JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................532-533

Sura ya: 532 

Sarah alikuwa katili kupita kiasi. Alikuwa ni mtu mbovu kiasi kwamba Alvin alitaka kujipiga risasi. Je, Rodney alikuwa kipofu? Hakuwezaje kuona jinsi alivyokuwa btch? "Rodney, utaharibiwa na mwanamke huyu mapema au baadaye," Alvin alisema kwa meno ya kusaga.

“Alvin, imekuwaje ukawa hivi? Ni sawa ikiwa humtaki, lakini pia hutaki niwe naye?” Rodney alikunja uso sana. “Sarah, ninapochora mstari, na hili likitokea tena, nitaita polisi. Haijalishi tulikuwa marafiki, nitaacha kila kitu kitatatuliwe kwa mujibu wa sheria.”

“Sawa.” Alvin aliitikia kwa kichwa, karibu kufa kwa hasira. “Sitazungumza na wewe upuuzi. Sarah Njau, nataka tu kukuambia kwamba ndani ya siku mbili, nirudishie pesa zote nilizowahi kukupa, pamoja na pesa zote nilizotumia kwa ajili yako katika siku hizi tatu. Ikiwa hauko tayari, nitakutumia barua ya wakili."

Sarah alisema kwa uchungu, "Alvin, wewe bado ni Alvin ninayemjua?"

Rodney alikasirika. “Alvin Kimaro, huna aibu sana. Una ujasiri wa kudai ulichotoa?"

"Kwanini isiwe hivyo? Sikuwahi kumgusa, lakini nilimpa bilioni 10, jumba hili la kifahari na kuifadhili New Era Advertisings kwa miaka mitatu. Nilimuacha aishi maisha ya juu. Hah, miaka hii, ni afadhali nitoe sadaka pesa zote hizo kuliko kumpa yeye.” Alvin alifoka na kuingia kwenye gari na Hans, na kuondoka.

Sarah alikua na wasiwasi. “Rodney, imekuwaje Alvin ghafla akawa hivi? Nilichukua pesa zote hizo na kuziwekeza. Sikuwahi kufikiria kwamba angetaka kurudishwa.”

"Sikuwahi kufikiria kuwa Alvin hakuwa na aibu pia." Rodney alimpigapiga begani asijue la kusema. "Ikiwa kweli anakata rufaa na kwa ushawishi wake wa kisheria, ni nani awezaye kumpinga?"

Rangi zilitoka kwenye uso wa Sarah. Kumtaka arudishe pesa zote ilikuwa sawa na kuomba maisha yake. Bila pesa hizo, angewezaje kuishi maisha ya anasa wakati ujao? Wanawake matajiri wa Nairobi wasingeweza kumpenda tena.

"Lakini mara ya mwisho, alienda kortini na Lisa na akapoteza ..."

“Hiyo ni kwa sababu hakubishana. Kwa ufasaha wake mahakamani, anaweza kufpinga mtu aliyekufa aonekane yu hai.” Rodney alifikiri juu yake na kusema, 'Nitajadiliana na Chester na kumwacha amshawishi Alvin. Ikindikana, itabidi tu na umrudishe kwa mali isiyohamishika. Nitavunja urafiki wetu kutoka kwake katika siku zijazo. Zaidi… tutakata uhusiano naye.” Rodney alihisi kwamba Alvin wa sasa alikuwa amemkatisha tamaa sana.

Sarah alitaka kutapika damu. Mali isiyohamishika ilikuwa na thamani ya makumi ya mabilioni. Mwishowe, ni Rodney tu ambaye hakuwa na maana sana kwa sababu alishindwa kumsaidia.

Alvin aliporudi kwenye kampuni, mara moja aliwasilisha hati ya mashtaka.
Chester alienda KIM International mchana huo. Alimtazama Alvin kwa sura nzito.

"Alvin, umepungukiwa na pesa sasa? Ungeweza kuniambia. Mimi ni ndugu yako. Nitakukopesha kadri niwezavyo.”

Alvin akatikisa kichwa. "Kwa jinsi KIM International ilivyo sasa, haiwezi kuboreka mara moja kwa kuwekeza pesa ndani yake. Sitaki tu kumpa Sarah pesa. Hafai. Mwanamke mwovu kama yeye hastahili kabisa kuishi katika ulimwengu huu.”

Alvin alipozungumza, yake yalionyesha uadui dhahiri.
Ilikuwa ni karaha na chuki ambayo Chester hakuwahi kuona hapo awali. Alishindwa kuelewa kwanini Alvin alimchukia sana Sarah ghafla. Je, ni kwa sababu ya kesi ya utekaji nyara na Logan hapo awali? Alikuwa na mashaka yake tu, kwani hakukuwa na ushahidi mwingine wa kuthibitisha kwamba Sarah alikuwa nyuma yake.

“Nini hasa kilitokea?” Chester aliuliza.

"Utaniamini kama ningesema?" Alvin alitabasamu kwa kejeli. "Rodney anamwamini. Haniamini hata kidogo.”

Uso mzuri wa Chester ulijikunja kidogo. " Niambie. Rodney anampenda Sarah kupita kiasi. Linapokuja suala la mihemko, kuna baadhi ya mambo ambayo hayawezi kuchambuliwa kwa utulivu.”

"Je, mimi pia sikuwa hivyo?" Alvin alifoka na kuunyooshea ubongo wake mwenyewe. “Miaka mitatu iliyopita, Sarah alinilaza usingizini alipokuwa akinitibu. Nilimuuliza Profesa Aurelius ambaye alinishughulikia nilipokuwa hospitali ya vichaa nikiwa mdogo.

"Kuna mbinu ya kizamani ya hypnosis katika Ugiriki wa kale ambayo inaweza kuharibu hisia za mtu kama roboti. Kisha, unaweza kuprogamu kile unachotaka mtu ahisi, afanye na kufikiri, na kukiweka ndani ya mtu ili kumbadilisha. Sasa, unaelewa kwanini ghafla nilibadiika na kumchukia Lisa. Unajua ni kwanini niilitaka kumpa talaka na kuwa na Sarah miaka mitatu iliyopita? ”

Chester alipigwa na butwaa kidogo. “Unawaza kupita kiasi? Kama ingekuwa kweli, si ungeielewa hapo awali?”

"Ndio, hicho ndicho cha kutisha juu ya mbinu hii ya hypnosis. Ni sawa na mtu aliyelishwa limbwata. Kwani huwa anajitambua? Si ulisema niliwahi kula huko Coco Beach na Lisa? nikamvunja miguu Bwana mdogo Kelly na wengine kwa ajili yake? Hayo yote nilikuwa nimeyasahau kabisa. Nilianza kuhisi kuna kitu hakipo sawa, kwa hivyo nilikwenda Dar kuchunguza. Nilimpata Sam na yaya ambaye alinipikia huko Dar.

“Walichokijua na kuona kilikuwa tofauti kabisa na kumbukumbu nilizokuwa nazo akilini mwangu. Kumbukumbu zangu zilikuwa zimejaa makosa ya Lisa, na kumbukumbu hizo zilinifanya nimchukie. Nilifikiri kwamba alinikaribia kwa sababu hakuwa na maana na alitamani hadhi yangu!

"Mtazamo wangu juu yake katika kichwa changu ulikuwa wa mwanamke mkatili sana, na hakuna kumbukumbu kwamba niliwahi kumpenda." Alvin alitabasamu kwa huzuni. “Chester, najijua mwenyewe. Ikiwa nilimpenda hapo awali, hata kama simpendi tena, nisingewahi kumfanyia ukatili kiasi hicho mwanamke ambaye ana mimba ya watoto wangu. Wakati huo, akili yangu ilikuwa na upendo kwa Sarah tu. Alinifanyia mengi sana, kwa hiyo nililazimika kuwa naye.

“Lakini katika miaka mitatu iliyopita, kila nilipojaribu kumshika, nilihisi kichefuchefu na kutapika. Alidanganya ubongo wangu, lakini mwili wangu ulimpinga bila kujua. Sikuwa na tatizo lolote nilipomgusa Lisa.”

Chester hakuweza kuufunga ubongo wake kwa kile alichokuwa anasikia. Kama daktari, ilikuwa mara ya kwanza kusikia juu ya kitu kama hiki. "Je, inaweza kuwa bahati mbaya? Au labda ilifanywa na wengine."

"Hapana, ilibidi awe yeye. Hakuna hata moja kati ya hisia zangu nilizozipata zilizopotea kuhusu Sarah, na nilianza kumpenda ghafla. Baada ya hisia zangu kubadilika, Sarah pekee ndiye aliyenufaika nami.

“Zaidi ya hayo, Profesa Aurelius alisema kwamba mtu aliyefanya hivyo lazima awe ni mtu niliyemwamini kabisa, vinginevyo asingefanikiwa! Kiwango cha mafanikio pia kilikuwa cha chini sana. Kama ingeshindikana, ningekuwa zezeta.” Alvin alitabasamu kwa uchungu. “Siyo hivyo tu. Haiwezekani kutibika kwa sababu kiwango cha mafanikio ya matibabu ni cha chini zaidi. Ni 0.01% tu.
Ikishindikana, mimi pia nitakuwa zezeta.”

Usowa Chester ulikuwa na mgongano na wa kukata tamaa. Haikuwa ajabu Rodney hakumwamini Alvin. Ilikuwa haiaminiki kabisa.

Hans hakuweza kujizuia kusema, “Bwana Choka, Bwana Mkubwa yuko sahihi. Kwa kweli, Bi Jones na mimi niliona miaka mitatu iliyopita kwamba kuna kitu hakikuwa sawa kwa Bwana Mkubwa. Tuliuliza wanasaikolojia wakuu na madaktari na wote walisema kitu kimoja, kama alivyoeleza hapa Bwana Mkubwa, kwa hivyo tukaacha kujaribu kumtibu. Hatukutarajia kwamba angevunja uchawi ghafla yeye mwenyewe sasa."

“Chester, wewe na Rodney hamkuwa nami wakati wote tofauti na Hans na Lisa, ambao waliishi chini ya paa moja na mimi kila siku.
Labda ndio maana hamkugundua.” Alvin alisema kwa unyonge, "Zaidi ya hayo, nimekuwa na Sarah kwa zaidi ya miaka kumi, kwa hivyo ni kawaida kwamba nyinyi watu mnadhani sijamsahau, lakini fikiria, je, niliwahi kusahau kumbukumbu kuhusu Rodney na wewe?"

Sura ya: 533

Chester alishtushwa na utambuzi huu. Hakika, walipokutana wote watatu, Alvin bado aliwakumbuka marafiki zake wa zamani. Alichanganyikiwa tu alipokuja kwa Lisa.

"Ikiwa unachosema ni kweli, basi Sarah ... ni mbaya sana." Chester akatetemeka. Alikuwa ameona wanawake wengi wenye mawazo finyu, lakini hakuwahi kuona mtu mzuri katika kudanganya kama Sara.

"Hapana, yeye sio mbaya tu. Yeye ni mkatili.” Alvin alicheka. "Profesa Aurelius alisema kuwa hakuna mtu aliyethubutu kujaribu hypnosis hii kwa sababu ya kiwango cha kutofaulu na pia kwa sababu haikuwa ya kibinadamu, lakini aliitumia kwangu. Alisema kwamba ananipenda, lakini bado alifanya hivyo licha ya kujua kwamba ningekuwa zezeta ikiwa itashindikana.”

“Basi, unafikiri… ataitumia pia kwa Rodney?” Chester aliuliza kwa kusitasita.


“Anahitaji hata kujisumbua? Si wazi kwamba Rodney kishajiroga mwenyewe?" Alvin alisema kwa sauti nzito, "Zamani, nilikuwa nadhani ni vizuri kwa Sarah na Rodney kuwa pamoja. Baada ya yote, Rodney anampenda. Lakini Sara si mwanamke mzuri. Hampendi Rodney. Anachopenda ni asili ya familia ya Shangwe. Yeye si mtu ambaye ameridhika na mali yake mwenyewe.

“Unakumbuka kuhusu Hisan Gadaffi?” Alvin aliinua uso wake. “Sarah amejaa uongo. Nilimwamini wakati huo aliposema kwamba alilazimishwa na Hisan, lakini simwamini sasa. Ukiniuliza, labda alilala na Hisan kwa hiari. Alisema aliangukia mikononi mwa watekaji nyara alipotoweka kwa miaka mingi, lakini siamini.”

Chester alimsubiri kimya kimya aendelee.

“Fikiria jambo hilo. Wakati huo, miili ya wanafunzi wenzake na marafiki zake ilipatikana, lakini maiti yake haikupatikana. Tulimwamini hapo awali, kwa hiyo tulisadikishwa na lolote alilosema. Nini ikiwa alikuwa amejaa uwongo?" Alvin alikisia kichwa, " Alisema Hisan alimtishia kwa picha chache, lakini kwa kweli, sote tunajua kuhusu kile kilichompata katika tukio hilo wakati huo. Ikiwa ningejali, nisingependekeza kumuoa hata kidogo. Kuna uwezekano mkubwa kwamba Hisan hakutumia hata picha! ”

“Huenda alikubali kulala na watekaji nyara hao ili aendelee kuwa hai wakati huo! ” Chester alishtuka tena. “Ni bahati mbaya kwamba Hisan amekufa. Hakuna ushahidi.”

“Ndiyo amekufa. Hilo ndilo jambo baya zaidi.” Alvin alisema kwa mawazo.


Chester alikaa kimya kwa muda mrefu.
Ilimbidi akubali kwamba alimchukulia Sarah kama dada yake, kwa hiyo alihitaji wakati wa kuyatafakari mafunuo hayo yote ipasavyo.

"Kuna jambo moja zaidi," Hans alizungumza ghafla. “Bwana Mkubwa, miaka mitatu iliyopita, ukiwa bado na utu wako wa kawaida, ghafla uliniambia niende makaburini kuchunguza jeneza la Jennifer kujua kilichomo baada ya Sarah kumwambia B. Jones kuwa aliweka mwili wa mbwa kwenye jeneza lake. Nilishtuka wakati huo lakini nilifanya kama ulivyosema, nikagundua kuwa jeneza la Jennifer halikuwa na mwili wa binadamu hata kidogo.”

Chester alishtuka. "Ikiwa sio mwili wa mwanadamu, basi ulikuwa wa nini?"

Alvin alinung'unika, "Nadhani ... ulitaja hilo hapo awali."

"Ndio, lakini ulilazwa baada ya hapo na ukapata mshituko nilipokuambia kuhusu hilo. Huo pia ndio wakati nilihisi kwamba kuna kitu kibaya sana kwako, lakini sikuthubutu kueleza tena.” Hans aliongeza, “Wakati huo, pengine ulishuku kwamba Sarah alibadilisha mwili wa Jennifer na kuniambia nichunguze. Kwa kushirikiana na wasimamizi wa makaburi, tulibaini kuwa ndani ya jeneza hilo kulikuwa na mwili wa mbwa kweli.”

"Sarah alibadilisha mwili wa Jennifer na kuweka mwili wa mbwa?" Chester aliganda kabisa.

Alikiri kwamba neno “katili” halipaswi kamwe kutumiwa kumfafanua Sarah. Kuchukua mwili wa mtu aliyekufa na kuubadilisha na ule wa mbwa, mtu huyo anaweza kuwa na akili gani? “Kwa maiti iliyozikwa kwa Jennifer ni mwili wa mbwa?”

"Unaweza kusema hivyo." Hans akaitikia kwa kichwa.


Alvin na Chester wote walikuwa hawana la kusema kwa wakati mmoja.

Baada ya ukimya wa muda mrefu, Chester alisema kwa sauti ya chini, "Labda ... ilifanywa na Thomas."

"Huamini kwamba ni Sarah?" Alvin hakuthubutu kumwamini tena Sarah. “Nimemfahamu muda mrefu zaidi, lakini angeweza kuniharibu kwa hypnosis.
Kilichotokea kwa Logan pia hakika ilikuwa kazi yake ya mikono. Thomas ana akili kiasi hicho?"


“Sema ana akili ila ana akili mbovu.” CHester alisema.

"We unadhani ana akili hata hiyo mbovu? Kwa jinsi anavyosimamia New Era Advertisings, unaweza kusema kwamba hana ubongo. Angekuwa na akili kampuni hiyo isingedumaa hata mimi nikiwaunga mkono kwa miaka mingi. Kama tusingalikuwa tumemdhamini mara kwa mara, angeenda gerezani zamani.”

Chester akashusha pumzi ndefu. “Tumemfahamu Sarah kwa zaidi ya miaka kumi. Moyoni mwangu, amekuwa msichana mkarimu sana. Alibadilika lini? Je, ni kwa sababu alipitia mambo mengi sana katika miaka michache aliyokuwa nje?”

"Labda alibadilika, au labda… amekuwa hivi kila mara na hatukumjua. Yeye ni mzuri katika kujificha." Alvin ghafla alisema, “Nikifikiria juu yake, tulipokuwa wadogo, kila mara tulimlenga Charity ili kumlinda Sarah kwa sababu tulifikiri kwamba alikuwa akimdhulumu Sarah kila mara. Labda…"

Uso mzuri wa Chester ulibadilika ghafla. Jina la 'Charity' lilikuwa mwiko kwake. "Unafikiri ni Sarah ndiye aliyemfanyia njama Charity pia?"

Alvin alimtazama kwa kutatanisha. "Sijui. Hayo ni mawazo yangu tu.”

"Sarah ni mbaya ndiyo, lakini Charity pia hawezi kuwa mzuri." Uso wa Chester ulionyesha kuchukizwa. “Usisahau kwamba alipanga watu kumchoma moto Maurine hadi kufa. Ni wazi kuwa yeye pia ni mtu mbaya.”

Alvin akabetua midomo yake myembamba na hakuongea. Chester akavua miwani yake na kupangusa macho yake. “Thomas, Sarah, Charity. Watu hao watatu hakuna hata mmoja aliye tofauti na mwenzake. Wote ni watu wabaya.”

Alipomaliza tu kuongea, Rodney akampigia simu.
Chester alitazama simu lakini hakujibu.
Alvin akamkumbusha, “Rodney atakuwa anakupigia ili unishawishi. Sarah lazima awe anamsukuma kwa nyuma. Hataki kunirudishia pesa. Anapenda pesa na nguvu. Tangu alipokutana nasi, amezoea kuishi maisha ya mtu ambaye anasimama juu ya wengine.”

Mwishowe, Chester hakupokea simu. Aliendesha gari na kuondoka KIM International.

Zamani alikuwa mtu mtulivu sana, lakini wakati huo akili yake ilikuwa ikiwaza juu ya alichokisema Alvin. Labda… Alvin alijaribu kusema nini? Labda Charity hakuwahi kumnyanyasa Sarah hapo awali, na yote yalikuwa ni kitendo kilichoelekezwa na kuratibiwa na Sarah? Hah. Ushahidi ulikuwa wapi? Kwa sababu tu hawakuwa watoto wa mama mmoja?

Gari hilo lilikuwa barabarani kwa muda hadi hatimaye akageuza usukani kwenda kwenye makaburi City Park Cemetery.
Alipofika kwenye makaburi ya Boris na Jennifer, aliona yamefukuliwa. Majeneza mawili yaliyokuwa ndani hayakuwemo!.....ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA..