JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................810-811
Sura ya: 810
Katika hospitali.
Lisa pia alikuwa akifikiria juu ya jambo linalomhusu Matthew. Alikuwa na wasiwasi kidogo. Hakujisikia raha, akampigia Sam Harrison simu. Hapo ndipo alipogundua kwamba Matthew alikuwa ametoweka huko Dar es Salaam na kwamba msaidizi wake alikuwa amekufa pia.
“Lisa, huyu Matthew ana uhusiano gani nawe?” Sam alidadisi sana.
"Yeye ni kaka yangu kutoka kwa baba tofauti." Lisa akahema. “Ninashuku ni Kelvin aliyefanya. Je, ushawishi wa familia ya Mushi huko Dar uko vipi?"
"Unazungumzia familia ya Mushi?" Sam alishtuka. Alikuwa amekasirika kidogo. “Hapo awali, sisi, familia ya Harrison, tulionwa kuwa familia ya kishua kuliko zote huku Dar. Hata hivyo, ni nani angeweza kufikiri kwamba Golden Corporation ingekuwa kwenye orodha? Sasa, zaidi ya asilimia ya watu walio mamlakani hapa Bongo wanamuunga mkono Kelvin, na hata anataka kuishinda familia ya Harrison. Hata hivyo, sina hamu na huyo jamaa. Familia ya Mushi imekuwa ikituzingua sana. Kama si kwa…”
“Kama sivyo?” Lisa aliuliza kwa haraka.
Sam alisema kwa huzuni, "Kama isingekuwa kwa ushirikiano wetu na Forrest, familia ya Harrison ingeshindwa kukaa Dar. Wakati fulani uliopita, nilikuwa nikifikiria kuja Nairobi pia ili kukuza kampuni yangu. Hata hivyo niliachana na wazo hilo nilipoona hali ya Alvin. Sikutaka kuwapa nyinyi shida zaidi.”
“Kwanini hukutuambia kuhusu hili?” Lisa alikasirishwa kwamba hakujua kama Kelvin amekuwa kibopa huko Dar es Salaam. La sivyo, angemkumbusha Matthew kuwa mwangalifu.
Matthew lazima hakutarajia pia. Alikwenda Dar es Salaam kwa tahadhari, ili tu habari zifikie masikio ya Kelvin.
"Wewe na Alvin mmekuwa mkikabiliwa na matatizo mengi, kwa hiyo sikutaka kuwasumbua nyie." Sam alisema kwa kuudhika, “Huyu jamaa, Kelvin, ni kama mende ambaye hatakufa. Anaudhi sana. Nyie lazima muwe makini."
Lisa alitabasamu kwa uchungu. Hakumwambia Sam kuwa Alvin amekuwa chizi.
Wakati huo nesi aliita kwa nyuma. "Familia ya Alvin, tafadhali njoo haraka ...."
“Nitazungumza nawe tena wakati ujao.” Lisa alikimbia kurudi wodini, ambapo alimuona Alvin akilia kwa sauti. “Sitaki kuchomwa sindano. sitaki sindano...”
Muuguzi alitazama jinsi mwanamume mzuri akilia kwa machozi na kwikwi. “Bi Jones, inabidi umshawishi. Ikiwa hatatumia IV, majeraha yake yatapungua."
“Sawa, nitamshawishi sasa hivi.” Lisa hakujali kwamba kulikuwa na watu mahali hapo. Kwa haraka alimkumbatia Alvin na kumbembeleza kwa upole,
“Alvlisa, usipochomwa sindano, utaumwa na kichwa na homa. Hilo likitokea, itabidi ukae hospitalini kwa muda mrefu na upate sindano kila siku. Je, uko tayari kufanya hivyo?”
“Lakini... sindano ni chungu. ” Alvin alifoka huku akihema.
“Kwa nini tusifanye hivi? Mradi tu uwe mvulana mzuri na uchome sindano zako, nitakupa peremende, sawa?" Lisa hakuwa na la kufanya zaidi ya kutumia turufu yake. Hata hivyo, alikuwa mwanamume ambaye alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 3o, hivyo ilikuwa sawa kula pipi zaidi, zisingemdhuru kama mtoto.
Baada ya mawazo kidogo, Alvin aliongeza kwa sauti ya kwikwi. "...Nataka kutazama katuni pia."
“Sawa.” Kwa kuwa Alvin alikuwa mkubwa, angeweza kumruhusu atazame katuni tani yake hata kama angegeuka kipofu. Lisa hakuwa na wasiwasi juu ya hilo hata kidogo.
Hatimaye, Lisa aliweza kumbembeleza bwana mkubwa huyo. Nesi alimtazama kwa huruma. Haikuwa rahisi kuwa mke na mama.
Ingawa Alvin alilalamika kwa muda tena wakati wa kudungwa sindano, aliacha kulia wakati Lisa alipomchezea katuni ili atazame. Baada ya hapo, Lisa alimwomba Shani ashuke chini ili akapate vitafunwa kwani Hans hakuwa na mtoto na hakujua anunue nini. Lisa alimwambia Shani anunue chokoleti na biskuti ambazo Suzie alipenda kula. Baada ya Shani kuleta vitafunio wodini, Alvin alikula chokoleti kwa uchangamfu.
Hans aliweza kulia baada ya kuona hivyo. "Mwishowe najua Binti Mdogo alifuata mapenzi ya nani." Kwanini hakutambua kabla kwamba Bwana Mkubwa Kimaro alipenda kula chokoleti?
Lisa aliwaza, 'Alvin alinyanyaswa na yaya wake alipokuwa mdogo, kwa hiyo alijizuia kila mara. Baada ya hapo, alipelekwa hospitali ya magonjwa ya akili. Angewezaje kula chokoleti?' Alichukulia tu kama kumrudishia Alvin maisha yake ya utotoni yenye furaha kwa kumtendea vyema kuanzia hapo na kuendelea.
Jioni, Chester, Rodney, na Pamela waliingia. Alvin alikuwa amejilaza kitandani, akimwangalia PAW Patrol kwa makini. Hata alikuwa na kidakuzi cha chokoleti mikononi mwake na uso wake ukiwa mzito. Hakuwaona walioingia hata kidogo.
“F*ck, Alvin. Uliishiaje hivyo?” Rodney aliumia moyoni. "Unakula hata chokoleti na kutazama PAW Patrol.
“Wewe bado ni Alvin ninayemjua?" Rodney aliendelea kuzungumza kwa muda mrefu, lakini Alvin bado hakumjali. Mwishowe hata aling’ata kipande cha chokoleti, akionekana kuridhika.
Pamela alinyanyua maziwa na chokoleti mikononi mwake. Alitabasamu kwa uchungu na kumwambia Lisa, “Hatimaye nimeelewa ni kwa nini uliniambia ninunue hizi na kuleta.”
“Ziweke hapa.” Lisa alichukua vitu hivyo kutoka mikononi mwa Pamela.
Pamela alimpiga Lisa begani. Alimuonea huruma sana rafiki yake wa karibu. "Uko salama? Ninatambua kuwa... wewe na Alvin mna vikwazo vingi sana. Kwanini usimwache tu?”
"Pamela, unazungumza nini?" Rodney hakufurahishwa na maneno yake. "Huoni jinsi Alvin alivyokuwa anatia huruma sasa?"
“Anatia huruma, lakini Lisa wetu naye hatii huruma? Yeye bado ni mdogo sana. Nani anajua ni lini Alvin atapona?” Pamela alikasirika. “Kwa maoni yangu, mtu mwenye matatizo kama Alvin hafai kuwa na mke hata kidogo. Isitoshe, kama si yeye kudanganywa na Sarah wakati huo, kusingekuwa na matatizo mengi sana ya kudanganyana sasa.”
Rodney alifungua kinywa chake. Uso wake mzuri ulionekana kukinzana. “Hilo...Hilo haliwezekani, sivyo? Je! Sarah ana uwezo kama huo?"
“Nilikuambia kuwa Alvin alidakwa na Sarah, lakini hukuniamini. Vinginevyo, unafikiri kwanini mtu mzuri kabisa angeishia hivyo ghafla?” Chester alisema kwa unyonge, “Sarah alikuwa ametengeneza bomu kichwani mwa Alvin, alikuwa anasubiri tu muda muafaka ufike ili aliripue.”
Rodney alichanganyikiwa. Hakuelewa ni kwanini Sara akawa mwovu kiasi hicho?
“Bwana Choka, umefanikiwa kushauriana na hao wanasaikolojia na wataalamu wa neva? Utafiti wako unaendeleaje?” Lisa aliuliza.
Chester alimtazama kwa sura ngumu machoni mwake. "Wanasaikolojia wakuu nilioongea nao wamesikia juu ya ustadi huo wa hypnotic hapo awali. Ni ujuzi uliokatazwa ambao umepigwa marufuku kutumika kote duniani kwa zaidi ya miaka 1oo. Kufikia sasa, hakuna habari ya kesi za uokoaji baada ya kulazwa kwa njia hiyo. Hata hivyo, tayari nimewaomba wanasaikolojia hao kuchunguza kesi za kihistoria zinazohusiana na hali ya Alvin. Tutegemee wanaweza kupata fununu lolote.”
“Sawa. ” Lisa alitulia kinyonge. Ilikuwa bora kuliko kutokuwa na tumaini hata kidogo.
Rodney kwa taabu alitembea hadi upande wa Alvin na alijaribu kumriwadha. "Alvin, unaweza kunipa keki zako na chokoleti?"
Alvin akamtazama. Kisha, alitazama kaki iliyokuwa mkononi mwake kabla ya kuichomeka haraka mdomoni na kuimalizia kwa kufoka. Ingawa Alvin alikuwa na umri wa kiakili wa miaka miwili tu, bado alikuwa mbaya sana.
Chester alicheka. "Inaonekana kama akili yake inaboreka."
"Hiyo ni sawa." Lisa pia aliweza kuhisi. "Yeye ni kama mtoto sasa. Kuna mambo mengi ambayo natakiwa kumfundisha kwa vitendo, lakini anaweza kujifunza yote kwa haraka.”
Sura ya 811
Rodney alitikisa kichwa kwa mawazo. “Basi naweza kumfundisha Alvin kuchumbiana. Hivi karibuni, utakuwa kwenye uhusiano tena na Alvin.”
Bila kusema, Pamela alimchoma, "Alvin ana akili tu ya mtoto wa miaka miwili hivi sasa. Anamchukulia tu Lisa kama shangazi. Unaweza kumfundisha kuchumbiana, lakini unafikiri atachumbiana na shangazi?”
Lisa alihisi amechomwa kisu cha moyo. Pamela aliongeza, "Mbali na hilo, ulikuwa bila ndoa kwa miaka 30. Je, unadhani unaweza kumfundisha Alvin jinsi ya kudate na uwezo wako huo? Sahau. Usimpotoshe.”
Rodney alihisi kupigwa kofi usoni. “Pamela Masanja, hakuna mtu atakayefikiri kuwa wewe ni bubu hata kama ukikaa kimya.”
Pamela alimtazama, bila kupendezwa. “Huwezi kukasirika kwa sababu tu nimesema ukweli. Wanaume wanapaswa kuwa na mioyo mikubwa zaidi." Rodney alilitazama tumbo kubwa la Pamela. Akashusha pumzi ndefu na hakusema neno mwisho.
Badala yake, alitoa simu yake na kufungua mchezo. Akaenda upande wa Alvin. "Njoo hapa, ol' Alvin. Nitakufundisha kucheza michezo ya simu, sawa?"
Uso wa Alvin ulijikunja. “Mimi si mzee. ”
“Oh, nilikosea. Nitakuita Alvlisa pia, sawa?" Rodney alitabasamu na kusema, “Kutazama katuni hakupendezi. Mchezo huu ni wa kufurahisha sana ... "
Kabla hajamaliza sentensi yake, Chester akaichukua simu yake. "Chester, unafanya nini?" Rodney hakuwa na furaha. "Hata hivyo, yeye si mtoto. Kuna ubaya gani kucheza baadhi ya michezo?”
“Ikiwa una wakati mwingi sana wa kucheza michezo, kwanini humsomei baadhi ya vitabu, kutazama televisheni pamoja naye, au kumfundisha kusoma? Anachohitaji kwa haraka hivi sasa ni kuongeza umri wake wa kiakili wa miaka miwili.” Chester hakukubaliana na vitendo vya Rodney. “Nikikutazama, ningependekeza usiingilie kati elimu ya mtoto wako. Mke wako yuko sahihi. Unapotosha watu.”
“Umesikia hivyo? Hata kaka yako ananiunga mkono. ” Pamela alikasirika baada ya kumsikia Chester. Hata hakujali jinsi Chester alivyotumia maneno “mkeo” kumfafanua.
Rodney alipiga kelele. Kwa hilo, hakuwa na la kufanya zaidi ya kuweka simu yake. Kwa bahati nzuri, Alvin hakutaka kujua jambo hilo, na kwa haraka akazama tena kwenye katuni.
Baada ya nusu saa, Rodney na Pamela walisimama na kuondoka.
Lisa aliwatoa nje.
“Sasa, Titus alienda kumuona baba mdogo wangu leo.” Rodney alisema ghafla, "Sijui walizungumza nini."
Moyo wa Lisa ulirukaruka. Lakini, aliutuliza haraka. Mbaya zaidi mambo yalikuwa tayari yametokea, hivyo hakuwa na la kuogopa.
"Bwana Choka tafadhali nijulishe alipo Sarah." Lisa alisema, “Hata kama sina ushahidi wa kuthibitisha kwamba anahusika na jambo hili, sitaki awe na maisha mazuri.”
"Amekwenda Marekani kuhudhuria kongamano la majadiliano lililofanywa na wanasaikolojia," Chester alisema.
"Hiyo ni bahati mbaya sana," Pamela alinong'ona.
“Ameenda kujificha kwanza. ” Lisa alifoka. "Tutazungumza juu ya hili tena atakaporudi. Wacha tuone ikiwa anaweza kukaa mbali milele. Bwana Shangwe, ikiwa unataka kumwokoa, tunaweza tu kuwa maadui."
“Tayari nimemalizana naye muda mrefu uliopita. Alvin ni kaka yangu, hivyo mimi pia nina hasira sana kuona yeye yuko hivyo. Sitamsaidia Sarah tena.” Rodney alikata haraka uhusiano wake wote na Sarah.
Pamela alimtazama kwa ubaridi. "Ukithubutu kumsaidia Sarah tena, nitazima d*ck yako."
“Una wazimu?” Rodney alitetemeka. Mtazamo wa mwanamke huyo ulimfanya ajisikie hana mzaha hata kidogo.
Jioni, Lisa alimchukua Alvin kufanyiwa vipimo vya mfululizo tena. Waliporudi wodini, tayari ilikuwa ni usiku.
Lea aliwaleta watoto wawili na kupeleka chakula cha jioni. Suzie na Lucas walikaa kitandani, wakaongozana na Alvin kula chakula.
“Alvlisa, tazama. Hivi ndivyo unavyoshika kijiko kula.” Suzie akawa mwalimu mdogo. “Usidondoshe wali.”
Kama vile Suzie alivyosema, Alvin alidondosha wali kwa bahati mbaya kutoka kwenye uma, na kufanya fujo kwenye meza.
“Mjinga,” Suzie alifoka. Sauti yake ilisikika kama vile Lucas alivyokuwa akimdhihaki.
Alvin akapepesa macho. Kisha, akapiga kelele kuelekea kwa Lisa na kuanza kulia. "Aunty, mimi sio mjinga ..."
“Sawa, wewe si mjinga. Alvlisa ndiye mwenye akili zaidi.” Lisa alikumbatia kichwa haraka na kumtizama Suzie kwa siri.
"Mama, ndivyo ulivyonifundisha, na nilijifunza mara moja," Suzie alisema huku akipiga kelele.
"Una uhakika umejifunza mara moja?" Lucas alimchoma.
"...Hata iweje, siwezi kumuona Baba katika hali hii, kumfundisha ni jukumu langu."
Pembe za mdomo wa Lisa zilitetemeka. "Inatosha, nyinyi mnapaswa kula haraka. Nitamlisha.” Baada ya kuongea alishika bakuli na kuanza kumlisha Alvin kijiko kwa kijiko.
Suzie alihisi huzuni. "Mama, nilipokuwa na umri wa miaka miwili, ulikuwa mkali sana na mimi kula peke yangu.”
Lucas alimtolea macho. “Huyo ni mume wake. Anampenda. Usiwe mtu wa kuona wivu.”
Suzie alifoka. “Hatimaye nimeelewa. Mimi si muhimu kwa Mama kama Baba.”
Lisa hakuweza kuvumilia. Suzie alimuonea wivu hata Alvin.
“Sawa, maliza chakula chako haraka na urudi nyumbani pamoja na Bibi. Kumbuka kuwahi kesho shuleni,” Lisa alisema kwa uchovu.
Watoto hao wawili kwa utii walimaliza mlo wao. Suzie alipokaribia kuondoka, alichukua hata sanduku la chokoleti kutoka kwenye meza. "Mama, hii sio nzuri kwa meno. Nitachukua hii kwa ajili yako. Kuiacha hapa ni kupoteza nafasi."
Alvin alianza kulia baada ya kuona hivyo. “Hapana, hapana. Aunty, yeye... alichukua... peremende zangu...”
Suzie alisema kwa msemo mzito, “Alvlisa, meno yako yatang’atwa na wadudu ikiwa utakula chokoleti nyingi. Kufikia wakati huo, utaonekana kuwa mbaya sana, meno yako yataoza, na kutakuwa na mende nyingi kwenye tumbo lako. Lisa hatakupenda tena.”
“Nataka Lisa anipende...”
Alvin alishtuka sana mpaka kwenye kope zake bado machozi yalikuwa yakimtoka. Sura hiyo ya kusikitisha nusura iufanye moyo wa Lisa kuyeyuka.
“Suzie, unaweza kuchukua chokoleti moja tu. Rafiki ya baba yako ndiye aliyempa.” Lisa akamwambia binti yake, “Usimtie hofu. Ana mwili wa mtu mzima lakini akili za mtoto, kwa hivyo kula chokoleti ni sawa.”
Suzie alikanyaga miguu yake. “Mhh. Mama unampendelea tu.”
“Sawa, baba yako bado ni mgonjwa. Bibi atakununulia.” Lea aliona ni kichekesho, na haraka akambeba mjukuu wake mdogo.
Lisa kichwa kilimuuma. “Aunty Lea, usimnunulie chokoleti nyingi.”
“Mama usijali. Nitamdhibiti Dada vizuri,” Lucas alisema kwa ukali.
"Asante, Lucas." Lisa alifarijika. Angalau bado kulikuwa na mtu mwenye busara.
Mara wodi ile ikanyamaza, Alvin akatoa mlio wa ghafla. “Aunty, simpendi... huyo... Dada.”
‘Jamani huyo si dada yako. Yeye ni binti yako,' Lisa aliwaza.
“Alvlisa, Suzie yuko sawa. Unaweza kula chokoleti, lakini huwezi kula nyingi. Kula chokoleti nyingi kutakufanya unenepe. Kufikia wakati huo, hautakuwa mzuri kama ulivyo sasa, na napenda wanaume wazuri," Lisa alisema kwa umakini.
Alvin alishikwa na butwaa. Alianguka katika mtanziko. "Lakini mimi si mwanaume. Mimi ni mtoto. Lakini sitaki... kuwa mnene. Nataka kuwa... mzuri. Nataka unipende.” Alvin aliinua kichwa chake, macho yake safi yakionekana kuwa mbaya sana......ITAENDELEA......
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA...
