JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................584-585
Sura ya: 584
“Ethan wangu alikuwa handsome, lakini alipokufa hatukuona sura yake wala mifupa, amegeuka majivu tu!” Sonya alilia kwa uchungu sana.
Lisa alichanganyikiwa kabisa. Kwanini watu wenye afya njema walikuwa wanatoweka ghafla? Kwanza ilikuwa Jack Kimaro, na sasa ni Etnah Lowe? Ingawa hakumpenda tena Ethan, alikuwa ni kipenzi chake walipokuwa wadogo, aliwahi kumpenda na kumchukia pia hapo mwanzo, lakini hakumchukia kiasi cha kutamani afe kifo cha mateso kiasi hicho. Na ingawa wote walikuwa kwenye ndoa, bado alimjali. Aliposikia kuhusu habari za kifo chake, kila kitu mbele ya macho ya Lisa kilififia kwa ukungu.
Wakati mikono ya walinzi waliomshika Sonya ilipolegea kidogo, alichukua tena kisu na kujaribu kumchoma tena Lisa.
“Kuwa mwangalifu, Lisa!” Mwanamume mrefu alijitosa ghafla na kumsukumia Lisa pembeni.
Sonya alipoona kwamba mwanamume huyo aliyemwokoa Lisa ni Alvin, alilalamika, “Lisa, ona jinsi ulivyo malaya. Wewe ni mke wa Kelvin, lakini bado hujaachana na wanaume zako wa zamani, unakumbatiwa mbele ya watu na Alvin, na ulikuwa unamtongoza Ethan hadi ukamsababishia ajali. Hufai duniani wala mbinguni malaya mkubwa wewe.”
Uso angavu wa Alvin ukasinyaa ghafla wakati anamsogelea Sonya. Alikipokonya kisu kutoka kwenye mkono wa Sonya taratibuna kumkabidhi Sonya kwa polisi ambaye ndiye kwanza alikuwa amewasili eneo la tukio. ”Mwanamke huyu alikuwa anajaribu kumuua mtu, kwa hiyo, ni bora mkamfunga pingu kwanza.”
Sonya alichanganyikiwa alipofungwa pingu na polisi na kuanza kulia, “bado sijamzika mwanangu, lazima nimsindikize kwenye safari yake ya mwisho.”
Lisa alishindwa kuvumilia na akajongea mbele ya polisi, “ingawa alijaribu kuniua, sina haja ya kufungua mashitaka yoyote. Najua hakufanya makusudi pia, amepoteza kijana wake na lazima awe katika hali ya kuchanganyikiwa.”
Polisi walitazamana na mmoja kati yao akasema, “kosa ni kosa tu, mradi kavunja sheria, lazima twende naye kituoni. Tutamhoji na akikili kosa lake na kuahidi kutorudia tena, basi tutamuachia.” Kwa hayo, Polisi wakaondoka na Sonya.
Lisa alihangaika wakati akielekea eneo la maegesho huku akimpigia Kelvin, “nasikia kuna kitu kimemtokea Ethan?”
“Ndiyo,” Kelvin alijibu kwa sauti ya uchovu, “tunaandaa mazishi sasa. Mambo mengi sana yametokea leo kwa hivyo nilisahau kukuambia.”
“Ninakuja sasa hivi.”
Lisa alikuwa karibu kufungua mlango na kuondoka lakini mkono wenye nguvu ulimshika na kumzuia kwa nyuma. “Huwezi kuendesha katika hali kama hii, unaenda wapi? Nitakupeleka.” Alvin alimwangalia kwa wasiwasi sana. Ingawa alifika kwa kuchelewa, aliweza kupata picha ya kitu kilichokuwa kikiendelea.
“Hakuna haja, nitakwenda mwenyewe.” Lisa alipuuza msaada wake na kumsukumia mbali kwa nguvu.
Akini Alvin asingemruhusu kuondoka, kwa hiyo wakati anamvuta tena Lisa alijigonga mguu akaaunguka kimgongomngongo kifuani mwake. “Alvin, niache niende bwana, ondoka…”
Alvin hakutaka kumwachia na Lisa akaendelea kujikomboa kutoka kwenye kumbato lake kwa kumpiga viwiko vya mikono au vipepsi. Alipoona Alvin hataki tu kumwachia, Lisa alibidi aangue kilio. Alvin aliendelea kumkumbatia kwa nyuma, na Lisa akashusha jazba zake na kutulia. Hapo ndipo Alvin akamfuta machozi yake taratibu huku akimliwaza.
“Tulia kwanza, huna haraka ya kuwahi huko hata hivyo. Wewe si mchungaji unayekwenda kuongoza ibaada ya mazishi.”
“Ni makosa yangu, Alvin, alisema alitaka kuonana na mimi. Kwanini nilikubali? Pengine ningekataa huenda asingekufa.” Lisa alikilaza kichwa chake kwenye kifua cha Alvin huku akiongea kwa sauti ya huzuni sana.”
“Usijibebeshe lawama zisizostahili, wewe si malaika kwamba ungejua kitu kinachoenda kutokea. Kwa kuwa alikuwa anakuja kukuona yeye mwenyewe na hukumuita, huenda kulikuwa na jambo muhimu.”
Alvin aliweza kuhisi mapigo ya moyo wa Lisa yakikita kwa nguvu hadi nyuma ya mgongo wake, akazidisha kumbato lake na kumfanya Lisa atulie zaidi. Bila fahamu yake, Lisa alijihisi faraja isiyo kifani kutokana na kumbato hilo.
“Lakini sikupaswa kukutana na Ethan. Ikizingatiwa kuwa nimepitia naye mambo mengi, nilipaswa... niwe mbali naye.” Uso wa Lisa ulikuwa umejaa machozi. “Zaidi ya hayo, alinipigia simu asubuhi ya leo na hakutokea baadaye, lakini nilisahau kuhusu hilo. Nilipaswa kumuuliza…”
Alvin aliinamisha kichwa chake na kujifuta machozi kwa upole usoni mwake. “Hata ungemuuliza, usingeweza kubadilisha chochote.
Kitu kilikuwa tayari kimemtokea wakati huo. Aidha... Kwa hatua hii, nadhani hujui kabisa kwanini alikutana na ajali bado. Unapaswa kusubiri matokeo ya uchunguzi. Je, unapanga kutoa heshima zako za mwisho kwake? Acha nikupeleke kwenye chumba cha mazishi.”
"... sawa."
Kwa maneno yake ya upole na ya kufariji, Lisa alipata utulivu wake taratibu. Hakika ilibidi angalau ajue chanzo cha ajali ya Ethan.
“Nitakupeleka huko.” Alvin alimpeleka kwenye siti ya abiria na kumfunga mkanda.
Wakati wa safari, Lisa alitazama nje ya dirisha bila kusema neno. Kumbukumbu zake zote na Ethan zilikuwa zikipita kichwani mwake kama mkanda wa video uliorekodiwa. Kadiri alivyozidi kuzifikiria, ndivyo alivyohisi vibaya zaidi.
Baada tu ya kufika kwenye jumba la mazishi ndipo alimnong'oneza Alvin, “Afadhali urudi. Wanafamilia wa Mushi labda wako hapa, kwa hivyo inaweza kuwa haifai kwako kuhudhuria mazishi.
“Mm.” Alvin alimpitishia funguo za gari na kusema kwa upole, “Kama kuna chochote, unaweza kunipigia simu mara moja. Jitunze. Usiruhusu mtu yeyote akunyanyase.”
Lisa aliitikia kwa kichwa. Kutokana na akili yake ambayo ilikuwa imechanganyikiwa, hakuweza kuhangaika kufikiria kitu kingine chochote.
Mara tu alipoingia chumbani, aliona hali ya huzuni ya Kelvin. Bw. Zacharia Lowe alikuwa amekuja kutoka Dar es Salaam. Familia ya Lowe, familia ya Mushi, na familia ya Laizer wote walikuwepo na nyuso zao za huzuni.
Tracy Laizer alionekana amepauka kama kikaragosi asiye na roho. Mama yake alikuwa akijifuta machozi pembeni yake. “Mbona binti yangu ana bahati mbaya hivi? Mumewe ameondoka punde tu alipopata mimba.”
Lisa alishtuka huku akihisi maumivu yasiyoelezeka.
Bibi Laizer ghafla alimkimbilia Lisa ili kumpiga kofi mara tu alipomwona. "Ni kazi yako! Ikiwa Ethan asingeenda kukutafuta, asingekufa.”
Lisa aliruhusu kofi lile limtue usoni bila kukusudia kulikwepa. Hata hivyo, Bi. Laizer alipokuwa karibu kumpiga kofi Lisa, Kelvin alimkimbilia mwanamke huyo na kumzuia. Kisha akaropoka, “Kwa nini nyie mnamlaumu? Polisi waligundua kwamba kulikuwa na matatizo na gari, hivyo fundi aliyetengeneza gari anapaswa kuwajibika badala yake.”
"Kulikuwa na shida na gari?" Lisa aliuliza huku akiwa ameduwaa.
“Ndio. Kamera ya uchunguzi ilionyesha kuwa gari lilipoteza udhibiti na kuongeza kasi katika sekunde kumi hkabla ya kupinduka." Kelvin alieleza, “Hata kama Ethan asingeenda kukutafuta, angeweza kwenda kukutana na mtu mwinginewe na shida kama hiyo ingeweza kutokea pia. Kwa kweli, gari hilo ambalo aliendesha lilikuwa jipya zaidi na lenye teknolojia ya kisasa. Baada ya kusema hivyo, kumekuwa na ajali nyingi zinazohusisha magari ya hali ya juu katika miaka miwili iliyopita.”
Sura ya majonzi ilitanda usoni mwa Lisa. Je, Ethan alipoteza maisha yake kwa sababu hiyo tu?
“Nini zaidi...” Kelvin akaongeza ghafla, “Angeweza kwenda kukutafuta kwa sababu yangu. Tulikuwa na mzozo jana usiku. Pengine alijua kwamba nilikuwa katika hali mbaya, hivyo alitaka kupatanisha mambo bila kuniruhusu kujua. Katika hali hii, lawama ziende kwangu badala yako.”
Baada ya Kelvin kujikanyaga, Lisa alikuwa na mwanga sasa. Haishangazi Ethan alisema alikuwa na jambo muhimu la kumwambia. Hata alikuwa amemwomba asimjulishe Kelvin kuhusu hilo.
Tracy aliinua kichwa chake na kumtazama Kelvin. Kwa sauti ya kishindo, alisema, “Ni sawa, Mama. Sina bahati tu, na vile vile Ethan. Tusimsingizie mtu yeyote.” Bi. Laizer alishusha pumzi.
Ingawa Bwana Zacharia Lowe alihuzunishwa sana na kifo cha mwanawe, bado alikuwa na mtoto mwingine wa nje wa kiume. Aidha, yeye hakutaka kuona Ethan na Kelvin wakitofautiana. Ikizingatiwa kuwa hali ya sasa ya Kelvin ilikuwa tofauti na hapo awali, Bw. Lowe alihitaji kujipendekeza kwake katika siku zijazo.
Kwa hayo, alisema, “Mzikeni Ethan haraka iwezekanavyo. Kumuona hivi... Najisikia kuumia sana moyoni.” Baba Ethan alitoa amri.
Sura ya: 585
Siku iliyofuata, shughuli ya mazishi ya Ethan ilifanyika. Lisa alimuona kwa mara ya mwisho. Ilikuwa ya kushangaza sana, lakini hakuwa na hofu. Hakuhisi chochote ila huzuni. Yule ambaye alikuwa akimwita 'kaka Ethan' tangu alipokuwa mdogo alikuwa ameondoka hivyo hivyo. Kwanini maisha ya mwanadamu yalikuwa dhaifu sana?
Baada ya Ethan kuzikwa, Lisa hakwenda ofisini kwa siku tatu mfululizo. Alikuwa kama kobe aliyejificha kwenye gamba lake, haendi popote.
Siku ya nne, ghafla alipokea simu isiyo ya kawaida. “Huyu ni Lisa? Mimi ni Tracy.”
“Bi Laizer...” Lisa aliishiwa nguvu. Alifikiri Tracy angemsababishia matatizo.
“Ningependa kukutana nawe. Tafadhali usimwambie mtu yeyote kuhusu hilo,” Tracy alisema chini ya pumzi.
Akiwa amepigwa na butwaa, Lisa akawa macho kisilika. Hata hivyo, mara tu aliposikia Tracy akitaja kwamba wangekutana katikati ya jiji, aliondoa mashaka yake.
Punde, aliendesha gari hadi kwenye cafe moja maarufu katikati ya jiji na akaingia kwenye chumba cha kibinafsi. Tracy alikuwa amekaa mezani. Alikuwa amevaa miwani ya jua na kofia. Kwa vile alikuwa amekata nywele zake fupi na vipodozi vizito usoni mwake, Lisa hakuweza kumtambua.
"Kwanini ulitaka kukutana nami?" Lisa aliketi kinyume chake. Siku zote alikuwa akimfikiria Tracy kuwa mwanamke mtulivu, lakini alihisi kwamba Tracy hakuwa mtu wa kudharauliwa. Licha ya kujua kwamba Lisa hapo awali alikuwa kwenye uhusiano na Ethan, Tracy hakuwahi kumuonea wivu wala hakuungana na Sonya kumsema vibaya.
"Tazama hii." Tracy alipitisha simu yake kwa Lisa.
Lisa akabonyeza kuufungua. Ilikuwa ni picha ya skrini ya ujumbe ambao ulikuwa haujatumwa. [Jihadharini...]
Mtu angeweza kusema kuwa ulikuwa ujumbe usiokamilika kwani neno 'Mu… ' lingeweza kuonekana kwenye kisanduku cha ujumbe kilicho chini.
Rasimu ya ujumbe huo ilikusudiwa kwa Lisa.
“Hii ilikuwa meseji ya mwisho ya Ethan kupatikana kwenye simu yake. Polisi waliiona simu hiyo msituni baada ya tukio hilo, lakini hawakujua neno la siri la simu yake. Baada ya kupata simu yake, niliiwasha na kuifungua. Picha hii ya skrini ilionyeshwa kwenye skrini." Tracy alimtazama kwa hisia tofauti. "Nadhani Ethan anaweza kuwa anajua kitu wakati wa tukio hilo. Angeweza kutambua kwamba angekufa, kwa hiyo alitaka kukutumia ujumbe ili kukuonya kwa mara ya mwisho. Lakini ilikuwa ni kuchelewa sana gari lilipoanza kuwaka moto. Kwa hivyo, alitupa simu yake nje ya dirisha.”
Mapigo marefu ya Lisa yalitetemeka. Je, hii ilimaanisha kwamba Ethan alikuwa akijaribu kumkumbusha hata katika dakika zake za mwisho?
"Kwanini ni picha ya skrini, na si meseji?" Lisa aliuliza ghafla, "Naweza kutazama simu yake?"
Tracy alijibu kwa kufikiria, “Baada ya simu ya Ethan kupitishwa kwa polisi, familia ya Lowe na familia ya Mushi waliiangalia pia. Lakini nilikuwa wa kwanza kuitazama. Baada ya kuona ujumbe ulioandaliwa, niliskrinishoot na kutuma picha ya skrini kwenye simu yangu na kuiondoa kwenye simu yake.”
Lisa alishtuka. Tracy aliunganisha mikono yake pamoja. “Umefikiria kuhusu sababu iliyomfanya Ethan kutaka kukutumia ujumbe huu katika dakika yake ya mwisho badala ya maneno yake ya mwisho kuhusiana na mambo mengine? Alitaka uwe makini na nini? Au alikuwa anakutafuta jana kwa sababu ya jambo gani?”
"Sijui." Akiogopa kwamba Tracy angefikiria kupita kiasi, Lisa alieleza kwa haraka, “Sijamwona Ethan tangu wakati wa harusi yangu. Alipowasiliana nami ghafla siku hiyo, nilishangaa sana. Lakini kulingana na Kelvin, pengine ilikuwa ni kwa sababu niligombana na Kelvin siku moja kabla ya tukio, huenda Ethan alitaka kupatanisha mambo kwa ajili yetu.”
Alipomaliza kuongea, alikaza macho yake kwenye skrini. Jihadharini...Jihadharini na nani? Ethan alikuwa ameandika mtu ambaye jina lake lilianza na 'Mu'. Hii ilimaanisha kuwa jina la mtu huyo lilikuwa na herufi hizi tatu. Wazo likamjia kichwani Lisa. Je, Ethan alikuwa amejaribu kuandika 'Kelvin Mushi'? Uso wake ulipauka.
Alipoona jinsi alivyo, Tracy alisema, "Inaonekana kama umekisia."
"Hapana. Hili haliwezekani. ” Lisa akatikisa kichwa. Je, Ethan angewezaje kutaka kumkumbusha kumchunga Kelvin katika nyakati zake za mwisho?
Tracy alisema, “ Kwa kuwa Ethan aliandika 'Mu', inamaanisha kwamba unapaswa kuwa mwangalifu na watu ambao majina yao yanaanza na hii. Katika dakika zake za mwisho, angeweza hata kuandika Mjomba Kelvin. Kwa hivyo sasa unajua kwanini nililazimika kufuta ujumbe huo."
Lisa alielewa. Alimtazama Tracy kwa kupendeza na kwa hisia ngumu kwa wakati mmoja. Kwa mara ya kwanza, Lisa alimwona mwanamke huyu kuwa mwenye akili na mzuri. Labda Tracy alikuwa mkimya sana, kwa hivyo Lisa hakuwahi kumjali kabla ya hii.
“Je, hunichukii?” Lisa aliuliza ghafla. “Sonya anatamani angenichuna ngozi nikiwa hai. Ethan aliuawa katika ajali alipokuwa njiani kunitafuta. Kwa sababu yangu, mtoto wako alimpoteza baba yake. ”
"Bila shaka, nakuchukia." Sura ya uchungu ilivuka uso wa Tracy. “Baada ya kusema hivyo, Ethan aliniambia kwa uwazi kwamba amekukosea sana. Alikuumiza na kukuacha. Alihisi kuwa ana deni kwako. Pia alijiita mtu wa kudharauliwa kwa sababu aliungana nami kwa ajili ya faida. Lakini kwa vile alinioa, aliniambia atanitendea mema na hatanisaliti. Ingawa ulikuwa mchumba ndani ya kina cha moyo wake, sijawahi kukuonea wivu. Baadhi ya watu wanaweza kumiliki mapenzi na kuyanyang’anya, lakini nilichotaka ni kubaki karibu naye.”
Lisa alishtuka. Ilibidi akubali kwamba Tracy alikuwa mwanamke mwenye mawazo mapana. Ilistaajabisha kwamba Ethan alikutana na mwanamke kama Tracy licha ya kujihusisha na Lina, mwanamke yule mwovu.
Tracy aliongeza, “Pia, ninaamini kwamba Ethan angeniachia maneno yake ya kufa katika dakika zake za mwisho kama isingekuwa jambo muhimu sana. Ninakuambia kuhusu hili kwa sababu nataka utimize matakwa ya mwisho ya Ethan.” Tracy alitabasamu huku akifikia mwisho wa sentensi yake. Macho yake yalikuwa mekundu taratibu.
“Samahani,” Lisa aliomba msamaha kwa huzuni kubwa.
“Si lazima ujute. Nadhani jambo la muhimu zaidi hapa ni kwamba kifo cha Ethan kinaweza kisiwe ajali bali ni kitendo cha kukusudia.” Tracy alimwambia habari nyingine ya kushangaza. “Niliwaomba polisi kuangalia picha ya mwisho ya ajali ya Ethan. Ilithibitisha kuwa ujumbe huo uliandikwa sekunde 20 au zaidi baada ya gari kuanguka. Je, huoni ni ajabu? Kwanini alijaribu kukutumia ujumbe baada ya jambo fulani kumtokea na si hapo awali? Je! ni kwa sababu aligundua kitu baada ya ajali?"
"Unasema kwamba aligundua mtu alitaka kumuua baada ya ajali?" Lisa alishtuka kwa hofu. "Lakini haikusababishwa na hitilafu kwenye gari?"
“Baadhi ya makosa yanasababishwa na wanadamu,” Tracy alinong’ona, “.
Fikiri kwa makini kuhusu mazungumzo uliyofanya na Ethan. Alisema jambo lisilo la kawaida?"
“Alisema alikuwa na jambo muhimu la kuniambia, lakini akaniomba nisimjulishe Kelvin...” Lisa alipokuwa akitafakari jambo hilo, alijihisi baridi sana.
Baada ya kusikia hivyo, Tracy alinyamaza kwa muda mrefu kabla hajainuka. “Je, kweli alikuwa anakutafuta ili kupatanisha mgogoro kati yako na Kelvin? Hakuna anayejua ukweli, lakini jambo pekee ambalo tuna uhakika nalo ni kwamba alikuwa ameendesha gari kutoka ofisini wakati huo. Nadhani unapaswa kuwa makini. Ni vyema kutomjulisha mtu yeyote kwamba nilikutana nawe leo.”......ITAENDELEA......
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA..
