JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................437-438
Sura ya: 437
Lisa aliamka siku iliyofuata huku tumbo likiwa limechafuka kidogo kutokana na hungover za bia alizokunywa jana yake usiku. Alipoinuka na kunawa uso, alipokea simu kutoka kwa Alvin. Sauti yake ilikuwa chini na kali. “Ulienda wapi jana usiku?”
"Nilikuwa na jambo la kufanya na rafiki ..."
"Jambo gani la kunywa naye kwenye baa?" Alvin aliuma meno yake na kusema kwa huzuni, “Ingia mtandaoni usome habari zinazokuhusu, Lisa, nakuja baada ya dakika kumi. Afadhali unipe maelezo ya kueleweka.”
Kisha, akakata simu.
Lisa alishtuka na kutumia simu yake kutafuta habari hizo. Habari za hivi punde zaidi zilisema: [Mrithi wa Ngosha Corporation akizungumza na kucheka na mpenzi wake wa ajabu, wakionekana kuwa karibu sana.]
Picha hiyo ilikuwa ya Logan na umbo lake lilizofifia kwenye mwanga mdogo wa baa. Aliyakodoa macho yake na kuyapapasa. Kwa bahati nzuri, uso wa Logan haukufunuliwa, vinginevyo, ingekuwa shida.
Baada ya yote, Logan ndiye msaidizi wake pekee ambaye angeweza kumwamini kabisa.
Alikuwa ametoka tu kubadilisha nguo zake wakati aliposikia mtu akibisha mlango kwa nguvu. Alipofungua mlango, uso wa kutisha wa Alvin ulileta ubaridi wa kutisha.
“Ni nani huyo mtu?” Alvin alikuwa akipandisha kichaa kwa hasira. Alimjali sana na kumshikilia kila wakati, lakini alimzunguka na kwenda kwenye baa na mwanaume mwingine. Jambo lililo baya zaidi ni kwamba aliweza kutambua kupitia kwa mgongo wa mtu huyo kwamba hakuwa na sura mbaya. Mwili wake ulikuwa mzuri pia. Haikuwa rahisi kwake kumuondoa Kelvin na Erick Malugu, na sasa kulikuwa na mtu mwingine wa kumuumiza kichwa.
Alvin akamshika mabega kwa hasira. “Lisa Jones, huwezi kunipa amani ya akili? Utakufa usipochokoza wanaume kutwa nzima? Au unamaanisha siwezi kukuridhisha?”
Mabega ya Lisa yalimuuma kutokana na mkandamizo wake. Alipomtazama mwanaume aliyekuwa mbele yake, maneno ya Logan jana yake usiku yakamjia kichwani. Alipaswa kudhibiti hisia zake. "Alvin Kimaro, nilikubali kuwa nawe, lakini huwezi kunizuia kuwasiliana na watu wa jinsia tofauti."
Uso wake ulijawa na hali ya kutojali, tofauti kabisa na sura ya aibu na haya aliyokuwa nayo kitandani jana yake. Alvin alihisi ndoo ya maji ya baridi inamwagiwa na kumtuliza.
"Lisa Jones, kwa kuwa uko pamoja nami, kujitenga na watu wa jinsia tofauti ndiyo kanuni ya msingi ya kuwa mpenzi wangu." Alvin alisema kwa uso wa baridi, “Nilikuruhusu utoke jana, lakini ukatoka na mtu asiyejulikana. Unanichukulia mimi kama nani?”
"Nimekwambia kuwa ni rafiki tu. Ikiwa hutaki kuniamini, basi hakuna ninachoweza kufanya." Lisa aligeuka na kutoa maziwa kwenye jokofu bila kujali.
Alvin alimkazia macho mgongoni. “Usiponipa maelezo yaliyoshiba, nitamchunguza mtu huyo na kujua yeye ni nani.” Kisha, akageuka kwa hasira na kutoka nje.
“Subiri,” Lisa alimwita huku sauti yake ikipanda kwa hasira. “Umemaliza? Unachunguza watu walio karibu nami kama nani yaani?
Wewe ni mume ni wangu? Ulimchunguza Erick hapo awali na sasa unamchunguza mtu mwingine. Alvin Kimaro, usiponipa heshima hata kidogo, basi tutaachana.”
Alvin alishtuka. Uso wake ulikuwa umejawa na uhasama na alikuwa na hasira sana hadi akaupiga mlango kwa ngumi, huku akitoa sauti nzito ya mguno. Lakini, Lisa alimimina tu kikombe cha maziwa na uso uliotulia, bila kuathiriwa kabisa na hasira yake.
Kwa muda, Alvin alishtuka kidogo. Alikuwa amekasirika waziwazi, lakini kwa nini Lisa hakumfariji kwa upole, au kujielezea? Maadamu angemsihi na kuahidi kutotoka na mtu wa jinsia tofauti siku zijazo, angeweza kujilazimisha kumsamehe.
Lakini, mtazamo wa mwanamke huyu ulikuwa wa kiburi sana.
"Lisa Jones, sidhani kama unatambua, lakini kwa kuwa wewe ni mwanamke wangu, si rahisi kuachana. Nitakutupa mbali ikiwa sikutaki, lakini haiwezekani wewe kuanza kuniacha.” Kisha akaufunga mlango kwa nguvu na kuondoka zake.
Chumbani, Lisa alimpigia Logan kinyonge. "Ulipigwa picha na mtu kwenye baa. Jifiche kwa sasa na usijionyeshe hadharani. Nitawasiliana nawe ikiwa chochote kitatokea."
Siku iliyofuata, Alvin hakuwasiliana naye. Lisa alikwenda kwenye jumba la familia ya Ngosha ili kumsalimia Lucas. Alipofika, Lucas alikuwa akicheza na seti ya Lego Star Wars.
"Babu alikununulia hii?" Lisa alitazama sanduku. Ilikuwa toleo ndogo, kwa hivyo ilikuwa ghali kabisa.
“Anko Kelvin alinipa. Alikuja shule ya chekechea kuniona jana.” Lucas alitazama juu na kutabasamu, akifunua safu ya meno ya lulu.
Lisa alishangaa. Alijua kuwa Lucas alitabasamu mara chache, lakini sasa alikuwa akicheka kwa sababu ya zawadi ya Kelvin. Ilionyesha kwamba alikuwa akiipenda sana zawadi hiyo.
Kelvin alikuwa hivyo kila mara. Alikumbuka kile watoto wale wawili walipenda, na alikuwa mpole na msikivu.
Moyo wake ukawa mzito ghafla.
Alijua kwamba Kelvin alikuwa akimfuatilia kimyakimya kwa nyuma. Aliogopa kuvuruga mpango wake na mara chache sana aliwasilina naye.
"Lucas, unampenda Anko Kelvin sana?" Lisa aliuliza kwa upole.
"Mama, najua kwamba anakupenda na atakuwa mwema kwangu," Lucas alisema kwa uzito. “Jambo muhimu zaidi kwangu ni kwamba Mama atakuwa na furaha na hataumia.” Lisa aliinamisha kichwa chini na kubusu paji la uso la mwanae.
Joel alikuja huku akitabasamu. “Lucas ndiye mtoto mwenye busara zaidi ambaye nimemwona. Ana akili sana tofauti na umri wake.”
“Ndiyo.” Lisa alikigusa kichwa cha mwanae. "Baba, unajisikia vizuri?"
"Chembechembe za sumu ziliondolewa hivi majuzi, kwa hivyo sasa najisikia bora zaidi." Joel akahema. “Nilienda ofisini jana na nikagundua kuwa babu yako alichukua nafasi ya kuongoza. Alitaka nifanye mazoezi nyumbani kwa muda na akasema kwamba angetazama kampuni. Bila kuficha, lazima awe amejazwa upepo na Damien. Babu yako hata alikubali kuanzisha ubia na Kampuni ya Campos. Sina hisia nzuri kuhusu hili…”
"Baba, ukiniuliza, unapaswa kuwaacha wafanye wapendavyo," Lisa alisema kwa unyogovu. “Uza tu hisa zako na uachane na kampuni ya Ngosha. Afya yako itakapokuwa bora, unaweza kuanzisha kampuni nyingine peke yako.”
Uso wa Joel ulizama. “Lisa, Ngosha Corporation ni moyo na roho ya Baba. Nilitumia muda mwingi wa maisha yangu kuijenga kampuni hiyo…”
“Baba, nitakuwa mkweli. Sina matumaini kuhusu ushirikiano wa Campos na Ngosha. Nilisikia kidogo kutoka kwa Alvin. Familia ya Campos ni bora katika kujifanya dhaifu, lakini wanataka kuipita familia ya Kimaro na kuwa familia kuu nchini. Nadhani anataka kutumia familia ya Ngosha kama hatua.” Lisa alieleza, “Fikiria jambo hilo. Kuanzisha kampuni ya ubia. Familia ya Ngosha haijui chochote kuhusu biashara ya fedha na haina timu inayojulikana au wataalamu. Hatutajua jinsi familia ya Campos itakavyobadilika katika siku zijazo.
“Zaidi ya hayo, babu amerudi na kujihusisha na mambo yote ya kampuni. Damien na Melanie ni sawa tu na wanahisa wake. Ikiwa unataka kupata udhibiti tena, huwezi kupambana na Damien tena. Ukigombana na babu, na mambo yakienda kusini, utaitwa mtu asiyefaa.”
Uso wa Joel ukawa mzito. Aliona hilo likija. Ubaridi ulikimbia chini ya uti wa mgongo wake huku akifikiria juu ya kile baba yake alichofanya. Damien na binti yake walifanya mambo mengi sana ili kumdhuru Joel, lakini bado baba yake aliwasamehe.
Lisa aliongeza, “Ikiwa ni lazima niseme, thamani ya soko ya Ngosha Corporation iko juu sasa, na hisa ziko katika bei kubwa zaidi.
Kuziuza mapema ni wazo bora. Baba, wakati mwingine, kung’ang’ania kitu ni kujikosehsa fursa ya mafanikio. ”
“Labda uko sawa…” Joel alishangazwa na maneno yake kwa muda na akaugua kwa huzuni.
Lisa alipoona anasitasita akasema, “Baba ukishindwa niachie mimi hili jambo. Baada ya yote yaliyotokea, huelewi? Unathamini sana mapenzi. Mapenzi yako kwa Nina, upendo wako wa kindugu kwa Damien, na upendo wako kwa Bibi na Babu. Kama si wote hao, je wewe na mama yangu mngeanguka hadi mlipo leo? Niambie kwa uaminifu. Una furaha?"
Joel alitabasamu kwa uchungu. Angewezaje kuwa na furaha? Tangu alipogundua kuwa Melanie hakuwa mtoto wake, alijuta kila dakika.
Watu hao walimchukulia kama mpumbavu na kumuumiza na hakukuwa na msamaha wa dhati hata kidogo.
“Sawa, Lisa. Nitakuachia hili.” Joel aliitikia kwa kichwa. "Nitakabidhi haki zangu zote kwako."
"Baba, unapoanzisha kampuni mpya, bado unaweza kufungua mipaka mipya na kikundi cha watu ambao ni waaminifu kwako." Lisa alimkumbusha. “Lakini usiweke jambo hili hadharani. La sivyo, Bibi na Babu watakasirika wakijua.”
Sura ya: 438
Siku iliyofuata, Lisa aliunda kamati ndogo ofisini kwake ili kufuatilia habari fulani katika mzunguko wa biashara.
Muda mfupi baadaye, Amba alimletea habari hiyo. “Mwenyekiti Jones, Bwana Kawada kutoka Delta Co., Ltd. nchini Japani anavutiwa sana na Ngosha Corporation. Kwa bahati mbaya, anasafiri kwa ndege kwenda Afrika Kusini leo kuhudhuria maonyesho ya kimataifa ya sanaa ya Afrika Kusini.”
"Kawada anapenda sanaa?" Lisa aliinua uso wake.
"Ndiyo, Bwana Kawada anavutiwa sana na picha za kubuni," Amba alielezea.
“Nikatie tiketi ya ndege. Nitasafiri kwa ndege hadi Johannesburg leo. ”
Lisa alisema mara moja.
•••
Ndani ya Kampuni ya KIM International, Saa mbili usiku, taa katika ofisi ya Alvin ilikuwa bado inawaka. Wale waliokuwa katika ofisi ya sekretari walipiga miayo na kumtazama Hans kwa kusihi. “Hans, tafadhali umsihi bosi asichelewe sana na kuturuhusu twende nyumbani mapema. Hatuwezi kuvumilia tena.”
"Unasema hivyo kama naweza." Hans alitaka kulia.
Alichukua picha ya nyuso za huzuni za kila mtu ndani ya idara ya sekretari na kuzituma kwa Lisa. [Bi. Jones, unaweza kumshawishi Bwana Kimaro asifanye kazi ya ziada kwa kuchelewa sana? Tunataka kwenda nyumbani. PS: Tulifanya kazi ya ziada hadi saa saba usiku jana.]
Lisa alijibu: [Mmemwendekeza, komaeni tu. Sijawahi kuwalazimisha wafanyakazi wangu wanisubiri kila wakati ninapofanya kazi saa za ziada.]
Hans: [Sio kila mtu ni mzuri kama wewe.]
Lisa: [Niko busy. Nina safari ya ndege, kwa hivyo ninazima simu yangu.]
Hans akaingiwa wazimu kusikia Lisa hakuwa Nairobi tena. Haraka akaangalia mashirika ya ndege. Dakika kumi baadaye, aligonga mlango wa bosi wake. “Bwana Kimaro…”
“Usinisumbue,” Alvin alionya kwa ukali na kuchukua simu yake na kuitazama. Jamani. Mwanamke huyo alikuwa hata hajampigia simu kumwomba msamaha bado? Je, alikuwa akimfanyia mjinga? Je, hii ilikuwa malipo kwa nyakati hizo ambapo alimkosea walipokuwa kwenye ndoa hapo awali? Alipofikiria uwezekano huo, moyo wake ukaingiwa na maumivu makali.
"Hapana, Bwana Mkubwa. Nilitaka kukujulisha kwamba Bi Jones alichukua ndege hadi Johannesburg. ” Hans alisema kwa unyonge.
Alvin ghafla akaketi kwenye kiti cha ngozi na kumtazama kwa macho makali. “Anaenda huko kwa ajili ya nini?”
"Kuna maonyesho ya sanaa ya kimataifa huko kesho. Pengine yupo kuhudhuria.”
Alvin alikasirika. Sio tu kwamba Lisa hakumwomba msamaha, hata alienda kuhudhuria maonyesho ya sanaa nje ya nchi bila kumuaga? Vizuri. Vizuri sana, Lisa Jones.
"Sawa, ulijuaje kwamba alienda huko?" Alvin aliuliza kwa ukali ghafla.
“Nilimtumia ujumbe wa WhatsApp. Yeye…”
“Unayo WhatsApp yake?” Alvin alimkazia macho Hans. "Na ulizungumza naye kwa faragha?"
Hans alishuka. “Kama msaidizi wako, niliongeza WhatsApp ya Bi Jones kwa manufaa yako. Kwa mfano, unapokasirika, naweza kumwomba akufariji.”
“Lakini sijafarijiwa naye kwa sasa.” Alvin alikoroma kwa ukali. "Je, alikuambia kwamba anaenda Johannesburg?"
"Alitaja, lakini mimi ..."
“Najua. Alitaka kunieleza kuhusu jambo hili kwa kutumia mdomo wako.” Alvin alicheka kwa kujifariji. “Anafikiri ningekuwa na wasiwasi akiondoka Nairobi. Anaweza kuendelea kuota.”
Hans alikosa la kusema.
Alishuku kuwa Alvin alikuwa akiwaza sana.
“Nikatie tiketi ya ndege sasa hivi. Ninaenda Johannesburg usiku wa leo.” Alvin aliamuru ghafla.
"Utaenda ... kumfuata Bi Jones?" Hans alipigwa na butwaa na kushtushwa na maamuzi yake ya ghafla.
"Bila shaka hapana. Nitaenda kununua baadhi ya kazi za sanaa, inaelekea Lisa anapenda sanaa. ” Alvin alinyanyuka na kufungasha vitu vyake.
Hans alitamani kulia. Tayari muda ulikuwa umekwenda sana, hata hivyo ilimbidi aandamane na Alvin hadi Johannesburg. Kihelehele chake kilimponza. Kuwa msaidizi wabosi kama Alvin kulichosha sana.
•••
Usiku, Lisa alifikia katika hoteli ya nyota nne huko Johannesburg.
Kwa kuwa kulikuwa na watu wengi sana waliofika kutoka kote ulimwenguni kuhudhuria maonyesho hayo, hoteli nyingi nzuri zilichukuliwa mapema, kwa hivyo hiyo ndiyo ilikuwa hoteli bora zaidi ambayo angeweza kupata.
Baada ya kuoga alitoka kwenda kulala. Ghafla aliamshwa na milango ikigongwa kwenye chumba kilichofuata.
"Hawa watu wana wazimu? Kwanini wanagonga mlango kwa nguvu namna hii?” Lisa alifoka moyoni.
Chini ya dakika kumi baadaye, kulikuwa na muziki wa mdundo mzito wa ‘amapiano’ kwenye chumba hicho. Kulikuwa na kelele kiasi kwamba hakuweza kulala. Hakuweza kujizuia na kupiga simu mapokezi kulalamika.
Dakika tano baadaye, mhudumu wa mapokezi alimpigia simu na kumjibu. "Samahani bibiye. Wafanyikazi wetu walienda kumtafuta bwana huyo wa chumba jirani, lakini alisema kuwa muziki wake hauzidi decibel 50, ambacho ni kiwango kinachokubalika kisichoweza kusababisha kero. Hata polisi hawawezi kufanya lolote kuhusu hilo.”
"Inawezekanaje kuwa ni kiwango cha kawaida kwa kelele zote hizo?" Lisa alikasirika. “Sauti iko juu sana. Lazima iwe zaidi ya decibel 50."
“Tumepima. Ni decibel 49 tu."
Lisa alikosa la kusema. Jamani. Alikuwa akimfanyia makusudi au? Ni lazima awe mtu aliyeijua sheria vizuri.
"Unaweza kunibadilishia chumba changu?" Lisa aliomba.
"Samahani, hatuna vyumba vingine vilivyobaki."
Lisa aliumwa na kichwa. Alichoweza kufanya tu ni kuingiza tishu kwenye masikio yake kujaribu kupunguza sauti kuingia masikioni mwake. Mwishowe, hakuweza kulala vizuri usiku na aliendelea kuota ndoto mbaya.
Siku iliyofuata, aliamka mapema na kujipodoa vizuri kabla ya kuelekea kwenye maonyesho ya sanaa. Baada ya kuangaza sana kwenye umati mkubwa wa watu, hatimaye akamwona bwana Kawada. Alikuwa mtu wa miaka arobaini, lakini alionekana kijana sana.
Wakati huo, Bwana Kawada alikuwa akitazama picha kubwa ya michoro ya mtindo wa Tingatinga. Wajapani wanaipenda sana michoro hiyo.
Muuzaji alisema, “Hii ni michoro maarufu ya Tingatinga, na ni mkono halisi wa Said Tingatinga, mwanzilishi wa mtindo huo wa michoro. Ni hazina kubwa kabisa. Sikuiuza hata wakati mtu alitoa milioni 4 mara ya mwisho.”
"Naweza kuangalia kwa karibu?" Lisa akasogea na kuuliza huku akitabasamu.
Bwana Kawada akamkabidhi ile picha kubwa na kutabasamu.
"Je, mwanamke huyu anajua jinsi ya kutathmini kazi za sanaa?" Muuzaji aliuliza kwa wasiwasi.
"Najua kidogo." Lisa aliitazama na kutikisa kichwa. "Hii ni bandia."
"Haya, usizungumze ujinga." Muuzaji alimtazama kwa hasira. "Hujui chochote, msichana mjinga wewe."
Lisa aliashiria motifu ya joka kubwa na kusema, “Ikiwa ni mchoro halisi wa mwanzilishi wa mtindo wa tingatinga, ilipaswa kuwa imechorwa mwanzoni mwa miaka ya sitini kwani yeye alifariki mwaka 1965 au 1966 hivi kama sikosei. Ukitazama saini yake hapa inaonyesha picha hii imechorwa mwaka 1971. Ni mwigo mzuri lakini siyo kazi original ya Said Tingatinga. Natoa elfu mbili.”
Uso wa muuzaji ulikuwa mwekundu kwa aibu kwa madai ya Lisa.
Bwana Kawada alimkazia macho. “Ulitumia kazi bandia kunitapeli. Unafikiri mimi ni rahisi kudanganya kwa sababu mimi ni Mjapani?”
"Sio. Hata mimi sijui historia ya kweli ya Tingatinga.” Muuzaji alinyanyuka na picha mikononi mwake kwa aibu....ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
