JINA LA SIMULIZI............................LISA

AUTHOR...........................JOMBA WAJO

SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY

WHATSAPP...........................0628924768

SEHEMU YA................................544-545


Sura ya: 544


Saa kumi na mbili jioni, Pamela hatimaye alifanikiwa kupata mchanganyo sahihi wa bidhaa yake kwenye maabara. Mara akasikia sauti ya Rodney masikioni mwake.


“Bado hujatoka kazini?” Mkono wa Pamela ulitetemeka. Alimtazama Rodney kana kwamba ameona mzimu. “Mimi ndiye napaswa kukuuliza hivyo. Mpaka sasa hujaenda  kumtafuta Sarah?”


"Unamaanisha nini?" Rodney alikuwa kama nungu. Nyusi zake zikawa zimenyooka.

"Kweli, kwa kawaida ungekuwa umeenda hata kabla ya saa kumi na moja jioni Kama bosi, wewe huwa wa mwisho kuingia .na wa kwanza kuondoka.

 Kila mtu katika kampuni anajua kwamba huwa unamfuata  Sarah mara tu unapotoka kazini.” Pamela alivua miwani yake na kusema ukweli.


Uso wa Rodney ukasisimka kwa mshangao kutokana na kusikiliza maneno yake.

 Hata hivyo, hakuweza kumkanusha hata kidogo. Baada ya yote, huo ulikuwa ukweli.

 "Je! watu wengi  wanazungumza juu yake katika kampuni?" hakuweza kujizuia kuuliza.


“Si kweli. Nani anathubutu kulizungumzia? Wewe ndiye bosi.” Pamela aliuliza kwa udadisi, “Si unaelekea kwake sasa? Ninachojua, labda anakuhitaji sana sasa hivi.”


Rodney alihisi kuchomwa kisu tena. Hakuweza kujizuia kuwa na huzuni. Hivi Saraha angeweza kumhitaji kweli? Hakuweza hata kupata wakili mzuri. Pia, alikuwa na bilioni moja tu mikononi mwake, ambazo hata angemkopesha Sarah zisingetosha kulipa deni… Sara alitaka kukopa pesa kutoka kwake, lakini hakuweza kumpa kiasi kilichohitajika. Kisha akamwambia aondoke. Alihisi kama anadharau hali yake mbaya ya kifedha. Kama mwanamume, alitaka kulinda kiburi chake pia.


Pamela alishtuka. "Vipi, Sarah amekubali kutoa pesa za Alvin, au yupo tayari kupambana naye mahakamani?”


“Hapana, alisema pesa zote ameziweka kwenye akaunti ya muda maalumu, hataweza kuzitoa kwa sasa hata kama atazihitaji vipi. Alitaka nimkopeshe pesa, lakini kwa sasa sina bilioni kumi za kumkopesha. Hivyo nadhani suluhu itakuwa mahakamani.” Rodney alijibu kwa utulivu.


Pamela alifikiria. Angeweza kukisia kwamba Rodney alikuwa akihisi wasiwasi kwa sababu ya Sarah. "Ningekuwa mimi ndiyo Sarah, ningerudisha pesa zote kwa Alvin na kubakisha bilioni moja tu. Bilioni ni zaidi ya kutosha ikiwa unataka kuishi maisha ya anasa.

 Jumba la kifahari tayari analo, tena siyo moja. Magari anayo, zaidi ya yote, bado ana taaluma kubwa tu ambayo inaweza kumwingizia mamilioni ya pesa. Hana dhiki. Anaweza hata kuwa na ndege ya kibinafsi. Yote haya bado yanawezekana. Ni asilimia kumi tu ya watu ulimwenguni kote wanaweza kufanya kile nilichotaja sasa hivi. Asilimia iliyobaki ya watu bado wanafanya kazi kwa bidii ili kupata riziki. Sarah ana moyo wa kutotosheka tu na usio na shukrani.”


Rodney alimtazama akiwa ametoa macho na kumshangaa. Moyo wake ulijihisi kupona ajabu.

 Ingawa maneno ya mwanamke huyo kila mara yalimkera, wakati mwingine yalimfariji pia.

 "Lakini wanawake huwa na matumaini ya kuwa na pesa zaidi, sawa?" Alisema kwa huzuni.


“Kupata zaidi ni sawa, lakini iwe ni kwa kufanya kazi au kwa kipato halali, siyo kwa ujanja ujanja wa kulaghai wengine.”


Rodney alifikiri ilikuwa na maana alipokuwa akisikiliza. Hata hivyo, Sara hakufikiri hivyo. Ingependeza sana kama Sarah angekuwa kama Pamela ...

Baada ya mawazo hayo kupita kichwani mwa Rodney, alishtuka. Jamani, alikuwa anafikiria nini?


Huku akiwa ameduwaa, Pamela alikuwa tayari ameshavua koti lake la maabara na kufunga kila kitu. "Bwana Shangwe, nitnaondoka sasa."


“Haya, ngoja. Naenda kwako kuangalia mfanyakazi niliyekupangia.” Rodney alimfuata ghafla.


Pamela alipigwa na butwaa. Uso wa Rodney ulionyesha kuwa alikuwa na wasiwasi. "Sikumwambia mfanyakazi wa nyumbani aandae chakula cha jioni usiku wa leo. Nilimwambia Sasha tutaenda kula mgahawani.”


Rodney alitaka kusema. Pamela alijua alichotaka kusema, kwa hivyo alisema haraka, "Najua kuwa chakula cha nje sio safi na sio nzuri kwa mtoto, lakini nataka sana kuwa na kachumbari leo. Sikuwa hivi hapo awali, kwa hiyo lazima ni mtoto ambaye anataka kula.”

"Unajua tu jinsi ya kusukuma lawama kwa mtoto." Rodney alisema kwa hasira, “Nilishakwambia kachumbari inayotolewa huko migahawani siyo nzuri sana. Viungo vingi havioshwi vizuri … Sahau. Ukitaka kula kachumbari, twende nyumbani nitakutengenezea.”


Pamela alipigwa na butwaa. “Ah?”


“Unamaanisha nini unaposema ‘Ah’? Unafikiri siwezi kufanya? Au unashangaa kwanini napenda kupikapika?" Rodney alilalamika.


Pamela akaangaza macho. Ghafla, aligundua hobby ya Rodney. Ilionekana alipenda sana mapishi.


Mwishowe, Rodney alimpeleka Pamela kwenye duka kubwa la vyakula wakanunua mapochopocho ya kutosha. Pamela hakuweza kupinga kuchukua picha ya Rodney kwa siri akichagua mapochopocho hayo. Walipokuwa wakitoka kwenye duka, akaitumaa kwa Lisa.


Pamela: [Mwangalie Rodney anachagua mapochopocho dukani Je, mtu tajiri na wa kujisikia kama yeye anaweza kweli kufanya hivi kwa ajili yangu? Macho yangu yanakaribia kutoka kwenye soketi zake.]


Lisa: [Ah, Sarah hastahili kuolewa na yeye. Ni bahati mbaya.]


Pamela: [Ni bahati mbaya sana. Ninahisi kama amekatishwa tamaa kidogo na Sarah sasa. Zaidi ya hayo… ninashuku kwamba Sarah hampendi kwa kuwa hajampa pesa ya kumlipa Alvin.]


Lisa: [??? Naam, bilioni 10? Bora ameshtuka mapema. Asiwe mjinga kama Alvin.]


Pamela alicheka alipoona ujumbe huo.

 Mara akasikia sauti ya mwanaume akimkaripia.


Lisa:  [Pamela… Kuwa mwangalifu. ..]


Kabla hajajibu ujumbe wa Lisa, gari ndogo ikafunga breki mbele yake ghafla. Moyo wake ulienda kasi kwa hofu. Ikiwa Rodney asingemvuta, angegongwa na gari hilo. Angeweza hata kuharibu mimba yake. Alitaza mapembeni na kuona sura ya huzuni ya Rodney.


“Pamela, unaweza kuwa makini zaidi? Tayari una mimba, bado unacheza na simu yako unapotembea. Kwa kweli sijui utaniambia nini ukiharibu mimba ya mtoto wangu kwa uzembe wako.” Rodney alimkemea Pamela kwa hasira.


Alipoona Rodney amekasirishwa na kuhuzunishwa kwa sababu yake, moyo wake uliruka kwa hofu. Hakuwa akifikiria kwamba Rodney alimjali sana mtoto wake aliyekuwemo tumboni. Kwa kweli, haku…chukia kuwepo kwa mtoto kama vile alivyofikiri. Kwa hiyo kama alimpenda mtoto, inawezekana pia ange… angemdondokea mama yake siku moja?


Hata hivyo, Pamela alipata mshtuko fulani baada ya Rodney kumvuta ghafla kukwepa lile gari.

 “Rodney, ninasikia maumivu…” Pamela alikunja uso ghafla na kulalamika.


Rodney akawa na wasiwasi mara moja. “Wapi… wapi kwenye maumivu? Tumbo lako?" Aligusa tumbo lake kwa hofu. “Kuna damu huko chini…”


"Hapana, ni mkono wako kwenye bega langu ndio unaumiza." Pamela akauma meno yake na kumkumbusha kwa uso uliojaa haya huku akimtazama mtu mzima aliyejiinamia mbele yake na kugusa tumbo lake kwa woga.


“… Oh.” Hapo ndipo Rodney akakumbuka kuwa alikuwa amemshika bega kwa nguvu. Haraka alijiachia, na sauti yake ilikasirika. “Mbona hukusema kuwa ni mkono? Niliogopa hata kufa.”


Pamela alimpa macho ya kando yaliyochanganyikiwa. “Kunanini cha kuogopa? Kama mimba itatoka, unaweza kupata mtoto na  Sarah, sawa?"

“Huyo mtoto pia ni kiumbe wa Mungu. Sio lazima useme kana kwamba ni jambo dogo na kunifanya nionekane kama sina maana, mtu asiye na moyo," Rodney alinong'ona.


Pamela alidhihaki. "Je, si mara nyingi umekuwa mkaidi na usiye na moyo? Moyoni mwako, maadamu Sarah na watu walio kando yake wana furaha, hujali mema au mabaya hata kidogo.”


"Huwezi kuacha yaliyopita?" Rodney alisema. Alianza kuhisi maumivu ya kichwa.


Sura ya: 545


Baada ya kuingia kwenye gari, Rodney akatoa pakiti ya chips za viazi kwenye mfuko wa shopping na kumpa Pamela. "Hii ni kwa ajili yako."


Pamela akamtolea macho. "Si ulisema hautaniruhusu kula chakula cha mitaani?"


Rodney alisema kwa sauti iliyokusudiwa kumfurahisha, “Ninakupa hii kama msamaha kwa makosa niliyokufanyia siku za nyuma.”


Tayari Pamela alikuwa kishalainika kwa kuitazama tu sura yake tata. Sasa kwa kuwa Rodney alikuwa anajaribu kumbembeleza, alizidi kuufanya moyo wake kupondekapondeka na kutepeta kabisa. Baada ya Pamela kupigwa na butwaa kwa sekunde chache, hatimaye alielewa ni kwanini wasichana wengi walivutiwa vijana mashuhuri wa kiume. Ilikuwa ni faida kwa mtu kuwa na sura nzuri.

Akihema chinichini, Pamela alichukua mfuko wa chips viazi na kuufungua. "Maumivu yote uliyonisababishia yamechorwa moyoni mwangu. Nitakubali msamaha wako nitakaposikia Thomas yupo jela.”


“Thomas tayari ni mlemavu. Sio kama hujui kuhusu hilo,” Rodney alinong’ona.


“Wewe ndiye uliyemlemaza?”


"Ingawa sio mimi niliyefanya hivyo, nilikuwa kwenye eneo la tukio."


"Sipati picha ulipokuwa kwenye eneo la tukio, itakuwa lazima ulisema, 'Haya, kwa kweli, hakuna haja ya kuwa mkatili sana. Baada ya yote, yeye ni kaka ya Sara. Hii haifai sana’…” Pamela alisema huku akiiga sauti yake.


Rodney hakuwa na neno. Mwanamke huyo aliwezaje kusoma mawazo yake? Ndivyo hivyo alivyosema kweli! Aliona aibu sana.


Pamela alimpuuza na kujikita katika kula chips zake. Hata hivyo, uso wa Rodney uliwaka moto kwa sababu hiyo. Alijisikia hatia.


Walipofika nyumbani kwa Pamela, mfanyakazi wa nyumbani aliyeletwa hapo na Rodney, Sophia, aliwasalimu na kuwapokea mizigo. Rodney  akaelekea moja kwa moja jikoni kuanza kuandaa madikodiko.


 “Bwana Mdogo Shangwe, niruhusu nifanye hivyo—” Sophia aliona aibu na kutaka kumsaidisa Rodney.


“Hakuna haja. Hujui jinsi ya kutengeneza kachumbari, nitafanya mwenyewe.” Rodney alikunja mikono yake, akavaa apron na kuingia mzigoni.


Muda mfupi baadaye, harufu kali ya maungi ilitoka jikoni. Pamela alikuwa akiitamani sana hivi kwamba mate yalimjaa mdomoni.

Sophia aliingia jikoni kutazama na kutoka nje. Alitabasamu na kusema, “Bi. Pamela, una bahati sana. Bwana Shangwe ni mjuzi sana wa kupika. Ah, sijui hata jinsi alivyokatakata na kuunga hiyo kachumbari. Nyanya, kabichi, vitunguu na karoti, limao vimeoshwa na kukatwakatwa vizuri. Wanaume wanaojua kupika ni wachache sasa.”


Pamela alihisi uchungu alipokuwa akisikiliza. Alihisi hakuwa na bahati kabisa kwa sababu Rodney alimpenda Sarah tu. Kwa kweli, mtu yeyote ambaye Rodney alimpenda angefurahi sana. Alikuwa mtu mwenye nia moja. Ikiwa alimpenda mtu, angemtendea mtu huyo vizuri. Angeweza pia kumtendea mtoto wake vizuri katika siku zijazo pia. Mtoto bado alikuwa tumboni mwa Pamela, hata hivyo Rodney alikuwa tayari anaogopa mtoto asingekuwa na afya njema kutokana na kula chakula kisicho na ubora.


Pamela alikuwa na maisha magumu ya mahusiano. Hapo zamani, Patrick aliibiwa kutoka kwake na yule b*tch, Linda. Wakati huu, aliishia kulala na Rodney bila kutegemea nakupata ujauzito siku hiyohiyo. Tatizo Rodney hakuvutiwa hata na uzuri wake.

 Siku hizi, uzuri wa asili haufai chochote. Wanaume wanaonekana kuvutiwa na wanawake wenye uzuri wa kutengenezwa maabara.



Saa moja usiku, Pamela na Rodney walikula mlo safi ulioandaliwa na Rodney kwa pamoja.

 Kachumbari ilikuwa ya kufurahisha tu ikiwa ilisindikiza chakula kitamu. Rodney walifanya hivyo.

 Rodney aliandaa pilau nyama ng’ombe la hatari, ambalo hata Pamela asingeweza kumudu. Ilikuwa ni kilo moja ya mchele na kilo moja ya nyama, lakini watatu wale walikomba kila kitu kutokana na chakula kunoga.


“Ni ajabu. Huogopi kunenepa?” Rodney alimtazama Pamela. Alikuwa tofauti na Sarah, ambaye aliogopa kunenepa bila kujali anakula nini.


Sara hakuweza kula vitu vingi. Kusema kweli Rodney hakuwahi kufurahia kula chakula pamoja na Sarah.

 Alikuwa akidokoadokoa tu chakula kwa mashauzi na kukiacha.


"Samahani, lakini sitanenepa hata nikila kiasi gani." Pamela alijiinamia kivivu kutokana na shibe.


Uso wake mdogo ulikuwa na jasho kutokana na kula kachumbari yenye pilipili kali. Mdomo wake mdogo pia ulikuwa umevimba kidogo kana kwamba kuna mtu amembusu.


Rodney pia alihisi wimbi la joto likiongezeka kutoka sehemu ya chini ya tumbo lake. Kwa sababu fulani, alikumbuka mambo kadhaa kutoka usiku ambao alifanya mapenzi na Pamela. Mwanamke huyu alikuwa kama shujaa. Kiuno chake kilikuwa chembamba, mapenzi yalizidi kupita kiasi, na alikuwa mkali sana. Ahem...

 Jamani. Alikuwa anafikiria nini? Akageuza uso wake pembeni. Alifarijika sana.  Japo alikuwa katika hali ya nusu-fahamu, kwa kweli siku hiyo alifurahia sana. Akili yake ilichafuka baada ya kuwaza hayo.

 


Baada ya kumaliza kula, ilikuwa tayari saa tatu usiku. Pamela alienda bafuni kuoga. Sebuleni hapo chini Rodney alikuwa bado anapiga soga na Sophia kuhusu lishe ya Pamela.


“Sophia, hutakiwi kumruhusu kula vyakula visivyofaa. Ikiwa hatasikia, unaweza kunipigia simu mara moja. ”


Baada ya Pamela kutoka kuoga, Rodney alikuwa tayari ameondoka. Sophia alimpatia simu. “Bi. Pamela, Bw. Shangwe alisahau simu yake hapa.”


“Nipe. Nitamkabidhi kwenye kampuni kesho.”


Pamela alipanda na simu hiyo juu ghorofani kulala. Haukupita muda mrefu, simu ya Rodney ikaita. Sarah ndiye aliyepiga simu.

 Midomo myekundu ya Pamela ilitabasamu. Akapokea simu.

Sauti ya Sarah akilia ilisikika. “Rodney, uko wapi? Nimeku’miss sana… Samahani, mtazamo wangu kwako ulikuwa.

 mbaya leo. Sikufanya makusudi… nilikasirika tu…”


Pamela alisikiliza kilio chake cha kusikitisha. Aliuliza kimoyomoyo. Si ajabu Sarah aliweza kuwapumbaza kabisa wanaume wale wawili. Kama ilivyotazamiwa, Sara alikuwa na njia zake. “Samahani, Bi Njau. Rodney ameondoka. Alisahau simu yake nyumbani kwangu.”


Kila sentensi yake alitamka baada ya kutafakari kwa kina.

 Mara Sarah alilipuka kwa hasira. “Pamela?”


"Ah, sikutarajia utaitambua sauti yangu." Pamela alicheka na mkono wake juu ya mdomo wake.


"Kwa nini Rodney awe nyumbani kwako mpaka saa hizi? Ulimtongoza?” Sarah alipiga kelele.


“Unamaanisha nini kusema nilimtongoza? Yeye ni mchumba wangu. Mimi ndo natakiwa nikuulize hilo. Unafikiria nini kwa kumpigia simu mchumba wangu usiku sana na kusema umem’miss?” Pamela alipaza sauti na kusema, "Je, unajaribu kuwa hawara tena?"


“Hawara wa nani? Rodney na mimi tulikuwa tunapendana tangu mwanzo.” Sarah alikasirika. "Rodney ataishia tu kufanya tu uchumba na wewe, hatakuoa."


"Inawezaje? Ahadi hii ilitolewa na wazazi wetu baada ya kukutana. Ni halali. Mbali na hilo…” Pamela ghafla alifunika mdomo wake na kutoa sauti ya kutapika. “Samahani. Sijisikii vizuri kwa sababu ya kichefuchefu baada ya kupata ujauzito. Tafadhali usijali.”


“Wewe… una mimba?” Sarah alipigwa na butwaa. Ni kana kwamba shoti ya umeme ilimpitia ghafla. "Ni ya Rodney?"


"Nani mwingine? Kaka yako mpenzi ndiye aliyefanikisha hili.” Pamela alilalamika kwa makusudi, “Rodney hakukuambia? Anamtaka sana mtoto huyu.”


“Haiwezekani. ” Sarah alifadhaika kabisa. Hakuweza kutulia. "Rodney hakupendi hata kidogo."


"Lakini anampenda mtoto. Hata aliniandalia chakula sasa hivi.” Pamela alicheka. "Ujuzi wake wa upishi ni mzuri sana. Nafikiri… ninakaribia kumpenda. Sitaki kukuacha uwe na mwanaume mzuri hivyo.”


“Pamela, ngoja tu. Hata ukiwa mjamzito, haina maana,” Sarah alifoka na kukata simu.......ITAENDELEA.....


Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA..