JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................640-641

Sura ya: 640

KIM International

Msimamizi alitoka nje ya ofisi ya Mwenyekiti. Hans aliingia mara moja huku akiwa ameshikilia pakiti za dawa. "Bwana Mkubwa Kimaro ..."

Baada ya kumkabidhi Alvin ile dawa, Alvin aliinua kichwa chake kutoka kwenye laptop yake na kuzitazama bila kujali huku akiwa amekunja uso.

“Mbona umenipatia dawa nyingi hivyo? Mimi si dhaifu. Kuna hata chai ya tangawizi, inatosha kupambana na mafua. Unataka kuniua?”

Hans alieleza kwa tabasamu, “Si mimi niliyenunua hizi. Alikuwa Bi Jones ambaye alimwomba Katibu wake kuzituma hizi hapa.”

Alvin alipigwa na butwaa kwa muda kabla ya macho yake meusi kuangaza.

“Kweli?”
“Ndio. Katibu wake amezituma hapa. Wewe— ”

Hans alikuwa karibu kumwomba achague zile ambazo zingesaidia kwa homa yake. Hata hivyo, kabla hajamaliza sentensi yake, Alvin alichukua chai ya tangawizi na kuiteremsha tumboni moja kwa moja. Baada ya kumaliza chai ya tangawizi, alitoa tabasamu la kuridhika kama vile alivyokuwa anakunywa. "Ina ladha nzuri."

Hans alipigwa na butwaa. Je! ni nini?! Hakuwahi kuona mtu mwingine akinywa chai ya tangawizi haraka hivyo. Zaidi ya hayo, tagawizi ilikuwa imekaa hapo kwa muda mrefu, kwanini hakujisumbua kunywa kabla?

Kabla Hans hajapata fahamu zake, Alvin alikuwa tayari amefungua chupa ya ‘acyclovir oral suspension’ na akainywa pamoja na vidonge vichache vya mafua.

Hans alipokuwa akimwangalia akila aina kadhaa za dawa, alisema mara moja, “Bwana Mkubwa Kimaro, sio lazima unywe kila kitu. Kuna aina kumi za dawa hapa. Hakuna mtu anayetumia dawa kama vile unavyofanya."

“Lisa alininunulia hizi, na ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo. Ni lazima nithamini fadhili zake.” Alvin alichukua kila aina ya dawa kama ilivyo.

Hans alishindwa kabisa kusema. Alvin alikuwa kama mjinga tu aliposikia kuhusu Lisa.

Baada ya Hans kuondoka, hakuweza kujizuia kumpigia simu Lisa. “Bi Jones, kwa nini ulimnunulia dawa za aina nyingi sana Bwana Mkubwa? Alimeza zote.”

"Hiyo ni nzuri, sivyo?" Lisa alisema, "Anaweza tu kupona mapema kwa kutumia dawa."

“ .. Hapana, tatizo hana homa wala tumbo. Alimeza kila dawa kama anakula pipi tu au anakunywa chai bila kufikiria.”
Lisa alinyamaza. Hakujua kama Ambah alikuwa amenunua dawa nyingi kiasi hicho, yeye alimwambia anunue aina mbili tu za dawa. Ilionekana kuwa alikuwa amesahau kumwambia Ambah kuhusu dalili za Alvin. Ambah asingeweza kununua kila kitu, sivyo?

Hata dawa zingenunuliwa na kupelekwa, Alvin angetumia kila kitu bila kuzingatia dalili zake? Alifikiri alikuwa anakula peremende?

Hans alicheka kwa uchungu. “Tafadhali jaribu kumshawishi bwana Mkubwa. Ikiwa atafanya hivi kwa siku nzima, atakuwa mgonjwa kwa kutumia dawa ingawa alikuwa sawa hapo awali."

“Yeye ni mtoto? Hajui jinsi ya kuangalia maelezo ya dawa kabla ya kuzitumia?" Lisa alisema kwa hasira.

“Kwa sababu dawa hizo zilitoka kwako. Ni sawa na wanaume kuwapa wanawake chokoleti. Ilimradi ni kutoka kwako, hata kahawa chungu ingekuwa na ladha tamu,” Hans alieleza.

Mwishowe, Lisa akapiga namba ya Alvin. “Lisa, nimemaliza kunywa dawa ulizonitumia. Asante." Sauti ya Alvin ilikuwa ya upole kama upepo wa joto wa mwezi Mei. Ilimfanya Lisa aone aibu kidogo.

“Hakuna haja ya kunishukuru. Ni ishara ya shukrani kutoka kwangu kwa ushahidi ulionipa asubuhi ya leo,” Lisa aliweka uso wa ujasiri na kusema.

"Kwa hivyo ... dawa hizo zilikuwa zawadi ya kunishukuru?" Sauti ya Alvin ilishuka ghafla.

“Mm.”

Alvin mara moja akasema, “Basi sitaki. Nitamwomba Hans azirudishe. Thawabu ninayotaka ni busu. Ninaweza kununua dawa mwenyewe. Na usiniambie nibonyeze mdomo wangu wa juu na wa chini pamoja ili nijibusu, nataka nibonyeze mdomo wangu na wako. Hisia ya kukubusu ni tofauti.”
"Alvin, je homoni za kiume ziliziba ubongo wako?" Lisa alikasirishwa naye sana.

“Hapana, nina kizunguzungu tu kutokana na mapenzi. ” Alvin alicheka. Kwa vile alikuwa na mafua, koo lake lilikuwa limetoka sauti zaidi.

Koo la Lisa likamkaba. “Sawa, hizo dawa hazina hesabu, sawa? Ninataka tu kukukumbusha kwamba huwezi kumeza dawa hovyohovyo tu. Ikiwa unakohoa, unapaswa kuchukua dawa ya kikohozi. Kwanini ulichukua dawa zote bila mpangilio? Unafikiri unakunywa Coke au supu ya maharage?"

"Lisa, najua kuwa dawa haziwezi kunywewa tu. Lakini... ni mara ya kwanza ulininunulia dawa. Sikutarajia kwamba ningeweza kupata matibabu haya katika maisha haya yote. Ninahisi kama ndoto." Alvin alisema ghafla, “Ninapotumia dawa unazonipa, moyo wangu huhisi mtamu sana hivi kwamba unakaribia kuyeyuka.”

“Inatosha.” Lisa alikaribia kushindwa na Alvin. "Nitanunua chakula cha mchana baadaye na kiletwe hapo. Angalau haitakuwa kosa langu ikiwa utapata shida kwa kula chakula kingi." Alikata simu baada ya kumaliza kuongea.

Ndani ya nusu saa, Alvinalipokea zawadi ya kifurushi cha chakula cha mchana kutoka kwenye hoteli kubwa ya nyota tano iliyokuwa karibu.
Alichukua picha kwa simu yake na kuiweka kwenye Facebook ili kuwajulisha kila mtu kuhusu luch hiyo. [Lunch box tamu niliyotolewa na mtu fulani. Ooh! Ni tamu sana! Asante sana @LisaJones]

Wanamtandao ambao mwanzo walikuwa wakimtukana Lisa, walienda kwenye posti yake na kuanza kumlaani papo hapo.

[Hana aibu! Ulishikana na mke wa mtu mwingine, na bado unathubutu kuonyesha ma-lovey-dovey hadharani?]

[Ndugu, amka. Lisa si mwanamke mzuri. Hata alikuwa na uhusiano usio na utata na Ethan.]

[Je Lisa alikuroga? Hukuwa hivi zamani.]

[Wewe na Lisa mnapaswa kufa tu.]


Alvin aliwaacha tu wamlaani vile walivyotaka. Hakujali hata kidogo. Kitu pekee alichojali ni lunch iliyokuwa mbele yake.

•••
Kwa upande mwingine, Lisa alipokuwa akifanya kazi, ghafla alipokea simu kutoka kwa Pamela. Sauti ya Pamela ilikuwa na utata.

“Ah, unaendelea haraka sana na Alvin, eh? Sisi bado dada? Hata hukuniambia.”

“Nikuambie nini?” Lisa alishangaa.

“Haya, acha kujifanya. Kila mtu anajua kwamba ulimpa Alvin lunch mchana huu. Tena anasifia ni kitamu kabisa. Nataka unitumie na mimi pia. Labda ni kwa sababu nina mimba, lakini kila kitu kinanipendeza kwa sasa,” Pamela alisema huku akitabasamu.

“Umejuaje kuhusu hili?”

"Alvin aliichapisha kwenye page yake ya Facebook." Pamela alishangaa. “Ulikuwa hujui?”

Lisa alifungua Facebook yake na kutazama. Hakuwa na la kusema. Ilibidi kweli ampe salute Alvin. Ulikuwa wakati mgumu, lakini bado alionyesha mapenzi yake mtandaoni bila woga.

Lisa alimweleza Pamela sababu. Pamela alicheka na kusema, "Alvin ni mtoto sana."
"Ndio, yeye ni mtoto kama Suzie." Lisa alicheka kwa uchungu.

“Lakini ni lini utatoa ushahidi? Wanamtandao wanakulaani tena. Inaonekana sasa wana wazimu zaidi kuliko mara ya mwisho."

"Jioni hii.” Lisa alijibu. “Kelvin na Sonya wanaweka juhudi nyingi katika kuigiza. Tusiwafichue haraka,” Lisa alisema huku akitabasamu.

"Basi nitasubiri kwa hamu."

Sura ya: 641

Ilikuwa saa kumi na moja jioni ambapo Lisa alipakia habari alizokuwa ametayarisha kwenye mtandao. Alishambulia mara moja habari iliyotolewa na Kelvin hapo kabla.

[Nilisikia kwamba mtu fulani alipoteza figo ili kuniokoa mimi. Ninataka tu kujua kwamba tangu upoteze figo miaka mitatu iliyopita, kwa nini CT scan ya hivi majuzi kutoka hospitali ilionyesha kuwa figo zako mbili ziko sawa kabisa? Ulipoenda kuchunguzwa mwili kwa siri katika miaka hii mitatu, figo zako zote zilikuwa sawa. Kwanini ulihamisha kiasi kikubwa cha pesa kwa daktari huko Dar es Salaam ambaye aliniambia wakati huo kwamba ulipoteza figo?

[Unadhani unaweza kuendelea kuuhadaa umma kwani ulifanikiwa kunihadaa kwa miaka mitatu? Ninataka tu kusema kwamba umeweka show nzuri. Ungefanya kana kwamba mwili wako haukuwa sawa mbele yangu kila wakati na kunifanya nijisikie hatia. Kwa kweli, mwili wako una afya bora kuliko wangu. Ujuzi wako wa kupigana ni bora zaidi kuliko wangu pia. Kofi kutoka kwako linaweza hata kufanya nusu ya uso wangu kuvimba.
[Haikuwa mara ya kwanza kunipiga hivyo. Mara ya mwisho ulinipiga kofi uliniomba msamaha huku unalia. Nilikusamehe, lakini nilipata kipigo kikali mara ya pili.

[Kelvin, acha kujifanya. Ikiwa singekuwa nafikiria kwamba ulipoteza figo kwa ajili yangu wakati huo, nisingejisikia hatia na kujilazimisha kukukubali tena na tena. Imethibitishwa kuwa upendo haupatikani kwa kukokotoa, kula njama na kudanganya.

[Usinishirikishe katika matendo yako potovu na maovu. Si jambo langu. Ulikuwa mtu mbaya tangu mwanzo. Kwa upande mwingine, nadhani nina bahati mbaya sana. Je! ni dhambi gani niliyotenda katika maisha yangu ya awali hata nikatokea kuangukia moyoni mwa mtu mwovu kama wewe?

[Zaidi ya hayo, Madam Sonya Mushi, ninabeba jukumu la kifo cha mwanao. Ni kwa sababu alimuona Kelvin akiwa na mahusiano ya kimapenzi na sekretari wake siku hiyo. Alitaka kunitafuta ili kunionya juu yake. Hata hivyo, kabla hajafika kwenye kampuni yangu, alipata ajali njiani.

[Kwa nini najua haya yote? Maana Ethan alinitumia ujumbe dakika chache kabla ya ajali kutokea. Aliniambia niwe makini na Kelvin. Kuanzia siku hiyo na kuendelea, nilianza kumchunguza Kelvin kwa siri.

[Namshukuru sana Ethan. Kama asingejaribu kunionya kuhusu maisha yangu, bado ningedanganywa na Kelvin hadi sasa.

[Wakati huo huo, ninatumai kila mtu ataacha kuongea vibaya kuhusu Ethan. Yeye hayuko hai tena. Maneno ya kashfa ya kila mtu yanaumiza mjane wake.

