AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................490-491
Sura ya: 490
Saa kumi alfajiri. Dar es Salaam.
Kelvin hakuwa amelala bali amesimama kwenye kibaraza kama sanamu. Macho yake yalikuwa mekundu yakiwa na damu kutokana na kukaa macho usiku kucha. Trei ya majivu iliyokuwa kando yake ilikuwa tayari imejaa virungu vya sigara.
Nyuma yake kulikuwa na kitanda.
Ilitakiwa kuwa Lisa na yeye wawe na usiku wao wa kwanza ndani ya chumba hicho baada ya harusi yao, lakini Alvin alikuwa amemnyakua.
Alikuwa wapi? Alikuwa anafanya nini sasa? Kelvin alifadhaika sana hata hakuweza kutuliza akili yake.
Ghafla, sauti ilisikika kutoka kwenye simu yake. Akapokea ujumbe wa ajabu.
Akabonyeza fungua na kulikuwa na video fupi. Katika video hiyo, taa hazikuwashwa lakini aliweza kuona vizuri vivuli viwili kitandani. Aliitambua sauti ya kilio iliyokuwa ya Lisa.
Ghafla, alihisi kama kifua chake kimepasuka. Kelvin hakuwa mpumbavu. Aliweza kujua walichokuwa wakifanya. Hata hivyo, hakutaka kuamini. Aliogopa kufikiria juu yake ...
Usiku huo ulipaswa kuwa usiku wake wa kwanza na yeye. Alikuwa ameutarajia siku nyingi kwa kile kilichoonekana kama umilele.
Tangu alipokutana na Lisa huko Dar es Salaam, alikuwa amempenda. Alipokubali pendekezo lake, kwa kweli alikuwa amefurahi. Ingawa walifanya harusi ndogo tu, alikuwa ameweka juhudi nyingi katika mapambo. Hakutarajia kuwa mwanamke wake angeishia kuwa na Alvin usiku huo.
"Alvin Kimaro, nitakufanya uteseke kuzimu hivi karibuni au baadaye."
Kelvin alipiga teke meza ya kahawa iliyokuwa mbele yake. Uso wake wa kifahari na mzuri uligeuka kuwa mbaya sana.
"Pia, Lisa Jones, kwanini ... kwa nini unanitendea hivi?"
Mtazamo wake ulibeba alama za hasira. Alikuwa akimwekea kinyongo, lakini upendo wake kwake ulikuwa na nguvu zaidi. Alipaswa kuwa mchumba wake miaka mitatu iliyopita. Hata hivyo, alijua kwamba alipanga tu kuolewa naye kwa sababu tu alikuwa amemuokoa.
Baada ya kurudi kutoka Marekani miaka mitatu baadaye, aligundua kwamba Lisa alitaka kumrudisha Alvin. Bado alivumilia tabia yake kwa uchungu. Baada ya yote, yeye alikuwa hajamuahidi kuwa naye, lakini ilikuwa hadithi tofauti sasa. Kama mke wake wa ndoa, alilala mikononi mwa mwanamume mwingine usiku wa harusi yao?!
'Lisa Jones, huna aibu hata kidogo? Hata kama Alvin angekulazimisha, si ungemtishia maisha yako?' Kelvin alikunja ngumi. Aliwachukia wote Alvin na Lisa.
Macho yake yalikuwa na hasira kali kwa muda mrefu. Mara akampigia simu sekretari wake. “Regina, umelala? Njoo chumbani kwangu sasa hivi."
“Bwana Mushi…” Regina Gwakisa alifurahi na kushangaa. Alishangaa kwanini Bwana Mushi alikuwa akimwita chumbani kwake muda huo. Haikuwezekana kwamba alitaka kuzungumza naye juu ya kazi. Alikuwa akifanya kila awezalo ili kumtongoza Kelvin, lakini siku zote alikuwa akijiweka mbali naye.
Endapo Lisa asingenyakuliwa na Alvin, Kelvin asingekuwa katika hali mbaya na kumtaka aaende chumbani kwake. Hakika, ilikuwa fursa nzuri kwa Regina kumfanya asogee kwake usiku huo.
“Sawa, Bwana Mushi. nakuja sasa hivi.”
Dakika kumi baadaye, Regina alionekana katika chumba cha Kelvin. Alikuwa kavaa tu nightdress fupi. Kwa makusudi, alifunua paja lake.
Kelvin alimwendea akiwa na uso wa huzuni na mzuri. Regina aliinua kichwa chake na kumtazama, mapigo ya moyo yakimuenda mbio sana.
Alikuwa amempenda kwa muda mrefu. Sio tu kwamba mtu huyu alikuwa mzuri na mtanashati lakini pia alikuwa kijana na mwenye uwezo. Angekuwa karibu naye angefaidika sana. Angekubali hata angeombwa afanye naye jambo la aibu.
“Bwana Mushi…” Alipepesa macho yake kwa upendo. Kabla hajapata fahamu zake, Kelvin alimvuta kwa karibu mikononi mwake na kumbusu kwa mapenzi.
Baada ya kupigwa na butwaa kwa muda, Regina alifurahi sana.
Hakutarajia hili. Kwa kweli ilikuwa zaidi ya matarajio yake.
Fungate ya Lisa usiku huo iligeuka kuwa ya kwake.
•••
Katika kisiwa.
Jua la rangi ya machungwa lilipanda polepole juu ya upeo wa macho juu ya bahari. Ilipofika saa sita mchana Lisa alifumbua macho yake ya uchovu taratibu. Alipoinuka, alikuwa peke yake kwenye kitanda kilichochafuka na maua ya rose.
Upepo wa baharini ulipovuma, mapazia kwenye madirisha yalisogea.
Macho yake yalikuwa yameduwaa. Hakuwahi kufikiria kwamba angemsaliti Kelvin japo hakupenda. Alijaribu kumpinga Alvin kwa nguvu zake zote jana usiku, lakini mtu huyo alikuwa mkaidi na alijifanya mwendawazimu. Mwili wake ulikuwa bado unauma hata sasa.
Aliinua blanketi na kujificha chini yake. Alikuwa amejikunja ndani kama mpira. Hakuthubutu kujiwazia angekabiliana vipi na Kelvin wake mpendwa hata kama angeweza kukimbia kutoka mahali hapo. Hakustahili tena kuwa na yeye. Kwa kweli hakustahili.
Ghafla, mlango wa chumba hicho ukasukumwa. Mwanamke mwenye umri wa miaka 40 aliingia akiwa na rundo la nguo nadhifu. “Bi Mkubwa, umeamka. Hapa kuna nguo ambazo unaweza kubadilisha. Unataka kuoga—”
“Potelea mbali!” Lisa alifagia kila kitu kutoka kwenye sinia iliyokuwa kwenye meza ya kando ya kitanda kama kichaa. Alizungusha mikono yake kichwani kwa sura ya kutisha, huku nywele zake zilizotibuka zikianguka juu ya mabega yake.
Mwanamke huyo alishtuka sana hadi akarudi nyuma na kugongana na mtu.
Alipogeuka na kuangalia, aliita kwa woga, "Bwana Mkubwa…"
"Nipe nguo na uende nje." Alvin alielekea kitandani huku akiwa ameshika nguo.
Lisa alipomwona tu, alichukua maua na kumtupia usoni. Uso wake mzuri ulikuwa mzito kwa chuki.
“Umemaliza?” Macho ya Alvin yalibaki ya upole. “Una uhakika unataka nipotee? Hutaki kuvaa nguo? Au unapanga kukaa kitandani milele?"
Baada ya kukumbushwa, Lisa aligundua kuwa alikuwa uchi. Pia, vazi la harusi alilovaa jana yake lilichanika. Ikiwa angekataa nguo hizo, asingekuwa na chochote cha kuvaa.
"Kwa kuwa hutaki nguo, ni sawa." Alvin aliinua uso wake. Alijifanya mnyonge na akashusha pumzi. "Kwa kweli, napenda sana jinsi unavyoonekana ukiwa uchi."
Huyu mhuni mbaya...Lisa alikasirika sana hadi uso wake ukakunjamana.
Alipoona kwamba angeondoka, hakuwa na la kufanya ila kusema kwa kuudhika, “Simama hapo hapo. Nipe nguo.”
“Sawa mke wangu.” Alvin alitoa tabasamu kidogo. Aligeuka na kumpitishia nguo mara moja.
“Mke wako ni nani? Umekosea. Mimi ni mke wa Kelvin.” Lisa alicheka kwa kuudhika.
Mtazamo wa upole wa Alvin uliganda kwa muda kabla haujawa laini tena. “Lisa, sina hasira. Nilikuwa nakutesa, kwa hiyo sasa ni zamu yako kunitesa. Maadamu una furaha na unaweza kutoa hasira yako, ni sawa."
Lisa hakuweza kujizuia kuruka kwa hasira. “Sitaki kukutesa. Ninataka tu kukaa mbali kutoka kwako. Nakuchukia.”
"Ndio, unanichukia, lakini nashangaa ni nani aliyekufurahisha jana usiku?" Alvin alikodoa macho.
Uso mzuri wa Lisa ukabadilika na kuwa wa kutisha mara moja. Alitamani angemchuna usoni.
“Lisa hata ukinichukia na kutonipenda tena, mwili wako bado umenizoea.” Alvin aliinamisha kichwa chake na kumbusu kwenye midomo yake myembamba.
Lisa hakukwepa lakini alisema bila kujali, “Ni mahitaji yangu tu ya kimwili. Nina tabia kama hii ninapokuwa na wewe. Zaidi ya hayo, nadhani huwezi kulinganishwa na Kelvin…”
"Jaribu na useme tena." Alvin akayaminya mashavu yake, macho yake yakidhihirisha hisia kali za kuudhika. Punde, uso wake ukawa mbaya.
Lisa alimuangalia kwa makusudi. “Nimekuwa naye kwenye uhusiano kwa muda sasa. Si ni kawaida tu hata tukilala pamoja kwa sasa?”
“Lisa kwanini unilazimishe kuchukia? sitaki kukuumiza.” Alvin alihisi hasira zake zikimpanda.
Jinsi Alvin alivyokuwa akifanya kwa wakati huo ilimtia hofu tena Lisa. Ghafla, alijuta kidogo. Wakati fulani alimuumiza sana hivi kwamba alipelekwa hospitali katikati ya usiku.
Tukio hilo lilikuwa bado ni ndoto mbaya inayomsumbua.
“Alvin… Alvin Kimaro, umesema kwamba hutaniumiza tena. Je, utarudi kwenye neno lako?” Lisa alisema kwa wasiwasi, "Vema, hujawahi kutimiza ahadi yako hata hivyo."
Sura ya: 491
Ghafla, sura ya Alvin yenye hasira iliganda kana kwamba amepooza.
Akashusha macho chini huku Lisa akimtazama kwa kejeli.
"Mimi huwa sirudi nyuma kwa neno langu." Sekunde tatu baadaye, alijiweka sawa mwili wake. Moyo wake ulijawa na taabu na uchungu.
“Lisa, usinichokoze. Ninakuchukulia kama mwanamke wangu. Ingawa nilikuwa kwenye uhusiano na Sarah, sijawahi kumgusa mwanamke mwingine isipokuwa wewe tu.”
Lisa alipigwa na butwaa kabla ya kudhihaki, “Usinidanganye kwa kunichukulia kama mjinga. Umekuwa kwenye uhusiano na Sarah kwa zaidi ya miaka kumi. Haiwezekani kwamba hujawahi kulala naye hata kidogo. Siamini, ukizingatia kwamba wote wawili mmekuwa pamoja kwa muda mrefu.”
"Bado alikuwa mdogo wakati huo. Baadaye, nilikuwa na shughuli nyingi za kusimamia KIM International, kwa hivyo sikujihusisha na aina hiyo ya mambo kwa sababu ya ubize. Baada ya hapo, alijinga na chuokikuu huko Garisa na akapotea baada ya kutekwa na magaidi wa Al-Shabaab, sikuonana naye tena mpaka aliporudi miaka mitatu iliyopita. Amini usiamini, niimefanya mapenzi na wewe tu.” Alvin mwenyewe aliona ni muujiza pia baada ya kumaliza kuongea.
Kwa kweli, hakuwa amemwambia Lisa jambo lolote—yaani kwamba hakuwa na tamaa zozote za ngono wala msisimko alipokuwa na Sarah.
Hakuelewa hapo zamani, lakini sasa, polepole aliielewa.
Alipoendelea kumlinda Sara bila kujali mengine yote, haikumaanisha kwamba alimpenda. Alimchukulia tu kama familia yake au mwangaza pekee wa gizani. Alikuwa akiamini kwamba Sarah alikuwa mwema na wa ajabu, akisahau ukweli kwamba watu hubadilika.
Ni pale tu alipokutana na Lisa ndipo alipogundua mapenzi yasiyosahaulika ni nini. Kuwa naye kulimfanya ajisikie mtulivu sana, mtamu na mwenye furaha. Asipomuona, angemkumbuka sana. Alipokula chakula alichotengeneza, kilikuwa na ladha ya chakula kitamu zaidi duniani.
Haijalishi alikuwa katika hali gani, bado angeendelea kufikiria kwamba alikuwa mtu mzuri zaidi.
“Nguo zipo hapa. Baada ya kuvaa, nitakuandalia kifungua kinywa.”
Kwa hayo, Alvin aligeuka. Akafunga mlango na kuondoka.
Baada ya kuachana kitandani kwa muda, Lisa alijikokota nje taratibu na kuoga. Maji ya moto yalipomwagika mwilini mwake, bado hakuamini.
Yeye ni mwanamke wa kwanza kwa Alvin kuwa naye? Ilikuwa haiaminiki.
Baada ya kuoga, alivaa jozi mpya ya jeans na T-shati nyeupe. Ingawa nguo hizo hazikutoka kwenye brand za kifahari, ilikuwa ya kustarehesha sana. Lakini, hakuweza kuficha alama za mabusu ya Alvin kwenye shingo yake. Baada ya kufikiria kidogo, hakujali kuhusu alama hizo kwani hakumjua mtu mwingine yeyote kwenye kisiwa hicho zaidi ya Alvin.
Katika hali ya kukata tamaa kama hii, ilibidi ajue mahali alipokuwa na kuwasiliana na mtu wa nje.
Alikuwa na aibu sana kuwasiliana na Kelvin, kwa hiyo angeweza tu kuwasiliana na Logan na Austin. Baada ya kutoka nje ya chumba hicho, akakutana na mtumishi wa kike mweusi ambaye alikuwa akielekea kwake. Alijaribu kuazima simu kutoka kwake, lakini aligundua kuwa kulikuwa na kizuizi cha lugha kati yao. Kwa kuzingatia kwamba mtumishi huyo hakuweza kuzungumza Kiswahili wala Kiingereza, Lisa alihisi ajabu sana hivi kwamba alitumia ishara kuwasiliana.
Hatimaye mtumishi huyo alipotoa simu yake mfukoni, Lisa alipigwa na butwaa. Kulikuwa na watu ambao bado walitumia simu za zamani kama hizo? Kwenye skrini kulikuwa na maneno ambayo hajawahi kuona hapo awali. Hakuweza kuelewa chochote, na wala hakuweza kupakua programu zozote za mitandao ya kijamii alizokuwa anazifahamu. Aliuliza watumishi wengine wachache baadaye lakini yote yalikuwa sawa.
Hatimaye alizama katika kukata tamaa. Hii ilikuwa wapi jamani?
Baada ya kushuka ngazi kwa huzuni, Alvin alitoa kifungua kinywa nje ya jiko akiwa amevaa aproni. Alitazama kwenye kifungua kinywa. Kulikuwa na mayai yaliyokaangwa, maziwa fresh, sandwichi, juisi ya parachichi, na aina mbalimbali za matunda mapya kwenye meza.
"Ulikuwa unakamata tumbo na moyo wangu kwa kupika kwako, kwa hivyo sasa nitatumia upishi wangu kushinda moyo wako tena." Alvin aliondoa apron na kuiweka kando. Siku hiyo, alivaa fulana nyeupe iliyofanana na ya Lisa na jozi ya jeans pia.
Akiwa amepunguza kabisa nywele kichwani mwake, alionekana kama mvulana mdogo.
Lisa alishindwa cha kusema. Je, alikuwa amevaa mavazi yanayofanana naye kwa makusudi? Ikiwa angekuwa na seti nyingine ya nguo, angevua nguo zake zote mara moja.
“Sahau kuhusu hilo. Kwa upikaji wako mbovu, siamini kwamba ulitengeneza vyakula hivi vyote wewe mwenyewe.” Lisa alikoroma.
'Kwa kweli nilifanya mwenyewe. Siku chache zilizopita, nilijifunza jinsi ya kupika kutoka kwa mpishi. Kwa vile wewe ndio ulinipikia enzi zile, nitakupikia kuanzia sasa. Ikiwa huamini, unaweza kutazama mikono yangu… ” Alvin alinyoosha vidole vyake vyote. Vidole vyake vilivyokuwa nadhifu sasa vilikuwa na makovu. Pia kulikuwa na mikunjo kwenye viganja vyake.
"Inauma." Alvin alimtazama kwa macho yake meusi. Sambamba na uso wake mzuri wa kuvutia, mwanamke yeyote labda angeyumba kwa kumtazama. Lakini, Lisa hakuyumba hata kidogo.
“Kama mwanaume, unanung’unika kuhusu maumivu kidogo hivyo. Huna aibu? Kelvin asingefanya hivi.”
Alvin alikosa la kusema.
Hali yake nzuri iliharibiwa kabisa baada ya kusikia neno 'Kelvin'.
Mara Lisa alianza kula kifungua kinywa bila kujisumbua kutazama sura yake ngumu. Licha ya kuwa na kinyongo dhidi yake, asingetesa tumbo lake kwa njaa. Ikiwa angepata ugonjwa wa tumbo uliosababishwa na njaa, asingeweza kufurahia chakula kitamu tena.
“Kina ladha nzuri?” Mara Alvin aliuliza huku akionekana kutarajia jibu la kupendeza.
Lisa bila huruma alitazama pembeni. "Ni wastani tu. Sio nzuri kama upishi wa Kelvin.”
Uso wa Alvin ukatiwa karaha, na akaonya vikali, “Sitaki kusikia neno ‘Kelvin’ likitoka kinywani mwako tena. Nisemaje?”
Lisa alimdhihaki. “Kwanini? Unataka kuniumiza tena, huh? Hakika, ahadi zako ni rundo la bullsh*t."
Alvin akasaga meno. Alikuwa akitumia udhaifu wake kumshinikiza kupita kiasi.
“Sitakuumiza.” Macho yake makali kama tai yalitua mdomoni mwake. "Lakini ukiendelea kumtaja Kelvin, sina la kufanya ila kuifunga midomo yako."
Alipomaliza tu kuongea, ghafla aliuegemeza mwili wake na kumbusu midomoni akiwa bado amezama kwenye mawazo.
Akiwa amemaliza tu kunywa maziwa, harufu hafifu ya maziwa na utamu bado ilitanda kwenye midomo yake.
Hapo awali, alitaka tu kumfanya afunge mdomo wake, lakini hakuweza kupinga kumbusu baada ya hapo.
Kwa hasira, Lisa alijaribu kumsukuma kwa nguvu, lakini hakusogea hata sentimeta moja. Kwa hasira kali, alishika uma juu ya meza na kumchoma mgongoni.
Alihisi mwili wake kutetemeka kwa muda. Baadaye, alikutana na busu la mapenzi zaidi. Busu hilo lilidumu hadi akakaribia kukosa hewa.
"Hebu tuone kama utathubutu kumtaja tena mtu huyo." Alvin aliinuka na kumkazia macho mdomo wake uliokuwa umevimba.
Lisa alijifuta mdomo kwa nguvu kabla hajamkazia macho. Lakini, hakuthubutu kusema chochote kingine kwa kuogopa kwamba angembusu tena.
"Unaweza kula kwanza." Kwa hayo, akageuka.
Hapo ndipo Lisa alipoona dimbwi la damu nyuma ya fulana nyeupe ya Alvin karibu na bega lake.
Aliinamisha kichwa chini na kutazama kwenye uma mkononi mwake. Uma ulikuwa umetapakaa damu nyingi.
Akashtuka.
Alikuwa kichaa gani! Ingawa alikuwa amemchoma kisu mwilini, angeweza kuendelea kumbusu kwa muda mrefu. Je, maumivu hayakuwa kitu kwake?
Alvin akavua fulana yake pale juu. Alipogeuka na kujitazama kwenye kioo, aliona matundu manne nyuma ya bega lake ambapo damu ilikuwa ikitoka.......ITAENDELEA.......
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA..
