JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................445-446
Sura ya: 445
Alvin alikaa kimya, lakini alikubaliana na Rodney waziwazi.
Lisa alipotazama mwanga wa macho ya Alvin ukififia kidogo kidogo, moyo wake ulitawaliwa na kejeli. Alijidhihaki kwa kuguswa na maneno yake saa 24 zilizopita. Baada ya kupitia magumu mengi, bado haikumpata kuwa mtu huyu ni mwongo? Alipomtaka, angeweza kusema kila kitu.
“Alvin, nataka kukuuliza jambo moja tu. Nifanye nini ili umruhusu Logan aende zake?” Lisa aliuliza kwa sauti ya chini.
“Amwache aende zake?” Rodney aliitikia kana kwamba amesikia mzaha. “Unaota? Kamuumiza Sarah, halafu aachwe hivihivi tu? Watu kama yeye wanapaswa kuteswa hadi kufa. Hata hivyo, kwanini una wasiwasi naye sana? Inawezekana una uhusiano naye wa kimapenzi?”
"Angalia mdomo wako." Mara tu Lisa alipomwonya Rodney kwa ukali, aliweza kuhisi hasira ya ghafla katika macho ya Alvin yenye baridi kali.
Moyoni alikuwa akimlaani Rodney.
"Ninaweza kumwacha aende," Alvin alitamka kila neno kwa uchungu, "lakini ni sehemu moja tu anayopaswa kwenda, nako ni kaburini!"
“Alvin, Logan na mimi hatuna hatia. Afadhali uamini maneno ya Rodney kuliko yangu licha ya kulala na mimi kitandani? Hatimaye nimeelewa sasa.” Lisa alishusha macho chini, kope zake zikificha mng'ao wa hasira machoni pake.
Alvin aliumia moyoni baada ya kuona sura yake. Alikuwa akijaribu kumbana kupitia sehemu zake dhaifu, yote ni kwa sababu ya msisitizo wake wa kumokoa Logan.
“Lisa Jones, umeniangusha. Sikuwahi kufikiria kama ungekuwa mwovu sana.” Alvin alimtazama Lisa kwa moyo uliovunjika, hakuweza kujizuia kutoa tabasamu hafifu.
Macho ya Lisa yakawa mekundu. Alikuwa akimwita mwovu? Ni nani aliyekuwa mwovu kati yake na Sarah? Baada ya miaka mitatu, bado alikuwa kipofu kama zamani. Bado alishindwa kuona rangi halisi za Sarah.
“Vipi bado unatabasamu wakati huu?!” Rodney alifoka kwa hasira.
“Inachekesha sana, kwanini nisitabasamu? Lisa alijifuta pembe za macho yake kabla hajageuka na kuelekea kwenye lifti.
“Simama.” Rodney mara moja aliamuru wasaidizi wake kumzunguka.
“Unapanga kwenda wapi?”
“Kwanini? Unapanga kunikamata?" Sura ya mawe iliangaza machoni mwa Lisa. “Nyinyi si ndio mnaongoza Kenya sasa. Mnadai kuwa nilimteka nyara Sarah, lakini mna ushahidi? Kwa sababu tu mlimshika mtu ninayemjua, mna uhakika kwamba ilikuwa kazi yangu. Je, mtu mliyemkamata aliwaambia kuwa mimi ndiye niliyemuagiza kufanya hivyo?”
Akiwa ameudhishwa na shutuma zake, Rodney alikasirika sana hivi kwamba akafungua macho yake. “Sijali! Ikiwa unakubali au la, huwezi kuondoka leo.”
"Vema, Bwana Mdogo Shangwe, hii inamaanisha kuwa unaniteka nyara kwa nguvu." Lisa akamsogelea ghafla. "Naweza kujua kama wewe ni afisa wa polisi?"
“Polisi? Polisi watanifanya nini nikiamua kukukamata?”
"Umesahau kwamba baba mdogo wako atagombea Urais mwakani? Je, unafikiri unaweza kujifanya jeuri na kumshika mtu yeyote bila mpangilio? Sasa, unajaribu kuweka mikono yako juu ya mwenyekiti wa kampuni kubwa kama Mawenzi. Zaidi ya hayo, mimi ni binti wa Joel Ngosha, mmoja wa watu kumi bora zaidi mahiri nchini Kenya.”
Macho ya Lisa yalimtoka kwa ukali. "Bwana Shangwe, ba’mdogo wako ana washindani wengi sasa. Kila mtu katika familia ya Shangwe amekuwa na tabia ya tahadhari kwa ajili ya uchaguzi mwaka ujao, lakini wewe unataka kumburuta ba’mdogo wako chini.
Una uhakika unataka kuharibu sifa ya familia yako na kuwa mtu wa kulaumiwa?”
“Wewe…” Mishipa ya Rodney ilibubujika kwa hasira. Alihisi hamu kubwa ya kutaka kumnyonga. Hata hivyo, aliyosema Lisa yalimwingia taratibu. Alijua vizuri jinsi uchaguzi wa ba’mdogo wake mwaka ujao ulivyokuwa muhimu.
Rodney aliwahi kuharibu sifa ya familia ya Shangwe hapo awali, lakini hiyo ilihusiana na maisha yake ya kibinafsi. Ikiwa angechukua hatua dhidi ya Lisa wakati huo tena, pengine ingesababisha kila mtu kususia familia ya Shangwe kwa ajili ya uchaguzi mwaka ujao.
“Ikiwa unapanga kunikamata, afadhali uwe na ushahidi kwanza,” Lisa alisema bila kujali. Kwa hayo, akageuka ili kuondoka.
"Subiri. Unaondoka, nani amekuruhusu?" Alvin alimsogelea kwa sura nzito.
“Nilisema unaweza kuondoka?” Macho ya Rodney yakaangaza. "Alvin, mshike na umpeleke ONA kumtesa."
“Unapanga kunikamata, huh?” Lisa alitazama machoni mwa Alvin, macho yake yakionyesha sura adimu ya huzuni.
Moyo wake ukasisimka mara moja. Ghafla, hakujua la kusema. Alijua akifanya hivyo, mzozo kati yao ungezidi. Hata hivyo, kwa kuwa sasa alikuwa amefanya jambo hilo baya, je, angeweza kujiafanya kwamba hakuna jambo lolote lililotukia?
"Alvin, mbona unasitasita?" Rodney alinguruma, “Umesahau kwamba Sarah alikaribia kupoteza maisha yake? Je, umesahau sura ya kukata tamaa usoni mwake alipotaka kujiua?”
Lisa alipigwa na butwaa. Kweli Sarah alijaribu kujiua? Hakika, alikuwa amedhamiria kujifanyia ukatili kwa ajili ya Alvin.
"Wewe, utaenda ONA pamoja nami." Macho ya Alvin yalionyesha hali ya mshangao. Kisha, alinyoosha mkono wake kumshika Lisa.
Kabla hajamsogelea, yule mwanamke aliyekuwa mbele yake, akatoa bastola na kumlenga nayo. Tangu litokee lile tukio la kuvamiwa saluni, Lisa alimua kuchukua hatua biafsi ya kuimarisha ulinzi wake kwa kununua bastola.
Alvin aliganda palepale huku akionekana kutokuamini machoni mwake. Haikuwa wazi kama alishtuka kwa sababu alimuona Lisa akiwa na bastola au kwa sababu alikuwa akimlenga nayo.
“Sitaondoka na wewe. Ukithubutu kuniondoa kwa nguvu, sitakuwa na budi ila kukupiga risasi.” Lisa alionya bila masihara yoyote machoni.
Macho ya Lisa yalikuwa tulivu isivyo kawaida. Alihisi kama angempiga risasi kweli ikiwa angesisitiza kumchukua.
Huzuni ilimtawala Alvin ndani kabisa. Alisema kwa sauti ya kishindo, “Unathubutu vipi kuwa na wazo la kunipiga risasi?”
"Kwa hiyo nikae tu kizembezembe na kukuacha unishike badala yake?" Lisa alikoroma. “Sikufanya kosa lolote, kwanini nikubali nikateswe huko ONA? Alvin, ninafanya hivi kwa kujilinda. Unaweza kufikiri kwamba ninakuumiza kwa kukunyooshea bunduki, lakini vipi kuhusu wewe? Unajaribu kunishika, si unaniumiza pia? Kwa kuwa unaweza kuniumiza bila kufikiria mara mbili, kwanini mimi usiweze?”
Aliinua bastola kidogo na kulenga mguu wake. "Unaweza kujaribu kunisogelea ikiwa unadhani natania. Jaribu tu.”
"Ukithubutu kunipiga risasi, utaenda kunyea debe gerezani," Alvin alionya vikali.
“Ukithubutu kunisogelea, utakuwa kilema,” Lisa alimkumbusha bila kulegea.
Alvin alikunja ngumi kwa nguvu. Macho yake yalijawa na hasira, hatia, huzuni, na kukata tamaa. Lakini, Lisa hakuonekana kuliona hilo. Alirudi nyuma hadi akaingia kwenye lifti.
Ni baada tu ya lifti kupanda ndipo moyo wake uliokuwa na wasiwasi ulianza kutulia.
Hakuna aliyejua kwamba alikuwa amepitia mambo mengi sana. Tangu alipovamiwa nyumbani kwake, na baadaye saluni akiwa na Pamela, alikuwa ameweka bastola kwenye gari lake ili tu apate silaha ya kujihami.
Baada ya yote, alijua Sarah angetaka kumuua dakika yoyote. Hata hivyo, hakuwa amepanga kufyatua risasi kwa Alvin, alikuwa akimtisha tu ili asimkamate.
Baada ya kusema hivyo, Lisa hakuweza kumruhusu Alvin ampeleke ONA. Ilimjaza hofu sana. Miaka mitatu iliyopita, Alvin alimpeleka hospitali ya magonjwa ya akili na karibu kumfanya awe mwendawazimu. Miaka mitatu baadaye, ni nani alijua ni matokeo gani ambayo angeyapata katika makucha yake?
Pia, ni nani angemuokoa Logan ikiwa angechukuliwa? Kwa bahati nzuri, alikisia sawa. Alvin hakumfuata tena.
Sura ya: 446
Kwenye maegesho ya magari.
Baada ya lifti kupanda juu, Alvin alipiga kwa nguvu ngumi kwenye kioo cha gari lake. Damu zilimtoka kwenye ngumi hadi chini, hata hivyo hakusikia maumivu hata kidogo. Macho yake yalikuwa mekundu, na huzuni nyingi zilimjaa.
Lisa kweli… akamnyooshea bastola? Ni nini kinachoweza kuwa na uchungu zaidi kuliko kujua kwamba mwanamke wake mpendwa alikuwa na wazo la kumpiga risasi? Ha! Je, hata alikuwa anampenda? Angewezaje kuwa mkatili hivyo?
"Alvin, si tayari umeelewa tabia ya Lisa kwa sasa? Amebadilika kwa muda mrefu. Amebadilika sana hivi kwamba hatuwezi kuona kupitia kwake sasa. Nani angetarajia kuwa angekutishia kwa bastola?” Rodney alisema kwa hasira, “Amekuwa akificha mambo mengi kutoka kwako. Pengine yeye si mkweli kuwa katika uhusiano huu na wewe. Hata hakupendi. Alirudiana na wewe kwa sababu tu alitaka kulipiza kisasi kwa Sarah.
Je, huoni?”
"Nyamaza!" Alvin alimtazama kwa ukali.
“Nasema ukweli tu. Amka na uangalie kilicho mbele yako. Angalia ni nani anayekupenda kweli." Rodney alipomaliza tu sentensi yake, alifungua mlango wa gari kwa mshituko. “Sijamaliza na hili
jambo bado. Hata ingawa angeweza kutoroka leo, sitamwacha atoke kwenye hili. Naenda ONA sasa kumhoji huyo bwege wake.”
Muda mfupi baada ya kuondoka, Pamela alikuja kwa haraka kwa Lisa. "Ni kweli Alvin alimkamata Logan?"
“Mm.” Lisa alikuwa ametoka bafuni na kubadilisha nguo safi.
Kwa vile hakuwa amelala kwa usiku mmoja, uso wake mzuri ulijawa na uchovu. “Kulingana na walivyosema, Logan alinaswa akimfanyia Sarah kitendo kichafu eneo la tukio. Baada ya Sarah kuokolewa, alihisi aibu sana hivi kwamba alijigonga kichwa chake kwenye mwamba ili kujiua.”
"Ni wazi, yote ni mipango ya Sarah. Je, Logan angewezaje kupendezwa na mwanamke kama Sarah? Anamjua Saraha vizuri na anaogopa kupata ugonjwa! ” Pamela alitukana kwa hasira.
Lisa alikuwa anaumwa na kichwa na kujipapasa paji la uso. “Hii ni ajabu sana. Lakini siwezi kumuacha Logan huko ONA kwani Alvin atachukua maisha yake.”
“Una mpango gani?” Pamela aliuliza.
"Sijafikiria chochote bado." Macho ya Lisa yalimtoka kwa kuchanganyikiwa. "Nahitaji kukutana na Logan ili kufahamu suala hilo ili niweze kuthibitisha kuwa hana hatia."
“Sahau kuhusu hilo. Mastaa hao wawili, Rodney na Alvin, wamevurugwa na Sarah. Wana imani naye kabisa. Mara Sarah atakapolia na kuwatishia, bado watamwamini hata kama kuna ushahidi dhidi yake. Pamela akashusha pumzi. "Sielewi kwanini wanaume hao wanamwamini sana Sarah ingawa yeye ni mbaya sana."
“Hasa.” Lisa alikunja ngumi. "Kwa kuwa siwezi kulishughulikia hili peke yangu, wacha nimshilikishe baba."
•••
Saa moja na nusu baadaye.
Joel na Lisa walikwenda kwenye makazi ya familia ya Shangwe pamoja.
Familia ya Shangwe ilikuwa imemaliza kula chakula chao cha jioni. Mbali na Mzee Shangwe, wanawe na wajukuu pia walikuwepo. Hata Nathan Shangwe, ambaye angegombea Urais wa Kenya mwaka ujao, alikuwepo.
"Joel, nini kimekuleta hapa saa hizi?" Mzee Shangwe aliuliza huku akitabasamu.
"Bwana Shangwe, nina jambo la dharura la kuzungumza nawe." Mwonekano wa hasira ukauosha uso wa Joel. “Kama ningekuwa na chaguo lingine, nisingemleta binti yangu hapa. Jason, ukizingatia sisi ni marafiki, natumai utaendelea kumfuatilia mwanao.
”
Jason alipigwa na butwaa. Alikuwa na watoto wawili. “Unamaanisha…”
"Mchana wa leo, Rodney alienda Karen Estate kwa Lisa na kumletea shida."
Lisa aliwasha simu yake na kumuonyesha video. "Hii ni picha niliyopata kutoka kwa kamera ya uchunguzi. Iangalie. Alinigonga na kuharibu gari langu.”
Washiriki wengine wa familia ya Shangwe walikuja kutazama video kwenye simu. Wote wakamuona Rodney akimvuta nywele Lisa huku akimtoa nje ya gari. Hata alimnyonga baada ya kuligonga gari lake. Kutokana na picha hizo, waliweza kuona kwamba aliambatana na watu wengi pia. Mzee Shangwe, Jason, na wengine wote waligeuka kwa hasira mbaya mara moja.
Familia ya Shangwe ilikabiliwa na suala muhimu wakati huo. Ikiwa video kama hiyo ingeenea kwa umma, ingempa wakati mgumu Nathan Shangwe kwenye kampeni zake za Urais.
“Ni nini hasa kilitokea?” Jason punde akajivuta. "Lazima kuna sababu nyuma ya hii."
“Bwana Shangwe, ikizingatiwa kuwa wewe ni mtu mwenye busara na pia mtu wa hekima, nitakuwa wazi na wewe. Sarah alitekwa nyara jana. Ikatokea mtu aliyenaswa ni mlinzi wangu. Kwa sababu hiyo, Rodney alikuwa anashuku kwamba mimi ndiye nilifanya hivyo.
“Kwa kweli tukio hili naona ni la ajabu. Nilikuwa Johannesburg siku chache zilizopita. Niliporudi, Rodney aliniangukia akiwa na gari lake na hata akajaribu kunishika ili… kuwafanya watu wake kunishambulia. ”
Uso wa Jason ukawa giza mara moja. Kulikuwa na giza zaidi kuliko mkaa. Kila kizazi cha familia ya Shangwe kilikuwa kikikwepa sana kashfa na kiliimarisha sifa safi kama filimbi. Jason hakutarajia kuwa angekuwa na mtoto wa hovyo kama huyo.
Lisa aliendelea kinyonge, “Nilijaribu kubishana naye, lakini aliendelea kushuku kuwa mimi ndiye niliyesababisha utekaji nyara wa Sarah. Nisingejali kama angetaka kuwaita polisi, lakini lazima awe na ushahidi. Hata yule aliyemkamata hakusema kuwa mimi ndiye nilitoa maagizo.
“Nilitaka kumwelewesha Rodney, lakini hakuweza kujisumbua kunisikiliza hata kidogo. Alichokifanya ni kunifokea na kunipiga ngumi.
Kusema kweli, sidhani kama mlinzi wangu angemteka nyara Sarah. Kunaweza kuwa na mbinu chafu kuhusiana na suala hili.”
“Bi Jones, ni kweli kwamba hukumteka nyara Sarah?” Mzee Shangwe aliuliza ghafla kwa sauti nzito. "Nijuavyo, una kisasi cha kibinafsi dhidi ya Sarah."
“Mzee Shangwe, kama ningetaka kumteka nyara Sarah, nisingemwomba mlinzi wangu kufanya hivyo. Sikuhitaji kuajiri mtu mwingine kufanya hivyo.” Lisa alitoa kicheko cha uchungu. "Zaidi ya hayo, nimekuwa kwenye urafiki na maeleweno mazuri na Alvin siku hizi. Hata tulienda safari pamoja siku mbili zilizopita. Kwanini nijisumbue kumteka nyara Sarah na kusababisha uhusiano wangu na Alvin kuwa mbaya?”
Familia ya Shangwe ilikuwa smart. Baada ya kusikia maneno ya Lisa, waligundua kuwa alikuwa sahihi. Kando na hayo, Mzee Shangwe bado alikumbuka kwamba Alvin alikuja kumchukua Lisa pale kwake ana kwa ana siku kadhaa nyuma.
Joel alisema kwa mkoromo, “Binti yangu asingemteka nyara Sarah. Kwa upande mwingine, Sara ni mwovu sana. Licha ya kujua kuwa Alvin na Lisa walikuwa tayari wameoana enzi hizo, bado alimsogelea Alvin na kumtongoza bila aibu. Baada ya wawili hao kunaswa na waandishi, watu wengi walimkosoa Sarah kama mchepuko.
“Lakini Alvin alimfanya Lisa atangaze kuwa wameachana kutokana na ugonjwa wake. Pia alilazimika kusema kwamba alikuwa akimpenda sana Sara. Wakati kwa kweli, Alvin na Lisa waliachana tu mwezi uliopita. Ikiwa huniamini, unaweza kwenda kwa ofisi ya usajili na uangalie tarehe yao ya talaka. ”
Baada ya kusikia haya, wanawake wote katika familia ya Shangwe walikasirika juu yake. Wendy alishangaa. "Hii ina maana kwamba Sarah amekuwa mchepuko tu kwa Alvin katika miaka hii mitatu?”
"Sarah alikuwa mpenzi wake wa kwanza na pia mchumba wake wa utotoni. Ninajilaumu tu kwa kuangukia mtu ambaye alikuwa akimpenda mtu mwingine kwa siri.” Lisa alisema kwa huzuni, “Huenda hamjui kwamba Alvin alikuwa akipanga kumuoa Sarah kabla ya hapo, lakini… Nadhani nyote mliona jinsi polisi walivyomchukua Sarah wakati wa harusi yao. ”
“Ndio. Sarah hakuolewa na Alvin mwishoni, na nikasikia… Alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine?” Jason alikohoa kidogo na kujibu.
“Ndiyo. Sarah alipokuwa kwenye uhusiano na Alvin, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mteka nyara wake wa zamani ambaye alikuwa pia ni mraibu wa madawa ya kulevya. Kama sijakosea, walijuana tangu alipokuwa ametekwa. Kila juma, Sarah alikuwa akienda kwenye nyumba yake na kulala naye.
Mtu aliyemuua mtu huyo hajapatikana. Hapo awali, polisi walimshuku Sarah, lakini hawakupata ushahidi wowote wa kumtia hatiani.”.....ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
