JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................383-384

Sura ya: 383

Alvin hakujua la kusema.
"Kweli, ni kawaida kwa watoto kupata njaa wakati huu. nitakufanyia… chips maya.” Lisa alikipapasa kichwa cha Suzie na kugeukia jikoni. Suzie alimfuata mara moja nyuma nyuma kama paka anayetamani kulishwa.

“Si vizuri kwa mtoto kula chipsi usiku sana." Alvin alimkosoa huku akikunja uso. Alikuwa analipisha kwa kumlaumu kwa kumpa Suzie simu mapema.

Lisa hakumjali na kutoa viazi kadhaa kutoka kwenye kikapu. Kisha, akaanza kuvimenya kwa ustadi mkubwa. Viazi vitano tu vilitoshea sahani ya kumtosha Suzie. Wakati huo mafuta tayari yalikuwa yamechemka.

Alipotumbukiza viazi kwenye mafuta alitoa mayai matatu kwenye friji. Kisha, alitenganisha maganda na ute wa ndani.
Viini vya yai nyangavu vilifanya vidole vyake vionekane vyembamba, na viganja vyake vilivyo safi na vyeupe vilimpa Alvin shauku ya kumshika.
Alvin alipoteza mawazo kwa muda hadi Suzie akamjibu, “Chipsi anayofanya Aunty Lisa ni tamu sana.”

“Suzie, unaonekana unajua kila kitu. Ni kana kwamba unamfahamu sana.” Alvin alikuwa na shaka.

Lisa alijibu bila kuinua kichwa chake, "Ni kwa sababu Jack mara nyingi humleta hapa, haswa ... baada ya mama yake kuondoka."

Hapo ndipo Alvin alipoelewa, lakini alizidi kuchukizwa.
Aliifanya chipsi kuwa ya haraka sana kwani ilimaliza kutengenezwa kwa chini ya dakika kumi.
Alvin aligundua kuwa mayai yake yalikuwa yamekaangwa pembeni kwa mafuta ya blue band na kuongezewa humo vipande vya karoti, hoho na kitunguu kwa mbali. Alimtengea mtoto pamoja juisi ya zabibu na tomato sauce ya kutengenezwa nyumbani. Ilionekana kunoga sana, yenye afya zaidi kuliko chipsi kutoka huko nje. Ilikuwa nzuri kwa watoto kula.

Wakati harufu hiyo ilipojaa jikoni, hata mtu mzima kama yeye alitamani kula. Suzie aliketi kwenye meza ya kahawa na akala chipsi yenye harufu nzuri. Kwa kweli, Alvin alikuwa na wivu kidogo. Alikuwa na wivu kuwa Suzie ni mtoto. Alichokifanya ni kusema tu, na Lisa angemfanyia chochote.

Alipokwenda jikoni tena, ilikuwani kwa ajili ya kusafisha tu jiko. Mwanga wa njano ulimwagika juu ya kichwa chake. Ijapokuwa kwa kawaida alionekana kama vixen mwenye kupendeza wakati wa mchana, sasa alionekana kama mwanamke aliyetoa haiba ya uzazi.

"Inaonekana ... unajua mengi kuhusu watoto. ” Alvin ghafla akasema, “Kwa kawaida, wanawake ambao si wazazi huwa hawana msaada sana linapokuja suala la watoto, lakini Suzie anakupenda sana na kukuchukulia kama mama yake.”

Moyo wa Lisa ulirukaruka. Alvin hakujua kwamba Suzie hakumchukulia Lisa kama mama yake, bali Lisa alikuwa mama yake. Lakini, hakuthubutu kuweka wazi hilo.
Alijifanya mtulivu huku akipiga mswaki. “Bila shaka najua mengi. Nimesoma vitabu vingi sana vya malezi nilipokuwa mjamzito, lakini kwa bahati mbaya, sikupewa fursa ya kutumia ujuzi huo. Labda hutaelewa hisia hiyo.

“Nilipokuwa ng’ambo, nilifikiria watoto niliowapoteza nilipowaona watoto wengine, na moyo wangu ulitulia. Nilifikiria kwamba ikiwa watoto wangu wangekuwa bado hapa, bila shaka wangekuwa wazuri kama wao. Kwa hiyo, baada ya muda, nilianza kupenda kucheza na watoto na kuwazoea polepole.

"Hah, sahau. Kuzungumza na wewe ni kama kutupa lulu mbele ya nguruwe, lakini nina furaha sana kwamba Suzie ananipenda. Ni mtoto maskini sana.”

Kulikuwa na maumivu yasiyoelezeka moyoni mwa Alvin. Asingeelewaje? Kama yeye, kumuona Suzie mara nyingi kulimkumbusha kuhusu watoto wake mwenyewe. Alikasirika, kisha akabadilisha mada. “Kwa nini umsaidie Jack kumtunza binti yake? Je! huoni yeye ni…mtu aliye na maisha machafu ya kibinafsi?”

"Samahani, sidhani kama yuko." Lisa alimtazama kwa kuchukia. “Angalau hakuwa na mchumba aliyemchumbia na kumuacha na hakumlazimisha mke wake kutia sahihi hati za talaka kwa ajili ya mwanamke mwingine. Hata awe mchafu, uchafu wake haupo wazi, lakini wewe ni mpuuzi kabisa. ”

Alvin, ambaye alipuuzwa tena, hakuweza kupata maneno ya kujibu.
Alijihisi mnyonge, mnyonge kweli kweli. Hata hivyo, Lisa alikuwa tayari amempuuza. Alipotoka nje, Suzie alikuwa amemaliza kula na kububujikwa furaha.

“Ni kitamu. Ninahisi usingizi sasa."

“Wewe nguruwe mdogo. Unatakiwa kupiga mswaki kwanza." Lisa akatoa mswaki mpya kabisa wa watoto na dawa ya meno kwenye begi lake.
Alvin alishtuka. "Kwanini unayo hiyo kwenye begi lako?"

“Nilinunua pale chini mapema. Kwa kuwa umechelewa kumleta Suzie, nilidhani atakulazimika kulala hapa.” Lisa kisha akamuongoza Suzie mpaka bafuni.

"Subiri, mswaki wangu uko wapi?" Alvin aliuliza, “Sijisikii vizuri kumuacha Suzie hapa peke yake. Mimi pia nalala.”

“Samahani, lakini siruhusu wanaume kulala nyumbani kwangu, na sitaki ndugu wa Sarah waharibu nyumba yangu tena,” Lisa alisema kwa ukali.

“Sarah… hajui kama niko hapa,” Alvin alisema bila kufafanua. “Nitalala kwenye chumba cha wageni. Kwa vyovyote vile, siwezi kumuacha Suzie peke yake.”

“Aunty, mwache tu Anko alale hapa,” Suzie alimuomba kwa upole. "Nataka abaki pia."

Lisa alimtazama kwa siri, na Suzie aliinamisha kichwa chini na kutoa ulimi nje.

“Sawa. Ikiwa unataka kulala hapa, unaweza kulala kwenye sofa. Mlango unaofuata ni chumba cha Pamela. Amerudi Dar es Salaam, lakini vitu vyake vyote viko kitandani, kwa hivyo sidhani kama ni vizuri kulala huko.” Baada ya hapo, Lisa alimpeleka Suzie chumbani kwake na kufunga mlango.

Alvin aliusukuma mlango wa chumba cha pili na kukata tamaa kwa kutazama. Kulikuwa na vitu vingi vya kike ambavyo Alvin alihisi kinyaa kuvigusa. Mwishowe, aliamua kulala kwenye sofa.

Ingawa ilikuwa karibu majira ya joto, usiku ulikuwa bado baridi. Baada ya kulala kwa muda, alihisi baridi. Alichoweza kufanya ni kugonga mlango wa chumba cha kulala Lisa.

Suzie alifungua mlango na kusugua macho yake yenye usingizi. “Anko, kuna nini?”

“Suzie, Aunty Lisa yuko wapi? Je, unaweza kuniruhusu nichukue blanketi?” Alvin alichungulia ndani na hakumuona Lisa, lakini kulikuwa na sauti ya maji ya bomba bafuni.

“Aunty anaoga. Tuna blanketi moja tu, lakini nadhani kuna shuka."

"Shuka itafaa." Mara Alvin akaenda kuchukua shuka. Ikiwa angengoja hadi Lisa atoke, labda asingempa blanketi.

Akiwa anarudi sebuleni, alitazama bafuni bila kujijua. Taswira ya Lisa ilimfanya damuyake kuongeza mbio kwenye mishipa yake. Hiyo ni kwa sababu Lisa alikuwa anaoga huku mlango ukiwa umefungwa nusu tu.

Ubongo wake ulimtoka machoni. Lisa alipogeuka kutoka kuoga, haraka Alvin akachukua shuka na kutoka nje. Mlango ulipofungwa, Lisa alifikiri alikuwa amesikia harakati kutoka ndani ya bafu. Mara akatazama nje lakini hakuona mtu yeyote.

Hata hivyo, kulikuwa na hisia ya aibu isiyoelezeka ndani ya moyo wake.
Hapo zamani, Lucas alipokuwa na Suzie, alihisi utulivu na kufunga mlango wa bafu wakati wa kuoga. Sasa, kulikuwa na mtu mmoja tu chumbani. Ingawa Suzie alikuwa amejilaza, kama mama, bado alikuwa na wasiwasi. Kwa hivyo, hakufunga mlango.

Hakusahau kuwa kulikuwa na mwanaume ndani ya nyumba pia. Ingawa alifunga mlango wa chumba cha kulala, vipi ikiwa Suzie angeufungua?
Kwa hayo, haraka akavaa nguo zake na kutoka nje. Suzie alikuwa amelala kitandani, lakini shuka kwenye kitanda ilikuwa imetoweka.

Sura ya: 384

"Alvin aliingia sasa hivi?" Lisa alimuuliza Suzie.

"Ndio, baba mchafu alisema alikuwa anasikia baridi, kwa hivyo nilifungua mlango na kumruhusu aingie kuchukua shuka," Suzie alisema kwa sauti ya usingizi.

Lisa alitazama kwa mbali kutoka mlangoni hadi kwenye bafu. Hakika ilitosha kwa Alvin kuona kilichokuwa kikitokea bafuni, na mlango ulikuwa umefungwa nusu wakati akioga. Kwa kufikiria tukio hilo, mara moja alitaka kujiua kutokana na aibu na hasira.

Alivuta sikio la Suzie na kulifinya, “Kwa kuwa unamwita baba yako mchafu, kwanini unamjali? Kama anasikia baridi, kwanini usimuache. Kwanini ulimruhusu aingie? Hukujua nilikuwa naoga?”

“Mama kwani kuna kosa gani?” Suzie alipepesa macho kwa kuchanganyikiwa.

“Hujui kosa lako?” Lisa alieleza kwa hasira, “Mama alikufundisha kwamba huwezi kuruhusu watu usiowajua wauone mwili wako. Ndiyo sababu sipendi Alvin anione nikioga. Unaelewa?"

"Lo, baba mchafu lakini alishawahi kukuona zamani, si hivyo?” Suzie alisema, nusu-ukweli. Uso mzima wa Lisa ukawa mtupu.

"Mama, basi samahani, sitarudia tena," Suzie alisema kwa wasiwasi.

"Nyamaza!" Lisa alijikuta ghafla akishindwa kuongea na bintiye.
"Mama, haujaniambia nini kitatokea ikiwa baba mbaya atakuona ukioga." Suzie alikunja uso na kuuliza kwa udadisi, “Je, alifanya jambo baya? Je, anapaswa kukamatwa? Je, tunapaswa kuwaita polisi?”

“Kwa kifupi… Kwa kifupi, si vizuri. Ni mbaya sana.” Kwa hasira, Lisa alibadilisha mada akiwa amefadhaka. “Sawa, umeumiaje leo? Niambie ukweli haraka.”

“Ni kwa sababu mimi... nilimruhusu yule mama wa kambo mbaya aniogeshe. Wakati huo, nilimtesa kwa makusudi, na akanisukuma chini, "Suzie alisema kwa furaha. “Mama, hukuona jinsi baba alivyokuwa na hasira. Uso wa yule mama wa kambo mwovu ulikuwa mbaya sana wakati baba mchafu alipomkaripia…”

Nusu ya kuongea, ghafla Suzie aligundua uso usiopendeza wa Lisa. “Mama, kuna nini?”

"Wewe mtoto hivi unafikiria nini?" Lisa aliinua kichwa chake ghafla na kumpiga vibao kadhaa. “Nilikuambia nahitaji unifundishie somo Sarah? Una miaka mingapi?"

“Mama…” Suzie alilia kwa uchungu.

Lisa alimtazama kwa macho mekundu. "Susan Jones, wewe ni mtoto mjinga sana. Unaweza kumfanyia Sarah hivyo leo kwa sababu yeye bado hujui wewe ni nani. Shukuru Mungu kwamba alikusukuma tu leo. Itakuwaje kama hutamwona mama tena?”

Suzie aliingiwa na hofu. Lisa akamshika mikononi mwake. “Mama hataki umlipizie kisasi, sawa? Mama ana mipango yake mwenyewe. Ninachotaka ni wewe kukua na afya njema. Usiende kwenye nyumba ya Alvin tena. Kuanzia sasa, unapaswa kukaa kwa bibi yako kwa utii.
Kwa nini usiende chekechea na Lucas? Hujammiss Lucas?”

"Ndio, nimemkumbuka." Suzie alikabwa na kusema kwa sauti ya chini, “Pole mama. Nilikupa wasiwasi.”
“Mama hataki uumie kwa sababu mama anakupenda sana, kwa hiyo lazima ujipende pia. Umeelewa? ” Lisa alisema kwa upole.

“Ndiyo.” Upesi Suzie alilala mikononi mwa mama yake.

Kwenye sofa sebuleni, akiwa na shuka tu, Alvin hakuwa na baridi tena. Kwa kweli, mwili wake ulihisi joto kama volkano. Alipofumba macho tu, akili yake ikajawa na picha za Lisa akioga. Ilikuwa ni hisia ya ajabu lakini iliyozoeleka.

Zamani, hata Sara angekuwa amevaa kwa kuvutia kiasi gani, hakuwahi kuhisi hisia kama hizo mbele yake. Hata hivyo kumtazama Lisa mara moja tu kulitosha kuufanya mwili wake kuwaka moto.

Hii haikuwa mara yake ya kwanza kumuona hivi, lakini haijalishi ilikuwa kabla au baada ya kuachana, alikuwa na mvuto mkubwa kwa mwanamke huyo. Mwishowe, hakuwa na la kufanya zaidi ya kuoga maji baridi. Baada ya kuoga maji baridi, alijilaza kwenye sofa akihisi baridi kuliko hapo awali. Shuka ilikuwa nyembamba sana hivi kwamba alilala kwa shida usiku kucha.

Siku iliyofuata, Alvin, ambaye mara chache aliugua, aliamka na mafua na homa kali. Suzie bado alikuwa amelala fofofo. Hata hivyo, Lisa alikuwa na mazoea ya kuamka mapema na kuandaa kifungua kinywa.
Kwa kuwa mtoto huyo alilala hapa usiku kucha, ilimbidi aandae chakula kizuri. Wakati akipita sebuleni, alijitahidi kutoitazama sura iliyolala kwenye sofa.

“Ahem.” Kikohozi cha Alvin kilisikika.

Alijifanya hasikii na akatoa pakiti ya tambi kwenye jokofu.

"Nina mafua." Sauti ya mzuka ya Alvin ilisikika mlangoni.
Alimpuuza. Aliogopa kwamba ikiwa angegeuka, angeweza kukumbushwa tukio la aibu jana na asingeweza kujizuia kumpiga teke.

"Nimesema nina mafua," Alvin alisema tena kwa upole huku akimsogelea.

"Sijali kama una mafua." Lisa aligeuka na kumtazama kwa macho yake meusi na matupu.

Macho makali ya Alvin yalimtazama kwa haya usoni mwake. Kisha, akatazama juu na kusema bila kupenda, “Yote ni kwa sababu nilikuona jana unaoga. Mwishowe, sikuweza kujizuia kuoga maji baridi, kisha nikashikwa na homa.”

Wote walikuwa watu wazima, hivyo Lisa alijua vizuri kwa nini alienda kuoga maji baridi. Hata hivyo, ilimfanya aaibishwe na kukasirika zaidi. “Vipi bado una ujasiri wa kusema hivyo? Ni nani aliyekuruhusu kuingia chumbani kwangu jana?"

"Nilikuwa najisikia baridi, na hukunipa shuka. Ni kosa lako kutofunga mlango.”

"Ninawezaje kuwa na uhakika na kufunga mlango wakati mtoto yuko peke yake chumbani?"

Alvin aliacha kuongea na kumtazama kwa umakini. Kadiri alivyokuwa akimjali Suzie, ndivyo alivyozidi kuuona utu wake. Alikuwa makini kwa Suzie bila kujali ni mtoto wa nani, tofauti na Sarah, ambaye alikuwa mzembe kiasi cha kumfanya Suzie asongwe na mfupa wa samaki. Ikiwa Lisa angekuwa mama, bila shaka angekuwa mama mzuri.

“Mbona unanitazama?” Lisa alijisikia vibaya kutokana na kumtazama.

Midomo yake ikaachana kidogo, na alikuwa anakaribia kuongea wakati alihisi kooni kuna mwasho. Akatazama pembeni na kukohoa kwa nguvu.

Mkono wa Lisa uligusa paji la uso wake ghafla, na Lisa akashusha macho yake. "Una homa kidogo."

“Mm. ” Akamtazama kwa shauku. Wakati huo, alionekana kama mtoto dhaifu. Alifanana kidogo na Suzie alipokuwa mgonjwa.

Lisa akasema, “Nenda hospitali. Usimwambukize Suzie.”

“Huh?” Uso mzima wa Alvin ukawa mweupe kwa hasira. Alifikiri kwamba, angalau, angejali kuhusu homa yake, na amwandalie kifungua kinywa kitamu, lakini kumbe alikuwa na wasiwasi kwamba angemwambukiza Suzie badala yake.

"Lisa Jones." Akauma mdomo. Hisia zilizochanganyika za mfadhaiko, kuudhika, na manung’uniko zilimjaa, na mwili wake ukayumba bila raha.

Lisa bila fahamu alinyoosha mkono kumshika mkono wake na kukuta mikono yake pia inawaka moto. Alipumua kwa upole. Hakukuwa na namna zaidi ya kumsaidia. "Kwanini usilale kwanza kitucha moto? Unapaswa kula kitu cha moto kabla ya kuchukua dawa. Kunywa dawa kwenye tumbo tupu kutaumiza tumbo lako."

Uso wa Alvin uligeuka juu chini huku uso wake ukiwa umewaka kwa furaha. “Una wasiwasi na mimi?” Alifurahi kuona alikuwa na wasiwasi kuhusu yeye kuumiza tumbo lake.

“Jamani, huo ni ushauri wa kawaida tu, sawa? Kama hujali kuumiza tumbo lako, nitakupa dawa sasa hivi.” Lisa alikosa la kusema kwa kuhisi aibu.

“Je, ni vigumu kukubali kwamba unanijali?" Alvin alijiamini kabisa.

"Kwa hivyo ikiwa nitakubali? Jamani, dunia nzima imeshajua kuwa unaoa. Utamwacha mchumba wako wa utotoni kwa msichana mbaya kama mimi?” Lisa alimdhihaki kabla hajaingia jikoni kupika tambi.....ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.