JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................365-366
Sura ya: 365
Wakati huo huo, Thomas alimpigia. "Sarah, yule b*tch Pamela Masanja amerudi. Wakati huu, hakika nitammaliza!”
Uso mrembo wa Sarah mara moja ukaangaza kwa mguso wa karaha. "Funga mdomo wako. Huu ni wakati mgumu kwani nitafunga ndoa na Alvin hivi karibuni. Usiniletee balaa.”
Thomas alishtushwa na karipio la ghafla. "Lakini haukuona alichosema Pamela kwa waandishi wa habari"
“Alvin tayari ameweka mtu wa kuzima jambo hilo. Ikiwa una kinyongo, basi subiri baada ya harusi yangu.” Sara alisema neno baada ya neno, “ ikiwa kitu kitaenda vibaya, sitakusaidia."
“… Sawa.” Thomas alikata simu bila kupenda, lakini moyoni hakufikiri kwamba jambo lolote lingeharibika. Akageuka, akapiga simu. "Nenda utafute anapoishi huyo b*tch Pamela Masanja."
•••
Katika hoteli ya kifahari ya ‘The Concord Hotel & Suites.’
Mhudumu alimuongoza Pamela na kusimama kwenye mlango wa chumba cha faragha. "Hiki ndicho chumba ambacho Bwana Malugu alipanga kwa ajili yako."
"Asante." Pamela aliusukuma mlango na kuingia ndani.
Rodney alikuwa ameketi mbele ya skrini ya kale. Alivaa shati la kahawia na vifungo viwili vya kwanza vilikuwa vimefunguliwa. Mikono ya shati ilikuwa imekunjwa, na macho yake yalikuwa makali kwenye uso wake mzuri, na kumpa mtazamo mbaya lakini wa mapenzi.
“Keti.” Akaelekeza kwenye kiti kilichokuwa kando yake.
Pamela hakuweza kuwa na wasiwasi naye na akageuka kuondoka, lakini alipojaribu kufungua mlango, aligundua kuwa umefungwa.
“Usiondoke. Kula. Chakula hakitakuwa na ladha kikiwa cha baridi.”
Rodney aliinuka na kumburuta hadi kwenye kiti. “Bi. Masanja lazima ulijisikia vizuri ulipokuwa ukizungumza kwenye kongamano leo. Nakubali, umenishangaa. Nilikosea juu yako hapo awali. Ninakupa toast hii kama msamaha, sawa? Una furaha sasa?"
Rodney alijimiminia glasi ya mvinyo mwekundu na kuinywa. Pamela aliitazama glasi ya mvinyo iliyokuwa mezani kwa muda kabla ya kwenda kumimina mvinyo ndani yake.
Rodney alifurahi, akifikiri kwamba alitaka kutoa toast, lakini bila kutarajia, aliinua mkono wake na kumwaga mvinyo wote kwenye uso wake mzuri.
"Pamela Masanja!" Uso wa Rodney ulibadilika sana. Alipokaribia kukasirika, Pamela alichukua chupa ya divai, akaifungua kola yake na kumimina vilivyomo ndani ya shati lake. Mvinyo ulikuwa baridi, na kusababisha Rodney kupiga kelele.
Aliruka pembeni na kuvua shati haraka, lakini suruali yake ilikuwa tayari imelowa. Suruali yake ilishikamana kwa nguvu kwenye mapaja yake, ikionyesha mistari ya kuvutia.
"Pamela Masanja, unataka kufa?" Rodney alikasirika. Hakuna mtu aliyewahi kuthubutu kumfanyia hivi. Mwanamke huyu alikuwa mwendawazimu! Anathubutu vipi kummwagia mvinyo?!
Alikuwa amepoa sana baada ya kuvua nguo zake. Alitetemeka, na kwa macho yake, hakutaka chochote zaidi ya kumla akiwa hai.
Kwa upande mwingine, Pamela alikuwa akitabasamu kwa furaha. “Nilifikiri haujaamka kabisa, kwa hiyo nilikumiminia mvinyo. Rodney Shangwe, nadhani umezoea sana kutetemekewa kwa kuwa bwana mdogo tajiri sana. Hujawahi kunitendea haki hata kidogo. Wakati ule, ili kumsaidia Sarah Njau, ulitamka sentensi ya kawaida ambayo karibu kuharibu maisha ya juhudi zangu. Kama hukunipenda, ungenifukuza tu. Kwanini ulilazimika kunifungia kabisa kwenye tasnia?”
Kadiri alivyozidi kusema ndivyo alivyozidi kupata hasira. Aliivunja chupa, na kusababisha vipande vya chupa kusambaa kila mahali.
Rodney aliruka kwenye kiti kwa woga na nusura ateleze kwenye vipande vya chupa. Baada ya yote, hakuwa amevaa shati. "Pamela Masanja, usifikiri kwamba sitathubutu kukupiga!" Rodney alimfokea.
"Endelea. Hata usiponipiga nitakupiga.” Pamela alitumia uma kuokota kipande cha nyama ambavyo vilikuwa bado vya moto kutoka kwenye sahani na kumrushia Rodney.
Rodney aliitazama jinsi chumba kilivyokuwa kimechafuka kwa fujo za kila aina na kumtisha, "Pamela Masanja, nitaita polisi ikiwa utatupa kipande kingine."
"Endelea. Zaidi sana, nitaambiwa kulipa pesa. Naweza kumudu.” Pamela alimtupia kila kitu mezani.
Rodney hakuweza kukwepa na aliweza tu kukimbilia kushika mikono ya Pamela. Mikono ya Pamela ilikuwa imezuiliwa, hivyo akageuza kichwa chake na kumng'ata kwa nguvu sikioni.
“Sawa!” Rodney alipiga kelele baada ya kuumwa na kuushika sehemu fulani ya mwili wake bila fahamu. Matokeo yake, alihisi kitu laini mikononi mwake. Alipogundua alichokuwa akikamata, tayari alikuwa amepigiwa goti katikati ya mapaja yake na Pamela. Macho yalimtoka kwa maumivu.
Ghafla, aliweza kuelewa maumivu ya Alvin siku nyingine. Haishangazi alikwenda hospitali kwa uchunguzi. Inaumiza sana.
"Tamu eeh?" Pamela alimtazama kwa dhihaka. “Yako haina maana hata hivyo.”
"Yangu hayana maana?" Rodney alijikunja kwa maumivu na nusura apoteze pumzi.
“Umewahi kuitumia kwa nani?” Pamela alicheka. “Umejitolea kwa Sarah Njau, lakini ataolewa na Alvin Kimaro hata hivyo. Hatakuwa na nafasi katika maisha yako. Unapaswa kuwa towashi tu. Sijawahi kuona mwanaume mjinga kama wewe.”
"Pamela Masanja, thubutu kusema neno moja zaidi…" Macho meusi ya Rodney yalikuwa yamefunikwa na hasira.
“Nimesema kitu kibaya? Nilishakuambiaga muda mrefu. Wewe ni mwanaume lakini bado una kelele kuliko mwanamke. Kuwa mwanamke katika maisha yako yajayo basi…”
Kabla Pamela hajamaliza, Rodney alimkimbilia na kumg’ata.
Macho yalimtoka Pamela na bila fahamu akajaribu kumpiga tena goti sehemu zake za siri. Wakati huu, Rodney alikuwa amejiandaa na kubana miguu yake haraka. Pamela alipoteza stepu na mwili wake ukaanguka moja kwa moja kwenye mikono ya Rodney.
Wakati huo, sauti ya hasira ya Bwana Malugu ilisikika nje ya chumba akimfokea mhudumu. "Mara nyingi mimi huja kwenye hoteli hii. Siamini kuwa ulimleta mgeni wangu kwenye chumba cha mtu mwingine. Mgeni wangu akipata madhara yoyote, sitakusamehe…”
Ndani ya chumba, Pamela aliogopa na kujitahidi sana. "Rodney Shangwe, niachie!"
"Hapana." Rodney aliuma mdomo wake kwa ukaidi na hakumuachilia.
Pamela hakuwa na chaguo ila kuuma, na kwa sababu hiyo, wote wawili waliangukia kwenye sofa.
Kisha, mlango ukafunguliwa. Bwana Malugu na meneja wa hoteli waliingia ndani haraka. Waliona tukio la shauku ndani na walipigwa na butwaa mara moja.
Bwana Malugu alikasirika sana hadi uso wake ukakunjamana. Rodney alilegea, na Pamela akamsukuma kwa nguvu. Ingawa nguo zake zilikuwa safi, kulikuwa na alama za meno kwenye midomo yake na rangi ya lipstick yake iliacha alama kwenye uso wa Rodney kwa uwazi sana.
“Bwana Malugu, uko kwa wakati. Yeye-”
"Nicole, ninaelewa. Alikutongoza, sivyo?”
Bwana Malugu alikatisha maneno yake. Alimkazia macho Rodney kwa ujeuri ambaye hakuwa amevaa shati na suruali yake ikiwa imelowa. "Bwana Shangwe, unaenda mbali sana. Kwa ajili ya kupata fomula tu, unawezaje kufanya kitu kama kuuza utu wako?"
Ingekuwa ni mtu mwingine, angekuwa na hasira kabisa. Lakini, Radney hakuwa na aibu. Alijipangusa kwa utulivu pembeni ya mdomo wake na kutabasamu huku akiinua nyusi zake. "Bwana Malugu, unaweza pia kujaribu kuuza utu wako, lakini Bi. Masanja anaweza kufikiria kuwa wewe ni mzee sana."
Uso wa Bwana Malugu ulilegea.
Pamela alichukua kitambaa na kujifuta pembeni ya mdomo wake kwa nguvu huku akimkazia macho Rodney. “Pole, Bwana Shangwe, lakini nadhani wewe ni mchafu sana. Mdomo wako huo ni kama choo cha umma. Nimechukizwa.”
Sura ya: 366
"Ulibusu choo hiki cha umma kwa furaha." Rodney akakonyeza macho. “Na ulinivua nguo zangu na kunimwagia divai. Nimependa michezo yako ya kusisimua kama hii.”
Kwa maneno yake, meneja wa hoteli na Bwana Malugu wote walimtazama Pamela kwa njia isiyo ya kawaida. Alionekana mrembo sana, lakini bila kutarajia, alikuwa jasiri na asiyejizuia kwa ndani.
“Bullsh*t!” Uso wa Pamela ukawa mwekundu kwa hasira.
Rodney alihisi faraja kadiri alivyozidi kumuona vile, na macho yake yalimtoka kwa fujo. “Sahau, sitasema mengi kuhusu mambo fulani. Baada ya yote, mwonekano wangu wa sasa unaweza kuthibitisha kila kitu.”
“Wewe una wazimu!” Pamela akampiga kofi na kuondoka.
"Halo, vipi kuhusu formula?" Rodney alifoka nyuma yake bila aibu.
"Endelea kuota!" Pamela aliondoka, na Bwana Malugu akamfuata mara moja.
Mara tu walipotoweka, Rodney alipiga chafya mara moja. Alianza kutetemeka huku akimpigia kelele msaidizi wake pale nje. "Herbert, vua koti lako na unipe."
Damn it! alikuwa anaenda kuganda hadi kufa kwa baridi la Nairobi.
Hakuwa amekula pia.
Herbert alimvulia Rodney koti lake kimyakimya. "Bwana Shangwe, mazungumzo ya fomula yaliendaje?"
“Ilikuwa sh*t. Hatukuwa hata tumeanza kuongea kuhusu fomula na yule mwanamke tayari ameshaanza kugombana nami.” Rodney alimtazama kwa ukali. “Mfuatilie Bwana Malugu. Haijalishi ni njia gani unayotumia, usiwaruhusu tu kusaini mkataba. Narudi nyumbani kuoga.”
Baada ya kuoga kwenye jumba lake la kifahari, Rodney alikasirika zaidi alivyofikiria juu ya Pamela. Akampigia Chester, akisema, “Uko wapi? Niko katika hali mbaya. Njoo tunywe pamoja nami.”
"Njoo mahali pa kawaida. Nipo na Alvin.” Chester alimwambia.
Rodney alipofika aliwakuta Alvin na Chester pekee yao. “Ni nyinyi wawili tu? Wako wapi Cindy na Sarah?”
Uso wa Alvin ulikuwa umezama kwenye giza la mawazo totoro. Hakuongea, na haikuwezekana kukisia hali yake.
Chester alitazama juu na kutabasamu. "Kwa hiyo tunatakiwa kuongozana na wanawake kila mahali tunapokwenda? Halo, nini kilitokea kwa mdomo wako? Hiyo ni nadra. Umeumwa na mwanamke?"
Kwa maneno hayo, Alvin naye alimtazama kwa uvivu.
Rodney alisema kwa hasira, “Sio mdomo wangu tu. Angalia sikio langu. Iiling’atwa hadi likatoka damu. Pamela Masanja, lazima alikuwa mbwa katika maisha yake ya zamani. Kitu cha kwanza alichofanya ni kunimiminia chupa nzima ya divai mwilini. Nilikaribia kuganda.” Kufikia hapo aligugumia kidogo kabla hajasema kwa aibu, "kwa hiyo, Chester, nisaidie kufanya uchunguzi. Sehemu yangu ya chini inauma kama nini baada ya Pamela kunipigia kwa goti. Alvin, hatimaye ninaelewa uchungu uliohisi.”
Chester alitoa macho kwa kuchukia. “Potelea mbali. Mimi si daktari wa andrology, lakini usijali. Alvin hakuweza kutembea moja kwa moja alipokuwa amepigwa nyeti zake na Lisa wakati huo, lakini alikuwa sawa mwishowe. Sidhani kama kuna shida yoyote itakutokea.”
“Sawa.” Rodney aliguna, “Pamela na Lisa kimsingi ni mtu na dadake. Hata mienendo yao ni sawa. Je, walikuwa na mshauri mmoja walipopotea katika miaka michache iliyopita?”
"Labda." Chester alimtazama Alvin kimaana.
Alvin aliwasha sigara. Alipokuwa akisikiliza maneno ya Rodney, moyo wake ulijikunja na kutabasamu.
"Alvin, unatabasamu nini?" Rodney aliuliza.
“Hakuna kitu.” Alvin akainua midomo yake. Hapo awali alitaka kutoka nje na kupumzika kwa sababu alikuwa amekasirika, lakini Rodney alipokuja na kueleza mambo yake, moyo wake ulipumua kidogo.
•••
Masaki. Dar es Salaam.
Lisa aliwarudisha nyumbani watoto wake wawili baada ya kucheza siku nzima.
"Mama, nataka kucheza kesho pia." Suzie alimkumbatia Lisa na kukataa kumuachia.
"Sawa, tutaenda kwenye aquarium kesho."
Lisa alikuwa akijiandaa kwenda kuoga wakati alipopokea ujumbe wa whatsapp kwenye simu yake uliotumwa na muuguzi wa hospitali kupitia simu ya baba yake. [ Bi. Jones, tafadhali njoo hospitalini sasa. Shinikizo la damu la Bwana Ngosha lilipanda ghafla usiku huu. Tulimpiga dripu lakini halijashuka.]
[Sawa, haraka mjulishe daktari kuhusu hali yake. Nitakuwa hapo muda si mrefu.]
Baada ya Lisa kukata simu, hakuwa na namna zaidi ya kupanga safari ya haraka kuelekea Nairobi. Alikata tiketi kwenye mtandao ya ndege iliyokuwa inaondoka muda wa karibu zaidi na baada ya kuoga na kujiandaa haraka haraka, aliwakusanya watoto wake na kuelekea uwanja wa ndege. Masaa manne baadaye alikuwa amefika kwenye makazi yake huko Karen Estate, Nairobi.
Ilikuwa ni usiku tayari, mida ya saa nne hivi. Aliwaambia watoto wake wawili, “Babu yenu hajisikii vizuri, kwa hiyo ni lazima niende hospitali sasa hivi kumuona. Mtabaki hapa nyumbani mlale sawa? Godmother wenu atarudi baada ya muda mfupi."
"Mama, tunaweza kwenda kumsalimia babu pia?" Lucas aliuliza huku amekunja uso.
“Sasa si wakati mzuri. Zaidi ya hayo, babu ni dhaifu sana hawezi kuzungumza na nyie. Tunaweza kwenda kumtembelea wakati fulani baadaye.” Lisa alijua wanawe hawakuwa wasumbufu. Aliwabembeleza hadi alipoona wameanza kukole usingizi.
Baada ya kuwafariji watoto wake wawili wapenzi, alikimbia hospitali akiwa hoi. Akiwa njiani kwenda huko, alimpigia simu Pamela, akimtaka arudi nyumbani mapema.
Kumbe wale watoto wawili walikuwa wamevunga tu kulala ili kumridhisha mama yao. Baada ya Lisa kuondoka, Suzie alikuwa wa kwanza kuamka. Alikagua nyumba nzima kutafuta vitafunwa. “Hehe. Nilijua mama angeficha chokoleti hapa. Alidhani nisingejua.”
Suzie akamtupia Lucas pakiti ya chokolate. “Unaitaka?”
“Sili kitu alichotukataza mama, alisema tutakuwa bubu.” Lucas alimjibu huku akiifuata laptop ya mama yake iliyokuwa mezani. Alipenda sana kuchezea kompyuta tangu akiwa mdogo kabisa.
Suzie hakuelewa ni kwanini mama yao aliwakataza kula chokoleti mara kwa mara. Aliona aina hii ya chakula ni tamu sana. Alihisi kwa kuwa mama yake hakufurahia yeye kula chokoleti, baba yake huenda angemruhusu. Hivyo Suzie akatamani kumtafuta Alvin.
Lucas aliwasha laptop. Na kwa kuwa eneo lile lilikuwa limeunganishwa na wi-fi, laptop ilishika mtandao wa internet mara moja. Lucas alikuwa anapenda sana kutazama katuni kwenye mtandao wa Youtube. Pamela alimfundisha jinsi ya kuingia huko kupitia simu na kompyuta na kwa sababu Lucas alikuwa na akili nyepesi ya kitoto, alikariri haraka.
Baada ya kufungua Youtube, mtandao ulionyesha video ambazo Lisa alipenda kutazama mara kwa mara. Kwa hivyo video nyingi zilizomuonyesha Alvin na Sarah zilionekana.
“Woooh! Lucas, ni baba yetu mchafu!” Suzie aliruka kwa mshangao. Wote waliifahamu vizuri sura ya baba yao kwani walionyeshwa na mama yao kwenye picha na video za simu.
“Bonyeza hiyo video tumuone baba…” Suzie aliingiwa na shauku ya ajabu.
Muda mfupi baadaye, Lucas akabofya video mojawapo na video ikaanza kutembea. Suzie aliyekuwa anakula chokoleti alimsogelea Lucas. "Wow, ni mtu mzuri sana! Yeye ni mzuri zaidi kuliko mjomba Kelvin. Lazima nipate mchumba ambaye ni mzuri kama yeye nikikuwa mkubwa."
“Baba yetu ni mchafu.” Lucas alimkazia macho. "Mama labda alidanganywa kwa sababu alikuwa na mawazo kama yako."
“Woooh, baba anaongea, anasemaje baba?” Suzie akatoa macho yake. Alvin alikuwa akihojiwa na waandishi wa habari kwenye video hiyo.
Lucas alijibu kwa sauti ya chini, “Mm. Kulingana na habari, anaenda kuoa mapema mwezi ujao. Mwanamke ambaye atamuoa ni Sarah Langa, na hivi ndivyo anavyoonekana.”
Suzie akaikazia macho sura ya Sarah aliyeonekana pembeni mwa Alvin, kisha akakunja midomo yake. “Ni mbaya sana. Yeye siyo mrembo kama Mama. Baba yetu mchafu ana mke mbaya sana."
“Ndiyo.” Lucas alikodoa macho. “Wamemuumiza mama. Ni lazima tulipize kisasi kwa ajili ya mama.”
“Hakika, hakika. Kwa hivyo tutalipaje kisasi?" Suzie alisisimka.
Wakati huo, ghafla sauti ya ajabu ilisikika kutoka nje. Kulikuwa na watu wanakuja!......ITAENDELEA.....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
