JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................548-549

Sura ya: 548

Saa moja baadaye.

Baada ya Pamela kukaa katika hali nzuri, alifahamishwa kuhusu mipango ya familia ya Shangwe. Angekuwa mtoto wa hiari wa Nathan, mgombea urais katika siku zijazo? Hakujua kama alie au kucheka.

"Pamela, ukimtoa huyu mtoto, utapoteza haki ya kuwa mama, na mtoto wa Rais ajaye" Lisa alisema kwa husuda.

“Ha! Inaonekana mbingu tayari zimeniamulia.” Pamela hakutarajia maisha yake kufikia hatua hiyo.

Alifikiria kuwa katika uhusiano wa kawaida wa kimapenzi hapo awali. Mwanamume huyo hakuhitaji kuwa baba wa familia yake, hivyo alipanga kumzaa tu huyo mtoto. Baada ya hapo, angejenga familia na mwanamume mwingine na kupata watoto. Lakini sasa, maisha yake yalikuwa yamechukua sura mpya.
Wendy alimfariji, akisema, “Usijali, Pamela. Kwa utambulisho wako huu katika siku zijazo, wewe ndiwe utachagua wanaume. Bila shaka, unaweza kuwa na wasiwasi kwamba wanaume watajali kwamba umejifungua mtoto hapo awali. Lakini wanawake wengi walioolewa wakiwa na watoto wa nje ya ndoa wanaishi vizuri na kwa furaha pia. Isitoshe, ikiwa mtu yeyote atathubutu kukuonea, familia ya Shangwe itasimama kwa ajili yako.”

Pamela aliweza kucheka kwa uchungu tu. Kwa kweli, hakupaswa kuwa na malalamiko mengi. “Lakini sitamruhusu mtoto wangu amtambue Rodney kama baba yake. Kwanza, yeye hamtaki hivyo hastahili. Pili, sitaki mtoto wangu amwite Sarah mama yake wa kambo siku za usoni.”

“Hilo hakika halitatokea. Hatuna uhusiano wowote na Rodney tena. Tayari nimepanga kampuni iandae hati ya kumvua umiliki kampuni. Tutaitangaza kwa umma hivi karibuni,” Jason alisema bila kusita.


Pamela alishtuka. Familia ya Shangwe ilikuwa nzuri sana katika kufanya maamuzi. Alihisi kuridhika na kushangazwa. Rodney lazima alitaka kutapika damu alipopoteza familia yake. Pia, Sarah angemvumilia Rodney kwa muda gani? Alijawa na matarajio ghafla.

Siku hiyohiyo, ukurasa rasmi wa Facebook wa Shangwe Corporation ulitoa taarifa: [Mkurugenzi wa Shangwe Corporation, Jason Shangwe, anatangaza rasmi kwamba amefuta uhusiano wa baba na mtoto na Rodney Shangwe. Wakati huo huo, Rodney hatakuwa tena na chochote cha kufanya na familia ya Shangwe kuanzia sasa na kuendelea. Wanafamilia wa Shangwe pia hawatakuwa na mwingiliano wowote na Rodney. Haki ya Bw. Rodney Shangwe ya urithi kwa mali zote za familia ya Shangwe ni batili. Inatarajiwa kwamba kila upande utaenda kivyake kuanzia sasa na kuendelea na hawataingiliana tena.]

Kisha, Jessica alitoa taarifa pia. [Nimekata uhusiano wa kaka na dada na Rodney Shangwe.]

Carson Shangwe: [Nimekata uhusiano wa ukaka na Rodney Shangwe.]

Nathan Shangwe: [Sina uhusiano wowote wa kindugu na Rodney Shangwe.]

Taarifa za familia ya Shangwe zilitolewa moja baada ya nyingine. Taifa zima likashtuka. Wanamtandao wakatiririsha maoni yao kama kawaida:

[Rodney alifanya nini hadi kufukuzwa kutoka kwa familia ya Shangwe? Kila mtu katika familia ya Shangwe hata alikata uhusiano naye?]

[Rodney lazima awe mpumbavu. Ana baba na ndugu ambao wana mali yenye thamani mabilioniya dola. Ana hata baba yake mdogo ambaye atakuwa Rais, lakini aliikasirisha familia yake.]

[Nilisikia kwamba ni kwa sababu Rodney anasisitiza kuwa pamoja na Sarah. Familia ya Shangwe haijaridhika naye. Wanampendelea zaidi mchumba wake, Pamela.]

[Hii ndiyo familia ya Rais mtarajiwa tunayoizungumzia. Je, hiyo ni familia ambamo mwanamke mwenye pupa ya mali kama Sara anaweza kujiunga?)

Baada ya nusu saa, Nathan alichapisha picha nzuri ya Pamela kwenye Facebook yake ikiwa na maelezo: [Mimi na mke wangu tumeoana kwa miaka mingi.
Tunamshukuru Mungu kwa kutujaalia mtoto wa kiume. Kwa kuongezea, tumekuwa tukitamani kuwa na binti lakini majaaliwa hayo hatukuwa nayo. Kwa bahati nzuri, mke wangu na Pamela Masanja wamekuwa wakielewana vizuri sana. Tumeamua kumchukua kama binti yetu wa hiari. Ingawa hataweza kuwa binti-mkwe wa familia yetu, kuwa binti yetu ni nzuri pia.]

Wanamtandao walipigwa na butwaa tena:
[Nimechanganyikiwa. Kwa hivyo Rodney alifukuzwa kutoka kwa familia ya Shangwe kwa sababu alikataa kumuoa Pamela?]
[Nilimhurumia Pamela hapo awali, lakini sasa ninamuonea wivu. Binti wa Rais mtarajiwa? Kweli kila mtu na bahati yake duniani.]

[Kama anaweza kuwa binti wa Rais, kwanini ni lazima awe mchumba wa Rodney? Ahhh, si kuwa binti wa Rais ni bora zaidi?]

[Je, bado unakumbuka kwamba watu walikuwa wakimrushia mayai yaliyooza Pamela alipokuwa akitembea mitaani miaka mitatu iliyopita? Habari hii inatuambia tusiwadharau wanawake. Nani anajua ni lini atakuwa na nguvu na kuinuka tena?]

Wakati huo, Rodney alipigwa na butwaa akitazama mfululizo wa taarifa hizo. Hakufikiri kwamba baba yake alikuwa akizingatia jambo hilo kwa uzito. Kwa njia ya haraka, alikuwa amemkana hadharani na wanafamilia wengine wa Shangwe walifuata nyayo.

Zaidi ya hayo, Nathan alimchukua Pamela kama binti yake wa kike pia.
Huyo mwanamke amekuwa dada yake? Hapana, si dada yake. Hakuwa hata na damu ya familia ya Shangwe kwanza.

Alikuwa kwenye hatihati ya kulia. Ingawa tayari alikuwa amefikiria matokeo mabaya zaidi yanayoweza kutokea asubuhi yake alipoamua kumlazimisha Pamela akatoe mimba, bado alihuzunika sana wakati huo ulipofika.

Wakati huo, Rodney alihitaji sana mtu wa kumfariji. Aliweza tu kumwita Sarah. “Sarah, nimekataa kumuoa Pamela. Lakini…nimefukuzwa kutoka kwa familia ya Shangwe. Hutajali, sawa?"

“Kwanini… Kwanini nijali? Umefanya mambo mengi kwa ajili yangu… nimeguswa sana.” Sarah alishikilia msukumo wa kumkaripia. Kisha akasema kwa sauti ya chini, “Laiti ningejua mapema kwamba familia yako hainipendi sana…”

“Sarah, usiseme zaidi. Tayari nimefanya uamuzi wangu. Mtoto wa Pamela hatakuwa na uhusiano wowote nami katika siku zijazo,” Rodney alimkatisha kwa kuudhika.

Akimzungumzia Pamela, Sarah alikaribia kutema damu. "Kwanini baba yako mdogo alimchukua kama binti yake wa kike?"

Kuwa binti wa Rais mtarajiwa kulimuuma sana Sarah Hakupata picha ikiwa ni yeye ndiye angepata cheo hicho. Ingawa hakuwa binti yake wa kumzaa, utambulisho huo ulikuwa na nguvu za kutosha hivi kwamba Pamela angeweza kufanya chochote anachotaka nchini Kenya sasa. Pamela angeweza kuolewa na kuwa na familia bora katika siku zijazo pia.

"Labda familia yangu ilifanya hivyo ili kufidia hatia yao." Rodney pia alishuka moyo. "Sahau. Wacha tu. Mwanamke huyo ana mahesabu makali sana. Mwishowe, alifanikiwa kupata alichotaka.”

Asahau? Je, jambo hili lingewezaje kufutika hivi hivi kwenye kichwa cha Sarah? Sarah alikuwa na hamu ya kumtukana kwa sauti.
Alimwonea wivu sana Pamela. Yule b*tch amewezaje kuwa binti wa Rais wa baadaye? Alitaka utambulisho huo pia. Afadhali kuachana na Rodney.

Japo Rodney kweli alirudi upande wake mwishoni, lakini, bila usaidizi wa familia ya Shangwe, angekuwa tu mtu wa kawaida sasa bila kujali kama kampuni yake ya Osher Corporation ingefanya vizuri au la. Isitoshe, familia ya Shangwe ilikuwa imemkataa. Ingekuwa ngumu zaidi kwa Rodney kuendelea katika ulimwengu wa biashara.
Hakuna mtu ambaye angemjali tena hata kidogo. Rodney angekuwa maskini kuliko Sarah sasa.

“Rodney, nadhani lazima utakuwa umekasirika sasa. Pumzika vizuri kabla ya kuomba msamaha kwa familia ya Shangwe. Hakuna chuki zinazodumu usiku mmoja kati ya baba na mwana.” Sarah akakata simu na kumwacha hivyohivyo.

Rodney alipigwa na butwaa. Alikuwa akitaka kuzungumza naye zaidi ili kupunguza hisia zake za kukata tamaa.

Akawaza na kumpigia Chester. "Chester, niko katika hali mbaya. Twende tukanywe usiku huu…”

“Siendi.” Chester alimkataa mara moja.

“Bado wewe ni rafiki yangu?” Rodney alikasirika.

"Sitaki kunywa kwa sababu ya ujinga wako." Chester alimkemea kwa ukali, “Rodney, sikuwahi kufikiria ungekuwa mjinga kiasi hicho! Ulimlazimisha Pamela kutoa mimba na hata kumfanya aanguke kwenye ngazi? Ulikuwa unafikiria nini?”

“Mimi… nilitaka tu kumridhisha Sarah. Sitaki kupata mtoto wa nje ya ndoa. Sarah na mimi tutapata watoto siku zijazo,” Rodney alisema akijitetea.

"Mm, basi natamani nyinyi wawili mpate watoto katika siku zijazo. Kikumbusho tu, lazima uwe na adabu wakati wowote unapomwona Pamela katika siku zijazo. Yeye ni binti wa baadaye wa Rais. Sentensi moja tu kutoka kwake inaweza kukuangusha chini.” Chester alicheka kabla ya kukata simu.


Uso wa Rodney ulijawa na aibu na huzuni. Alikuwa akiufuata moyo wake tu, kwanini kila mtu alikuwa akimtenga?

Sura ya: 549

Jioni.
Lisa alipeleka chakula hospitali. Pamela alimpa macho ya kuomba msamaha. “Lisa, nakuonea huruma kwa kukusumbua unihudumie. Kwanini usirudi? Nitamwomba Sasha aje.”

“Ni sawa. Ningekuwa rafiki gani ikiwa ningekutekeleza nyakati hizi? Isitoshe, nilipokuwa mjamzito huko Marekani, hukunitunza vizuri pia?”

Lisa aligundua kuwa Pamela hakuwa na furaha sana. Hata hivyo, aliweza kuelewa. Kuzaa mtoto ambaye hakuwa na baba ni vita vya ujasiri kwa mwanamke yeyote.

“Hiyo ni sawa. Nilijisikia furaha sana kutumia wakati na Suzie na Lucas huko Marekani. Kwa kweli, watoto ni wazuri sana pia.” Pamela ghafla alijisikia faraja alipokuwa akiwaza jambo hilo. "Siku hizi, kuna wanaume suruali wengi sana. Ni bora kuzaa mtoto wako tu. Wengi wanaishia kuchumbiana tu na kutofunga ndoa.”

"Bado utakuwa na fursa nyingi, haswa baada ya kuwa binti wa Rais wa Kenya. Kutakuwa na wanaume bora tu wanaokufuatilia."

"Mm-hmm." Pamela alicheka. "Nani anajua? Labda baada ya miaka michache, nitakuwa nikitembea kwenye ukumbi mkubwa wa karamu nimevaa gauni refu. Nitakapowaona wale shetani wawili, Rodney na Patrick, wakiinamisha vichwa vyao kwa unyenyekevu na kusimama kando, nitapunga mkono wangu na kusema, 'Walinzi, toeni vipande hivi viwili vya takataka hapa. Hawastahili kuwa hapa na kuchafua macho yangu matukufu kwenye hafla kama hii.”

Lisa alishusha pumzi baada ya kumuona Pamela hatimaye akitabasamu.
Baada ya kumaliza kula, alimpigia Kelvin simu. " Samahani. Siwezi kuhamia kwako usiku wa leo. Sikujua hili lingetokea kwa Pamela…”

“Ni sawa. Yeye ni rafiki yako. Unapaswa kuendelea kumhudumia zaidi."
Kelvin alisema kwa upole, “Mko wodi gani? Nitakuja kuwatembelea baadaye.”
"Ni sawa, hakuna haja. Watu wengi sana kutoka kwa familia ya Shangwe wanapishana hapa kila dakika. Pamela pia anahisi kizunguzungu Tunapaswa kumwacha apumzike.”

“Sawa, nitakuja kesho.” Kelvin alisitasita kwa muda kabla ya kuuliza ghafula, * Je, kweli Nathan anamchukua kama binti yake wa kike?”

“Bila shaka. Nathan mwenyewe hata alitoa taarifa binafsi. Pamela atakapokuwa sawa, familia ya Shangwe itafanya sherehe kubwa ya kumtambua Pamela.”

Kelvin alisema kwa kina, "Inaonekana kama ajali hii ilikuwa baraka kwa Pamela. Binti wa Rais, utambulisho huu kwa kweli ni wa ajabu."

'Ni sawa tu. Pamela sio mtu anayejali mambo haya.” Lisa alikunja uso aliposikia maneno yake.
Hakufikiria kuwa ajali ile kweli ilikuwa baraka kwa Pamela. Ilikuwa sawa ikiwa watu wengine wangesema hivyo, lakini Kelvin alikuwa mtu aliyewaelewa. Kwa kusema maneno hayo… Ilikuwa ni ajabu kidogo.

Muda si mrefu baada ya Lisa kurejea wodini, sauti ya mtu akigonga mlango ilitoka nje. Aligeuka nyuma na kumuona Alvin akiingia ndani huku taa nyeupe za wodini zikimulika. Alikuwa amevaa shati jeupe lililochomekewa kwenye suruali nyeusi. Alionekana kama mwanafunzi

“Kwa nini uko hapa?” Lisa alikunja uso tena.

Pamela alimpa Alvin jicho la pembeni pia. "Alvin, hatuko karibu na wewe, sawa?"

“Nilisikia kutoka kwa Chester kwamba rafiki yako amelazwa na uko hapa ukimhudumia. Nilikuja kutembelea." Alvin aliweka vitu mkononi mwake kwenye meza. "Hii ndiyo juisi fresh ambayo hutengenezwa pekee kwenye hoteli ya nyota tano na imetengenezwa hivi punde, na—"
"Sijali kuhusu juisi hata kidogo," Pamela alinung'unika, "Unaona hii meza? Vitu hivi vyote ni — ”

“Basi kuna samaki kamba hapa. Nilinunua kwa ajili yako.” Alvin alimtazama ghafla Lisa. Macho yake yalikuwa ndani sana hata mtu angeweza kuzama ndani yake.

Maneno ya Pamela yalimkaba kooni. Kamba? Walikuwa ni samaki aliowapenda sana, lakini angeweza hata kula?

Uso wa Lisa ulilegea kidogo. “Asante, lakini naweza kununua mwenyewe ikiwa nataka kula. Aidha, Pamela hawezi kula hii kutokana na hali yake. Utakuwa unamjaribu tu.”

“Lisa hata kama hunipendi, si lazimaunijibu kikatili hivi.”

Alvin aliumia sana kukataliwa na Lisa. Uso wake mzuri ulikuwa umelegea kwa kukata tamaa. Uso huo, ambao ulionekana kana kwamba ulikuwa umechongwa kwa ustadi na miungu, ulionekana mpweke sana hivi kwamba mwanamke yeyote asingeweza kuuvumilia. Hata Lisa alikuwa ameduwaa kwa muda. Ni kana kwamba alikuwa amemuumiza. Lakini, baada ya muda, alisema bila hisia, "Yaliyopita ni ya zamani. Nilikupenda sana zamani, lakini sikupendi tena kwa sasa.”

Pamela hakuweza kupinga kushusha pumzi. Maneno hayo yalikuwa makali sana. Alipoona sura ya Alvin ikionekana kupauka na kuumia, akataka kupiga makofi.

Hata hivyo, Alvin hakutaka kukasirika. Aliweka vitu vyake kwenye meza.
Hali yake ya unyenyekevu na mvumilivu ilikaribia kumfanya Pamela kuwa kipofu.

Alvin alifungua bakuli lililokuwa na samaki. Samaki wakubwa wa kamba mle ndani na harufu yake kali iliyafanya tumbo la Lisa na Pamela kuunguruma.
"Alvin, ikiwa unataka kula, unaweza kwenda kula nje?" Lisa alisema huku akihisi kuchanganyikiwa.

"Ninawachamgua kwa ajili yako. Nitaondoka nikimaliza.” Alvin alisema bila kuinua kichwa chake, “Hata sawa usipokula. Nitawaacha tu hapa baada ya kuwachambua hata hivyo.”

Wakati huo, mtu mwingine aliyekuja kutembelea Pamela alitokeza mlangoni. Alikuwa Jerome. Mikononi mwake kulikuwa na waridi na baadhi ya vyakula vya wagonjwa. Alikuwa na tabasamu la shauku kupita kiasi. "Halo, Lisa. Ni sadfa iliyoje! Tunakutana tena.”

"Jerome, kwanini uko hapa?" Uso wa Lisa ulizidi kukosa raha.
"Pamela, unafahamiana na Jerome?"

"Simjui." Pamela akatoa macho yake.

Jerome alijifanya kana kwamba hakusikia hivyo. Alitabasamu na kusema, “Nilikuja kumtembelea Bi. Pamela. Bi. Pamela ni binti wa Seneta Nathani Shangwe. Uncle wangu na Nathan Shangwe ni watu wanaofahamiana, kwa hiyo akaniomba nikutembelee.”

Uncle wake aliyekuwa akimzungumzia alikuwa Mason. Lisa alidhani mara moja kuwa familia ya Campos ilikuwa ikichukua fursa hiyo kuanzisha uhusiano na Nathan. Pamela alikuwa ngazi ambayo walitaka kuitumia. Lisa alikosa la kusema. Familia ya Campos haikuwa na aibu kabisa.

Jerome aliendelea kuzungumza kwa uso wa kiungwana. “Sikutarajia ungekuwa mrembo zaidi ana kwa ana kulinganisha na picha, Bi.
Pamela. Ingawa wewe ni mgonjwa, uzuri wako bado unafanya moyo wa mtu kudunda…”

Alvin, ambaye alikuwa akichambua wale samaki wa kamba pembeni, ghafla alidhihaki kwa kusonya.
Jerome alimkazia macho kwa hasira. “Alvin, unafanya nini hapa? Nijuavyo, ulimsaidia Thomas kumuumiza Bi Pamela hapo awali.
Mtu kama wewe ana haki gani ya kuwa hapa?"

“Bado hawajanifukuza. Mbona una haraka sana? Tayari umekuwa mkwe wa Rais mtarajiwa?” Alvin aliinua uso wake mkali. KIM International ilikuwa tayari imeharibiwa, lakini umaridadi wake na macho yake ya kutoboa yalimfanya Jerome ahisi kufedheheshwa.

Pamela na Lisa walipigwa na butwaa. Lisa akasema mara moja, “Jerome, si wewe na Melanie tayari mmeoana?”

Jerome alipokuwa karibu kusema jambo, Alvin alimuwahi na kusema, “Ndoa inaweza kuvunjika kupitia talaka. Isitoshe, utambulisho wa sasa wa Melanie haulingani tena na wa Jerome, ambaye ni Bwana Mdogo wa familia tajiri kabisa ya Campos.
Je, haitakuwa bora kwake kama angeweza kuanzisha uhusiano na Rais wa baadaye?”

“Alvin, funga mdomo wako! ” Jerome alikasirika. Ingawa alikuwa na mawazo hayo, haukuwa wakati wa kuyajulisha. “Naupongeza tu zuri wa Bi Pamela, sijamtongoza. Je, unafikiri kila mtu ni kama wewe, kutoridhika na ulicho nacho na kutoa talaka kama mchezo wa kitoto?”

Alvin alimtazama kwa ukalii. “Huenda ikawa mara yangu ya kwanza kusikia mwanamume aliyefunga ndoa akisema maneno yenye utata kama vile ‘Uzuri wako hufanya moyo wa mtu udunde… ’ kwa mwanamke mwingine.”

Uso wa Jerome ulikuwa umetoka kwa aibu. Macho yake yalikuwa yakimtazama Alvin kwa ubaya. “Chunga mdomo wako, Alvin. Unahitaji nikukumbushe mimi ni nani hasa?"

“Unataka kunikumbusha vipi?” Alvin alitabasamu kwa kumkazia macho.
Jerome hakuwa na maneno ghafla.
Hakuweza kusema kwamba angetafuta mtu wa kumfundisha Alvin somo. Kulikuwa na watu wengine wodini, kwa hivyo hakuthubutu kuwa mbabe sana.
Alipata wazo na kumtazama Pamela kwa shauku. “Bi. Pamela, unahitaji mimi kumfukuza mtu huyu?"

Pamela alipigwa na butwaa. Alimtazama Lisa kwa hisia. Mwishowe, alisafisha koo lake. "Lisa, unaonaje?"

Kila mtu alimkazia macho Lisa. Hata Alvin alimkazia macho. Lisa alikuwa na hamu ya kuwapiga teke Pamela na Jerome. Kwanini walimpkazia yeye aamue? Angeweza kumruhusu Jerome afanye. Hata hivyo, alipotazama sura ya Jerome ya kiburi na kisha akatazama macho ya Alvin ya huzuni… hakutaka kuegemea upande mmoja.

“Ningependa mwondoke wote wawili. Mgonjwa anahitaji kupumzika. Tunaelewa nia yenu nzuri, lakini tafadhali ondokeni." Lisa aliwataka wageni kuondoka. Aliwapa wote wawili maagizo sawa.

Alvin alishusha pumzi kidogo. Alishukuru kwamba hakumruhusu Jerome kumfukuza. Lakini, Jerome alihisi aibu kabisa. Alikuwa bosi wa Campos Corporation, lakini alifukuzwa pamoja na Alvin.
Lakini hata hivyo alitii, Hadhi ya Pamela ilikuwa maalum sasa na Lisa alikuwa rafiki yake.

Jerome aliweza kuvumilia tu. Alilazimisha tabasamu na kusema, “Basi, hatutawasumbua tena. ”

Jerome alipoondoka, alimtazama Alvin kwa ukali. Alvin akasimama. Macho yake meusi na yenye kuvutia yalikuwa yakimtazama Lisa. “Nimemaliza kukuchambulia kamba, nitaondoka sasa.” Baada ya kuongea aligeuka na kuondoka......ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA..