JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................570-571

Sura ya: 570

Mwishowe, Lisa alikubali hatima yake. Alikuwa amemvalisha kabla hata hivyo. Aliinamisha kichwa chini na kujilazimisha kumsaidia kuvaa nguo zake. Matendo yake hayakuwa ya upole, lakini pembe za mdomo wa Alvin bado ziliinua tabasamu la joto. Ilikuwa hasa alipoona uso wake mrembo ukiwa na haya ya kupendeza. Mwanzo alikuwa mke wake. Kwa nini hakumthamini? Kwanini alimwacha aende zake? Wakati Lisa alisimama kumsaidia kumvalisha shati lake, Alvin alishindwa kujizuia kumkumbatia.

Lisa alipogundua kinachoendelea, alipandwa na hasira. "Alvin, si ulisema mkono wako unauma sana?"

"Unauma sana. Huoni kwamba uso wangu umepauka kwa sababu ya maumivu?” Alvin alijibu kwa sauti ya unyonge. Ili kumkumbatia, misuli iliyojeruhiwa katika mkono wake wa kulia iliuma sana.

Lisa alipigwa na butwaa. Katika muda huo mfupi, Alvin alimbusu. Lisa alinyoosha mkono wake kumsukuma. Hata hivyo, shati lake lilikuwa bado halijakaa ipasavyo, hivyo mkono wake uligusa ngozi yake ya moto.
Aliutoa mkono wake kwa silika kutokana na joto.

Alvin alichukua nafasi hiyo na kumsukumia kwenye kitanda kilichokuwa nyuma yake. Macho ya Lisa yalikuwa mekundu kwa kumtazama.

“Alvin, haya ndiyo mapenzi uliyomaanisha? Unachojua ni kunionea tu. Ikiwa unanipenda kweli, nitendee heshima zaidi, na siyo kunifanya nijisikie mwenye hatia kwa mume wangu tena na tena. Unafanya hivi kila wakati. Ilikuwa vivyo hivyo kwenye kisiwa pia.”

Lisa alipokuwa akiongea, machozi yalitiririka. Alvin alipoona hivyo aliingiwa na hofu, na moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali. “Usilie. Sikuonei. Nataka kukubusu tu. Ikiwa hutaki nikubusu, basi sitafanya hivyo."

Kufikia mwisho wa sentensi yake, sauti yake ilisikika ya kukasirika na ya kusikitisha pia. Alikuwa kama mbwa asiyeweza kula chakula chake ingawa kimetengwa. Lisa alishika nafasi hiyo na kumsukumia mbali. Alijiweka mbali naye na hakuthubutu kumkaribia tena.
Alvin alikaa na kufunga vishikizovya shati kwa mkono wake mmoja kwa upole.
Lisa hakutaka tena kuchezewa naye, akageuka na kutoka nje.

Hata hivyo, alipoketi mbele ya meza ya ofisi na kuwasha kompyuta yake ya mkononi, hakuweza kuelewa kilichomo katika ripoti aliyokuwa akiisoma.
Pumzi za Alvin zilikuwa bado kwenye midomo yake, na kumfanya ajisikie amebebwa na minyororo mizito mgongoni. Lakini, ilikuwa ukweli usiopingika kwamba alifurahia busu la Alvin. Kinyume chake, angejisikia vibaya sana wakati wowote Kelvin alipokuwa karibu naye. Moyo wake ulianza kuzama taratibu huku akiendelea kuwaza.

Muda si mrefu Alvin akatoka nje. Lisa alijifanya kana kwamba anafanya kazi kwa umakini na akamchunia kama hajamuona. Hiyo ni kwa sababu aligundua kuwa mara Alvin alipofungua mdomo wake, alihisi kana kwamba alikuwa na ulimi wa ulimbo. Maneno yake yalimfanya awe katika hali ya sintofahamu mara kwa mara.

Wakati kidonge cha kuzuia mimba ambacho alikiona juzi tu usiku kilipowekwa mbele yake, maumivu yalizuka moyoni mwake kutokana na hasira. “Alvin unapanga kuja kila siku kunilazimisha kula hiki kitu? Umesahau kuwa nilikula jana usiku? Kuzidisha sio salama kwa mwili."

Mkono wa Alvin ukakakamaa. Baada ya muda mrefu, alisema kwa hisia tofauti, “Nani anajua kama Kelvin atakugusa usiku wa leo…”

Lisa akafunga laptop yake. Alikaa kimya kwa muda wa nusu dakika kabla ya kusaga meno yake na kusema, “Lengo lako si nisipate tu mimba ya mtoto wa Kelvin? Hutakiwi kunipa tena hizo dawa za uzazi kwa sababu tayari nina mtoto wake.”

Mwili wa Alvin ulitetemeka. Alisema kwa tabasamu, "Lisa, usinidanganye."

"Sisemi uwongo." Lisa alisimama ghafla na kusema kwa dhamira, “Mimi na Kelvin tuna mtoto ambaye ana zaidi kidogo ya miaka miwili. Wakati Kelvin alipokuwa nami huko Marekani wakati huo, nilipata mtoto huyo baada ya kuwa naye mapenzi chini ya ushawishi wa pombe.”

Hakutaka kuendelea kuchanganyikiwa katika uhusiano huo wa ajabu na Alvin tena. Ingawa usiku wa jana ulimfanya atambue kwamba huenda bado ana hisia fulani kwa Alvin, asingeweza tena kumkosea Kelvin.

Alvin alimtazama kwa butwaa. Taratibu, uso wake mzuri ulianza kuwa mbaya. Mikono yake iliyokuwa imetulia kwenye mapaja yake, taratibu ikakunja ngumi. Hata hivyo, midomo yake myembamba ilikuwa bado inatabasamu kwa ukaidi.

“Lisa, unafikiri ninakuamini? Ulisema una mtoto. Yuko wapi huyo mtoto?”

"Nilitaka kukutongoza na kulipiza kisasi kwako baada ya kurudi, kwa hivyo sikutaka kuwa karibu na mtoto wangu." Lisa alisisitiza midomo yake kwa hisia tofauti.

Kwa kweli, tayari alikuwa amefikiria kisingizio hicho mara tu aliporudi kutoka Marekani. Kwanza, kisingizio hicho kingeweza kuficha utambulisho wa Lucas kwa kawaida. Pili, ingeweza kama kisasi cha kumuumiza Alvin. Kwa bahati mbaya, alipitia mambo mengi na kughairi kutumia kisingizio hicho. Pia alikata tamaa na mawazo ya kulipiza kisasi kwa Alvin. Sababu ya kutumia kisingizio hicho tena muda ho si kutaka kulipiza kisasi kwake bali kumfanya aachane naye kabisa.

“Siamini.” Alvin akatikisa kichwa. Hata kama moyo wake ulijawa na uchungu na woga mwingi, bado alikataa kwa ukaidi. “Tayari una mtoto wa Kelvin, lakini ulikuja kunitongoza na hata uliwahi kufanya mapenzi nami hapo awali. Je, Kelvin atakubali hilo?”

"Hawezi kukubaliana na mipango yangu kwa sababu kuzaliwa kwa mtoto huyo ilikuwa ajali." Lisa akageuza macho yake. Hakutaka kutazama macho yake ambayo yalikuwa karibu kupoteza udhibiti. “Hapo awali, nilitaka kusubiri hadi wewe pia uanguke kwa undani katika upendo na mimi, kisha kukuambia kuhusu mtoto. Ilikuwa ni aina ya kulipiza kisasi kwako pia. Hata hivyo, niliachana na wazo la kulipiza kisasi kwako baadaye. Kwa kweli, unajua kuhusu hili pia. Mtoto amekuwa kando yangu wakati wote, analelewa nyumbani kwaa baba yangu. Unaweza kuchagua kutokuamini, lakini utaamini baada ya kuona sura ya mtoto.”

Mvulana ambaye Alvin alimwona katika shule ya awali aliangaza akilini mwake ghafla. Alvin alipokutana na mvulana huyo kwa mara ya kwanza, alifikiri kwamba mvulana huyo anafanana sana na Lisa. Hata hivyo, aligundua baada ya hapo kijana huyo alionekana kuwa mtoto wa mpwa wa Joel. Je, inaweza kuwa… mtoto alikuwa kweli… wa Lisa?

“Mtoto huyo… anasoma katika shule ya awali… kama Suzie, sivyo?” Koo lake lilijitahidi kusema sentensi hiyo.

Lisa alifunua kwa makusudi uso wa mshangao. "Ulijuaje?"

Alvin alihisi kana kwamba akili yake imemlipuka, na moyo wake ukavunjika.
Alifikiri jambo lililomsumbua zaidi ni kujua kwamba aliolewa na mwanamume mwingine. Hata hivyo, ikawa kwamba yeye na Kelvin walikuwa na mtoto ambaye alikuwa na umri wa zaidi ya miaka miwili.

“Hapana, niambie hii si kweli. Unanidanganya.” Alvin alikimbia kama mwendawazimu. Akamshika Lisa mabega na kumtingisha kwa nguvu. Machozi ya uchungu yalimtoka. “Hata kama ulimzaa huyo mtoto lazima ni mtoto wetu sivyo? Najua sasa. Lazima umenidanganya miaka mitatu iliyopita. Kwa kweli watoto wetu hawakuondoka, na huyo mtoto ni wangu.”

Moyo wa Lisa ulitetemeka kwa sauti ya Alvin. Kumuona mwanamume huyo mbele yake akilia kwa namna isiyoelezeka kuligusa moyo wake.

Baada ya muda mrefu, alicheka kwa nguvu. “Umesahau kuwa watoto wetu walitoweka kwa sababu yako? Bado unakumbuka nilipoteza damu kiasi gani siku hiyo?"

Sura ya: 571

Alvin alipigwa na butwaa. Mikono yake ilikuwa ikitetemeka, lakini mwili wake ulihisi kana kwamba umebanwa mahali pake. Hiyo ilikuwa sawa. Alikuwa akisema nini? Watoto wake walikuwa wamekwenda miaka mitatu iliyopita. Alipoteza nafasi. Hakujua jinsi ya kutunza vitu wakati huo. Ndio maana alizaa mtoto na mwanaume mwingine.
Mito miwili ya machozi ilitiririka kutoka kwenye kona za macho yake. Katika maisha haya, Alvin hatimaye aliweza kuhisi kuvunjika moyo na kupoteza matumaini. Hatimaye alikuwa amepata tumaini dogo, kwa ajili yake tu kulivunja kikatili tena.


Lisa alishuhudia mwanga machoni mwake ukitoweka. Aliinamisha kichwa chake taratibu pia.
“Na iwe, Alvin. Tafadhali usije kunitafuta tena. Tusivuke njia tena.”

Aliogopa kwamba ikiwa wangeendelea kujihusisha na maisha ya kila mmoja, angeingia katika hali ambayo kila mtu atamdharau. Kwa wakati huo hakutaka kumuumiza Kelvin. Kwa hiyo angeweza tu kuchagua kumuumiza Alvin.

Mwishowe, Alvin aliondoka. Alitoka nje ya ofisi yake. Hata hakumuaga.
Lisa alisimama mbele ya madirisha akitazama nje bila wazo lolote.
Kisha, Ambah akaingia. “Mwenyekiti Jones, Bwana Kimaro ameondoka. Alionekana kama ana msiba wakati anaondoka ... "

Ambah alikuwa na shauku kubwa ya kujua ni nini Lisa alifanya kumtesa Alvin katika hali hiyo. Ilikuwa ni kama Alvin amepoteza sehemu ya nafsi yake.
“Mm! Unaweza kuendelea na kazi yako,” Lisa alisema kwa huzuni.

•••
Alvin aliendesha gari moja kwa moja hadi kwenye lango la shule ya awali.
Ilikuwa ni mapumziko ya chakula cha mchana, kwa hiyo mlinzi hakumruhusu aingie.

Alisimama chini ya jua kali hadi Hans alipompigia simu. “Bwana Mkubwa, uko wapi? Si ulisema utamtembelea Mwenyekiti wa Garson Inc. saa tisa alasiri?”

“Hans, niambie. Miaka mitatu iliyopita mliwahonga madaktari hospitalini? Lisa hakutoka mimba hata kidogo, sawa?” Sauti ya Alvin ya kupotea kwenye mawazo ilisikika.

Hans aliposikia maneno ya Alvin kwa upande mwingine upande wa simu, ni kana kwamba bomu lililipuka kwenye ubongo wake. Baada ya muda mrefu, aligugumia, “Bwana Mkubwa, vipi… Uligunduaje?”

Alvin, ambaye alikuwa akihangaika kwa uchungu na huzuni, alinyamaza.
Hans alijiuliza sana akili mwake. Amesikia nini? Je, alikuwa akiona maono?

Japokuwa Alvin alipitia misukosuko mingi hapo awali, bado alikuwa ameduwaa kwa wakati huo, kiasi kwamba alisahau hata kuzungumza.
Hata hivyo, hakujua kwamba ukimya wake ulimfanya Hans azidi kufadhaika.

“Bwana Mkubwa, samahani. Sikufanya makusudi.”

“Kwahiyo Lucas ni mtoto wangu?” Akili ya Alvin ikamzunguka, na haraka akarusha bomu.

Kujua kwamba Alvin alikuwa amejua kuhusu Lucas kulimfanya Hans kuwa na wasiwasi zaidi. Alichoweza kufanya ni kuomba msamaha. “Bwana Mkubwa, samahani. Unaweza kumuuliza Bibi Jones kuhusu jambo hili. Hii ni kati ya nyinyi wawili. Nimemuahidi Bibi Jones kutomwambia mtu yeyote.”
Kutoka kwa sauti ya Hans, Alvin tayari alikuwa na uhakika wa asilimia 80. Alimfahamu sana Hans. Ikiwa haikuwa ukweli, Hans angekataa mara moja.
Ilionekana kuwa mvulana kutoka shule ya awali ambaye alionekana kama Lisa labda alikuwa mtoto wake.
Sasa hivi, Lisa alimwambia mvulana huyo alikuwa mtoto wa Kelvin na Lisa.
Ilimfanya apate ajali njiani. Alikuwa na uchungu mkubwa kiasi cha kutaka kuligonga gari hilo na kufa.
Hakutarajia Lisa angemdanganya.

Subiri. Alikumbuka Lisa alikuwa amebeba mapacha enzi hizo, kwahiyo ikitokea Lucas alikuwa kweli ni mtoto wake… Kwa ghafla, Alvin alimfikiria Suzie. Mwanzoni, alifikiri kwamba Suzie alikuwa ameshikamana sana na Lisa kwa sababu Suzie alikuwa amefiwa na mama yake na Lisa alimtunza sana. Hata hivyo… Vipi kuhusu Lisa? Ilionekana kana kwamba alimtendea Suzie vizuri sana.

Kama ingekuwa hapo awali, Alvin asingeshuku chochote kwa sababu alikuwa na uhakika kwamba mapacha hao walikuwa wametoweka. Lakini, akifikiria nyuma sasa, watoto wote wawili walikuwa katika shule moja ya awali, na walikuwa na uhusiano mzuri. Zaidi ya hayo, Jack alihusika katika kudanganya kifo cha Lisa wakati huo. Labda Jack alijua tangu mwanzo kwamba watoto wa Lisa walikuwa bado hai. Kwa hiyo, Suzie alikuwa binti wa Alvin? Wazo hilo lilipomjia kichwani, Alvin alihisi kana kwamba ubongo wake umemlipuka. Alikuwa akiwaza hadi mwili wake wote ukatetemeka.

"Hans, bosi wako ni nani haswa?" Alvin aliuma meno na kuonya kwa ukali, “Hebu nikuulize. Je, Suzie ni binti yangu au wa Jack?”

Hans hakujua jinsi ya kujibu. Kwa kweli, alikuwa na wasiwasi na alishangaa katika kasi ya ghafla katika kuamka kwa akili ya Alvin, ambayo ilikuwa imelazwa kwa miaka mitatu.

Alvin alicheka. "Hata usiposema, si nitafanya mtihani wa DNA mwenyewe?"

Kichwa cha Hans kilimuuma. Alijua mara tu kipimo cha DNA kingefanyika, asingeweza tena kumficha chochote Alvin. Kwa hivyo, hakuwa na lingine ila kusema, “Bwana Mkubwa, Bi Jones kweli alizaa watoto hao, lakini hawana uhusiano na wewe. Umechangia manii yako tu.”

Tangu Hans afanye kazi kwa Alvin, hii ilikuwa mara moja na pekee ambayo alithubutu kutoa jibu la kutomheshimu Alvin.
Hata hivyo, Alvin hakumlaumu Hans hata kidogo. Macho yake hata yakawa mekundu kihisia. Yeye, Alvin Kimaro, alikuwa na watoto kweli. Ilikuwa ni jozi ya mapacha ndugu pia.

Mbingu zinajua jinsi Alvin alivyokuwa na wivu aliposikia kwa mara ya kwanza kwamba Suzie ni binti wa Jack. Hata hivyo, hakutarajia kwamba Suzie alikuwa binti yake. Haishangazi yeye, ambaye hapo awali hakupenda watoto, angefikiria kuwa Suzie alikuwa mzuri sana.

“Hans, niambie. Nataka kujua ukweli,” Alvin alisema kwa furaha.

Hans alipigwa na butwaa. “Ikiwa bado hujui ukweli, ulipataje kujua kwamba watoto hao wawili walikuwa bado hai?”

“Hakuna haja ya wewe kujua hilo.” Sauti ya Alvin inayotetemeka ilikosa subira. "Hans, nakuomba."

Kwa mara ya kwanza, yeye, kama bosi, alikuwa akimwomba Hans, mtumishi wake, kwa dhati. Ilimpa Hans mshtuko mkubwa.

“Bwana Mkubwa usiseme maneno hayo. Kwa kweli, kudanganya mimba kuharibika lilikuwa pendekezo la Miss Jones. Ilikuwa ni kwa sababu wakati ule, ulisisitiza kukabidhi watoto kwa Sarah ili awalee mara tu wanapozaliwa. Wakati huo, sikuamini kwamba Sarah angewatendea watoto vizuri hata kidogo. Niliogopa watoto wangeishia kunyanyasika na tabia ya Sarah. Hiyo ndiyo sababu nilikubali ombi la Miss Jones.
Lakini, sikuweza kufanya peke yangu. Ndiyo maana Bwana Mkubwa wa pili pia aliingia.”
Hans alipumua huku akisema, “Kwa kweli, mtu unayepaswa kumshukuru ni Bwana Mkubwa wa pili, Jack. Ni yeye aliyempeleka Miss Jones ng'ambo na kuajiri madaktari bora kuwaokoa watoto. Hujui hili, lakini hali ya watoto ilikuwa mbaya sana kwa sababu Miss Jones alilazimika kutumia dawa nyingi za antipsychotic wakati huo. Bi Jones alilazimika kukaa hospitalini kwa miezi michache baada ya kuwasili ng'ambo. Watoto walizaliwa kabla ya wakati pia. Walinusurika baada ya kukaa kwenye incubator kwa miezi miwili.”......ITAENDELEA.....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA..