JINA LA SIMULIZI............................LISA

AUTHOR...........................JOMBA WAJO

SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY

WHATSAPP.........................0628924768

SEHEMU YA...............................114, 115


Sura ya 114


Mara tu baada ya kumaliza kuzungumza, watendaji wachache waliokuwa wakijadili muundo huo walikunja uso.

Lisa kisha akauliza, “Kwa nini unahitaji kabati kubwa katikati hapa?”

"Kwa ajili ya nafasi kubwa ya kuhifadhia." Lina alijibu bila kujiamini.

Lisa alifoka. “Ni kwa sababu kuna nguzo kubwa katikati ambayo haiwezi kung’olewa, nikachagua kuweka kabati kubwa hapo.” Lina akabaki ameduwaa, hana cha kumkosoa Lisa. “Na kwa kuongezea, ni jumba lenye ghorofa mbili na ukubwa wa mita za mraba 128.7. Iinakaa mashariki, likitazama magharibi.” Uso wa Lina ulipauka mara moja kwa aibu.

Lisa alikodoa macho. "Unadai kuwa ulitengeneza hizi, lakini hujui chochote kuhusu maelezo yake ya kitaalamu, ungewezaje kuwashauri mafundi? Wewe ndiwe msimamizi wa mradi, ilhali hujui lolote kuhusu aina ya nyumba na ni majengo mangapi yanajengwa katika mradi huo, unafaa kweli wewe?”

Lina hakuweza kukanusha neno lolote kwa sababu hakuwa anaelewa chochote kuhusu michoro hiyo. Kundi la wafanyakazi waliokuwa kwenye mkutano huo lilitingisha vichwa vyao mmoja baada ya mwingine, wote wakiwa wamekata tamaa sana.

Wakati huo huo, Shani aliingia na maafisa wachache wa polisi. Mmoja wao alimfunga pingu mikononi Lina. “Bi. Jones, tulipokea ripoti kwamba umeiba kazi ya mtu mwingine. Tafadhali fuatana nasi hadi kituoni kwa ajili ya uchunguzi.”

“Hapana, sitaki! Sikufanya hivyo!” Lina alipiga kelele kwa hofu.

“Acha kupiga kerere weye, hiri ni jeshi ra porisi, tii sheria bira shuruti.” Polisi mmoja mwenye sura mbaya zaidi alimuadabisha Lina. Polisi hao wawili walimnyanyua na kumtoa nje bila subira.

“Ninafanyiwa njama tu! Mimi sikuiba. sikufanya hivyo!” Lina alilalamika bila msaada.

Mayowe yake yalipofifia, Lisa alitazama kwenye chumba cha mikutano kabla ya kumgeukia Lazaro Changala. “Meneja Mkuu Changala, nilisikia kuwa wewe ndiye uliyemteua Lina Jones kuwa meneja wa mradi huu. Nina shaka na maono yako na uwezo wako wa kuongoza kampuni."

Lazaro Changala akaingiwa na hamaki na kujibu kijeuri. “Kama Mwenyekiti Jones unatilia shaka uwezo wangu basi niondoe kama unaweza.”

Alimwangalia moja kwa moja Lisa alipomaliza kuongea. Hakuamini kama Lisa alikuwa na ujasiri wa kumwondoa kwenye nafasi yake. Bodi ya wakurugenzi wa Kampuni wasingemwacha salama.

“Inawezaje kuwa hivyo? Meneja Mkuu Changala ameongoza utendaji wa kampuni kwa mafanikio mengi. Kwa kawaida, nakuamini.” Lisa alitabasamu ghafla na kubadilisha mawazo yake. "Mkutano huu nitakuachia ili uendelee nao." Kisha akamaliza kuongea na kuondoka zake. Lazaro Changala alimtazama nyuma kwa dharau. Alifamini kwamba asingemfanya lolote kwa sababu alikuwa na uzoefu zaidi kuliko yeye.

Hata hivyo, baada tu ya Lisa kuondoka tu, kuna kituko kilitokea ghafla. Mke wa Lazaro Changala aliingia ndani ghafla na kumpiga kofi usoni. "Lazaro Changala, wewe mwanaharamu! Unathubutuje kuwa na mchepuko nje?

“Kama nisingekuoa enzi hizo, leo hii ungeweza kuingia Mawenzi Investiments ukiwa na jeuri hivi?” Changala alichukia kupitiliza.

“Kwa hiyo unanifanyia makusudi siyo? Umenitumia miaka yoote hiyo hadi umenizeesha ndiyo unaamua kurudi kwa mabinti? Nitapambana nawe.” Mama yule wa makamo aliwaka kwa hasira.

Habari za ghasia kwenye chumba cha mkutano zilienea haraka katika kampuni nzima. Tunu alicheka wakati wa kuripoti habari hiyo kwa Lisa. “Hukuona jinsi uso wa Meneja Mkuu Changala ulivyokuwa karibu kupasuka alipopigwa kofi. Alifedheheka kabisa. Hata aliamua kumpiga vibaya mke wake hadharani.”

'Huu ni mwanzo tu." Lisa alitabasamu na kumpigia simu Sam. “Sam, huna namba yoyote ya mwandishi wa habari? Kuna mambo ya kuruhashisha hapa nataka yaripotiwe kwa jamii.”

“Haha, hakuna shida, nitakutafutia.” Sam alijibu kwa furaha. “Ni mara chache sana shemeji yangu huwa anaomba msaada wangu…lakini ni jambo gani hilo?”

Lisa akaeleza kituko kilichomtokea Meneja Lazaro Changala.


Kabla Sam hajaendelea kusema, ghafla alihisi kushtuka. Akatazama upande wake alipokuwa amekaa Alvin huku uso wake ukiwa unapunguza furaha taratibu. Alijiuliza kimykimya. “Lisa, kwa nini haombi msaada wa Alvin? Kwani Alvin hawezi kushughulikia mambo kama haya? Au kwa sababu Meneja Changala ni mkorofi na mtu hatari anahofia atamsababishia Alvin matatizo?”

Lakini Alvin asingeshindwa kushughulikia hilo. Familia ya Kimaro ilimiliki kampuni yenye nguvu zaidi ya vyombo vya habari nchini, lakini Lisa hakuwa amepata nafasi ya kufahamu hilo kwa hiyo ikabaki kuwa ni siri ya Alvin hadi muda huo.

Sam alikosa la kusema. “Lisa, unaenda mbali sana. Huogopi kwamba Meneja Mkuu Changala ataniletea shida?”

"Atakuletea shida gani? Wewe ni kijana wa familia tajiri ya Harrison, atathubutuje kukugusa?” Lisa alicheka. “Ukinisaidia, Mawenzi Investiments itashirikiana nawe katika siku zijazo. Ninahakikisha kwamba familia ya Harrison inashirikiana na Mawenzi katika miradi ambayo familia yenu inashughulikanayo. Familia ya Jones haitakuwa na nafasi.”

“Oh jamani, shemeji hakika unajua kunipanga.” Sam akakosa ujanja.

“Usiseme hivyo. Wewe ni rafiki wa Alvin, kwa hiyo sisi sote ni familia.”

Sam karibu aanguke kwa kicheko. “Sawa, uko sawa.”

Baada ya kukata simu, Sam alifurahi sana. "Lisa ni mcheshi sana. Kila kitu anachosema ni sehemu ya mkakati. Nilikuwa na wasiwasi asingeiweza nafasi yake kama mwenyekiti. Inaonekana kwamba yuko thabiti kuliko nilivyokuwa namfikiria.”

“Unajua unazungumzia mwanamke wa nani?” Alvin alitabasamu kwa kiburi, lakini ghafla alifikiria kitu na kumtazama Sam kwa uso kuchukia.

Sam alijibu akiwa na uso uliotulia. “Una wivu kwa sababu Lisa amenipigia simu kuniomba msaada? Lisa ni mjanja sana, anataka kukulinda. Ana wasiwasi kwamba utaumizwa na Lazaro Changala. Nakuonea wivu sana kwa kuwa na mwanamke kama huyu."

Alvin akatabasamu. Alichokisema Sam kilionekana kumwingia akilini. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mwanamke kujaribu kumlinda. Moyo wake ulijawa na hisia za furaha sana. “Uko sahihi. Alisema atanitunza.”

Tabasamu tata lilichanua kwenye uso wake mzuri, na kusababisha uso wa Sam kuwa na matuta kila mahali. “Alvin, huna aibu sana. Tayari wewe ni tajiri sana lakini una ujasiri wa kuruhusu mwanamke akutunze?”

Macho ya Alvin yalimtoka kwa furaha. Aliukumbuka usumbufu wote ambao Lisa alimsababishia hapo awali, sasa ulikuwa umefika muda wa kula matunda.

 

Sura ya 115


Siku iliyofuata, habari za mambo ya meneja mkuu wa Mawenzi Investiments kupigwa na mkewe ofisini zilienea mtandao mzima. Lazaro Changala alikasirika. Sifa yake iliharibiwa kabisa. Picha zake akipigwa na mke wake hadharani zilienea kila mahali, na hata video yake iliyomwonyesha akiwa na mchepuko wake ilisambaa.

Katika ofisi ya mwenyekiti, Meneja Mkuu Changala aliingia kwa hasira na kumwelekeza Lisa kidole cha usoni. “Umefanya nini? Kwanini umesambaza picha zangu mtandaoni, zinakuhusu nini?”

“Sijui unazungumza nini Bwana Changala.” Lisa alikaa tuli kwenye kiti chake huku akionyesha uso wa kujiamini. "Meneja Mkuu Changala, sikuwahi kutarajia ungekuwa mtu kama huyo. Umetukatisha tamaa sana. Umeharibu hata sifa ya kampuni.”

“Unawezaje kuthubutu kusema hivyo, wewe b*tch?! Usifikirie kuwa sijui kwamba wewe ndiye upo nyuma ya hili. Unafikiri unaweza kunichezea mimi?"

Lazaro Changala alimwendea Lisa na alikuwa karibu kuinua mguu wake ili kumpiga teke, lakini Shani alimkimbilia na kumsukuma kwenye ukuta.

"Wewe b*tch, niachie!" Lazaro Changala alipiga kelele bila kujizuia.

Lisa alipiga intercom kuita usalama. “Fanya haraka umtoe. Nadhani hali ya Meneja Mkuu Changala si nzuri kwa sasa, kwa hivyo nitamkabidhi Naibu Meneja Ngololo masuala ya kampuni.”

"Lisa Jones, we subiri tu! Unathubutuje kunifanyia mambo kama haya? Endelea, siku yako yaja!" Baada ya Lazaro Changala kuvutwa nje, Naibu Meneja Ngololo aliingia kwa haraka.

Akiwa amekabiliana na sura nzuri ya Lisa tena, ghafla alihisi hofu moyoni mwake. Watendaji wa kampuni hiyo hawakumchukulia Lisa kwa uzito hapo awali, lakini ilikuwa ni siku moja tu na sifa ya Meneja Mkuu Changala iliharibiwa kabisa. Kila mtu sasa alitia adabu kwa Lisa. Hakuna aliyekuwa na ushahidi wowote, lakini wote walikuwa na uhakika kwamba Lisa alikuwa na mchango mkubwa katika hilo.

"Naibu Meneja Ngololo, wewe ni mtu mwenye uwezo na uzoefu, lakini daima ulikuwa unakandamizwa na Meneja Mkuu Changala kwa makusudi. Lazima ulijisikia vibaya, sivyo?" Lisa mwenyewe aliinuka na kummiminia kikombe cha kahawa.

Naibu Meneja Ngololo alishtuka na akapokea kahawa haraka, kisha akasema, “lakini Meneja Mkuu Changala amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Watu wengi katika kampuni wanatii maagizo yake, na wakurugenzi wengi wanampenda pia.”

Lisa akaenda moja kwa moja kwenye maamuzi yake kwa uhakika. “Nitakupa muda wa wiki moja. Amua ikiwa unataka kupaa angani au ubaki chini ya Lazaro Changala kama nyumbu wake maisha yako yote." Moyo wa Naibu Meneja Ngololo ulitetemeka sana.

Wakati huo huo, Tunu alikimbia kutoka nje. “Mwenyekiti, Meneja Mkuu Changala alipigwa na kundi la wanawake wakati alipotoka nje ya geti la kampuni. Ni wanawake kutoka umoja wa wanawake wanoteswa na waume zao majumbani, wanaochukia watu wote wanaosaliti wake zao. Walimpiga nusura kumvunja mguu na kichwa kilikuwa kikivuja damu. Anapelekwa hospitali sasa hivi.”

Naibu Meneja Ngololo ghafla alitazama juu na kuona uso wa Lisa usio na hisia. Miguu yake ilitetemeka kwa hofu. “Nitafanya hivyo. Namfahamu Lazaro Changala vizuri sana. Ninaweza kuchukua udhibiti wa kampuni katika wiki moja. Nitakufanyia kazi Bibi Mwenyekiti,” alisema kwa sauti.

“Vizuri sana, nakuamini. Fanya hivyo ili Changala asiwe tena na nafasi katika kampuni hii.” Lisa aliongea kwa umakini na mamlaka. Pembeni, Shani alimtazama na kugundua kuwa tabia ya Lisa ilizidi kufanana na Alvin wakati anafanya kazi.

Baada ya Naibu Meneja Ngololo kuondoka, Lisa alijilaza kwenye sofa kwa uchovu na kusema kwa sauti yenye hatia, “Mimi ndiye niliyemtengenezea njama hizi Lazaro Changala. Shani, unafikiri mimi ni mbaya?"

"Hapana," Shani alijibu kwa urahisi, "Kama hutakuwa mkatili, utawaongozaje mbwa-mwitu hao chini?"

"Ndio, nahitaji kuwa na udhibiti kamili juu ya Mawenzi Investiments. Lazima nilipize kisasi kwa bibi yangu." Lisa alikunja ngumi. Ilibidi alipize kisasi cha mama yake pia. Mzigo uliokuwa juu yake ulikuwa mzito sana kwa yeye kuwa na huruma tena.


Katika wiki moja tu, Naibu Meneja Ngololo alipanga upya kila kitu katika kampuni ya Mawenzi Investiments haraka. Aliwafukuza wafanyakazi wote ambao walikuwa kinyume na Lisa kutoka kwenye uongozi wa juu.

Kuhusu Lina naye alifukuzwa kazi bila huruma. Lina hakujua juu ya suala kubwa lililokuwa linaloendelea huko nje. Alipokuwa kizuizini, wafungwa walimpiga na kumwagilia maji baridi kila siku. Kwa sababu ya hii, ngozi yake iliharibiwa kabisa. Baada ya Lina kuteseka kwa siku saba hadi nane, Jones alijitahidi kumwokoa kutoka katika kituo hicho baada ya kutumia kiasi kikubwa cha pesa. Alitoka akiwa amebebwa.

Alipoona uso wake umevimba, Mama Masawe alimkumbatia na kulia kwa uchungu.

“Mpenzi wangu, umepatwa na nini? Nani alikupiga? Sitamwacha mtu huyo abaki salama.”

“Baba, mama, lazima mlipize kisasi kwa niaba yangu. Inauma sana… Ooohoo-hooo!” Lina alilia sana. Uso wa Lina ulimuuma sana hata akashindwa kuinua macho.

Uso wa Lina uliokuwa umevimba ulimjaa Stephen kwa karaha. Mwanamke huyu alizidi kuwa mbali na mawazo yake. “Usijali, msichana mzuri. Baba yako hakika atawarudia watu hao kwa kukuumiza.” Stephen Kileo alisema mdomoni lakini moyoni alikuwa amekerekea sana.

Jones alipandwa na hasira. Alipogeuka, aliona kwamba Stephen alikuwa ametulia tuli. Alimwamia kwa hasira, “Stephen, fanya haraka umchukue Lina. Anahitaji kupelekwa hospitali sasa hivi.”

“Sawa, sawa.” Stephen alitenda kulingana na maagizo ya Jones bila kupenda. Tangu Lina aingizwe kwenye kituo cha polisi, hakuwahi kuoga. Harufu mbaya iliyotoka kwake ilikaribia kumfanya ashindwe kuvumilia. Wakati huo, alijuta sana. Ikiwa angejua mapema kwamba hii ingetokea, wala asingejihusisha na Lina kabisa.

Katika hospitali, akiwa na macho mekundu, Lina alimwamuru daktari, “Nipe dawa bora zaidi. Nahitaji kupona ndani ya siku tatu zijazo nirudi ofisini.”

"Samahani, hatuna dawa kama hiyo." Daktari alimshangaa.

“Mnafanya nini hapa kama hamna dawa? Kundi la watu wasio na maana. Mama, nataka kuhamishwa hospitali nyingine. Nataka kupona haraka iwezekanavyo na nirudi ofisini kushughulika na Lisa.” Akiwa na uso uliovimba, Lina alionekana kuwa mbaya zaidi alipokasirika.

Akivumilia chuki yake kwa Lina, Stephen alisema kwa unyonge, “Huwezi kurudi ofisini tena. Umefukuzwa kazi.”

"Nini?" Lina alitoa macho akiwa haamini kabisa. “Lisa amerukwa na akili? Anathubutuje kunifukuza kazi?! Meneja Mkuu Changala alitoa idhini yake kwa hili?"

Jones Masawe alikunja uso na kujibu kwa kuudhika, “Lazaro Changala ni majeruhi na sasa yuko katika wodi maalumu ndani ya hospitali hiihii. Hawezi kuruhusiwa katika siku kumi zijazo au hata nusu ya mwezi. Hivi sasa, Freddie Ngololo ndiye anayesimamia kampuni nzima. Lisa alimpandisha cheo na kuwa meneja mkuu.”

Lina alipigwa na butwaa kujua jinsi mambo yalikuwa yamebadilika sana alipokuwa kizuizini kwa siku chache tu. “Hili haliwezekani, ni yeye ndiye aliyepanga njama za kumpiga Meneja Mkuu Changala? Umepiga simu polisi?"

"Hapana." Akiwa amechoka kabisa kimawazo, Jones aliongeza, “Iilikuwa ni kundi la wanawake wanaoteswa na waume zao ndio ambao walimpiga Lazaro Changala. Nilisikia kwamba ni kwa sababu walikasirika kujua kwamba Lazaro Changala alimsaliti mkewe. Lazaro Changala sasa yuko kwenye kina kirefu, na wafanyakazi wengine walio kwenye usimamizi mkuu wa kampuni tuliowahonga wote wanaogopa sasa kumuudhi Lisa. ”

Lina alipatwa na wazimu. "Hujafanya lolote?"

"Lisa amebadilika kabisa. Tulitumia miaka mingi kumlea na haya ndiyo anayotulipa sasa.” Mama Masawe alisema kwa chuki, “Jones, lazima ulipize kisasi kwa niaba ya Lina na upate mamlaka tena kwenye kampuni ya Mawenzi Investiments.”

Katika siku chache ambapo Jones Masawe alikuwa kama mwenyehisa mkuu wa Mawenzi, Mama Masawe alifurahia kupendelewa na wanawake wengi matajiri. Hakutaka fahari hiyo ipotee na kurudi katika siku zile za dhiki baada ya kufirisika.......ITAENDELEA....


Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.