JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................664-665
Sura ya: 664
Logan aligundua kuwa uso mzuri wa Lisa uliochanganyikiwa ulibadilika polepole, na hakuweza kujizuia kuhema.
“Kusema kweli, uliporudiana na Alvin, nilijiuliza kama hakuna mwanaume bora katika dunia hii. Sikuelewa kwanini ulilazimika kung'ang'ania kwake. Lakini kusema kweli, huenda alidanganywa na Sara zamani, lakini anakupenda kikweli sasa. Kama si wewe, angewezaje kujikata kidole? Alifanya hivyo kwa madhumuni ya kupunguza umbali kati yako na yeye.”
Lisa, bila shaka, alielewa hoja yake.
Alikuwa amekubali kwa mdomo kurudiana pamoja na Alvin siku hizi chache. Kwa kweli, alifanya hivyo kwa ajili ya watoto. Isitoshe, alikuwa akimsumbua sana hivi kwamba asingeweza kufanya lolote wala kuhangaika kumpinga. Hata hivyo, alikuwa bado hajaufungua moyo wake kwake.
Logan alishtuka. “Uliporudi kutoka ng’ambo, uliendelea kusema kwamba unataka kulipiza kisasi kabla ya kurudiana naye. Lakini, niliweza kukuona ukiyumba. Ni kwa sababu alinikata kidole ndipo ukamkatisha tamaa kabisa.
“Kwa kweli, nimeshaelewa kwa muda mrefu. Wewe ndiye uliyekata tamaa, na pengine ni kwa sababu unafikiri ulishindwa kunilinda. Lakini ninatumai kuwa nyinyi wawili mnaweza kurekebisha mambo yenu wakati huu.”
Baada ya kumaliza kuongea, aligeuka na kuelekea upande mwingine.
Hatua chache baadaye, aligeuka tena na kuongeza, “Nimetoka tu kwake, na hakuonekana kuwa na hali nzuri sana.”
Lisa alisimama kwa muda hadi Ambah alipokuja na kusema, "mwenyekiti, Meneja Mkuu anataka kukuomba kwa chakula cha mchana na kuzungumza kuhusu biashara..."
“'Sitapatikana. Naondoka sasa hivi, na sitarudi ofisini.”
Lisa kisha akamtupia ile hati na mara akatoka ofisini.
Aliendesha gari moja kwa moja hadi KIM International.
Alipofika, alichukua lifti hadi ghorofa ya juu na kuupiga teke mlango wa ofisi. Kulikuwa na watendaji watano hadi sita ndani, na wote walimtolea macho ya ajabu.
"Lisa, nini kinakuleta hapa?" Alvin alisimama mara moja. Kulikuwa na sura ya mshangao juu yake
“Bwana Kimaro, tutaondoka kwanza. ” Watendaji walijipa udhuru kwa kujiongeza.
Watendaji hao walipoondoka bado walikuwa wanapiga minong’ono.
"Inaonekana kama BwanaKimaro amerudiana pamoja na mke wake wa zamani."
“Duh. Uvumi ulikuwa ukiruka juu yake hapo awali. Inawezaje kuwa kweli?"
“Haya, sijawahi kuona Lisa akija kumtafuta Bwana Kimaro hapo awali, lakini sasa, nimeshawishika. ”
“Mnadhani mimi ni kiziwi? Haraka na mtoke nje. ” Alvin aliangaza macho ya watendaji hao kwa kukosa subira kabla ya kuufunga mlango kwa nguvu.
Kisha, akauliza kwa furaha kwa sauti ya upole, “Lisa, je Logan amekuambia jambo fulani?”
"Ulikata kidole chako kutoka kwa mkono gani? Nionyeshe.” Lisa aliamuru kwa hasira.
"Hakuna haja ya kuona. Inasikitisha, na inaweza kukutia hofu.” Alvin alirudi nyuma vibaya.
Hakuwahi kupata hali ya kujistahi hivyo hadi alipomtazama uso wa mbweha kwa wakati huu.
“Alvin.” Lisa aliinua macho yake mekundu na kumtazama. "Kwanini hukufikiri kwamba ingenitisha kabla hujakata kidole chako?"
Midomo ya Alvin yenye kupendeza na myembamba ilitetemeka. Hatimaye, alinyoosha mkono wake kwa utii. Miongoni mwa nafasi za vidole vyake vitano, kulikuwa na sehemu moja tupu iliyofunikwa na safu nene ya bandeji.
Lisa alihisi kama macho yake yanachomwa na kitu.
Alijaribu kuvumilia, lakini bado macho yake yalikuwa mekundu.
"Alvin, kuna kitu kibaya na wewe?" Alishindwa kujizuia na kumkemea.
Alvin aliyatizama macho yake yaliyokuwa mekundu, na ghafla, hakujihisi kujisumbua au woga tena. Kinyume chake, midomo yake iliinuliwa kwa tabasamu tamu. “Una wasiwasi na mimi?”
Lisa alikasirishwa sana na Alvin na hakuweza kusema chochote.
Alikuwa katika hali hii, lakini bado alisema alikuwa na wasiwasi juu yake. Je, hiyo ndiyo ilikuwa maana?
“Lisa, nina furaha sana. Inaonekana kama kukatwa kidole changu kulikuwa na thamani yake.” Alvin alisema kwa upole, “Kama ningejua mapema, nisingalichelewesha hadi leo. Ningekuwa nimekikata zamani.”
“Alvin, kwa kweli, mimi...” Lisa alihisi uvimbe kwenye koo lake.
“Lisa, usiseme chochote. Nisikilize."
Alvin alitumia mkono wake mwingine mzuri kabisa kuziba mdomo wake. “Uliniambia hapo awali wewe unamchukulia Logan kama familia yako na kwamba ikiwa ningemkata vidole vyake, isingewezekana tuwe pamoja. Lakini, sikujali na bado nilifanya hivyo. Kwa kweli, nilikuwa na sababu nyingine. Nilimwonea wivu Logan. Nilikosa raha sana kukuona unamjali sana mwanaume mwingine. Lakini imethibitishwa kwamba nilikosea.”
“Ingawa umekubali kuungana nami, lakini naelewa umefanya hivyo kwa ajili ya watoto. Huchukui hatua ya kunipigia simu, kutuma ujumbe au kukutana nami. Kuna vikwazo kati yetu. Sarah ndiye kikwazo cha kwanza, wakati Logan ni wa pili. Huenda nisiweze kukufidia kwa kikwazo cha kwanza, kwa hivyo lazima nikulipe fidia ya pili. Ikiwa sivyo, hata tukirudiana, hatuwezi kamwe kurudi kwenye uhusiano tuliokuwa nao hapo awali.”
Baada ya kuongea, alimkumbatia kwa nguvu Lisa. “Lisa, kumbukumbu zangu za siku za nyuma zimechanganyika, na siwezi kuzikumbuka tena. Lakini, baada ya kurudi Kenya, tulikuwa kwenye uhusiano kwa muda mfupi. Ingawa ilikuwa muda mfupi sana, ilikuwa isiyoweza kusahaulika kwangu. Nilikujua wazi ulinikaribia kwa makusudi ili kulipiza kisasi kwangu, lakini bado nilikuwa na furaha sana. Nilikuwa mjinga kwa kutojua jinsi ya kukuthamini ipasavyo. Unaweza kunipa nafasi nyingine tena?”
Akainamisha kichwa chake na kumtazama kwa macho mazito yaliyojaa matarajio.
Lisa hakusema chochote. Badala yake, aliinamisha kichwa chake, akamshika mkono wake uliojeruhiwa, na kuunganisha vidole vyao. Wangeweza kufanya hivyo hapo awali, lakini sasa, mkono wake mmoja ulikuwa na vidole pungufu, na usingeweza kuingiliana na mkono wake sawasawa. Machozi yake yalimdondoka bila kujizuia.
Hakujua ni kwanini analia. Hakuweza kujizuia kufikiria jinsi walivyokuwa wakifunga vidole vyao kila wakati wakati walipopendana sana wakati huo.
"Lisa, maishani mwangu sikuwahi kufikiria kukuona ukimwaga machozi kwa ajili yangu."
Alvin aliinamisha kichwa chini na kutumia midomo yake myembamba kumbusu machozi usoni mwake. “Je! machozi si yana chumvichumvi? Kwanini yako ni matamu sana?"
“Hahah.” Lisaalitaka kulia, lakini baada ya kusikia maneno yake, hakuweza kujizuia kuangua kicheko. Aliinua mkono wake kwa silika na kumpiga kidogo. Alvin alifoka kwa maumivu.
Lisa alisema kwa woga, “Usijifanye. Nilikuwa nikipiga kifua chako, sio kidonda chako."
"Mwili hutetemeka, na jeraha litaumia pia. ” Alvin alitabasamu kwa uchungu.
Lisa alikunja uso kwa ukimya. Ghafla alisema, “Wewe ni dhaifu sana. Logan alipata majeraha makubwa kama hayo hapo nyuma na hata alipoteza kidole, hata hivyo hakulalamika nilipompeleka hospitali.”
Alvin hakuridhika na kudharauliwa na mwanamke aliyempenda. “Nilikuwa natania. Sina uchungu. Ikiwa huniamini, unaweza kukikandamiza sana kidonda changu na uone."
Kisha akainua mkono wake na kuinamisha uso wake mzuri kana kwamba hana cha kupoteza. Lisa ghafla aligundua kuwa anaonekana mtoto mzuri kwa njia hiyo. Alikuwa mtoto kiasi kwamba alionekana mzuri sana, haswa wakati uso huo mzuri ulikuwa umepauka sana. Mwonekano huo unaweza kuumiza moyo wa mwanamke yeyote.
“Kweli? Ngoja nijaribu basi.” Wakati Lisa alinyoosha mkono wake na kufanya kama alikuwa karibu kukandamiza chini, aliona Alvin akifumba macho haraka, na kope zake zilikuwa zikimtetemeka. Hata paji lake la uso lilikuwa gumu.
Pembe za midomo ya Lisa zilijipinda kidogo. Mwishowe, aliweka mikono yake chini, akainama, na kumbusu.
Sura ya: 665
Alvin alipigwa na butwaa hadi akafumbua macho. Maumivu makali hayakuja. Badala yake, kilichokuja ni midomo ya maji yenye juisi ya mwanamke.
“Fungua mdomo wako.” Sauti nyororo na ya kuvutia ya mwanamke huyo ilisikika bila kueleweka.
Alvin alihisi kana kwamba moyo wake ulikuwa karibu kuyeyuka. Je, si kawaida wanaume waliozungumza mambo machafu? Hata hivyo... Ahem, ilionekana kuwa ya kuvutia zaidi kutoka kwa Lisa.
Alvin alisisimka sana. Akamkumbatia kwa nguvu na kulizidisha lile busu kwa ukali.
Alikuwa amembusu Lisa kabla ya hili, lakini hakuwa mpumbavu. Aliweza kuhisi kwamba busu hili halikuwa sawa kabisa na zile za zamani. Angalau alikuwa akiitikia kwa jazba, kiasi cha kufanya damu ya Alvin kuanza kuwaka moto. Alipotaka kuendelea zaidi, Lisa alimshika mkono.
“Lisa...” Koo la Alvinla kuvutia lilitoa sauti ya kubembeleza.
“Alvlisa, usichanganyikiwe sana. Je, si ulisema kwamba inauma wakati mwili wako unapotetemeka? Tazama jinsi unavyotetemeka sasa. Wewe ni kama ungo. ” Lisa alipepesa macho bila hatia na kumkumbusha kwa mzaha.
Alvin alikasirika. Laiti angejua, asingesema maneno hayo. "Ukinibusu, haitaumiza."
“IAchana nayo.” Lisa akatoa macho yake mazuri.
Hata hivyo, sura hiyo ya kutaniana ilimfanya Alvin ahisi kukosa subira zaidi. “Lisa, najisikia vizuri sana unaponiita hivyo. Uliniita hivyo huko nyuma pia? Inasikika kimahaba zaidi.”
“Mmmh.” Lisa aliinamisha macho yake chini. Hakutaka ajisikie kukumbuka mambo ya zamani. Aliogopa kwamba kumbukumbu zake zingerudi polepole ikiwa angehisi hisia za zamani, na wakati huo, angeweza kuchnganyikiwa.
"Je, ulichoma sindano ya kuzuia tetenasi kwenye kidonda chako?" Lisaaliuliza.
"Nilitundikiwa dripu ya IV wakati wa alfajiri. Lakini lazima niwe kwenye dripu ya IV kwa angalau siku tatu hospitalini,” Alvin alijibu kwa uaminifu.
"Itakuwa ngumu unapofanya kazi au kuandika?" Lisa aliuliza. Alvin alikuwa tofauti na Logan. Logan hakuhitaji kutumia kompyuta sana, ilhali, kama bosi wa KIM International, Alvin alilazimika kutumia kompyuta au kuandika mara kwa mara.
"Nitazoea polepole." Alvin alisema huku akitabasamu, “Ukilinganisha na wewe, haya yote si lolote si chochote. Ni sawa hata nikipoteza mkono.”
"Hilo haliwezekani." Lisa akamkatisha kwa uso ulionyooka. "Ningekudharau ikiwa ungekata mkono."
Alvin alikuwa akisema maneno ya kugusa na ya kimahaba. Hakukuwa na haja ya yeye kutupiwa maneno ya huruma namna hiyo. Taratibu akakunja sura kwa huzuni.
“Lisa, ni mchana tayari. Unataka kula chakula cha mchana pamoja nami?" Alvin aliuliza akijaribu kujiridhisha.
“Sawa.”
"Unataka kula nini? Kuna mikahawa michache karibu na kampuni yetu—”
“Twendeni tukale.” Lisa alimkatisha. "Hali yako ya sasa haifai kufanya kazi, kwa hivyo unapaswa kurudi nyumbani na kupata nafuu."
"Lakini sitaki kurudi kwenye makazi ya familia ya Kimaro ili kupata nafuu. Nataka kukaa na wewe. ” Alvin alimtazama kwa upendo.
“Kwa sasa ninaishi na baba yangu. Nikikupeleka kwa baba, nitapata karipio nzuri kutoka kwake.” Baada ya hapo, Lisa alikaa kimya kwa muda. Kisha, akasema, “Twende Palm Springs. Si una nyumba huko? Wewe unaweza kupumzika huko mchana na kurudi kulala na watoto usiku.”
“Sawa.” Alvin angefanya hivyo kwa furaha. Ilimradi Lisa alikuwa tayari kuandamana naye, angeweza hata kupumzika kwa mwezi mmoja.
Wakiwa njiani Lisa aliendesha gari huku Alvin akiwa amekaa kwenye siti ya abiria. Alijisikia furaha kama mtoto. "Lisa, hakuna chakula chochote kwenye nyumba yangu huko Palm Springs. Hebu tununue chakula.”
"Tutaenda kwenye duka kubwa baadaye." Lisa naye alikubali.
Walipokuwa wanafanya manunuzi kwenye duka kubwa, Lisa alienda sehemu ya nyama na kununua vipande vitatu vikubwa vya mbavu za nguruwe. Alvin alikuwa juu ya mwezi. “Lisa, unakumbuka hilo
Napenda nyama ya nguruwe zaidi."
“Ndiyo hivyo, na Suzie alikufuata. Anapenda hizo nyama za nguruwe pia.”
Kwa mawazo ya binti yake, Lisa hakuweza kujizuia kwenda kwa moyo mpole. “Kwanini tusiende kwenye makazi ya familia ya Kimaro? Kisha, watoto wanaweza kula pia.”
“Sio leo. Nataka kuwa na muda wa kuwa peke yetu,” Alvin alisema huku akimshika mkono.
“Si tumejipatia muda mwingi? Ulisema unataka kuwa na sisi wenyewe jana pia, na hata nilikubali kuwa na wewe kwenye nyama choma."
Lisa alihisi akizidi kuwajutia watoto kadiri alivyozidi kuwaza juu yake. Wakiwa wazazi hawakuwa wameandamana nao hata kidogo.
"Lisa, ulinipuuza katikati ya nyama choma," Alvin alielezea kwa ukali. "Ilinifanya nishuke moyo sana hivi kwamba nilikata kidole changu mara moja nilipofika nyumbani."
Lisa alikosa la kusema. “Sawa, sawa. Nitatumia muda na wewe peke yangu tena.”
“Mmmh.” Alvin aliitikia kwa kichwa na kusukuma kigari cha shopping kwa utii. Wakati mmoja, alisema alitaka zabibu na Strawberry. Kisha, iliyofuata, alisema alitaka mtindi. Lakini, vyakula hivyo vyote vilikuwa vyakula vya Lisa.
Lisa naye hakuongea chochote na kumwachia yote.
Mara baada ya kulipa na kutoka nje, waliona kwamba walikuwa wamefuatwa na baadhi
watu.
"Waandishi hao ni wagumu sana." Alvin alikunja uso kwa dharau.
“Waache watufuate watakavyo. Karibu kila mtu anajua kwamba nimerudiana pamoja nawe bila talaka bado. Sijali tena,” Lisa alisema bila kujali.
“Mm.” Alvin alitikisa kichwa sana.
Huko Palm Springs, Lisa alivaa aproni na alikuwa karibu kuanza kupika. Hata hivyo, Alvin alijisikia vibaya sana. “Lisa, kwa nini nisipike? Ingawa kupika kwako kutamu, wanawake wanapaswa kujaliwa. Sijisikii vizuri kukuruhusu unipikie.”
"Sahau. Una jeraha sasa, na zaidi ya hayo, sitapika sana. Nitapika sahani mbili tu.” Lisa kisha akamfukuza nje.
Kupika kwake kulikuwa kwa haraka. Katika muda usiozidi nusu saa, alikuwa amepika sahani mbili za nyama choma ya nguruwe na madikodiko kibao. Alvin alikuwa hajaonja upishi wake kwa muda mrefu sana, kwa hivyo alifikiri chakula kingekuwa kitamu haswa. Mwishowe, alimaliza hata akaona chakula kimekuwa kidogo. Baada ya kumaliza kula, alilalamika, "Hapo zamani nilikuwa mjinga."
"Mradi unaijua." Lisa alikubali huku akitabasamu.
Alvin akasonga. Aliendelea kusema, “Ni wazi tayari nilikuwa na wewe, mke mzuri ambaye angeweza kupata pesa na alikuwa na ujuzi mzuri wa kupika. Kwanini bado nilijihusisha na Sarah? Angewezaje kulinganisha na wewe? Yeye si mrembo au mwenye uwezo kama wewe, na ujuzi wake wa upishi ni mbaya pia. Lazima nilikuwa nimerukwa na akili.”
Lisa aliinua uso wake mzuri lakini hakusema neno. Alimtazama tu huku akimbembeleza.
“Lisa,” Alvin aliweka mkono wake kiunoni. "Kwanini wewe ni mkamilifu sana?"
“Itabidi nimuulize mama yangu kuhusu hili. Yeye ndiye aliyejifungua mtoto mzuri sana kama mimi.” Lisa alikubali kubembeleza kwake kama jambo la kweli.
Alvin alicheka kabla hajainamisha kichwa na kumbusu midomo yake bila kusema chochote. “Usifanye fujo. Ni lazima nioshe vyombo.”
Lisaalimsukuma.
“Usioshe. Nitafanya,” Alvin alisema.
“Mkono wako una jeraha. Utaoshaje vyombo?"
“Si nilinunua gloves tulipokuwa supermarket? Nilikuwa napanga kuitumia kuosha vyombo.” Alvin alichukua jozi ya glavu nje. "Maji hayataingia kwenye jeraha ."
Lisa alipigwa na butwaa. Alifikiri ni mapenzi tu aliposema ataosha vyombo.
"Hakuna haja. Unaweza kuosha utakapopona.” Lisa alichukua glavu na kuziweka mbali.
"Lisa, siwezi kuvumilia kukuruhusu kuosha vyombo." Alvin alikunja uso. "Sikujua vizuri zaidi hapo awali. Kuanzia sasa na kuendelea, nataka kukuthamini ipasavyo. Chakula unachotengeneza ni kitamu, siwezi kula vyakula vilivyotengenezwa na watu wengine.”.......ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA...
