JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................367-368
Sura ya: 367
“Shhhh!” Lucas alimfanyia Suzie ishara ya kunyamaza. Haraka akafunga laptop. Kisha, akamvuta Suzie na kutafuta mahala pa kujificha.
Akiwa na wazo, alimwaga nguo chache kutoka kwenye sanduku kisha akamvuta Suzie ndani ya lile sanduku na kuweka nguo chache juu yao, halafu akalifunika bila kufunga zipu. Wawili hao walikuwa wamejikunja ndani kwa pamoja kama sungura.
Suzie alipokuwa amejikunja huku akishusha pumzi, alijisikia vibaya sana. Aliuliza, “Unafanya nini Lucas? Lazima ni Godmother anarudi—”
Kabla hajamalizia sentensi yake, Lucas alimziba mdomo. "Nyamaza. Godmother havuti sigara, we hujasikia harufu ya sigara?” Lucas alijibu kwa sauti ya kunong’ona. Alipomaliza tu kuongea, mlango wa nje ukafunguliwa kwa nguvu. Baadaye, sauti ya mtu wa kushangaza ilisikika.
“Vega, sioni mtu yeyote hapa, lakini taa zimewaka.”
"Anaweza kuwa kajificha. Nenda ukaangalie pande zote."
Watu wachache walisikika wakiingia chumbani. Walipekua kabati la nguo na chini ya kitanda na kuonekana kukata tamaa. "Hakuna mtu, bana, Vega."
“Umeangalia mpaka bafuni, stoo, jikoni… ?” Mtu yule kwenye simu alizidi kusisitiza. Wale jamaa mle ndani wakasambaa kila kona kutafuta, lakini hawakuona mtu.
Macho ya jamaa mmoja yakaangaza kwenye chumba hicho. Akakazia macho kwenye sanduku lililokuwa kwenye kabati la nguo. Je, anaweza kuwa kajificha humu? Aliponyoosha mkono wake kulifungua, mtu aliyekuwa nyuma yake alimpiga teke. “Una akili kweli wewe! Unafikiri mtu mzima anaweza kutoshea kwenye sanduku dogo kama hilo?”
Alinyamaza kwa muda kabla ya kuangaza huku na kule na kusema kwenye simu, “Bwana Vega, hakuna mtu humu.”
“Sawa. Vunja kila kitu ndani ya nyumba."
Kwa hayo, nyumba ya Lisa ikageuka kuwa Ukraine. Vurugu ya vitu vikivunjwa hovyohovyo ilisikika kwa kishindo. Walivunja chupa za mvinyo, vioo vya makabati na dressing table, madirisha, vyombo vya jikoni, TV, pamoja na kupora vitu vya thamani. Baada tu ya kumaliza kuvuruga kila kitu ndipo waliondoka wakiwa wameridhika.
Dakika kumi hivi baada ya wao kuondoka, Lucas alifunua sanduku na kutangulia kutoka kisha akamtoa pia Suzie nje. Suzie alitoka akiwa na mawenge ya woga, hivyo alihisi kizunguzungu na kuanguka. Kwa bahati mbaya aliangukia kipande kikubwa cha chupa ya mvinyo ambacho kilimchoma kichwani. Kichwa chake kilianza kuvuja damu kwa wingi.
“Kaka, inauma sana…” Suzie alimtazama kwa sura ya maumivu akiwa na pakiti ya chokoleti mkononi mwake.
“Usiogope, Suzie. Nitakupeleka hospitali sasa hivi.” Lucas alikuwa na wasiwasi sana hivi kwamba machozi yalitiririka kwenye uso wake ambao kawaida ulikuwa mtulivu.
Muda mfupi baada ya Suzie kuumia, Pamela akaingia, alishangaa kukuta nyumba ikiwa kwenye vurugu kiasi kile huku Lucas akiwa anahangaika na Suzie. Hakukuwa hata na jirani aliyejitokeza kusaidia.
Lucas alilia alipomuona Pamela, “Godmother, Suzie ameumiaa.”
"Nini kimetokea?!" Pamela aliuliza kwa mshtuko huku akimtumbulia macho Suzie aliyekuwa akivuja damu kwa wingi. Hapohapo akapiga simu kuita ambulensi kishaakawabeba wale watoto kushuka chini.
Wakiwa njiani kwenda hospitali, Pamela alimpigia simu Lisa kumpa taarifa. "Mungu wangu! Nimerudi tu na kukuta nyumba yako kwenye fujo. Nimewaita polisi. Suzie ameumia.”
“Nini kimetokea? Suzie kaumia? Hali yake ikoje?” Lisa ambaye alikuwa amewasili hospitalini, mara baada ya kusikia maneno ya Pamela aliingiwa na huzuni nyingi. “Alijijeruhi vipi? Je, ni serious?”
“Lisa, hata mimi sijui kilichotokea. Nitazungumza nawe baadaye. Suzie amezimia. Nimepiga simu ambulensi na sasa nampeleka hospitalini.” Pamela alisikika akiwa amekabwa.
Wimbi la hofu lilimkumba Lisa, karibu kumfanya apoteze akili yake.
Haraka akakimbia kwenda kwenye hospitali nyingine. Alipofika alimuona Lucas akiwa amesimama kinyonge kwenye korido peke yake. Mikono na uso wake ulikuwa umetapakaa damu.
Mara alipomuona Lisa, akajitupa kwenye mikono yake huku akilia.
“Mama, Suzie ameumiaaa....”
“Usilie. Niambie kilichotokea.” Lisa alifuta madoa ya damu usoni mwake kwa uchungu.
“Muda mfupi baada ya wewe kuondoka, watu wachache waliingia ndani ya nyumba yetu, kwa hiyo nikaenda kujificha kwenye sanduku la suti pamoja na Suzie. Hawakutuona, lakini mwisho walivunja kila kitu. Tulipotoka kwenye sanduku, Suzie aliangukia chupa ikamkata kichwani.”
Katikati ya maelezo yake, Lucas alidondosha kilio. “Nilikuwa nimemziba mdomo Suzie muda wote ili asipige kelele.”
Lisa alitetemeka kwa hasira. Kamwe katika ndoto zake za ajabu hakutarajia kwamba kuna mtu angekuwa na ujasiri wa kuvunja na kuingia ndani ya nyumba yake. Aliogopa kufikiria nini kingetokea kwa watoto hawa wawili ikiwa Lucas asingechukua hatua ya kijasiri kama hiyo. Alikuwa amevunjika moyo na mwenye hatia. Kama mama, alishindwa kuwalinda watoto wake waliporudi hapa.
Muda mfupi baadaye Pamela alitoka kwenye chumba cha daktari. Alikuwa kampakata Suzie wakielekea kwenye wodi kwa ajili ya mapumziko.
“Vipi hali ya Suzie?” Lisa aliuliza kwa wasiwasi.
"Ametoka kwenye hatari." Pamela alimkazia macho yake ya huruma kwa Suzie ambaye alibaki amepoteza fahamu. Kipaji cha uso cha mtoto huyo mdogo kilikuwa kimefungwa kwa kutumia bandeji, na mashavu yake ya rangi ya waridi yalikuwa yamepauka.
"Hawa watu ni wakatili. Wanawezaje kumdhuru mtoto?" Pamela alinyamaza kwa muda kabla ya kuuliza bila kujali, "Hii haimuhusu Thomas kweli?"
“Pengine.” Lisa aliitikia kwa kichwa bila huruma. Alikuwa na maadui wengi sana. Ikiwa Melanie na Damien wangetaka kuchukua hatua dhidi yake, wangefanya hivyo lakini wasingetumia nguvu kiasi hicho.
"Yote ni makosa yangu," Pamela alisema kwa hatia, "nilimchana makavu Thomas hadharani wakati wa mkutano wa waandishi wa habari leo. Lazima alichukia. Anajua nitakuwa nimefikia kwako. Tayari alikuwa na ujasiri wa kutosha kuingia nyumbani kwangu miaka mitatu iliyopita, kwa hiyo sidhani kama kuna jambo lolote anaogopa kufanya.”
“Ndio. Alipokamatwa miaka mitatu iliyopita, hata hakwenda jela. Ndiyo maana sasa hana woga.” Sura ya kusikitisha iliosha uso wa Lisa.
Pamela akainua midomo yake. "Naogopa kwamba Alvin ... atamtetea."
Kifua cha Lisa kilihisi kubana. Aligeuza kichwa chake na kumtazama Suzie. Hasira kali ikamjia. Sarah Njauna Thomas Njau! Ilimbidi kuwalipa waliomuumiza bintiye!
Wakiwa kwenye wodi ya faragha, Lucas alimwangalia Suzie na kusema kwa huruma. “Mama, lilikuwa kosa langu. Nilipaswa kuzima taa. Nilishindwa kumtunza vizuri Dada!”
“Lucas, acha kujilaumu. Ulifanya kazi nzuri. Ulikuwa sahihi kwa kuacha taa ikiwaka.” Lisa alimkandamiza mabegani. "Lazima watu hao walikuwa wakitazama nyumba yetu kutokea chini. Walijua kuwa taa zetu zinawaka, ungezima ghafla, wangejua kuna mtu amejificha ndani ya nyumba. Kwa hali hiyo, wangegundua kuwa wewe na Suzie mko kwenye sanduku. Mwishowe, nyote wawili mngetekwa.”
"Mama, ni nani hao watu waovu?" Lucas aliuliza huku akiwa amejilaza mikononi mwake. "Nataka kulipiza kisasi kwa niaba ya Suzie."
“Wewe ni mdogo sana kufikiria mambo hayo. Suzie atakuwa sawa tu.” Lisa alimtuliza mwanaye, lakini asingewaruhusu wale waliomuumiza Suzie kutoka kwenye ndoano.
Kwa wakati huo, daktari aliwatembelea wodini. “Uchunguzi unaonyesha mtoto amepoteza damu nyingi, lakini hatuna damu ya kutosha aina ya AB hapa. Kwa kuwa wewe ni mama yake, je, damu yako ni AB pia?”
"Hapana." Uso wa Lisa uligeuka kuwa mbaya.
Lucas alikunja mikono yake na kusema, “Mama, yangu ni—”
"Hapana. Wewe ni mdogo sana kuweza kutoa damu yako,” daktari akakatisha sentensi yake. “Mgonjwa anahitaji mililita 500 za damu.
Hata mtu mzima hawezi kuvumilia ikiwa atatoa damu nyingi hivi. Mtoto hakika ataanguka. Baba wa mtoto yuko wapi?"
“Baba?” Lisa alikunja ngumi. Ikiwa Alvin angejua kuhusu hili, bila shaka angemnyakua Suzie kutoka kwake.
Sura ya: 368
Kwa wakati huu, Lucas alivuta mkono wa Lisa. “Mama, tunaweza kwenda kumtafuta mjomba Jack.?” Jack Kimaro ndiye pekee kutoka familia ya Kimaro aliyefahamu uwepo wa watoto hao. Alimsaidia Lisa kutoroka na mara kwa mara alikwenda Marekani kumsalimia hadi alipojifungua. Lucas na Suzie walimfahamau vizuri.
Baada ya kupigwa na butwaa kwa muda, Lisa mara moja akampigia Jack simu.
Jack aliharakisha kifka hospitalini pale ndani ya dakika kumi. “Vipi hali ya Suzie? Mara tu nilipojua kuwa kuna jambo limempata, nimepita taa nane nyekundu kuwahi hapa.”
"Asante, Jack." Lisa alimshukuru sana. “Suzie bado anaendelea na matibabu ya dharura. Anahitaji mililita 500 za damu.”
"Nina damu sawa na yeye. Fanya haraka uchukue damu yangu.” Jack alikunja mikono yake bila wasiwasi zaidi.
“Subiri kidogo. Tunahitaji kuthibitisha aina ya damu yako kwanza.”
Nesi alimshusha haraka haraka. Baada ya kuthibitisha aina yake ya damu, mililita 500 za damu yake zilitiwa mishipani Suzie. Pamoja na hayo, hali ya Suzie iliboreka taratibu.
"Jack, sijui jinsi ya kutoa shukrani zangu kwako wakati huu." Lisa alihisi kwamba alikuwa na deni kubwa la Jack.
"Hakuna wasiwasi. Baada ya yote, Suzie ni mwanangu kiukoo.”
Kwa sura ya kuhuzunisha, Jack alimaliza chupa ya maziwa. Alikuwa mzima wa afya, lakini kutoa mililita 500 za damu bado kulimfanya ahisi kizunguzungu kidogo. “Nenda ukamwangalie Suzie. Nitapumzika hapa kwa muda.”
•••
Kulipopambazuka, polisi walifika na kumwambia Lisa, “Tumewatambua watu waliovunja vitu vya nyumbani kwako. Walikuwa wahuni kutoka jirani, na tayari tumewakamata. Walikiri kwamba walivunja nyumba yako kufanya wizi. Tulipata vito na pesa taslimu. Angalia na uhakikishe kama hivi ndivyo vitu walivyoiba nyumbani kwako.”
“Ndiyo.” Lisa alivitazama vile vitu na kuvipokea.
“Sawa. Kesi imefungwa."
Polisi walipokuwa tayari kuondoka, Pamela alisema kwa kutoridhika, “Ni wazi, haukuwa wizi. Kuna mtu aliwalipa ili kulipiza kisasi kwetu.”
“Inatosha, Pamela. Polisi wamefanya walichoweza.” Lisa alimsimamisha na kuwaacha polisi waondoke.
"Nina uhakika Thomas amewahonga," Pamela alisema kwa hasira.
Lisa alicheka. “Bila shaka. Naam, mazoea hujenga tabia. Kadri Thomas anavyofanya matendo maovu zaidi, ndivyo anavyozidi kuwa stadi. Kabla ya hili, Alvin alilazimika kusafisha uchafu wake. Sasa, anaweza kushughulikia mambo peke yake vizuri hivi kwamba hatahitaji hata msaada.”
"Kwa hiyo tutamwacha tu?" Pamela aliuliza bila kuridhika.
"Tutaenda naye polepole. Lakini… sitaweza kuishi vizuri hadi niwalipe.”
Lisa alimkabidhi Lucas kwa Pamela. “Natoka nje mara moja, mtazame.”
“Mama, unaenda wapi?” Lucas aliuliza kwa wasiwasi.
“Naenda kununua kifungua kinywa. Nitarudi hivi karibuni. Mwangalie dada yako kwa sasa.” Lisa alitoka hospitali baada ya kumtuliza Lucas.
•••
8:00 asubuhi, katika jumba lake la kifahari, baada ya Alvin kumaliza kifungua kinywa, Sarah alitabasamu kwa upole na kusema, “Kwa kuwa bado ni mapema, unaweza kunisindikiza hospitalini? Nahitaji kuchoma sindano."
Siku hizo, Sarah ilibidi atembelee hospitali mara nyingi sana kuchoma sindano ya kuchochea mwili ili aweze kufanikiwa matibabu ya In vitro Fertilization (IVF), au upandikizaji wa mimba kwa njia ya matibabu.
Aliposikia ombi lake, Alvin aligeuka na kumkazia macho yake magumu. “Kwa kweli, hakuna haraka ya sisi kupata mimba. Kwa kuwa bado ni vijana, hatujachelewa kufanya hivyo baada ya kufunga ndoa.”
“Alvinic, mimi si kijana tena. Ninataka kuwa na watoto haraka iwezekanavyo na kujenga familia na wewe. Siogopi maumivu. Sijali kuteseka kwa ajili yako,” Sarah alijibu kwa upole huku akiizungusha mikono yake shingoni.
"Sawa, nitakupeleka huko." Alvin aliinamisha macho chini kwa kuomba msamaha. Ikiwa sio kwa sababu hakuweza kufanya naye mapenzi, asingelazimika kwenda kwenye shida zote za kupitia IVF.
Lisa alikuwa sahihi kwa kusema kwamba uzazi kwa njia ya IVF kuliwaweka wanawake katika hali mbaya.
Gari ilipowashwa tu na kuelekea nje ya geti, ghafla gari aina ya SUV ilipita kwenye geti la chuma na kuelekea kwenye gari la Alvin.
Alvin aligeuza usukani kwa haraka ili kulikwepa. SUV ilielekea kwenye maua na kugonga kwenye dirisha la nyumba. Baadaye, vioo vilivunjika na vipande kutawanyika ardhini.
Lisa alifungua mlango kwa teke. Akiwa amevaa jozi ya buti za Dk. Martens na jeans, aliruka kutoka kwenye SUV kwa macho ya kutisha.
Alvin alimkazia macho, huku Sarah akiiweka mikono yake kiunoni huku akitetemeka. Alionekana kuwa na hofu.
“Anapanga kufanya nini Alvinic? Hii inatisha. Karibu atugonge.”
Alvin alifungua mlango kwa huzuni na kutoka nje ya gari. Kuona fujo pale uani, aliruka kwa hasira. "Lisa Jones, unatamani kifo mapema asubuhi? Nimetosha na vitimbi vyako sasa.”
“Mimi pi nimechoshwa na nyinyi wawili pia.” Lisa akamsogelea taratibu huku macho yake yakionyesha hasira. “Kwanini sikufaulu kuwaua ninyi wenzi wasio na aibu sasa hivi?”
“Wewe ni mgonjwa! Nenda ukachukue dawa yako.” Alvin alimtazama Lisa kana kwamba ni kichaa.
Sarah alishuka kwenye gari na kumshauri Lisa kwa huzuni, “Tulia Lisa. Najua habari za ndoa yangu na Alvin labda zimekuchanganya, lakini unachofanya sasa ni kinyume cha sheria. Nimepiga simu polisi hivi punde.”
Alvin alishikwa na butwaa. Kisha, Sarah akaeleza bila kujali, “Ameenda mbali sana wakati huu. Umeona uharibu kwenye ua wetu? Kwa bahati nzuri, hakuna mtu aliyegongwa. Ikiwa hatutamfundisha somo sasa hivi, atafanya ujinga wa kiwango kikubwa wakati ujao.”
Alvin alinyamaza kwa muda. Alijua kwamba Lisa alikuwa bado anampenda, lakini tabia yake ya ukichaa ilimtia hofu sana. Aliona hitaji la kumfundisha somo pia.
Akiwatazama wawili hao, Lisa alidhihaki. “Acha kuwaza mambo kupita kiasi. Nilikuja hapa sio kwa sababu nina wivu na ndoa yako. Ninataka kukuonya kwamba hasira yangu ina mipaka yake. Sarah Langa, bora uendelee kumkanya Thomas. Watu wachache waliingia ndani ya nyumba yangu na kuvunja vitu vyangu jana usiku. Ni Thomas tu ndiye aliyewatuma.”
“Kwanini umsingizie kaka yangu, una ushahidi?” Sarah alichukia.
"Pamela alimuumbua Thomas mbele ya vyombo vya habari wakati wa mchana na tukio la uvamizi lilifanyika nyumbani kwangu usiku huo huo. Inawezaje kuwa bahati mbaya?” Lisa alifoka. “Ijapokuwa wale watu ambao wamekamatwa kwa kuingia ndani ya nyumba yangu ni wahuni tu, aliyewaelekeza atakuwa ni Thomas. Haiwezi kuwa mtu mwingine yeyote.”
Uso wa Alvin ulibadilika kidogo. Hapo ndipo alipoona sura ya Lisa iliyopauka na macho yaliyovimba. Ilionekana kuwa hakuwa amelala jana yake usiku.
"Ni Thomas ndiye amefanya?" Alvin akageuza kichwa chake na kumtazama Sarah kwa ukali.
“Hapana… Hapana.” Bila kujua lolote kuhusu jambo hilo, Sarah alianza kuingiwa na hofu. “Nilimpigia simu kaka yangu jana. Alisema kuwa hatajali maneno ya Pamela na hatamletea shida. Lisa, nadhani umewaudhi watu wengine. Huwezi kumlaumu ndugu yangu kwa sababu tu unanichukia.”
“Sihitaji kukukumbusha jinsi Thomas alivyo na jeuri ya kijinga, sivyo? Miaka minne iliyopita, tayari alikuwa na ujasiri wa kutosha kuingia ndani ya nyumba ya Pamela na kutaka kumbaka. Licha ya kujua kuwa nilikuwa mjamzito wakati huo, alithubutu kunisukuma! Zaidi ya hayo, dada yake ataolewa katika familia ya Kimaro hivi karibuni. Angeogopa kufanya nini?"
Lisa alimtazama Alvin kwa hasira. "Endelea kumtetea Thomas milele. Kwa sababu yake, sifa yako itaharibiwa mapema au baadaye. Kila mtu atachukizwa na jinsi unavyomsaidia na kumsaidia.”.....ITAENDELEA.....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA
