JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................558-559

Sura ya: 558

"Nimemaliza." Baada ya Pamela kupita, alimkonyeza Lisa.

Lisa alikuwa anakaribia kuongea mara ghafla aligundua kuwa Alvin alikuwa akimtazama. Kwa kuwa alikuwa mbali, hakuweza kuona macho yake vizuri, lakini bado ilimfanya ajisikie vibaya. "Hukumwambia chochote, sawa?"

"Sikusema chochote." Pamela akatikisa kichwa. "Hajui kuwa una wasiwasi juu yake."
“Sina wasiwasi naye hata hivyo." Mara Lisa aliangaza macho kana kwamba alikuwa amechomwa kwenye kidonda.

"Usikatae, naelewa." Pamela aliweka mkono begani mwa Lisa. " Baada ya yote, yeye ni mwanamume uliyempenda hapo awali. Unapomwona katika hali hiyo mbaya, moyo wako utahisi tofauti na wengine. Kwa kifupi, ni ngumu. Kuna chuki kidogo, huruma kidogo, na labda kitu kisichojulikana - ”

"Nyamaza. Nitamfuata Kelvin. Siwezi kuhangaika na wewe tena.” Lisa alimsukuma mbali na kugeuka.

Ingawa alikuwa akimtafuta Kelvin, maneno ya Pamela yalijirudia akilini mwake. Ndio, hapo awali alimchukia Alvin na hata alimlaani kupoteza kila kitu. Hata hivyo, kwa kuwa sasa alikuwa amekuwa hivyo, hakuhisi furaha hiyo yote—hasa alipomwona akionewa na kila mtu. Lakini, alikataa kukiri kwamba alikuwa na wasiwasi juu yake. Angewezaje kuwa na wasiwasi juu yake? Ilikuwa ni kwa sababu ya Suzie tu.

Baada ya kuzunguka-zunguka, hatimaye alimkuta Kelvin kwenye chumba cha kahawa kwenye ghorofa ya pili. Alikuwa akinywa kahawa na wanaume wachache wa makamo. Ukiwatazama watu hao, hawakuonekana kuwa wafanyabiashara. Ilikuwa wazi kwamba walikuwa watu wenye ushawishi katika siasa. Kelvin alikuwa akiongea na kucheka nao. Mara kwa mara, alikuwa akiwamiminia watu hao kahawa kwa bidii.

Kuonekana kwake akiwabembeleza wengine pale kulifanya Lisa asimame katika hatua zake bila kujua. Alijisikia vibaya kidogo. Ni mara chache sana alimuona Kelvin namna hii. Katika kumbukumbu yake, Kelvin alikuwa mpole na mtaratibu siku zote, lakini aliweza kuona kwamba Kelvin alikuwa akijipendekeza kwa watu hawa. Aliona tabia hiyo ya Kelvin kuw ngeni kwake. Alijua hakutakiwa kuwa hivyo. Kila mtu ilibidi azungumze vizuri na kuwabembeleza wengine linapokuja suala la biashara, lakini bila fahamu alihisi ajabu sana kwenye hilo.

Ghafla akakumbuka jinsi Kelvin alivyojitolea kumsindikiza kwenye karamu.
Je, ni kwa sababu aliogopa kwamba Alvin angemuibia? Kwa kweli, je, ni kwa sababu alitaka kufanya urafiki na kundi hili la watu mashuhuri?

 “Huyo anayejiita mumeo? Yeye ni mzuri sana katika kujipendekeza kwa watu mashuhuri" Sauti ya Alvin ya dharau ilisikika juu yake.

Lisa aligeuka na kuiona sura yake ya kejeli. Alihisi moyo wake ukichomwa na kitu. "Ni bora kuliko mtu fulani ambaye anataka wengine wajipendeke kwake" wake lakini hakuna anayemjali sasa.”

"Ndio, najipendekeza sana kwako lakini haunijali." Macho ya Alvin yalipomtazama aliyeyuka ghafla kama theluji wakati wa masika; yalikuwa yamejaa huruma.

Kona za mdomo wa Lisa zilimsisimka, lakini kabla hajajibu, akavutwa upande wa pili na Alvin.

"Alvin Kimaro, niache  niende." Lisa alipunguza sauti yake na kujaribu kumpungia mkono. Macho yake yalimtazama Kelvin kwa woga, akiogopa kwamba angemwona.

“Usijali, akili yake sasa imeganda kwa Seneta Gitaru. Hana muda wa kuwa makini na wewe.” Alvin alifungua mlango mdogo wa pembeni na kumuingiza ndani, akamkandamiza ukutani.

Taa hazikuwashwa ndani. Mwili wa mwanamume ulimjaa huku harufu yake ikijaa puani. Lisa alikasirika na kupunguza sauti yake, akiuliza, "Alvin Kimaro, kwa nini umenileta hapa?"

“Je, hutaki kujua Seneta Gitaru ni nani? ” Alvin alibadilisha mada kana kwamba hakusikia maneno yake.

Lisa aliganda, na akasema, “Seneta Gitaru ndiye mgombea mwenza wa Nathan katika uchaguzi wa Rais mwakani. Kelvin anafanya kazi kwa bidii ili kumfurahisha sasa, ambalo pengine ndilo kusudi lake kuu la kuja usiku wa leo.”

Lisa alishtuka kabisa. Alifikiri kwamba Kelvin alikuwa akijaribu tu kujipendekeza kwa mtu mwenye nguvu, lakini hakutarajia kuwa makamu wa Rais wa baadaye.

"Pia, unaweza usijue hili, lakini Seneta Gitaru na Nathan Shangwe wako kwenye mashua moja. Ikiwa atakuwa na uhusiano mzuri na Seneta Gitaru, atakuwa pia akijenga daraja na Nathan.” Alvin aliinamisha kichwa na kumtazama kwa upole. "Unajua ni kwa nini Seneta Gitaru anazungumza naye?"

Kichwa cha Lisa kilisisimka huku akisema kwa kuudhika, “Labda Kelvin tayari anamfahamu. Hakuna cha ajabu katika hilo.”

“Hapana, Kelvin hakumfahamu kabla ya hapa hata kidogo. Hana mtaji wa kuungana na watu wa hadhi hiyo.” Alvin alisema kwa unyonge, “Usiku wa leo, familia ya Shangwe inamsherehekea rafiki yako mzuri, Pamela. Wamealika watu kutoka sekta za siasa na biashara. Familia ya Shangwe inataka kuweka wazi kwa ulimwengu wa nje kwamba wanamfikiria sana Pamela na kuthibitisha msimamo wake wa baadaye nchini.”

“Kwa hiyo…” Lisa hakujua alichokuwa anajaribu kusema.

“Baada ya Kelvin kuingia nawe, Pamela binafsi alikuja kukutana nawe na pia kumtambulisha Aunty Tabia kwako. Watu waliopo wote ni werevu. Watafikiri kwamba Kelvin anamjua mke wa Rais mtarajiwa na mhusika mkuu wa leo, Pamela. Kwa kawaida watavutiwa naye. Kisha akatumia fursa hiyo kujenga uhusiano na Seneta Gitaru.”

Macho ya Alvin taratibu yakawa baridi na yenye kina kirefu.
 Hapo zamani, alishuku tu kwamba Kelvin hakuwa mtu wa kawaida, lakini baada ya usiku wa huo, alikuwa na hakika. Asingekubali Lisa kuwa na mwanaume mnafiki namna hiyo.
Lisa alipigwa na butwaa kabisa.
 Asingeweza kamwe kushuku kwamba kusudi halisi la Kelvin kwenda naye pale lilikuwa kujuana na watu mashuhuri.
 Lakini, baada ya kusikia maneno ya Alvin, ilionekana kama Kelvin alikuwa na mipango ya kina.

Uso wake ulikunjamana, na sekunde moja baadaye, alimtazama Alvin usoni kabla ya kudhihaki. “Sawa, hata kama ulichosema ni kweli, vipi kuhusu hilo? Je, unajaribu kusema kwamba Kelvin hawezi kueleweka? Alvin Kimaro, wote ni watu ambao wamejitahidi katika ulimwengu wa biashara. Ili kufanikiwa, kujipendekeza kunahitajika. Yote hayo ni ya kawaida sana. Kelvin anataka kuendeleza na kuimarisha msimamo wake, kwa hivyo ni kawaida kwamba angejaribu kufahamiana na makamu wa Rais. Na wewe je? Ulikuja hapa usiku wa leo kwa sababu ulitaka kupanua mtandao wako na kujuana na vigogo pia, sivyo?"

"Hapana." Midomo myembamba ya Alvin ikasogea huku akikanusha. "Nilikuja hapa kwa sababu nilijua utakuja."

Macho ya mwanamume huyo yalibeba miali ya moto iliyomulika sana.
Uso wa Lisa ulizidi kuwaka moto huku akiona aibu. Alimkazia macho tu, kana kwamba anauliza 'Unadhani mimi ni mjinga?'

Alvin alitazama macho yake makubwa na angavu kabla ya kufichua tabasamu la kuvutia ghafla. "Asante kwa kumwomba Pamela anisaidie mapema."

“Ni lini nilimwomba Pamela akusaidie?” Lisa alidhihaki, “Usijibembelezeshe kwangu tafadhari.”

“Sijipendekezi. Nadhani ... wewe ni mkarimu sana. ” Tabasamu la Alvin lilikuwa na utata sana.

Lisa alijiona amejitoa kwa kujaribu kuficha nia yake, lakini Alvin alimgundua tu. Alihisi aibu sana. “Ondoka njiani, mimi natoka.”
Alimsukuma kwa nguvu, lakini kifua cha Alvin kilikuwa kama ukuta. Hakuweza kufmsogeza hata kidogo.

Sura ya: 559

"Alvin Kimaro, unataka nini?" Lisa alikuwa hana nguvu. “Unajua jinsi sifa yako ilivyo mbaya kwa sasa? Watu wakigundua kuwa niko peke yangu katika chumba kimoja na wewe, wataelewa vibaya.”

Alvin alishusha macho chini. Mwangaza wa mwezi mkali uliangaza kupitia dirishani, ukionyesha pua yake iliyonyooka na kope nene. Alionekana mzuri na mzuri kama sanamu la kuchongwa.

Ni wazi alikuwa mwanamume mwenye umri wa miaka 30, lakini alipokunja midomo yake myembamba na kunyamaza, alionekana kama kijana katika miaka yake ya mapema ya 20. Alionekana mnyonge kana kwamba alikuwa… mtoto wa mbwa aliyeachwa.

Lisa hakuweza kujizuia kukumbuka kile Pamela alisema. Bado alikuwa mwanaume ambaye alikuwa akimpenda. Ingawa hapo awali alimchukia, alipomwona akiwa amekata tamaa na kuonewa na wengine, angehisi tofauti na wengine.

Ndiyo, mambo yalikuwa tofauti kidogo sasa. Alifikiri kwamba hali ya wakati huo ya Alvin ilionekana kuwa ya kusikitisha kidogo—ilisikitisha sana hivi kwamba iliufanya moyo wake kulainika. Hapana, hakuweza kufikiria juu yake. Angeweza tu kupandwa na wazimu.

Lisa akainama chini na kujaribu kulazimisha kupenya chini ya mkono wake.
Hata hivyo, mkono wa mwanamume huyo ulijibana na mara moja akaushika mwili wake mikononi mwake. Hapo mwanzo alikuwa amemnasa tu kati ya ukuta, lakini sasa, walikuwa wamebanana dhidi ya kila mmoja.

"Alvin Kimaro, umemaliza?" Lisa alilipuka, lakini hakuweza kuwa na sauti kubwa sana. Hata kama alikuwa akipiga kelele, angeweza kufanya kwa upole tu. “Ulisema huwezi tena, kwanini unaendelea kunisumbua? Mbona una ubinafsi sana? Kama ningejua, ningekuacha ufukuzwe mapema.”

Kope za Alvin zilitetemeka huku macho yake yakimtoka. "Kwa hiyo... kweli ulimwambia Pamela kunisaidia?"

Lisa aliuma midomo kwa kuudhika na kumfokea, “Ni kwa sababu nina moyo mwema na nilitokea kumwona Chelsea akikufanyia mchezo mbaya.
 Ingawa sikupendi, mimi si mtu wa roho mbaya kiasi hicho.”

"Kwa hivyo ... umekuwa ukinitazama kila wakati." Alvin alitabasamu kwa upole.

Lisa alikasirika na akaelezea kwa wasiwasi, "Nimekuona tu kwa bahati mbaya. Ilikuwa ni kwa bahati. Isitoshe, hata kama si wewe ila mwanaume mwingine, ningefanya vivyo hivyo.”

"Je! unaweza kuwajali wanaume wengine?" Alvin aliinua mkono wake kwa mawazo na kumgusa uso wake laini. “Lisa, kama mwili wangu ungekuwa sawa, hata mimi si tajiri zaidi nchini, nisingeuacha mkono wako. Lakini kwa sasa…”

Chini ya macho yake kulikuwa na maumivu makali. Baada ya muda kidogo, akatoa kidonge mfukoni na kumpatia.
 “Nitakuruhusu, lakini kunywa kwanza hiki kidonge.”

Lisa aliitazama kwa udadisi na kuona kwamba ilikuwa kidhibiti mimba.
Alipigwa na butwaa na kumrushia usoni kwa hasira. “Alvin Kimaro, kwanini unanipa hivi? Una wazimu?”

“Chukua." Alvin alichukua kidonge na kushika mkono wake, akisema kwa uthabiti, "Sitakuruhusu kupata mtoto wa Kelvin."

Kelvin na yeye walikuwa wakiishi chini ya paa moja. Hakuwa na njia ya kuwazuia kulala pamoja, hivyo angeweza kutumia njia hiyo tu.

Lisa alikodoa macho. Je! alifikiri yeye… alikuwa amefanya hivyo na Kelvin?
Hakuwa na la kusema kabisa, lakini hakutaka kumwambia kuhusu mambo yake na ya Kelvin.

“Wewe ni kichaa. Mimi na Kelvin tayari tumeoana. Ni kazi yetu iwe tunataka watoto au la. Haikuhusu.” Lisa alijitahidi sana lakini hakuweza kujinasua. Aliishia kumpiga teke Alvin kwa hasira.

Alvin akakwepa na kumuonya, “Una uhakika unataka kupigana na mimi hapa? Sijali kuhusu sifa yangu, lakini wewe unapaswa kutunza sifa ya Kelvin na sifa yako.”

“Bila aibu!” Macho ya Lisa yalijawa na chuki. Kwa hakika, hakupaswa kuwa mpole kwa mtu huyu mnyonge.

“Lisa, meza. Nitakuruhusu uende ukimeza.” Alvin alichukua kidonge na kumkandamiza mdomoni.

Ilikuwa ni kidonge tu, kwa hivyo haikujalisha kwa Lisa ikiwa angemeza au la. Hata hivyo, hakutaka kutishiwa naye. “Kwanini nimeze kwa sababu umeaniambia nimeze? Sitachukua. Utafanya nini kuhusu hilo?” Lisa alikitupa kidonge chini na kumkazia macho.

Alvin alikiokota tena kidonge kile mkononi mwake na kukunja uso kwa nguvu sana. “Lisa, usinilazimishe…. ”

“Ninakulazimishaje—”

Kabla Lisa hajamalizia, ghafla mtu huyo aliinamisha kichwa chini. Kisha, midomo yake ilifungwa na wake. Midomo yake ilikuwa sawa na hapo awali, laini kama jeli. Alvin hakujua usiku wa huo alikuwa amepaka lipstick gani, lakini ilikuwa na harufu nzuri. Hapo awali alitaka kumlazimisha kidogo, lakini baada ya kumbusu, hakuweza kuacha. Ni kana kwamba ni mtoto anayekula peremende.
 

Macho ya Lisa yalimtoka. Alipopata fahamu, alikisukuma kifua chake kwa nguvu. Hata hivyo, ulimi wa mtu huyo ulikuwa kama nyoka mjanja. Kadiri alivyozidi kumbusu, ndivyo alivyozidi kuingia ndani. Alitumia vidole vyake kwa hasira kumbana.

Alvin akashusha pumzi. Wakati huo, alikuwa mkali  kama pilipili. Ilikuwa busu zuri sana na ilimfanya atamani kuonja zaidi.

Wakati huo, sauti ya wanaume kadhaa wakicheka ilisikika kupitia mlangoni.
"Kelvin, unajua kupika kahawa."

"Ni heshima yangu kuonyesha ujuzi wangu mbele yako, Seneta Gitaru."
Sauti ya Kelvin ilisikika mlangoni.

Lisa aliogopa sana hadi moyo wake ukaanguka. Wakati huo, Alvin alizidisha busu. Mkono wake ulimshika kiunoni, na akasema kwa sauti ya upole, “Ikiwa haujali Kelvin kujua, unaweza kupiga mayowe.”

Kupiga kelele? Angewezaje kupiga kelele? Angethubutu vipi? Ikiwa Kelvin angeingia na kumuona Alvin akimbusu, asingeweza kusafisha jina lake hata baada ya kuruka mtoni.

Alipoona utiifu wake hauthubutu kufanya chochote, Alvin aliukunja uso wake mdogo na kumbusu kwa uhuru.
 Alijua kwamba alikuwa akienda mbali sana. Alikuwa mbinafsi na mwenye dharau.
 Hata hivyo, alipopata ladha yake, ilikuwa kama dawa za kulevya. Hakuweza kuacha.

Katika giza, pumzi za chini za mwanamume zilijirudia masikioni mwake. Lisa hakuthubutu kupumua kwa woga. Angeweza tu kumuombea Kelvin aondoke haraka ili aweze kumsukumia Alvin mbali. Lakini, busara yake iliibiwa polepole na pumzi za Alvin.
 Nyuma ya mlango, sauti za kundi la watu zilisikika.

Akiwa katika hali ya kutatanisha, simu yake iliita ghafla. Aliruka kwa woga na kumsukuma Alvin kwa haraka.
 Alvin aliyekuwa amezama alishikwa na butwaa na kupiga hatua mbili nyuma. Alitoa simu yake nje kwa hofu na kuona maneno 'Kelvin Mushi'. Alijisikia kama fujo. Aliweza tu kuinyamazisha na kuirudisha haraka mfukoni. Kisha akaufikia mlango ili kujaribu kutoroka. Hakuthubutu kubaki hapo tena.
 

“Una uhakika unataka kutoka hivyo?” Sauti ya Alvin yenye mvuto ilisikika kutoka nyuma.

Mwili wake uliganda. Alichanganyikiwa mwanzoni, lakini alipotazama chini, aliona kwamba upande mmoja wa kamba ya bega yake ilikuwa imechanika. Sehemu kubwa ya kifua chake ilikuwa wazi.

Uso wake mdogo na wa kupendeza uligeuka rangi mara moja.
 Aliinua mkono wake na kumpiga kofi usoni. "Una laana wewe!"

"Ndio, mimi ni mlaaniwa, nimelaaniwa na penzi lako." Alvin alitumia ncha ya ulimi wake kuibua kidonda kinywa chake. Akasogea karibu na kuegemeza mikono yake pande zote mbili za masikio yake. Macho yake yalichomwa na joto lisilojificha.

Lisa alipigwa na butwaa. Uso wake ulionekana kana kwamba amepigwa na radi. Tayari Alvin alikuwa hivyo wakati hajapona. Je, nini kingetokea atakapopata nafuu? Angeweza kuruhusu maisha yake yaende kwa amani kweli?

“Wakati mwingine, inabidi ujifunze jinsi ya kuruhusu maisha mengine yaendelee. Kuna baadhi ya mambo hayawezi kutibika kwa sababu tu unataka.” Lisa alijitahidi sana kurudisha busara zake na kuyaondoa mawazo hayo. “Kwa nini kujisumbua? Ikiwa huwezi kufanya, kwanini kujitesa kwa makusudi namna hii?” Lisa alipepesa macho yake makubwa. Wale ambao hawakujua wangefikiri kwamba alikuwa akimshawishi kijana ambaye alikuwa amepotea njia.

Alvin alimtazama kwa makini kwa muda kabla ya kutabasamu ghafla. Alisema maneno machache, "Baada ya kukuonja, sitaki kukuacha pamoja na hali yangu."

Lisa alikasirika. “Umewahi kuniomba ridhaa yangu? Hata ukipona sikutapenda na sitakusamehe.
 Fikiri juu ya mambo yote ya kuchukiza uliyofanya kabla ya haya.”

“Ndiyo, nilikuwa mtu wa dharau. Ndiyo maana nitatumia maisha yangu yote nikijisafisha kwako.” Alvin alikiri kwamba alikuwa mtu wa kudharauliwa.

Katika siku chache zilizopita, alijaribu kumwacha na  na kujiondoa kabisa kwa Lisa. Lakini, aliishia tu kuchanganyikiwa kila siku alipojilazimisha kumsahau. Hata kama alikuwa akifanya kazi ofisini, ilikuwa ni kama alikuwa amepoteza ghafla uwezo wake wa kufikiri.

“Meza. Ukimeza nitakuruhusu utoke.” Alvin akatoa kidonge kingine cha uzazi na kukiweka mkononi.

Lisa alikosa la kusema kabisa. Hakuna kitu kilikuwa kimetokea kati ya Kelvin na yeye, kwa hiyo kwanini alikubali? Hata hivyo, hakutaka ajue hilo.
Mwishowe, alichukua kidonge na kutabasamu kwa makusudi. “Sawa, nitameza. Kelvin na mimi tunafanya hivyo kila siku hata hivyo, kwa hivyo hata nikimeza leo, bado kupata mimba siku nyingine.”......ITAENDELEA.....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA..