JINA LA SIMULIZI............................LISA

AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................143-144

Sura ya 143

“Unafikiri bado nitaamini maneno yako?” Alvin hakujisumbua kumtazama Lisa machoni.

Lisa aliinamisha macho yake kimya kimya. Kwa mtazamo wa mambo, ilionekana kuwa hakuna kitu ambacho angeweza kuelezea zaidi akaeleweka. Alichukua kalamu na kusaini karatasi. Moyo wake haujawahi kuwa mzito hivi alipokuwa akisaini 'Lisa Jones'.

"Nimemaliza. Naenda ghorofani kufunga vitu vyangu, nitaondoka mara baada ya hapo.” Aligeuka na kuelekea juu. Alvin hakuwa na mpango wa kugeuza kichwa chake. Lakini, mwishowe alitazama nyuma na kujikuta anamtazama licha ya yeye mwenyewe kutaka.
Alikuwa amevaa nguo za kulalia za waridi, na nywele zake zilianguka juu ya mabega yake kama maporomoko ya maji. Harufu kama ya mwerezi ilitanda mahali alipotoka.

Alvin alikunja ngumi. Kadri alivyozidi kukunja ngumi ndivyo alivyokuwa akikosa hewa kifuani. Hapo awali alifikiria alikuwa anamtisha tu na asingesaini karatasi. Bila kutarajia, alisaini bila kusita zaidi. Pengine hakungoja kukutana na Kelvin tena. Hah…
Alidhihaki kwa kejeli. Kwa kuwa alikuwa amepitia vikwazo vingi, hakika asingekufa kwa sababu tu ya kuondoka kwake.

Nusu saa baadaye, Lisa aliburuta masanduku yake chini. Kwa wakati huo, hakuna mtu aliyekuwa sebuleni, na kifungua kinywa kizuri alichotayarisha hapo awali kilikuwa kimeishia kwenye pipa la takataka. Alikunja midomo yake kwa huzuni, akajifuta machozi kwenye kona za macho yake, akaondoka.

Alipotazama jumba hilo likiwa mbali zaidi kupitia kioo cha nyuma cha gari, alinung'unika ndani kwa ndani, 'kwaheri, Alvin.' Alikuwa akipaona mahali hapo kama nyumba yake pekee na Alvin kama mwanafamilia wake pekee. Lakini sasa, hatimaye alikuwa peke yake tena.

Kwa kuwa hakuwa na pa kwenda kwa wakati huo, Lisa alielekea kwenye nyumba ya Pamela. Baada ya Lisa kubonyeza kengele ya mlango kwa muda, Pamela alifungua mlango. Nywele zake zilikuwa chafu na kulikuwa na harufu kali ya pombe juu yake.

“Kwa nini umekuja na masanduku yako?” Akiwa amechanganyikiwa na kustaajabu, Pamela alitazama masanduku mawili yaliyokuwa kando ya miguu ya Lisa.

“Nimepewa talaka, na nimefukuzwa nyumbani kwa Alvin. Kwa vile sijanunua nyumba, sina pa kukaa isipokuwa mahali pako.” Lisa akaburuta masanduku yake ndani ya nyumba. Alijilaza kwenye kochi kama kikaragosi asiye na roho.

"Nini?" Pamela alipandwa na hasira. "Ni kwa sababu ya picha? Kama mpenzi wako, asingewezaje kukuamini? Mimi naenda kumfanya alipe. Ameenda mbali sana…”

“Usiende kwake.” Lisa alimsimamisha Pamela. “Tayari anafahamu kuwa mwanzoni nilimwendea kwa sababu nilimdhania kuwa ni mjomba wa Ethan. Pia amegundua kuwa ulimdanganya kabla ya hili kwa ajili ya kunitoa jela.”

"Nini? Aliwezaje kujua?” Pamela alipigwa na butwaa.

"Sina uhakika. Ni mimi na wewe tu ndo tulikuwa tunajua kuhusu suala hili." Lisa alimtazama kwa sura ya kinyonge. “Sikumwambia chochote. Kwa kuzingatia harufu kali ya pombe juu yako, labda ulikunywa sana jana usiku. Una tabia ya kuzungumza upuuzi baada ya kulewa.”

“Usinituhumu…” Pamela alishikwa na wazo alipokuwa akizungumza. Alishika nywele zake. “Sasa nakumbuka. Nadhani Sam ndiye aliyenirudisha nyumbani jana usiku, na nilikuwa nimelewa sana wakati huo. Kulikuwa na mwanamume mwingine ndani ya gari, na alidai kuwa mpenzi wako."

Lisa alikosa la kusema. Alikuwa kishajua tangu aliposikia akinuka pombe. Bila shaka, Pamela alikuwa ameropoka bila kujijua. Pamela aligonga kichwa chake kwa nguvu. Alitamani angepasua kabisa ubongo wake.

“Samahani, Lisa.” Akiwa amehuzunika, Pamela alipiga magoti mara moja mbele ya Lisa. “Nimekuingiza kwenye matatizo tena. Sijui jinsi ninavyoweza kukusaidia wakati wa maisha yangu. Naona aibu sana kukukabili. Vipi kuhusu kukutolea ndugu yangu kama fidia ya kosa langu? Ninaahidi kwamba atakupenda kikweli na atabaki mwaminifu kwako.”

"Acha kuongea ujinga." Lisa alipunga mkono wake akimaanisha kuwa alikuwa amechoka sana asiweze kumkaripia. “Hata hivyo, bado ingekuwa vigumu kwetu kuendelea na uhusiano wetu hata kama hukusababisha tatizo. Kuna suala kuhusiana na Kelvin na... mpenzi wake wa zamani ambaye hawezi tu kumshau. Kila mara hutaja jina lake anapokuwa amelewa.”

"Nini? Kwa nini wanaume huwa na macho ya kupepesuka?” Pamela alisaga meno kwa kufikiria kile kilichomkuta yeye mwenyewe.

“Vipi, ulimpeleka Patrick pamoja na familia yako kula chakula cha jioni jana usiku, sivyo? Kwa nini uliishia kunywa pombe?” Lisa alianza kushangaa ghafla. “Inaweza kuwa hivyo… Patrick alikutosa tena?”

Pamela alisema kwa uchungu, “Linda alipata ajali, Patrick akaenda kumwangalia. Hakunipigia hata simu. Nimeachana naye moja kwa moja safari hii.”

“Jamani. Ni balaa gani hili?” Lisa alitukana kwa hasira. Ghafla, akahema. “Sawa. Ulinifanya niishie kuachwa, na wewe uko single sasa hivi pia. Ngoma droo. Nitakuchukulia tu kama kampani yangu. Hata Patrick akikuomba urudiane naye wakati huu, usikubali kukutana naye tena.”

“Ndiyo, bila shaka. Mimi ndiye niliyekuumiza. Maadamu haujaolewa, sitathubutu kuolewa. Ikiwa hutapata hata mwanamume mzuri wa kukuoa, tunaweza kushiriki katika uhusiano wa jinsia moja. Kwani wanawake wangapi wanasagana?”

“Potelea mbali. sina hamu na wewe.” Lisa, ambaye mwanzoni alikuwa amekasirika, hakujua kulia au kucheka wakati huo.

•••
Chini ya dakika 20 baada ya kuondoka, gari la Sam lilionekana kwenye jumba la Alvin. Alikimbia kwa kasi hadi ghorofani, akamkuta Alvin akiwa amesimama kwenye kibaraza huku macho yake yakiwa barabarani. Alikuwa ameshika sigara, na sinia ya majivu iliyokuwa kando yake ilikuwa imejaa virungu vya sigara.

"Alvin, kweli utarudi Nairobi?" Sam alisema kwa hisia, "Nitaku’miss sana, na itakuwa tofauti kutokuwa na wewe karibu."

"Utani’miss kama rafiki au utakosa kuwa nami kama chanzo cha mapato cha kampuni yako?" Alvin aliacha majivu ya sigara yadondoke bila kujali.

Kwa aibu, Sam alitoa kikohozi chepesi. "Angalia, ingawa umekuwa hapa kwa muda mfupi tu, umeipatia zaidi ya shilingi bilioni moja kampuni yangu ya sheria mwaka huu."

Alvin akaingiza mikono yake mfukoni. Macho yake meusi, mazito yalionyesha hali ya ujeuri.

Sam akahema. “Sawa. Kama ningelijua hili mapema, nisingekualika Dar es Salaam. Kwa hiyo unaondoka lini?”

“Kesho. Tafuta mtu wa kuuza nyumba hii." Baada ya kuongea kwa sauti ya kupuuza, Alvin aligeuka na kuingia ndani ya nyumba.
•••

Asubuhi iliyofuata. Kitu cha kwanza alichofanya Lisa baada ya kuinuka kitandani ni kumuandalia Alvin kifungua kinywa. Dakika akitoka chumbani, alipigwa na butwaa baada ya kuiona sebule hiyo asiyoifahamu. Alisahau kuwa Alvin alikuwa ameachana naye. Hakuhitaji kuamka mapema ili kumpikia tena. Isitoshe, kusingekuwa tena na mlinzi wa kumuangalia. Kwa kweli, alikuwa ameachwa kama jongoo na mti wake.

Kama mwenyekiti wa kampuni yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 500, alipaswa kuishi maisha kwa uhuru mkubwa zaidi. Alipaswa kufurahishwa na jambo hilo, lakini hakuweza kuhisi furaha hiyo hata kidogo. Baada ya kifungua kinywa, Lisa aliendesha gari hadi hospitali kumtembelea Kelvin. Hakuwa amemtembelea tangu siku alipopoteza fahamu.

Sura ya 144

Lisa alikuwa akijisikia hatia kwa jinsi alivyomtendea Kelvin.
Alisimama mbele ya wodi akiwa na maua na matunda. Wakati anakaribia kugonga mlango, mara akasikia mwanamke akilia kwa sauti ya chini ndani ya chumba hicho.

“Usilie mama.” Kelvin alimfariji mama yake.

“Siwezi kulia vipi? Wewe ndiye mwana pekee wa kiume katika familia ya Mushi. Nilitarajia uendeleze ukoo wa familia ya Mushi, lakini angalia nini kimetokea. Najiuliza ni nani aliyefichua suala hilo kuhusu figo yako? Wanawake wote ambao mwanzoni walitaka kuolewa na wewe sasa watakukwepa. Hakuna atakayetaka kuolewa wewe.”

Kelvin alijibu, “Haijalishi, Mama. Hata hivyo, sijisikii kuoa bado.”

“Mimi ndiye niliyekuzaa. Unafikiri nitajisikiaje? Huwezi kuacha kumfikiria Lisa? Hata ulihatarisha maisha yako kwa sababu yake.”
Akiwa ameshikilia kikapu cha matunda kwa nguvu, Lisa alisikiliza kile ambacho Mama Mushi alisema mwishoni. “Hata hajali kuhusu wewe. Umelazwa hospitalini kwa siku nyingi, lakini hajakutembelea hata kidogo.”

“Inatosha mama. Ni chaguo langu. Kumpenda mtu haimaanishi kuwa lazima uwe naye. Kumlinda na kumwangalia akiishi kwa furaha ni zaidi ya kutosha.” Kelvin alieleza.

Lisa alihisi uvimbe kwenye koo lake. Kuna kitu kilionekana kukwama kwenye koo lake, jambo ambalo lilimfanya akose raha. Kamwe hakutarajia kwamba Kelvin angempenda sana.

“Mbona umesimama hapa?” Mzee Mushi alikoroma kwa hasira nyuma ya Lisa nje ya wodi.

Lisa alishtuka, na wale waliokuwa chumbani wakamtazama.
Kwa hayo, aliingia chumbani kwa kusitasita. Kelvin aliguswa kuwa huenda Lisa alikuwa amesikia alichokisema. Kwa hiyo, uso wake mzuri ulianza kuona haya usoni. “Lisa, kwa nini umenitembelea leo, Alvin hatachukia?”

“Nimefika hivi punde. Mimi na yeye tayari tumeshaachana.” Lisa aliinua kichwa na kumtazama. Alionekana kuwa mwembamba sana ndani ya siku chache tu. Gauni alilovaa lilionekana kumlegea huku uso wake wa kifahari na mrembo ukionyesha kama mgonjwa anayesumbuliwa na utapiamlo.

"Mbona mmeachana ghafla?" Kelvin alipigwa na butwaa. "Ilikuwa kwa sababu yangu?"

"Hapana. Kuna matatizo mengi sana kati yetu.” Lisa alibadilisha mada. “Unaendeleaje sasa?”

"Anaendelea vizuri?" Mama Mushi aliinuka akiwa na uso mchangamfu. “Alipoteza figo, sasa figo moja si sehemu ya nyama yake tena. Hawezi hata kurejesha kimetaboliki chake bado. Kwa kuwa mikono yake inakabiliwa na uharibifu wa neva, anahitaji kupitia miezi michache zaidi ya matibabu. Mbaya zaidi, maisha yake ya baadaye yataathiriwa. Daktari alisema kuwa hatakiwi kufanya kazi ama mazoezi magumu, na anapaswa kuwa mwangalifu katika lishe yake. Vinginevyo, atapoteza maisha yake. Kwa kuzingatia kwamba kwa kawaida anahitaji kusimamia kampuni kubwa kama hiyo, nadhani hawezi kuishi maisha marefu.”

Mzee Mushi alimkemea, “Unaongea upuuzi gani? Zingatia maneno yako."

“Nimekosea? Tayari tuko katika miaka ya mwisho ya uzee wetu, kwa sababu tulikuwa na mtoto wetu mmoja tu wa kiume, pengine tunapaswa kumtunza milele.” Mama Mushi alijifuta machozi usoni mwake. “Unafikiri kuna mwanamke yeyote kutoka katika familia yenye heshima ambaye yuko tayari kuolewa naye? Maskini mwanangu, nina wasiwasi na maisha yako ya baadaye.”

Akiwa ameshikwa na hatia, Lisa alihuzunika sana. Alikuwa mwishoni kabisa mwa akili zake.

“Acha, Mama.” Kelvin alimsimamisha katikati ya maumivu ya kichwa chake.

“Nimekosea? Ulijeruhiwa kwa sababu yake. Alikutunza hata siku moja? Ingekuwa afadhali ungeokoa mtu usiyemjua kuliko yeye,” Mama Mushi aliongeza kwa uchungu, “Kwa maoni yangu, yeye ndiye anapaswa kuwa mwangalizi wako milele ili akusaidie. Hata hivyo, huwezi kupata mke kwa sasa, basi yeye awe fidia yake.”

“Mama…” Kelvin alishindwa kujizuia, na uso wake mzuri ukageuka kuwa wa kustaajabisha ghafla. Maumivu yalikuwa makali sana hadi akatoka jasho la baridi. Wakati huo huo, shinikizo lake la damu lilionekana kupanda juu ya kiwango.

Kila mtu aliingiwa na hofu na kumpigia simu daktari haraka.
Daktari alifika haraka na kuwakemea, “Mgonjwa amefanyiwa upasuaji mkubwa, badala ya kumfariji, mnampandisha presha. Mnataka afe?”

Kila mtu alinyamaza mara moja. Hata Mama Mushi alifunga mdomo kwa aibu. Kelvin alichoka sana hata akapitiwa na usingizi muda si mrefu.

Tena, Mama Mushi alimtazama Lisa kwa hasira. Lisa aliinamisha macho kwa hofu. “Acha kulalamika mama. Nitalipa fadhila kwake. Kuanzia leo na kuendelea, nitamtunza. Hata baada ya kupona, nitashughulikia lishe na maisha yake hadi apate mke.”

"Lakini vipi ikiwa hawezi kupata mke?"

"Hilo halitawezekana." Lisa alimtoa wasiwasi.

Mama Mushi alidhihaki. “Nani yuko tayari kuolewa na mwanaume aliyekosa kiungo? Ikiwa kuna matatizo na figo nyingine, labda atakufa kwanza. Isitoshe, sidhani kama kuna mtu mwingine yeyote ulimwenguni angekuwa tayari kuhatarisha maisha yake ili kukuokoa.”

Lisa alikaa kimya kwa muda wa nusu dakika kisha akaongea taratibu kwa sauti ya ukali, “Sawa. Ninaahidi atanioa.”

•••
Katika mgahawa, Pamela alipopata habari hizo, karibu amwage kahawa. “Umerukwa na akili? Unapanga kurudisha fadhila kwa kutoa maisha yako, huh?"

"Sina la kufanya tena." Lisa aliinywa kahawa iliyokuwa na ladha chungu sana. "Zaidi ya hayo, picha yetu imesambazwa kila mahali. Kila mtu ana hisia kwamba tuna uhusiano wa karibu. Hata hivyo ni sawa tu, alitoa figo yake moja kwa sababu ya kuniokoa…”

Pamela alishtuka baada ya kusikia hivyo. “Kelvin anakupenda sana. Siku zote amekuwa akikulinda kwa siri, lakini wewe na
Alvin…”

"Hatutarudiana kamwe." Lisa alionyesha sura ya uchungu. Hakumwambia Pamela kwamba Alvin alikuwa mtoto wa familia ya Kimaro. Lisa na Alvin walitenganishwa na bahari, na wote wawili walikuwa katika ulimwengu tofauti. Kwa kuongezea, mawazo yao yalikuwa tofauti kabisa.

“Sawa basi. Kwa kweli, wakati mwingine ni bora kwa mwanamke kutafuta mwanaume anayempenda zaidi kuliko yeye. Kwa njia hii, mwanamke hatahisi kuchoka.” Akikumbushwa kuhusu uzoefu wake wa mapenzi, Pamela aliugua. "Kwa upande wangu ninapanga kufanya kazi huko Nairobi mara tu baada ya mwaka mpya."

Lisa aliinua kichwa chake kwa mshangao. "Kwanini unaenda huko ghafla?"

“Si ghafla. Mwaka jana, kampuni ya Osher kutoka Kenya lilinipa nafasi ya mkemia mkuu wa vipodozi. Sikuweza kuvumilia kuachana na Patrick, kwa hiyo nilikataa kazi hiyo. Kampuni hiyo ilinipa kazi hiyo tena mwezi uliopita, na niliikubali jana.”

Pamela alitazama nje ya dirisha kwa huzuni. "Nimekuwa nikifikiria juu ya Patrick katika wakati wangu wote nikiwa hapa Dar. Natamani kuona ulimwengu mpya, na ninaamini nitasahau kuhusu uhusiano huo polepole baada ya muda."

"Inaonekana kama wazo zuri." Ghafla, hali hiyo iliacha pengo kwa Lisa kwani rafiki yake wa pekee naye angemuacha. "Ninaweza kuelekea Nairobi pia na kukuza biashara ya Mawenzi Investments huko mwaka ujao. Kuhusu kifo cha mama yangu… nataka kuja kuchunguza pia.”

“Uko sahihi. Baba yako anatoka Nairobi pia. Nitakusubiri uje.”

Usiku, Lisa alipakua masanduku yake. Alipofungua moja, ghafla akakuta Mkufu wa Malkia ndani yake. Wakati anahama kwa Alvin alikuwa amepakia vitu vyake haraka na kusahau kuviangalia kwa uangalifu. Kwa kushangaza, alikuwa amebeba na Mkufu pamoja. Kwa kuzingatia kwamba kitu hicho kilikuwa cha gharama kubwa, asingeweza kubaki nacho.

Siku iliyofuata, aliendesha gari hadi kwa Alvin tena. Alitumia muda mwingi akibonyeza kengele ya mlango, lakini hakuna aliyefungua mlango.

“Huna haja ya kuibonyeza tena. Mmiliki ameondoka Dar es Salaam.” Mwanaume aliyevalia suti nyeusi akatokea nyuma yake.

"Wewe ni…" Lisa aliuliza.

“Mimi ni dalali wa nyumba. Nilikuja kuchukua picha chache za jumba hilo ili kuisambaza kwa wateja na kuiuza,” mwanamume huyo alitabasamu na kusema, “Mmiliki alisema anataka kuiuza kwa bei nafuu. Kwa kuzingatia eneo na muundo wake, ninaamini itauzika hivi karibuni......ITAENDELEA.....

Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.