JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................401-402

Sura ya: 401

Alvin alikaa peke yake kwenye kiti cha ofisi kwa muda mrefu hadi mlango ukagongwa. Kisha, kichwa kidogo cha Suzie kikaingia kutoka nje. "Anko, naweza kuingia?"

Ingawa Alvin alikuwa katika hali mbaya, moyo wake ulibadilika mara moja baada ya kumuona yule mtoto akiwa makini na mwenye shauku ya kutaka kuongea naye.

“Suzie, si ulienda shule ya awali leo?” Alvin aONA bado amevaa sare nyekundu ya shule ya awali.

Suzie aliinamisha kichwa chake na kusema. "Bibi alisema una hali mbaya, kwa hivyo nimekuja kukufariji."

Moyo wa Alvin ukapata joto ghafla. Hakutarajia Lea angemjali hata kwa wakati kama huo.

"Uncle, hii ni kwa ajili yako." Suzie alikimbia na kupanda kwenye mapaja yake. Alifungua kiganja chake, akifunua kipande cha chokoleti ndani yake. "Kila wakati nikiwa katika huzuni, nitaacha kulia baada ya kula chokoleti."

Alvin alimtazama na kutabasamu. Kisha, msichana mdogo alifunua chokoleti na kuitia kinywani mwake. Alvin mara chache alikula pipi, lakini wakati alipouma kipande cha chokoleti, kilikuwa kitamu.

"Uncle, unajisikia vizuri sasa?" Suzie alimtazama kwa macho ya kumetameta.

"Vizuri zaidi. Asante, Suzie.” Akamsugua kichwa kidogo.

“Mmh. Anko, mwili wako… unanuka!” Suzie alisema ghafla kwa sura ya kuchukiza.

Alvin aliganda. Hakuwa amelala sana katika siku mbili zilizopita, hata kuoga. “Nimekuwa… nimekuwa bize na kazi siku hizi na kusahau kuoga. Nisubiri hapa. Nitaenda kuoga mara moja sasa. ” Alvin kwa shida akamuwashia Suzie TV.

“Sawa.” Suzie aliketi kwenye sofa kwa utii na kuangalia katuni.

Alvin aliingia kwenye bafu lillilo katika ofisi yake. Alijiosha kuanzia kichwani hadi miguuni. Alibadilika na kuvaa suruali nyeusi na shati jeupe. Alitoka na mwonekano wa kupendeza na wa kifahari.

Macho ya Suzie yakaangaza. “Anko wewe umekuwa mzuri sana. Twende kwenye miadi.”

Alvin alishindwa kujizuia kucheka. "Wewe mpuuzi mdogo, unajua hata miadi ni nini?"

"Niliiona kwenye TV. Watu kwenye TV huwa wanaenda kwenye miadi." Suzie alicheka. "Twende kwenye amusement park. Nataka kwenda kucheza."

“Sawa.” Alvin alikubali bila kufikiria.

Kwa kweli, pia alikuwa ameona kuwa inachosha sana kufanya kazi mfululizo kila siku. Hata hivyo, hakutaka kwenda nje kukabiliana na Rodney na Chester. Ikiwa asingekuwa Suzie, angependa kutumia wakati wakati wake peke yake.

Alipoendesha gari kuelekea kwenye uwanja wa burudani wa Two Rivers Theme Park, simu ya saa ya Suzie iliita. Mama yake alikuwa amemnunulia simu ndogo ya saa ambayo ilikuwa ikipokea na kupiga simu kutoka kwa Lisa tu. Sauti ya kupendeza ya kike ilisikika. “Suzie, nipo getini. Uko wapi?” Ilikuwa sauti ya Lisa.

Moyo wa Alvin ulirukaruka. Aligeuka nyuma kumwangalia Suzie na kumuona akiinamisha kichwa chini kumwambia kujibu sauti ile kwenye saa yake, “Tupo kwenye gari. Tutafika hapo sasa hivi.”

Baada ya simu kuisha, Alvin aliuliza haraka. “Umemwalika Aunty Lisa?”

“Ndiyo.” Suzie alitikisa miguu yake.

“Kwanini hukuniambia mapema?” Alvin alikasirika.

"Hata Aunty Lisa hajui kama nipo na wewe, anajua kuwa nipo na baba." Suzie alitoa ulimi wake nje. “Bibi alisema mmeachana na Aunty Sara, kwa hiyo nikamuuliza baba wanaume wanapaswa kufanya nini wanapoachana. Baba alisema kuwa jambo bora kwa mwanaume baada ya kuachana ni kutafuta mke mwingine. Mtu mwingine ninayemfahamu ni Aunty Lisa.”

Alvin alikosa la kusema. Kweli? Alionekana kwamba machoni pa wengine alikuwa ameachana? “Um… kwa hiyo wewe ukamkaribisha Aunty Lisa na alikubali kirahisi hivyo?”

“Ndiyo.” Suzie aliitikia kwa kichwa. “Kwa sababu nilimdanganya na kumwambia nilikuwa na Baba.”

Alvin akaishiwa pozi. Ilibainika kuwa mwanamke huyo alikubali kwenda kwenye uwanja wa burudani kwa sababu tu… ya Jack? Je angemwambia kwamba alikuwa na yeye angekubali? Alvin alikasirika kwa siri. Lisa bado alikuwa naye moyoni.

“Kwa hiyo ungemwambia kuwa upo na mimi asingekubali?” Alvin aliuliza ghafla.

“Ndiyo.” Suzie alipiga kelele. “Nilimwambia Aunty Lisa kuwa nataka unipeleke kwake kwa chakula cha jioni kwake, lakini akasema nikiwa na wewe hataniruhusu niende kwake. Alisema kwamba anakasirika akikutazama tu.”

Mara Alvin alihisi moyo wake ukimuuma kwa hasira. Je! msichana huyu alikuwa akijaribu kumfariji au kumkasirisha? “Kwanini basi unataka nimuoe mtu anayenichukia?”

“Nilifanya jambo baya?” Suzie aliinua midomo yake alipoona hasira usoni mwake. “Basi nitampigia baba simu na kumwambia aje. Anko, unaweza kurudi.”

"Uliniita hapa na sasa unaniambia nirudi?" Alvin alihisi kana kwamba kisu kilikuwa kikimpasua moyoni. Msichana huyo alianza kumkera.

“Siwezi kumwambia Aunty Lisa arudi. Yeye ni mwanamke.” Suzie alimuangalia bila hatia.

Alvin alikosa la kusema. Msichana huyo alipokaribia kupiga namba ya Lisa kwenye saa yake tena, Alvin alitamka, “Acha, usipige. Tayari nimeshawasha gari kwa hiyo sitaweza kurudi.”

“Kwa hiyo upo tayari kuchumbiana na Aunty Lisa?” Uso wa kitoto wa Suzie ulionyesha dokezo la ucheshi.

“Uchumba gani? Usiseme ujinga. Ninakusindikiza tu kwenye uwanja wa burudani."

Safari nzima ikawa ya kimyakimya hadi wakafika kwenye viwanja vya burudani vya Two Rivers Theme Park, Limuru Road jijini Nairobi. Baada ya Alvin kuufungua mlango na kushuka chini, alijitazama kwenye kioo cha dirisha. Kwa bahati nzuri, alikuwa ameoga kabla ya kutoka nje. Kasoro pekee ni kwamba, shati lake halikupigwa pasi ipasavyo.

Alichomekea shati lake kwenye suruali kwa haraka huku akijitazama dirishani. Kisha akazitazama ndevu zake ambazo hazikunyolewa. Hakuwa amepumzika vizuri siku hizi mbili, hivyo miacho yake yalikuwa yamevimba kidogo pia.

Mlango ukafunguliwa ghafla na Suzie akatoka akiwa amekunja mikono yake kiunoni. "Anko, mbona unajitazama kwenye dirisha?"

“Shati langu lilikuwa limekaa vibaya kwa hiyo nilikuwa naliweka sawa. ” Alvin akapunguza sauti yake na kubadilisha mada. “Angalia, kuna peremende pale. Nitakununulia moja.”

“Sawa! ” Suzie alikengeushwa kwa mafanikio.

Dakika tano baadaye, wawili hao hatimaye walitembea hadi kwenye mlango wa bustani ya burudani. Kabla hawajafika, tayari Alvin aliiona sura ya Lisa pale getini. Alikuwa amevaa jeans na fulana nyeupe, pamoja na jozi ya viatu vyeupe. Nywele zake ndefu nyeusi zilivutwa na kufungwa nyuma kama mkia wa farasi. Kwa sura yake nzuri, alionekana mrembo kiasi kwamba Alvin hakuweza kung'oa macho yake kutoka kwake.

Hapo hapo, Alvin aONA wanaume kadhaa wakimtazama. Kijana aliyefanana na mwanafunzi wa chuo kikuu alisimama mbele yake ili kuanzisha mazungumzo. "Dada, naweza kukuongeza kwenye WhatsApp?"

Chini ya mwanga wa jua, uso safi wa kijana huyo ulionekana wenye haya. Lisa alishtuka. Alikuwa karibu kutabasamu na kukataa, lakini sauti ya chini na ya sumaku ilisikika ghafla. “Mke, samahani kwa kuchelewa.”

Kijana huyo aligeuka nyuma na kuiona sura ya Alvin, nzuri na yenye heshima. Hakutarajia Lisa angekuwa ameolewa kwani alionekana mdogo sana. Mtoto wao pia alikuwa mkubwa. “Mimi… samahani. Sikujua kama umeolewa. Samahani kwa kukusumbua." Yule kijana aligeuka haraka na kukimbia baada ya kuongea.

Lisa alimkazia macho yule mtu aliyelaaniwa ambaye alitokea ghafla. “Mke wako ni nani? Afadhali uangalie mdomo wako."

"Ndio Anko, tangu lini Aunty Lisa akawa mke wako?" Suzie aliuliza kwa udadisi huku akila pipi yake.

“Niliogopa kwamba angedanganywa na wavulana hao wadogo wa chuo.” Alvin alionyesha dharau ya ndani kabisa. “Lisa Jones, una miaka mingapi? Je, huoni aibu kutabasamu kwa wavulana wadogo kiasi hicho? Je, unajua maana ya neno ‘kujiheshimu’? Unataka kuwabemenda vijana wadogo?”

“Nina umri wa miaka 26. Mvulana huyo anaweza kuwa na umri wa miaka 20. Nitambemendaje?” Lisa alimrukia kwa maneno ya hasira. "Kuna wanawake wakubwa wanaoolewa na vijana wadogo kila mahali sasa hivi, pole!"

“Kwa hiyo unatamani kuolewa na kijana mdogo, sivyo?” Hewa karibu na Alvin ilikua na joto ghafla.

Lisa alikunja mikono yake na kudharau, “Kwa hiyo ni sawa kwa mwanamume mkubwa kuoa binti mdogo na siyo kinyume chake? Wewe si ni mkubwa kuliko mimi? Ulipokuwa shuleni, hata sikuwa nimetungwa mimba. Mbegu za baba yangu zilikuwa bado hata hazijatarajiwa kukutana na yai la mama yangu.”

Alvin aliduwaa. "Lisa Jones, afadhali ufikirie kabla ya kuongea. Kumbuka kwamba kuna mtoto hapa."

Lisa akabadili mada haraka haraka. “By the way, mbona upo na Suzie? Jack yuko wapi?" Lisa alimtazama ghafla Alvin kwa unyonge.

Sura ya: 402

“Kwa hiyo mimi sijakaribishwa mahali hapa? Au ndo umem’miss Jack kiasi hicho?" Tabia yake ilimfanya Alvin kuwa na hasira.

“Jack ni mwokozi wangu. Kwa upande wako wewe ni mwanaume ambaye tayari una mwanamke mwingine.” Lisa alidhihaki, “ Ninaogopa kushtakiwa kwa ugoni ikiwa nitapigwa picha kwa bahati mbaya na mapaparazi nikiwa na wewe. Kwani, mradi kuna jambo lolote linalomuumiza mpenzi wako Sarah Njau, hutasita kusukuma lawama kwangu.”

Alvin alihisi huzuni kwa kukosolewa kwake. Alijua kwamba alikuwa amefanya mambo mengi ya kumuumiza kwa sababu ya Sara zamani. "Mimi na Sarah hatutafunga ndoa."

"Unatania?" Lisa aliinua kichwa chake makusudi kwa mshangao. “Si utafanya harusi nyingine? Je! yale ambayo polisi walisema ni kweli? Alifanya hivyo na mwanamume mwingine - "

"Lisa Jones," Alvin alimkatisha kwa ukali na jeuri. Sauti yake ililipuka kama ngurumo.

Suzie aliogopa sana hata mkono wake ukatetemeka na ile pipi ya bigboom ikaanguka chini. Kisha, akaanza kulia. “Anko unamtisha Aunty!” Alijificha nyuma ya Lisa kwa hofu.

Lisa haraka akamchukua msichana yule mdogo. Alipoona machozi ya Suzie, alimtazama Alvin kwa hasira.” Sarah ndiye aliyekusaliti, mbona unanikaripia mimi tena? Nenda kamkoromee Sarah kama una uthubutu. Unapenda tu kunifokea kila wakati. Potelea mbali. Nitaache na Suzie wangu. Kampani yako haihitajiki.” Kisha, akambeba Suzie hadi kwenye uwanja wa burudani.

Alvin aliyebaki nyuma alikunja ngumi kwa kuudhika. Alipowatazama wawili hao wakimwacha mbali zaidi na zaidi, miguu yake mirefu ikawafuata kwa haraka. “Suzie ni mwanangu. Hata kama anataka kucheza, atacheza na mimi.”

“Anko sikutaki. Wewe ni mkali sana.” Suzie alimkataa bila huruma.

Alvin alisimama na kusema kwa sauti nyororo, “Suzie, sikumaanisha hivi sasa hivi…”

“Anko, hutakiwi kuniomba mimi msamaha, bali Aunty Lisa,” Suzie alisema kwa uzito.

Alvin alimtazama Lisa lakini alimuona tu akiendelea kusonga mbele. Hakumtilia maanani hata kidogo. Alihisi huzuni.

Suzie alimtazama kwa kumtia moyo. “Mwalimu wangu alisema kwamba mwanamume wa kweli huomba msamaha anapojua kwamba amekosea.”

Alvin akaishiwa pozi. Alipotazama macho ya mtoto yule asiye na hatia, alihisi kana kwamba asingekuwa mwanamume ikiwa asingeomba msamaha. Alinyamaza kimya na kuushika mkono wa Lisa. Akipunguza sauti yake, alisema, “Samahani. Nimekuwa katika hali mbaya tangu majuzi na nilmekukaripia kwa sauti kubwa sasa hivi. Usiichukulie vibaya.”

Lisa aligeuka kwa hasira kumtazama machoni, lakini Suzie akawahi akasema, “Aunty Lisa, msamehe tu. Anko pia anatia huruma. Tayari ni mkubwa sana lakini aliachana na mke wake bila hata mtoto. Baba yangu ni mdogo kuliko yeye lakini tayari ana binti mkubwa kama mimi.”

Alvin alionekana kuchomwa vibaya na kisu kisichoonekana. Uso wake mzuri uligeuka na kuwa mbaya kwa huzuni. Ikiwa asingemsukuma Lisa kwa bahati mbaya wakati huo, mapacha wake wangekuwa wakubwa vile vile, sawa? Lakini sasa, hakuweza kuhimili uchungu wake.

Lisa alitazama sura yake iliyojawa majuto na wasiwasi. Alijisikia furaha. "Sawa, sitabishana na wewe kwa vile Suzie amezungumza kwa ajili yako, lakini ikiwa bado unataka kufuatana na sisi, basi kuwa mstaaribu. Hasira zako usizimalizie kwetu." Kisha, akamwongoza Suzie kwenye michezo ya kushangaza.

Alvin aliwafuata wawili hao kwa nyuma. Kwenye michezo yote ya awali Lisa hakumpa nafasi Alvin ya kucheza ya Suzie. Hatimaye, walipoenda kwenye gurudumu la Ferris, Lisa alimruhusu ampeleke Suzie kwa vile yeye aliogopa urefu.

“Kwanini unaogopa gurudumu la Ferris? Mbona mimi siogopi?" Suzie hakukubali na kumsisitiza Lisa ajiunge. Wote watatu walikaa kwenye kibanda kimoja. Alvin alikaa upande mmoja huku Suzie na Lisa wakikaa upande wa pili.

Ilikuwa sawa mwanzoni, lakini kibanda chao kilipoinuka, miguu ya Lisa ilidhoofika. Alishika nguzo pembeni kwa woga na hakuthubutu kutazama chini. Alvin aliitazama sura yake ya uoga na kuhisi kufurahishwa bila kuelezeka. Alikuwa amemjua kwa muda mrefu, lakini hakujua kamwe kwamba alikuwa akiogopa urefu. Hakuthubutu hata kukaa kwenye gurudumu la Ferris.

Kwa sababu fulani, ghafla alitaka kumtisha. Wakati gurudumu la Ferris lilipofikia kilele chake, alitikisa kibanda kwa makusudi. Jumba liliyumba polepole, lakini Lisa aliogopa sana hivi kwamba moyo ulimdunda kwa kasi ya ajabu. Mwili mzima ulikuwa ukimtetemeka, lakini hakutaka kumtisha Suzie, akachuchumaa pembeni ya siti na kujikunyata kama mpira. Meno yake yalikuwa yakigongana kwa sababu ya hofu.

Moyo wa Alvin ulijawa na raha kumuona Lisa akiogopa vile. Alinyoosha mkono, akamvuta Lisa mikononi mwake na kumkumbatia kwa nguvu. Joto kali la mwili wake lilimfunika, na kumfanya amtegemee bila kujua. Hakuweza kujizuia kulishika shati lililokuwa kifuani mwake.

Hata hivyo, alipokumbuka kuwa alimtisha, aliinua mkono wake na kukibana kifua chake kwa nguvu. “Alvin Kimaro, wewe ni mkorofi! Kwa nini ulinitisha?”

Alvin alitaka kukasirika, lakini aliposikia sauti nyororo ya mwanamke huyo, hakuweza kukasirika hata kidogo. Alisikia harufu nzuri ya nywele zake na kuukumbatia mwili wake laini, akihisi moyo wake ukijaa hadi ukingoni.

Kisha, sauti ya Suzie iliyokasirika ikasikika. "Hmph, nyinyi wawili mnakumbatiana na kuniacha pembeni?" Lisa aONA haya na kutaka kujitoa kwa Alvin, lakini gurudumu la Ferris bado lilikuwa juu na alizidi kuogopa, kwa hivyo miguu yake ilikuwa dhaifu.

"Endeleeni na mambo yenu, nitajiangalia mwenyewe.” Suzie alichungulia dirishani bila woga.

Lisa aliinamisha macho chini kwa huzuni na aibu. Alvin alitazama chini na kuona kope zake zikicheza mithili ya feni. Takriban dakika tatu baadaye, kibanda chao kilikuwa hatua chache kutoka chini na mara moja Lisa alijitenga na mikono yake na kuketi kando ya Suzie.

Macho ya Alvin yaliganda kwenye kumbatio lake tupu na akamkumbusha, “Hiyo ilikuwa ni raundi ya kwanza tu. Bado kuna raundi moja zaidi."

“Nashuka. Nyie mnaweza kuendelea. ” Lisa aliogopa sana. Suzie alikuwa mdogo na hakuwa na hofu ya kupanda gurudumu la Ferris, lakini yeye, aliogopa sana.

"Sitaki kukaa hapa tena. Haifurahishi hata kidogo. Nataka kupanda mashua.” Suzie alikuwa tayari ameona kitu cha kuvutia zaidi sehemu nyingine.

Alvin alihuzunika kwa kutoswa, lakini aliweza tu kuwafuata wawili hao nje. Walizunguka kwa muda mrefu kwenye uwanja huo wa burudani. Hatimaye, waliingia kwenye mgahawa kula.

Baada ya Lisa kuagiza chakula, wote watatu walikaa kwenye meza ya dirishani na kula. Alvin hakupendezwa na vyakula hivyo na alipata chupa ya soda tu kunywa wakati sauti za wanandoa wachanga zilisikika ghafla kutoka upande mwingine.

'Kipapatio hiki cha kuku ni kitamu. nitakupa.” Msichana huyo kwa furaha alichukua kipapatio cha kuku na kukiweka kwenye sahani ya mvulana.

Mvulana huyo alimtazama msichana huyo kwa unyonge. “Sijakuelewa. Unanipa tu vitu ambavyo hutaki kula mwenyewe.”

“Hehe, ni kwa sababu wewe ni mpenzi wangu. Ni jukumu la mpenzi kula kile ambacho mpenzi wake hataki.”

"Woi, ni kazi sana kuwa mpenzi wako."

“Hebu jaribu kusema hivyo tena?”

“Nilikuwa natania tu. ” Mvulana huyo alichukua vipande vya kuku na kula kwa huzuni.

Alvin aliganda. Tukio hilo lilimpa hisia alizozizoea, kana kwamba aliwahi kuzipata hapo awali. Ghafla, sauti ya mwanamke ilisikika akilini mwake. ‘Kwa nini huwezi kula nilichokula? Je, ni kwa sababu unanichukia? Au hunipendi tena?’

Hata hivyo, kabla hajafikiria zaidi, kulikuwa na maumivu ya kutoboa kichwani mwake. Soda iliyokuwa mkononi mwake ilianguka chini na kumwagika. Uso wake mzuri ulibadilika kwa maumivu.

Suzie na Lisa walishtuka. Wakamtazama kwa wakati mmoja. “Anko , uko sawa?” Suzie alionekana kuwa na wasiwasi.

“Niko sawa tu. Nitaenda uani kunawa uso wangu. ” Alvin alienda chooni kwa haraka....ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.