JINA LA SIMULIZI............................LISAAUTHOR...........................JOMBA WAJO SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY WHATSAPP...........................0628924768 SEHEMU YA................................169 -170
Sura ya:169
Siku mbili baada ya Nina na Melanie kuondoka, Lisa alianza kuishi maisha ya starehe. Baada ya kumaliza kifungua kinywa, aliendesha gari lake kuelekea ofisini. Gari hilo lilipokuwa likisafiri kwenye barabara inayozunguka milimani, ghafla alikumbana na zahama kali. Alijaribu kupiga breki, na kugundua kuwa breki hazifanyi kazi.
Alipojitambua, Lisa aligeuza usukani haraka. Gari hilo lilikimbia kwa mwendo wa kasi katika barabara hiyo kutokana na hitilafu ya breki. Gari jingine aina ya VW lilionekana mbele yake ghafla. Harakaharaka Lisa aliamua kupenyeza gari kutoka kando ya barabara nyembamba na kuingia kwenye kolongo.
Dereva wa VW iliyokuwa imemchukua Bwana Jack Kimaro, alipata mshtuko. “Huyu mtu amerukwa na akili, anaendesha gari kwa mwendo wa maili 150 hadi 160 kwa saa utadhani yupo kwenye mbio za magari?”
Jack aliinua kichwa chake na kushangaa kuona gari jeupe aina Mercedes Benz likisafiri kama upepo kwenye barabara ya makolongoni. Ilionekana kuwa dereva hakuwa akipiga breki hata wakati wa kupita kwenye kona mbaya Hata yeye hakuwa na ujasiri wa kuendesha gari kwa kasi kama hiyo.
"Kutakuwa na kitu hakiko sawa kwenye gari. Lifuate.” Dereva wa Jack alianza kulifukuzia gari la Lisa kwa nyuma. Gari la Lisa sasa lilikuwa likikimbia kwa kasi kubwa ya karibu maili 200 kwa saa. Wakati gari lilipokaribia kupinduka, Lisa aliendesha mara moja hadi kwenye njia yenye matope iliyokuwa ikijengwa. Mshindo mkubwa ulisikika wakati upande wa kulia wa gari ulipogonga mti mkubwa.
Jack alitoka nje kwa haraka na kufungua mlango wa gari lile. Puto la hewa ndilo lilimuokoa Lisa asifyatuke kutoka kwenye siti yake. Alikuwa amepoteza fahamu, lakini hakukuwa na dalili zozote za majeraha.
“Lisa…” Jack alistaajabu baada ya kuutazama vizuri uso wa binti aliyekuwa kwenye gari hilo. Haraka akambeba kutoka ndani ya gari pamoja na dereva na kumpeleka hospitali ya karibu baadaye.
Muda si mrefu Joel alifika hospitali huku akiwa na sura ya wasiwasi. Jack alimfariji, “Usijali, Uncle Joel. Binti yako ana akili na jasiri. Niliona kwamba gari lake lilikuwa halina udhibiti kwa muda, hata hivyo alitulia huku akilishika gari kwenye barabara inayozunguka-zunguka. Baadaye, aliendesha gari hadi kwenye njia yenye matope iliyokuwa ikijengwa ili kupunguza mwendo wake. Wakati gari lilipoanguka, hakukuwa na mtu aliyeketi upande wa kulia wa gari. Ingawa alipoteza fahamu, hakuna majeraha yoyote ya kimwili juu yake. Labda alizimia kwa sababu ya mshtuko wa moyo."
"Asante Mungu." Hatimaye Joel alishusha pumzi. Alimwambia Jack kwa shukrani, “Asante sana, Bwana Jack. Nitakumbuka wema wako daima.”
"Hapana usijali. Ndicho nilichopaswa kufanya.” Jack alijibu kwa dhati.
