Nataka tu kusuluhisha suala la ndoa ya Alvin haraka.” Bibi Kimaro alisafisha hali ya hewa mara moja.
Melanie aliona haya. Nina kwa haraka alisema, “Bwana Kimaro ni jitu miongoni mwa wanaume. Ikiwa Melanie angeweza kuolewa naye, itakuwa heshima kwa familia ya Ngosha.”
Valerie alicheka na kuachia vigerere kwa furaha. "Kwa kuwa kila mtu yuko hapa leo, kwanini tusiflimalize hilo?"
"Nilikuwa nikifikiria kitu kimoja." Bibi Kimaro akamgeukia kijakazi mkuu. “Nenda uniletee ile bangili ya urithi.”
Mkwewe, Iveta, aliuliza kwa wivu, “Unamaanisha ile bangili ya urithi kutoka kwa mababu?”
"Ndiyo,” Bibi Kimaro alijibu huku akitabasamu. “Alvin ndiye mrithi wa familia ya Kimaro, kwa hivyo bangili hiyo inapaswa kupitishwa kwa mke wake mtarajiwa,"
Lisa aliinamisha macho yake huku sura ya uchungu ikimulika ndani yake. Pembeni, Melanie na mama yake tayari walikuwa wameshusha pumzi nyingi za msisimko.
Muda si muda, bangili ile ililetwa, na Bibi Kimaro akamwita Melanie. Alipotaka kuunyanyua mkono wa Melanie na kumvika, mara kishindo cha miguu kikasikika kutoka nje. Kila mtu alitazama wakati Alvin akiingia ndani. Alikuwa amevalia suti ya kijivu yenye tai ya hariri. Kulikuwa na saa ya kifahari imefungwa kwenye mkono wake. Mwili wake mzima ulionekana kama sanamu linalotembea- alionekana mtukufu, wa kifahari, na wa ajabu.
"Mnafanya nini?" Alvin aliwatazama wanawake wote pale sebuleni na hata baadhi ya wanafamilia wa Ngosha. Macho yake yalitulia kwa sekunde mbili kwa Lisa bila kusogea kabla ya kuiona bangili ya urithi mkononi mwa Bibi kimaro.
Valeria alieleza kwa tabasamu, “Bibi yako anataka kumpa mke wako mtarajiwa bangili ya urithi wa familia.”
Paji la uso wa Alvin liliinuka huku akitembea na miguu yake mirefu. Alinyoosha mkono kuinyakua bangili ya thamani kutoka mkononi mwa Bibi Kimaro na kuanza kuichezeachezea.
"Kuwa mwangalifu. Usiidondoshe,” Bibi Kimaro alimuonya.
Queen Kimaro alitabasamu. "Bibi, Alvin anataka kumvika Melanie bangili yeye mwenyewe."
"Hiyo ni kweli. Ina maana zaidi ikiwa mpenzi ndiye anayefanya hivyo,” Valeria alichombeza.
Melanie aliingiwa na woga na kuning'iniza kichwa chake kwa aibu, uso wake tayari ulikuwa na furaha ya wasiwasi. Lisa akatazama pembeni na kuinamisha kichwa chini huku akijifanya anatazama simu yake.
Alvin alimtazama Melanie na ghafla akatabasamu kabla ya kurudisha bangili ndani ya boksi. “Kwa kuwa ni urithi wa familia, ni afadhali kuuthamini na kungoja siku ya harusi yangu kabla ya kuutoa. Hata hivyo… Ni nani anayejua harusi yangu itakuwa lini, au… ikiwa bibi-harusi atabadilika au la?”
Sauti yake ya sumaku kama zumari ilikuwa ya kuvutia, lakini baada ya kuongea, ukumbi mzima ukawa na kimya cha kutisha. Nyuso za tabasamu za Nina na Melanie zilionekana kuganda, na hawakuweza kuzungumza hata baada ya muda mrefu.
Macho ya Melanie yalikuwa mekundu huku machozi yakimtoka. Bibi Kimaro alimshika mkono kwa sura ya huzuni na kumtazama Alvin. “Kubadili mchumba? Kwa hiyo ungependa kubadilisha awe nani? Wewe ndiye uliyemchagua Melanie, na kila mtu nje tayari anajua kwamba yeye ni mpenzi wako. Ulifikiri kuhusu hisia za msichana huyu uliposema hivyo? Nakwambia nimeshaamua mjukuu wangu. Ni yeye.”
Alvin alionekana kutosikia na kuokota chungwa bila kujali kabla ya kulimenya. Kila mtu aliangalia harakati zake isipokuwa Lisa, ambaye alikuwa akicheza na simu yake tangu mwanzo.
"Alvin, umesikia alichosema bibi?" Valeria alimkumbusha, “Melanie ni msichana mzuri. Usimwangushe.”
Nina aliuma meno yake na kusema, “Bwana Kimaro, ikiwa humpendi Melanie, basi sema tu moja kwa moja badala ya kumchezea kama mpumbavu. Melanie ni mboni ya jicho la familia ya Ngosha.”
"Nini? Je, ni lazima nikubali kumuoa leo?” Alvin alitupa maganda ya machungwa kwenye meza. Macho yake meusi hayakuwa na mwisho. “Inachukua angalau nusu mwaka hadi mwaka wa kuchumbiana ili wengine waanze kuzungumzia ndoa, lakini unanilazimisha kumuoa siku chache tu baada ya kukutana naye. Je, binti wa familia ya Ngosha ni wa kipekee kiasi hicho? Nisingethubutu kukusumbua kama ningelijua hili kabla.”
Sura ya:166
Baada ya kumaliza chungwa, Alvin hakushiriki mazungumzo mengine na wanawake wale na akageuka kuondoka. Muda si mrefu baada ya kuondoka, vijana wengine wawili waliingia. Mmoja alikuwa Willie Kimaro, ambaye Lisa alikutana naye huko Dar es Salaam, na mwingine ni Jack Kimaro. Lisa aliigundua bila kuambiwa na mtu kuwa huyo alikuwa ni mdogo wa Alvin kutoka kwa baba tofauti.
Bibi Kimaro akawapungia mkono wajiunge nao. Jack aliunga nao mara moja lakini Willie aliondoka na kuelekea kwenye bwawa la kuogelea nyuma ya nyumba.
Saa kumi na mbili jioni, chakula cha jioni cha familia kilianza kuseviwa. Zaidi ya watu 20 walikuwa wameketi kwenye meza ndefu ya pamoja ya chakula. Mpishi alisambaza sahanai za mbele ya kila mtu. Hata hivyo, hakujua ikiwa ni makusudi au la, lakini ilipofika zamu ya Lisa, chakula cha maana chote kilikuwa tayari kimekwisha.
Mpishi akatabasamu akiomba msamaha. “Samahani, nyama nzuri imeisha, imebaki mifupamifupa tu. Hutajali, sawa, Bi Jones?"
Queen alifoka kwa hasira. “Mpakulie chakula kilichopo maneno mengi ya nini? Pengine hajawahi hata kuona chakula kama hiki hapo awali. Hata hicho kilichobaki kinamtosha kabisa.”
Uso wa Lisa ulikuwa umetulia. Haikuwa rahisi kwa kwa familia ile kubwa ya kifahari kuwa na uhaba wa chakula. Tayari alikuwa ametarajia mambo fulani yatokee, kwa hiyo hakukuwa na jambo la kumkasirisha.
Hata hivyo, sura ya Joel ilionyesha hali ya kutoridhika. “Bi. Kimaro, Lisa ni binti yangu. Tafadhali angalia sauti yako."
Sauti ya Joel haikuwa ya kawaida, na Mzee Kimaro mara moja alichukizwa na Queen. "Funga mdomo wako ikiwa hujui kuchagua maneno yako."
“Lisa, unaweza kula sehemu yangu…” Joel alijaribu kumsukumia sahani yake.
Alvin aliyekuwa amekaa mbele akichezea simu yake ghafla akaingilia kati na kusema. "Tumbo langu halijisikii vizuri tangu majuzi, kwa hivyo siwezi kula. Lisa , unaweza kuchukua sehemu yangu. Uncle Joel anaweza kuendelea kula shea yake mwenyewe.”
Kila mtu alipigwa na butwaa na kugeuka kumwangalia Melanie.
Valeria alitabasamu. "Melanie, Alvin anakupenda sana. Afadhali kuacha sehemu yake kuliko kumtendea vibaya baba mkwe wake wa baadaye.” Melanie alifurahi kwa siri. Alikuwa na wasiwasi kidogo hapo awali, lakini ilionekana kama Alvin bado anamjali.
Alvin alipuuza mazungumzo yao na kumgeukia mpishi huku akisema kwa tabasamu hafifu, “hatujawahi kuwa uhaba wa chakula kwenye meza. Kwa hili lililotokea leo limeidhalilisha sana familia hii. Kwa uzembe huu hupaswi kufanya kazi tena kwenye familia hii, ondoka mara moja!”
Mpishi aliingiwa na hofu. "Bwana Kimaro, mimi ..."
“Hukunisikia? Chukua vitu vyako na utoke nje." Alvin taratibu akavifuta vidole vyembamba kwa kitambaa, lakini maneno aliyoyatema yalikuwa kama upanga uliowafanya watu wasithubutu kukaidi.
Punde, jamaa mmoja aliingia na kumchukua mpishi. Mpishi mpya aliingia kutoka jikoni. Mpishi aliyefuata alikuwa mwangalifu asitumikie vibaya asije akamkasirisha Alvin.
Lisa aliinamisha kichwa na kula chakula chake kwa umakini. Sehemu yake ilikuwa ya Alvin, na ingawa kila mtu alisema kwamba Alvin alifanya vile kwa ajili ya Melanie na Joel, yeye alihisi tofauti moyoni mwake. Ghafla alikuwa na maumivu makali moyoni mwake. Alikuwa anawaza nini? Alikuwa na mchumba sasa, na Alvin pia alikuwa na Melanie.
Baada ya chakula cha jioni, familia ya Kimaro ilimtazama Melanie kwa heshima zaidi. Willie tu ndiye aliyekuwa anajua kilichokuwa kikiendelea kati ya Alvin na Lisa na wengine wote walikuwa gizani. Hawakuweza hata kugundua kwamba Alvin alikasirika kwa sababu ya Lisa, Melanie alikuwa nani kwake?
Wakati huo, Bibi Kimaro alisema, "Alvin, fuatana na Melanie chumbani kwako mkatazame sinema kukuza hisia zenu kwa kila mmoja.”
Alvin alitazama ukumbini na kumuona Lisa ameinamisha kichwa chini. Alikuwa fasta kwenye simu yake tena. Moyo wake ulimpanda kwa hasira akiamini alikuwa akichati na Kelvin, akainuka na kutembea. Melanie alimfuata kwa furaha.
Kisha, Nina aliongozana na wanawake wengine wa familia ya Kimaro kuangalia tamthilia. Joel naye alivutwa na wanaume wenzake ili acheze poker, Lisa pekee ndiye aliyekaa kimya kwenye sofa akicheza na simu yake. Hakuna aliyemjali wala hata kupiga naye stori.
Willie alikimbia na sinia la matunda ili kumriwadha. Haijalishi ni nani aliyeolewa na Alvin katika familia yao, chakula cha jioni cha familia hapo awali kilimfanya aone kwamba Alvin bado anamjali Lisa. Hakika lilikuwa ni wazo zuri kwake kujipendekeza kwake sasa.
“Bi. Jones, hujazoea mazingira ya hapa na unaonekana mpweke sana, tunaweza kupiga stori kidogo?"
"Hakuna haja, nitakaa tu hapa kimya mtu yeyote asije akashuku kuwa nina kitu kuhusu wewe." Lisa alikataa kwa heshima.
"Hiyo ni sawa. Sina sifa nzuri katika familia hata hivyo, kwa hiyo ni bora nisikuharibie.” Willie alitabasamu na kuondoka zake.
Alipofika tu kwenye ngazi, Jack Kimaro alishuka kutoka juu na kuinua uso wake kwake. “Unampenda?”
"Hapana." Willie akatikisa kichwa kwa haraka.
"Ninaelewa, yeye ni mrembo sana, ni mrembo zaidi kuliko hata Melanie.” Jack alibofya ulimi wake. "Ikiwa si kwa ukweli kwamba yeye ni binti haramu, ningeweza hata kumfuata."
Willie alishtuka na kusema kwa aibu, "Ndio, hastahili hadhi yetu."
“Najua.” Jack aliinua macho yake kwa sura isiyoeleweka.
Willie alihisi kukosa uvumilivu ikambidi tu amwage umbea wake “Unahisi nini? Unaelewa kuwa yeye ni mwanamke wa Alvin Kimaro?"
Jack akashangaa, “nilikuwa sijui hilo.” Na papo hapo macho yake yakadhihirisha dhamira isiyo njema dhidi ya Lisa.
•••
Lisa alikaa kwenye sofa akicheza michezo ya kwenye simu kwa zaidi ya dakika 40 wakati kijakazi mmoja alimwendea ghafla.
“Bi. Jones, tafadhali fuatana nami. Bibi Kimaro anasema anataka kukuona."
“Anataka kuniona kwa ajili ya nini?” Lisa alibumbuwaa.
“Sina uhakika kabisa. Nafuata tu maagizo yake.” Kijakazi alionekana mwenye hofu.
Bibi Kimaro aliishi katika makazi ya nyuma, na Lisa akamfuata kijakazi huyo kwa wasiwasi kidogo. Alichokifanya mpishi kwenye meza ya chakula kilimfanya Lisa asiwe na imani na mtu yoyote ndani ya jumba lile. Hakuwa akifahamu mazingira ya jumba lile la kifahari. Alipokaribia ua, chemchemi ndogo ya maji moto ilionekana kati ya mianzi ya kijani kibichi.
“Bibi Kimaro…” Kabla Lisa hajamalizia usemi wake, nguvu kubwa nyuma yake ilimsukuma kwenye chemchemi ile ya maji moto.....ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.
