JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................283-284

Sura ya: 283

“Ooh! Mungu wangu, ni kosa letu. Hatukuwa makini,” Lisa alinong’ona kwa masikitiko.
'Ni kweli." Pamela alikasirika. “Mjomba Boris alisema kuwa hakuweza kuwasiliana na Aunty Jennifer tangu alipoondoka nyumbani asubuhi ya leo kwenda kufungasha, kwa hiyo nilikuja kumtafuta nyumbani kwao. Watumishi wao wote walikuwa wameondoka na ilinibidi kupanda juu ya ukuta ili niingie. Alikuwa amelala kwenye dimbwi la damu kwenye sakafu ya bafuni na alikuwa ameacha kupumua nilipomkuta. Polisi walikuja hapo awali na kusema lazima alianguka na kugonga kichwa chake chini. Wanafikiri alikufa baada ya kupoteza damu nyingi.”
“Inawezekanaje?” Lisa alisisimka hadi kwenye uti wa mgongo wake. "Alionekana kuwa mzima kabisa, angewezaje kuanguka bila sabau. Uliangalia kamera za uchunguzi?"
"Kamera zote zimezimwa tangu juzi," Pamela alijibu, "Lakini niliangalia kamera za cctv za nyumba ya jirani. Sarah alionekana akiingia asubuhi ya leo lakini aliondoka baada ya nusu saa.”
Lisa alikuwa anatetemeka kwa hofu na hasira. “Hakika anahusika katika hili. Anamchukia Aunty Jennifer.”
"Najua, lakini daktari wa magonjwa alisema haina uhusiano wowote na mauaji ya kupangwa. Hawakuweza kupata alama za vidole vya mtu mwingine wala dalili inayoonyesha kuwa ameuawa. Mbali na hilo, Aunty Jennifer inakadiriwa kuwa alifariki majira ya saa 9:00 asubuhi lakini Sarah alitoka nyumbani saa 8:30 asubuhi”
Baada ya kimya kifupi cha pande zote, Pamela alisema huku midomo ikimtetemeka, “Lisa, nilisoma hapo awali kwamba baadhi ya wanasaikolojia wanatisha kwani wanaweza kutumia njia ya hypnosis kumpumbaza mtu ili…”
“Unamaanisha… Sarah alimpumbaza kisaikolojia Aunty Jennifer?” Lisa alikuwa akitetemeka mwili mzima.
“Hilo linawezekana. Angeweza kumpambuza Aunty Jennifer katika hali ya nusu fahamu ili aanguke kwa bahati mbaya. Kwa njia hii, hakutakuwa na ushahidi wowote unaoelekeza kwa Sarah kama muuaji.”
Lisa alisugua paji la uso wake. Kifo cha Jennifer kilitia shaka sana. Charity angejisikia vibaya kiasi gani ikiwa angejua kuhusu jambo hilo akiwa gerezani? Boris pia. Angeachwa peke yake bila mtu kando yake. “Wacha tujaribu tuwezavyo kumficha mjomba Boris hili kwa sasa. Ninaogopa hataweza kuchukua habari hii kwa sasa. Tunapaswa kuingilia kati na kushughulikia mazishi ya Aunty Jennifer.”
•••
Saa mbili usiku Lisa alirudi kwa Mzee Kimaro akiwa amechoka. Alipoingia tu mlangoni, akawaona Alvin na Sarah wakiteremka kwenye ngazi wakiwa wamekaribiana. Mwanamume alikuwa amevalia nguo za mapumziko zenye mistari myeusi na myeupe. Nywele zilizostawi kwenye kichwa chake zilifanya macho yake ya ukali yaonekane laini na tulivu. Mwanamke, kwa upande mwingine, alikuwa amevalia suruali ya jeans ya kubana na kitop kilichofichua kiuno chake chembamba na ngozi nyororo. Ilionekana kana kwamba walikuwa wamiliki wa nyumba hiyo. Lisa alikosa raha kuona jambo hili. Alikuwa mrembo sana kuliko Sarah lakini ngozi yake haikuwa katika hali yake nzuri tangu kuharibika.
“Bi. Kimaro, umerudi. Tumemaliza matibabu ya leo kwa Alvinic,” Sarah aliongea kwanza kwa sauti ya upole.
“Unajua ni saa ngapi sasa hivi? Tayari saa usiku ndiyo unarudi. Baada ya kukuruhusu urudi kazin tayari ushaanza kuruka ratiba ya chakula cha jioni nyumbani.” Alvin alikunja uso, akionekana kuchukizwa. Yeye ndiye alitaka Sarah amtibu pale nyumbani lakini alifika tu nyumbani baada ya matibabu yake kuisha.
“Alvinic, usiseme hivyo. Wanawake wanahitaji kuwa na uhuru wao pia,” Sarah alisema huku akitabasamu.
Lisa alihisi kukasirishwa na sauti zao. "Bi Njau, umesikia kwamba mama yako wa kambo amefariki bafuni leo?"
“Nilisikia…” Macho ya Sarah yalimtoka. "Nilienda kumsalimia tu asubuhi ya leo na muda mfupi baadaye, nikasikia taarifa za kifo chake.”

“Kweli?” Kengere ya tahadhari iligonga kichwani mwa Lisa huku akikumbushwa ghafla dhana ya Pamela. Mwanamke huyu alitisha. "Nilienda kumtembelea baba yako hospitalini leo. Anatia huruma sana. Alikuwa anamtegemea tu mkewe llakini naye amekufa na hakuna mtu wa kumtunza. Hata alikuwa akihangaika kuchukua beseni la kujisaidia peke yake. Wewe na kaka yako mmefanikiwa na ni matajiri sasa. Angalau mnapaswa kumwajiri mlezi hata kama humpendi baba yako.”
“Uko sahihi. Mimi si binti bora.” Sarah alionekana kujuta.
"Kweli, hajui kuwa umejitahidi kwa kadri anavyoweza?" Alvin alimtazama Lisa kwa sura ya kuchukizwa kidogo baada ya kusema vile. “Lisa, hayo ni mambo yao ya kifamilia. Hujui mengi kuhusu hilo, na hupaswi kuingiza pua yako ndani yake pia. Sarah alikuwa amejaribu kuajiri mlezi lakini baba yake alimkataa. Nilimsikia akizungumza kuhusu hili mapema mchana wa leo. Anapanga kuandaa mazishi ya kifahari kwa mama yake wa kambo, unataka afanye nini zaidi ya hapo?”
Lisa alijisikia kumpiga Alvin kichwani alipoona jinsi alivyokuwa amechukua upande wa Sarah kabisa. Ina maana hakuona kwamba Sarah alikuwa ni mwanamke mjanja?
“Ni sawa, Alvinic. Inaonyesha kwamba Lisa ni mkarimu kwa vile anamjali rafiki yake. Niondoke sasa. Nahitaji kwenda kushughulikia mazishi ya kesho,” Sarah alisema huku akitabasamu kwa uchungu.
Lisa alikosa la kusema. Huenda Jennifer asingepumzika kwa amani ikiwa Sarah ndiye aliyekuwa akiandaa mazishi yake. "Hapana, mimi na Pamela tutashughulikia mazishi ya Aunty Jennifer."
“Usilete matatizo. Unaweza kufanya nini na tumbo lako kubwa la ujauzito?" Alvin alisema kwa hasira, "Wewe si binti ya Jennifer, kwa hivyo huwezi hata kushika maiti yake."
“Lisa, usijali. Nitalishughulikia hili.” Sarah alitabasamu.
Lisa aliuma mdomo. Angewezaje kutokuwa na wasiwasi? Sarah aliweza hata kuwa sababu ya kifo cha Jennifer. Mtu matata kama yeye hakika angemfanya Jennifer ashindwe kupumzika kwa amani.
Baada ya Sarah kuondoka, Lisa moja kwa moja alikataa kukubaliana na Alvin.
“Lisa, bado una hasira na mimi kuhusu kilichotokea asubuhi? Kwanini kila mara tunagombana kuhusu familia ya Njau? Nakuahidi nitakaa mbali na Sarah baada ya ugonjwa wangu kupona.” Alvin alimshika mkono.
Lisa aligeuka ghafla na kumtazama kwa hasira. “Alvin, unatambua kwamba huwa unamtetea sana Sarah anapokuwa karibu? Inafanya nionekane kama mimi ni mtu asiye na akili.”
Alijisikia huzuni. “Lisa, unaweza kuacha kunikera kila unapokutana na Sarah? Kwanini unajali sana mambo ya familia ya Njau?”
"Sawa, kwanini na wewe unamjali sana Sarah?" Akashusha pumzi ndefu kwani hakutaka kubishana naye. Baada ya yote, umbali kati yao uliongezeka zaidi baada ya kila mabishano. Hata hivyo, hakuweza kujizuia kulipiza kisasi baada ya kusikia maneno ya kijinga yaliyotoka kinywani mwake.
Lisa aliufunga mlango kwa nguvu huku akihisi kuishiwa nguvu. Hakuweza kufikiria jinsi Charity angehuzunika baada ya kujua kwamba mama yake alikuwa amefariki.
•••
Siku iliyofuata. Pamela alimpigia tena wakati Lisa anakula kifungua kinywa. "Lisa, mjomba Boris amekufa kwa mshtuko wa moyo asubuhi ya leo."
“Clang!” Kijiko alichokuwa ameshika kilianguka kwenye sahani.
Pamela akaendelea. “Nilipotoka kwenda kununua kifungua kinywa cha Mjomba Boris asubuhi ya leo, Thomas alifika na kumwambia kuhusu kifo cha Aunty Jennifer. Mjomba Boris alipata mshtuko wa moyo papo hapo na alikimbizwa kwa huduma ya dharura. Daktari alisema mjomba Boris amekufa baada ya kupoteza matumaini ya kuishi.” Pamela alianza kulia.
“Nakuja mara moja.” Lisa alisimama haraka na kuacha kula.
Alvin akamshika mkono. "Unaenda wapi? Keti na upate kifungua kinywa.”
Lisa aliusukuma mkono wake kwa nguvu na kumfokea kwa macho ya machozi, "Mjomba Boris amekufa! Thomas alienda hospitali na kumweleza kuhusu kifo cha Aunty Jennifer. Wenzi hao walipendana kwa mioyo yao yote. Huyo mjinga Thomas ndiye wa kulaumiwa kwa hili. Yote ni kwa sababu yako. Kwanini ulimsaidia mtu kama huyo? Hakuna jambo baya lingetokea kama angefungwa muda mrefu uliopita.”

Uso mzuri wa Alvin uliganda na Lisa akaendeleakumsomea. “Una furaha sasa? Charity amefungwa maisha na wazazi wake wote wamekufa. Hatimaye, Sarah na Thomas wako mpendwa ndio pekee waliosalia katika familia ya Njau.” Lisa alimtazama kwa masikitiko na kunyata bila kuangalia nyuma.

Sura ya: 284

Pamela alikuwa akibishana na ndugu wa Njau wodini wakati Lisa alipofika hospitalini baada ya muda mfupi sana.
"Ondoka mbele yangu, Pamela. Sina neno kama unataka kuchukua maiti ya baba yetu. Lakini kama kweli unataka…” Thomas alitania na kutabasamu kwa hasira. "Kubali kwanza kuwa mwanamke wangu na ninakuhakikishia kwamba unaweza kupanga mazishi ya baba yangu."
“Una akili kweli wewe, au laana inakusumbua? Baba yako amekufa tu lakini unacheka huku unawaza mapenzi?” Pamela alikasirika. "Asingekufa kama si wewe kumletea habari za kushtukiza."
“Kosa langu ni vipi?” Thomas akacheka tena kifedhuli. “Kujua ni lazima angejua tu hatakama nisingemwambia. Kama ni kufa angekufa mapema au baadaye,” alijibu, bila kujali. "Kwa kweli sioni hata maana ya kuwa na huzuni juu ya mzee huyo. Hakika alistahili hilo.”
“Thomas Njau, wewe ni shetani kabisa.” Pamela alishangaa kabisa. “Ni sawa kweli kumwambia maneno hayo mtu aliyekuleta katika ulimwengu huu na kukulea?”
“Ni kosa lake kwa kututelekeza na kuwa karibu na Jennifer na binti yake. Kwanza nimemfanyia upendeleo sana hata kuja kuchukua mwili wake leo.”
“Utapigwa na radi!” Kwa hasira, Pamela alimpiga ngumi ya kifua.
“Unathubutu vipi kunipiga ngumi? Mwanamke mjinga, nitakuchuna ukiwa hai!” Thomas akainua mkono kumpiga Pamela.
Lisa haraka alimkinga Pamela nyuma yake na kumtazama kwa jeuri. “Jaribu kunipiga. Nimebeba vitukuu vya familia ya Kimaro. Ukithubutu kutuumiza, basi huenda ukalazimika kujiondoa kwenye nafasi ya ukurugenzi ambayo ndiyo umetoka kuichukua tu.”
Thomas aliganda kwa sekunde moja kabla ya kumdhihaki. “Vitukuu wa familia ya Kimaro? Kwa hiyo? Dada yangu atakuwa na Alvin muda si mrefu.”
“Kaka...” Sarah alikunja uso kabla ya kumtikisa kichwa.
“Kwani uongo? Ninasema ukweli tu. Nafasi hii ni yako hata hivyo na yeye ndiye aliyeiba nafasi yako. Nadhani anapaswa kujiongeza kwa kuwa umerudi. Hupaswi kuingilia furaha ya dada yangu na Alvin,” Thomas alisema na kutoa mkoromo wa dharau.
Lisa akajibu kwa kejeli, “hakuna maana ya kuniambia mimi hivi. Kama una ubavu ongea maneno hayo mbele ya Alvin uone.”
Thomas alimuangalia sana mwanamke yule. “Nimekosea? Hebu tazama jinsi Alvin anavyomjali dada yangu! Alinisaidia kurejesha New Era Advertisings mara tu aliporejea na hata kuwezesha biashara kubwa yenye thamani ya shilingi bilioni kumi kwa kampuni yetu jana. Angalia vizuri uso wako mbaya kwenye kioo. Unawezaje kujilinganisha na dada yangu na sura yako ya kutisha?"
Pamela akaruka kama risasi iliyofyatuliwa ghafla. "Kama Lisa asingeharibika sura, angeonekana mrembo mara elfu zaidi ya yule mjinga."
“Unamwita nani mjinga? Omba msamaha kwa Sarah sasa hivi!” Rodney, ambaye alikuwa ameingia tu chumbani na kusikia sentensi ya mwisho, alionya kwa uso wa mawingu.
Tabasamu baridi lilienea kwenye uso wa Pamela. “Nimesema kitu gani kibaya? Kwanini niombe msamaha? Ulisikia kile Thomas alichotuambia kabla?"
“Bwana Shangwe, umekuja kwa muda muafaka. Wanawake hawa wamekuwa wakimfokea dada yangu,” Thomas alisema mara moja, “Lisa hata alitutishia kwa sababu ana ujauzito wa Alvin. Pamela hata alinipiga ngumi. Angalia, alama ya uvimbe bado inaonekana."
Rodney alimtazama kabla ya kuelekeza macho yake ya chuki kwa wanawake hao wawili. “Ombeni msamaha.”
Jambo hili lilimkasirisha sana Pamela. "Rodney Shangwe, unaumwa kichwani? Je, unaamini ujinga wowote wanaosema…”
Rodney akamjibu kwa kofi. Pamela aliganda kabisa, huku Lisa akiwa amekasirishwa na hilo. “Unawezaje kumpiga rafiki yangu…”
Kabla hajamalizia sentensi yake, Pamela tayari alikuwa amejitupa kwa Rodney kama mnyama wa porini, akimng’ata na kumpiga kwa fujo.
“Unathubutuje kunipiga makofi wewe mbwa?! Wewe usiye na akili, tena nimekupania kwa muda mrefu sana.” Alivuta na kuvuta nywele zake. Kumbe mtu mwenyewe alikuwa na mikwara tu hakuwa hata na nguvu. Mwishowe, alimng'ata usoni.
“Unapaswa kula korosho zaidi ili kuimarisha ubongo wako wenye akili za matope. Lakini nadhani umechelewa sana na hali yako. Sina cha kupoteza na sikuogopi kwa lolote. Tayari umenifukuza kazi yangu na kuniweka kwenye blacklist, kwa hiyo sikuogopi tena.” Pamela alifoka.

Pamela alikasirika sana. Alimpiga ngumi na teke Rodney, na kuchana shati lake na karibu amnyofoe nywele kwa kuzivutavuta. Hata uso wake ulikuwa umejaa alama za meno na alama za vidole. Wengine walitazama tu, wakiwa wamepigwa na butwaa.
Rodney, ambaye hakuwahi kupigwa ngumi na teke namna hiyo na mwanamke, alitumia juhudi nyingi kuhangaika kujinasua kutoka kwa Pamela aliyekuwa mkali kama paka aliyekanyagwa mkia.
“Unabipu kifo!” Rodney alikakamua na kumsogelea kwa hasira huku akionekana kudhamiria kumwangamiza mwanamke huyo. Lisa haraka akakimbia kwenda kumkumbatia rafiki yake kwa nguvu.
“Rodney!” Sauti ya Alvin ya onyo ilisikika pale chumbani ghafla. Alijivuta na kumkinga mkewe ndani ya sekunde chache.
Alvin alikuwa amekimbilia eneo la tukio baada ya kujua kwamba Rodney alikuwa ameenda hospitali pia. Lisa na Rodney hawakuwa wakipatana vizuri tangu ishu ya Maurine itokee, hivyo Alvin alihisi wangeonana macho kwa macho ingeleta shida kubwa na pengine wangembana kabisa. Hakuwa amekosea.
“Alvin mbona bado unawasaidia? Angalia hali niliyo nayo! Yote ni kwa sababu ya Pamela Masanja!” Rodney alipiga kelele.
"Ni wewe uliyempiga Pamela kwanza." Lisa alimtazama kwa hasira.
“Kwa sababu alimwita Sarah mjinga. Isitoshe, ninyi wawili mmekuwa mkimdharau Sarah na kaka yake tangu mwanzo. Naapa nitakufundisha somo leo hata iweje!” Rodney alikasirika kadri alivyozidi kuwaza.
Pamela pia hakurudi nyuma. "Nilifanya hivyo kwa sababu Thomas alisema Lisa ana sura mbaya."
"Ulisema mke wangu ana sura mbaya?" Alvin alimtupia macho ya kutisha sana Thomas.
Thomas alitetemeka kabla ya kusema kwa sauti ya kigugumizi, "Sikusema."
Pamela alikoroma. "Sio tu kwamba alisema Lisa ana sura mbaya, alisema pia ajipange kuachana na wewe kwa sababu dada yake mdogo amerudi. Hata alijisifu kuwa hivi karibuni Sarah atakuwa na ujauzito wa mtoto wako pia.”
"Pamela Masanja, acha uongo!" Thomas alipiga kelele. “Sarah, uwe shahidi yangu. Sikusema lolote kati ya hayo. Kinyume chake, hao wawili walikuita mjinga.”
"Nilisikia hivyo pia," Rodney alisema kwa upole.
"Sarah, nataka kusikia kutoka kwako." Alvin akahamishia macho yake kwa Sarah.
Sarah alitabasamu kinyonge. “Achana nayo tu, Rodney. Wacha yaliyopita yawe yamepita. Kipaumbele sasa ni kumpeleka baba yangu kwenye nyumba yake ya milele. Bi Masanja, Bi Kimaro, kwa kweli siko katika hali ya kubishana hivi sasa.”
Lisa alikunja uso kwa jibu lake la kijanja. Sio tu kwamba aliweza kuonyesha kuwa alikuwa anasamehe, lakini alidokeza kwa hila kwamba ni Lisa na Pamela ambao ndio walikuwa wakorofi.
"Alvin, umesikia hivyo?" Rodney alitabasamu kwa kejeli. “Mpeleke mkeo nyumbani na umuonye. Sarah kasamehe, lakini sitawaacha tena wakati mwingine nitakapowaona wanamnyanyasa tena. Hata na wewe ukiwepo.” Rodney alimaliza. Alvin alikunja uso lakini hakuzungumza kitu.
Ghafla, Lisa alicheka. “Nilijua haya yangetokea. Nilijua hakuna ambaye angetuamini mimi na Pamela hata tujitetee kiasi gani. Ndiyo maana… nilikuwa ninarekodi.”
Akatoa simu yake. Rekodi ya sauti ilichezwa. Maluweluwe yalionekana kwenye sura ya kila mtu. Thomas aliogopa na kufadhaika huku uso wa Sarah ukiwa umepauka kama mzimu. Uso wa Rodney pia ulikunjamana. Kwa kweli hawakutarajia Thomas angesema maneno yale ya kutisha.....ITAENDELEA..

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.