Karibu nusu saa baadaye, wafanyakazi wa hospitali walitoka. Sawa na kile alichokitaja Jack, kugongwa kwa mwili na kichwa cha Lisa ilimsababishia mshtuko wa ubongo, ambao ulieleza kwanini alizimia. Lakini hakuwa na majeraha katika sehemu zingine za mwili wake.
Baada ya kujua kuwa Lisa yuko sawa, Jack alielekea ofisini kwani alikuwa na jambo la kushughulikia asubuhi hiyo, Njiani dereva aliuliza, "Bwana Jack, unafikiri gari lake litakuwa limechezewa?"
Jack alicheka. Sababu ya kushindwa kwa breki ya gari lile la kijerumani lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia moja ilikuwa dhahiri ni kutokana na kuchezewa.
Dereva akahema. "Ni mara yangu ya kwanza kuona mtu akiishia kupata majeraha mepesi baada ya kukutana na ajali mbaya kama hii. Mwanamke yeyote wa kawaida angechanganyikiwa kutoka kwa akili zake, na gari labda lingeanguka kutoka kwenye mwamba. Bi Jones anaweza kuwa binti mdogo, lakini ustadi wake wa kuendesha gari hakika ni mzuri sana. Ingawa mimi ni dereva mzoefu, ni aibu kwamba siwezi kuwa mtulivu na jasiri kama yeye.”
“Ndiyo.” Jack aligonga vidole vyake kwenye magoti yake. Alikuwa amekutana naye katika familia ya Kimaro siku chache zilizopita, akidhani kwamba alikuwa ni mrembo tu mwenye uso mzuri bila kina, lakini alishangazwa kabisa na ujasiri aliomuona nao siku hiyo.
Hapo awali, alifikiria kwamba Alvin alivutiwa tu na uzuri wake, lakini kumbe kulikuwa na hazina nzurizaidi ndani yake. Alvin angefanyaje baada ya kugundua kuwa amepata ajali?
••• Saa sita mchana Jack alielekea kwenye ukumbi wa chakula wa kampuni hiyo. Majumba ya kulia chakula kwa wasimamizi wakuu na wafanyikazi wa kawaida yalikuwa kwenye sakafu tofauti.
Alipokuwa akielekea kwenye chumba cha chakula cha mabosi wa kampuni, alimuona Alvin ambaye alikuwa amevalia suti nnyeusi akitoka kwenye korido. Uso wake mzuri ulionekana katika hali mbaya. Watendaji wachache walikuwa wakifuatilia kwa karibu nyuma yake kuripoti utendaji wa kampuni.
Midomo ya Jack ilitetemeka kishetani. “Kaka.”
Alvin alimpa macho ya makali ya onyo. “Nilikuwa napanga kukutafuta. Kwanini hukuhudhuria mkutano asubuhi ya leo?”
“Kaka, sikukusudia kukosekana,” Jack akajibu kwa unyonge, “Nilipokuwa nakuja kutoka Sherman Mountain asubuhi ya leo, niliona ajali. Ilinibidi kumpeleka mwathirika hospitalini.”
"Wakati ujao, unahitaji kuifahamisha kampuni hata kama umepata udhuru." Alvin akanyanyua miguu yake mirefu na kuingia kwenye chumba cha chakula.
“Sawa, Kaka. Hata hivyo, unahitaji kumtembelea mwathirika? Yeye ni binti kutoka kwa familia ya Ngosha. Ni yule aliyekuja majuzi, si Melanie.”
Alvin aliganda baada ya Jack kumaliza kuzungumza. Alitazama nyuma, na macho yake meusi yakatua kwa Jack. Macho yake yalionekana kuwasilisha msukosuko wa hisia. “Lisa?”
"Ndio." Uso wa Jack ulionyesha huruma.
Alvin akaingiza mkono wake wa kulia kwenye mfuko wa suruali yake na kuuma mdomo wake mwembamba. "Amejeruhiwa vibaya?"
“Sina uhakika na hili. Nilikuja ofisini baada ya kumpeleka hospitali.” Jack akamtazama Alvin aliyekuwa amekunja uso. “Lakini nilisikia kwamba breki zilifeli. Ilikuwa hatari sana kaka. Nilipoenda kumuokoa, tayari alikuwa amepoteza fahamu.
Alvin akaufungua mlango wa chumba cha chakula. “Twende ndani.”
Baada ya kuketi kwenye chumba cha chakula, alimpa Hans jicho la kumaanisha. Hans alielewa maana ya jicho hilo kwake ndani ya sekunde moja na akaenda kutafuta ukweli juu ya jambo hilo mara moja.
Alvin alikaa kwenye kiti cha heshima, huku kundi la watendaji waliokuwa pembeni yake wakiendelea kupiga soga. Hata hivyo, hakujali walichokuwa wakisema. Fikra zake zote zilikua kwa Lisa. Siku mbili zilizopita, hata alikuwa amesimama mbele yake akiwa na uso uliokunjamana, akimruhusu kumbusu apendavyo. Sasa, alikuwa amepata ajali, na haikuwa hakika kama alikuwa hai! Moyo wa Alvin ulimuuma sana.
Ghafla, alisimama na kusema. “Sitakula kwani kuna kitu kimetokea. Nyie endeleeni tu na mlo wenu.” Watendaji hao walitazamana huku wakimtupi macho ya mshangao wakati akiondoka kwa kasi.
Jack siku zote alihisi kwamba hakukuwa na kitu kinachoweza kumdhoofisha Alvin, kutokana na ukweli kwamba alianza kuwaweka wanawake mbali tangu kifo cha Sarah. Kwa kushangaza, sehemu yake dhaifu ilikuwa imefichuliwa.
Alvin alikuwa akiendesha gari kwa kasi katika safari yake yote kuelekea hospitali. Akaongeza mwendo hadi kwenye wodi ya watu mashuhuri. Alipokaribia kuingia tu, ghafla akamuona Kelvin Mushi akiwa amekaa mbele ya kitanda na kumshika Lisa mkono. Mara moja akaacha kutembea na kujificha nyuma ya ukuta badala yake.
Alimsikia Kelvin akiuliza kwa upole, “Je, bado unahisi kizunguzungu?”
"Ndio, kidogo. Najisikia kutapika.”
"Daktari alisema kuwa ni kawaida kwa mtu aliye na mtikiso wa ubongo kupata hii. Umenitisha sana akili. Hapo awali nilipanga kusawazisha mambo kadhaa huko Dar es Salaam kabla sijaja hapa, lakini sikuweza kumudu kusubiri baada ya kusikia umepata ajali. Sitarudi nyuma. Nahitaji kubaki hapa ili kukuweka salama ili nisiwe na wasiwasi na wewe.” Kelvin alimshika Lisa mkono akauweka karibu na uso wake.
Lisa alitazama chini kwa uchungu. “Hata haujapona majeraha yako—”
“Ninaimarika zaidi. Sitaki kabisa kukupoteza, Lisa,” Kelvin alisema kwa upendo, “Tufunge ndoa mwaka huu. Nitakuwa kando yako siku zote.”
Sura ya: 170
Ghafla, Alvin alijiona mjinga kwa kumhangaikia Lisa na kukimbia kwa mwendo wa kasi hadi hospitalini. Sawa na yale yaliyokuwa yametokea huko Dar es salaam hapo awali, alidanganywa naye tena na tena.
Kila mara alijifanya kuwa msafi na mwenye haya mbele yake, hata hivyo alimtendea Kelvin kwa mapenzi mazito nyuma ya mgongo wake. Alimchukuliaje? Macho yake yalionyesha sura ya huzuni. Alvin alishindwa kuvumilia tena kusikiliza mazungumzo kati ya Lisa na Kelvin. Akageuka na kuiendea lifti.
Joel aliyetoka tu kwenye lifti alishangaa kugongana na Alvin. "Bwana Kimaro, ni nini kinakuleta hapa?"
"Rafiki yangu alilazwa hapa, kwa hivyo nilikuja kumtembelea." Kwa hali ya huzuni, Alvin alijibu bila mpangilio kabla hajaingia kwenye lifti. Upweke wake ulimfanya Joeli ashindwe la kusema.
Joel alipoingia wodini, Kelvin alikuwa akimpa maji Lisa. Joel alipumua na kusema kwa msisimko, “Kelvin anakutendea vizuri sana. Alinipigia simu asubuhi ya leo baada ya kukukosa hewani usiku mzima. Alipojua kuwa kuna jambo limekutokea, mara moja akaruka hapa. Alikuwa tayari amefika hapa kabla hata wewe haujaamka.”
Lisa hakujua la kusema, lakini alikuwa na tabasamu hafifu likienea katika uso wake uliopauka. Joel alivuta kiti na kuketi juu yake. Akashusha pumzi. “Ikilinganishwa na mtu kama Kelvin, Bwana Kimaro niligongana naye kwenye lifti sasa hivi. Alikuja kumtembelea rafiki yake. Baada ya yote, mimi bado ni baba ya Melanie mchumba wake na wewe ni shemeji yake mtarajiwa, lakini hakujali na hakuweza kuhangaika kujua kwa nini niko hapa.”
“Bwana Kimaro?” Kelvin alishikwa na butwaa. "Unamzungumzia Alvin Kimaro?"
“Ndiyo. Yuko kwenye uhusiano na Melanie,” Joel aliongeza, “Lakini sidhani kama atamuoa Melanie. Melanie amechanganyikiwa tu. Kwa kile nilichoona, yeye pia hayuko ndani yake. Hivyo sivyo anapaswa kufanya ikiwa anampenda kikweli.”
Lisa hakusema neno, lakini kichwa chake kiliendelea kumuuma. Kwa nini Alvin alikuja hospitali? Je, alikuwa ameenda kumtembelea? Je, alikuwa nje ya wodi muda ule na kuamua kutoingia baada ya kumuona Kelvin? Ilikuwa ni dhana yake tu. Hata hivyo, ilikuwa vigumu kuelewa ni nini kilikuwa kikiendelea kichwani mwa Alvin.
“Bado hujapeleka gari kwa uchunguzi, baba?” Lisa aliuliza swali huku akilini mwake akiwa na mawazo. “Hilo ndilo gari jipya uliloninunulia. Kwa nini breki zifeli?”
Joel alionekana kukosa raha. “Nilipiga simu polisi, lakini hadi polisi wanafika, gari lilikuwa limeteketea kabisa. Kutokana na uchunguzi wa awali wa polisi, mafuta ya injini yalivuja kutokana na ajali hiyo na kusababisha mlipuko wa moto.”
Lisa aliuma mdomo. “Nina hakika gari liligonga upande wa kulia nakuangukia upande wa kushoto. Haiwezi kuwa uvujaji wa mafuta uliosababisha mlipuko huo.” “Nitamwomba mtu achunguze jambo hilo kwa kina,” Joel alisema kwa hasira, “hakika nitamuua mtu ambaye alijaribu kumuua binti yangu baada ya kujua ni nani.”
Lisa alifikiria kidogo na kusema, “Baba unaweza kuwaomba polisi wasambaze habari kwa umma kuwa mtu aliyehujumu gari langu amepatikana? Kisha funga nyumba ya familia ya yako na usiruhusu mtu yeyote kuingia kwa wakati huu.”
Joel alipigwa na butwaa. "Lisa, unashuku kuwa kuna mtu kutoka kwa familia yetu alihujumu gari lako? Hili haliwezekani kabisa. Watumishi wote katika nyumba yangu wametumikia familia yetu kwa zaidi ya miaka kumi. Wao ni waaminifu na wa kutegemewa—”
“Baba siku hizi mbili nimetembelea ofisini na nyumbani tu, kwa hiyo hizi sehemu mbili ndizo sehemu ninazozishuku. Mtu aliyefanya hivi lazima awe mtu ambaye hatoki mbali. Akisikia hivyo hakika atashtuka,” Lisa alisema kwa uzito, “Shirikiana nami tu. Nisipomjua mtu huyo ni nani, huenda nikapoteza maisha yangu wakati ujao.” Joel aliitikia kwa kichwa baada ya kusikiliza ushauri wake. ••• Baada ya kuingia ndani ya gari, Alvin aliufunga mlango kwa nguvu. Kisha akawasha sigara na kuanza kuivuta. Hans alipoingia ndani ya gari, tayari moshi ulikuwa umetapakaa ndani ya gari. “Bwana Kimaro, nimechunguza ajali…”
Alvin akawasha gari na kuondoka kwa kasi. Huku gari likisafiri kama roketi barabarani, Hans aliogopa sana hivi kwamba alishika mpini juu ya kichwa chake. Mara Alvin alipofika ofisini, alipanda ghorofani moja kwa moja.
Hans akammiminia kikombe cha kahawa. Alipogeuka tu kuondoka, ghafla Alvin akamuita, “Simama. Umegundua nini? Ni mtu gani aliyefanya hujuma hiyo?” . Hans alitazama nyuma na kuripoti kwake kwa umakini, "Gari lilichezewa na mtu kutoka familia ya Ngosha, na ilikuwa kazi ya mtunza bustani. Alipokea kiasi cha pesa kutoka kwa Beka Pongo, Nijuavyo, Beka na Farres hujumuika mara kwa mara. Baada ya kuchunguza suala hili, hata hivyo, inaonekana kwamba Farres anahusika nalo moja kwa moja.”
“Hilo halishangazi. Ikizingatiwa kwamba Farres amefanya mambo mengi mabaya, ana uzoefu wa mambo kama hayo.” Alvin aliinua yake kikombe cha kahawa na kupuliza juu yake. “Joel amegundua nini kuhusu jambo hili?”
"Amefanya uchunguzi wa gari, lakini gari tayari limeteketea. Zaidi ya hayo, hakukuwa na kamera zozote za uchunguzi kwenye eneo la tukio. Nadhani hataweza kujua chochote," Hans alisema, "labda hakutarajia familia ya Mahewa kuwa katili sana."
"Joel ni mtu mzuri, lakini kwa bahati mbaya, watu kama yeye hudanganywa kwa urahisi sana." Alvin alicheka.
“Bwana Kimaro, nimfahamishe Lisa—”
“Kuna faida gani kumwambia?” Alvin ghafla akatupa kikombe cha kahawa juu ya meza. “Si yeye anayekulipa, achana naye.” Alvin alipandwa na hasira.
••• Siku ya pili baada ya Lisa kulazwa hospitalini. Saa sita mchana, Kelvin alikuwa akimlisha Lisa. Jack alienda kumtembelea. Jack Kimaro alikuwa amevalia sweta ya kahawa na suruali ya kijivu, ambayo ilikuwa imekunjwa ili kuonyesha vifundo vyake vya mikono vilivyopendeza. Vijana wote wa familia ya Kimaro walivutia sana hivi kwamba wangeweza kuwa waigizaji mashuhuri katika tasnia ya burudani.
"Ni nini kimekuleta hapa, Bwana mdogo wa familia ya Kimaro?" Hali ya mshangao ikapita usoni mwa Lisa. Alikuwa amekutana naye mara moja tu katika jumba la familia ya Kimaro, na hawakuzungumza hata kidogo wakati huo.
"Hata hivyo, mimi ndiye niliyekuokoa, kwa hiyo nilikuja kukuona unaendeleaje." Macho ya Jack yalimwelekea Kelvin.
Kelvin alisimama na kujitambulisha, “Hi, mimi ni mchumba wa Lisa. Asante kwa kumuokoa usiku huo, Bwana Kimaro.” Kelvin alionekana mpole na mnyenyekevu, lakini mwenendo wake haukuwa wa kujikweza wala kujidharau.....ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.