JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................794-795
Sura ya: 794
Zaidi ya yote, alisema mambo yasiyofurahisha na kujaribu kumfanya Jack kunyakua nafasi ya mwenyekiti. Wakati Alvin alikuwa na watoto, bado alikuwa na furaha juu yake.
Lakini, Lisa alinyamaza na hakujibu.
Alvin akahema. "Mama, Lisa alipigwa kofi na mama yake."
Mike aliwasha sigara. Baada ya kitambo kidogo, alisema, “Kwa hali hiyo, sitakwenda kwa Titus kwa wakati huu. Pia... awali ulipanga kuondoka wiki ijayo. Bado mpango upo palepale?”
Kila mtu alimtazama Lisa. Lisa alikaa kimya kwa muda kabla ya kutikisa kichwa. "Nataka kukaa kidogo na kujua ukweli."
Alvin akazishika nywele zake ndefu. Nuru kali ilimulika katika macho yake meusi huku taratibu akipata wazo. "Baba, nguvu halisi ya familia ya Tshombe ikoje?"
Mike alisita kwa muda kabla ya kusema kwa njia ngumu, “Nakumbuka nilikuambia kuwa familia ya Titus ndio wamiliki wa benki za Congocom, zilizotapakaa huko Kongo na baadhi ya nchi za Ulaya ambazo zina Wakongo wengi, kama Ufaransa na Ubelgiji. Wanamiliki pia migodi mikubwa ya Colbat, Copper na Zinc huko Kongo kwenye jimbo la Katanga. Na pia wanamiliki mnyororo wa mahoteli makubwa ya kifahari kwenye nchi nyingi duniani. Wanaishi Lubumbashi ambao ni mji mkuu wa jimbo la Katanga huko Kongo lakini mara kwa mara hupendelea kwenda Ufaransa na Ubelgiji na kumuachia majukumu ya kuongoza biashara zao huko Kongo kijana wao. Kwa upande wa rasilimali fedha, Titus na Sheryl wako sawa. Mmoja wao anadhibiti madini, na mwingine anadhibiti mahoteli na mabenki. Haijalishi wanaenda nchi gani, utambulisho wao unatosha kwa Rais wa kila nchi kuwapokea yeye binafsi.”
Lisa alishtuka. "Mama yangu amepata nafasi yake ya sasa kwa sababu aliolewa na Titus?"
"Hapana, watu hawa wawili ni muungano wenye nguvu." Mike alimtazama kwa huruma kidogo. “Wewe ni binti yake wa kumzaa. Ikiwa Sheryl atakiri hadharani kuwa wewe ni binti yake na anakupa hata tone moja la utajiri wake, itatosha kukufanya kuwa miongoni mwa wanadada tajiri zaidi duniani.”
“Baba acha kunyunyiza chumvi kwenye kidonda cha Lisa, hajali pesa.” Alvin akakatiza haraka. “Baba, nina wazo. Tulitoa idadi kubwa ya watu wa Titus leo. Ninakisia kwamba hakika atatuma wanaume zaidi kutoka Lubumbashi, lakini mradi tu watu hao wasiweze kupita forodha na kuingia nchini, Titus na Sheryl watakuwa hoi nchini Kenya bila kujali ni pesa ngapi wanazo. Hilo likitokea, tunaweza kukabiliana nao jinsi tunavyotaka.”
Mike alishangaa kidogo. “Una uthubutu sana. Ikiwa kitu kitatokea kwa Titus na Sheryl nchini, Nathan atapata shida. Hatakubaliana na unachofanya. Familia ya Shangwe haiwezi kumudu kulipiza kisasi kwa familia ya Tshombe.
"Baba, ulisema kwamba familia ya Tshombe na Jimbo la Katanga ni sehemu mbili za nguvu kubwa. Ambapo kuna pesa na nguvu, kutakuwa na mabishano. Familia ya Tshombe imejaa vipaji, hivi si watatokea watu wanaomuonea wivu Titus? Maadamu tunaweza kupata mtu anayefaa katika familia ya Tshombe wa kushirikiana naye, kifo cha Titus kinaweza hata kuwa jambo la furaha kwa watu wa familia ya Tshombe.”
Maneno ya Alvin yalikuwa na maana, na kila mtu alielewa. Mike alimtazama mwanae kwa macho yaliyojaa hofu.
Lisa alipigwa na butwaa kidogo. "Je, kuna haja ya kwenda mbali hivyo?"
“Hili litakuwa suluhu la mwisho tunalotumia kujilinda. Usijali, hata siku hiyo ikifika, sitamuumiza mama yako. Zaidi... nitamweka chini ya kizuizi cha nyumbani.” Alvin alimtuliza kwa upole. "Kwa sasa, bado tunapaswa kukutana na Titus na mama yako ili tuzungumze na kujua kutokuelewana ni nini. Ni bora ikiwa tunaweza kuondoa kutokuelewana. Lakini ikiwa hatuwezi, basi hatutabaki na chaguo.”
Lisa aliitikia kwa kichwa. Bila shaka angejua ukweli haraka iwezekanavyo.
Alvin aligeuka kumwangalia Mike. “Baba, tafadhali nenda Lubumbashi na ujue ni nani mshiriki mwenye tamaa sana katika familia ya Tshombe na vile vile ni nani anayemwonea wivu zaidi Titus. Lazima uende kwenye Kisiwa acha Lupita pia kwenye ziwa Tanganyika. Sheryl aliookolewa hapo na mmiliki wa kisiwa hicho baada ya kutuwa na kimbunga, na baadaye akarithishwa kisiwa hicho baada ya mmiliki wake kufariki. Kwa hivyo lazima kuna watu kisiwani hapo ambao hawamkubali.
“Sawa, nitasafiri kwa ndege kesho. ” Mike alitikisa kichwa kwa jeuri.
•••
Wakati huo huo.
Katika jumba la familia ya Tshombe.
Titus akawatazama wale walinzi wawili waliokuwa wamepiga magoti mbele yake. Uso wake ulikuwa mweusi kama wino. "Kwa hivyo kati ya watu 30 niliowaleta kutoka Lubumbashi, ni nyinyi wawili tu ambao mmesalimika?"
Walinzi wawili wakatetemeka. Lina naye aliingiwa na hofu kidogo moyoni. Hata hivyo, alipofikiri kwamba Sheryl alikuwa upande wake, macho yake yalimtoka kwa manung’uniko aliposimama. "Ilikuwa kazi ya Lisa. Alileta kila mtu kutoka ONA na hata kuazima watu kutoka kwa familia ya Choka. Wanaume wa ONA na wa Choka waliwazunguka watu wetu kwenye maabara na kuwalemaza kimakusudi.”
“Inatia hasira! ” Sheryl alipiga meza kwa hasira na kusimama. "Kama ningejua hili lingetokea, ningemlemaza papo hapo."
“Mama, Uncle Titus, samahani. Sina maana sana.” Lina alianza kulia. "Nilitaka tu kuchukua maabara mapema, lakini Alvin alikuwa na watu wengi sana. Nilitaka kupeleka watu wengi zaidi, sikutarajia wangekuwa wakatili kiasi hicho.”
“Sawa, usilie. Nilimchukulia poa sana Lisa. Mara moja nitaagiza watu zaidi wa kuja kutoka Lubumbashi. Nitawalipa kwa hili." Sheryl alisaga meno yake.
Titus alizipapasa nywele zake kwa ishara ya uchovu. Alijuta sana kuja Kenya sasa. “Kama ningekuwa Alvin, nisingeruhusu watu wetu kuja Kenya. Hawataweza kupitia forodha.”
Lina alipigwa na butwaa, huku Sheryl akiwa amekunja uso. "Unamaanisha nini? Je, Alvin atathubutu kuwazuia watu wetu wasiingie Kenya?”
"Sheryl, familia ya Kimaro ni familia yenye ushawishi hapa na wako kwenye mashua sawa na familia ya Shangwe. Ingawa 70% ya KIM International imepatikana, miunganisho yake sio ya kawaida.” Titus alieleza wasiwasi wake. “Nawashauri wawili mtulie kwa sasa. Majeshi yetu yamechukuliwa sasa. Tumenaswa.”
Sheryl alidhihaki. "Titus, unajaribu kunitisha kwa makusudi ili nimwache Lisa?"
Titus aliutazama uso wa Sheryl kwa ukali na moyo wake ukamtoka kwa hisia kubwa ya kutomfahamu. “Sheryl, lini ulikosa akili kiasi hiki? Wewe si kama ulivyokuwa zamani hata kidogo.”
"Sikubadilika. Wewe ndiye uliyebadilika,” Sheryl alijibu kwa ukali.
"Mama, Uncle Titus, msipigane." Lina alishauri kwa haraka. “Yote ni makosa yangu. Kama si kwa sababu yangu, msingekuja Kenya.”
“Sio kosa lako. Ikiwa kuna mtu wa kulaumiwa, ni Lisa, "Sheryl alisema kwa kuchukizwa.
"Bwana Tshombe, habari mbaya." Wakati huo, msaidizi wa Titus alitoka nje kwa haraka. "Hospitali za Nairobi hazitakubali walinzi wetu waliojeruhiwa."
Lina alipigwa na butwaa, huku Sheryl akionekana kutokuamini zaidi. “Hawakubali watu wetu? Wanataka kufunga?"
Msaidizi akatabasamu kwa uchungu. "Kuna nguvu nyuma ya hospitali zote hapa Nairobi, na hiyo ni familia ya Choka. Chester Choka na Alvin Kimaro ni marafiki wazuri.”