[Tulikuwa tunachumbiana, lakini tuliachana kwa amani miaka minne iliyopita. Alikuwa mchumba wangu wa utotoni na yeye akawa rafiki yangu mkubwa baadaye. Hatuna cha kuficha.

[Hii ni mara ya mwisho nitatoa taarifa kuhusu jambo hili. Sitatoa sauti tena katika siku zijazo. Natamani tu kupata talaka yangu kutoka kwa Kelvin sasa.]


Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Lisa kutoa taarifa ndefu kama hiyo. Kila mtu alifikiri kwamba Lisa hangeweza kubadilisha hali hiyo. Hawakutarajia kwamba angeanzisha shambulio kali zaidi. Hata alivua nguo ya mwisho ya Kelvin.

Wanamtandao walivamia chapisho lake kama nzige. [Je, CT scan inaweza kuwa bandia?]

[Bandia? Huoni muhuri wa muda katika nyeusi na nyeupe? Imeelezwa wazi.]

[Mimi ni daktari kitaaluma. Hiyo CT scan inapaswa kuwa kweli. Muhuri wa muda na jina la mgonjwa vyote vimo. Ni ngumu kudanganya. Matokeo ya ukaguzi wa mwili yanaonekana halisi kulingana na muhuri pia. Madaktari wengine hawana maadili yoyote. Nadhani Kelvin amekuwa akiigiza kwa muda mrefu sana hata akatuhadaa kuwa ana figo moja tu.]

[Kelvin ndiye bosi mkuu wa kampuni ya madawa ya binadamu. Kwa kweli ni rahisi sana kwake kuhonga daktari.]

[Hivyo Kelvin alijifanya kuwa alipoteza figo kwa ajili ya Lisa ili kumdanganya na kumfanya ajisikie mwenye hatia. F*ck, huyu ni mtu wa aina gani? Anajidai sana. Nilitazama video yake akilia leo asubuhi eti alipoteza figo wakati akimuokoa Lisa. Inachukiza sana.]

[Ni rahisi kuelewa. Kelvin kuwa na uhusiano wa kimapenzi na katibu muhtasi wake ni ukweli thabiti. Anataka kutumia suala la figo yake kwa usaliti wa kihisia. Kwa kushangaza, Lisa alikuwa tayari amechunguza kila kitu kwa siri. Lisa alifanya vizuri. Ni kofi zuri kwenye uso wa Kelvin.]
[Hapana, nadhani hoja ni kwamba si mara ya kwanza Kelvin kufanya unyanyasaji wa nyumbani. Nilisema hapo awali kuwa amepotoshwa kiakili. Nyinyi hamkuniamini.]

[Nina shaka kali. Ethan alituma ujumbe kumuonya Lisa kuhusu Kelvin kabla hajafa. Je, kifo cha Ethan kilisababishwa na Kelvin kwa sababu alitaka kumnyamazisha?]

[Uliyetoa maoni hapo juu, lazima uwe wazimu. Ethan ni mpwa wa damu wa Kelvin Hakuhitaji kwenda mbali sana kumuua Ethan ili kumnyamazisha kwa jambo kama hilo.]

Mawazo ya wanamtandao yalizidi kuwa mabaya na zaidi. Lisa alifurahi sana kuona hivyo. Alifikiri kwamba pengine Kelvin angetaka kutapika damu wakati huo. Haha, angeona kama angeendelea kujifanya katika siku zijazo.

Mwanaume aliyekua akilia huku akitubu mbele ya waandishi wa habari... Hakuamini kuwa Kelvin atakuwa na uso wa kujifanya hivyo.

Lisa alipokaribia kutoka kazini, ghafla alipokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu. Kama ingekuwa hapo awali, asingepokea simu kutoka kwa wageni. Lakini siku hiyo…

Pembe za mdomo wa Lisa ziliinuliwa. Karipio la hasira la Sonya lilitoka kwenye simu. “Lisa Jones, siamini ulichosema ni kweli. Kelvin ni kaka yangu mzazi. Angewezaje kufanya kitu ambacho kingeweza kumuumiza Ethan? Wewe b* tch, unataka kuweka mizozo kati yetu kimakusudi?”

“Anti Sonya, kama huamini katika mambo niliyoweka kwenye mtandao, kwanini unanipigia simu?” Lisa alikanusha kwa utulivu na tabasamu.

Sonya alisita kwa muda. Kisha, akasema kwa ukali, “Unamtungia Kelvin kimakusudi, sivyo? Ulisema Ethan alikutumia ujumbe kabla hajafa, lakini nilikuwa nimeangalia simu yake hapo awali. Hakuna rekodi zake hata kidogo."
“Labda aliifuta mara baada ya kuituma. Fikiria, je, angethubutu kuweka kitu muhimu kama hicho kwenye simu yake baada ya kuituma?” Sauti ya Lisailipungua sana. “Aunty Sonya, najua hunipendi. Lakini hata iweje, nilikua na Ethan tangu tukiwa wadogo. Tumefahamiana tangu shule ya awali. Ingawa mambo mengi yalitokea baadaye, urafiki wetu wa utotoni hauwezi kufutwa. Nimesikitishwa na kifo chake pia. Zaidi ya hayo... Nimekasirishwa na jinsi kifo chake kilivyokuwa kibaya.”

Kuelekea mwisho, koo lake lilikuwa limetulia kidogo. Alikuwa amekasirika kweli.

Sonya alikasirika. “Haiwezekani. Kelvin hatawahi kufanya jambo kama hilo.”

“Anti Sonya, ngoja nikuulize hivi. Je, Kelvin ana sura ya kiungwana moyoni mwako?” Lisa alijibu. “Ulifikiri alikuwa ananipenda sana? Ulijua kuhusu uhusiano wake na Regina?"

Sonya alishangazwa na maswali yake. Hakika alifikiri kwamba Kelvin alikuwa akimpenda sana Lisa. Alikuwa amemshauri aache naye hapo awali. Haikuwa kama hakuna wanawake wengine duniani. Lakini, Kelvin kila wakati alionekana kana kwamba mwanamke aliye kando yake lazima awe Lisa na Lisa pekee.

Sonya alikuwa ametazama video hiyo pia. Kusema kweli, alishangaa, lakini hiyo haikuwa tabia ya wanaume wengi? Kama tu babake Ethan—hata alikuwa na mtoto wa nje ya ndoa.

Lisa aliendelea kuuliza, "Je, unajua kwamba hakuwahi kupoteza figo kwa ajili yangu?"

Sonya na familia yake wote walifikiri kwamba Kelvin alipoteza figo kwelikweli.
Alipoona Sonya yuko kimya, Lisa alicheka. “Ina maana humuelewi kabisa kaka yako wa damu. Basi kwa misingi gani unaweza kusema kwamba hatamuumiza Ethan?”

“Unaweza kunionyesha ujumbe ambao Ethan alikutumia kabla hajafa?” Sonya aliuliza kwa ukali.

“Samahani, siwezi.” Lisa alikataa.

Sonya alidhihaki, “Unanichukulia kama mjinga? Baada ya yote uliyosema, huna ushahidi hata kidogo. Unaichokoza familia ya Mushi makusudi.”

“Ushahidi nilio nao nikikuonyesha nahofia nitakuwa nimekuingiza matatani bure,” Lisa alisema ghafla.

"Unamaanisha nini?" Sonya alipigwa na butwaa.

“Umewahi kufikiria Kelvin anaweza kukufanya nini baada ya kujua kwamba unamshuku? Umewasiliana nami baada ya kuona chapisho langu la Facebook, Je, hakuna mtu yeyote anayekutazama kutoka gizani? Kelvin atakufanya nini kama atajua kuwa umewasiliana na mimi na kupata ushahidi? Ikiwa kifo cha Ethan kilisababishwa na Kelvin, basi unafikiri wewe, dada msumbufu, una umuhimu gani machoni pake?” Lisa alisema kwa sauti ya chini, “Hakuna ubaya naomba uwe makini. Sitaki tu kukuburuta kwenye fujo hii. Wewe ni mtu mzuri.” Alikata simu baada ya kumaliza kuongea.

Lisa alikuwa amesema kwamba Ethan alimtumia ujumbe kabla hajapata ajali lakini ni kwa sababu tu hakuweza kumjulisha Kelvin kwamba ni Tracy ndiye aliyemwambia ukweli. Vinginevyo, Tracy angedhurika. Hata hivyo, ikiwa asingesema, Sonya angejuaje ukweli? Je, familia ya Mushi ingekuwa katika fujo? Isitoshe, kama mama, Sonya alikuwa na haki ya kulipiza kisasi kwa mtoto wake......ITAENDELEA......

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA...