JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................155-156

Sura ya: 155

Ndani ya Yatch katikati ya ziwa Naivasha burudani iliendelea. Kijana mmoja aitwaye Kelly alimimina glasi ya whisky na kwenda mbele kucheza na Lisa. Mikono yake mikubwa ilianguka kwenye mabega ya Lisa, na akatamani kupenyeza ulimi wake kwenye ngozi yake ambayo ilikuwa laini kama satin. Alitaka kushindwa kudhibiti hisia, lakini mwanamke yule mikononi mwake aliteleza kama konokono.

"Unajua mimi ni nani? Usiwe msumbufu.” Kelly alipapasa uso wake.

"Samahani, mashariti ni kucheza tu usiku wa leo, siyo kushikwashikwa." Lisa aligeuza kichwa kumkwepa. Alifanya hivyo ili tu kumwokoa rafiki yake. Sasa mambo yalipokuwa yamefikia, si tu kwamba asingeweza kusema kuwa ni binti wa Joel, bali ilimbidi kuficha utambulisho wake pia. Vinginevyo, angeharibu sifa ya familia ya Ngosha.

"Sogea karibu, kama utakunywa glasi hii mara moja, nitakutuza dola elfu moja mara moja." Kelly aliitikisa glasi iliyokuwa imejaa pombe.

Lisa alitabasamu kwa ucheshi. “Glasi moja tu?”

“Ndiyo, nakupa glasi moja tu kwa sababu unavutia kwenye hayo mavazi." Kijana Kelly alicheka. Vijana wote waliokuwepo wakacheka kwa pamoja.

Lisa alitazama glasi ile kimyakimya. Sekunde chache baadaye, aliinyanyua glasi na kumeza kila kitu kilichokuwa ndani yake kwa mkupuo mmoja mkubwa. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kunywa pombe kali namna hiyo. Pombe ilikimbilia tumboni mwake kama moto unaowaka, lakini aliweza kuvumilia tu na kumrudishia glasi kwa utulivu.

"Si mbaya, unaweza kushikilia tu glasi yako." Umati ulishangilia, na kijana mwingine akaja kucheza naye na kumwongezea pombe. Kulikuwa na vijana kumi na alitakiwa wote acheze nao. Alikunywa kikombe baada ya kikombe hadi tumbo likafa ganzi kwa maumivu. Baada ya kumaliza kucheza na mtu wa tisa, Rodney Shangwe pekee ndiye aliyekuwa amebaki.

Lisa alikuwa ameanza kupoteza uwezo wa kuona vizuri kutokana na kuzidiwa na pombe. Alikuwa akiona dabodao na walionekana kina Rodney wengi. Alimtambua tu kwa koti lake la ngozi. Hakuweza hata kutofautisha sifa zake tena.

"Bwana Shangwe, unapaswa kuwa mtu wa mwisho kucheza nami kwa sasa sivyo? Glasi moja ya mwisho unamtoa rafiki yangu, sawa?" Lisa aliongea kwa rafudhi ya kilevi, pombe ilikuwa imeshaanza kumchukua kwa nguvu.

Rodney alimkazia macho ya mshangao mwanamke huyo aliyekuwa mbele yake. Wanaume wengi wasingeweza kumudu glasi tisa za pombe kali kwa mkupuo mmoja. Alikuwa amelewa, lakini macho yake yalikuwa yameng'aa huku akimkazia macho. Mgongo wake ulikuwa umenyooka na umejaa kiburi pia.

Rodney akacheka kwa sauti ya chini, na kabla hajaongea chochote, ghafla mlango katika chumba ulifunguliwa, na bila kutarajia mtu ambaye hakutarajiwa kabisa aliingia ndani.
Lisa alikuwa amelewa sana kiasi kwamba japo alimuona lakini hakuweza kumtambua mtu huyo. Alidhani ni kijana mwngine tu aliyeingia kucheza naye.

Macho ya Alvin yakaduwaa mara moja, akainamisha kichwa kumtazama. Kiasi cha kitambaa kilichomfunika kilikuwa cha kusikitisha. Alimtazama kuanzia chini ya nyayo zake, alichoweza kuona ni sehemu kubwa ya mwili wake mzuri ikiwa wazi. Mwanaume yeyote ambaye angemwona yuko vile angetamani kutaka kulala naye tu.

Alvin alisikitika sana hata hakujua ni kwanini alimuonea huruma licha ya kwamba alikuwa akimchukia sana. Hakujua Lisa alikuwa amekunywa kiasi gani kwani hata hakumtambua.

Macho ya Lisa yalikuwa yakitokwa na machozi. Hakuweza kuvumilia tena na alikuwa karibu kuanguka. Alvin akamdaka kwa mikono yake, Lisa akaangukia kifuani kwake.

"Unataka unibusu kwa nguvu eeh,?" Mdomo wa Lisa ulikuwa mzito kuongea.

Alvin alimshika kidevu chake. Alikuwa haoni vizuri baada ya kupofushwa na machozi na alikuwa kapoteza busara zake zote. "Ikiwa unataka kunibusu, basi omba. Usilazimishe kwa nguvu" Lisa akazidi kubwabwaja kilevi.

Lisa aliinamisha kichwa chake. Pombe kali ilikuwa ikiathiri busara zake zaidi kadiri muda ulivyopita. Alimfikiria Alvin ghafla. Alvin pekee ndiye aliyewahi kumshika kidevu namna ile. Ingawa wakati huo hakujua kama yeye, akili yake ya ndani kabisa ilimwambia kuwa huyo ni Alvin. Ikiwa ni yeye, hakujali kumbusu. Alisimama kwenye vidole vyake vya miguu na kumbusu. Alimbusu shavuni kwa sababu alikuwa amelewa sana kuona midomo yake.

Mwili wa Alvin ukakakamaa, na mwali wa kutisha ukawaka ndani yake. Ikiwa Lisa hakuweza kumtambua na kumwona tu kama mgeni, kwa hivyo angewezaje kumbusu kwa urahisi namna ile?
Daima alikuwa mwanamke mlegevu hivyo? Alimwachia ghafla kwa hasira.
Hata hivyo, kabla hajamwachia kabisa, Lisa aliyumba na kuanguka pembeni. Hakuwa na uwezo tena wa kuhimili. Alikuwa amelewa hadi kuzima.

Vijana wote waliokuwemo mle ndani walimtazama Alvin wakiwa wameduwaa. Kila mtu alijua kwamba Kaka Mkubwa Kimaro alijulikana kwa kutokuwa karibu na wanawake, ilikuwaje siku hiyo?

“Mkubwa… Mkubwa Bwana Kimaro, ni nini kimekuleta hapa?” Kelly, yule kijana wa kwanza kabisa kucheza na Lisa aliuliza kwa mshangao.

“Nani alimnywesha pombe?” Macho meusi ya Alvin yalitanda kwenye kila uso wa mtu aliyekuwa kwenye chumba hicho mmoja baada ya mwingine.

Kila mtu alihisi moyo wake ukitaka kuruka. Wangeweza tu kumtazamia Rodney kwa msaada. "Bwana Shangwe, ni wewe ndiye uliyetuambia."

“Ni sawa.” Rodney aliinuka na kumsogelea Alvin huku akicheka kwa sauti ya chini. “Alvin, nilikuwa nakusaidia tu kutoa hasira zako. Ilikuwa ni kosa lake kukudanganya na kucheza na wewe. Kwa kuwa amethubutu kuja Nairobi, jiji la wenyewe, bila shaka, sina budi kumfundisha adabu kwa niaba yako.”

Kabla hajamalizia, Alvin alimrushia ngumi nzito usoni. Rodney alishikwa na Alvin na kupigwa hadi mdomo wake ukapasuka.

“Alvin Kimaro, unathubutuje…?!” Rodney alikasirika sana.

Vijana wengine wote walitaka kukimbia haraka kutoka kwenye chumba kile. Mafahari wawili wakubwa wailitosha kuanzisha tetemeko la ardhi. Nani angethubutu kuingilia kati?

“Nani anathubutu kuondoka?” Alvin aliwakazia macho, na walinzi kadhaa wakasimama mlangoni.

"Kaka Mkubwa Kimaro, tumekukosea nini?" Kijana Kelly aliuliza kwa uso wa kuchanganyikiwa huku akizuia woga wake.

Mtazamo wa hasira wa Alvin ulienea na kutawala ndani ya chumba. Vijana wote waliokuwemo mle ndani walikuwa ni mabwana wadogo ambao walipenda sana kucheza na wanawake. Alipowaza jinsi macho machafu ya vijana hao yalipokuwa yanazunguka kwenye mwili wa Lisa na jinsi walivyoweza kumgusa kabla hajafika, hakutaka kitu zaidi ya kuwatoboa macho yao.

“Alvin, mimi ndiye niliyewaita. Ikiwa unataka kumlaumu mtu, basi nilaumu mimi.” Rodney akasogea mbele kuwalinda.

Macho makali ya Alvin yenye uwezo wa kutoboa ngozi yakahamia kwake. Chumba kile kikubwa kiilikuwa kimya sana hata pini ingeweza kusikika ikiwa ingeanguka.

“Matukio ya usiku wa leo… Ikiwa mtu yeyote atathubutu kueneza neno, picha, au video, nitaifanya familia yake yote kutoweka." Alvin alilitazama kundi hilo la watu. Haiba yake ya kutawala ilienea, ikidai utii.

Sura ya 156

Umati wote uliogopa sana. Hata mpumbavu angeelewa uhusiano wa mwanamke huyo na Bwana Kimaro. Watu ambao walijaribu kuchukua fursa ya kumchezea Lisa mapema wote walipauka kwa hofu.

“Pia, nataka uvunje mkono wa kila mtu aliyemgusa hapo awali. Kuna kamera za uchunguzi ndani ya boti hii, nitazikagua." Alvin alimnyanyua Lisa na kugeuka kuondoka.

Rodney alipandwa na hasira na kumfuata kwa haraka. “Alvin, hunioneshi heshima hata kidogo. Kweli sikuelewi. Mwanamke huyu hakujali hata kidogo na hata alitoka na mwanamume mwingine akiwa pamoja na wewe. Wanawake kama yeye wanapaswa kufundishwa adabu. Isitoshe, nilikuwa hapa. Nisingemruhusu mtu yeyote kumfanyia chochote. Nilitaka tu kumdhalilisha.”

"Hata ikibidi afundishwe somo, mimi ndiye ninayepaswa kufanya." Usemi wa Alvin ulibaki bila kubadilika. "Sio jukumu lako kumdhalilisha."

Baada ya kuondoka kwenye Yatch, Alvin alipanda helikopta na kuondoka moja kwa moja. Helikopta ilipopaa, mlio wa sauti yake ya kutetemesha ulimfanya Lisa apate kizunguzungu. Tumbo lilimchafuka, akajirusha juu ya kifua cha Alvin na kumtapikia. Harufu mbaya na kali ilipenya pua yake, na sura ya Alvin ikageuka kuwa mbaya kwa kinyaa. Akamtupa Lisa kwenye kiti na kulivua koti lake kwa haraka kisha akalitupa chini kwa kuchukia.

“Ugh….” Lisa aliguna na kujigeuza kwenye kiti. Kipande kile cha mtandio kilishindwa kumsitiri na kuifanya damu ya Alvin kuchemsha. Kumuona vile, moto uliokuwa tumboni mwa Alvin ulibadilika mara moja na kuwa wa aina nyingine. Harakaharaka akavua sweta lake safi na kuufunika mwili wake. Hakutarajia kwamba angewahi kumwona hivyo tena.

Hakurudi kwa bibi yake, dakika kumi baadaye, helkopta ilitua juu ya paa la makazi yake ya binafsi jijini. Alvin alimpeleka Lisa chumbani na kumtupa kwenye kitanda kikubwa.

Lisa alijikunja na sweta yake iliyomfunika mara moja ikaanguka kutoka mwilini. Alvin alishindwa kustahimili pale mapaja ya Lisa yaliyonona na kung’aa yalipowekwa wazi. Alikuwa karibu kumfunika blanketi mara ghafla Lisa alimshika mkono na kuugulia. “Tumbo langu linauma. Nisaidie kulisugua.”

Mwili wa Alvin ukawa mgumu. Alimshika mabega yake maridadi kwa hasira na kumuuliza kwa sauti ya hovyo, “Unataka nani akusugue tumbo lako?”

Alvin alidhani kwa kuwa Lisa alikuwa amelewa, angetaja Kelvin Mushi. Ikiwa ndivyo, bila shaka angemtupa nje ya chumba kupitia dirishani. Lakini Mungu alisaidia. Kumbukumbu zilimjia Lisa kwamba alipokuwa akipata maumivu ya tumbo wakati akiingia mwezini, ni Alvin ndiye aliyekuwa akimchua tumbo lake.

“Alvlisa, Alvlisa…” Lisa alitamka kwa butwaa..

"Lisa Jones, una uhakika kuwa umelewa?" Alvin alibana uso wake mdogo kwa nguvu. “Bado unacheza na mimi tena?"

"Inauma, namaanisha." Lisa kwa ulevi alinyanyua mguu ili kumpiga teke taratibu. Ohooo! Hapo sasa ndo kabisa hali ya hewa ikawa mvurugano mle chumbani. Njia ya kwa bibi ilikuwa nyeupe kabisa! Hakuwa na nguvu hata ya kupiga teke lenyewe, akaishia tu kupanua miguu yake iliyokosa nguvu.

Alvin karibu atokwe na damu puani. Ni mawazo gani mabovu yaliyompitia Rodney hadi kumfanya Lisa avae vazi hilo? Ilikuwa ni kumfedhehesha tu!

"Lisa Jones, unaweza kuota ikiwa unataka nikusaidie kusugua tumbo lako." Alvin alibana uso wake hadi ukawa mwekundu.

“Mm… Inauma… Alvlisa.” Lisa aliuma mdomo wake kitoto kabla ya kufungua macho yake makubwa na mazuri yaliyojaa majimaji, na kwa sababu alikuwa amelewa, yalikuwa yamelegea sana. Uvimbe wa hasira kwenye koo la Alvin ulipungua. Muda mfupi baadaye alimfunika na blanketi kabla ya kutoka nje.

Hakujua ni kitu gani kilimfanya kwenda jikoni. Alitumia simu yake ku-google ili kujua mtu anapaswa kula nini ikiwa tumbo lake litavurugika baada ya kunywa pombe. Ilionekana kuwa juisi ya nyanya ilikuwa wazo nzuri.

Hata hivyo, hakuwa ameishi katika nyumba hiyo kwa miezi kadhaa, kwa hiyo hapakuwa na chakula chochote nyumbani. Aliweza tu kumpigia simu Hans. "Niletee nyanya mara moja."

Hans ambaye alikuwa akijiandaa kwenda kulala, uso wake uligeuka kwa mshangao. “Bosi, unatarajia nipate wapi nyanya usiku huu wa manane? Unataka kutengeneza juisi kwa ajili ya Bi Jones?”

“Harakisha. Nazitaka ndani ya dakika 20." Alvin alikata simu bila kueleza zaidi.

Hans akaguna kwa hasira. Angezipata wapi nyanya usiku huo wa manane? Msaidizi ambaye hakuweza kufanya chochote alihofia angefukuzwa kazi kwa sababu ya nyanya. Mwishowe, Hans aliweza tu kumwomba mmiliki wa duka la karibu kuwafungulia walinzi milango ili wampatie nyanya. Kisha akazikimbiza haraka kwa Alvin.

Alvin alipozipata zile nyanya, alizitoboa tu na kuziminya ili kutengeneza juisi, kisha akapeleka glasi chumbani. Lisa alikuwa amejikunyata kitandani, akiwa amelala. Akamnyanyua na kumwesha ile juice. Lisa alifungua kinywa chake bila fahamu na kuinywa ile juisi. Juisi ya uchachu ilimfanya tumbo kujisikia vizuri na hakuhisi tena kichefuchefu.

Baada ya kunywa, alijilaza kitandani kwa utulivu huku kope zake zikitetemeka kama mbawa za mbayuwayu. Midomo yake iliachwa na rangi nyekundu na zile nyanya na kumfanya aonekane kama ametoka kunyonya damu. Alvin aliguna. Alikuwa ameonja midomo hiyo kwa mabusu mara nyingi hapo awali, lakini, wakati huo hakuwa na hamu nayo kabisa.

Simu ya Lisa iliyokuwa karibu na meza ilitetemeka ghafla. Skrini ilionyesha ujumbe uliotumwa na Kelvin Mushi. [Nimekumiss sana mpenzi]

Alvin ghafla alionekana kupoa. Muda mfupi baadaye, tabasamu la kujidharau lilionekana kwenye midomo yake. Alikuwa ni mpumbavu wa kiwango gani kwenda huko kwa helikopta ili kumuokoa Lisa ambaye moyo wake ulikuwa kwa mwanamume mwingine? Bora tu angemuacha adhalilishwe.
•••
Siku inayofuata, Lisa alifumbua macho na kuzinduka na kujikuta yupo kwenye kitanda asichokifahamu. Alikaa na kuwaza!

Matukio ya jana yake yakaanza kutiririka kwenye ubongo wake moja baada ya jingine. Lisa akakumbuka kuna jambo lililomtokea Pamela usiku wa jana yake. Alipokimbia kwenda kumuokoa, alikutana na rafiki wa Alvin ambaye alitaka kumfundisha adabu. Ili kupata dola 10,000 za kujikomboa yeye na Pamela, aliishia kunywa pombe sana. Zaidi ya hayo, kuna mtu alifika, alionekana… akambusu…Kisha, alikumbuka bila kuwa na uhakika kupanda helikopta!

Kama ilivyotarajiwa, kumbukumbu zake zote zilivurugika baada ya kunywa pombe kupita kiasi. Je, alipanda kweli helikopta au alikuwa anaota? Na kama alipanda iliruka kwenda wapi usiku huo? Kuna mtu alilala naye?

Akiwa anatetemeka kwa mawazo hayo, aliinua blanketi ili kujitazama na nusura kulia alipoona kwamba bado alikuwa amejifunga upande ule mtandio, lakini nguo yake ya ndani ilikuwepo na haikuonekana kuwa iliwahi kutolewa, kwa hivyo alikuwa salama. Alitazama pande zote na kuona kabati la nguo. Alihitaji kitu cha kujisitiri.

Alipoinuka tu kutoka kwenye kitanda, mlango ulifunguliwa ghafla.
Alvin aliingia ndani kwa umaridadi huku akiwa amevalia vazi la bluu bahari, na mwili mzima wa Lisa uliganda baada ya kumuona....ITAENDELEA...

Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.