JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP.........................0628924768
SEHEMU YA...............................136, 137
Sura ya 136
Alvin alikaa kwenye siti ya nyuma ya gari lake. Alikuwa ametawaliwa na maamuzi ya hasira mapema asubuhi, lakini sasa ghafla alihisi njaa sana. Tumbo lilianza kumuuma tena. Aliwasha sigara kwa hasira. Ikiwa angejua kwamba hilo lingetokea, angemaliza kula kifungua kinywa chake kwanza kabla ya kupandisha hasira zake za kijinga.
"Bwana Kimaro, ngoja nikununulie chakula." Hans alimtazama kwa wasiwasi.
“Sina njaa. Nenda uniletee Lina Jones hapa,” Alvin alisema kwa upole, “Sikuzote nilitaka Lisa ashughulike naye, lakini haina maana sana. Nitamalizana naye mwenyewe.”
Hans aliitikia kwa kichwa. Ilionekana kana kwamba ingemlazimu kumuombea Lina kwa kile ambacho alihisi kilikuwa kinaenda kumkuta.
•••
Katika kampuni ya Mawenzi Investments. Lina alifukuzwa moja kwa moja na walinzi. Hakutaka kuondoka na kuishia kupiga kelele mlangoni, “Hata kama baba yangu alikamatwa, bado ana hisa kwenye kampuni na mimi bado ni mtoto wake. Nina haki ya kurithi hisa zake na kufurahia gawio langu.”
“Potelea mbali!” Yule mlinzi alimtemea mate isivyostahili. “Kila mtu anajua kuwa wazazi wako walimuua bibi mzee ili wapate hisa za Mawenzi Investments. Walimuua Mzee Madam Masawe. Hawana utu kabisa. Mwenyekiti Jones tayari ameomba mawakili wengi kurejesha hisa za Jones Masawe. Utarithi nini? Endelea kuota!"
"Subiri. Nitakaporudi Mawenzi, nitafanya maisha yako kuwa mabaya zaidi kuliko kifo. Lina alitetemeka kwa hasira.
Hata mlinzi alithubutu kumdhalilisha sasa. Kweli dunia haikuwa ya haki. Ni wazi alikuwa ametuma picha zote za uchafu za Lisa na Kelvin kwa waandishi wa habari jana yake, lakini sio tu kwamba ilishindwa kuharibu sifa ya Lisa, bali watu walianza hata kumuoanisha na Kelvin sasa. Ilikuwa inakasirisha sana na kukatisha tamaa.
Alitembea kando ya barabara wakati gari lisilo na nambari ya leseni lilisimama ghafla mbele yake. Kisha, watu wawili wakamsukuma moja kwa moja kwenye gari.
"Unafanya nini?" Kabla Lina hajajibu, alifunikwa kwenye gunia na kupoteza fahamu. Muda si muda, ndoo ya maji baridi ilimwagiwa juu yake na akapiga kelele kutokana na baridi. Gunia lilipasuliwa.
"Baridi ilikuwa nzuri?" Hans alimtazama kutoka juu.
Lina alitazama juu na kufikiria kuwa anaonekana kuwa mzoefu kidogo. Baada ya muda, alimkumbuka. "Ni wewe. Wewe ni msaidizi wa Alvin Kimaro…”
"Ni vizuri kukumbuka." Hans aliachia tabasamu hafifu. Akageuka pembeni, akamfunua mtu aliyekaa kwenye sofa ambalo halikuwa mbali. Mwanaume huyo alivalia suti nyeusi na kushika sigara mkononi, moshi ukitanda hewani. Macho yake ya wino yaliangaza na mwanga mweusi uliokuwa mkali kama kisu. Mwanamume huyo alitoa sauti ya kutisha.
Lina alimtambua. Hofu isiyoelezeka ikapanda kutoka ndani ya moyo wake. "Bwana. Kimaro, unajishughulisha na kazi ya kisheria. Unataka kunyang'anywa leseni yako kwa kuvunja sheria? Ninakuonya, afadhali uniache mara moja, la sivyo sitakuacha kamwe.”
Hans alicheka kana kwamba amesikia mzaha.
“Unacheka nini? Huwezi kuelewa nilichosema?” Lina alicheka. “Hebu niambie, haufahamu kuwa mimi ni mwanamke wa Willie Kimaro? Unajua Bwana Kimaro ni nani? Unajua kuwa ananipenda sana? Ikiwa huniamini, unaweza kuchukua simu yangu na kuangalia picha zetu pamoja.”
Alvin alimaliza kuvuta sigara na kuitupa kwenye sinia ya majivu kabla ya kuinuka. Mwili wake mrefu ulitembea polepole kuelekea kwake. Lina alifikiri anaogopa na akacheka. “Alvin Kimaro, wewe ni mwanasheria tu. Willie Kimaro si mtu ambaye mtu kama wewe unaweza kudiriki kumuudhi—”
Kabla hajamaliza, Hans alimpiga kofi kwenye shavu na kumng'oa jino mdomoni. Lina alipiga mayowe, “Willie hatakusamehe—”
Smack! Kofi jingine likasikika. Baada ya makofi kadhaa, Lina alipoteza meno machache na hakuthubutu kuongea tena.
"Nyamaza." Hans alitabasamu. “Unafikiri Willie Kimaro ni nani? Hujaelewa kwa nini Willie alibadili mtazamo wake kwako haraka hivyo?”
Lina aliganda. Alimtazama Alvin na ghafla akakumbuka kuwa jina lake la mwisho lilikuwa Kimaro pia. “Hilo haliwezi kuwa. Sijawahi kusikia mtu anaitwa Alvin katika familia ya Kimaro."
“Unawajua watu wangapi katika familia ya Kimaro?" Hans alidhihaki. “Acha nikwambie, Alvin Kimaro ndiye kaka mkubwa katika familia ya Kimaro. Amekuwa akisimamia familia tangu akiwa na umri wa miaka 20.”
Ubongo wa Lina ulivuma kana kwamba anaota. Kila mtu alijua kwamba kaka mkubwa, wa ajabu wa familia ya Kimaro alikuwa mtoto wa Leah Kimaro. Mtu huyo alikuwa mtu wa chinichini sana, lakini mbinu zake za ukatili zilijulikana sana. Aliingia katika kampuni hiyo akiwa na umri wa miaka 20. Mjomba wake wa pili alipokaidi, alimvunja mguu wake mbele ya umati.
Baada ya kuchukua jukumu la kuongoza KIM International, alipanua biashara yake hadi ng'ambo kwa kasi ya radi na hata akaingia katika nyanja za mawasiliano, fedha, na teknolojia kwenye masoko ya nje ya nchi kwa haraka haraka. Kwa wakati huo, alikuwa ameingia kwenye orodha ya watu miamoja tajiri zaidi Afrika, akiachwa kwa karibu sana na kina Dangote, Mo Dewji, Bhakresa na wengineo. Kulingana na uvumi, alikuwa mtu wa tatu tajiri zaidi nchini Tanzania na pia wa kushangaza zaidi.
"Hiyo haiwezekani. Unasema uwongo!” Lina alikuwa akiingiwa na wivu. Lisa alimkamataje mtu kama huyo?
“Kwa nini nikudanganye? Huyo mjinga Willie Kimaro aliogopa sana hivi kwamba alikojoa kwenye suruali yake alipomwona Bwana Kimaro. Hans alifoka. “Lina Jones, Bwana Kimaro hakutaka kushughulika na wewe mara ya kwanza, lakini hukupaswa kumpa Lisa Jones dawa ya kulevya. Na kwa kweli hukupaswa kutoa picha hizo kwenye vyombo vya habari.”
Lina alishtuka. Alipiga magoti mbele ya Alvin na kutetemeka. “Bwana Kimaro, mimi ni mjinga. Nilikuwa mjinga. Tafadhali nisamehe sana.”
Alvin akampiga teke kwa kuchukia. Ujeuri wa macho yake ulidhihirisha kwamba hakutaka chochote zaidi ya kumwangamiza kabisa. “Unadhani nitakuacha ukipumua?”
"Hapana, hapana, hapana. Haikuwa mimi. Sikupiga picha.” Lina akatikisa kichwa kwa hofu. “Nilitumiwa na mtu nisiyemjua. Ni kweli nilimpa Lisa dawa usiku huo, lakini Kelvin Mushi alipokuja, kamera ya video iliyokuwa chumbani iliharibiwa.”
“Hukuwa wewe?” Uso wa Alvin ulikaza zaidi huku alama ya mshangao ikimulika machoni mwake, akiamini hadaa ya Lina.
"Naapa." Lina alikuwa amepoteza meno kadhaa na mdomo wake ulikuwa umejaa damu. “Kama ningekuwa na hizo picha ningezitumia kumtishia Lisa zamani. Ningewezaje kumruhusu kukaa katika nafasi ya mwenyekiti kwa muda mrefu hivyo na kuwaweka wazazi wangu jela?”
“Kiapo chako hakina thamani.” Uso wa Alvin ulizidi kutisha, lakini aliamini maneno ya Lina. Ikiwa hakuwa yeye, basi ni nani?
Alikuwa na wazo, na midomo yake ikachanua katika tabasamu. Usiku huo, mbali na Lisa, ilionekana kana kwamba kulikuwa na Kelvin pekee. Kwa Kelvin Mushi haikuwa rahisi hata kidogo kwa Lisa kumshuku. Lisa alijua kwamba anampenda, lakini bado alikuwa tayari kuendelea kuwa na urafiki naye. Kelvin alikuwa ameenda ng’ambo kufungua ofisi ya tawi alipokuwa kijana, kama yeye tu. Anawajua watu wenye uthubutu wa kuvuka mipaka na kwenda kufanikiwa nje ya nchi huwa wajanja wajanja sana. Alvin hakumwamini Kelvin hata kidogo.
Lina alijua kwamba alimwamini na akasema kwa haraka, “Bwana Kimaro, tafadhali niruhusu niende. Ninaahidi sitomsumbua Lisa tena. Nitaondoka Dar es Salaam.”
“Unadhani nitakuacha uondoke kwa amani?” Alvin alitabasamu kwa giza. “Nimechunguza mambo yako. Ulikulia kijijini baada ya kuibiwa ukiwa mtoto mdogo, ukatolewa usichana wako na mwanakijiji ukiwa na umri wa miaka 15. Baadaye katika shule ya sekondari, ulifumaniwa zaidi ya mara kumi na waume za watu. Uliwekwa kinyumba na tajiri mmoja na hata kutoa mimba zisizo na idadi. Ni aibu iliyoje. Hukuwa na maisha mazuri hata baada ya kurudi kwenye familia ya akina Masawe.”
Uso wa Lina ulikuwa umepauka kwa aibu. Hii ilikuwa historia yake ya giza. Alikuwa ameifunika kwa makini sana, lakini mtu huyu kwa kushangaza aliweza kujua juu yake. Alikuwa anatisha sana.
"Kwa kuwa unapenda wanaume sana, nitakuozesha mume wa kuishi naye." Alvin alisema na kuondoka bila kuangalia nyuma.
Punde, mzee mfupi na mbaya mwenye umri wa miaka 50 aliingia. Alipomwona Lina, alimeza mate ya uchu. "Bwana Kimaro, unaniruhusu nimuoe?"
Lina alimtazama Hans kwa uso wa kutisha. “Usimruhusu anioe. Nitakwenda na wewe. Unaweza kufanya chochote unachotaka. Unaweza kunifanya vile Willie alinifanya pia!”
Hans alikwepa nyuma kwa kuchukizwa. “Usinishike, nachukia mambo machafu. Usimwogope sana. Anaonekana kuwa mzee, lakini ana umri wa miaka 40 tu na amekuwa peke yake kwa miaka kadhaa kwa sababu hakuweza kupata mke. Utamfuata kijijini na kumpatia mtoto.”
Kisha, Hans akaondoka, akimuacha Lina nyuma. Alilia kwa kukata tamaa, lakini hakuna mtu aliyemjali. Wakati huo, alijuta sana. Hakupaswa kumlazimisha Lisa Jones kuondoka nyumbani wakati huo. Hakupaswa kumsukuma Bibi Madam Masawe chini ya ngazi.
Lakini, hakuna na dawa ya majuto katika ulimwengu huu.
Sura ya 137
Katika mlango wa kituo cha polisi, Lisa alikuwa amemaliza tu kurekodi ushahidi wake mara ghafla akasikia mtu akiliita jina lake.
“Lisa.” Aligeuka nyuma na kumuona Kelvin akija kwake huku akiwa na tabasamu usoni mwake. Hali ya hewa ilikuwa ya baridi, na alikuwa amejifunika kitambaa shingoni.
"Ni bahati tu nimekuona. Kwa nini upo hapa?” Lisa alilazimisha tabasamu kumsalimia. Kila alipokuwa akimuona, alizikumbuka picha zile na mgogoro kati ya Alvin na yeye.
"Kuna jamaa wa nyumbani alifanya tukio la ajabu, kwa hivyo nilikuja kumdhamini." Kelvin alionekana hoi. "Nilisikia kwamba Jones Masawe na Mama Masawe walikamatwa hivi majuzi. Je wewe…”
“Ndio, polisi waliniita hapa kuchukua maelezo yangu. Kesi hiyo itafikishwa mahakama wiki ijayo kisha watasomewa hukumu.”
"Hongera, hatimaye umelipiza kisasi kwa bibi yako." Kelvin alifurahi kusikia hivyo.
“Asante.” Tabasamu la Lisa halikumfikia machoni. Alionekana kuchoka kabisa.
Kelvin alitembea pamoja naye kuelekea sehemu ya maegesho, huku akimtazama njiani. “Unaonekana umechoka. Umekuwa ukipumzika vizuri kweli? Na Alvin bado hajakuelewa tu…?!”
"Hatuwezi kuzungumza juu ya hili?" Lisa alimkatisha.
"Ni kosa langu." Kelvin alionekana kuwa na hatia.
“Kosa lako kivipi? Ulinisaidia usiku ule. Kama si wewe, ningefanyiwa ukatili mbaya na pengine ningeweza kujiua muda mrefu uliopita. Jana, hata ulishirikiana nami kufafanua hali ilivyokuwa na kuokoa sifa yangu. Ninapaswa kukushukuru,” Lisa alitikisa kichwa na kusema kweli.
Wawili hao walizungumza huku wakitembea. Lakini kijana mmoja aliibuka kando yao ghafla na hawakumjali, wakidhani ni mpita njia tu. Hata hivyo, ghafla mwanamume huyo alitoa kisu cha matunda kutoka kwenye mfuko wake wa suruali na kukichoma kuelekea kifuani kwa Lisa.
“Lisaaa!” Kelvin aliona Lisa amechelewa sana. Alipoona kile kisu kinataka kumchoma, alinyoosha mkono haraka kukizuia, na kisu hicho kikapenya kwenye mkono wake.
Wakati Lisa anajibu, mtu huyo alikuwa amechomoa kisu haraka ili kumchoma Lisa tena. Kelvin angeweza tu kutumia mwili wake kumkinga, na kisu kikapenya sehemu ndogo ya mgongo wake.
“Msaada!” Lisa alilia. Kwa msukumo aliushika mkono wa mwanaume huyo. "Wewe ni nani?!”
“Hutakiwi kunifahamu. Ni kosa lako kuwa mwanamke wa Alvin Kimaro. Nimekuwa nikikufuatilia kwa muda mrefu sasa.” Mwanaume huyo alifichua uso wake wa kutisha huku akiendelea kudunga kisu kwenye mwili wa Kelvin kana kwamba alikuwa na wazimu.
Kwa bahati nzuri, walikuwa karibu na kituo cha polisi. Polisi mmoja alisikia kilio cha kuomba msaada na haraka akakimbia ili kumshika mhalifu.
Punde, ambulensi ilifika na upesi ikampeleka Kelvin hospitalini. Hata hivyo, tayari alikuwa amepoteza damu nyingi njiani na kupoteza fahamu. Lisa alipiga simu kwa haraka kwa Ethan, ambaye alikimbia mara baada ya Ambulance kufika hospitali.
Mlango wa Emeregence Room ulisukumwa, na daktari akatoka na fomu mkononi. “Kisu kilichomwa kwenye figo ya kushoto ya mgonjwa na inabidi itolewe mara moja ili kuokoa maisha yake. Familia ya mgonjwa iko wapi? Tafadhali saini mara moja.”
Lisa alipigwa na butwaa. Ethan pia aliona ni vigumu kukubali. "Daktari, lazima ni lazima figo iondolewe? Kwani hakuna namna nyingine?"
"Necrosis tayari imeingia kwenye figo ya kushoto, kwa hivyo haina maana sasa," daktari alisema bila msaada, "Kama tungeweza kuiokoa, bila shaka tungeiokoa."
Ethan hakuwa na la kufanya zaidi ya kuvumilia maumivu na kusaini zile karatasi. Lisa alitoa machozi ya uchungu. “Yote ni makosa yangu. Mtu huyo alitaka kuniua. Mjomba wako ndiye aliyetumia mwili wake kunisaidia kuzuia kisu."
Ethan alikuwa na hisia tofauti. Hakutarajia Kelvin angekuwa na hisia za kina namna hiyo kwake. Sasa, pia alikuwa na wasiwasi sana kuhusu usalama wa Kelvin. Angeweza tu kusema, “Usifikirie juu yake. Daktari alisema kuwa kuondoa figo yake kutaokoa maisha yake. Mwili wa mwanadamu bado unaweza kufanya kazi na figo moja tu. Anapaswa kuwa mwangalifu zaidi katika siku zijazo."
Lisa alitabasamu kwa uchungu. Kelvin alikuwa anaenda kupoteza figo. Angewezaje kuwa mzima kama hapo awali? "Umewajulisha babu yako?"
“Hapana, babu na bibi wamezeeka na sitaki kuwapandisha presha. Tusubiri hadi upasuaji wa Mjomba umalizike.” Ethan alimtazama na kuhema moyoni mwake. Aliogopa hasa kwamba babu na bibi yake wangezimia ikiwa wangejua ukweli.
Kwa bahati nzuri, saa tatu baadaye, Kelvin aliokolewa. Operesheni ilikuwa imekwisha, lakini bado hakuweza kufumbua macho.
Muda si muda, polisi walifika hospitalini. Walipomwona Lisa walimwambia. “Bi. Jones, tumemhoji mhalifu. Mtu aliyetaka kukuua anaitwa Zigi Kabwe. Yeye si mwenyeji wa hapa Dar.”
Lisa alikasirika. “Hata simfahamu mtu huyu.”
Afisa huyo alitikisa kichwa. “Kulingana na maelezo yake, alikuwa na dada yake pacha anayeitwa Lily Kabwe. Miaka mitano iliyopita, Lily Kabwe alikuwa na umri wa miaka 17 tu, lakini alivutia macho ya Thomas Njau kutoka kwa familia ya Njau huko Nairobi. Thomas alimbaka Lily kwa nguvu baada ya kukataa kulala naye na akaamua kujirusha hadi kufa kutoka kwenye jengo kutokana na fedheha. Familia ya Kabwe ilimshtaki Thomas. Wakati huo, kulikuwa na karibu ushahidi kamili, lakini familia ya Njau ilimwajiri Alvin Kimaro kutetea kesi yao. Alvin Kimaro alidai kuwa Lily alimtongoza Thomas lakini Thomas alimdharau, hivyo akaamua kujiua kwa sababu ya unyonge wake. Mahakama haikushindwa tu kumwadhibu Thomas, lakini hata ilimfanya Lily aonekane kama mtu duni asiye na maana. Mama yake hakuweza kuvumilia na na akapata presha. Amefariki hivi karibuni…”
Lisa alishtuka. Alijua tu kwamba Alvin hawezi kushindwa mahakamani, lakini hakujua kwamba alikuwa amechukua kesi nyingi zisizo na moyo wa utu. "Kwa hivyo, alitaka kuniua ili kulipiza kisasi kwa Alvin Kimaro?"
“Ndiyo. Alitoweka miaka mitano iliyopita baada ya kesi hiyo, na tuligundua tu kwamba alirudi Dar es salaam mwaka huu. Alitaka Alvin Kimaro ajue uchungu wa kufiwa na mpendwa wake, lakini… Alvin Kimaro amezungukwa na walinzi na ni mwangalifu sana, kwa hivyo Zigi Kabwe ameshindwa kutimiza lengo lake licha ya kujaribu kwa miaka kadhaa.”
Afisa huyo alimwambia, “Amekuwa akikufuata kwa muda, lakini umekuwa ukilindwa na mlinzi siku hizi za karibuni. Ni leo tu ndipo alipata nafasi hiyo kwa sababu hukuwa na mlinzi.”
Ghafla, Lisa alionekana kugundua kitu. Siku chache zilizopita, Alvin alikuwa amepanga ghafla Shani afuatane naye kama mlinzi wake. Haikuwa kumlinda dhidi ya Jones na binti yake bali kumtazama Zigi Kabwe. Hata hivyo, hakumwambia chochote.
Haukuwa ulinzi wake hata kidogo. Kama Kelvin asingetokea siku hiyo, angekufa. Hofu isiyo na kipimo ikaufunika moyo wake. Lisa ghafla alifikiri kwamba hakumfahamu kabisa Alvin kama alivyodhani.
"Kwa nini kulipiza kisasi kwako kwa kile Alvin Kimaro alichofanya kwa mtu mwingine?" Ethan alikasirika. “Lisa, nakushauri ukae mbali na Alvin Kimaro. Nani anajua ni maadui wangapi amewachokoza kwa miaka mingi? Nilisikia huwa anaenda mahakamani kuwatetea matajiri tu, madhalimu na mafisadi, je ni haki za wangapi amedhulumu? Lazima atakuwa amepata pesa nyingi kwa njia isiyo halali."
Lisa alinyamaza, akiinamisha kichwa chini na uso wa huzuni. Moyo wa Ethan uliumia. Ikiwa asingefanya chaguo baya hapo kwanza, Lisa asingeangukia kwa Alvin....ITAENDELEA.......
Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo ni moto mambo ni fire, lakini sina cha kusema nikuombe tuungane pamoja katika sehemu inayofuata ya mkasa huu wa kusisimua unaokwenda kwa jina la LISA.
