JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................492-493

Sura ya: 492

Mtazamo wa mjakazi mkuu ulibadilika alipoingia na kifaa cha huduma ya kwanza. “Bwana Mkubwa umejeruhiwa vibaya sana. Ni lazima utafute daktari wa kitaalamu akuhudumie.”

“Ni sawa. Nipatie tu bandeji na nitajifunga jeraha langu mwenyewe.” Alvin aliongea kwa kina na kutojali.

Baada ya jeraha lake kufungwa bandeji, alishuka na kukuta Lisa hayupo tena. Baada ya kumuuliza mtumishi fulani, alipata habari kwamba alikuwa ameenda kwenye maktaba.

Alielekea kwenye maktaba na kugundua kuwa alikuwa akijaribu kuwasha kompyuta.
Lisa aliposikia nyayo zake, alimtazama kwa macho ya kusitasita.

“Usijisumbue kuiwasha. Nimeondoa nyaya zote za mtandao. ” Alvin alimsogelea kwa utulivu. "Huhitaji kuazima simu za watumishi pia. Wao hata si Wakenya wala Watanzania. Kizuizi cha lugha ni jambo moja, lakini simu zao zinaweza zitatumika tu kuwasiliana na watu kutoka nchi zao wenyewe."

"Hivii ni wapi hapa jamani?" Lisa alizama katika kukata tamaa baada ya kumsikia Alvin akijigamba kwa maneno hayo. "Alvin, ikiwa una ujasiri, unaweza kunifunga milele. Uliniondoa hadharani, kwa hivyo inachukuliwa kuwa uliniteka nyara. Baba yangu anaweza kuripoti kwa polisi na kuwaamuru wakukamate.”

“Nimezungumza na baba yako. Nilimwambia asipige simu polisi ikiwa anajali usalama wako. ” Alvin aliubembeleza uso wake kimahaba. Wale ambao hawakujua hali hiyo wangefikiri kwamba walikuwa wanandoa wenye upendo.
“Hata hivyo, mimi ni mgonjwa wa akili. Nikikata tamaa, ninaweza kufanya jambo lolote la kichaa.”

Kwa sauti ya upole zaidi, alimwambia Lisa jinsi alivyomtishia baba yake. Alishtuka na kuutupa mkono wake.

Alvin kisha akatabasamu na kusema, “Bila shaka, siwezi kumzuia kukuona milele. Baada ya yote, baba yako bado anaweza kufanya jambo kuhusu hilo. Nilimwambia kwamba nitakuruhusu urudi mwezi mmoja baadaye ili kumfanya ajisikie vizuri. Ninataka tu kutumia muda fulani na wewe katika ulimwengu wetu mdogo na kukufanya uniangukie tena.”

“Sitamwangukia mtu aliyeniteka nyara. Endelea kuota!" Lisa alifoka kwa hasira, "Nitahakikisha kwamba tunatengana mara tu nitakapoondoka mahali hapa."

"Una uhakika unaweza kuftengana na mimi baada ya kupata mapumziko safi kutoka kwangu?" Alvin aliuma mdomo kwa mawazo.

Lisa aliona jambo la kushangaza mwanzoni, lakini alielewa maana yake haraka na akashtuka. Kwanini angetaka kumfanya akae naye hapo kwa muda wa mwezi mmoja? Ikiwa walngelala pamoja kwa mwezi huo mmoja, angeweza kupata mimba ya mtoto wake.

“Alvin Kimaro, wewe ni mtu mbaya sana! Ni afadhali nife kuliko kupata mimba ya mtoto wako,” alimfokea kwa hasira.

“Lisa, uliwahi kuwa na ujauzito wa watoto wangu, maana yake miili yetu bado iko sawa. Nikilala nawe kila usiku kwa mwezi huu mmoja, kuna uwezekano kwamba utapata mimba.”

Alvin alipokuwa akiongea hayo, damu iliyokuwa ndani yake ilianza kumchemka. Watoto wao hawakufaulu kuishi wakati huo, sivyo? Lakini wakati huu, angehakikisha kwamba wangezaliwa salama.

“Suzie ni mrembo sana, sivyo? Hakika tunaweza kuzaa mtoto mzuri kama Suzie.”

"Siwezi kujisumbua kukuburudisha."

Lisa alikuwa karibu kupandisha kichaa kwa sababu yake. “Acha kuota! Hata nikipata mimba ya mtoto wako nitaitoa.”

“Ukisisitiza kutoa mimba, sitakuwa na budi ila kukuweka hapa hadi utakapojifungua mtoto wetu.” Alvin alimtazama bila kujali. "Niamini, ninaweza kumudu kufanya hivi. Hivi karibuni, KIM International itavumbua aina mpya ya smartphone ambayo italeta mabadiliko katika soko la kimataifa wakati huu. Sio tu kwamba KIM International itaendelea kuwa kampuni bora zaidi nchini Kenya, lakini pia nitakuwa mmoja wa wajasiriamali mia moja bora ulimwenguni. Hakuna mtu katika Kenya nzima anayeweza kunizuia."

Lisa alishangaa.
Hajawahi kufikiria kuwa maendeleo ya KIM International yangefikia kiwango hicho.
Ikiwa alichosema Alvin ni kweli, hata Rais asingeweza kumfanya chochote.

"Maadamu utazaa mtoto wetu, bila kujali ni binti au mvulana, mali zangu zote zitakuwa zao." Alvin aliukunja uso wake kwa upole. "Lisa, nilikuwa nikishughulika na maendeleo yangu ya kazi kabla ya hii ili kufanya KIM International kupanda juu.
Lakini tangu nilipoanguka kwa ajili yako, nilitambua kwamba ni bure kabisa kupata pesa nyingi. Nataka tu kuwa na wewe. Wacha tufurahie wakati mzuri pamoja hapa katika kipindi hiki."
Akambusu kwa upole kwenye midomo.

Lisa alionekana kuduwaa.
Alikuwa amemdharau Alvin. Alijuta kurudi Kenya kwa lengo la kulipiza kisasi kwa Alvin.
Wakati huo, alikuwa amekazia akili yake kulipiza kisasi kwa Sara. Lakini, alipuuza jinsi Alvin angeweza kuwa mjanja dhidi yake.

'Kisiwa hiki ni kizuri. Acha nikupeleke nje tutembee.” Alvin aliukumbatia mwili wake uliokuwa mgumu huku akitoka nje.

Alvin alipokaribia kufika langoni, mjakazi mkuu alimsogelea akiwa na kidonge na glasi ya maji.
'Chukua." Alvin akampa Lisa kidonge.

"Hii ni nini?" Lisa alitetemeka sana. Yeye hakuthubutu kuichukua.

“Kidonge cha kuzuia mimba,” Alvin alieleza kwa macho yaliyotkaza kidogo, “nililala nawe jana usiku, lakini ulikuwa Dar es Salaam siku chache zilizopita, kwa hivyo unaweza kuwa umefanya hivyo na Kelvin. Lazima nihakikishe kwamba hutapata mimba ya mtoto wa Kelvin.”

Lisa hakujua la kusema. Hakuwa amefanya chochote na Kelvin, lakini kidonge hicho kingeweza kumzuia kupata mimba baada ya kufanya na Alvin jana yake usiku. Kwa hivyo, alichukua kidonge bila kusita.
Baada ya kukimeza, alizama kwenye mawazo mazito. Kwa kuzingatia kwamba kuna uwezekano mkubwa angepata mimba katika siku chache zijazo, ilimbidi afikirie njia ya kuepukana nayo.

Baada ya Lisa kuoga usiku, alijikata mguu wa nyuma kwa kitu chenye ncha kali.
Kisha, alipaka chupi yake kwa damu.
Mara tu alipomaliza kufanya hivyo, alimwambia Alvin, “Je, una pedi? Niko kwenye kipindi changu.”

"Ni bahati mbaya." Alvin aliinua kichwa chake. Ni wazi kwamba hakumwamini hata kidogo. "Unajaribu kutafuta kisingizio cha kuzuia kupata mimba, huh?"

“Sisemi uongo. Ikiwa huamini, unaweza kuangalia mwenyewe.”
Lisa alipomaliza sentensi yake, Alvin alimsukuma kitandani.
Alvin alikagua na kugundua kuwa kweli alikuwa anavuja damu.
Alikunja uso kwa huzuni, lakini uso wake ulififia muda mfupi baadaye.
Kwa kuwa alipanga kumweka hapo kwa muda wa mwezi mmoja, bado angepata hedhi. Ilikuwa haiepukiki.

“Nitamwomba mtumishi akuchukulie pedi.” Muda mfupi baadaye, mtumishi alimpitishia pedi.

Baada ya Lisa kuvaa pedi ya usafi, Alvin alimpeleka kitandani. Alikuwa amefungwa mikononi mwake usiku mzima.

Siku iliyofuata, aliamka kwa busu yake, ambayo ikawa utaratibu wa kila siku. Lisa bado alipaswa kuwa mwangalifu sana. Kila siku, alikamua damu kutoka kwenye jeraha lake na kuchafua pedi kwa damu. Alikuwa na wasiwasi kwamba mtumishi aliyetoa takataka angeona jambo lisilo la kawaida.

Siku ya saba. Alvin alichukua bikini na kwenda kwa Lisa. “Babe, hedhi yako imeisha sasa. Nitakupeleka ufukweni ili uende kuogelea leo.”

Lisa alitazama bikini ya waridi, ambayo ilikuwa nzuri na ya kuvutia.
Ikiwa angeivaa, Alvin bila shaka angeona jeraha kwenye mguu wake wa nyuma. Alikuwa na hisia kwamba hakika Alvin angelala naye usiku huo. Kwa hivyo, ilimbidi kuficha jeraha haraka au angemshuku.

"Hapana, sipendi kuogelea." Akatazama pembeni. "Nenda mwenyewe kama unataka lakini mimi sitajiunga."

“Kama hauogelei, kuna faida gani mimi kuogelea peke yangu? ” Alvin alimkumbatia na kumweka kwenye mapaja yake.

Lisa hakumpinga. Baada ya yote, haijalishi alijaribu sana kumpinga katika kipindi hicho, hakuwa na nguvu kama yeye. Kadiri muda ulivyopita, hakuweza kuhangaika kupoteza nguvu zake tena.

“Sawa basi. Nitatembea kando ya bahari pamoja nawe.” Alimfariji kwa upole. Akiwa amepigwa na wazo, Lisa alitikisa kichwa muda mfupi baadaye.
"Sawa, lakini nataka kupanda juu na kuvaa nguo ndefu."

Sura ya: 493

Baada ya kusikia haya, uso mzuri wa Alvin ukawa mpole.
Wiki nzima iliyopita, Lisa kila wakati alionekana kutojali na mwenye chuki bila kujali jinsi alivyojaribu kumfurahisha. Sasa, alikuwa tayari kubadili nguo na kutembea kando ya bahari pamoja naye. Je, hilo lilimaanisha kwamba polepole alikubali hali halisi?

"Endelea." Baada ya kumsihi kirahisi, ghafla alijuta kumletea nguo chache. Alimpigia Hans mara moja. "Chagua nguo nyingi zaidi za Lisa na uzitume hapa. Nataka zile zinazofaa kuvaliwa ufukweni na saizi ya mke wangu.”

Pembe za mdomo wa Hans zilitetemeka. 'Mke wako? Huna aibu? Kweli yeye ni mke wa Kelvin.' Aliwaza tu lakini maneno hayo bila shaka yasingejaribu kuvuka kinywa chake, vinginevyo…

"Bwana Mkubwa, tafadhali rudi ofisini ikiwa unapatikana." Hans aliongea kwa msisitizo, "Hivi karibuni, KIM International imekuwa ikipokea shutuma nyingi. Mzee Kimaro na Bibi Kimaro wamekasirika sana hivi kwamba wanakaribia kuugua. Na wanahisa wa kampuni huja ofisini kila siku kunitafuta. Umma umekuwa ukitushambulia, na bei za hisa za KIM International zinaendelea kushuka.”

"Je, si kawaida kwa bei ya hisa kupanda na kushuka?" Alvin alijibu kwa njia nyepesi, “Mwambie Chester atoe habari kuhusu kashfa za maadili ya baadhi ya watu mashuhuri. Kila mtu atasahau polepole kuhusu tukio hili."

Hans alikosa la kusema. 'Je, si unamweka Chester katika hali ngumu kwa kufanya hivi? Katika suala la kuzorota kwa maadili, hakuna mtu anayeweza kukushinda.' Hayo maneno pia yalibaki kwenye mawazo ya Hans, yangemponyoka mdomoni bila shaka matokeo yake yangekuwa hayaelezeki.

"Kuhusu Mzee Kimaro na Bibi Kimaro, wakiuliza kunihusu, waambie tu kwamba ninasaidia familia ya Kimaro kuzalisha wajukuu. Waambie wasiwe na wasiwasi juu yangu. Wanahisa hao hawatasumbuka juu ya kampuni mradi tu wanapata pesa za kutosha za kutumia. Mimi ndiye mfanya maamuzi wa KIM International. Yeyote ambaye hafurahii uamuzi niliofanya anaweza kupotea.” Alvin alipomaliza kuongea tu, akakata simu.

Aliinua kichwa chake baada ya kumuona Lisa akishuka kwenye ngazi akiwa amevalia gauni refu jekundu lililokuwa na mchoro wa alama za kizamani. Licha ya kuwa hakuwa amejipodoa, alionekana kama mrembo mwenye sura nzuri na ngozi yenye kuwaka.

Alvin akaenda mbele. Kisha, akafunga mikono yake kiunoni mwake na kumkumbatia. Kwa sauti ya kicheko, alisema, "Unaonekana mrembo."

Lisa aliweza kuhisi mara moja mabadiliko ndani yake. Mwili wake ulipozidi kuwa na msisimko, alijiuliza sana ikiwa mtu huyu alikuwa kweli
kazaliwa na binadamua alikuwa tolewa kutoka kwa mnyama wa porini. Kwanini badiliko kama hilo ndani yake lilitokea wakati alikuwa amebadilika tu kwa mavazi, je angekuwa mtupu muda huo ingekuaje?

"Inaonekana hutawahi kuwa na ngozi mbaya hata utajiweka kwenye jua vipi." Alvin alimpigapiga mabega yake. Mara chache walitoka nje kwa siku chache zilizopita, na jua kali kando ya bahari lilikuwa limechoma sana ngozi yake. Lakini, bado alikuwa mng’avu kama hapo awali.

Lisa alitazama chini na kumpuuza. Alvin hakujali. Alitoka nje ya nyumba ya kifahari huku mikono yake ikiwa imezunguka kiunoni mwake.
Pwani ya bahari ilikuwa safi sana. Lisa aliinua kichwa chake na kutazama kwa mbali. Laiti Alvin asingemleta hapo kwa njia ya mateka, angefikiri kwamba eneo hili lilikuwa kivutio cha ajabu cha watalii.

“Nimechoka." Baada ya kutembea kwa muda, Lisa alikaa chini ya mnazi ufukweni. "Ninakiu. Nataka kunywa maji ya madafu.”

“Sawa.” Alvin alifurahi sana kwamba alikuwa akitoa ombi kwa hiari yake mwenyewe. “Nisubiri hapa. Nitakuletea.”

Hakuwa na wasiwasi hata kidogo kwamba Lisa angekimbia, kutokana na bahari kubwa na kutokuwepo kwa boti hapo. Hakuna hata mgeni mmoja aliyeweza kupatikana kwenye kisiwa hicho.

Baada ya Lisa kugundua kuwa ameondoka, alisimama na kupanda kwenye mwamba karibu na bahari. Alijiumiza kwa makusudi kwenye mwamba mahali ambapo jeraha lake lilikuwepo. Alipomuona Alvin anakuja, alijifanya kuteleza kutoka kwenye mwamba na kutumbukia baharini.

“Lisa…” Alvin alitokea kuona tukio hili. Alishtuka sana hadi akaruka baharini bila kusita. Aliogelea kuelekea kwake na kumwinua upesi kutoka baharini. "Uko salama?"

“Niko sawa…” Baada ya Lisa kumaliza sentensi yake akiwa amekunja uso, sauti ya kugugumia maumivu ilisikika.

Alvin alimchukua haraka hadi ufukweni na kuangalia jeraha lake. Aligundua kuwa sehemu ya nyuma ya mguu wake ilikuwa imefugwa.
Inavyoonekana, kulikuwa na sehemu ya ngozi yake iliyokatwa na mwamba mkali na kusababisha jeraha kubwa.

Alvin akambeba Lisa na kukimbilia ndani ya jumba lile bila kufikiria tena.
Mjakazi mkuu haraka akamleta sanduku la huduma ya kwanza Kwa kuzingatia jeraha lake la kina, Lisa alihitaji kupigwa sindano ili kupunguza uvimbe.
Lisa aliendelea kuvumilia maumivu. Maumivu hayakuwa kitu ilimradi Alvin asijue asili ya jeraha hilo.
Kwa upande mwingine, Alvin aliumia moyoni na kujilaumu. "Ukienda kando ya bahari wakati ujao, nitahakikisha kuwa na wewe wakati wote ili usifanye jambo lolote la hatari tena."

Lisa hakuongea neno lolote. Alikuwa akiishi maisha kana kwamba yuko jela siku zote. Ikiwa alikuwa akimwangalia au la, haikujalisha.

Usiku, Lisa alijikunja kwenye kochi la kibarazani na kujitenga. Alikuwa kachoka kimawazo hadi kufa. Hapo, hakuweza kucheza na simu yake, kutazama runinga, au kufanya shopping. Hakujua mtu mwingine yeyote hapo pia. Ukiachna na kusoma vitabu maktaba, aliweza tu kutazama angani kila siku.

"Umeboreka?" Alvin akatoka bafuni. Moyo wake uliumia sana baada ya kuona sura yake dhoofu.
"Lala na mimi kwa sababu umechoka."

Alipomaliza tu sentensi yake, alimchukua hadi chumba chake cha kulala na kumuweka kitandani. Kisha akanyoosha mikono yake kumvua nguo za kulalia.

Akijua nia yake, Lisa alimpinga kwa kawaida. “Alvin, mguu wangu umeumia na unauma. Huwezi kuniacha nipumzike?”

Macho ya Alvin yalimtoka kwa hatia, akasema bila kupenda, “Nimemuuliza daktari. Alisema kuwa wanawake wana uwezekano mkubwa wa kupata mimba siku chache baada ya kipindi chao kuisha. Siwezi kukosa fursa ya siku hizi. Hata hivyo, usijali, sitakigusa kidonda chako.”

Pamoja na hayo, alifunga midomo yake na midomo yake kwa njia ya ujasiri lakini ya upole.

Lisa alikuwa dhaifu sana kumshinda hata kabla ya kujeruhiwa. Sasa kwa kuwa alikuwa ameumia, hakuna angeweza kufanya ili kumzuia. Alijua ya kwamba mtu huyo alikuwa ameazimia kufanya hivyo. Ingawa siku hizo uwezekano wa kupata mimba haukuwa juu, haikuwa na maana kwamba alikuwa salama kabisa.
Dakika aliyojiwazia kuwa ana mimba ya mtoto wake, moyo wake uliingiwa na hofu.
“Alvlisa, tafadhali usinitendee hivi.” Alimsihi ghafla huku akimshika mkono.

Mwili wa Alvin uliganda. Kwa kadiri alivyokumbuka, hakuwahi kumwita Alvlisa kwa muda mrefu sana. Hata hivyo, neno hilo kwa namna fulani liligonga kengele lilipotoka kinywani mwake. Ilionekana tu kuwa jambo la kweli wakati alipozungumza naye kwa njia hii.

“Lisa, unaweza kunilaumu na kunichukia kwa ninachotaka kufanya sasa. Lakini sijali. Nataka tu kukupa mimba ya mtoto wangu.” Alirudia kumbusu midomo yake kwa huzuni lakini kwa ujasiri wakati huo huo. "Ninaapa kwamba nitakutendea wewe na mtoto vizuri katika siku zijazo. Samahani, Lisa, sijui jinsi ya kukuzuia ubaki upande wangu. Ninakubali kwamba mimi ni mtu mbaya kwako, lakini nitapandwa kichaa ikiwa nitakupoteza.”.......ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA..