JINA LA SIMULIZI............................LISA

AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................157-158

Sura ya: 157

“Kwanini… uko hapa?” Lisa alitetemeka.

Alvin hakuongea. Macho yake mazito yalimwangukia, akimtazama kuanzia miguuni kupanda juu, jinsi kale kamtandio kalivyogoma kabisa kuyahifadhi maumbile yake kulimfanya aonekane kama kituko. Akainua miguu yake kumsogelea hatua kwa hatua. Lisa alishtushwa kwanza na sura yake na ndipo akagundua kuwa macho yake yalikuwa yameganda mwilini mwake. Kwa kutetemeka, alikumbuka alichokuwa amevaa na akageuka kwa aibu. Kwa haraka alijichimbia ndani ya blanketi, akisema kwa kubabaika, “Usi…Usije huku.”

Jinsi alivyokurupuka na kwenda kujifunika blanketi kulimfanya Alvin atamani kucheka. Alidhihaki, “Hukuona aibu kunengua mbele ya wanaume wote usiowafahamu usiku wa jana, kwa nini unajifanya kuwa na aibu mbele yangu sasa hivi?”

“Bado una ujasiri wa kusema hivyo?” Lisa alimtazama kwa mkazo huku macho yake yakiwa mekundu kwa aibu. “Ilikuwa ni kwa sababu ya rafiki yako…Hapana, ilikuwa ni kwa sababu yako. Wewe ndiye uliyemtuma rafiki yako anikamate na kunifundisha adabu, sijawahi kuona mtu katili kama wewe."

"Lisa Jones, usiupime uvumilivu wangu!" Alvi alikasirishwa ghafla na maneno ya Lisa. "Ulikuwa ukicheza na kunywa na wanaume hao jana usiku. Kama nisingejitokeza na kukunusuru unafikiri ungekuwa umesimama mbele yangu ukivimba na maneno yako ya kijeuri?”

“Unajua kila kitu usijifanye kupotezea. Hapo mwanzo uliniambia niondoke Nairobi sivyo nitajuta. Hazijapita hata siku tayari maneno yako yakatimia. Kwanini nisishuku kuwa ulikuwa unashirikiana na rafiki yako ili kunidhalilisha?” Lisa akashusha pumzi ndefu na kujaribu kutulia. "Pamela yuko wapi?"

Alvin alimtazama kwa jeuri na kukaa kimya. Lisa alikasirika na kusema kwa hasira, "Ikiwa chochote kitatokea kwa Pamela, sitakuacha uende hata kama nitakuwa kuzimu."

“Hakika. Ngoja tuone utafanya nini.” Alvin alitembea taratibu mpaka pembeni ya kitanda. Mikono yake ilikuwa imeegemezwa kitandani huku akiinamisha mwili wake. Alimkabili Lisa uso kwa uso, na macho yake yalikuwa yamejaa dhihaka. “Unafikiri wewe ni nani?”

Akiwa anahisi kudharauliwa kabisa, Lisa alipandwa na hasira kiasi kwamba alikuwa karibu kuua mtu. Hata hivyo, alikuwa hoi. “Sawa, sijali unafikiria nini, lakini nilikuwa nafanya vile rafiki yako alitaka nifanye. Heshima yangu imeharibiwa, kwa hiyo lazima utakuwa umefurahi sasa. Unaweza kuniacha niende?”

"Endelea kuota. Ni kosa lako kuonekana mbele yangu badala ya kukaa kwa kutulia huko Dar es Salaam.” Alvin aligeuka ghafla na kukaa kitandani. Alitoa simu yake na kufungua video, akisema kwa sauti ya kejeli. “Unadhani nini kitatokea nikiachia video hii? Unadhani Joel Ngosha bado atathubutu kujigamba kwamba wewe ni binti yake? Unajua Nina na Melanie watakuonaje?”

Lisa aliiangalia tu na aliona aibu hata akatamani kujizika kwenye shimo. Hakuthubutu kufikiria nini kingetokea ikiwa video kama hiyo ingetolewa hadharani. Sifa ya familia ya Ngosha ingeharibika. Na angefukuzwa katika familia ya Ngosha, angejuaje chanzo cha kifo cha mama yake?

"Alvin, ifute sasa." Alijaribu kushika simu, lakini Alvin alikwepa. Hakuweza kujizuia kwa wakati na akaanguka moja kwa moja kwenye kifua chake. Mikono ya Alvin nayo ikatua kwenye kiuno cha Lisa na kukutana na nyama laini, ulikuwa ni mguso wa kuvutia zaidi. Macho ya Alvin yalibaki kifuani mwake.

“Unanitega?” Alvin aling’aka.

“Hapana…” Kabla hajamaliza, alihisi mkono wake ukimpapasa kiunoni taratibu.

"Alvin, wewe…unafanya nini!" Uso wa Lisa ukawa mpole kwa aibu

Mikono ya Lisa ilikuwa imeegemezwa kila upande wa mabega ya Alvin, huku akimtazama kwa chuki. Lisa alifunika midomo yake minene bila kujua, na alihisi kuwa uso wake ulikuwa unawaka.

"Nyamaza.” Alvin aliuvuta mikono yake na kuitoa kiunoni mwa Lisa napapo hapo akaonekana kubadilika ghafla. "Lisa Jones, nimekuwa mbali na wewe kwa muda mfupi tu lakini haukuweza kusubiri kuchumbiwa na Kelvin Mushi. Niambie, anajua kuwa uko pamoja nami sasa?"

“Alvin, inatosha…” Lisa aliingiwa uchungu sana. Alipokumbuka ahadi yake kwa Kelvin, alimuonea huruma sana.

Muonekano wake wa kuchanganyikiwa ulimfanya Alvin kuwa na hasira kabisa, akainamisha kichwa chini na kubusu midomo yake kwa nguvu. Alifikiri alikuwa tayari amechukizwa naye, lakini ladha yake aliyoizoea ilipoziba hisia zake, alijisikia raha sana.

Lisa alijitahidi sana kufurukuta lakini haikufaa. Mikono yake ilikuwa imebanwa sana na mkono wa Alvin, na nguvu za mwanaume huyo zilimtawala kabisa.

Baadaye aliachwa na kizunguzungu kutokana na busu lake.
Kwa kuwa Alvin alipoondoka mara nyingi alipatwa na tatizo la kukosa usingizi na alikuwa akimfikiria katikati ya usiku, busu lile lilimfanya ajisikie vizuri. Ingawa sasa alikuwa amechumbiwa na Kelvin, kila Kelvin alipojaribu kumsogeza karibu, alimpinga bila kujua. Haikuwa kama jinsi alivyokuwa akihisi mbele ya Alvin, akitamani harufu ya mwili wake.

Alvin alishtushwa na sauti ya mlango ukigongwa chini ya ghorofa, lakini akaipuuza. Hata hivyo, muda si muda, mtu fulani akapaza sauti, “Bwana Kimaro, uko hapa?”

Mara Alvin na Lisa wakatawanyika. Hiyo ilikuwa sauti ya Melanie.

Lisa akachanganyikiwa na kumsukuma Alvin. Akakumbuka kuwa huyo hakuwa yule Alvin mume wake. Tayari alishamwacha na alikuwa na rafiki wa kike, na rafiki huyo wa kike alikuwa nje kwa wakati huo.

Mguso wa kero ukaangaza machoni mwa Alvin. Kwanini huyo Melanie aliingia ghafla na kuunguza picha? Haraka akainuka na kuelekea mlangoni. Alipofungua, alitazama nyuma na kumuona Lisa tayari amejificha kwenye kabati la nguo kama mwizi. Kwa namna fulani, aliona ni jambo la kuchekesha kidogo.

“Bwana Kimaro…” Melanie aliyekuwa amesimama mlangoni aliduwaa baada ya kumuona Alvin akitokea. Mwanamume aliyekuwa mbele yake alikuwa amevalia tisheti na bukta tu. Harufu yake ya kiume ilifanya moyo wake upige kama nyundo. Hata hivyo, muda mfupi baadaye, alisikia harufu ya mwanamke juu ya mwanamume huyo, na moyo wake ulipungua mara moja. Baada ya kuangalia kwa makini, aliona macho ya mtu huyo bado yalikuwa meusi. Alipigwa na butwaa kabisa.

Machale yalimwambia kuwa kunaweza kuwa na mwanamke chumbani, na anaweza kuwa amekatiza kitu kwa ujio wake.
Hii ilitokeaje? Baada ya Sarah Langa kufariki, Alvin alikuwa amejitenga mbali na wanawake kila mara. Nani alikuwa ndani?

“Umeingiaje?” Uso wa Alvin ulikuwa umetanda hasira. Alichochukia zaidi ni watu walioingia katika nyumba yake bila ruhusa yake.

"Nilienda kwa Bibi Kimaro asubuhi ya leo kukutafuta, lakini haukuwepo, kwa hivyo Bibi… alinipa ufunguo wa mahali hapa." Melanie aliogopa kwa sura ya hasira ya Alvin. "Nilitaka kula kifungua kinywa na wewe, kwa hivyo nilileta hii ..."

“Toka,” Alvin aliamuru bila huruma.

Sura ya:158

Macho ya Melanie yalibadilika na kuwa mekundu huku sura ya kutokuamini ikimuosha usoni mwake. “Bwana Kimaro, mimi ni mpenzi wako…”

“Unaweza kusahau kuwa ulikuwa mpenzi wangu wakati wowote.” Alvin akamshika mkono na kutoka naye nje. Hii ilikuwa mara yake ya kwanza kuchukua hatua ya kumgusa Melanie, lakini badala ya kujisikia furaha kuhusu hilo, Melanie alisukumwa moja kwa moja nje ya mlango.

“Melanie Ngosha, hukubisha hodi na uliingia bila ruksa kwenye nyumba ya mtu mwingine. Je, familia yako haikukufundisha adabu yoyote?” Alvin alifoka. “Na hata kama ulishindwa kupiga hodi ungepiga hata simu. Sipendi mwanamke anayekuja kunichunguza.”

Melanie alikabwa na huzuni. “Siyo kwamba sina adabu. Ni kwa sababu wewe unamficha mwanamke mwingine ndani na hutaki nimuone, sivyo?”

Uso wa Alvin uligeuka kuwa mkali. Mwanamke huyu mjinga alikuwa amevuka mstari wake wa mazoea. “Hata kama nina mwanamke, sina haja ya kukuogopa hata nikufiche. Jua mipaka yako." Kisha, akamaliza sentensi yake na kufunga mlango kwa kishindo kikubwa.

Melanie alisimama nje ya mlango akiwa ameduwaa. Hakuelewa. Alvin alikuwa ameonyesha kumpenda sana hapo awali. Hata alimchagua mara ya kwanza mbele ya mabinti wengine wengi, angewezaje kubadilika ghafla hivyo? Ni lazima kulikuwa na msichana aliyekuwa ndani ya nyumba ndiye aliyemfanya kuchanganyikiwa.

Alvin alifunga mlango kwa ndani na kumpigia simu Hans ili atafute fundi wa kubadilisha vitasa vya milango yote na aweke password. Baada ya kukata simu, Lisa alitoka kwenye kabati la nguo alimokuwa amejificha. Alikuwa amevaa shati la Alvin na suruali yake ya kulalia. Nguo zile zilizolegea zilimpendeza zaidi. Alvin alimtazama kwa macho makubwa. Ilikuwa ni mara ya kwanza kugundua kuwa mwanamke anaweza kuonekana mrembo sana akiwa amevaa nguo za kiume.

Lisa akazipiga hatua kwa umakini, lakini mguu wa suruali ya pajama ulikuwa mpana sana, akaukanyaga bila kujua na kumfanya kuteleza na kuanguka. Lisa alichanganyikiwa kwa sekunde chache, na kwa haraka akaikamata ile suruali ya kulalia. Kabla hajasema chochote, Alvin alimnyanyua na kumuweka kwenye sofa.

"Ulifanya hivyo kwa makusudi." Alvin alimuuliza kwa utani.

"Hapana, nguo zako za kulalia ni kubwa sana." Alvin alitaka kumbusu tena, lakini Lisa alipomfikiria Melanie akiwa amesimama nje, alimsukuma kwa aibu. "Inatosha. Ikiwa unataka mwanamke, mpenzi wako yuko nje."

“Kumbe?” Alvin alikoroma kabla ya kutema maneno ya kuumiza kwa sauti yake ya dharau, “Basi mpenzi wangu ndiye atakuwa Bi Kimaro. Kuhusu mwanamke kama wewe ... wewe ni wa kuchezea tu."

Macho ya Lisa yalimtoka. Alifikiri kwamba alikuwa ameaibishwa vya kutosha na mpenzi wake wa kweli ambaye alikuwa nje ya mlango, lakini hakutarajia kwamba maneno yake yangefikia kiwango hiki cha unyonge.

“Usiniangalie hivyo. Ulikuwa Bi Kimaro mara moja, lakini uliipoteza nafasi hiyo.” Alvin bila kujali alicheza na nywele masikioni mwake.

Moyo wa Lisa ulizama hadi chini. Alvin alishamweka wazi kuwa alichotaka zaidi sasa ni kumchezea tu. “Hujalidhika tu na mlivyonidhalilisha jana usiku?”

Alvin alipuuzia swali lake. Aliachia nywele zake ndefu na kusimama wima. "Kuanzia leo nikikuita basi ni lazima uje mara moja. Vinginevyo, usinilaumu kwa kupakia video yako mtandaoni. Ikiwa ungependa kuendelea kubaki Nairobi, itategemea na namna utakavyoniheshimu.”

Uso wa Lisa ulikuwa umepoa sana hata akashindwa kuongea.
Wakati fulani, alitaka sana kurudi Dar, lakini hakuweza kufanya hivyo alipomfikiria mama yake aliyekufa pamoja na Nina na binti yake. Alitaka kumlipishia kisasi mama yake ili moyo wake uridhike.

Alvin alipomuona amenyamaza, alitabasamu kwa kejeli. "Inaonekana hisia zako kwa Kelvin sio kali sana. Yeye si muhimu sana kuliko utukufu na utajiri wa familia ya Ngosha, huh?”

“Umemaliza?” Lisa alitabasamu kwa utulivu. "Alvin, ninachojutia zaidi ni kuzungumza nawe kwenye baa usiku ule!"

Uso wa Alvin ulikuwa umepoa huku akitoa ufunguo kutoka kwenye droo la kabati na kumtupia Lisa. "Chukua. Nitakupigia simu siku yoyote."

Uso wa Lisa uliangaza maruerue. “Huogopi Melanie ataniona?”

“Haijalishi akikuona. Yeye ni mwanamke tu. Nafasi yake inaweza kuchukuliwa pia na mwanamke mwingine muda wowote. Siku zote kutakuwa na watu wenye akili zaidi yake wanaotaka nafasi hiyo.” Alvin alikuwa amemaliza kuongea mara kengele ya mlangoni ilipogongwa. Alifungua mlango, na Hans akaingia na begi.
“Bosi, hizi hapa nguo ulizotaka ninunue. Pia, fundi wa vitsa amefika na lazima uhudhurie mkutano wa kampuni saa tisa."

“Mmh!” Alvin alivitupa vitu hivyo mikononi mwa Lisa na kusema, “Nenda ghorofani ukabadilishe.”

Lisa akachukua vitu hivyo na kuondoka kwenda kuoga. Wakati anabadilisha nguo zake na kushuka chini, Alvin alikuwa ameshatoka. Simu aliyokuwa amemuachia Rodney jana yake usiku kwenye Yatch ilikuwa mezani. Alipoitazama akakuta kuna meseji na missed call za Joel na Kelvin lakini hakukuwa na missed call yoyote kutoka kwa Pamela. Alipiga namba yake kwa wasiwasi, na simu ikapokelewa haraka. Sauti ya Pamela iliyochanganyikiwa ilisikika kutoka upande wa pili. "Lisa, kuna nini?"

“Uko salama?" Lisa aliona ni ajabu sana.

“Mimi, nipo sawa.” Pamela alisugua kichwa chake na kusema, “Nilikwenda kuonana na mwenyekiti wa kampuni jana lakini nikaishia kulewa kwa sababu nilikunywa pombe kupita kiasi. Kwa bahati nzuri, watu wa kampuni ni wema sana, walinirudisha salama tu nyumbani kwangu. Sitafanya hivyo tena kamwe.”

Ilivyoonekana Pamela hakuwa na tatizo lolote. Hatimaye Lisa alielewa kuwa jana yake usiku ulikuwa ni mpango mchafu wa Rodney kumdhalilisha yeye tu. Pamela alikuwa haelewi chochote.
Aliwaza na kuamua kutomwambia lolote Pamela. Ilikuwa ni kwa faida ya Pamela ili asizue matatizo katika kampuni hiyo, maana Pamela angesikia yaliyomkuta Lisa ni lazima angeliamsha dude. Rodney Shangwe hakuwa mtu ambaye wangeweza kumudu kumkosea. Kwa vyovyote vile, Lisa alikuwa kwenye kiganja cha Alvin sasa, hivyo Rodney asingemnyooshea mkono rafiki yake huyo.

“Ni vizuri kuwa uko sawa, lakini unapaswa kuzingatia katika siku zijazo. Wewe ni msichana, hivyo usilewe hovyo nje.” Lisa alimuonya.

“Sawa, lakini ni ajabu sana. Uvumilivu wangu wa pombe kwa kawaida ni mzuri sana, lakini nililewa baada ya glasi chache tu jana. Labda kwa sababu divai ilikuwa nzuri sana.” Pamela alijitetea. Lisa alitabasamu kwa hasira. Lazima kulikuwa na kitu kilichoongezwa kwenye divai.

Baadaye alimpigia baba yake simu na kumdanganya kuwa alilala kwa rafiki yake na kumwomba radhi kwa kutokutoa taarifa. Kisha akamalizia kwa kuongea machache na Kelvin....ITAENDELEA...

Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.