Titus aliuliza kwa msisitizo, “Namna gani ikiwa tutawapeleka hospitali mahali pengine?”
Sura ya: 795
"Ikiwa matibabu ya majeraha yao yatachelewa, kunaweza kuwa na madhara makubwa, kama vile ... kupoteza uwezo wa kutembea kwa miguu yao," msaidizi alisema kwa sauti ya chini.
“Kupoteza uwezo wa kutembea kwa miguu yao?” Titus alikasirika sana hata akataka kumuua Lina. Watu hao wote walikuwa wasaidizi wake wa kutumainiwa.
Lina aliona sura ya Titus yenye hasira. Alifikiria jambo kwa haraka na kusema kwa haraka, “Mchumba wa Chester ni rafiki yangu mzuri.”
“Lina, sikutarajia marafiki zako wangekuwa na nguvu kiasi hicho. Unapaswa kupiga simu na kuzungumza naye. ” Sheryl alimtazama kwa kumtia moyo.
Lina aliitikia kwa haraka na kumpigia Cindy.
“Lina, kuna nini?” Cindy alikuwa katika hali mbaya sana wakati huo. Madili na matangazo yake mengi yalikuwa yameghairiwa.
“Cindy, watu wa uncle wangu walijeruhiwa, na Alvin na Chester waliziambia hospitali za Nairobi zisiwachukue kwa matibabu. Unaweza kunisaidia?” Lina akatabasamu. “Bila shaka, nitakusaidia kwa hili. Ikiwa kuna sinema zozote nzuri za Hollywood baada ya hii, ninaweza kukupa connections.
Cindy aliguswa moyo, lakini aliweza kusema tu kwa tabasamu la kufoka, “Unanifikiria sana. Chester na Alvin ni marafiki wazuri. Hakuna jinsi atanisikiliza ... "
Kwa kuongezea, Chester alisema kwamba angeachana naye, kwa hivyo alikuwa na wasiwasi sana.
“Unaweza kwenda kwa wazazi wa Chester. Cindy, hukuwahi kutaka kujua ni nani watu nyuma yangu?” Lina alisema kwa sauti ya chini. "Watu walio nyuma yangu ni familia ya Tshombe. Wana udhibiti wa madini muhimu ulimwenguni na wanamiliki benki kubwa zaidi huko Kongo. Je, kweli unataka kukosa fursa hii ya kukutana nao?”
Moyo wa Cindy ulidunda kwa kasi. "Wewe... Mama yako si anatoka Dar es Salaam..."
“Hao si wazazi wangu halisi. Usiseme lolote kuhusu hili,” Lina alisema. "Unaweza kuchagua kama unataka kuchukua fursa hii au la. Ni wakati tu una connections zenye nguvu ndipo unaweza kupata msimamo thabiti katika familia ya Choka.
"Naelewa." Cindy akaitikia kwa kichwa. “Niachie mimi.” Cindy haraka akapiga simu kwa Michael Choka.
Michael aliposikia kwamba Cindy anafahamu kisa hicho, moyo wake ulijawa na msisimko mkubwa huku akipiga simu haraka hospitali kuwaruhusu walinzi wa Titus.
Familia ya Tshombe ilipogundua, Sheryl alijawa na sifa kwa Lina. “Una uwezo sana.”
“Usiseme hivyo mama. Haya yote yalianza kwa sababu yangu. Michael alisema kwamba anataka kula chakula na wewe na Uncle Titus,” Lina alisema, “Kama unavyoona, Chester na Alvin ni marafiki wazuri, lakini mradi tu tunamshinda baba yake Chester, familia ya Choka haiwezi tena kumsaidia Alvin. .”
“Ndiyo, hakika. Ni chakula tu.” Sheryl alikubali kwa urahisi.
Titus na Matthew walikuwa wamekaa kimya pembeni bila kusema neno lolote. Matthew alikosa raha sana kumuona Sheryl akimsifia Lina bila kukoma. Ni wazi ni kwa sababu ya uzembe wa Lina ndio ulisababisha walinzi wao kuumia, lakini Sheryl alimsifia tu kuwa ana uwezo. Ni nini kilikuwa kikiendelea? Matthew aliinuka na kuondoka.
Sheryl alimsimamisha kwa upole na kuonya, “Ukiwasiliana na Lisa tena, hutahitaji kuniita ‘Mama’ siku zijazo.”
“Hah. Nakuita mama yangu, lakini bado unakumbuka kuwa una mtoto wa kiume? Nilidhani una binti mmoja tu.” Matthew alivuta uso mrefu na kuondoka.
Sheryl alimtazama Titus kwa hasira. “Angalia jinsi ulivyomharibu adabu mwanao!”
Titus alichanganyikiwa kwa hasira. Hakuelewa jinsi Sheryl Jones ambaye mara moja alikuwa mwerevu, mwenye busara, mtulivu na mkarimu alivyogeuka kuwa mpumbavu.
“Ndiyo wacha nimharibu adabu, ni mwanangu.” Titus akainuka na kuondoka.
Kuangalia mitazamo ya kutojali ya baba na mwana, Sheryl alikasirika sana na alitaka kuvunja kila kitu mbele yake. Yote yalikuwa makosa ya Lisa. Lisa ndiye aliyesababisha wazidi kuchukiana na kutengana.
Baada ya Matthew kuondoka kwenye makazi ya Tshombe, alitoa simu yake na kuona missed calls kutoka kwa Lisa. Alimpigia simu baada ya kutoka kwenye cafe, lakini Sheryl alikuwepo wakati huo, kwa hiyo hakuthubutu kujibu. Alipofikiria sura ya Lisa iliyovimba, kwa hatia alirudisha simu.
Sauti ya kejeli ya Lisa ilisikika kutoka upande wa pili. "Bwana Mdogo Tshombe, ni taarifa gani nyingine unayohitaji kupata kutoka kwangu?"
"Samahani." Matthew alikasirika sana na kuomba msamaha. “Nilimwambia mama yangu hivyo kimakusudi. Niliogopa kwamba angekasirika. Nilipokutana nawe mara ya kwanza, sikujua kuwa wewe ni Lisa. Ulikuwa pia umesema uwongo na kusema kwamba jina lako ni Heroin, baadaye ukasema Carren Ngosha…”
“Lakini hukujua baadaye? Ulikuja Nairobi kunitafuta kwa makusudi, na nafasi hizo zote kukutana kwenye maduka ulipanga wewe."
Lisa alikasirika kweli. “Familia yako ya Tshombe ni tajiri sana, lakini wewe na baba yako ilibidi mjishushe kwenye ngazi ya ujasusi ili kunihadaa. Kwa kweli sielewi jinsi nilivyoichokoza familia yako.”
“Haukukasirisha familia ya Tshombe. Ulimkasirisha Lina na mama yangu. ” Matthew alisema hivyo na kuongeza moyoni mwake, 'Bila shaka, ulimdhuru pia bibi yangu.' Hata hivyo, alimfahamu Lisa kwa muda sasa. Katika mifupa yake, alihisi kwamba Lisa hakuwa ... mbaya.
“Nilimchokoza Lina? Siku zote amekuwa ndiye aliyenikasirisha. Alimuua hata rafiki yangu mzuri. Kuna chuki kubwa kati yetu,” Lisa alisema kwa ukali, “Lakini mama yako ana nini dhidi yangu? Sijamwona kwa karibu miaka 20. Inatosha kwamba simlaumu kwa hilo.”
“Lina ni binti wa mama yangu. Ukichafuana na Lina, ni sawa na kumfanyia fujo mama yangu,” Matthew alisema.
"Nini?" Lisa alipigwa na butwaa kabisa. Hata alifikiri kwamba masikio yake yalikuwa yakimchezea. “Lina ni binti wa mama yako?”
“Bila shaka.” Matthew alijua alichotaka kusema na kwa haraka akasema, “Usiniambie kwamba wewe ni binti yake na si Lina. Sitakuamini.”
Lisa akakosa usemi. Iwapo huyo mpumbavu Matthew angekuwa amesimama mbele yake muda huo, angeshika kichwa chake na kukiponda ukutani ili kumfanya mambo yawe sawa.
“Yeye si binti wa Sheryl. Lina ni binti John Jones! Yeye ni mpwa wa Sheryl” Lisa akafoka kwa hasira, “Nyie kundi la wajinga wote mmedanganywa na yeye! ”
"Wewe ni mjinga." Matthew alikasirika kidogo. "Lisa, usifikiri kwamba kila mtu ni rahisi kudanganywa kama Joel Ngosha."
Lisa akashusha pumzi ndefu huku akiwa na wasiwasi kwamba ubongo wake utalipuka kutokana na hasira. “Sikiliza. Sijui Lina alikuambia nini, lakini mimi ni binti wa damu wa Sheryl. Mimi ni dada yako. Ikiwa huniamini, unaweza kufanya kipimo cha DNA. Unapaswa kuwa na uwezo wa kusema kwa kuangalia tu nyuso zetu. Ninafanana zaidi na Sheryl, sawa?”
"Ni kawaida kwa mpwa kuonekana kama shangazi yake wakati mwingine." Matthew alidhihaki. “Na sitafanya nawe kipimo cha DNA. Chester na Alvin ni marafiki wazuri. Itakuwa kazi rahisi kwako kumfanya Chester avuruge matokeo ya vipimo.”...ITAENDELEA.....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA...
