JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................576-577

Sura ya: 576

Mawenzi Investiments.

Baada ya Lisa kumaliza kazi yake, ghafla alikumbuka kwamba alipokea missed call kutoka kwa Hans mwishoni mwa mkutano.
Alikuwa na shughuli nyingi sana wakati huo hata akasahau kumpigia simu tena.

Mara moja akampigia simu. "Hans, kuna kitu gani kimetokea huko?"

"Ndio, kuna jambo kubwa." Hans alitazama kwa siri sura ya Alvin aliyekuwa anaondoka. Hatua zake sasa zilikuwa za kusisimua na za haraka, na alikuwa katika hali nzuri sana.

Lisa alikuwa na hisia mbaya juu yake. Alvin alikuwa akitapatapa alipoondoka mchana huo. Je, alichukulia maneno yake kwa undani sana? “Fanya haraka uniambie.”

"Bwana Mkubwa tayari anajua kuwa Lucas na Suzie ni watoto wake." Hans alieleza kwa hatia, “Sijui jinsi alivyogundua, lakini alinipigia simu ghafla kuniuliza ikiwa nilimpa daktari hongo wakati huo na ikiwa kweli hukuwa na mimba. Alionekana kuwa ametambua jambo fulani, kwa hiyo sikuwa na chaguo ila kukiri.”

Lisa alidanganya na kusema kwamba Lucas alikuwa mtoto wa Kelvin na wake. Uongo huo ulifichuliwaje haraka hivyo? Ilikuwa ni masaa machache tu. Lisa karibu ateme damu. “Alikuuliza saa ngapi mchana?”

“Karibu saa nane mchana.”

Hiyo ilimaanisha kuwa haukupita muda mrefu baada ya kuondoka ofisini kwake. Aligunduaje kuwa Lucas alikuwa mtoto wake haraka hivyo?

Uso mzuri wa Lisa ukaingia giza. “Hakujua kabisa. Ndiyo, anajua kuwepo kwa Lucas, lakini anadhani mtoto ni wa Kelvin na mimi. Pengine alikuambia hivyo tu kwa sababu hakuweza kukubali ukweli huo, lakini wewe… ulimwambia ukweli kwa bahati mbaya.”

“Ndiyo hivyo?” Hans alipigwa na butwaa akiwa hoi. Ina maana alidanganywa?

“Hakika.” Lisa naye alijihisi mnyonge.

Mwanzoni, alifikiri angeweza kumfanya akate tamaa kabisa ikiwa angejua kwamba alikuwa na mtoto na Kelvin, lakini sasa, Alvin alikuwa amegundua watoto wote wawili ni wake. Ingekuwa ngumu zaidi kujiondoa kutoka kwake sasa. Alikuwa na hisia kwamba kuanzia wakati huo, Alvin angemng’ang’ania zaidi kuliko ruba.

"Samahani, Bi Jones." Hans alitaka kupiga mdomo wake. "Lakini Bwana Mkubwa alisema kwamba hatachukua watoto kutoka kwako."

“Ndiyo, hataninyang’anya watoto. Atanichukua pamoja na watoto. ” Lisa alisema kwa huzuni.


Hans alikosa la kusema. “Sasa Alvin ameenda wapi?”

"Aliondoka tu baada ya mkutano. Nadhani ataenda shule ya chekechea,” Hans alisema kwa upole.

“Sawa. Ni lazima niende pia.”

Lisa hakuwa katika hali ya kuendelea na mazungumzo. Baada ya kukata simu, haraka aliendesha gari hadi shule ya chekechea. Alvin alifika mapema kidogo kuliko yeye.
Saa kumi na nusu jioni, baadhi ya wazazi walikuwa tayari wameanza kuwachukua watoto wao. Sura nzuri ya Alvin ilijitokeza kati ya kundi la wanamama, na kumfanya aonekane haswa.
Mlinzi pale mlangoni alimfahamu na mara moja akamwambia mwalimu wa chekechea atoke na Suzie.

"Anko, wewe umekuja mapema sana leo." Suzie akaruka hadi kwake.

Alvin alimtazama kwa msisimko na sura ngumu machoni mwake. Ilikuwa sawa kwani hapo awali hakujua, lakini sasa alipojua kuwa ni binti yake, moyo wake ulianza kumwenda mbio. Hakika Mungu alimtendea mema Alvin. Licha ya kufanya mambo mengi ya kikatili, bado Mungu alimwachia jozi ya watoto wake wa kupendeza. Kadiri alivyozidi kuwaza juu yake, ndivyo machozi yalivyozidi kumtoka.

"Anko, una shida gani?" Suzie alihisi kuchoshwa na sura yake.

Alvin alichuchumaa na kupepesa paji la uso wake taratibu. Kisha, akasema kwa upole, "Binti mdogo mjanja."

Suzie aligusa paji la uso wake bila hatia. “Anko unazungumzia nini? mimi si mjanja. Mimi ni malaika.”

Alvin alicheka kwa sauti ya chini na kutabasamu sana. Macho yake yalikuwa yakipepesa kana kwamba kulikuwa na nyota ndani yake.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Suzie kuona tabasamu angavu namna hii kwenye uso wake mzuri, akapigwa na butwaa.

Alvin alinyoosha mkono tena kumbana uso wake mdogo. "Ulikuwa unajua wakati wote huo kuwa mimi ni baba yako?"

Akifikiria juu yake sasa, msichana yule mdogo alisema uwongo wa kila aina. Ingawa mara nyingi alijichanganya na kumuita Lisa ‘mama’, haikuwezekana kwamba hakujua kuwa Alvin ni baba yake.
Lakini, kila wakati alimficha na kumwita Anko. Alikuwa mtoto gani kama si mjanja?
Akiwa amepigwa na butwaa, macho ya Suzie ya duara na meusi yalimtoka. Siku zote alikuwa mwerevu na mjanja, lakini sasa alipigwa na butwaa kabisa.
Hakuelewa ni jinsi gani baba yake mchafu alikuwa amejua kuhusu siri hii ya kushtua.

“Mama yako aliniambia.” Alvin alitazama sura yake na kuanza kusema uongo tena.

“Mama ni mbaya sana…” Suzie alikanyaga miguu yake. "Kwanini hakuniambia mapema."

Ndani kabisa, Alvin alihema. Akifikiria mambo yote ya kusikitisha ambayo msichana huyu mdogo alikuwa amemwambia kuhusu mama yake, na alikuwa akiaminika kama malkia wa kuigiza. Lakini, ilikuwa bahati kwamba binti yake alikuwa na tabia hii. Msichana mjanja hatadhulumiwa na wengine. Ni yeye tu angedhulumu wengine.

"Niambie, kama ulijua kuwa mimi ni baba yako, kwanini hukunitambua?" Alvin alimtazama huku akiumia kidogo. "Afadhali umwite Jack baba yako lakini ukatae kuniita mimi hivyo?"

Suzie alimkazia macho bila kusita.“ Tafadhali, baba mchafu, fikiria mambo yote ya kihuni ambayo umemfanyia mama. Ikiwa sivyo kwamba Bibi aliniona nilipokuwa hospitalini kwa jeraha la kichwa, nisingefikiria kwenda kwa familia ya Kimaro hata kidogo.”

Uso mzuri wa Alvin ulibadilika. Alikumbuka kwamba kichwa chake kilijeruhiwa wakati alipokutana naye mara ya kwanza. "Je, haukuumiza kichwa chako kutokana na kuanguka kwa bahati mbaya?"

“Hapana, kuna watu walivamia nyumbani kwa Mama na kuvunjavunja vitu. Baada ya watu hao kuondoka niliogopa sana hadi nikaangukia vipande vya chupa na kufanya kichwa changu kuvuja damu.”
Suzie alimkazia macho kwa chuki. "Mama alisema kwamba mtu aliyesababisha uvamizi huo ni mtu wako wa karibu. Nilikuchukia sana wakati ule. Una macho mabaya."

Kadri Alvin alivyozidi kusikiliza ndivyo alivyoshtuka na kuona aibu. Alijua kwamba Thomas alivunja na kuharibu nyumba ya Lisa. Asubuhi hiyo, Lisa aliendesha gari ndani ya jumba lake la kifaharii kwa hasira na akaruka
kutaka kumfundisha Sarah somo. Hata hivyo, Alvin alimlinda Sarah. Ilibainika kuwa Thomas alikuwa ameharibu nyumba ya Lisa na kumjeruhi Suzie kichwani. Akiwa baba, si tu kwamba alishindwa kumlinda mtoto wake, bali pia aliunga mkono mhalifu. Uso wa Alvin uliwaka kwa aibu.

“Suzie, samahani. Ni kosa la Baba.” Alvin akamshika mkono wake mdogo na kumpigapiga usoni.

Suzie alidhihaki. “Bado ulimchukulia mwanamke huyo Sara kama mkeo mzuri na ulitaka kumuoa. Nimekuchukia kabisa baba.”

“Kwa hiyo… Lucas pia amekata tamaa juu yangu?” Alvin alisuliza kwa huzuni.

Suzie aliingiwa na hofu ghafla. "Oh, hata unajua Lucas ni nani?"

“Ndiyo. Suzie, ni sawa usiponikubali, lakini huwezi kunizuia kusafisha dhambi zangu,” Alvin alisema kwa upole. "Nipe nafasi. Nitakuwa baba mwema.”

Suzie akakunja midomo yake. “Siwezi kujizuia kwani naishi na wewe kila siku, lakini Lucas hatakupenda. Anakuchukia sana.”

Chuki? Neno hilo lilimuuma sana Alvin moyoni. Kwa hivyo, Lucas tayari alijua kuwa yeye ndiye baba yake.

Sura ya: 577

Wakati huo, alimuona mtu asiyemfahamu akiwa amemshika mkono Lucas akitoka nje ya shule ya chekechea. Alidhani kwamba mtu huyo alikuwa Sheldon Ngosha, mpwa wa Joel. Mara ya mwisho alipochunguza, Sheldon alisajiliwa kama babake Lucas katika shule ya chekechea.

“Lucas…” Alvin alimbeba Suzie na kumsogelea haraka.
Lucas alimtazama bila kujali kabla ya kukaza mkono wake kwa Sheldon na kuongeza mwendo wake.


"Lucas, nahitaji kuzungumza nawe." Alvin akakaribia, lakini Sheldon akamzuia mara moja.

"Bwana. Kimaro, tafadhali usimsumbue mwanangu.” Sheldon alimkazia macho kwa kujitetea.

“Ni mwanangu. ” Alvin aliinua uso mdogo wa Lucas kwa umakini. Alionekana kufanana. Hakika alifanana sana na Lisa.

Katika watoto hao wawili, Suzie alifanana naye lakini upole wake ulikuwa kama Lisa. Wakati huo huo, Lucas alionekana kama Lisa, lakini hasira yake labda ilimfuata.

Sheldon alikunja uso, na Lucas ghafla akatazama juu na kusema kwa ubaridi, "Sina uhusiano wowote na wewe, na sikujui kabisa." Kisha, akamvuta Sheldon na kuondoka.
Alvin alihisi uchungu, lakini kwa ukaidi aliwafuatilia kwa nyuma. “Lucas, ni kawaida kwako kunichukia, lakini kama baba na mwana, tunapaswa kukaa chini na kuzungumza. Je, huna la kuniambia?”

"Sina la kumwambia mgeni." Uso maridadi wa Lucas ulikuwa umenyooka, na sauti yake ilikuwa thabiti sana.


“Mimi si mgeni. Mimi ni baba yako mzazi. Una damu sawa na yangu. Huo ni ukweli ambao hauwezi kubadilishwa.” Alvin alimzuia kwa ukaidi.

Mzozo wao ulisababisha wazazi kadhaa, ambao walikuwa huko kuchukua watoto wao, kuwaangalia.

“Mama…” Suzie aliita ghafla.

Alvin na Lucas waligeuka nyuma na kumuona Lisa akikimbia kutoka kwenye gari. Alivaa gauni jeusi huku nywele zake za mawimbi zikiwa zimetanda begani. Alionekana mrembo lakini asiye na hisia. Macho ya Lucas nayo yakalainika kidogo.


"Lisa, umefika hapa kwa wakati." Sheldon alimtazama Alvin kwa mashaka. "Alisema kuwa yeye ni baba yake Lucas ..."

“Sheldon, asante kwa yote ambayo umefanya siku zote hizi. Unaweza kurudi nyumbani kwanza. Niachie Lucas.” Lisa alitoa shukrani zake na kumchukua Lucas.

“Sawa. Nitaondoka kwanza.” Sheldon akatikisa mkono na kuondoka.

Lisa kisha akamtazama Alvin aliyekuwa amemshika Suzie.
Tukio hili liliwafanya wazazi waliokuwa pembeni kushangaa. Mwanamke mrembo akiwa amembeba mtoto wa kiume aliyefanana naye, na mwanamume mtanashati aliyembeba binti aliyefanana naye - ilikuwa wazi kwamba walikuwa watoto wao wa kibaiolojia.
“Ni nini kinaendelea?”

“Nimesikia huyo kijana ni baba wa mtoto huyo?” Watu walianza kuwanyooshea kidole na kuwasengenya.

Lisa alimkazia macho Alvin. “Hebu tuondoke hapa kwanza.” Alimbeba Lucas na kuingia kwenye gari lake kwa kasi.
Alvin naye akambeba Suzie na kuingia kwenye siti ya nyuma haraka.

Lisa aliuma meno. "Alvin, si uliendesha gari kuja hapa?"

“Ndiyo, lakini nataka kutumia muda zaidi na mwanangu na binti yangu." Alvin alitabasamu kwa furaha.

Hakuwahi kufikiria kwamba angeweza kuketi kwenye gari na mwanamke wake kipenzi pamoja na watoto wao. Ilikuwa ni hisia kubwa.

Lisa alitazama kwenye kioo cha nyuma. Alipoona sura ya Alvin ya mbwembwe, alitamani sana kuvua viatu ili ampige navyo usoni. Lazima angefurahi sana kujua kwamba alikuwa baba wa watoto wake wawili.
Lucas aliona hivyo na kufinya macho yake, ambayo yalikuwa baridi.

"Kama ningekuwa wewe, nisingekuwa na ujasiri wa kutokea mbele yetu." Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mtoto wake kumwambia sentensi ndefu, na uso mzuri wa Alvin ukaganda.

Lucas aliendelea kuongea bila kujali, “una haki gani ya mimi kukukubali kama baba yangu? Unafikiri sisi ni watoto wako kwa sababu tu kulingana na mazowea, ulitoa mbegu za kiume. Hiyo sio haki sana. Umetufanyia nini?”

Uso maridadi na mzuri wa Alvin ulibadilika rangi kutokana na maneno hayo kutoka kwa mtoto yule mdogo. Lisa alitaka kupongeza maneno mazuri ya mwanaye. Ilikuwa kama ilivyotarajiwa kwa mtoto wake. Alisema kile kilichokuwa akilini mwake.

"Sijawahi kufanya chochote hapo awali, lakini nitafanya kuanzia sasa." Uso wa Alvin ulijawa na hasira. “Lucas, nililazwa na mtu fulani.
Vinginevyo, nisingemfanyia hivyo mama yako. Naamini ningetarajia ujio wako kama ningekuwa na akili za kawaida.”

"Ha" Lucas alidhihaki bila huruma. “Wewe ni mwanamume mwenye umri wa miaka thelathini na bado ulizidiwa akili na mtu fulani. Ningeona aibu kusema hivyo kama ningekuwa wewe.”

Alvin akasonga tena. Lucas alisema, “Sijui hata ulikuaje mtu tajiri zaidi nchini. Si ajabu nafasi hiyo haikudumu.” Alvin alikosa la kusema.

Mama yake alikuwa na ulimi mkali kama yeye. Sahau. Lucas alikuwa mtoto wake. Haijalishi jinsi alivyokuwa mkali - alikuwa na ulimi, Alvin bado alimpenda na hakumchukia.

“Uko sawa.” Alvin aliitikia kwa kichwa na kusema huku akionekana kushangaa. “Lisa, kama inavyotarajiwa kwa mwanao, amenipiga msumari kichwani. Ikiwa ningekuwa na nusu tu ya ubongo wake, nisingeishia kutengwa na mke wangu.”

Lisa alishindwa cha kusema. Lucas pia hakujua la kusema. Ili kumrudisha mkewe na watoto, kwa kweli hakujali sura yake tena.

Suzie alimtazama Alvin bila jibu na hatimaye akaangua kicheko. "Baba mchafu, mbona wewe ni mzuri sana?"

Alvin alipigwa na butwaa, alitabasamu tu na kusema, “Suzie, Baba anaweza kuwa mzuri zaidi mradi unipe nafasi ya kufanya upatanisho.”

Kimya kifupi kikatawala. Mara Alvin akasema, “Lisa, unaenda wapi? Kwa nini tusitafute mgahawa wa kula? Ninajua mkahawa wa watoto wenye uwanja wa michezo na aina mbalimbali za nyama tamu, keki na vitafunio.”

"Ndiyo ndiyo." Suzie mlafi alitikisa kichwa kwa kasi.

“We mtoto.” Lucas alikoroma na kumnyooshea kidole.


Suzie alifoka. "Mimi ni mtoto, kwa hivyo nina haki ya kuwa mtoto."

Lucas alikunja uso. “Suzie, unamtendea haki Anko Kelvin? Amekuwa mwema kwako tangu tukiwa wadogo.”

Macho ya Suzie yalitiririka na hatia, lakini bado alitabasamu. “Kwa kuwa unampenda sana Anko Kelvin, kwa nini hukuenda na mama? Hata hivyo, bado unaishi na Babu.”

Lucas alimtazama kwa hasira. Alvin alikipapasa kichwa kidogo cha Suzie kwa sifa na kuamua kumnunulia pipi kama zawadi baadaye. "Lazima uelewe kwamba Kelvin anakutendea vyema kwa sababu anataka kuuteka moyo wa mama yako. Anahitaji kukufurahisha kwanza kwa sababu anataka mama yako ampende.”

“Alvin…” Lisa alimuonya mwanaume huyo aangalie maneno yake.


“Nimesema kitu kibaya?” Alvin alishtuka bila hatia. “Lisa, wanaume si watakatifu. Yeye ni mkarimu kwa watoto kwa sababu tu anataka kukufurahisha. Anajua kwamba asipowafaa watoto, hata hutamfikiria.”

"Hiyo bado ni bora zaidi kuliko wewe." Lucas alijibu. “Tulipokuwa bado tumboni mwa Mama, ulitaka umpatie mwanamke mwingine atulee, na ulitaka tutenganishwe na Mama. Wewe ni mtu mbaya."

Alvin aliingiwa na aibu ghafla. Hakutarajia Lisa angewaambia watoto juu ya mambo hayo.
Suzie alisema kwa sauti, “Hatutaki mama wa kambo katili. Tunataka mama yetu tu."

“Hakuna tena mama wa kambo katili. Mama yako ndiye pekee moyoni mwangu sasa. “Alvin alisema kwa uzito, "Nitampenda hadi nife."
Uso mdogo wa Lucas uliojitenga ghafla ukatoa sura ya kufumba macho. “Uwongo tu."

Alvin alipata pigo kwa mara nyingine tena.
Lisa alitazama sura yake ya kupwaya na kutaka kucheka.
Mwishowe, aliendesha gari hadi kwenye mgahawa wa watoto ambao Alvin alitaja......ITAENDELEA.....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA..