JINA LA SIMULIZI............................LISA

AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................459-460

Sura ya: 459

Kwa upande mwingine, Alvin alikaa kwenye kiti bila kuamini kilichotokea. Macho yake yalikuwa kwa Lisa. Kila mtu alifikiri kwamba alikuwa amekasirika kwa sababu sifa yake kama wakili asiyeshindwa ilipotea kwa sababu ya wakili mdogo.

Hii haikuwa kweli. Sio kwamba hakuwa na nafasi ya kushinda. Kwa ufasaha wake, angeweza kupata sababu ya kupingana bila kujali ushahidi ulikuwa nini. Lakini, ushahidi ulipowekwa mbele yake, aligundua kuwa Logan alikuwa ameandaliwa. Sasa ni nani aliyefanya mchezo huo mchafu? Je, lengo lake lilikuwa ni kumharibia tu uhusiano wake na Lisa ama kulikuwa na sababu nyingine?

Kwa kweli, alipaswa kuchunguza kwa uwazi tangu mwanzo. Yeye aliamini tu pale pale pangoni siku hiyo, alipomuona Logan akimshambulia Sarah na kumfanya ajaribu kujiua. Kwa hivyo, alifikia hitimisho. Baadaye, aligundua kwamba Logan alifanya kazi kwa Lisa. Isitoshe, Logan na Lisa walikuwa wamekutana kwenye baa hivi majuzi, kwa hiyo alifikiri Lisa ndiye aliyempa agizo hilo. Ilikuwa ni kwa sababu Lisa alikuwa na nia ya kulipiza kisasi, na alimchukia Sarah na yeye.

Alisahau kuhusu kukusanya alama za vidole kwenye gari na kusahau kwamba hakukuwa na picha yoyote iliyoonyesha sura ya Logan wakati wa mchakato mzima wa utekaji nyara. Yote ilikuwa njama.

Labda Bw. Nelly alikuwa sahihi. Ilikuwa ni njama ya kuharibu kabisa uhusiano ambao Lisa na yeye walikuwa wameanzisha. Kwa kweli, haikupaswa kwenda mbali hivi. Kwanini alifanya hivi? Kwanini alimkata kidole Logan?
Kwanini aliamua yeye binafsi kuchukua kesi kwa Sarah? Shani na Hans walikuwa wamesema kwamba Lisa alikimchukulia Logan kama mtu wa familia. Mwishowe, alimkata kidole cha mtu wa familia yake.

Hans alisema kwamba ikiwa angechukua kesi ya Sarah, ingemaliza uhusiano wake na Lisa, bila kujali ni nani angeshinda. Kila hatua yake ya ukatili ilikuwa imesukuma uhusiano wao juu ya makali ya kuachana kabisa.

Lakini, hakutaka kufanya mambo haya pia. Alikuwa Sarah ambaye alisema kwamba anataka Kidole cha Logan, na Thomas ndiye alisema ni yeye pekee ndiye anayeweza kushinda kesi au Logan angeachiwa huru. Kwa hivyo, alikubali changamoto.

“Alvin twende…” Sarah kwa wasiwasi na kwa woga aliutazama uso wake mzuri ukiwa mtupu kabisa. Aliishiwa na mawazo, na kisha akawa mpole na mwenye huzuni.

Alinyoosha mkono kumshika mkono, lakini kabla hajaweza, alimkwepa.
Mwili wake ukakakamaa, na Thomas haraka akasema, “Bwana Kimaro, kwa nini uko hivi? Sarah tayari ni mnyonge sana.
Leo hajaumia vya kutosha?”

"Ndio, tayari ana huzuni sana." Alvin akatabasamu.

Alipofikiria jambo hilo kwa makini, je, Sarah alibakwa na Logan? Hapana. Badala yake, vipi kuhusu Logan? Kidole chake kilikatwa, akadungwa madawa ya kulevya ambayo hakuwahi kuyatumia hata kidogo, na mwili wake ulikuwa na makovu.

"Alvin, huniamini?" Sarah alimtazama kwa huzuni kwa uso uliopauka.


Alvin naye alimkazia macho. Huyu ndiye mwanamke aliyekuwa akimpenda. Hata kama hakumpenda tena, alitaka pia kumlinda vyema. Lakini, ghafla aligundua kuwa hakuweza kumuelewa tena.
Tukio la Hisan lilikuwa limenyong’onyesha sana.
Kwa wakati huu, ghafla alitekwa nyara wakati Lisa na yeye walikuwa wanaendelea vizuri. Kisha, kila kitu kilibadilika. Laiti si hawa ndugu, asingemkata Logan kidole na pia asingechukua kesi hiyo. Ikiwa haya yote yalipangwa na Sarah, yangemfanya adhalilike sana.

“Sarah, kesi yako itachukuliwa rasmi na polisi kuanzia leo. Watajaribu wawezavyo kukusaidia kuwapata watekaji nyara hao wawili.
Tayari nimeachana na wewe, kwa hivyo usije kwangu tena siku zijazo. ” Alvin alishusha macho chini na kumaliza kuongea kabla ya kunyanyua miguu na kujiandaa kuondoka.

Sarah alimshika mkono na kulia, “Alvin, haijalishi kama wengine wananitilia shaka, lakini tumefahamiana kwa miaka 20.
Je, huniamini? Mimi ni mwanamke dhaifu tu. Ningewezaje kuwa na uwezo wa kumteka nyara Logan? Uwezo wake wa kupigana ni sawa na wa Master Ganja. Isitoshe, sikujua kwamba Logan pia alitekwa nyara. Kitu cha kwanza nilichoona nilipofungua macho yangu ni yeye.”

“Hiyo ni kweli,” Thomas alisema kwa haraka, "Hata nikiharibu, mimi huharibu tu na punk ndogo ndogo. Sijawahi kugusa madawa hapo awali. Watu hawa ni dhahiri ni nguvu iliyopangwa. Nini kingetokea ikiwa wangefanikisha adhma yao juu ya Sarah tena?”

Sarah alimtazama Thomas kwa shukrani. Mtu huyu hatimaye alisema jambo muhimu.

Kichwa cha Alvin kilitikisika kwa kelele za ndugu wale wawili. Hakuwahi kuchanganyikiwa hivyo hapo awali. Alijisikia kama alikuwa akielea katikati ya hewa, bila nguvu na mwenye hofu. Alishtuka sana alipomuona Lisa akitoka nje ya chumba cha mahakama.

“Nitatafuta mtu wa kukulinda kwa muda, lakini tafadhali usiwasiliane nami tena." Alvin aliushika mkono wa Sarah. "Sarah, lazima uelewe. Nilipoachana na wewe, nilikupa nyumba, gari, na mabilioni ya pesa taslimu. Na wewe, Thomas, nimeilinda familia yako kwa miaka mingi sana na hata kukuokoa mara kadhaa. sina deni nanyi tena.”

Uso wa Sarah ulionyesha kushindwa na ulikuwa mweupe kama karatasi. Machozi yake yalimtoka.

Lakini, Alvin hakuweza kujali. Alikuwa amechoka sana kwa sababu alitambua kwamba uhusiano wake na Sarah ulikuwa umeharibu kabisa hisia ambazo yeye na Lisa walijenga kwa bidii.

Alvin alirudi nyuma hatua kwa hatua na kugeuka kumfuata Lisa bila kuangalia nyuma.

Kwenye korido, Pamela na Lisa walisimama wakingojea lifti.
Alvin akapiga hatua kubwa kuelekea kwa Lisa. Mwendo wake ulikuwa wa shauku, lakini kabla hajamkaribia, Austin alimzuia.
"Ondoka njiani. Nahitaji kuzungumza naye.”

Alvin alimtazama tu Lisa kwa wasiwasi. Aligundua kuwa japo siku chache tu zimepita bila kumuona, alikuwa ameshakuwa mnyonge. Macho yake yalikuwa mekundu na yakiwa na damu. Kwa kuongezea, kulikuwa na duru za giza chini ya macho yake. Lazima alikuwa na wasiwasi sana juu ya kesi ya Logan na labda hakulala kwa siku kadhaa.
Moyo wake ulimuuma sana.
Alikuwa amelazimisha haya yote yatokee. Ikiwa angekuwa na imani naye zaidi, mambo yasingekuwa hivyo.

Pamela alidhihaki, “Alvin Kimaro, unawezaje kukosa aibu kuja hapa? Sarah alipomshutumu Lisa, ulikuwa mkatili na huna huruma, ukimwita mwanamke katili. Hukuwa na imani naye hata kidogo. Sasa kwa kuwa umegundua kuwa hana hatia, unataka kuja kurudiana naye tena?”

Kifua cha Alvin kiliumia kwa maneno ya Pamela. Aliutazama uso wa Lisa uliokuwa umechoka na ghafla akakumbuka kuwa siku mbili tu ziliopita, wawili hao walikuwa wakila bata huko Afrika Kusini. Macho yake angavu na tulivu, jinsi alivyokuwa akijivinjari naye mara kwa mara, na jinsi kicheko chake kilivyokuwa kitamu… Je, yote yalibadilikaje kwa kufumba na kufumbua?

“Sorry…”
"Sio lazima useme samahani." Sauti safi na tulivu ya Lisa ilimkatisha. "Kwa sababu sitakusamehe kamwe."

"Afadhali uende kumlinda Sarah wako mpendwa," Pamela alisema kwa dhihaka, "Baada ya yote, ikiwa kitu kitamtokea, kila wakati na bila masharti utatoka mbio kwenda kumlinda,. Alvin Kimaro, machoni pako, na moyoni mwako, msimamo wa Sarah ni maalum sana. Kwa nini huwezi kukubali?”

“Kwa upande mmoja, unafikiri humpendi, lakini unataka kumlinda. Kwa upande mwingine, unataka penzi la Lisa, lakini unataka arudi kwako bila kujali jinsi ulivyomuumiza. Unafikiri unarekodi tamthilia?”

Uso maridadi na mzuri wa Alvin ulipauka. Pamela alikuwa na furaha isiyoelezeka kwa maneno yake. “Kumbe nilisikia kwa bahati mbaya kuwa ulimpa Sarah nyumba, gari na mabilioni ya pesa ulipoachana naye? Mungu wangu. Hiyo lazima iwe ada ya gharama kubwa zaidi ya kuvunja uhusiano katika ulimwengu huu. Naomba kuuliza ulimpa nini Lisa ulipoachana naye?”

“Lisa, sitafanya hivyo tena. Naapa! ” Alvin aliingiwa na hofu.
Kadri Pamela alivyozidi kuongea ndivyo alivyozidi kufahamu kuwa hakuwa akimtendea haki Lisa.

“Acha kutukana. Ahadi zako zinaniumiza. Alvin Kimaro, kaa mbali nami siku zijazo. Unachoweza kunipa si furaha; ni maumivu ambayo yananipeleka kwenye shimo mara kwa mara. Siwezi kamwe kukusamehe, kwa hivyo usije kunitafuta tena.
Unanichukiza.” Lisa aliingia kwenye lifti bila kuangalia nyuma.

Miguu ya Alvin ilijihisi kama imefungwa mawe wakati alipokabiliana na macho yake ya chuki. Alijaribu kumsogelea lakini hakuweza kusogea.
Ni mpaka alipoondoka ndipo alipohisi mwili wake umeishiwa nguvu zote.
Hakujua jinsi alivyotoka nje ya mahakama.

Alitembea mtaani peke yake kwa muda mrefu hadi akachoka kutembea. Alikaa kwenye kiti kando ya barabara kama kikaragosi asiye na roho.
Hans alitembea na mwavuli. “Bwana Mkubwa Kimaro, kuna jua sana. Unapaswa kurudi kwenye gari kwanza."

"Hans, unafikiri atanisamehe?" Alvin alitazama mikono yake kwa huzuni.
Mikono hii imemkata Logan kidole.

Alikuwa amemwomba mara kwa mara amwamini. Vipi kuhusu yeye? Alisema kwamba anampenda, lakini hakuwahi hata mara moja kumpa imani. Alijaribu kumfungia Logan na yeye kwenye chumba cha chini pia.
Ikiwa Lisa asingemtumia Suzie kutoroka na Logan, labda asingeweza kutambua ukweli.

Haishangazi aliuliza kwanini hakufungiwa katika hospitali ya magonjwa ya akili na kwa chuki nyingi. Angewezaje kuwa kipofu hivyo? Ndiyo, imekuwaje akawa kipofu hivyo? Je, alipatwa na kichaa gani cha kumuumiza mwanamke aliyempenda namna hiyo?

Hans aliitazama sura ya Alvin isiyo na matumaini na kugundua kuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumuona Alvin hivi. Ni kana kwamba alikuwa amepoteza hazina yake aipendayo sana na alikuwa amepotea.

Sura ya: 460

"Bwana Mkubwa, unapaswa kusahau kuhusu Miss Jones na kufanya mambo yako tofauti." Hans alihema moyoni mwake.

Alikuwa amemwonya bosi wake huyo mkaidi usiku huo, lakini kwa bahati mbaya, hakusikiliza. Alvin alimwamini Sarah kupita kiasi. Alijuta sasa, lakini hapakuwa na dawa ya majuto duniani.

“Nimsahau?” Alvin ghafla akainua macho, akainuka na kumshika kola Hans. Alionekana kama simba ambaye alikuwa karibu kuanguka. “Nitamsahau vipi?! ”
“Ulipomsaidia Bi. Njau katika kesi yake, si tayari umeacha kufikiria maisha ya baadaye na Miss Jones? Katika hali hiyo, ulipaswa kuwa tayari umejiandaa kiakili muda mrefu uliopita, "Hans alimkumbusha.

Alvin aliganda. Sauti ya Hans ilikuwa kama kofi kali usoni mwake.
Ndiyo, hapo awali alikuwa ameamua kutompenda Lisa tena, kwa nini asimwache aende zake sasa? Kwa nini ahisi kama maelfu ya mchwa walikuwa wakiutafuna moyo wake?

Hans aliendelea, “Je, unamuonea huruma Bi Jones? Lakini kwake, msamaha bora ni kuacha kumsumbua. Yuko sawa. Kama asingekuwa karibu nawe, labda asingeumia sana.”

“Hans…” Alvin alimkazia macho. Hakuwahi kufikiria kuwa Hans angekuwa na ujasiri wa kumwambia jambo kama hilo.

“Bwana Mkubwa Kimaro, samahani. Labda nimejikwaa maneno yangu leo." Hans alitabasamu kwa uchungu. "Kama mtazamaji, nadhani Bi Jones anasikitisha sana. Kabla ya kuachana naye mara ya mwisho, Maya alimvua nguo mbele ya Roy na wengine. Uliweza kukabiliana na Maya na kumfanya Miss Jones ahisi kuguswa kidogo, lakini tukio hili la utekaji nyara limeharibu matumaini yake. Ulimwomba akusamehe, lakini atakabiliana vipi na Logan na kidole chake kilichopotea katika siku zijazo?"

"Ndio, aliniambia mwenyewe kwamba kidole hakiwezi kukua tena."
Alvin alitabasamu kwa huzuni huku akirudi nyuma hatua mbili. Akageuka kuondoka.
“Bwana Mkubwa …” Hans alitaka kumfuata.

Alvin alisema kwa uchovu, “Nenda. Nataka wakati wa utulivu peke yangu."

•••
Katika gari, Pamela alipiga kelele kwa furaha, "Lisa, unafikiri Alvin Kimaro atamtilia shaka Sarah wakati huu?"

"Sina hakika, lakini nadhani Sarah atajaribu kila kitu kujiondoa tuhuma." Lisa hakuwahi kuthubutu kumdharau Sarah.

"Hiyo ni kweli. Nilidhani ulimshinda Alvin kabisa mara ya mwisho, lakini ni nani angetarajia aje na kesi ya utekaji nyara?” Pamela alibofya ulimi wake. "Alvin hakika anajuta hivi sasa. Nadhani atakuja kukutafuta tena. Hukuiona sura yake tulipotoka mahakamani. Majuto na huzuni machoni pake … Hehe, anatia huruma sana."

"Kwa bahati mbaya, haijalishi anatia huruma kiasi gani, kidole cha Logan bado hakipo." Lisa hakuweza kujizuia kuinua vidole vyake vyema na vyembamba.

Pamela alipoona hivyo moyo wake ukaingiwa na huzuni. "Ni sawa. Hivi karibuni au baadaye, tutashughulika na Sarah na kaka yake.

“Unapaswa kuwa mwangalifu,” Lisa alimkumbusha, “Sarah anaweza kuwa kichaa. Alijaribu hata kujiua ili kupata imani ya Alvin. Mwanamke wa aina hii anatisha."

"Ndio, nitakuwa mwangalifu sana."


Pamela aliona sura nzuri ya Kelvin imesimama nje ya jengo la nyumba ya Lisa kwa mbali. “Umeamua kweli kuolewa na Kelvin?”

"Ndio, yeye ni mzuri kwangu. Sitaki kumwangusha tena.” Lisa alilitazama sura ile na macho yake yaling’aa kwa mwanga wa upole.

Pamela alipigwa na butwaa. Aliweza kuhisi kwamba baada ya tukio hili, Lisa alikuwa akimtendea tofauti Kelvin. Zamani, mara nyingi alipinga alipogusia tu habari zake, lakini sasa, hakuwa hivyo tena. Kelvin alikuwa amepata faida wakati huu, sivyo?

“Naam, hiyo ni nzuri. Wanaume kama yeye ni wachache sana. Lakini ikiwa Alvin atagundua, hatakutishia kutengana kama hapo awali?" Pamela aliuliza kwa wasiwasi.
“Ndiyo maana sitaiweka hadharani. Angalau, hadi tutakapopata cheti cha ndoa." Lisa alitabasamu kwa unyonge.

"Hilo ni wazo zuri. Kisha, nitasubiri kuwa mpambe wako. Nimekuwa nikiisubiri siku hii kwa muda mrefu.” Pamela alikuwa na furaha ya dhati kwa Lisa.

Lisa alipigwa na butwaa. Ndio, aliolewa hapo awali, lakini hakuwahi kufanya harusi. Kufikiria juu yake, kwa kweli alikuwa na huzuni sana. "Sawa, basi jiandae kuwa mpambe."

Gari likasimama mbele ya Kelvin, Lisa akashuka.

"Nilisikia umeshinda." Kelvin alitabasamu na kuushika mkono wake kawaida.

“Ndio. Ni shukrani kwa ushahidi ulionipa. ” Lisa alimtazama. “Nitakupikia jioni ya leo ili kusherehekea?”

"Bila shaka, tunapaswa kusherehekea." Kelvin aliinua mkono wake na kutoa pete ya almasi kutoka mfukoni mwake, akamvisha.

Lisa aliitazama pete kubwa ya almasi kwenye kidole chake cha kati na kupigwa na butwaa. "Hii ni…?"

“Uko tayari?” Kelvin alimtazama kwa umakini. “Sitaki mambo ya uchumba wakati huu. Je, tunaweza kuoana tu mara moja?”

Lisa alipigwa na butwaa kidogo. Ingawa alikuwa ametaja ndoa na Pamela kwenye gari mapema, hakutarajia angependekeza hivi karibuni.

"Samahani, inaonekana nimekuogopesha." Kelvin alitabasamu kumtoa hofu. "Ninaogopa sana kwamba utakimbia tena."

“Sitaweza.” Lisa aliweka mkono wake chini na kutabasamu. “Sawa, nimekubali.”
“Kweli?” Kelvin alishangaa, lakini kulikuwa na tabasamu la furaha kwenye uso wake wa kifahari na mzuri.

“Bila shaka.” Lisa alinyamaza na kusitasita kabla ya kusema, “Lakini natumai hatutaiweka hadharani kwa wakati huu. Baada ya yote, unajua kwamba Alvin ana nguvu sana na mbinafsi. Ninaogopa kwamba anaweza kujaribu kukomesha ikiwa atajua kuwa tuko pamoja. Ngoja tusubiri baada ya harusi.”

“Hilo ndilo nililokuwa nikifikiria pia. Ni bora utangaze baada ya kupata mtoto,” Kelvin alisema kwa mzaha. Lisa alipigwa na butwaa na ghafla akawafikiria Lucas na Suzie.

“Usinielewe vibaya.” Kelvin alikisia alichokuwa akifikiria. “Nitawachukulia Lucas na Suzie kama wanangu, lakini napenda watoto. Bila shaka, ni sawa ikiwa hutaki…”

“Hapana, tukifunga ndoa, hakika nitapata watoto wako. Vinginevyo, itakuwa si haki kwako." Lisa alitabasamu. Hakuwa mbinafsi kiasi hicho.

“Lisa, asante. Bado nitakusikiliza. Maadamu ni watoto wako, nitawapenda wote sawa.” Kelvin alitabasamu na kumshika mkono.
“Twende nyumbani kwako. Nina wasiwasi kwamba Alvin atakuja hapa.”

"Ndio, pia ninapanga kuhamia kwa baba yangu kwanza. Angalau ninaweza kuwa karibu na Lucas kila siku katika siku zijazo.

Alikuwa akiishi hapo kwa urahisi tu wa kumtongoza Alvin, lakini kwa kuwa hakuwa na mawazo hayo tena, haikuwa na haja ya yeye kuendelea kuishi hapo. Zaidi ya hayo, aliomba msamaha kwa kutomjali Lucas katika kipindi hicho cha wakati.

“Sawa, nitakusaidia kuhama kesho.” Kelvin alishikilia mkono wake kwenye gari....ITAENDELEA...

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.