JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................433-434

Sura ya: 433

“Rodney! Nilikukosea nini katika maisha yangu ya nyuma?" Pamela hakuweza kujizuia na kulaani kwa sauti ya chini.

“Walikufanya nini?” Rodney alizidi kukosa raha.

Pamela alikuwa karibu kuongea wakati mkono mkubwa uliponyakua simu yake. Alvin kisha akasema, “Yupo hospitalini. Njoo hapa umpeleke nyumbani.”

“Alvin…”

"Vyombo vya habari vinaripoti kuhusu mambo mabaya ya Erick Malugu na SE Group. Jinsi unavyochukua fursa hii ili kumtoa mpinzani wako barabarani itategemea wewe mwenyewe.
 Juu ya hayo, unapaswa kuchukua hili kama somo. Ikiwa una mtu ambaye ni faida kubwa kwa kampuni, unapaswa kuwa macho kwa usalama wake."
Alvin akakata simu na kumtupia simu Pamela kabla hajageuka na kurudi kwa Lisa tena.

Dakika 20 baadaye, ripoti ya vipimo vya damu ilitoka. Daktari alithibitisha kuwa walikuwa sawa na walihitaji tu kupumzika vizuri usiku. Wangeweza kurejesha nguvu zao kesho yake.

Alvin aliposikia hivyo mara moja akamnyanyua Lisa. “Tunarudi nyumbani.”

Lisa alimtazama Pamela kwa wasiwasi. “Na yeye…”

“Nipo hospitalini. Nitakuwa sawa. Ninyi wawili mnaweza kwenda. Rodney atakuja hivi karibuni.” Pamela alipunga mkono. "Mkiendelea kukaa hapa, Rodney anaweza kuishia kugombana nawe tena."

“Ndio. Yuko sawa. Sina mood ya kubishana naye pia. ” Alvin hakutaka pia kukutana na Rodney.


"Basi, kuwa mwangalifu. Asipokuijia, nipigie.” Lisa alipomaliza kusema tu, Alvin akambeba.

Pamela aliwatazama kwa huzuni na wivu kidogo. Alikuwa akifikiri kwamba marafiki wa kiume hawakuwa wa lazima, lakini sasa aliona ni vizuri kuwa naye.


Ilichukua dakika nyingine 20 kabla ya Rodney kuwasili. Alipomuona Pamela akiwa amelala kwenye kitanda cha hospitali mithili ya kiumbe laini, mwenye nywele zilizochafuka na kuvaa gauni la wagonjwa, alijiona kuwa na hatia kidogo.

“Alvin yuko wapi?”

"Ameondoka.”

“Nini kilitokea huko?” Rodney aliuliza.

“Wakati mimi na Lisa tukiwa kwenye saluni tukiosha nyuso na kucha, chumba kiliwashwa kwa udi na uvumba, wakaingia wanaume wachache, kwa bahati nzuri Alvin alitokea kama malaika mlinzi. Viinginevyo tungekuwa tumekwisha.” Pamela alivuta kola yake, akifunua nguo zake zilizochanika na alama za michubuko ndani. “Angalia.”

Rodney alikunja uso. Lakini, kama mtu mwenye pesa na mamlaka, kwa kweli hakuweza kujishusha na kumwomba msamaha. “Hiyo ni…Huwezi kunilaumu mimi. Kuna jambo jingine ulilomkosea Erick? Yeye si mtu mzuri kwanza. Uliwahi kumuahidi kitu kabla…”

"Rodney Shangwe, funga mdomo wako. Nilimkosea kwa sababu yako.”

“Kwa sababu yangu? Kwa sababu nimekupa faida kubwa? Kwa sababu nilikupa hisa za Osher Corporation?”

“Kama usingekuwa na mdomo mkubwa hivi, Erick asingejua kuhusu ushirikiano wetu na asingenisumbua usiku huu. Laiti ningejua Erick ameshajua kuhusu ushirikiano wetu, ningekuwa makini.”

“Ni kosa lako ulipokubali mwaliko wake… “

"Ikiwa ulikuja hapa kunifundisha, basi unaweza kuondoka." Pamela akashusha pumzi. Alikuwa hana nguvu hata hivyo.

“Sawa. Sahau. Sitagombana na mwanamke kama wewe. Nitakurudisha nyumbani.”

Rodney alinyanyua kitako chake na kumnyanyua ghafla. Hata hivyo, hakutarajia Pamela angekuwa mwepesi kiasi hicho.
 Akiwa ameshtuka, Pamela aliweka mikono yake shingoni mwake bila fahamu. Ishara hiyo ya karibu iliwafanya wote wawili kukosa raha, hivyo akaweka mikono yake chini haraka.

Baada ya Rodney kumtazama, alitoka nje huku akiwa amembeba. Kwa kila hatua aliyopiga, misuli ya mikono yake maridadi iliyokuwa nje ya shati lake la mikono mifupi ilijikunja kidogo. Pamela alikoroma. "Sikujuwa kuwa una misuli mikubwa hivi."

"Nyamaza. Ninafanya mazoezi mengi, sawa?" Rodney alidhihaki.

Wakati wa kurudi, muziki laini ulikuwa ukipigwa ndani ya gari. Kwa sababu ya uvumba wa kulevya aliokuwa ameuvuta hapo awali, Pamela hakuweza tena kuinua kope zake.

Walipofika Brighton Gardens, Rodney alisimamisha gari na kupaki, akawasha taa na kugeuka nyuma na kukuta Pamela amepitiwa na usingizi kwenye siti. Nywele zake ndefu zilifunika nusu ya uso wake, na nusu iliyobaki ilifunua ngozi yake nyeupe iliyong'aa chini ya mwanga. Kawaida alikuwa na ulimi mkali, lakini wakati huo, alikuwa kama paka mpole na asiye na madhara, dhaifu na laini.

Alisita kabla hajatoa bkoti lake ili kumfunika. Kisha, akaketi na kusoma habari kwenye simu yake.


•••
Alvin alipomfikisha Lisa nyumbani kwake, alimuweka kwenye kitanda kikubwa kilichokuwa chumbani humo. Hakuweza hata kufunua kope zake wazi na alilala kwenye gari wakiwa njiani kurudi nyumbani.

Baada ya Alvin kumtazama kwa utulivu kwa muda, aligeuka kuchukua beseni la maji na kuvua nguo zake taratibu. Alipoona mikwaruzo mwilini mwake, uso wake mzuri uligeuka kwa hasira. Hata hivyo, kadri alivyozidi kumvua nguo, uso wake haukuweza kujizuia kutokwa mate ya uchu kidogo.

Hakuwahi kumtazama Lisa kwa makini hivyo hapo awali. Alikuwa na umbo zuri sana. Alikuwa mdogo mahali alipohitaji kuwa mdogo, na mkubwa mahali ambapo alitakiwa pawe pakubwa. Mahali ambapo palitakiwa kujaa, palijaa sawasawa. Hakuzidi wala kupungua.

Akiwa kijana na mwenye nguvu, Alvin aliguna bila kutarajia, macho yake yakiwaka mwale wa uchu. Mara baada ya kumsafisha, alimvalisha pajama na kwenda kuoga maji baridi peke yake.

Alitumia taulo lake, ambalo lilikuwa na harufu iliyojulikana ya mwili wake. Ilikuwa nzuri sana. Baada ya kuoga, alijilaza na kulala pembeni yake kwenye shuka moja. Aliridhika sana na kunusa harufu ya mwili wake.
Kisha, hakuweza kupinga kumshika mikononi mwake.

Lisa hakuamka. Hata hivyo, alimsugua uso wake mdogo kifuani mwake na kumkumbatia kwa mikono yake ndogo. Kitendo hicho kilikuwa cha asili sana. Ilikuwa kana kwamba walikuwa wamefanya hivyo mara nyingi sana hapo awali.

Siku inayofuata.
 Lisa alilkuwa amelala wakati Alvin aliposhtuka asubuhi na mapema, lakini hakujisumbua kumuamsha mpaka muda ukaenda sana. Alipofungua macho yake, Lisa alikabiliwa na misuli ya kifuani yenye rangi ya asali. Harufu iliyojulikana ya kiume iliyochanganywa na jeli ya kuogea aliyoitumia ilipepea puani mwake. Je, alimkumbatia Alvin usiku mzima? Haraka akainuka, lakini mkono wa kiunoni ukamkaza na kumrudisha nyuma.

“Umeamka?” Akiwa ameamka tu, sauti ya mwanamume huyo ilikuwa chini na ya kina kama kinubi, na kuufanya moyo wake udunde kwa kasi.


Lisa aliinua macho yake na kumuona Alvin akiwa na sura nzuri na iliyotulia vizuri. Aliuma midomo yake na akasema kwa hasira, “Kwanini unalala kitandani mwangu?”

“Babe, ulikuwa umedhoofika sana jana usiku. Nilikuwa na wasiwasi sana kukuacha ulale peke yako.” Alvin alitoa kicheko cha chini. Alikuwa amechukua fursa hiyo kujihesabia haki ya kulala pamoja naye.

“Huna aibu!” Lisa alimlaani. Aliketi, lakini kwa kuwa alikuwa hajapona kabisa, mara moja akaanguka kwenye kifua chake tena.
"Bado hujapata nguvu?" Ghafla macho ya Alvin yalimchoma kana kwamba yalikuwa na miale ya moto. Alinyoosha mikono yake kumshika kwa nguvu.

'Si…” Lisa alijitahidi kwa muda mrefu lakini hakuweza kujinasua kwenye mikono yake. Badala yake, aliweza kuhisi macho ya mwanamume huyo yakizidi kuwa ya moto zaidi. Alikuwa anajua fika ni nini ambacho kingefuata.

“Niache niende. Sitaki ku...”

"Nimekukumbuka sana babe. Unataka nisubiri hadi lini?" Alvin alimpindua huku akiweka mikono yake yenye nguvu ubavuni mwake. Pumzi yake inayowaka ilianguka usoni mwake.

“Umesubiri kwa muda gani? Zimepita siku chache tu. ” Lisa aligeuka kwa kukataa. Alilegea sana hata hakuthubutu kumwangalia machoni.

Lakini, hakujua kuwa mkao wake ulikuwa ukimpa Alvin nafasi ya kuanzisha mashambulizi ya taratibu.

"Lisa, sisi ni wapenzi." Alvin aligeuza uso wake na kumbusu midomo yake.

"Hapana…" Lisa alijitahidi.

Licha ya hayo, mwanamume huyo alikuwa na nguvu nyingi sana, na alimfahamu vizuri sana. Mbali na hilo, kujua kutoka kwa Maya kwamba hakuwa amefanya hivyo na Sara kwa miaka mingi, kulimvua wasiwasi kwa sehemu kubwa.
 Lisa, ambaye awali alikusudia kuinuka, aliljilegeza kabisa na kumwacha Alvin afanye yake.

Sura ya: 434

Wakati huo huo, huko Brighton Gardens.

Pamela alipofumbua macho baada ya usingizi wa kuridhisha, alijikuta amelala kwenye siti ya nyuma ya gari huku akiwa koti zito mwilini mwake. Alikuwa ameduwaa na kuchanganyikiwa kwa muda kabla ya kukumbuka tukio la jana yake usiku. Rodney alipokuwa akimrudisha, hakuweza kuhimili tena na akalala ndani ya gari lake wakati.

Kwa maneno mengine, bado alikuwa ndani ya gari la Rodney. Koti zito liliwekwa juu yake na Rodney, na mto chini ya kichwa chake uliwekwa hapo na Rodney pia? Hisia za ajabu sana zilimjia moyoni.

Baada ya kumfanyia Rodney tukio lililomvunjia heshima majuzi kati, alidhani kwamba Rodney angemtoa nje ya gari au kutafuta watu wa kumlipizia kisasi. Lakini wala Rodney wa watu hakuwa na mawazo hayo tena.

Pamela aliamka, akakaa kwenye siti na kumuona mwanaume huyo akiwa ameegemea kiti cha dereva bila kutikisika. Rodney alikuwa amepumzika huku akiwa amefumba macho. Kweli alizaliwa na mwonekano mzuri. Alikuwa na pua ndefu, midomo myembamba, ngozi safi, macho mazuri, ambayo kama yangemtazama mwanamke bila papara, yangeweza kumvuta kwake kama sumaku.

Hapo awali, Pamela alidhani kuwa Patrick ndiye mwanaume mzuri zaidi.
Lakini, Patrick alibadilika kuwa duni sana kwa kulinganisha na sifa za Rodney.

Wakati huo, kope za Rodney zilicheza. Rodney alipapasa macho na kuzinduka. Alipogeuka, jozi mbili za macho zilikutana.
 Ghafla hakuhisi usingizi hata kidogo. “Hatimaye umeamka.”

“Kwa nini hukuniamsha jana usiku?” Pamela alijifanya kutojali.

"Ulikuwa umelala kama nguruwe…”

"Rodney Shangwe, unajua unachozungumza?" Pamela alilipuka papo hapo. "Je, kuna nguruwe mzuri kama mimi?"

“Ndio. Nilimuona mmoja jana usiku. Bado yuko kwenye gari langu sasa hivi.” Rodney alikodoa macho na kudhihaki.

“Potelea mbali.” Pamela alimpiga kofi dogo na kufungua mlango wa gari kuondoka.

Rodney alishusha dirisha na kusema, “Usijali, Erick Malugu amekamatwa. Kama huna maadui zaidi, unaweza kwenda nje kwa amani ya uhuru. Unapaswa kupumzika kwa siku mbili kabla ya kurudi kazini.

“Nipe pesa kwanza kisha tutazungumza.” Pamela alimkazia macho kabla hajapanda ghorofani.

Alipofika nyumbani, Pamela alipitia habari mtandanoni. Tukio la yeye na Lisa kuvamiwa jana yake usiku na watu wa Erick Malugu lilichukua nafasi kubwa mtandaoni. Watu waliwashambulia Erick Malugu, mkurugenzi wa SE Group, na baba yake Lincoln Malugu, ambaye ni mwenyekiti wa kampuni hiyo. Waliwashutumu kwa kutumia mbinu za kikatili kushindana kibiashara.

[Pia kuna kashafa kwamba Lincoln Malugu, baba yake Erick, mfanyabiashara mashuhuri wa vipodozi nchini Kenya, ametelekeza familia yake kwa ajili ya vimada]

[Mke wa Lincoln Malugu alilia na kumshutumu mumewe kwa kutorudi nyumbani kwa nusu mwaka na alikuwa hajawajalipia gharama za maisha.]

[Mke na binti mdogo wa Lincoln Malugu wanaishi katika nyumba kuukuu ya vyumba viwili vya kulala, huku vimada wake wakiishi katika majumba ya kifahari yenye thamani kubwa.]

[Erick Malugu naye anahisiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja na wanaume kadhaa huko ughaibuni. Hana mke na hana mpango wa kuoa.]

[Bei ya hisa ya SE Group imeshuka. Wanawake wanatangaza kwamba wanaacha vipodozi vya SE.]

Uvumi mbaya kuhusu Erick Malugu katika nyanja mbalimbali ulianza, na hata mama yake alihojiwa na vyombo vya habari kuhusu tabia mbaya na mumewe na mwanaye.

Tabia ya Erick na baba yake waliwakasirisha wanawake kote Kenya. Lincoln akiandamwa kwa tabia zake za kuendekeza michepuko na Erick akizomewa kwa tabia zake za ushoga. Wakati huo Erick alikuwa bado anachunguzwa katika kituo cha polisi.

Pamela alipoisoma, alifurahia kwa siri jinsi Alvin na Rodney walifanya haraka. SE Group ilipata pesa kutoka kwa wanawake lakini haikuwaheshimu wanawake. Zaidi ya hayo, Erick alikuwa ametumia njia zisizofaa kuwakandamiza wenzake. Ingekuwa vigumu kwa SE Group kurudi barabarani.

Aliwaza na kumpigia simu Lisa. Simu iliita, lakini hakuna aliyepokea.
Mpaka mchana ndipo Lisa alimpigia simu tena. "Rodney alikurudisha nyumbani jana usiku?"

“Umezidi sana. Nilikupigia simu asubuhi, lakini unajibu mchana? Siyo kawaida yako.” Pamela ghafla aligundua kitu na kucheka. “Mbona sauti yako imelegea hivi?"

“Unaongea upuuzi gani? Nilikuwa nimelala, sawa?" Lisa alimtazama Alvin pale kitandani kwa mshtuko.
 Kisha, kwa haraka akaburuta miguu yake yenye maumivu na kutoka nje.

"Ni sawa, Alvin alitumia gharama kubwa sana kunihamisha, wacha ajilie vyake ..." Pamela alitania na kucheka.

"Acha kufikiria ujinga basi!" Lisa akamkatisha kwa umakini.

“Nasikia harufu ya mapacha wengine," Pamela alimtupia dongo la mwisho na kuhamisha mada. "Nililala kwenye gari la Rodney jana usiku na kwa bahati mbaya nililala hadi asubuhi."

Lisa alipigwa na butwaa. “Hakukutupa nje? Alikuacha ulale mpaka asubuhi? Hujapata homa?"

“Ndio. Ndivyo nilivyofikiria pia. Sikutarajia pia. Hakuniamsha na hata akanifunika koti lake,” Pamela alisema kwa hisia tofauti.

“Sikujua kama anaweza kuwa mtu mzuri hivi. Anaweza kupika, na yuko makini. Kama si kutuchukia kwa sababu ya Sarah, Rodney angechukuliwa kuwa mtu bora. Kwa bahati mbaya, alimpenda mtu mbaya. Ana jicho baya kwa wanawake," Lisa alisema kwa majuto. "Huna mapenzi naye, sivyo?"

"Shindwa pepo!." Pamela mara moja akakemea.

“Mbona unamuwazia sana?” Lisa alibonyeza ulimi wake na kukumbusha, “Lakini lazima nikukumbushe. Usijaribu kumpenda Rodney. Patrick ameshakufanya uteseke vya kutosha. Ikiwa utaangukia kwa Rodney, utateseka kuliko hapo awali. Mtu huyo ana macho kwa Sarah tu."

“Si lazima uniambie hivyo. Najua kuliko wewe.” Pamela mara moja akakata simu.

Lisaaliitazama ile simu huku akiwa na wasiwasi kidogo. Kulingana na miaka aliyoishi na kumfahamu Pamela, haikuwa kawaida kwa Pamela kumsifu mwanaume. Lazima kulikuwa na kitu ndani yake.

Alipokuwa ametekwa na mawazo hayo, mkono wa mwanamume ulikuja kutoka nyuma na kumshika kwa nguvu. Alishtuka Alvin akimuuma sikio.

"Rodney ni mtu mzuri?"
Lisa alitetemeka ghafla na kugeuka huku akitaka kumwangalia. Lakini, Alvin alifunga midomo yake. "Mzuri kuliko mimi?"

"Alvin Kimaro. Swali gani hilo?”

"Unamsifia mtu mwanaume mwingine, unadhani mimi nitajisikiaje?" Alvin alifoka kwa maumivu, macho na sauti yake ilikuwa na uchungu.

Lisa alikosa la kusema. “Nimesema kitu kibaya? Nilikuwa nikifikiria kuwa Rodney hakuwa na maana isipokuwa sura yake, lakini ikawa kwamba ana pointi nzuri pia."

“Amekunyanyasa sana hapo awali…” Alvin aliuma meno yake na kumkumbusha. Ilimkera sana kusikia mwanamke aliyempenda akimsifu mwanaume mwingine.

“Wewe hujawahi kuninyanyasa?” Lisa alimkumbusha. "Afadhali usiseme kwamba wengine ni wabaya, au nitaibua maudhi yako ya zamani tena."

Alvin akaachana nayo. Alizika uso wake mzuri kwenye shingo yake kimya. “Babe, nina njaa.”

Lisa alicheka. "Ni bahati mbaya. Nina njaa, pia. Sina hata nguvu ya kupika kiamsha kinywa, na sasa mwili wangu umedhoofika.”

“Nitakupikia.” Alvin alimwambia kwa upole. “Lakini kinaweza kisiwe kitamu kama chako. Usijiepushe nayo.”

“Kama kweli huwezi, basi pika mayai tu. Au na yenyewe yatakushinda?”.....ITAENDELEA...

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.