JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................161-162
Sura ya:161
Macho ya Melanie yakaangaza. Alihisi Alvin kwa kweli alimpenda zaidi! “Asante, Bwana Kimaro. Mimi… nakupenda.”
Baada ya kusema maneno hayo matatu, aliinamisha kichwa chini kwa aibu bila kuona dalili ya dhihaka machoni pa Alvin. Upendo?
Alikuwa amekutana naye mara chache tu, lakini tayari alikuwa anazungumza juu ya mapenzi.
•••
Ofisini, Meneja wa Mawenzi Investments Bwana Freddie Ngololo aliripoti kwa Lisa kwa uso wa huzuni alipofanya naye mkutano kwa njia ya video. "Mwenyekiti Jones, ardhi ya shamba ambayo tumekuwa tukiifuatilia huko Nairobi imepewa kampuni ya Cosmos."
Lisa alipigwa na butwaa. "Si ulisema jana kwamba taratibu zote zinashughulikiwa?"
"Ndiyo, wakati nashughulikia niilisikia kwamba Bwana Kimaro ameingilia kati na kuagizwa ardhi hiyo ipewe Cosmos.” Meneja alifafanua. “Cosmos Limited ni kampuni ambayo ipo chini ya familia ya Mahewa. Nilisikia kwamba familia ya Mahewa iko pamoja na familia ya Kimaro kwa sasa.” Meneja Mkuu Ngololo alieleza kwa sauti yenye uchungu. "Tulitumia pesa nyingi katika shamba hili, lakini sasa limepotea."
Lisa alikuwa kimya na hakuzungumza kwa muda mrefu. Alijua vizuri jinsi familia ya Mahewa ilivyopatana na familia ya Kimaro. Kwa kweli hakutarajia kwamba Alvin angeisaidia familia ya Mahewa bila kusita. Alifikiri kwamba angalau angefikiria mapenzi ambayo walikuwa wameshiriki hapo awali…Hapana, hakukuwa na mapenzi hata kidogo!
"Tunaweza kubadilisha ardhi?" Lisa aliuliza.
"Makampuni mengi yanapigania kupata ardhi huko. Bado kuna ardhi, lakini ni ghali sana. Kulingana na bajeti ya kampuni, hatutaweza kupata faida yoyote.” Meneja Mkuu Ngololo alisema kwa huzuni, “Mwenyekiti Jones, labda hatuko tayari kwa sasa kujipanua huko Nairobi. Hatuna ushawishi huko Kenya, kwa hivyo ni vigumu sana kuingia kwenye mduara wa biashara huko.”
"Kama hatuwezi kupambana kupata hiyo ardhi, basi badilisha mbinu. Ninavyojua ni kwamba Mawenzi inaweza kujipanua katika nyanja nyingi tofauti. Matibabu, fedha, utalii… Mji huu una sifa ya kimataifa. Kuna fursa za kupata pesa kila mahali,” Lisa alisema kwa upole, “Ni kwa kukujipanua katika nyanja mbalimbali tu ndipo hatutaohofia ushindani katika siku zijazo.”
Meneja Mkuu Ngololo alikubaliana. “Uko sahihi. Nitaitisha kikao kujadili hili mara moja.”
Saa nne usiku, Lisa aliuburuta mwili wake uliochoka hadi ndani ya jumba la kifahari la baba yake na kumuona Melanie akiwa amejiegemeza kwenye sofa. Macho yake yalijaa dhihaka.
“Mambo yaliendaje? Vipi, baba yako alikusaidia kupata lile shamba?” Melanie alidhihaki. “Kwa neno moja tu kutoka kwangu, Bwana Kimaro akanisaidia bila masharti. Hakuna anayeweza kushindana na Bwana Kimaro.”
Lisa hakujishughulisha hata kumtilia maanani na moja kwa moja akaelekea chumbani kwake. Baada ya kuufunga mlango, aliuegemea kwa muda. Kifua chake kilimbana, na kilikuwa kikimuuma. Alvin kweli alikuwa ni mshenzi! Haijalishi kama alikuwa wakili hapo awali au kijana tajiri wa familia ya Kimaro sasa, alikuwa anaweza kumshawishi mtu yoyote kufanya anachotaka. Alimpa saluti!
Lisa alikuwa kamaliza tu kuoga na kuwa tayari kwenda kulala na mara simu yake ikaita ghafla. Ilitoka kwa nambari isiyojulikana. Alibonyeza kitufe cha kujibu na sauti ya kijeuri ikasikika. "Njoo. Chumba changu ni kichafu na kinahitaji kusafishwa.”
Lisa akashusha pumzi ndefu. Baada ya kuisikia tu sauti hiyo ilimtosha kupasuka kwa hasira. Alitaka akafanye usafi chumbani kwake katikati ya usiku, alikuwa na wazimu? Au alikuwa na ajenda gani?
“Samahani, umepiga nambari isiyo sahihi. Nadhani ni sahihi zaidi kwako kuita kampuni ya usafi wa nyumba,” Lisa alijibu kijeuri.
Alikuwa karibu kukata simu ambapo Alvin alicheka tena kwa dharau. “Hakika, nitatuma tu video hiyo nzuri ya binti wa thamani wa familia ya Ngosha akiwa amejifunga mtandio akinengua ndembendembe mbele ya kundi la wanaume. Aidha uje au uandae majibu ya kuridhisha kumpa Bwana Ngosha." Alvin kisha akakata simu.
Lisa alishika kichwa chake kwa maumivu na kumlaani yeye na mababu zake wote kabla ya kuendesha gari hadi mtaa wa Oasis ambako Alvin alikaa.
Mtaa wa Oasis ulikuwa katika eneo lenye ustawi zaidi katikati mwa jiji. Bei ya futi moja ya mraba ya ardhi inaweza kuuzwa kwa mamia ya maelfu ya dola, na Alvin alikuwa na upenu wa futi za mraba 400 katika eneo hilo.
Alifungua mlango kwa ufunguo aliopewa jana yake na Alvin na kuingia ndani, katika sebule hiyo yenye kung'aa, Alvin alikuwa amekaa kwenye sofa la ngozi huku mguu mmoja ukiwa juu ya mwingine katika mtindo wa kukunja nne, mikono yake ikiwa juu ya kisigino. Mikono na miguu yake iliyoinuliwa ilimfanya atoe haiba ya kifalme. Alitoa sauti ya uvivu lakini ya kifahari.
Bila hata kumwangalia, Lisa alienda moja kwa moja jikoni kutafuta zana za kufanyia usafi. Hata baada ya kutafuta kwa muda mrefu, hakuweza kupata japo fagio tu. Alikwenda kwenye kibaraza.
Alvin alikuwa ameketi kimya kwenye sofa kwa muda sasa, na uso wake ulikuwa ukizidi kuwa jeuri. Nini kilikuwa kikiendelea? Kwa nini hakumuuliza wala kumkaripia kwa kumpa Farres Mahewa shamba alilikuwa akilipambania mara tu alipomwona? Kwa nini hakuwa akimbembeleza ampatie yeye badala yake? Maandishi yalikuwa tofauti na vile alivyofikiria, na akainuka kwa jeuri kumfuata hadi kibarazani.
Lisa hatimaye alipata ufagio kwenye kibaraza. Alipogeuka, aligongana naye kwa nguvu na kujibamiza katika kifua chake. Pua yake iliuma kana kwamba imevunjika. "Alvin, unafanya nini?"
“Umechukua maneno yangu mdomoni.” Alvin alihisi kama amewekewa sumu na Lisa. Alikasirika zaidi wakati akimwona yeye hajakasirika.
“Si uliniambia nije nikusafishie nyumba yako? Nimechelewa sana sasa, kwa hiyo nataka tu kumaliza harakaharaka nikalale. Tafadhali nipishe nipite.” Lisa alimzunguka na kuanza kufanya usafi sebuleni kwa umakini.
Alvin alimtazama akifagia sakafu kwa makini na akatamani sana kumnyang’anya na kuutupa ule ufagio. Mwanamke mjinga huyo! Ina maana, kweli alifikiri kwamba alimuita hapo kusafisha nyumba?
"Lisa Jones, huna la kuniambia?" Alvin alijikuta akifoka bila kujua. Ikiwa angeweza kumwomba na kumbembeleza kwa uradhi wake, angefikiria kurudia ahadi yake kwa Melanie na kumrudishia shamba hilo.
Lisa alinyamaza na kutikisa kichwa. "Hapana."
Alvin alimtazama kwa muda na kuamuru kwa sauti ya kijeuri, “Nenda kasafishe bafuni kwanza kabla ya sebuleni na chumbani. Safisha sinki la kuogea na ujaze maji. Nataka kuoga.”
Lisa alijisalimisha akaweka ufagio pembeni na kupanda juu. Bafu ilikuwa kubwa, karibu mita mbili kwa upana, na lililojengwa kifahari. Sinki la kuogea lilikuwa kwa chini, angeweza tu kuchukua kitambaa na kuinama ili kulifuta kabla ya kujaza maji.
Alvin alipoingia ndani, alimuona Lisa akiwa ameimana katika hali ya kutatanisha sana. Kiuno chake kilikuwa kimejipinda juujuu na suruali yake ilikuwa imeshuka chini kidogo, ikifichua sehemu kubwa ya kiuno chake chenye ngozi iliyofanana na satin huku iking'aa sana. Mgongo wote pia ulikuwa wazi.
Sura ya: 162
Macho ya Alvin yalitiwa giza, na alikuwa karibu kumfuata kwa nyuma na kumshika kiuno, lakini mara simu ya Lisa iliita na akasimama ghafla.
Lisa hakumuona Alvin akiwa amesimama nyuma yake akatoa simu yake ili kuipokea. Jina la Kelvin Mushi liliangaza kwenye skrini. Alikuwa akisitasita kujibu simu. Baada ya yote, hii ilikuwa nyumba ya Alvin, ambayo ilimfanya ahisi hatia.
Aliinyamazisha na kuamua kuipuuza, lakini mkono uliokuwa nyuma yake ghafla ukaipokonya simu yake. Lisa aliruka kwa mshtuko na kutazama nyuma. Alvin alicheza na simu yake huku akilitazama jina kwenye skrini. Tabasamu la dhihaka lilienea kwenye midomo yake. “Kwanini hutaki kujibu simu ya mchumba wako?”
"Alvin, nirudishie simu yangu!" Kwa haraka Lisa alinyoosha mkono kuikamata, lakini Alvin alikuwa ameinyanyua juu kiasi kwamba hakuweza kuifikia.
“Una wasiwasi?” Macho ya Alvin yalikuwa kama barafu huku dharau yake ikizidi kuongezeka. “Unaogopa kwamba mchumba wako atagundua kuwa uko nami usiku huu?”
“Umemaliza?” Lisa alikasirika sana sasa.
"Una mjali sana eeh?" Macho ya Alvin yalimkazia, moja kwa moja akabonyeza kitufe cha kujibu. Sauti ya joto ya Kelvin ilisikika kutoka upande mwingine.
“Lisa, unafanya nini? Imekuchukua muda mrefu kujibu simu.” Lisa aliogopa sana hivi kwamba moyo wake ulikuwa karibu kusimama. Alimtazama sana Alvin asije akaongea.
Hata hivyo, Alivin alikaa kimya na kuweka simu kwenye kipaza sauti. Kisha, akaegemea sikio lake na kusema kwa sauti ya sumaku, “Usipomjibu, basi nitamjibu.”
Lisa hakujua alichokuwa akipanga na aliweza tu kumjibu Kelvin kwa pumzi ya shwari. "Oh, nilikuwa naoga na sikusikia simu."
“Hujanipigia simu siku nzima ya leo, kwa hiyo nimekumiss kidogo,” Kelvin alisema kwa upole. “Unaendeleaje lakini?”
Hali ya hewa katika bafu ilishuka ghafla hadi kiwango cha kuganda. Lisa alimtazama Alvin kwa macho makali na nusura apige kelele kwa maumivu. Mwanaume huyo alimng'ata sikio kweli!
Aligeuka na kuutazama uso wa Alvin wenye chuki. Alikuwa akitabasamu vibaya na kumshika mikononi mwake, akiuzika uso wake shingoni mwake na kumbusu shingo yake bila ya kujali.
Kelvin aliendelea kuuliza, “Mbona huongei? Je, hukunimiss?”
"Mimi ... Pve nimekuwa na shughuli nyingi sana siku hizi chache zilizopita." Lisa alijitahidi kujizuia.
“Umechukua hilo shamba?”
"Hapana." Lisa aliuma meno huku akiachia sauti ya msisimko. Alvin alikuja mbele yake na kumbusu kwenye midomo yake. Alihamia mbali, lakini bado Alvin alimfuata na kuendelea kumsumbua.
Kelvin alisikika akiwa na huzuni. “Ni bahati mbaya kwamba sipo na wewe na siwezi kukusaidia kwa lolote.” Mdomo wa Lisa ulizibwa na Alvin hivyo hakuweza kusema lolote. Kelvin aliendelea, “Nitakuja Nairobi hivi karibuni, kisha tutakuwa pamoja, sawa?---Lisa, mbona huongei chochote?”
Lisa alibanwa kabisa na busu la Alvin na aliweza kutoa sauti laini tu. Kwa haraka akainyakua simu kutoka mkononi mwa Alvin na kusema, “Bado nina mambo ya kufanya hapa. nitakata simu sasa hivi.” Kwa haraka akabonyeza kitufe cha mwisho na kumsukuma Alvin kwa nguvu. Macho yake mazuri yalijawa na aibu na hasira.
"Alvin, umezidi sana sasa!"
“Nimezidi?” Alvin alicheka. "Je, ulikuwa na uhusiano wa karibu sana nilipokuacha naye kwa siku hizi chache eeh?"
"Hapana! Huwezi kuamini hata hivyo, haina maana.” Lisa alisema kwa kukata tamaa. “Bafu lipo tayari. Nenda kaoge!” Alimsukuma na kuondoka. Moyo wake ungesimama ikiwa angemwacha Alvin aendelee kumbusu.
“Nenda uniletee nguo za kubadilisha” Alvin aliamuru kwa jeuri nyuma yake.
“Siendi…” Kabla hajamaliza aliona tayari Alvin ameshavua shati lake huku akiudhihirisha mwili wake wenye nguvu.
Aligeuka na kumtazama kwa tabasamu baya. “Usipoenda, nitamtumia baba yako kipande hicho cha video—”
“Basi sawa, nitakwenda.” Lisa adabu ikamrudia, aliinamisha kichwa haraka na kutoka nje. Alipoelekea mlangoni, alitazama nyuma na kumwona Alvin akitupa suruali yake kando. Macho yake yalimuuma, akageukia kabati la nguo.
Baada ya kuchukua muda wake mtamu wa kumtafutia seti ya nguo za kulalia, alisogea tena bafuni na kumuona Alvin akiwa amejilaza ndani ya sinki la kuogea huku akiwa amefumba macho. Kope zake zilikuwa kama kipepeo aliyetulia, na kifua chake chenye misuli kilikuwa kimefunikwa na matone ya maji ya mpovu.
Lisa alikuwa akimshangaa huku moyo wake ukirukaruka kifuani mwake, na hakuona maji ya sabuni yaliyomwagika kutoka kwenye sinki la kuogea chini ya hatua zake mbele yake. Aliteleza, na kwa kwa bahati alikuwa karibu na sinki la kuogea, akaanguka ndani juu ya kifua cha Alvin.
Alvin alifumbua macho ghafla. Lisa aliyekuwa mikononi mwake alijitahidi sana kufurukuta ili anyanyuke, nguo zake, kuanzia tisheti suruali, na nywele zilikuwa zimelowa kabisa. Matone ya maji yaliteleza chini ya mashavu yake, na kumfanya aonekane mwenye kupendeza sana.
Macho ya Lisa yalimtoka, na uso wake ukawa na aibu huku akitoka nje kwa haraka. “Samahani, sikukusudia. nitaondoka mara moja.”
“Ninawezaje kuamini hivyo?” Alvin akamsogeza karibu na kifua chake na kumkumbatia kwa nyuma. Uso wake mzuri ulitulia begani mwake huku akihema sana. "Unataka kutumia ujanja kama huo kunifanya nikupe shamba hilo, huh?"
Kwa muda, Lisa alishangaa kwanini Alvin afikiria hivyo. “Hapana, mimi si…”
“Wewe mwanamke mwongo. Kumbuka, wewe ndiye uliyeyataka haya!” Alvin alisema na kumbusu kwa ukali.
Akiwa amekumbana na busu kali la mwanaume huyo, Lisa alijaribu kumsukuma lakini hakufanikiwa. Alijua ikiwa angeendelea hivyo, Je, angekabiliana vipi na Kelvin katika siku zijazo? Alimuuma kwa nguvu kwenye mdomo wake, akatoa damu. Alvin alifoka kwa maumivu.
Lisa alichukua nafasi hiyo kumsukuma. Uso wake ulikuwa umejaa udhaifu na unyonge. "Alvin, ukinilazimisha hivi, nitavunja kichwa changu kwenye sinki la kuogea!"
"Sawa, endelea!" Macho ya Alvin hayakuwa na huruma yoyote. "Nitapiga simu kwa Bwana Joel kesho na kumwambia kuwa binti yake alijaribu kunitongoza lakini alijiua kwa aibu kwa sababu nilimkataa."
Lisa akaguna tu kwa hasira, “mpuuzi wewe!” Macho yake yakawa mekundu kwa hasira. Kwanini matukio ya ajabu yalikuwa yanamlazimisha kuwa na mtu huyo? Kwa kweli hakutaka kuwa na uhusiano wowote naye, lakini kwanini dunia haikutaka kuwatenga? Kila alipojitahidi kumwacha lingetokea tukio ambalo lingemlazimu tu amrudie tena, kwanini iilikuwa hivyo? Kutokana na hasira kali, machozi yalimtoka.
"Alvin, nakuchukia!" Lisa alimfokea, akampiga begani bila kujizuia.
Alvin alishusha macho na kumtazama. Paji la uso wa Lisa lilikuwa limekunjamana kwa hasira, lakini hakuwa na namna. Alvin alikuwa amemzidi kwa kila kitu, nguvu, maarifa, ujanja, ilibidi tu amwangalie na kumwacha afanye anachotaka.
“Sawa, nyamaza!” Alvin aliendelea kumbusu. Baada ya zaidi ya dakika kumi, Lisa akatoka bafuni. Alvin alimtazama mgongoni akitoka huku pembe za mdomo wake zikiwa zimejikunja kwa kuridhika......ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.
