JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................153-154

Sura ya:153

Siku chache zilizofuata, Lisa alitoka mapema na kuchelewa kurudi. Hakuwahi kukutana tena na Alvin baada ya tukio lile.

Pamela naye alikuwa amefika jijini Nairobi baada ya mwaka mpya kwa ajili ya kuanza kazi kwenye kiwanda cha vipodozi cha Osher. Siku moja Lisa alifanya miadi ya kukutana na Pamela mjini. Wawili hao walikutana mida ya mchana mahali fulani katikati ya jiji na Pamela akampeleka kwenye hoteli ya hali ya juu kupata chakula.

“Niilitambulishwa mahali hapa na mfanyakazi mwenzangu. Mahali hapa ni pazuri sana. Ni ghali sana, lakini bado ninaweza kumudu kukununulia chochote unachotaka.” Pamela alifurahi sana kwamba hatimaye aliweza kuungana tena na rafiki yake mpendwa katika jiji lile.

Baada ya kuagiza chakula, Lisa alimtazama Pamela kwa makini. Ingawa alikuwa amepungua uzito, bado alionekana mzuri.
“Unaendelea vizuri?”

“Kabisa. Kampuni inanijali sana, inanihudumia vyema na hata meneja mkuu amesema kampuni itanipeleka kusoma nje ya nchi katika nusu ya pili ya mwaka.” Pamela aliinamisha kichwa chake na kukoroga kahawa yake.

“Patrick amewasiliana tena na wewe?” Lisa aliuliza.


"Hapana." Pamela alitabasamu kwa uchungu. "Labda anafurahi hatimaye nimeondoka karibu naye, sasa atakuwa huru."

“Acha kumfikiria. Kwani hakuna wanaume wazuri hapa Nairobi?” Lisa alitazama nyuma ya Pamela na kumtingisha kidevu chake. “Tazama, kuna mmoja mlangoni sasa hivi anakutazama.”

Pamela alitazama kwa wakati na kuona mwanamume mmoja akigeuka. Alikuwa amevaa koti jeusi la bei ghali, na miguu yake mirefu ilifanana na ya mwanamitindo. Wanaume wawili ambao walikuwa katika umri wao wa ujana walikuwa wakimfuata nyuma kama mbwa wa kufugwa. Pamela aliwatambua wanaume hao. Mmoja alikuwa meneja mkuu wa kampuni aliyokuwa imewajiri huko Nairobi, mwingine alikuwa naibu wake, na yule mwanamume mtanashati zaidi kuliko wote hakumjua mara moja lakini sura yake haikuwa ngeni.

“Yeye ni handsome sawa lakini si kiasi hicho. Unatia chumvi.” Pamela alitoa mawazo yake aliporidhika kumwangalia. Hatimaye akamkumbuka yule kijana handsome, “unajua yeye ni nani? Ni rafiki wa Alvin. Niliwakuta pamoja kwenye hoteli ya ‘Villa Rosa Kempinski’ siku ile nimemfuata Alvin kumbembeleza akutetee kwenye kesi yako. Nimemkumbuka sasa.”

“Wee! Kwa hiyo marafiki wa Alvin wote ni matawi ya juu!” Lisa akapepesa macho. “Mwangalie vizuri, anaweza hata kumzidi Alvin Kimaro.”

"Kama hadi wewe umemkubali bali inamaanisha kuwa yeye ni mzuri sana." Pamela alicheka. Ijapokuwa hakuwa katika hali nzuri baada tu ya kuachana na Patrick, hilo halikumzuia kuwahusudu wanaume watanashati.

•••
Juu, katika chumba kimoja cha hoteli hiyo hiyo, waliingia vijana watatu. Mmoja alikuwa Rodney Shangwe, mwenyekiti wa kampuni ya kutengeneza vipodozi ya Osher Corporation na mwingine alikuwa Meneja mkuu wa Kampuni hiyo pamoja na msaidizi wake. Msaidizi wa meneja alimimina pombe kwenye glasi mbili na kuzigawa kwa mabosi wake kwa uangalifu.

Meneja mkuu aliyasoma mawazo Rodney kutokana na jinsi alivyokuwa akimtazama Pamela wakati wanaingia. "Bwana Shangwe, mwanamke aliyevaa sweta ya hudhurungi uliyekuwa ukimwangalia kule mgahawani hapo awali ni mkemia mkuu wa vipodozi wa kampuni yetu, Pamela Masanja."

"Oh, kwa hiyo yeye ni mfanyakazi wa kampuni yetu?" Mpasuko wa tabasamu ulitokeza kwenye midomo yake. "Sura yake si ngeni, lakini sikumbuki nilimwona wapi.” Rodney aliwaza. Baadaye kumbukumbu ikamjia. Ni rafiki wa Lisa aliyekuja Nairobi kumbembeleza Alvin, na yeye ndiye aliyemfungulia mlango wa chumba cha hoteli waliyokuwemo siku hiyo.

“Basi yule ambaye alikuwa ameketi karibu naye lazima awe rafiki yake, sivyo?" Rodney alihisi.

“Bila shaka.” Meneja mkuu alimuunga mkono.

Rodney alichezea glasi ya pombe mkononi mwake. “Nataka kuonana nao baadaye. Fikiria njia ya kuwaalika Pamela Masanja na rafiki yake.”

Meneja mkuu alihisi wasiwasi. "Bwana Shangwe, Pamela Masanja ni kipaji adimu ..."

“Usijali, sitampa wakati mgumu. Nina shida na rafiki yake, ni kwamba rafiki yake alimfanyia mambo ya kishenzi rafiki yangu hapo awali,” Rodney alisema kwa unyonge, “Uwe mwangalifu usiwatahadharishe.”
•••
Lisa na Pamela walizungumza kwa muda mrefu na kukubaliana kwenda kwenye sinema baadaye wakati Pamela ghafla alipokea simu kutoka kwa meneja mkuu wa kampuni yake.

“Shoga, kuna dharura imejitokeza. Naenda kujadiliana na bosi kuhusu pendekezo la kipodozi kipya nilichokifanyia utafiti hivi karibuni, tutaonana baadaye au siku nyingine, muhimu nitakupigia simu.” Pamela alitangaza udhuru kwa Lisa baada ya kuzungumza kwenye simu na meneja wake.

“Unaniacha peke yangu?” Lisa aliinua kichwa chake kwa mshangao.

“Sina ujanja.” Pamela alisikitika. “Meneja mkuu amesema kuwa Mwenyekiti wa kampuni amekuja kwa ukaguzi leo, na wakazungumzia kuhusu bidhaa hiyo mpya ya urembo ninayoitafiti. Anataka niende kuripoti kwa Mwenyekiti sasa na kutoa maelezo ya utafiti wangu. Sijawahi kumuona huyo mwenyekiti mwenyewe ila nasikia si mtu wa kuchezea hata kidogo. Familia yake ni moja ya familia bora hapa Nairobi. Wanatisha kama familia ya Kimaro."

Lisa alikosa la kusema. "Kwa hiyo jiji hili lina matajiri wengi kushinda Dar?"

“Haswa. Familia za kina Harrison, Kileo na Zongo zinaweza kuchukuliwa kuwa na ushawishi mkubwa huko Dar es Salaam, lakini kwa hapa Nairobi, wao ni watu wa chini tu.” Pamela alishtuka. “Wewe rudi nyumbani kwanza, tutaonana baadaye.”

“Basi sawa, mimi wacha nirudi kwa mzee Ngosha tu nikapumzike.” Lisa alijibu kinyonge sana.

"Sawa kuwa makini, usibaki hapa peke yako, sitaki nikuponze tena. Tayari nimeshakuponza vya kutosha.” Pamela alipunga mkono wake na kuondoka haraka.

•••
Usiku mida ya saa mbili hivi, Lisa alikuwa ametoka kuoga na alikuwa tayari kulala wakati ghafla alipokea simu kutoka kwa Pamela, lakini ni mtu asiyejulikana ambaye alizungumza. “Wewe ni Bi Jones?”

“Ndiyo!” Lisa aliitikia kwa wasiwasi.

“Rafiki yako amelewa sana. Tafadhali njoo umchukue.”

"Wewe ni nani…?" Lisa aliuliza kwa mshangao. Hakumjua mtu huyo.

"Ni meneja mkuu wa kampuni anayofanyia kazi." Mtu huyo akamjibu.

Lisa hakuwa na ujanja zaidi ya kubadilisha nguo zake na kujiandaa. Aliposhuka chini, akakutana na Melanie ambaye ndo kwanza alikuwa amerudi.

“Unaenda wapi usiku huu? Usiniambie kuwa unaenda kudanga na wanaume wa Nairobi?" Maneno ya Melanie hayakuwa ya kufurahisha sana.

“Rafiki yangu amelewa hivyo nitaenda kumchukua.” Lisa hakuweza kuhangaika kujieleza zaidi kwa Melanie na akaendesha gari moja kwa moja hadi alikoelekezwa.

Lisa alielekezwa kwenda katika Ziwa Naivasha. Ziwa hilo lipo katikati ya Nairobi na Nakuru. Aliendesha gari kwa masaa mawili hadi kufika huo akifuata maelekezo ya GPS.

Kulikuwa na boti za kifahari maarufu kama Yatch zikiwa majini kando ya ufukwe wa ziwa. Lisa aliekezwa kuingia kwenye boti moja ya kifahari. Ndani yake akakuta wanaume na wanawake zaidi ya kumi na mbili kwenye chumba kilichochangamka sana. Wanawake wote walikuwa wamevaa bikini. Hali hiyo ilimfanya Lisa aweke mikono mdomoni kwa mshangao.

Sura ya: 154

Lisa alitaka kumpigia simu Joel. Hata hivyo, kabla hajaipiga ile namba, ghafla mwanaume mmoja alimrukia kwa nyuma na kuuzuia mwili wake. Akachukua simu yake na kumburuta juu juu. Lisa alijitahidi sana lakini hakuweza kujinasua. Alijua kwamba alikuwa amenasa mtegoni, lakini haikuwa muda mrefu tangu akanyage Nairobi. Hakuwa amemkosea mtu yeyote pia. Inaweza kuwa Nina?

Baada ya kufika kwenye ghorofa ya juu ya Yatch hiyo ya kifahari, alimuona mwanamume mtanashati mwenye haiba ya kuvutia aliyevalia koti jeusi la ngozi akiwa amekaa kwenye sofa. Mwanamume huyo alikuwa na macho makali yaliyotulia kwenye uso mzuri na nywele safi. Macho yake yaling'aa, na alikuwa na mdomo uliozungukwa na ndevu zilizotunzwa vyema. Alikuwa ni mwanaume yule yule ambaye walikuwa wamemwona na Pamela mgahawani hapo awali.

“Ni wewe." Lisa alipigwa na butwaa. "Sijawahi kukutana nawe hata siku moja na sijawahi kukukosea pia, kwanini umenileta hapa?"

"Hujawahi kunikosea, lakini umemkosea rafiki yangu." Rodney akasimama taratibu huku mikono yake ikishika mkanda. Uso wake mzuri ulijaa ukatili kama Alvin tu. “Unaonekana mzuri sana. Si ajabu uliweza kumdanganya Alvin.”

"Wewe ni rafiki wa Alvin?" Hatimaye Lisa aliekumbuka kile alichoambiwa na Pamela hapo awali na kusema kwa hasira, “Hiyo ni kati yangu na Alvin. Rafiki yangu yuko wapi?”

“Mpelekeni akamwone rafiki yake.” Rodney aliagiza na mara Lisa akapelekwa kwenye chumba kingine cha kifahari sana. Pamela alikuwa amelala kwenye kitanda kikubwa kama yupo chumbani kwake vile, hoi hajitambui. Baada ya kumwona, Lisa hakuruhusiwa hata kumgusa tu, alirudishwa mara moja kwa Rodney.

“Mnataka kumfanya nini?” Lisa alimuuliza kwa hasira. “Yeye si mfanyakazi wa kampuni yako?"

“Sina uhaba wa wafanyakazi. Kutokuwepo kwake hakuwezi kuathiri chochote.” Tabasamu la Rodney lilikuwa zuri sana, lakini liliwafanya wengine wahisi hofu. "Ikiwa unataka kumuona tena rafiki yako, itategemeana na utii wako."

"Unataka nifanye nini?" Lisa aliuma mdomo na kuuliza.

"Vua suruali yako na ujifunge hiki kipande cha nguo na ushuke chini kunengua ili kila mtu aone. Nitakuachia wewe na rafiki yako endapo utacheza hadi kila mtu awe tayari kukuzawadia dola elfu kumi.” Rodney alichukua kitambaa kidogo sana saizi ya mtandio mwepesi na kukitupa mbele yake.

Lisa alitaka kutapika damu. Kilikuwa ni kitambaa kidogo sana ambacho alitakiwa kujifunga ambacho kisingeweza kumsitiri hata kidogo. Isipokuwa kwa maeneo muhimu tu, kila kitu kingine kingefunuliwa. Kilikuwa pia ni chepesi sana hata kisingeweza kustahimili mtikisiko wake wa nyuma. Hakuwa na maumbile makubwa, sawa, lakini kwa mtandio ule bila shaka ingekuwa ni uchochezi tu wa kihisia kwa wanume wale. Hakika kilikuwa kitu ambacho hakipaswi kuvaliwa mbele ya watu, achilia mbali wanaume wale. Ikiwa angejifunga kitu hicho asingekuwa tofauti na wanawake wanaojiita kangamoko ndembendembe waliokuwa na kazi za kunengua katika mabaa.

“Hey, unaweza usijue hili, lakini mimi ni binti wa Joel Ngosha. Ikiwa baba yangu atajua - " Lisa alikatishwa hata kabla hajamaliza sentensi yake.

"Nilisikia kwamba Joel Ngosha amemleta binti yake wa nje, lakini ili iweje? Hata kama Melanie Ngosha angesimama mbele yangu, nisingejali.” Rodney aligonga saa yake. "Una dakika moja, au rafiki yako nitamtosa ziwani!"

"Hakika sijawahikufanya jambo kama hili kabla, unaweza ukanibadilishia mashariti?" Lisa alijawa na hofu.

“Hakika, ninaweza.” Rodney alicheka kijeuri. “Ulale na vijana wote hawa mmoja baada ya mwingine.”

“Yesu wangu! Nitaweza wapi ikiwa kucheza tu nimeshindwa?” Lisa aliendelea kuvuta muda akiota huenda muujiza wa kumuokoa ungetokea ghafla.

“Inatosha, Lisa Jones. Alvin hana akili ndiyo maana ukamdanganya kirahisi, lakini usifikirie kuwa na mimi sina akili kama yeye. Siamini kuwa mwanamke kama wewe hujawahi kuwa na wanaume chini ya saba hadi wanane. Sasa ni kipi cha ajabu?” Rodney alionekana kukosa subira. "Tatu, mbili -"

“Sawa, nitaivaa.” Lisa mwishowe aliamua kujitoa mhanga.

Asingeweza kupambana nao hata hivyo. Kwa kundi lile la vijana matajiri, yeye hakuwa kitu zaidi ya mdori. Lakini alikuwa radhi kufanya chochote ili kumwokoa Pamela. Dakika tano baadaye, alienda kwenye chumba cha kubadilishia nguo na kubadilisha suruali yake kwa kipande cha mtandio, bahati nzuri alikuwa amevaa tight kwa ndani. Alijifunga kle kipande ha mtandio kwa ustadi kiasi kwamba ni nusu ya mapaja yake tu ndiyo yalikuwa wazi. Alitoka na kushuka chini taratibu. Wanaume waliokuwa pale chini walipiga miluzi papo hapo.

"Halo, Bwana Shangwe, umepata wapi binti mzuri kama huyo? Anaonekana mzuri sana." Wanaume hao walimtazama mrembo huyo aliyekuwa amejifunga si chochote zaidi ya mtandio mwepesi na papo hapo wakahisi kuchoka. Wote wakamkazia macho ya uchu.

Uso wa Lisa ulikuwa umeshuka kutokana na unyonge na machozi yaliyogoma kutoka, lakini Rodney alisema tu kwa msisimko, “Baadaye, kila mmoja atacheza naye. Mnaweza kumtuza, lakini ataacha kucheza atakapofikisha dola elfu kumi.”

Meno ya Lisa yaligongana kwa hasira. Kwa kuwa alisema kimakusudi kwamba angeacha kunengua baada ya kupata dola elfu kumi, ni nani alijua ingemchukua muda gani kupata kiasi hicho?

Hakika, wanaume wale walicheka. "Katika hali hiyo, itabidi tumtuze kidogokidogo ili tufurahie muda mrefu zaidi."

"Ni kweli...."

Umati ulipotazama, alijizungusha polepole kwenye nguzo na kuanza kucheza. Angeweza kucheza vizuri, lakini alijua kwamba jinsi alivyokuwa akicheza vizuri zaidi mbele ya umati, ndivyo angeweza kuwafanya wapoteze akili zao.

Lakini, alipuuza kuzingatia umbo lake la uzuri wa kushangaza alipokuwa akicheza. Alicheza taratibu ili kuepusha makalio yake yasitikisike katika mtandio ule mwepesi aliojifunga.

Rodney alirekodi video ya Lisa akicheza na kuituma kwa Alvin. [Alvin, ninakusaidia kumfundisha adabu mwanamke huyu...]
•••
Katika makazi ya familia ya Kimaro, Alvin ambaye alikuwa anaelekea kulala mara moja alihisi ubongo wake kuwaka moto alipoiona ile video. Katika video hiyo kulikuwa na mwanamke aliyejifunga mtandio mwepesi mwekundu. Kitambaa kilimbana sana kiasi kwamba kiliyafedhehesha maumbile yake. Ngozi yake ilikuwa niking’aa kama theluji kwenye taa za rangi, na uso wake mdogo ulikuwa mzuri na wa kuvutia kama waridi. Kiuno chake kiliyumba kidogo, na matako yake yalikuwa yamejaa na kutuna kwa kubanwa na mtandio ule. Alvin alifikiria idadi ya wanaume wengi waliokuwa wanamuangalia Lisa, na bila kujielewa alihisi kupasuka kwa hasira. Alimpigia simu Rodney lakini akagundua kuwa alikuwa anaongea na simu nyingine.

Mawazo tu ya Lisa kuangaliwa na watu wengi yalimfanya atamani kumpasua Rodney. Alinyanyuka na kutoka nje ya chumba kile. Dakika tatu baadaye, alipanda helikopta. Ilikuwa usiku sana, na matajiri wengi wanaoishi katika kitongoji kile cha Mlima wa Sherman walijawa na msisimko.

“Hiyo si helikopta ya Bwana Kimaro? Anaenda wapi usiku huu?” Baadhi ya majirani waliulizana.

"Lazima liwe jambo muhimu. Bwana Kimaro mara chache sana husafiri kwa helikopta yake binafsi.”.....ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.