JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................542-543
Sura ya: 542
Alvin alimpeleka Suzie kwa KIM International. Baada ya kujua kuwa Suzie yuko hapo, Lea alipanga kumchukua mjukuu wake ana kwa ana ili kucheza naye.
Kabla Lea hajaondoka, aliuliza, “Ilikuwaje kwa kuomba bilioni 10 kutoka kwa Sarah?”
"Hapanga kuirejesha," Alvin akajibu.
Lea alikoroma kwa hasira. “Nilikuambia kwa muda mrefu kuwa huyu mwanamke si mtu mzuri, lakini ulikataa kunisikiliza na hata kumpa bilioni 10 bila mimi kujua. Wewe ni mkarimu kiasi gani?”
“Wewe je? Si ulimpa Mason pesa nyingi pia? Kwa kuwa ninyi mmekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka 20, huenda mlimpa zaidi ya bilioni 100.” Alvin aliinua uso wake. “Bila shaka, mimi ni mwanao wa kuzaa. Nimekurithi.”
Akiwa ameumizwa na kauli za Alvin za dhihaka, Lea alikosa la kusema.
Kimsingi alikuwa amejipiga risasi mguuni.
"By the way, unajua ni mtu gani aliyenunua nyumba ya zamani ya familia ya Kimaro?" Alvin aliuliza ghafla.
"Sina uhakika. Hakuonyesha sura yake hata kidogo.” Lea aliuliza huku akiwa amekunja uso, “Kwa nini unauliza hivi?”
“Hakuna kitu. ” Alvin akatikisa kichwa. Kisha akamtazama Lea akiushika mkono wa Suzie huku akimnyanyua juu juu.
Simu iliyokuwa mezani kwake ilitetemeka tena, ikionyesha namba ngeni. Aliitikia wito na sauti ya Sarah ikasikika. "Alvin, kwanini uliblock namba yangu?"
"Kwa hiyo utanirudishia pesa?" Alvin aliuliza bila kujali.
"Hapana, Alvinic. Umenielewa vibaya. Sijawahi kufikiria kukuumiza—” Alvin alikata simu kabla Sarah hajamalizia sentensi yake.
Sarah alikasirika sana hivi kwamba alipiga kelele kama mwanamke mwendawazimu. Rodney aliingia ghafla na kutokea kuliona tukio hili. Alipata mshtuko kwani aliona upande huu wa Sarah kuwa wa ajabu.
"Rodney, nini kinakuleta hapa?" Sarah naye alishtuka. Hakutarajia mlinzi angemruhusu aingie bila yeye kujua. Harakaharaka alitoa machozi machache na kujifanya kana kwamba amevunjika moyo. “Nilimpigia simu Alvinic sasa hivi na akanikasirikia. Amekuwa wa ajabu na wa kutisha sana. Ingawa sisi si marafiki tena baada ya kuachana, hatuhitaji kuwa maadui.”
"Alvin amebadilika." Rodney aliona ni kwanini alishindwa kujizuia na kutikisa kichwa. "Nilienda kumtafuta na akanipuuza pia."
Akivumilia hali yake ya kutokuwa na uwezo, Sarah aliuliza kwa msukumo, “Umemtafuta Chester?”
"Chester hataki kuingilia kati." Rodney alimtazama na kusema, “Chester pia anafikiri kwamba unapaswa kurudisha takriban bilioni 8 kwa Alvin. Kwa kweli, hata ukibaki na bilioni 2 ni nyingi. Watu wengi hawawezi kupata milioni 100 tu hata kama hawatakula au kunywa maisha yao yote.”
Chester hakuwa ametoa maoni kama hayo. Hata hivyo, Rodney alikuwa na aibu sana kumwambia Sarah moja kwa moja. Kwa hiyo, alijaribu kumshawishi kwa kutumia jina la Chester.
“Nimesema kwamba siwezi kutoa pesa nyingi kwa sasa kwa sababu niliziweka kwenye fixed account. Kwanini usinikopeshe kwanza? Nitakurudishia baadaye.” Akiwa na mawazo, Sarah alisema kwa huzuni.
Rodney alipigwa na butwaa. “Kama ningekuwa na kiasi hiki cha pesa, bila shaka ningekukopesha. Lakini nina bilioni chache tu mkononi.”
Familia ya Shangwe ilikuwa imezuia kadi zake za pesa za familia ili kumzuia kuwa na Sarah. Kwa hivyo, angeweza tu kutegemea Osher Corporation sasa. Hata hivyo, pia alifhitaji pesa taslimu, ikizingatiwa kuwa kutangaza bidhaa mpya ya Osher kungehitaji pesa nyingi pia.
Rodney alimshawishi, akisema, “Sarah, lazima uniamini. Ninaweza kupata pesa nyingi katika siku zijazo. Ninaweza kukupa bilioni 20…”
“Inatosha. Acha tu.” Akiwa katika kilio chake, Sara alisimama kwa unyonge. "Alvin aliniacha ghafla, kwa hivyo nimepoteza imani katika uhusiano. Nataka tu kushikilia kile nilichonacho sasa. Isitoshe, ni nini kinampa Alvin haki ya kunitendea hivi? Sifurahii jambo hilo.”
Akiwa amehuzunika, Rodney alishusha macho yake. “Natamani nikusaidie pia. Nimewauliza wanasheria wengi kuhusu hilo. Kwa walichokisema, hutaweza kushinda kesi hii…”
“Naomba uondoke sasa. Nataka kutumia muda peke yangu.” Sarah aligeuka bila kuwa na wasiwasi juu yake.
Rodney alikasirika sana. Alimtazama kwa muda kabla ya kuondoka. Alikata tamaa sana. Alijiuliza Sarah alikataa kurudisha pesa kwa sababu ya kutoridhishwa na jinsi Alvin alivyomtendea au kwa sababu anashindwa kuvumilia kuziachia zile pesa? Alimkuta Sarah wa sasa wa ajabu sana.
Mtu anaweza kupenda pesa lakini si vyema kuwa na tamaa kupindukia. Zaidi ya hayo, Rodney alikuwa akizunguka huku na huko kila siku ili kumtafutia Sarah wakili. Alikuwa amechoka sana hata hakufika ofisini kwa siku kadhaa. Hata hivyo, Sarah hakuweza kuelewa nia yake.
Mwishowe, Rodney aliendesha gari hadi Osher Corporation. Alipofika huko, alimwona mfanyakazi wa kike akitoka nje ya lifti kwa kasi akiwa na pakiti mbili za pilipili za ‘jalapeno’ mikononi mwake.
"Je! wewe sio msaidizi wa Pamela?" Jina lake lilikuwa kwenye ncha ya ulimi wa Rodney. Alikuwa amekutana naye mara chache katika mikutano iliyopita.
"Sasha," mfanyakazi wa kike alisema, "Mkurugenzi Pamela aliniagiza nikamnunulie."
“Unamaanisha hizi…?” Rodney alielekezea pilipili za jalapeno mikononi mwake na uso wake mzuri ukaganda.
"Ndio ... Kwani haziruhusiwi katika kampuni?" Msahangao wake ulimtisha Sasha.
Bila shaka, kampuni yao haikuweka sheria yoyote kuhusu chakula. Baada ya kusema hivyo, je, angeweza kula pilipili kali namna ile ikizingatiwa kwamba alikuwa mwanamke mjamzito? Subiri! Rodney aligundua kitu kingine.
"Mkurugenzi Pamela bado yuko kazini?"
“Bila shaka. Si wakati wa kupumzika hata…” Sasha aligundua kuwa uso wake ulikuwa na hasira, lakini hakuwa na uhakika kama alifanya kitu kibaya.
“Niachie hizi. Nitampelekea. Yuko wapi?” Rodney alinyakua zile pakiti za pilipili.
"Katika maabara."
Rodney alipiga hatua kuelekea kwenye maabara iliyokuwa nyuma yake.
Alipoingia ndani, alimuona Pamela akichanganya madawa kutengeneza vipodozi akiwa ameinamisha kichwa chini. Alikuwa amevaa koti jeupe na miwani. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumuona hivi. Ingawa wote wawili walikuwa wakifanya kazi katika kampuni moja, hakuwahi kufika kwenye maabara. Pia, hakuwa kumtembelea alipokuwa akifanya kazi.
Pamela alisikia nyayo, kwa hivyo alifikiria ni Sasha aliyerudi. Alinyoosha mkono wake tu kuelekea kwenye nyayo huku macho yake yakiwa bize kutazama matokeo ya kazi yake.
Rodney aliutazama mkono wake mzuri na msafi. Baada ya hapo, alielekeza macho yake kwenye uso wake mzito. Alipigwa na butwaa. Baada ya muda wa kusitasita, hatimaye aliweka mkono wake kwenye kiganja chake. Pamela aliubana mkono ambao ulikuwa mkubwa zaidi kuliko wake. Aligeuka ghafla, na kumuona Rodney akiwa ameduwaa. Kisha akautupia macho mkono mkubwa wa mwanaume huyo uliokuwa umemshika.
Macho yake nyuma ya miwani yalidhihirisha sura iliyochanganyikiwa. Baada ya hapo, alikasirika na kuuvuta mkono wake. "Rodney Shangwe, umerukwa na akili? Kwanini unanibinya mkono wangu?”
“Wewe ndiye ulininyoshea mkono wako na mimi nikakushika.” Akiwa ameudhishwa na kukaripiwa kwake, Rodney alijibu kwa ukali, “Kwa nini unapiga kelele? Kwani nimekosea kukushika?”
“Wewe ni mbwa?” Pamela alikosoa, "Ni mbwa tu ndiye atakayeweka makucha yake kwenye mkono wa mmiliki wake."
"Rudia tena kunitukana kama una ujasiri." Uso mzuri wa Rodney ulijaa hasira. “Mimi ni bosi wako. Je, hivi ndivyo unapaswa kuongea na bosi wako? Zaidi ya hayo, ni nani aliyekuomba uninyoshee mkono wako ovyo ovyo?”
“Nilikuwa nanyoosha mkono wangu kwako? Nilifikiri Sasha alirkuwa ameleta pilipili za jalapeno.”
Wakati wa kutajwa kwa pilipili hizo, Rodney alikoroma bila huruma. "Nilizitupa."
Sura ya: 543
"Rodney Shangwe ..." Pamela alikasirika sana hivi kwamba alimtazama Rodney kwa macho yake angavu. "Wewe ni nani hata kutupa pilipili zangu?"
“Mimi ni nani?” Rodney aliitikia kana kwamba anasikia mzaha. Akainamisha kichwa na kulitazama tumbo lake. “Kwa sababu tu una mimba ya mtoto wangu. Ninahitaji kuwa na wasiwasi juu ya lishe ya mtoto wangu. Siwezi kukuacha umwangamize mtoto wangu kwa vyakula vya ovyo ovyo.”
Pamela alisugua kichwa chake. Kwa vile mdomo wake ulikuwa umetulia kwa sasa, alitaka kula kitu kilichotiwa pilipili ili kuamsha hamu yake.
Hata hivyo, Rodney alikuwa ameharibu mipango yake. Kwanini alimkera hasa?
“Mbali na hilo…” Rodney aliendelea, “Kwa kuwa una mimba, kwa nini bado unafanya kazi katika maabara? Nenda nyumbani ukalale.”
"Lala, mwenyewe." Pamela alikosa la kusema. “Nina ujauzito wa mwezi mmoja tu, lakini tayari unanizuia kuja kazini. Unataka kunichosha hadi kufa na kunifanya niteseke na unyogovu, huh?”
“Acha kuutupa mkono unaokulisha. Ninafanya hivi kwa faida yako mwenyewe.” Rodney alijibu kwa ukali, “Wanawake wengi hubaki tu nyumbani na kulea watoto wao baada ya kuwa wajawazito. Mtoto wetu ameandikiwa kuishi maisha ya anasa katika siku zijazo. Familia ya Shangwe haina uhaba wa pesa. Unaweza kuishi maisha ya anasa za maisha milele bila kufanya kazi kwa bidii.”
Mtoto wetu? Mara tu Pamela aliposikia maneno hayo kutoka kinywani mwake, alishangaa sana. Hakuwahi kufikiria kwamba angeshea mtoto na Rodney siku moja. Kwa hayo, hisia zake zikawa ngumu ghafla.
"Mbona ghafla umenyamaza?" Rodney alishtuka kumuona akimwangalia.
Pamela alipumua. "Rodney Shangwe, hata bila familia yako, ninaweza kuwategemea wazazi wangu na kuishi kwa raha maisha yangu yote.
Lakini, siwezi kujibwetesha tu namna hiyo. Ninapaswa kuishi maisha yenye matokeo. Kwangu, kuwa na uwezo wa kutengeneza bidhaa za vipodozi ambazo zinaweza kuwafanya wanawake kuwa warembo na kuchelewesha mchakato wao wa kuzeeka ndio hunifanya nihisi kuridhika.
Ninapoingia kwenye maduka na kuona bidhaa ambazo nilitengeneza zikiuzwa, nitajivunia na kuridhika, ninajisikia furaha ambayo hakuna mtu mwingine anayeweza kunipa.”
“Kwa hiyo…” Rodney alipigwa na butwaa.
“Kwa hiyo nitaendelea na kazi ingawa nina ujauzito. Haitaniathiri katika kulea mtoto kwa sababu ninafanya kitu ninachofurahia. Wakati huohuo, nitamlinda mtoto.”
Baada ya kumsukuma, Pamela alivaa glovu na kuchukua bomba la majaribio. Kisha, alitumia pamba na kuichovya kwenye kioevu kilichokuwa ndani ya bomba. Baadaye, aliweka pamba karibu na ncha ya pua ili kuinusa.
Rodney alijitenga huku akimtazama. Ghafla akapiga kelele, “Pamela Masanja, umejipodoa wakati una mimba, unataka kumharibu mtoto?" Pamela, ambaye alifadhaika kwa mara nyingine tena, alishindwa kujizuia. “Je, wewe ni kipofu? Nimeweka wapi make-up?”
“Naam… Macho yako.” Akimnyooshea kidole, Rodney alisema, “Ona, umeweka hata kope bandia na mascara…” Alikumbuka kuwa uso wa Sarah haukuwa wa kupendeza hivyo isipokuwa angejipodoa.
“Hivi ndivyo ninavyoonekana kiasili, sawa? Sijajipaka kiipodozi chochote.” Pamela alijibu kwa unyonge huku akiuma mdomo.
“Siamini." Rodney alikunja uso. “Usijaribu kunidanganya.”
"Angalia mwenyewe, basi." Pamela akaondoa miwani na kumtazama bila kupepesa macho.
Rodney hakuwa na la kufanya zaidi ya kujiinamia ili kumtazama kwa karibu. Baada ya kugusa kope zake ndefu, aligundua kuwa hakukuwa na chochote juu yake. Zaidi ya hayo, alifurahi kuona kope zake zikipepea kama kipepeo alipozigusa. Hakuweza kujizuia kugusa kope zake mara chache zaidi. Sura yake ilionekana katika macho angavu ya Pamela, ambayo yalifanana na kioo.
Kwa namna fulani, alijisikia vibaya.
Alikasirika, akidhani kwamba lazima amerukwa na akili.
Pamela alikosa la kusema na pia aliona aibu kidogo.
Ilikuwa ni kwa sababu Rodney, mwanaume ambaye ambaye kwa namna fulani alimchukiza, alikuwa karibu naye sana wakati huo. Uso wake wa kuvutia bila shaka ungeweza kuwashinda vijana wengi, lakini, moyoni mwake alihisi kero fulani kuuona.
Haishangazi Roney na wenzake walikuwa maarufu sana. Hakika sura zao zilikuwa karamu kwa macho. Rodney alifurahia kuvaa nguo za kujionyesha hasa. Kwa jinsi alivyokuwa amevalia, mtu asingeweza kusema kwamba tayari alikuwa na umri wa miaka 30.
“Ahem, kweli hukujipodoa. Sahau. Bado nina mambo mengi ya kushughulikia. Unaweza kurudi kazini, lakini usimchoshe mtoto wangu.”
Rodney alikunja kiganja kama kikombe na kukinga mdomo wake kukohoa. Alirudisha nyuma macho yake ya aibu na kutoka nje.
Pamela alimtazama kwa nyuma. Alihitimisha kwamba alikuja tu kugombana naye.
Kurudi ofisini, Rodney alikuwa akipitia taarifa ya mapato ya mwezi huo. Upande wa pili wa meza, sekretari mwanamke alikuwa akiripoti hali ya jumla ya mapato ya kila ofisi za mikoani. Sekretari wa kike alikuwa na umri wa miaka 30. Alivaa suti ya vipande viwili.
Rodney aliinua kichwa chake na kumpungia kwa kidole chake. "Njoo hapa, karibu."
Sekretari akasonga mbele bila kuwa na wasiwasi wowote. Baada ya yote, kila mtu alijua kwamba isipokuwa kwa Sara, wanawake wengine hawakuwa kitu machoni pake. Hawakuwa na wasiwasi juu ya yeye kumfanyia chochote cha kushangaza, japo ingetokea angefurahia sana.
“Macho yako… Umejipodoa, sivyo?” Ghafla, Rodney akakunja uso wake.
Sekretari alijibu kwa woga. "Ni kawaida kwa mwanamke kujipodoa. ”
“Kwa hiyo kuna tofauti kati ya wanawake? Mbona wanawake wengine huwa hawajipodoi na bado wanaonekana warembo?” Rodney hakuweza kujizuia kugugumia.
"Unazungumza juu ya Mkurugenzi Pamela?" Sekretari aliingia kichwani kwa Rodney moja kwa moja, akatabasamu na kusema, “Uso mzuri wa Mkurugenzi Pamela unaonekana kama mtu wa rangi mchanganyiko. Yeye ni mrembo hata bila vipodozi. Atakuwa na mchanganyiko wa makabila
"Yeye ni maarufu sana, huh? Mbona umeweza kugundua mara moja hilo?" Rodney aliinua macho yake kwa udadisi.
“Ndiyo, wafanyakazi wengi wa kiume katika kampuni humchukulia kama mungu wao wa kike. Wengi wao wanataka kumfuatilia pia,” sekretari wa kike alisema huku akitabasamu.
Rodley akavuta tai yake. Macho yake yakamtoka huku akiwa na sura ya hatari. "Kampuni yetu hairuhusu mahusiano ya mapenzi kazini, sivyo?"
Katibu wa kike alichanganyikiwa. "Kuna sheria kama hiyo?"
“Kunayo. Na kama haipo ndiyo naiweka sasa. Mapenzi kazini huathiri ufanisi wa kazi. Nitamfukuza mtu yeyote anayejihusisha na mapenzi kazini.” Rodney alisema kwa ukalii.
Je, Pamela alikuwa anafikiria kuanzisha mahusiano na wanaume wengine huku akiwa amembeba mtoto wake? Katika ndoto zake!.........ITAENDELEA......
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA..
