JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................698-699

Sura ya: 698

Mkutano huo wa wanahabari ulikuwa umerushwa moja kwa moja.
Watu kwenye mtandao walikuwa wanazungumza juu yake kama wazimu.

[Holy Sh*t! Pamela ana ujauzito wa miezi minne? Sikuweza kujua hata kidogo. Bado ni mrembo sana akiwa na mimba ya miezi minne.]

[Tafadhali, hilo si jambo la maana, sawa? Jambo ni kwamba Pamela hakuwahi kuilenga kampuni ya Jackson hata kidogo.]

[Je, uliona arifa ya dharura ambayo idara ya usimamizi imetoa sasa hivi? Kwa kweli kuna kitu kibaya na biskuti na keki za Jackson & Sons Company. Usizinunue siku zijazo.]

[Nilikuwa nikifanya kazi katika kampuni ya Jackson & Sons Company. Uhusiano wa Patrick na Linda ndivyo Pamela alivyouelezea. Wakati huo, ingawa kila mtu alijua kuwa anatoka na Pamela, lakini kila siku alikuwa akija kazini na kutoka kazini na Linda. Wageni wengi katika kampuni hawakuelewa kuwa wao ndio walikuwa kwenye uhusiano badala yake.]

[Si kwenda tu na kutoka kazini. Mara nyingi nilimwona Patrick akifanya shopping na Linda wakati huo. Nilikuwa tayari nimechanganyikiwa wakati huo. Nilikuwa nikijiuliza ikiwa Pamela kweli hakujali.]

[Nilikwenda chuo kikuu na Patrick na Pamela. Ninaweza kushuhudia kwamba Pamela alikuwa mzuri sana kwa Patrick. Alikuwa mtiifu kwake, lakini siku zote alikuwa akimjali. Siku moja, Pamela alipougua, nilimtazama akinywa dawa peke yake.]
[Katika siku ya kuzaliwa ya Patrick, Pamela aliwaita wanafunzi wengi wa zamani kusherehekea siku yake ya kuzaliwa pamoja, lakini hata hakutokea.]

[Hiyo si kitu. Patrick alipotakiwa kukutana na wazazi wa Pamela ili wazungumze kuhusu ndoa yao, badala yake alikimbia kukutana na Linda. Kama matokeo, aliwasimamisha wazazi wa Pamela na kuwafanya wasubiri masaa mawawili.]

[Holy sh*t, ni kweli? Yeye ni mpuuzi sana. Anaweza kushindana na Kelvin Mushi.]

[Kelvin ni mtu wa kudharauliwa asiye na maadili. Patrick ni fisadi aliyepoteza ujana wa Pamela.]

Lisa alimjibu Mwanamtandao mmoja: [Patrick hajawahi kutambua jinsi alivyo mtupu. Anafikiri kwamba Pamela hapaswi kujali kuwepo kwa Linda. Alichumbiana na Pamela kwa miaka mitano, lakini mtu ambaye alisafiri naye Pamela alikuwa ni mimi, mtu ambaye huwa anakula nae ni mimi, mtu ambaye alikuwa anatazama naye filamu ni mimi, niliyeenda naye shopping pia ni mimi. Hakuwahi kufanya chochote kwa Pamela. Aliongozana na Linda kwa kila kitu na bado angelalamika kuwa Pamela hakuwa mzuri. Hah. Je, anafikiri kwamba Pamela bado angekuwa na mapenzi ya zamani kwake? Katika ndoto zake!]

[MUNGU WANGU. Lisa alinijibu. Ninaota?]

[Lisa na Pamela ni marafiki wakubwa.]

[Hatimaye ninaelewa kwanini Pamela alimpuuza Linda. Ikiwa ningekuwa mimi, ningeweza kupata wehu. Ninahisi ghafla kuwa Pamela ana hasira nzuri.]

Alvin alimjibu Lisa: [Nakuunga mkono, babe. Ndiyo, Patrick Jackson si mzuri. Yeye ni takataka.]
Lisa alimjibu Alvin: [Hmph. Alimtumia Pamela kukata uhusiano nami, akisema kwamba niliwatia moyo waachane. Ikiwa ningeweza kufanya hivyo tena, nisingemtia moyo tu kuachana naye. Ningemkasirisha pia.]

Alvin akamjibu Lisa: [Ngoja nifanye hivyo. Usichoke mikono yako.]

Wanamtandao: [Aha, Bwana Kimaro anacheza kimapenzi na Bibi Jones tena.]

Kwa upande mwingine.
Katika Jackson & Sons Company.

Baba na mama ya Patrick walikimbilia jijini Nairobi mara tu walipopata habari juu ya mkutano wa waandishi wa habari na familia ya Shangwe.

Bwana Jackson alipomuona Patrick, kitu cha kwanza alichokifanya ni kumpiga kofi kali. “Mjinga wewe! Ulikuwa mjinga kiasi cha kuwa kibaraka wa wale vigogo wanaopigana dhidi ya Nathan Shangwe. Unafikiri wewe ni nani? Unathubutu kweli kwenda kinyume na familia ya Shangwe na Rais wa baadaye?! Umerukwa na akili?"

Kichwa cha Patrick kikaunguruma kutokana na kofi lile.
Hakuwahi kufikiria kuwa Pamela angekuwa mjamzito. Alikuwa mjamzito na kuolewa? Kwa sababu fulani, mara tu alipopata habari hiyo, akili yake ikawa tupu sana.

“Uncle...” Linda alikimbia na kusimama mbele ya Patrick. “Usimlaumu Patrick. Pamela kweli alilenga Jackson & Sons Company, lakini wao ni matajiri na wenye nguvu, kwa hivyo wanakataa kukubali. Jana katika kituo cha polisi, Jessica Shangwe pia alionya kwamba hataruhusu familia za Jackson na Shebi kusimama. Patrick alikata tamaa na hakuwa na chaguo.”

"Nyamaza! ” Bwana Jackson aliwahi kuwa na picha nzuri ya Linda. Baada ya yote, familia zao zilikuwa na uhusiano mzuri, lakini alipoona maoni kwenye mtandao, hakuweza kujizuia kumchukia sasa. Patrick na Pamela walikuwa karibu kufunga ndoa wakati huo, lakini waliachana kwa sababu yake.
Chini ya uongozi wa Forrest, Kampuni ya familia ya Masanja lilistawi na hata kuipita Jackson & Sons Company. Ikiwa sivyo kwa Linda, familia za Jackson na Masanja zingeunganishwa kwa ndoa. Sasa, kuhusu Jackson & Sons Company, kinachowangojea kinaweza kuwa mwisho wao.

“Uncle...” Mwili wa Linda ulitetemeka huku macho yake yakimtoka.

“Baba usimlaumu Linda. Ilikuwa chaguo langu,” Patrick alisema kwa unyonge.

Bw. Jackson alisema kwa hasira, “Wale vigogo walipanda ushahidi wa uongo dhidi ya Rais wa baadaye. Je, unafikiri familia ya Shangwe itaiacha tu? Jason Shangwe tayari alisema kwamba wataifuatilia hadi mwisho. Watu wanaoshindana dhidi ya Nathan Shangwe watajificha mara moja na kukusukuma nje kuwa mbuzi wa sadaka. Unafikiri kuna ugumu kwa wao kuiharibifu Jackson & Sons Company? Familia ya Shangwe ina kila sababu ya kusema kwamba wewe ndiye mpangaji mkuu. Umesababisha matatizo mengi kwa familia ya Shangwe wakati huu. Hawatakuacha kamwe.

"Nathan Shangwe atakutumia kama mfano kwa wengine na kuonya ulimwengu wa nje kwamba familia ya Shangwe si rahisi kuhangaika nayo. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuikasirisha familia ya Shangwe."

Mwili wa Patrick ukatetemeka.
Bibi Jackson naye alilia. “Mwanangu, wewe ni mpumbavu sana! Familia yetu inatakiwa kupiganaje na familia ya Shangwe?”

Mara tu maneno hayo yalipoanguka, kundi kubwa la maafisa wa polisi liliingia kutoka nje. "Samahani, tulipokea ripoti kutoka kwa familia ya Shangwe kwamba Patrick Jackson aliajiri watu mtandaoni kumpaka matope Waziri Shangwe na bintiye. Patrick Jackson, uko chini ya ulinzi.”
Afisa mmoja aliifunga mikono ya Patrick nyuma ya mgongo wake.

“Sikufanya hivyo!” Patrick aliingiwa na hofu kabisa.
“Unathubutu kusema kwamba si wewe uliyepakia video hiyo?”
Afisa huyo aliuliza kwa ukali, “Ni kwa sababu ulipakia video hiyo ndipo ulimwengu wa nje ulianza kufikiria kwamba Waziri Shangwe aliruhusu familia yake kuwanyanyasa wengine. Jambo hilo lilipozidi kuwa mbaya, ulikaa kimya na kuruhusu wanamtandao kukemea familia ya Shangwe, ambayo ni sawa na kukubaliana na maneno yao kimya kimya. Wakati huo huo, ulipata watu wa kueneza uvumi kwamba Pamela Masanja alilipiza kisasi kibinafsi dhidi ya Jackson & Sons Company. Anwani ya IP iliturudisha kwenye kampuni yako."

Sura ya: 699

Moyo wa Patrick ukasisimka. Alikiri kwamba alikubaliana kimyakimya na matusi ya wanamtandao, lakini hakuwahi kupata mtu wa kueneza uvumi.
Alimtazama Linda bila kujua.

Moyo wa Linda ulitetemeka. Alilia na kuwatazama polisi. “Hatukufanya hivyo. Hii ni tuhuma ya uwongo."

Afisa huyo alidhihaki, “Imetosha. Ni shtaka la uwongo la familia ya Shangwe kwamba kuna tatizo na bidhaa za Jackson & Sons Company, na ni shtaka la uwongo la polisi kwamba ulikashifu familia ya Shangwe...”

“Hilo silo alilomaanisha...” Patrick alieleza kwa haraka.

"Mwondoe." Maafisa wawili wakamtoa Patrick nje moja kwa moja.

“Patrick...” Bi. Jackson alilia kwa wasiwasi. “Tunapaswa kufanya nini sasa? Mpendwa, fikiria njia. Tunapaswa kumuokoa Patrick.”

Bwana Jackson alikunja ngumi. “Tunapaswa kumuokoa vipi? Nani atathubutu kuwaudhi familia ya Shangwe ili kumwokoa sasa? Linda, ulikuwa unafanya nini? Kwanini hukumzuia Patrick kufanya vile?”

Linda alipauka kwa hofu. Sio tu kwamba hakumzuia, lakini kwa kweli yeye ndiye alianzisha jambo hilo. Alikasirishwa tu kwamba Pamela alikua binti wa hiari wa Nathan. Alifikiri kwamba ikiwa sifa ya Nathan ingeharibiwa, Pamela pia asingekuwa na wakati mzuri.

"Tutaenda ... na kumsihi Pamela.” Baada ya muda mrefu, Bwana Jackson alishusha pumzi nzito.

“Basi... kwanini tusimuambie Linda akaombe msamaha?” Bibi Jackson aliuliza kwa kuhema.

“Kuna maana gani kumwambia aende? Ili akapige magoti na kubamiza kichwa chake chini? Au kung'ang'ania mkono wa Pamela na kukataa kuondoka?" Bwana Jackson alitupa mkono wake na kuondoka.

Bibi Jackson alimfuata. Baada ya wao kuondoka ofisini, alimwambia mumewe, “Umeenda mbali sana sasa hivi. Najua umemkasirikia Linda, lakini ikiwa Jackson & Sons Company itaanguka kweli, Patrick ataweza tu kutegemea familia ya Shebi.”

“Huelewi? Familia ya Shangwe haitaruhusu familia ya Jackson kunyanyuka, na pia hawatairuhusu familia ya Shebi Mbali na hilo ... Tutazungumza juu yake ikiwa Patrick ataachiliwa. Ninachohofia ni kwamba... familia ya Shangwe haitamwacha aende zake.” Bwana Jackson alihema sana.

Bibi Jackson aliganda.
•••
Katika makazi ya Shangwe.

Pamela alikuwa amemaliza chakula chake cha jioni kwenye meza kubwa ya duara wakati Jessica alipokea simu na kumwambia Nathan, "Ba mdogo, Patrick Jackson amekamatwa."
“Mh.” Nathan alikunja uso sana na kunywa chai. "Hali ikoje kwa familia ya Karama?"

"Waziri Karama anadaiwa kuwa ni mgonjwa na haonani wageni wowote. Amechukua likizo ya siku chache,” Jessica alisema kwa unyogovu, “nadhani atakuwa na tabia nzuri huku mkia wake ukiwekwa katikati ya miguu yake kwa sasa.”

"Ataweka mkia wake katikati ya miguu yake kwa muda mfupi na kisha kufufuka ili kunipa wakati mgumu tena?" Nathan alimtazama Ian. "Hapo awali nilifikiria kumwacha Waziri Karama afurahie maisha yake wakati wa kustaafu, lakini inaonekana hakuna haja ya hilo. Ondoa familia ya Karama kwenye nyadhifa zao zote ndani ya siku mbili. Wanaweza kutupwa kwenye vyeo vya chini.”

“Sawa.” Ian alitikisa kichwa kwa sura kali kwenye uso wake mzuri ambao Pamela hakuwahi kuuona hapo awali.

Pamela alipigwa na butwaa. Nathan daima alikuwa mkarimu mbele yake, kiasi kwamba alikuwa karibu kusahau kwamba hakuna mtu katika siasa ambaye angekuwa rahisi hivyo.

“Kuhusu Patrick...” Nathan alitabasamu na kumtazama Pamela. "Kwa kuwa alimuudhi bintiye mdogo wa familia yetu, mwache akae gerezani kwa muda."

Pamela akavuta pumzi ya baridi.

Ian alimtazama. "Kwa kuwa alithubutu kwenda kinyume na familia ya Shangwe, anapaswa kuwa tayari kwa mabaya zaidi. Mbali na hilo, ikiwa hatutamfundisha somo baya, watu wengine watajuaje kuitendea familia ya Shangwe kwa heshima?”

"Familia ya Shangwe daima ilikuwa na sifa nzuri, lakini ilikuwa karibu kuharibiwa na Patrick Jackson. ” Mzee Shangwe alitikisa kichwa kukubaliana na maneno ya Ian.
Midomo myekundu ya Pamela ilisogea, lakini mwishowe, hakujua la kusema.
Alimchukia sana Patrick, lakini si kiasi kwamba alitaka aoze gerezani maisha yake yote. Hata hivyo, alikuwa amemchukiza Rais wa baadaye, ambaye mamlaka yake hayangevumilia kuudhiwa.

"Lakini, Rodney," Wendy alisema ghafla, "Kwa kuwa umeoa sasa, unapaswa kuandamana na Pamela kwenda Dar es Salaam na kukutana na wazazi-wakwe wako. Nenda kesho.”

“Sawa. ” Rodney alitii na kumtazama Pamela. “Um... Alvin na Chester walisikia kwamba nimepata jiko na wakaniomba nijumuike no kwenye klabu jioni hii.”

“Mmh.” Pamela alicheka kwa kukiri. “Kama unataka kwenda we nenda tu.”

Ikiwa alitaka kwenda, basi aende tu. Kwanini alikuwa akimwambia hivi?
Rodney alijisikia vibaya kidogo na tabia yake ya kutojali. “Nakwambia tu endapo utafikiri nitamwona Sarah.”

“Ukithubutu kumuona Sarah tena, nitakuvunja miguu,” Jason alimuonya.

Miguu ya Rodney ilitetemeka huku akitabasamu. "Sina uhusiano naye tena."

Baada ya chakula cha jioni, Rodney aliendesha gari hadi ClubHouse.
Chester alifika kwanza na kukaa kwenye sofa peke yake. Alikuwa anacheza na sigara mdomoni mwake kwa mawazo.

“Unawaza nini? Umepoteza mawazo.” Rodney akaketi karibu naye.

“Alvin yuko wapi?”

“Anapaswa kuwa njiani. Nilipopiga simu saa moja iliyopita, alisema atakuja baada ya kucheza mpira wa kikapu na watoto wake. Anapaswa kuwa njiani sasa,” Chester alijibu kwa kawaida.
Rodney alikosa la kusema. “Kuna tatizo gani la kuwa na mwanamke na watoto? Lakini ... hehe. Nina mwanamke na mtoto pia sasa. Chester, wewe tu na Sam bado hamjaoa. Naam, bahati nzuri."

“Siwaonei wivu wale waliofunga ndoa,” Chester alisema kwa unyonge.

"Hiyo ni kweli. Afadhali ujinyonge juu ya mti,” Rodney alitania.

“Unaonekana kuwa na furaha sana kuhusu ndoa yako. Tulipokuomba umwoe Pamela hapo awali, ulifanya kama ungependa kufa." Chester alimtazama na kumpa tabasamu lisiloeleweka.

“Nina furaha?” Rodney alionekana kuchanganyikiwa. “Mimi nipo kawaida tu. ”

“Kawaida?”
Chester alikoroma.

Uso wa Rodney ulikuwa umejaa kiburi, lakini yeye mwenyewe hakuliona hilo. “Nahisi tu... unajua, watu lazima wafunge ndoa mapema au baadaye. Hata kama sitamuoa Pamela, mama yangu ataendelea kunipangia watu nisiowajua. Angalau Pamela amembeba mtoto wangu. Yeye ni mrembo na mwenye talanta. Familia yangu inampenda sana pia, kwa hivyo yeye ni mwenzi mzuri wa ndoa,” Rodney alikariri na kusema.

“Hongera sana. Lakini kama si tukio hili na Patrick, Pamela ungemsikia kwenye bomba tu.” Chester akatabasamu. "Umepata mwisho mzuri wa mzozo."

“Usiseme hivyo. Mimi pia si mbaya.”

Rodney alikuwa amemaliza kuzungumza mara mlango wa chumba hicho ulisukumwa. Alvin aliingia huku mikono yake ikiwa mfukoni. “Tunazungumza nini? Haraka na umalize. Nataka kwenda nyumbani kwa mke wangu na watoto wangu.”

“Hata huwezi kufanya hivyo. Kuna faida gani ya kuja?” Rodney alimvamia bila huruma.
Uso wa Alvin ulitiwa giza. "Rodney Shangwe, unataka kufa?"

Chester alitabasamu. "Ameoa leo, kwa hivyo mpongeze kidogo.

“Njoo, Rodney, furahia. Nakutakia usiku mwema wa harusi! ”

Rodney alijikaza. Chester alimnong’oneza kwa siri sikioni, “Mimba ya mwanamke hutulia baada ya miezi mitatu. Haijakuwa rahisi kwako. Ulifanya mara moja tu katika miaka 3o ya maisha yako, na haukufanya katika hali ya ufahamu pia. Je!... unataka nikufundishe mbinu chache?”

“Ondoka nje!” Rodney akaruka juu akiwa na uso mwekundu.

“Sisi sote ni wanaume hapa. Kunanini cha kuwa na aibu?" Chester hakujua acheke au alie.

Rodney alitaka kulia. “Unawaza sana. Kabla hatujafunga ndoa, Pamela alitia saini makubaliano nami. Siruhusiwi kumshika baada ya ndoa. Sisi ni wanandoa tu kwa jina."

Alvin alifurahi kwa msiba wake. "Hiyo ni nzuri."

“Ina uzuri gani? Mimi ni mwanamume wa kawaida—”


“Je, si umekuwa ukiishi hivi kwa muda wote? Usimguse tu.” Chester alitabasamu.

"Hapana. Sikuwa nimeoa hapo awali, lakini kwa kuwa sasa nimeoa, jambo la aina hii ni sawa. Kwanini siwezi kumgusa?” Rodney hakuweza kukubali hili. "Nisaidieni kufikiria njia."

“Hakuna cha kufikiria. Ni mjamzito sasa, hivyo huwezi kutumia nguvu kwani itamuumiza mtoto.” Chester alimpa maneno matatu, "vumilia."

Rodney, akaguna. Kwa hasira akapiga funda kubwa kutoka kwenye glasi yake.
Alvin naye taratibu akanywa glasi mbili hadi tatu. Hakuthubutu kunywa pombe kupita kiasi kwa kuogopa kulewa.....ITAENDELEA.....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA...